Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, December 19, 2013

Mkuki ni kwa Nguruwe-51




‘Bila kupoteza muda nikanywa yale maji yaliyochanganywa na sumu , sumu ambayo ukiinywa kutokana na maelezo ya muuza dawa za mifugo, haichukui muda, kama binadamu anafariki dunia,, ndivyo alivyoniambia muuza madawa ya mifugo, japokuwa sikumwambia dhamira yangu, nilimuuliza tu kuwa dawa kama hizo zina madhara kwa binadamu, ndio akanipa maelezo hayo....’akasema shahidi, aliyekuwa mfanyakazi wangu wa ndani.

Wakati anaendelea kutoa ushahidi wake huo mimi nilikuwa napigana na dhamira yangu, maana, nilihisi chuki, hasira, na kutaka kufanya jambo, sijui hali hiyo ilikuwa ikielekezwa kwanani, kwani mimi nilishaapa kuwa yoyote atayeingilia ndoa yangu, nikamgundua, basi sitasubiria polisi au kwenda kumshitaki, nitachukua hatua mimi mwenyewe, na nilishabuni njia ya kuwaadhibu watu wa namna hiyo.

Hata hivyo, kila nilipofikiria kwa undani zaidi, niliona kisa cha huyu binti ni tofauti na hawo wabaya wangu, kwani yeye bado ni mdogo, na alikuwa hana tabia ya uhuni, , yeye tunaweza kusema alibakwa, na mbakaji ni mume wangu, na kwahivyo mkosaji ni mume wangu, lakini kilichoniuma zaidi ni kuwa mambo hayo yalifanyika ndani ya nyumba yangu mimi nikiwepo japokuwa sikuwa na fahamu,  na kwa maelezo ya huyo binti, inaonekana kama mimi nilikuwa sijali yanayoendelea ndani ya nyumba yangu mwenyewe.

Yule binti mtoa ushahidi akawa anaendelea kutoa maelezo yake;

Nilikunywa yale maji ambayo nilikuwa nafahamu kuwa yana sumu, kwanza nikapiga fundo moja, nikaona yananyweka, nikaweka la pili, na baadaye nikayanywa yote hadi tone la mwisho halafu nikaweka kile kikombe, juu ya karatasi niliyokwisha iandika, na mimi taratibu nikapanda juu ya kile kitanda, kilichonitesa, nikalala kichwa juu, nikisubiri kufa, dakika tano zikapita, kumi zikapita, robo saa,sikuoni hata dalili zozote za kufa, sikusikia maumivu ya tumbo, tofauti na maelezo ya muuza duka..

‘Ina maana hii dawa imeexpire nini, ‘nikajiuliza,akilini nikapanga nichukue ile dawa iliyobakia, ambayo niliicha chumbani kwangu,nikataka niinuke nienda kwenda kuimalizia,  na mara mlango ukagongwa,...nikashituka, ina maana naota sijafa, au ni kweli, nikainua kichwa, na wakati huo mlango ulikuwa bado uangongwa, tena, unagongwa kwenye hicho chumba nilichokuwa nimelala.

Nilihisi huenda ni baba mwenye nyumba,...lakini yeye hana tabia ya kugonga mlango, huwa akija anaingia moja kwa moja hajali kuwa upoje,...akili ikanituma kuwa huyo ni mtu mwingine kabisa, sikutaka kusimama, maana nilikuwa najiandaa kufa, lakini kufa kwenyewe hakuji, na mara mlango ukafunguliwa...’hapo mzungumzaji akatulia kidogo.

Nikiwa nimefumba macho nikiwaza kuwa huenda nimeshakufa, mlango ulifunguliwa, na nikahisi mtu akikaribia pale kitandani nilipolala, nikaanza kufungua macho taratibu,, na sura niliyoiona ikanifnaya nifungue macho kwa haraka, na kujikunyata , nikiogopa, na kuuliza kwa haraka;

‘Wewe umefuata nini huku chumbani?’ nikauliza na yule mtu akasema kwa sauti ya pole pole, kama mwalimu anayefundisha watoto wadogo;

‘Unafahamu nilikuwa nakuamini sana, kama binti jasiri...’yule mtu akaniambia

‘Lakini sasa nimekutoa katika hilo kundi, ....’nikaona mikono yangu niliyokuwa nimejikunyata kama mtu anayejikinga asipatwe na baya, nikainuka kwa haraka pale kitandani na kukaa, nikanyosha lile gauni vizuri, na kumwangalia huyo mtu aliyeingia, alikuwa mkononi kashikilia kikombe, kinachofanana na kile kile nilichokuwa nimeweka sumu. Vikombe vile vipo vingi hapo nyumbani. Nikamuuliza

‘Unataka kunifanya nini, kwanini unanifuata huku chumbani?’ nikamuuliza nikiwa nimeshamuweka kwenye kundi hilo hilo la watu wabaya, ....

