Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, December 13, 2013

Mkuki ni kwa Nguruwe-47‘Ndugu mwenyekiti, sio kwamba nakataa kusema ukweli, unanifahami fika kuwa mimi sio mtu wa kusema uwongo, na wala siogopi kusema ukweli, lakini ninachotaka kukifanya hapa ni kumpa mwenzetu muda wa kutafakari, kwani huenda ana kitu anakiogopa, lakini ninamuhakikishia kuwa akisema ukweli, sisi tutamlinda, sisi hapa tupo kama familia, tunachohitajia ni kusawazisha haya mambo ili tuwe na msimamo wa kifamilia, .....’nikasema.

‘Mimi kama mwenyekiti ndiye ninayefahamu ni kitu gani kinakiwa kifanyike, sioni kwanini uingiwe na kigugumizi kusema ukweli, sisi tumeshampa muda wa kutosha huyo mume wako,na hata ukimpa siku nzima, inavyoonekana, ni kuwa hatageuza kauli yake,  kama na wewe unaogopa kusema ukweli kwasababu ni mume wako, basi wot e lenu ni moja, lakini sisi kama kikao bado tunahitaji jibu lako, ...umenisikia swali langu au nirudie...?’ akauliza mwenyekiti.

‘Nimelisikia swali lako mwenyekiti, ukweli upow azi, hii katiba sio katiba halali, hii katiba...’nikaanza kusema na mume wangu akanikatisha, na kusema;

‘Ina maana mke wangu unanisaliti, siamini, ni wapi ulisikia mke anakuwa kinyume na mume wake, ....hujui ni kosa kubwa, kumkana mume wako, tena mbele ya watu, hapo umetenda kinyume na maadili ya ndoa,umenikana mimi  mume wako, ili nionekanae muongo, hebu angalia hii katiba, ina makosa gani, hii katiba ni ile ile, kama kuna makosa yamejitokeza, nilishakuambai tutayaangalia na kuyamaliza kama familia, kwakweli umenivunja nguvu...’akasema

‘Mume wangu, katiba ipi, unayozungumzia, maana hii sio katiba yetu halali, sisi tunaitafuta katiba halali, ambayo mimi na wewe tulikubaliana, na wakili wetu akaipeleka kusijali,...hadi hapa tulipofikia inaonyesha hii katiba sio halali, na sisi tunajaribu kukupa muda, ili useme ukweli, na wewe hutaki kusema ukweli...’nikasema.

‘Ukweli ndio huo niliousema na katiba ninayoitambua mimi ni hii hapa, haya, kama kuna katiba nyingine unayoifahamu wewe nionyeshe, na iwe imetimia, kisheria,iko wapi hebu nionyesheni, mbona tunabishana kitu kidogo tu..’akasema.

‘Hilo tu, usiwe na shaka.....’nikasema huku nikitaka kuuchkua mkoba wangu, lakini kabla sijafanya lolote mwenyekiti akasema;

‘Mim ndiye mwenyekiti wa hiki kikao, heshimuni taratibu za kikao, .., na wewe mke wa familia yenu hiyo, huwezi kufanya anavyotaka mume wako,  mpaka nikuamuru mimi ufanye hivyo, na ningelipenda kutoa angalizo, ...’akasema mwenyekiti.

‘Sitaki tena kurudia, hili, nataka mfuate taratibu, mimi ndiye ninyeongoza hki kikao, na ninasema hivi, hili swala huko linapokwenda ni kubaya, maana kama muhusika mkuu anasama katiba halali ni hiyo ambayo mwanasheria kasema ni batili, na mwenza wake, ambaye ni mke wake waliyeshirikiana naye pia kasema katiba hiyo sio halali...yeye bado aanendelea kusema ndiyo katiba halali, mnataka sisi tufanye nini, ina maana  kitakachofuata hapo nisheria ichukue mkondo wake, ...’akasema mwenyekiti.

