Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, November 27, 2013

Mkuki ni kwa Nguruwe-36


Nilishaanza kumshuku shemeji yangu kuwa anafahamu mengi, na siku ya leo niliona ndio siku pekee ninayoweza kumbana , na kusema ukweli wote, lakini sikutaka niongee naye peke yangu, nilishaongea na watu wa usalama, ambao nafahamiana nao,na niishawaeleza ni nini lengo langu, na nikaona niwaite watu waja wanisaidie, ...

Kwa hatu iliyofika, huruma ilikuwa haipo tena, nilishaona kuwa hawa watu nikawahurumia, wataniumiza, wao hawanijali tena, wanachojali ni masilahi yao ....ndio maana nikaamua kuwaita watu wa usalama.

Wakati nampigia simu, niliona kama shemeji yangu alitaka kuniambia jambo, kuwa yupo tayari kuniambia kila kitu, lakini nilishamfahamu kuwa anaweza akapoteza muda tu na asiniambie kitu, na hata kile nilichotaka kukipata nisikipate, na wakati huo nilishamuweka huyo askari kanzu hewani, sikutaka kurudi nyuma, nikamwambia aje...

Endelea na kisa chetu

*********
Shemeji yangu huyo alipooa nafanya kweli akageuka huku na kule akitaka kukimbia, na kabla hajafanya hivyo nikamuonyeshea ishara ya kumuonya..., akatulia nikamaliza kuongea na huyo ofisa upelelezi, ambaye nilishamgusia kuhusu hayo mambo yanayoendelea katika nyumba yangu  na yeye akaahidi kuwa atalifuatilia hilo tatizo kwa karibu.

‘Shemeji ...ina maana unataka sisi tufungwe?’ akauliza shemeji yangu huyo.

‘Ukweli wako ndio utakaokusaidia wewe na kaka yako, nilishawapa muda wa kutosha, sasa wakati umefika, kama kweli  unataka kumuokoa kaka yako na wewe mwenyewe sema ukweli, niambia kila kitu nitakachokuuliza kabla huyo jamaa hajafika..’nikamwambia.

‘Lakini shemeji mimi nitakuambia nini, nimeshakuambia kila kitu nianchohitajia kukuambia, mengine ukitaka ni bora ukamuuliza kaka..’akasema.

‘Sawa ...basi kama umeshaniambia kila kitu ngoja hawo polisi wafike, ....tutajua ukweli, maana wewe uanfikiri natania, ..’nikasema na mara mlinzi akaja, na kutuambia kuwa kuna jamaa wamefika wanataka kuonana na mimi.

‘Ni watu gani?’ nikauliza.

‘Wanasema wao ni watu wausalama, wamenionyesha vitambulisho vyao...ni kweli ni watu wa usalama’akasema huyo mlinzi, na hapo shemeji yangu ambaye alifikiria nafanya utani, akasimama na kushika kichwa, na mimi nikamwambia huyo mlinzi.

‘Waambia waje huku bustanini’nikasema huku nikiweka ile mashine yangu vizuri, sikutaka mazungumzo hayo yaishie hewani.

‘Shemeji umafanya nini sasa, mimi nilijua unatania tu...ina maana unataka kaka afungwe,...aeri haat mimi ningelifungwa, lakini mume wako ni mgonjwa’akawa aansema huku anataak kulia.

‘Muda wa utani umekwisha ndugu zanguni, , maana mimi wakati nawaonea huruma nyie mnafanya kweli..hamnionei huruma, sasa ngoja na mimi nifanye kweli tuone mwisho wake utafikiawapi, nina ushahidi wa kutosha wa kukuweka wewe na kaka yako ndani ..’nikasema.

‘Ina maana hata kaka, mumeo humpendi tena,...unataka umweke ndani hujali kuwa anaumwa, siamini shemeji?’ akauliza.