‘Nilikuona ukitaka kujiua, nikaja kwa pikipiki kwa haraka kuja kukuokoa,...hutakiwi kujiua, nafahamu yote yaliyotokea dhidi yako, na nilikuwa natafuta njia za kukusaidia, lakini imekuwa vigumu kukupata, na kila nikija hapa unanikwepa, unaniogopa...kama vile mimi ni mtu mbaya, mimi sio mtu mbaya, nakujali sana’akasema.

‘Umejuaje hayo wakati sijamwambia mtu dhamira yangu?’ nikamuuliza

‘Mimi macho yangu yanaona mbali, kila wanachokifanya watu kwenye majumba yao, nawaona,hasa wale ninaowajali, mimi nakupenda sana, na nilishakuambia awali kuwa mimi nakupenda sana, na mimi ningeliweza kukusaidia kwa kila hali, nilikuomba uwe rafiki yangu, ukawa unamjali sana huyo unayemuita baba yako, sasa kipo wapi...’akasema

‘Uliingije ukachukua hicho kikombe,?’ nikamuuliza

‘Hilo sio muhimu sana, ila usijaribu tena kutumia hii sumu, usijaribu tena kujiua,kwanini ujiue wakati aliyekufanya hivyo, anastarehe, atakusahau, na hataona lolote baya alilolitenda juuu yako, kwanini unajipa shida wakti keshakutengenezea njia ya kuondokana na huo umasikini ulio nao..usijali, mimi nitakufundisha kila kitu, na kuanzia leo jihesabu kuwa wewe sasa ni tajiri...’akaniambia huku akinusa ile dawa kwenye kile kikombe.

‘Hii ni sumu mbaya sana, kama ungekunywa, ungeharibika matumbo yote, na ungekufa kwa machungu makali, sana, kwanini unataka kujitesa kiasi hicho?’ akaniuliza

‘Kuna haja gani ya kuishi baada ya haya yote..’nikasema

‘Hayo yote uliyoyaandika kwenye hiyo karatasi, niliyasoma, ni ujumbe tu usio na maana na ambao wangeusoma, wangelikuona wewe ni mjinga tu, wangekuzika, wakakusahau, usiwe mjinga kisai hiki,...mimi nilishaanza kuwafuatilia wote kwenye hii nyumba, nayafahamu yote yaliyotokea, ...hebu angalai hii hapa...’akatoa kitu kama simu, lakini kubwa, kama komputa ndogo, akaiwasha, halafu akawa anafanya kitu kwenye hicho kidude, akainama kunionyesha

‘Unaona yote yaliyotendeka hapa ndani nayafahamu, ...’akasema huku akinionyesha, ilikuwa kama unaangalai picha, za sinema za mambo machafu, niliwahi kuzisikia, lakini kibaya ni kuwa mchezaji wa hiyo sinema ni mimi na baba yangu mbakaji, ilikuwa sio sinema bali ni tulio halisi , lililonikuta mimi, sikuamini, ilikuwaje mpaka akayaweka yote hayo kwenye simu yake, wakati hakuwepo, nikaamini kuwa kweli huyo ni mchawi.

‘Sasa sikiliza fuata yote nitakayokuambia, ili upate haki zako, ...sasa ninakuap mbinu za kuwa tajiri, kama kweli utayafuata hayo nitakayokuambia,... kwa hivi sasa, akija baba yako mwambie una mimba yake, usimfiche kabisa, kama ulivyoeleza kwenye huo ujumbe kuwa una mimba yake, umweleze hivyo hivyo, na baada ya hapo unamdai pesa, tena pesa nyingi...’akasema na mimi nikamtolea macho ya kushangaa.