‘Ndugu mume wa  familia, unafahamu hatima ya haya yote, kuwa sasa hivi tutashindwa kufanya lolote kwasababu kile tunachokitaka kituongoze, kama ulivyotaka, kinaonekana kina mashaka,....na kwahiyo sisi tunashidnwa tufuate lipi, kwani mwanzoni wewe mwenyewe ulituzuia, ukasema nyie mna mkataba  wenu, katiba yenu inayowaongoza, ..lakini katiba unayoiamini wewe,  imeonekana, ina walakini, ina utata,....sasa unataka sisi tufanye nini, tunakuuliza maana muda unakwenda?’ akauliza mwenyekiti.

‘Ndugu mwenyekiti, mimi  ni nani?’ akauliza

‘Wewe ni mmoja wa wajumbe kwenye kikao hiki, au unauliza kuwa wewe ni nani kisifa ya ndoa, kama ni hivyo wewe ni mume, wa mkeo....’akasema mwenyekiti.

‘Mimi ni mume wa familia tunayoizungumzia hi leo, na wote wamfeika hapa kwa ajili yah ii familia, . Mimi kama mume ninaheshima yangu, na moja ya heshima, ni kuwa kiongozi wa hii familia, na kama ni kiongozi, ninabeba majukumu yote ya familia, ...na ninachosema ndio msingi, wa familia,....kama hamuniamini mimi, mtamuaminini nani....’akasema.

‘Sikiliza mume wa familia, ...hapa ni kwenye kikao, na mnapoitisha kikao, kuna viongozi wanaokiongoza, wewe kama ni mume wa familia, ni kwako kwenye familia yako, hapa unakuwa mjumbe wa kikao, na unatakiwa kufuata taratibu za kikao,....kikao kinakutaka useme ukweli, ukisema kinyume chake, kikao kitakuhoji, ili kijue ni kwanini, na hicho ndicho kitafuta, tutahitajai kujua ni kwanini, mkafana hivyo, ni kwanini kukawa na katiba, au mikataba miwili, ...’akasema mwenyekiti.

‘Kwahiyo mnataka nisema mnayotaka nyie, sio ukweli wenyewe, kama mnataak ukweli ndio huo,nimeshasema kama mume wa familia kuwa katiba ni hii hapa, kama kuna katiba nyingine itoeni,...mbona hiyo katiba nyingine haitolewi,....’akasema.

‘Kabla hatujafanya hivyo, unavyotaka wewe, tunarudia maswali yetu kwako, ili tuwekane sawa, je kama ikitolewa hiyo katiba ambayo ndiyo halali, ikathibitishwa hivyo, kuwa ndio katiba halali, upo tayari kuwajibika nayo,kwani kwanza utakuwa umesema uwongo, pili umevunja sheria, tatu, umekaidi kikao ,hapo hatujaingia kwenye makosa yaliyosababisha kukiitisha hiki kikao.....je upo tayari kuwajibika?’akauliza mwenyekiti.

‘Hiyo katiba nyingine ipo wapi, ..hilo ndilo la msingi, kwanini mnapoteza muda, kama ipo,...nasema , naapa, nipo tayari kuwajibika nayo, maana mimi ninavyofahamu hakuna katiba nyingine zaidi ya hii hapa..’akasema na mdogo wake aliyekuwa kainama akainua kichwa na kumuangalia kaka yake kwa macho ya mshangao, nahisi kama angelikuwa karibu angemtuliza kaka yake asiendelee kuongea.

‘Unaona eeh, dalili za watu kama hawo zilivyo...mke wa familia, umesikia mwenyewe,..sasa usisite kujibu maswali yetu ukimtegemea mume wako, jibu ukijitegemea mwenyewe, mwenzako yupo kivyake,....’akasema mwenyekiti.

‘Ndugu mwenyekiti, mimi naona tuendelee, kwani nahisi kuna tatizo, sizani kama mume niliyemfahamu .....angaliweza kufanya hivi, ..naona kuna tatizo....mimi nilitarajia mume wangu ungekiri kosa, ili tukayaweka haya mambo sawa, lakini naona una ajenda ya siri, sikuelewi’nikasema.