‘Wewe ndio utakwenda ndani kuisaidia polisi, ....kaka yako atasubiri hadi hapo akipona, mjue mna makosa mengi ,kwanza kwa kuniibia, pili kwa kugushhi mikataba halali, tatu kwa mauaji ya Makabrsha , nne kwa wizi, na mengine...’nikasema na mara hawo jamaa wakafika mmoja akiwa na pingu tayari mkononi kuonyesha yupo kazini.

‘Shemeji, mimi sitaki kwenda jela, kwasababu sihusiki kabisa, yote niliyafanya kwasababu ya kaka..kwasababu ya kumsaidia kaka, angalia ali yake ilivyo, ...muhurumie kaka, shemeji...’akasema huku akiniangalia kwa macho ya huruma, lakini mimi nikaangalia pembeni, sikutaka kurudi nyuma kwa maamuzi yangu hayo, nilitaka nijue ukweli, na hakuna njia nyingine iliyobakia.

`Ukitaka usalama wako ongea ukweli, maana mengi yanafahamika, wao watakachofanya ni kupima ukweli wako,...sema yote unayoyafahamu, ukipindisha na kusema uwongo, jela inanukia, jela sio mchezo, isikie hivyo hivyo, mimi nimeionja na niliwekwa sehemu wanayosema ni nzuri, lakini taabu niliyipata siwezi hata kusimulia....’nikasema na wale jamaa wakaja wakajitambulisha na kuonyesha vitambulisho vyao.

‘Mimi nimewaita hapa kwasababu ya upotevu wa mali zangu , zikiwemo mikataba halali, na silaha yangu...’nikaanza kuongea , japokuwa nilishaongea naye, lakini sikutaka shemeji yangu afahamu kuwa nawafahamu hawo watu.

‘Una maana ile silaha iliyotambulikana kuwa ndiyo iliyomuua Makabrasha?’ akauliza huyo ofisa usalama.

‘Ndio ..’nikasema.

‘Kwahiyo tunaweza sasa kumpata muuaji ..’akasema huyo mwingine, na mimi nikageuka kumtambuslisha shemeji yangu ambaye alikuwa kaduwaa haamini kinachotokea.

‘Huyu hapa ni shemeji yangu, na anaweza kutusaidia kwa hilo..’nikasema na shemeji yangu akaniangalia kama haniamini kuwa mimi ningeliweza kufanya hivyo hivyo, alibakia kaduwaa, akanywea na kukaa kimiya na nilioana jicho la chuki, ...jicho ambalo hujionyesha pale mtu anapoona kasalitiwa, na hana cha kufanya.

‘Haya ndugu yetu, tuambie ukweli ili tusipoteze muda, maana mengi tunayafahamu....’

‘Mimi nilishamwambia shemeji yale ninayoyafahamu, mengine anayafahamu kaka yangu’akasema.

‘Sikiliza sisi hatuja kupoteza muda, kama huongei ukweli sisi tunakubeba, utakwenda kuongeala huko mbele, unafahamu ukifika huko utaongea kila kitu, hapa tunamstahi shemeji yako tu,..’akaambiwa.

‘Sasa mnataka niseme nini?’ akauliza huku akijaribu kujitutumua, naona alishaniona sio mtu wake tena, alishaniona mimi ni msaliti wake.

‘Kwanza kuna mkataba wa shemeji yako uliibiwa, je upo wapi?’ akaulizwa

‘Mimi sijaiba mkataba,...muulizeni kaka....’akasema.

‘Ok, shemeji tunaomba tuondoke na huyu mtu, sisi tunakuhakikishia tukifika naye huko atataja kila kitu, sisi tulishamchunguza nyendo zake kwa kirefu, tuna ushahidi wote kuwa anahusika kwa kiasi kikubwa sana,kuna mambo mengi anayafahamu,na ameyafanya sasa hatuna muda wa kupoteza tena ...’akasema na mimi nikamuangalia shemeji yangu huyo ambaye alikuwa kama kamwangiwa maji. Alikuwa hataki hata kuniangalia, nahisi chuki dhidi yangu zilikuwa kubwa, lakini sikuwa na njia nyingine.