‘Usishangae, hawa watu wana pesa nyingi sana, ndio zinawapa kiburi cha kufanya hayo waliyokuanyia, sasa ni wakati wa wewe kuzifaidi,...sikiliza ni kuelekeza jinsi gani ya kufanya...akasema na kunielezea kwa kirafu jinsi gani niongee na baba wa hiyo nyumba akija...aliyoniambai niliona kama ni mambo yasiyowezekana, lakini yeye akanipa moyo kuwa hayo yanawezekana, maana baba w ahiyo nyumba, ataogoa siri hizo zikimfikia mke wake...’akaniambia

Mimi sikuwa na chohote cha kusema au kukataa, maana yale niliyoyaona kwenye hiyo simu yake,yalinifanay nimuogope zaidi huyo mtu, na nilifahamu nisipofanya hayo anayoyataka, ataweza kunifanyia lolote, na kuzionyesha kwa watu, na sikutaka uchafu ule uje uonekane kwa watu, kwani...yalikuwa ni ya aibu tupu, nikawa sina jinsi nikamkubalia hayo aliyonielekeza, na mwishoni akaniambia.

‘Milioni kumi kwa hawa watu ni pesa ndogo sana, ukizishika hizo umeanza kuwa tajiri, na huo utakuwa ndio mwanzo tu,...maana kwa sasa una ushahidi wa kumfanya lolote unalolitaka, ukizipata hizo pesa, nusu kwa nusu..unanielewa...’akaniambia na mimi nikamuitikia kwa kicha kukubali,na hakukaa sana akaondoka zake...

Mimi nikatoka pale chumbani na kwenda kuendelea na shughuli nyingine nikimsubiria baba mwenye nyumba, nilifahamu kuwa muda kama huo atakuwa anarudi, na kweli kabla sijatulia, mlango ukafungulia na mwenye nyumba akaingia, akiimba nyimbo zake za kilevi...

Kama kawaida yake, alikuwa kalewa, na siku hizi alikuwa kazidisha kweli kweli, utafikiri sio yeye, niliyemfahamu kipindi cha mwanzoni,  alikuwa kalewa, anapepesuka, na moja kwa moja akaingia kwenye chumba hicho anachopumzikia, na nilijua baada ya muda ataniita,  mimi nilikuwa nimeshatoka nipo nje, na nikasikia akiniita, nikaingia ndani na kumkuta kavua nguo kabakia na chupi tu, yaani hana hata aibu mbele yangu, akaniambia niende tulale naye, nikakataa..

‘Unaleta kiburi eeeh, kwanza leo sikutaki, nilikuwa nakujaribu tu, nimechoka, nimeshastarehe huko nilipotoka, na watu wanaofahamu ampenzi, sio wewe mpaka tushikane miereka,..lakini kumbuka kuwa nikikuambia kitu, ukanikatalia ujue kuwa mama yako nitam-maliza,kwanza nilihsmpigia simu kuwa wewe uan kiburi, ...’akasema kilevi

‘Fanya unalota, sasa hivi siogopi, maana mimi sina maana tena kwenye hii dunia..ulichoniafnyaia ni kama kunizalilisha mimi na mama yangu na familia yangu kuwa sisi hatuna maana kwenu’nikasema na yeye akasimama, na kutaka kuja kunishika kwa nguvu kama kawaida yake, mimi nikamsukuma, akadondoka chini, alikuwa kalewa,..lakini akikukamata ana nguvu za ajabu, sikupenda aniwahi kunikamata, nikamwambia;

‘Mimi nina mimba yako..’nikasema, na kauli hiyo ilimfanya asimame juu, na ikawa kama pombe zote zimemuishia, akatikisa kichwa na kupangusa macho akaniuliza

‘Unasema nini wewe...?’ akaniuliza

‘Umenipa mimba, ulivyokuwa ukinibaka , nimepata mimba yako, nilikwenda kupima leo mchana, nikaambiwa nina mimba, na mimi simjui mwanaume mwingine zaidi yako wewe, ..wewe ndiye uliyenianza, na sasa nina mimba yako, nitamwambia mama akija..’nikamwambia.

‘Nitakuua,..unasema nini wewe Malaya, , kwanza toka kwenye nyumba hii, nsikuone kabisa, toka kimbia na potelea mbali Malaya mkubwa wewe....’akasema

‘Mimi nitaondoka tu, sin haja ya kukaa hapa, ...lakini kwa masharti, nataka pesa za kujenga nyumba kama ulivyoniahidi, pesa za kutosha, nyumba nzuri kule kijijini, kwa sasa utanipa kiasi cha kuanzia, nataka pesa za kunitosha kuilea hii mimba yako, unawajibika nayo, , ...’nikasema

‘Wewe Malaya mkubwa, ina maana unanisingizia kuwa nimekupa mimba ili nikupe pesa, pesa hupati, na humu utatoka...’akaniambia huku akinitolea jicho.