‘Kuna tatizo gani wewe, kwanini unaogopa katiba hii isifanye kazi yake, ..eeh, wewe mwenyewe umekimbilia kwa wazazi wako ukasema mume wangu sio mkweli, kafanya hivi kafanya vile, sasa tumefika hapa, katiba ipo uwanjani,  unaanza kulalamika, katiba hii hapa, acha ifanye kazi yake...’akasema na mimi nikamwangalia kwa mashaka, nikasema.

‘Upo tayari katiba halali ifanye kazi yake?’ nikamuuliza.

‘Nipo tayari,...katiba hii hapa ifanye kazi yake...’akasema

‘Ndugu mwenyekiti, mume wangu, keshakubali kuwa katiba halali ifanye kazi yake, naomba tuingie kipengele cha pili, hili litajiweka sawa lenyewe, katiba anayoisema yeye, hiyo aliyo nayo sio halali, imeshathibitishwa hivyo, mbele ya kikao, labda kama anataka tuthibitishe kisheria....’nikasema.

‘Namuuliza tena muhusika, umekiri mwenyewe kuwa katiba halali ikipatikana, ndiyo itakayoongoza yote hayo yatakayofuata,ndivyo hivyo ....?’ akauliza mwenyekiti

‘Msinitege,..ndugu mwenyekiti mimi naona hapo mnanitega, katiba halali ninayoitambua mimi ni hii hapa, sio nyingineyo, kwanza nyie muikubali hii katiba, halafu hayo mengine yatafuata...’akasema

‘Ni nani ataweza kuikubali katiba iliyogushiwa wewe...’nikasema kwa ukali

‘Ni nani kagushi hii katiba,....?’ nay eye akauliza kwa hasira

‘Unataka nikuthibitishie hilo, kuwa katiba hii imegushiwa..?’ nikamuuliza kwa hasira

‘Thibitisha, na ukithibitisha, mimi nitakubali kuwa ni mwongo, na nipo tayari kuendelea na hiyo Katiba mnayodai nyie kuwa ndiyo halali...thibitisha’akasema kwa kujiamini, na mimi nikamwangalia kwa mashaka, na kusema;

‘Sawa mwenyekiti endelea na kikao, nipo tayari kwa lolote lile, nimeamini kuwa mume wangu ana lake jambo, ...’nikasema na mweneykiti akasema

‘Mjumbe anataka tuthibitishe kuwa katiba hiyo aliyo nayo sio halali, na kwahiyo tunaingia kwenye kipengele cha kisheria,..hatukutaka tufikie huko, lakini kwa vile mwenzetu kashikilia msimamo wake, basi inabidi tumpe haki yake, kabla hatujaangalia ni jinsi gani swala hili tutakavyolipeleka kwenye nyimbo vya sheria ninataka kumuuliza tena mume wa familia...’akasema mwenyekiti.

‘Kwanini unasema hivyo, ni nani kasema tulipekele hili swala  kwenye vyombo vya sheria, ...wakati katiba ipo hapa,...mimi sijasema tushitakiane,mimi nimetaka ushahidi, na kuonyeshwa hiyo katiba nyingine mnayoikubali nyie...’akasema mume wangu.

‘Umesema kuwa hiyo katiba uliyo nayo ni halali, na hutambui katiba nyingine, mke wako anasema hiyo katiba uliyo nayo sio halali, imetengenezwa, wakili wenu kabainisha wazi kuwa hiyo katiba siyo ile aliyoisajili yeye, ina maana hapo unagusa sheria,, ...hivyo vyote vipo kisheria, na vimesajiliwa, je tutajuaje kipi ni kipi,kama hatutakwenda kwenye vyombo vya sheria, wakathibitisha hilo..’akasema mwenyekiti.