‘Shemeji hiyo ndio nafasi yako ya mwisho, kama unamjali kaka yako sema ukweli, kama unaona kukaa kimiya ndio kutamsaidia kaka yako haya, mimi nitawaruhusu muondoke nao, na unafahamu ni kitu gani kitakukuta huko mbele, unamkumbuka yule rafiki yako aliyejifanya anaweza kuvumilia mateso ya huko, alikuambia nini kilichompata,....kama wewe unajiamini zaidi yake niwaruhusu muondoke ....’nikasema na  yeye kwanza akaniangalia kwa jicho lenye chuki, halafu akasema.

‘Haya  mimi nitawaambia ukweli lakini naombeni mumuache kaka yangu , kaka yangu anaumwa, na mengi aliyafanya bila kujitambua..’akasema

‘Hiyo sio kazi yako, sisi tunalifahamu hilo ndio maana tunakuuliza wewe, hatujakwenda kumuliza kaka yako kwasababu anaumwa,...kama tungelikuwa hatulitambui hilo, kaka yako sasa hivi angelikuwa jela. Sasa  kwa vile wewe ni mzima huna matatizo unahitajika  utuambie ukweli, kwani wote lenu ni moja....’akaambiwa, na akatulia kimiya kwa muda kama anawaza, halafu akasema;

‘Haya ulizenu maswali yenu nitawajibu, kwa kile ninachokifahamu...’akasema

‘Swali la kwanza, tuambie mkataba wa wanandoa hawa ulioibiwa upo wapi?’ akaulizwa.

‘Mimi sijui huo mkataba ulioibiwa ni upi, ...’akasema

‘Wewe unafahamu mikataba mingapi?’ akaulizwa

‘Mimi nilishaiona mikataba zaidi ya mmoja, sasa sijui upi ni upi?’ akasema.

‘Kwa hivi sasa wewe una mikataba mingapi?’ akaulizwa

‘Sina hata mmoja....’akasema

‘Uliipeleka wapi?’ akaulizwa

‘Nilimrudishia mwenyewe....’akasema

‘Kulikuwa na mkataba uliokuwa nao wewe , ambao haujaonekana, mkataba aliokuwa nao kaka yako ni mkataba mpya, tunahitajia ule mkataba wa zamani,ambao tuna ushahidi kuwa unao wewe...’akasema huyo ofisa.

‘Nimesema nimeshaurudisha....’akasema na kukatisha

‘Sema ukweli, ilikuwaje mpaka ukaupata huo mkataba ulio nao wewe, huo mkataba wa zamani....ina maana uliuiba au sio?’ akaulizwa.

‘Kaka ndiye alinituma niuchukue...mimi sijaiba.’akasema.

‘Ehe, uliwezaje kufungua makabati, ya shemeji yako?’ akaulizwa.

‘Nilipewa ufunguo na kaka, ....’akasema

‘Hebu tuonyeshe hizo ufungua’akaambiwa, na akatoa zile ufunguo alizo nao akazionyesha kwa hawo watu, waliziangalia tu, kwa mbali bila kuzigusa, halafu wakauliza

‘Kwahiyo hizo ufunguo zote ulizo nazo, alikupa kaka yako, na zinaonekana ni za kuchonga?’ akauliza

‘Ndio,...’akasema.

‘Alikutuma pia ukachukue na ule mkataba uliokuwa ofisini?

‘Ndio alinituma yeye, kwanza huo wa nyumbani alikuwa nao yeye mwenyewe, alikuwa na nakala mbili, sikujua kuwa mmoja ni wa shemeji, baadaye, akaniambia nizipeleke kwa Makabrasha...’akatulia.

‘Nilipofika kwa Makabrasha akaniambia nihakikishe kuwa hakuna nakala inayobakia, mimi nilikuwa nimeshaficha nakala moja,...bila kaka kujua,..’akasema

‘Kwanini ulifanya hivyo?’ akaulizwa.