Nikachukua ile karatasi niliyopima hospitalini, na kuna picha aliniachia huyo jamaa ambaye alikuwa na kumbukumbu zote za hapo nyumbani, na matendo aliyonifanyia, nikampa, nakumwambia ushaidi huu hapa...hiyo ni picha tu, lakini kuna sinema yake ya yote uliyonifanyia,....’nikampa mkononi, alipoona, aliduwaa, akachukua na kutaka kuvichana,huku akisema;

‘Nitakuua, unasikia, ninaapa nitakuua,...ni nani kakusaidia kuyafanya haya, haya,, ...nitakuua, usipoondoka kwenye hii nyumba, usiku wa leo nitahakikisha unakuwa maiti..’akaniambia huku akisita kuvichana vile nilivyompa, sasa akawa anaviangalia huku katoa macho, kama kaona kitu cha kutisha, mimi nikamwambia;

‘Mimi siogopi kufa, nilishajiandaa kufa, lakini bahati nzuri kuna mtu kaja kaniokoa, na yupo tayari kunisaidia hili jambo, ikibidi tutalipeleka mahakamani, lakini kwanza ni lazima nimfahamishe mama..’nikamwambia

‘Ni nani huyo aliyekusaidia?’ akaniuliza kwa hasira

‘Haina haja ya kumfahamu, ninachotaka ni hizo pesa kwa haraka, ili niondoke hapa kabla mama hajarudi,na ikitokea akaja na kunikuta hapa nyumbani nitamwambia yote na ushahidi wote nitamuonyesha...’nikamwambia

‘Ohoooo, ni nani huyu..aliyekusaidia kufanya huu uchafu, kumbe ndio kazi yako, eeh.’akawa anajiuliza

‘Unapoteza muda, nataka kuondoka...sikuwa na tabia chafu, kama unavyosema, wewe mwenyewe uliona kuwa ndiye uliyeniharibu,....’nikamwambia

‘Wewe ondoka, nitakutumia hizo pesa,kwasasa sina pesa za kukupa ...’akasema sasa akiwa anaongea sauti ya kawaida sio kama ile ya ulevi, naona alishahidi hatari.

‘Mimi sitoi mguu wangu kwenye hii nyumba mpaka niwe na hizo pesa..’nikasema

‘Shilingi ngapi,...?’ akauniuliza huku akinitolea macho ya kunitisha, lakini niliona ajabu, sikuwa naogopa tena, utafikiri kuna nguvu za ajabu ziliniingia.

‘Milioni kumi...’nikasema, na aliposikia hicho kiasi akashituka, karibu adondoke, na kuniangalia kwa macho ya chuki, akasema;

‘Ni nani huyo kakufundisha uchafu huo, milioni kumi, wewe unaota, pesa zote zote hizo unazitaka za nini wewe masikini?’ akaniuliza

‘Ni mtu wa usalama wa taifa, nilimwambia akanifundisha jinsi gani ya kuwakomoa watu kama nyie..hata kama ni masikini , lakini ni bora ya uamsikini wangu kuliko utajiri wa kinyama, wenye tabia ay unyanyasaji, ubakaji,....’nikamwambia

‘Unasema usalama wa taifa...ni nani huyo?’ akauliza

‘Utanipa hizo pesa au niendelee na shughuli zangu nimsubiri mama, aje, nimwambia hayo yote?’ nikamuuliza

Hebu subiri nifikirie...’akasema na pombe zote zikaisha, na mara akachukua simu na kuanza kuongea na watu wake kama watatu, kila mmoja alikuwa akimuomba pesa, milioni tatu tatu, na wa mwisho milioni moja, akawaambia wampe mdogo wake, atazileta hapo nyumba...’akasema

Mdogo wake, alikuwa hakai sana hapo nyumbani, yeye alikuwa na chumba chake nje ya nyumba kubwa, kwahiyo mara nyingi hafahamu yanayotendekea ndani, lakini mara nyingi ndiye anayemtuma mambo mengi, na wanaelewana sana na kaka yake.