‘Vyombo vipi vya sheria zaidi yangu mimi na mke wangu ambao ndio tulioitengeneza hiyo katiba...hii katiba ipo kwa msajili, ndiyo sheria, mimi na mke wangu, ndio wahusika, tupo hapa, mnachptaka zaidi ni nini....’akasema

‘Kwahiyo hiyo katiba unayodai wewe ndiyo iliyopo kwa msajili, kumbe tusipoteze muda, ngoja tumuulize huyo mdhamini wa serikali, swali ni kuwa je tukimuuliza akisema kuwa katiba hiyo sio halali, ipo katiba nyingine utasemaje?’ akaulizwa

‘Labda muwe mume-mnunua....’akasema

‘Unasema nini?’ akauliza mwenyekiti kwa hamaki

‘Nasema hivi huko kwa msajili ipo nakala hii, huo ndio ukweli, hakuna katiba nyingine zaidi ya hii, kama atakataa ujue kuna jambo limefanyika..’akasema.

‘Jambo gani hebu liweke wazi, maana umetamka neno ambalo wengi wamelisikia, ni kauli ya dharau, mimi mwenyekiti sitaweza kuivumilia hiyo kauli, nataka maelezo kuhusu hiyo kauli uliyoitoa, vinginveyo  uifute hiyo kauli yako,...’akasema mwenyekiti.

‘Samahani mwenyekiti, kauli hiyo ilinitoka kwa bahati mbaya, sio dhamira yangu, nimeifuta,unafahamu hapa nimechanganyikiwa, najiona kama nipo peke yangu wote mnanisakama mimi...’akasema kwa kusikitika.

‘Hakuna anayekusakama hapa, acha kauli za kienyeji, hapa tupo watu wazima waliosoma, wanaojua sheria, usiseme kauli za kizalili, jitetee kisheria kama mume wa familia, kama unashindwa kujitetea kama mume wa familia, utakuwa hujui majukumu yako kama mume, wewe kila mara unatamba kwa neno hilo, `mimi mume, mimi mume,..’sasa thibitisha uume wako, kwa hoja, zenye mshiko na hapa tupo kwenye sheria..’akasema mwenyekiti.

‘Sijashindwa mwenyekiti , mimi ni mume wa familia,nipo tayari kwa lolote lile, tuendelee na kikao..’akasema

‘Haya tuendeee, mumemsikia mwenyewe akisema, kuwa yupo tayari kuwajibika kama katiba halali,itapatikana, kama katiba aliyo nayo itathibitishwa kuwa ni batili, ...sasa mimi naanza kazi yangu, ya kutaka uthibitisho, kwani katiba zote hizi kama ni halali, zitakuwa zimesajiliwa kwa msajili, na kama wao watakuwa na hii katiba, basi kisheria itabidi tuifuate, na kama wana katiba nyingine, itathibitisha kuwa hii katiba ni batili, na kwahiyo kuna uanganyifu umefanyika, kama kuna udanganyifu umefanyika, tunahitaji maelezo ya kina, kabla sheria haijachukua mkondo wake.....’akasema mwenyekiti na mume wangu akatulia akimwangalai mwenyekiti kuwa atasema nini zaidi.

‘Nikuulize kwanza mke wa familia, je wewe umethibitisha kuwa katiba hiyo aliyoshika mume wako ni batili, sio katiba halali, ?’ akauliza mwenyekiti

‘Ndio mwenyekiti, nimethibitisha hilo...’nikasema

‘Kwa vigezo gani?’ akauliza

‘Kwanza, kuna hizo alama zangu nilizokuwa nimeweka, kwenye hii katiba hazipo, ina maana hii ni katiba iliyotengezwa kivingine, pili kwa kupitia mwanasheria wetu kathibitisha kuwa hii katiba sio ile tuliyompa yeye kwenda kuisajili, na tatu yale yaliyoandikwa ndani yamebadilishwa, hayfanani kabisa na ile katiba halali, yamebadilishwa kiujanja ili kuleta maana nyingine tofauti na ile tuliyokubaliana...’nikasema

‘Ahsante, sasa naomba mnipe muda kidogo niweke mambo sawa, sio lazima twende kwa msajili, uzuri wenzetu nao wamejipanga wana vyombo vya kisasa,  ila ikibidi tufanye hivyo,tutakwenda. Kwanza nataka kumpa nafasi ndugu yetu, kwa ushahidi mwingine, ...kama atazidi kukaidi basi hili tatizo tutalipeleka kwenye vyombo vya sheria ili wathbitishe wenyewe, na wao watajua ni nini cha kufanya...ili haki itendeke’akasema mwenyekiti huku akifungua kumputa yake aina ya lap top, yake akafungua sehemu anayoitaka, halafu akachukua simu, na kupiga namba....