‘Nilitaka nitoe nakala nyingine, kwani nilihisi baadaye inaweza ikahitajika, sikujuwa malengo yao....’akasema
Ulijua lini malengo yao....?’ akaulizwa

‘Kuna siku waliniita kwenye kikao wakaniambia kwanini wameamua kuziharibu hizo nakala...’akasema

‘Walikuambiaje , lengo lao ninini?’ akaulizwa na hapo akaa kaa kimia, na hapo yule ofisa akauliza swali jingine.

‘Na kule ofisini uliwezaje kuingia , wakati muda wote kuna walinzi?’ akaulizwa

‘Niliingia muda wa kawaida tu, yule mhudumu alikuwa hayupo, na mimi niliwaonyesha kibali kuwa nimetumwa na shemeji, nikaweza kuingia kwasababu nilikuwa na ufungua, alionipa kaka....’akasema.

‘Kibali gani hicho, ina maana ulikwenda kwa shemeji yako ukamuomba hicho kibali?’ akulizwa

‘Aliwahi kunipa kibalia kabla,,...nikawa naendelea kukitumia..kuna siku nafika kwa ajili ya matengenezo ya ofisi yao’akasema.

Hicho kibali hakina tarehe?’ akaulizwa, na kukaa kimiya, na yule ofisa akauliza swali jingine.

‘Ina maana ligushi tarehe....?’akasema huyo mpelelezi

‘Kilikuwa hakijaandikwa tarehe....’akasema

‘Kwahiyo kumbe kaka yako alikuwa ana ufunguo zote za ofisini na za makabati ya mke wake?’

‘Mimi sijui, muulizeni  kaka, yeye alinipa ufungua akanituma niende ofisini akanielekeza wapi pa kuipata hiyo nakala ya mkataba, mimi nikafanya kama alivyoniagiza....’akasema.

‘Wewe kwanini hukumwambia shemeji yako ?’ akauliza

‘Kwanini nimuambie, kama kaka angetaka nifanye hivyo angeniambia nimwambie, kaka kafanya hivyo kama mume wake, na mume wake ana haki kwenye kampuni za mkewe, kuna ubaya gani hapo eeh , ‘akasema na kuniangalia mimi , na mimi nikawa nimemkazia macho, akaangalia pembeni.

‘Ohooo, kwa vile yeye ni mwanaume, ana mamlaka popote, hata kama kampuni sio yake,wewe hujui kuwa kampuni hiyo uliyokwenda kuchukua huo mkataba ni ya shemeji yako sio ya kaka yako ...huoni kuwa ni makosa?’akaulizwa

‘Hayo muulizeni kaka, mimi nimejitolea kuwaambia yale ambayo hata kaka hakutaka niwaambie, ...najua nimefanya makosa sana kuwaambia, kaka hatanisamehe kwa haya...’akasema kwa uchungu.

‘Swali la pili, je kaka yako ndiye aliyekutuma kuchukua bastola kwenye kabati la shemeji yako?’ akaulizwa na hapo akatulia kidogo, halafu akasema.

‘Lakini kaka sio yeye aliyemuua Makabrasha, ...’akasema

‘Una uhakika gani na hilo?’ akaulizwa na kukaa kimiya, na huyo ofisa hakutaka kumshinikiza kwa hilo, kwa vile wao wanafaahmu zaidi, wakauliza swali jingine

‘Kama sio kaka yako basi ni wewe uliyemuua Makabrasha?’ akaulizwa

‘Sio mimi wala sio kaka..’akasema

‘Unaposema sio kaka yako au wewe, ina maana unamfahamu muuaji, ni nani aliyefanya hivyo?’ akaulizwa

‘Kwakweli mimi sijui,....’akajibu na kutulia na yule ofisa akatabasamu na kutikisa kichwa, halafu akauliza swali jingine

‘Tuambie ilikuwaje siku hiyo ambayo Makabrasha aliuwawa,, maana usipotuambia ukweli , ujue hapo wewe utakamatwa kama muuaji, wewe na kaka yako’akaambiwa.