Nikaenda chumbani kwangu nikajiandaa, na huku nikiwa na tahadhari, kama nilivyoambiwa na huyo mtu aliyenifundihs hayo yote, maana niliambiwa kuwa nikimwambia hivyo huyo baba anaweza akaniua, kwahiyo nikawa nina kisu kikali tayari kwa kujihami, hakupita muda nikasikia pikipiki nje,...

Nikachungulia nje, nikamuona mdogo wa huyo  baba akiwa na pikipiki, akaingia ndani nikasikia wakiongea na kaka yake kwa muda, baadaye nikasikia mlango wa chumbani kwangu ukigongwa, alikuwa huyo mdogo wa baba mbakaji, akaniita nitoke pale chumbani, nikatoka , akaniambia kuwa kaka yake kasema nichukue kila kitu changu , yeye atanichukue na pikipiki, na kunipeleka sehemu nitakapolala hadi kesho,..

‘Yeye yupo wapi?’ nikamuuliza

‘Yupo ndani kalala, kasema kila kitu kipo kwenye huu mfuko, akanipa mfuko, nikaangalia ndani na kukuta mabulungutu ya pesa, nikayahesabu moja moja, hadi yakatimia idadi , kwa yalivyofungwa, sikuweza kuhesabu moja moja, lakini kwa bunda moja moja, ambalo liliandikwa juu, milioni moja, nilifahamu kuwa zimefika milioni kumi, nikazichukua na kuziweka kwenye mkoba wangu wa safari, nilizifunga vizuru sana.

‘Twende, kaka kasema hana haja ya kuonana na wewe...’akaniambia,na mimi nikafanya kama alivyosema huyo mdogo wake, tukaondoka naye kwa pikipiki , hadi sehemu aliyoniambia kuwa nitalala hapo hadi kesho.

‘Mimi nakwenda kukata tiketi, kaka kaniambia unaondoka asubuhi, sijui kuna nini kinaendelea kati yenu, sitaki kufahamu, ila nakuonya ,kama kuna mtu anayekudanganya ujue umajipalia mkaa, hizo pesa unaweza usionje utamu wake,  kaka kakasirika kweli...’akaniambia

‘Mimi sijali kukasirika kwake, alichonifanyia ni dhaidi ya hizo pesa,..., nimeshamuambia kwa hivi sasa sijali kufa, ameshaniua, moyoni, kilichobakia hapa ni kiwiliwili tu,...’nikamwambia, na yeye akaondoka baada ya kuhakikisha nimekula, na pesa za matumizi.

‘Mimi sitakuja leo, tutaonana asubuhi sana usitoke nje,...’akaniambia

‘Mimi sitoki niende, wapi, kama nikitaka kutoka ujue, narudi huko kuonana na mama, mwenye nyumba’nikamwambia.

‘Wewe..usiende kuonana na shemji yangu,  kaka kasema usirudi huko kabisa, wala usije kuonana na huyo mama mwenye nyumba, mimi nakuamini, ndio maana nakuacha peke yako, la sivyo, niliambiwa nikuchunge hadi hapo utakapoondoka kesho, niahidi kuwa hutatoka nje, mpaka kesho’akaniambia.

‘Niende wapi, siendi mahali, ..nakusubiri wewe na mkileta ujanja nimeshampigia huyo mtu wa usalama wa taifa, ananifuatilia kila ninapokwenda...’nikamwambia

‘Ndio maana eeh,  kuna mtu nimemuona akitufuatilia nyuma, toka tunatoka kule nyumbani, na nahisi yupo hapo nje,..’akasema

‘Habari ndio hiyo...’nikamwambia na hapo hapo akampigia simu kaka yake,akimwambia kweli kuna mtu ametufuatilia kwa pikipiki, na huenda ni usalama wa taifa. Mimi sikujua kuwa kuna mtu alikuwa akitufuatilia, na siwezi kujua ni nani, labda ni yule jamaa aliyenipa hizo mbinu, ambaye kwenye zile pesa, alitaka nimpe nusu.

Moyoni nikasema huyu mtu simpi hata senti moja, kwa kazi gani aliyonifanyia...na mimi tamaa za pesa zikawa zimeniingia.