‘Siku hizi mambo ya mitandao yapo mbele, dunia sasa imekuwa ni kijiji kimoja, tunaweza kuwashirikisha wajumbe wengine japokuwa hawapo kwenye hiki kikao, ..sasa hivi tunakwenda chumba cha msajili wa katiba, yeye atakuwa nasi, ...’akasema na mara simu yake ikawa hewani na kwenye lap top yake kukatokea sura ya mtu, akiwa kakaa kwenye meza, kwenye ofisi yake.

‘Ndugu muheshimiwa, mimi ni Malimoto, ...nikiwa na wajumbe kwenye kikao, ni kikao halali cha kifamilia, kikao hiki kinawajumuisha wanafamilia ambao kwa nia moja walikukabidhi mkataba wao, ambao ni katiba yao katika mambo yao ya kifamilia na makampuni yao,..natambua kuwa hilo ni jambo la siri la familia hiyo , lakini kutokana na sababu kubwa, kuna kutokuelewana kwa wanafamilia hawa waliopo kwenye kikao hiki, nakuonyesha, uwaone, na wao wajithibitishe..’akasema mwenyekiti na kuisogeza hiyo laptop, kuelekeza kwetu, halafu akawa anaionyesha kwa mtu mmoja mmoja, mimi na mume wangu na wakili wetu, tukatakiwa kujithibitisha kuwa tumekubali hilo lifanyike

Tukajithibitisha kuwa tupo tayari kwa hilo....na mwenyekiti akaendelea kusema;

‘Kutokana na matatizo hayo wanahitajia kutumia katiba yao halali kuhukumiana, kisheria, na sisi tupo kama wanafamilia kuhakikisha kuwa haki inatendeka, tunahitaji swala hilo limalizwe kifamilia, na kama kutakuwa na kutokuelewana zaidi tutalifikisha hilo swala mahakamani...’akasema mwenyekiti.

‘Lakini hilo ni swala ni la kisheria, mkataba wao umesajiliwa kisheria, ningeliwashauri kuwa kama kuna utata, ni vyema mkaufikisha kunapohusika, kuliko kulifanya kifamilia, inabidi wahusika waende mahakamani...’akasema huyo msajili.

‘Hilo litafuata baadaye, kama hatutaelewana, tunachotaka kuthibitisha kwasasa, ni kuhusu katiba uliyo nayo kwenye ofisi yako, tunahitajia kuiona, ili kuwekana sawa,...’akasema mwenyekiti, na huyo msajili akaonekana kuinuka kwenye meza yake, akachukua ufungua, huku akiuliza;

‘Je kuna tatizo lolote kuhusu katiba hiyo?’ akauliza

‘Tatizo lipo kidogo, lakini kama wanafamilia tunaweza kulisahihisha, ni tatizo kuwa kuna kutokuamini kuhusu nakala ya katiba tuliyo nayo sisi, je ndiyo hiyo uliyo nayo wewe,,...’akasema mwenyekiti na huyo msajili akasema

‘Mhh, ndio maana nilitaka swala hilo waje mawakili wenu, niliwaagiza wafanye hivyo, lakini hakuna aliyefiak tena, kwani kuna utata ulijitokeza hapa kwetu....na utata huo umesababisha hata mwenzetu mmoja kuwajibika, yeye ndiye alikuwa kwenye kitengo , ni baada ya malalamiko kwa watu, na sisi tukafanya uchunguzi na kugundulikana kuwa kulikuwa ma mapungufu ya hapa na pale,...na ndio maana kupitia kwa mawakili wote waliowahi kuleta mikataba yao, katiba zao, tuliwaomba waje hapa kuthibitisha mikataba yao tena, kama kuna mashaka...’akasema