‘Mimi sio muuaji, ..sijamuua Makabrasha, japokuwa ni kweli mimi ndiye niliyekwenda kuichukua hiyo bastola kwenye kabati la shemeji, ...nilifanya hivyo nikiogopa kuwa shemeji kwa jinsi alivyokuwa na hasira , angeliweza kuitumia kumuua kaka, nikaona bora niichukue hiyo silaha nikaifiche mbali kabisa na wao’akasema

‘Kwahiyo hukutumwa na kaka yako kuichukua hiyo bastola?’ akaulizwa

‘Hapana kaka hajanituma kuchukua hiyo bastola, niliichukua mwenyewe baada ya kuiona hapo, siku aliponituma kurudisha hiyo mikataba mipya...wakati nafungua kabati la shemeji nikaiona hiyo silaha, na najuta kwanini niilichukua hiyo silaha’akasema

‘Ulipoichukua hiyo silaha uliipeleka wapi?’ akaulizwa

‘Niliificha ofisini kwetu, na siku moja, nikaichukua kwenda nayo porini kuitupa...’akasema na huyo ofisa akaatbasamu, na kumwangalia mwenzake, ambaye alitikisa kichwa kama kukubali kitu.

‘Kwanini ufanye hivyo?’ akaulizwa

‘Kwa wazo hilo hilo kuwa ikiwemo mle ndani inaweza kuleta majanga, na bora niitupe mbalii kabisa,..’akasema

‘Ikawaje sasa, ...?’ akaulizwa

‘Nikiwa ndani ya gari, nikiwa naelekea huko porini , nilifika mahali gari likawa halina mafuta, ....kituo cha mafuta kilikuwa karibu tu, lakini gari lilikuwa haliwezi kufika hapo, kwahiyo nikaona nichukue galoni niende kununua...’akasema .

‘Unaweza kutuambia ni kituo gani hicho, na una risiti na mafuta uliyonunua siku hiyo, kama ushahidi?’ akaulizwa

‘Mh,hata sikumbuki, na hata jina la kituo, sikumbuki, na nakumbuka sikuchukua risiti...’akasema

‘Ehe, ikawaje?’ akaulizwa

‘Niliporudi kwenye gari langu sikuuona  ule mkoba wangu uliokuwa na silaha, ulikuwa haupo,....inaonyesha kuwa kuna watu walikuja kwa haraka wakafungua kiyoo, wakauchukua, sikuwa makini kufunga viyoo vya gari, ningelijua ningelifunga vyema, naona ndivyo ilivyopangwa itokee hivyo,...nilijaribu kuangalia huku na kule lakini sikuona dalili ya mtu, nikajua nimeibiwa, na silaha ya watu imeshachukuliwa, sikujua nifanye nini, nikaamua kukaa kimiya, ..hadi hapo niliposikia kuwa hiyo silaha ndiyo iliyofanyia hayo mauaji,..huo ndio ukweli wenyewe, ..’akasema

‘Hiyo hadithi yako hukuipanga vyema, inabidi ukaipange vyema, hiyo hadithi yako haina vina wala mizani, itakutia matatani, usiposema ukweli,..’akaambiwa.

‘Ndio ukweli wenyewe huo....’akasema

‘Sema ukwei ni nani uliyempa hiyo silaha, ujue ulichukua silaha ya watu inayomilikiwa kisheria, na silaha hiyo ikatumiwa kufanyia mauaji, na muuaji mpaka sasa hajapatikana, kwanini wewe usikamatwe kwa kosa hilo, tuambie ukweli ulivyo..’akaambiwa.

‘Ukweli ndio huo, sina ukweli mwingine, ...’akasema

‘Inavyoonekana ni kuwa kaka yako alikutuma hiyo silaha, ili ukampe mtu fulani, ambaye ndiye aliyemuua, 
Makabrasha,  na wakati yeye anangea na marehemu, wewe uifanye hiyo kazi....’akasema

‘Hapana,kaka hajawahi kunituma hiyo silaha, kaka kipindi hicho anaumwa, hajui kabisa kuhusu hiyo silaha, ....na mimi sijaua mtu, na siwezi kufanya hivyo..kwanini tumuue mtu kama yule ambaye anatusaidia sana, Makabrasha ni mtu wetu wa karibu,....’akasema akiwa na wasiwasi.