Alipoondoka huyo mdogo mtu, nikatoka pale ndani na kuangalia huku na kule, sikuona mtu, haraa nikachukua bego langu, kwa kupitia mlango wa nyuma, nikatoka,...na kuingia mitaani, nikachukua boda boda hadi sehemu nyingine, nikatafuta nyumba ya wageni nikalipia klwa siku moja, nikalala huko, na hiyo ilikuwa salama yangu. Nilikuja kupata taarifa kwa mtu anayenifahamu, ambaye aliniona nikifika pale, mtu huyo aliniambia kuwa kwenye ile nyumba, usiku kulitokea ujambazi,

Aliniambia kuwa kuna kundi la watu walifika wakinitafuta mimi,lakini waliponikosa, ikabidi wawapore watu pesa zao, ...aliniambia huyo jamaa ambaye nilikuja kukutana naye huko kijijini, baada ya siku nyingi.

Asubuni ya siku ile, niliwahi kituo cha Ubungo, nikampigia simu huyo mdogo wa baba, na akaniambia kuwa tikite zinakatwa hapo hapo siku hiyo, nikamwambia hana haja ya kuja kunifuata, nitakata tiketi mwenyewe,akaniambia yeye alipewa maagizo kuwa yeye ndiye atakata hiyo tiketi, nikamwambia nimeshakata tiketi tayari, na wala asisumbuke kuja kuniona, nikakata simu.

Ni kweli, nilinuna tiketi, ya usafiri wa kwenda huko kwetu, na mara kwa mara huyo mdogo wa baba, akawa ananipigia simu, lakini nikawa sipokei, hadi tunaondoka, sikuonana naye...’
Alipofika hapo akatulia na kusubiri, kama ataulizwa swali na mwenyekiti akamuuliza.

‘Huyo mtu aliyeweza kuchukua picha za tukio la hapo ndani, ulikuwa na mazoea naye kabla?’ akauliza mwenyekiti

‘Alikuwa mara kwa mara akija hapo kabla, lakini hakuwa akionana na mama wala baba, na kila mara akija alikuwa akiniuliza mambo ya hapo nyumbani, nilifahamu kuwa ni rafiki wa baba wa hiyo nyumba, kwani kuna siku nyingine walikuwa wakija wote, nakumbuka  kuna siku moja alikuja, akanituma kumchukulia maji, na niliporudi akawa ahyupo pale nilipomuacha, baadaye akatokea, nilimuona akbisa akitokea  chumba anacholala, huyo baba aliyenitenda hayo machafu.

‘Unafikiri alikwenda kufanya nini?’ akaulizwa

‘Kwa kipindi kile sikujua alichokwenda kufanya, lakini alikuja kuniambia kuwa kwenye ile nyumba,a likuwa kaweka vyombo vya kunasa matukio yote , hayo alikuja kuniambia baadaye wakati nipo kijijini...’akasema.

‘Kwahiyo mkajenga urafiki wa karibu kutokana na hilo tukio au ulikuwa unamfahamu toka siku nyingi?’ akaulizwa

‘Sikujenga urafiki naye, na ndio nilikuwa namfahamu kabla, ni mtu wa huko kijijini kwetu, urafiki ulikuwa ni kwenye pesa na hilo tukio, yeye kila mara alikuwa akija kijini na kudai pesa zake, nikawa simpi kama anavyotaka yeye, na ilifikia kipindi alitishia kuwa atanifanyaia kitu mbaya, kweli namuogopa, lakini moyo wangu ukajaa usugu fulani, sikujali kufa tena.

Baada ya kuondoka na zile milioni kumi, alinifundisha kuwa kila mara nitakuwa andai milioni mbili mbili, moja yake, kuna muda kija, anapandisha kiwango kuwa nimwambia huyo baba aitumie milioni tatu, hata tano,....kwani anasema alikuwa akidaiwa pesa na watu, nilimuuliza za nini, kwani yeye kafanya kazi gani, ndio akaniambia kuwa yeye kazi hiyo kaifanya muda mrefu, hadi kuhakikisha kuwa kaweka vyombo vya kunasa matukio yote kwenye hiyo nyumba.