‘Ndio kusema kuwa wakili wenu analitambua hilo, ila tulishangaa, siku ambayo tuliwaita mawakili wote wenye mikataba yao hapa,kwa familia hiyo walifika mawakili wawili, kinyume na ilivyokuwa awali, mume wa familia alituma wakili mwingine akimwakilisha yeye,kitu ambacho hakikuwepo awali,...huyo wakili,akasema katumwa kuthibitisha, kuwa mkataba uliopo ni huo huo,, cha ajabu zaidi, yeye alikuja na nakala tofauti na tuliyokuwa nayo sisi, ....

Nakala aliyokuwa nayo sio ambayo imesajiliwa hapa, nakala zote zikiletwa hapa siku hizi tunaziscan, na kuziweka kwenye mitandao, kwahiyo hata kama mtu atafanya mbinu na kuiba nakala, zilizopo hapa, lazima tutakuja kuligundua hilo,...’akasema

Wakili aliyetumwa na mume wa familia hii, alikuja na nakala, ambayo ilikuwa sawa na nakala iliyokuwa kwenye kabati letu, lakini tulikuja kugundua kuwa hizo nakala sio zile tulizoscani, na kuziweka kwenye mtandao kuna marekebisho yaliyofanyika. Kwahiyo tukawaambia mawakili hawo kama kuna marekebisho yamefanyika, basi waende wakaelewane, na walete maombi upya , na ndipo uchunguzi ukafanyika, kwanini ilitokea hivyo hayo ni mambo ya ndani hamuyahitajiii kuyafahamu, lakini mwenzetu kawajibishwa kisheria kwa makosa hayo .....’akasema

‘Lakini kwa ajili ya kuweka mambo sawa, na kwa vile ule mikataba sahihi, umeshatengenezewa nakala yake, na muhusika,mtu wetu  akakiri kuhusika kwa namna moja au nyingine, kwa shinikizo la mtu aliyemfanyia mlungula (blackmail), basi kila kitu kimewekwa sawa, na katiba halali nakala yake tunayo hapa, ....’akasema

‘Una maana gani kusema katiba halali?’ akauliza mwenyekiti

‘Kama nilivyosema awali, kuna ubadhirifu ulitokea, hilo ni swala la ndani ...kwenye kabati kulionekana nakala ambyo sio sahihi, lakini katiba halali iliyopo kwenye mtandao, haikuwa sawa na katiba iliyokuwepo kwenye kabati,..hayo maelezo yanatosha maana hilo ni swala la ndani, siwezi kuwaambia zaidi ya hapo kama kuna tatizo, basi mje mliwakilishe kisheria...’akasema.

‘Hii hapa ndio nakala halisi,....’akasema huku akiifungua na kwenye mtandao kukaonekana nakala iliyohifadhiwa kwenye mtandao na wakili wetu akasogea kwenye lap topo kuiangalia hiyo nakala, akawa anafungua ukurasa moja baada ya mwingine...na wakili wetu aliporizika akasema

‘Hiyo ndiyo yenyewe, ...hebu sogeza ukurasa wa hiyo nakala uliyo nayo mkononi mbele nione vizuri...’akasema na huyo msajili akafanya hivyo kama alivyooambwa, na kweli kwenye ule ukurasa kulionekana muhuri uliojificha kama ule uliopo kwenye noti, za pesa ukionyesha nembo ya wakili wetu wa familia.

Na wakili wetu akasema; `Huo ndio mkataba ninaoutambua mimi....'akasema na mwenyekiti wetu akamuuliza huyo msajili

‘Je hiyo nakala bandia ipo wapi? akauliza mwenyekiti

‘Hiyo nakala bandia ipo kwenye mikono ya sheria, tunalifuatilia hilo swala, na tulimuhitajia wakili aliyeletwa na mume, ajitokeze kuleta madai  yake, lakini kama mlivyosikia  , keshafariki, na kama mume, au familia, zina utata, kuhusu hilo, tunawomba wafike, kwetu na kuelezea utata huo...na kama kuna mtu ana nakala iliyo taofauti na sisi, tungelifurahi kumuona, na kutuleeta hiyo nakala...’akasema

‘Sawa tumekusikia, muheshimiwa...’akasema mwenyekiti.