‘Vyombo hivyo vinauzwa pesa nyingi, nataka nipate hizo pesa kuwalipa watu walioniazima hivyo vyombo, kwasababu asingeliweza kuvinunua, kwani vinauzwa pesa nyingi, kwahiyo alikuwa akiazima kwa muda fulani...’akasema

‘Je ulipofika huko kijijini ilikuwaje?’ akaulizwa

‘Sikuenda moja kwa moja kwa mama, nilikwenda kijiji cha jirani, huko nikajenga nyumba yangu nzuri, na ilipokamilika ndio nikaenda kumchukua mama...nilikaa huko mpaka nikajifungua, nikamlea mtoto wangu huku nikiendelea kudai pesa mwanzoni alikuwa akinitumia, baadaye akawa hafanyi hivyo, na siku zikawa zinakwenda, nikaona maisha yanakuwa magumu, kuhangaika na mtoto mgongoni, maji, kulima, na biashara, nikaona ni bora nije nimuone...aliyenifanya hivi,  nijue ni nini hatima ya mtoto.....’akasema huyo binti huku akimwangalia mume wangu kwa jicho baya, na mume wangu alikuwa kainama tu hainui kichwa.

‘Naona umeongea vya kutosha, ushahidi tulioutaka tumeupata je wakili mtetezi una swali dhidi ya huyo shahidi, ?’ akaulizwa.

‘Mteja wangu anakana yote aliyoyaongea huyo binti, je kama alifanyiwa hivyo, kwanini hakushitaki, hii inaonyesha kuwa huyo binti ana michezo yake ya namna hiyo, kuwarubuni wanaume ili aje kuwadai pesa, kwasababu mtu hivi hivi, asingeliweza kufanya jambo kubwa kama hilo, adai shilingi milioni kumi, mtoto wa kijijini...!’akasema wakili kwa mshangao.

‘Ushahidi ninao, kuna kanda alinipa huyo jamaa aliyenisaidia kama mnataka ninaweza kuwaonyesha..’akasema huyo binti, na wakili akanong’onezana na mteja wake, na wakili akasema;

‘Unasema ulipewa mimba, huyo mtoto yupo wapi?’ akaulizwa

‘Hilo lingelifuata baadaye, kwanza tulitaka kauli ya mlalamikiwa je, ni kweli hayo anayoyaongea huyo binti, kama si kweli, tutaonyesha hiyo kanda, ....ionyeshe tukio zima, ni ya aibu, lakini kwa ushaidi tutaionyesha,...kama anataka,..’akasema mwenyekiti.

‘Tunataka kumuona mtoto kwanza...’akasema wakili.

‘Kabla ya huyo mtoto, tunapenda kumuita docta, rafiki wa mlalamikaji, yeye atatoa ushahidi wa kitaalmu zaidi, ili kumuonyesha jamaa yako kuwa sisi tunamfahamu zaidi anavyojifahamu yaye...’akasema mwenyekiti.
Rafiki wa mume wangu alikuwa kama kashitukiziwa, na alionekana kubabaika, pale alipotajwa yeye kuwa anahitajika kutoa ushahidi.

‘Ndugu docta samahani kidogo, nafahamu hukutarajia hili, lakini inabidi uwajibike, wewe ni docta, na huyo binti unamfahamu kwasababu alikuwa jirani yako, tunataka ukweli wako, utuambia je wakati unafika hapo nyumbani kwao kwa jirani yako, uliyaonaje maisha ya hapo ?’ akaulizwa

‘Mh,h, yalikuwa ya kawaida, tu, sikuona tofauti yoyote...’akasema

‘Huyo mlalamikiwa hakuwahi kukuambia lolote kuhusu huyo binti?’ akaulizwa

‘Mhh, kama lipi, ..ndio kuna ya hapa na pale, kuwa huyo binti ana adabu mchapakazi, na mambo kama hayo, baadaye akasema ametoroka, lakini sio mambo kama alivyoyaongea huyo binti..’akasema

‘Hukuweza kuhisi lolote katika tabia za rafiki yako dhidi ya huyo binti?’ akaulizwa

‘Kwakweli hapana, kama yalikuwepo basi hayo aliyoyaelezea huyo binti yalifanyika kwa siri sana, mimi sikuwahi kuyashuhudia...’akasema

‘Huyu binti alikuwa anatibiwa kwenye hospitali yako mara kwa mara, kama sikosei, je aliwahi kuja kwako ukampima na kumwambia ana mimba?’ akaulizwa

Wakili wa mtetezi akalipinga hilo swali, na kusema doctari analazimishwa kusema jambo, hakupewa nafasi ya kuelezea yeye mwenyewe...’akasema

‘Niambia docta huyo binti aliwahi kuja kwako kutibiwa kabla hajatoweka hapa Dar?’ akaulizwa

‘Ni kweli kwa mara ya mwisho kuja kwangu, alifika akisema anajisikia vibaya, na alitaka kupima malaria, na alivyojielezea, kama docta nikahisi mbali zaidi, nikamwambia inabidi tumpime mkojo, damu na choo, na hakupinga, tukachukua vipimo vyake, na majibu yake, yakaonyesha kuwa ni mja mzito...’akasema.

‘Ulimwambia moja kwa moja, kuwa ana mimba...?’ akaulizwa

‘Mimi naifahamu hiyo familia, na sikutaka kuingilia ndani sana, nilipogundua kuwa ana mimba, nilitaka kuongea na mama, yaani mke wa hiyo familia, lakini nikaona nitakuwa nimeliingilia hili jambo kwa ndani sana, nikaamua kumhoji huyo binti kwa kadri ya kujua kama anafahamu ni nani aliyempa hiyo mimba..’akasema docta

‘Alikuwa kachanganyikiwa kwa siku ile hakuweza kusema kitu, na aliniomba sana, nisimwambia yoyote, mpaka atakapoweza kuliweka sawa,...nilimuelewa, hata hivyo, nilitaka niongee na rafiki yangu kuhusu hilo, na shughuli zikawa nyingi, nililikumbuka hilo baada ya siku mbili nikamuuliza rafikii yangu kuhusu binti, na rafiki yangu akaniambia kuwa huyo binti ni muhuni, katoroka, nikamuuliza kwanini katoroka yeye akasema, ni uhuni tu, hana lolote.
‘Hakuna lolote lilitokea ambalo limemfanya kutoroka, baada ya kupimwa, kuhusu afya yake, ?’ nikamuuliza

‘Achana naye, sitaki hata kumsikia, hata mke wangu hataki kusikia habari zake, usiongee lolote kumuhusu yeye kwa mke wangu,maana kakasirika sana, mtu anaondoka bila kuaga, kaniibia pesa zangu, tapeli mkubwa yule...’akaniambia

Mimi sikutaka kuliongea hilo la ujauzito, maana kama docta, unastahiki kuficha siri za mgonjwa,nikawa kimiya kuhusu hilo, lakini nilihisi kuna kitu zaidi ya hicho,lakini sikupenda kuyachimba sana mambo yao, kwani, nilikuwa na mambi yangu yanayonisumbua..’akasema

‘Kuna kipindi nilitaka kuongea na mke wa hiyo familia, nikaona na yeye hanipokei kama tlivyokuwa awali, baadaye nikaona hilo jambo halina nguvu sana, kwasababu huyo binti keshaondoka, na wenyewe waliokuwa nao hawalalamiki au kuulizia ulizia, nikaona yamekwisha, huenda wenyewe wamelimaliza kifamilia, sikuwahi kuliulizia tena...’akasema

‘Mnaona, ...huyo ni docta, ndiye aliyethibitisha kuwa huyo binti ana mimba..sasa niambie bado mteja wako anapinga,kuwa huyo binti hakuwa na mimba yake, au anataka ushahii gani mwingine?’ akaulizwa

‘Inawezekana alipewa mimba na mtu mwingine akaona sehemu ya kupatia pesa ni kwa mume wa familia, .ndio maana tunataka tumuone huyo mtoto wake.’akasema wakili.

‘Hebu mleteni huyo mtoto...’akasema mwenyekiti, na mama yangu akatoka nje, na aliporudi akawa kampakata mtoto, kila mmoja akawa na shauku ya kumwangalia huyo mtoto.

NB: Njia za muongo ni fupi, ukweli unazidi kubainishwa dhidi ya mume wa familia, je ni nini kitaendelea zaidi.

WAZO LA LEO: Usimtendee mtoto wa mwenzako ubaya, eti kwa vile sio mtoto wako, hiyo ni dhambi ambayo malipo yake ni hapa  hapa duniani, ulivyomtenda mtoto wa mwenzako ujue na wewe watoto wako watatendewa hivyo hivyo. Ukitaka kufanya lolote baya kwa mtoto wa mwenzako jiulize na mimi nikitendewa kwa mtoto wangu nitajisikiaje. Isiwe mkuki ni kwa nguruwe tu.


Ni mimi: emu-three

No comments :