‘Je nakala mliyo nayo, hapo ni tofauti na hii?’ akauliza msajili

‘Muheshimiwa tunaomba utupe muda kidogo, tuliongee, kama kuna lolote jingine tutakutafuta, samahani kwa kuchukua muda wako, ...’akasema mwenyekiti, na wakati huo mume wangu alikuwa anasogea huku akiwa kashikilia ile nakala yake kama vile anataka kumuonyesha huyo msajili, lakini rafiki yake akamuona na kumsogelea, na kumvuta pembeni na kumnong’oneza , mimi nilikuwa karibu nao, nilimsikia akimwambia rafiki yake;

‘Usionyeshe kabisa hiyo nakala yako, utafungwa, hiyo nakala yako imeonekana ni bandia, kwahiyo kuna ukiuwaji wa sheria, na wote waliohusika, wataweza kushitakiwa, ...achana na hiyo nakala yako, ikibidi uiharibu kabisa, huo ushahidi... kilichobakia sasa ni kukubali  kuwa kuna makosa yalifanyika, na ukubali mkataba wenu wa awali ufanye kazi yake, huna jinsi, ...’akambia rafiki yake, na mume wangu akatikisa kichwa kama kuukataa....alionekana hajakubali.

Mimi nikawa bado nipo naangalia yale yanayoendelea kati ya wakili wetu wa familia na msajili, walikuwa bado wakionyeshana huo mkataba uliopo huko kwa msajili, na baadaye mwenyekiti akasema;

‘Haya zoezi hili limekamilika,na ushahidi alioutaka mwenzetu umekamilika, sasa turejee kwenye viti vyetu, tuingie sehemu inayofuata, na huku tukijiweka sawa, nataka mume wa familia atueleze ukweli, kikao kinahitaji maelezo yake ya ukweli, kwa jinsi ilivyotokea, hadi kupatikana hiyo katiba iliyogushiwa ...hii sasa ni amri, tunataka ukweli, wenye mshiko, vinginevyo, baba, itabidi swala hili liende mbali zaidi,...’akasema mwenyekiti, akiweka vitu vyake sawa tayari kwa kuendelea na kikao.

Mume wangu alikuwa ameshafika kwenye kiti chake, na kukaa, alutulia akiwa hana raha, na baadaye akageuka kuangalia kulia na kushoto kwake, na sisi tukawa tunamuangalia kwa mashaka, kwa jinsi anavyo angalia huku na kule, halaf akauliza;

‘Mdogo wangu yupo wapi?’ akauliza na sisi ndio tukagundua kuwa mdogo wake hayupo, haonekani ndani ya chumba cha kikao, na hakuna aliyemuona wakati natoka kwani kila mmoja alikuwa akishangaa katoka muda gani.

‘Huyu mtu wenu kaenda wapi,?’ akauliza mwenyekiti na yeye akiangalia huku na kule

NB: Haya tunaishia hapo kwa leo, sehemu ijayo tutaingia sehemu nyingine ya kikao hicho, cha kifamilia,  je ni nini kitafuata.


WAZO LA LEO: Uwongo ni tabia chafu, ukiwa nayo, utagundulikana tu, mwenye tabia hiyo ni sawa na mtu mchafu anayetoa harufu mbaya, akikaa na watu watamgundua na hatakuwa na maisha ya raha. Tuepuke tabia hiyo, ili tuwe na masiha ya amani na raha.
Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

[url=http://buy-sildenafil.top/]buy sildenafil online[/url] [url=http://order-viagra-online.top/]viagra[/url] [url=http://cleocin-gel.in.net/]cleocin cream[/url] [url=http://buy-baclofen.cricket/]buy baclofen[/url] [url=http://buy-rimonabant.top/]rimonabant[/url]