‘Anaweza akawa mtu wenu wa karibu lakini mkaoana hawafai tena, akifa yeye, hisa zake mtachukua nyie, hakuna anayefahamu mipango yenu,...’akasema huyo mtu wa usalama.

‘Hapana hatujamuua Makabrasha, sijui ni nani aliyefanya hivyo...tunasikitika sana kwa kifo chake...’akasema

‘Ni nani aliyemchukua kaka yako hospitalini hadi kwa Makabrasha?’ akaulizwa

‘Ni mimi, alinipigia simu kuwa niende kumchukua,...kwani ana mazungumzo  muhimu na marehemu’akasema

‘Kwahiyo alikutuma pia ukachukue hiyo silaha, umpe mtu mwingine ...’akasema kabla hajamaliza shemeji akamkatisha na kusema;

‘Mbona mnanitungia uwongo, sijafanya hivyo, hata silaha yenyewe sijawahi kuitumia,...’akasema.

‘Unaweza usiweze kuitumia ukabahatisha,kwani ina ugumu gani , yoyote anaweza kutumia, kama anafahamu jinsi ya kufyatua risasi, hata hivyo hatujasema wewe ndoye uliyemuua, kuna mtu uliye mpa hiyo silaha, ndiye aliyefanya hayo mauaji, na unamficha, na kwahiyo wewe utashitakiwa kama ndiye uliyefanya hayo mauaji ...’ akaambiwa.

‘Mimi nimeshawaambia huko ukweli, na kwanini tumuue Makabrasha wakati ni mtu anayetusaidia?’ akauliza.

‘Hilo swali unatakiwa ujibu wewe,...’akaambiwa.

‘Mimi nimeshawaambia ukweli,....’akasema.

‘Hilo litajulikana baadaye, kama unasema ukweli, sisi tumeshaujua ukweli, nia yetu hapa ni kukupima, na ukweli ndio utakao-kuokoa wewe...’akasema.

‘Nimeshawaambia ilivyokuwa,...mnataka niseme ukweli gani zaidi ya huo’akasema.

‘Hujatuambia ni nani uliyempa hiyo silaha, ...hilo unatuficha, lini sisi tumeshamfahamu, ’akaambiwa.

‘Mimi nimeshawaambia hiyo silaha sijampa mtu...’akasema.

‘Ehe, ulipomchukua kaka yako wewe ulikwenda wapi,a u ulikuwa wapi, wakati kaka yako anaongea na Makabrasha....?’ akaulizwa.

‘Mimi nilimsubiria nje, barabarani..’akasema.

‘Ni nani aliyekuona ukimsubiria,maana hapo usipokuwa na ushahidi wa kutosha, utaingia matatani...’nikamwambia.

‘Yule mlinzi wa nje wa hiyo hoteli iliyopo karibu na lile jengo, nilicheza naye drafti, hadi kaka alipokuja, na tukaondoka...’akasema. Na huyo jamaa akaandika jambo kwenye karatasi yake, na kusema.

‘Hilo nilishalifuatilia, ni kweli...ulionekana ukicheza drafti na huyo mtu, lakini kabla ya hapo...sawa hilo tuliache hivyo, ila hatujamalizana na kipengele hicho, kuna ukweli mwingi unatuficha hapo, na hatujui kwanini unafanya hivyo,....’akasema na kukatisha.

`Swali la tatu, huo mkataba wa zamani uliokuwa nao upo wapi?’akaulizwa

‘Niliurudisha kwenye kabati la kaka.....’akasema

‘Lini?’ akaulizwa.

‘Leo asubuhi...wakati shemeji walipompeleka kaka, mimi nilibakai nyuma, nikaurudi nyumbani na kuuweka pale ulipokuwa,...’akasema.

‘Kwanini ulifanya hivyo?’ akaulizwa

‘Huo mkataba niliuchukua mimi, bila hata kaka kujua, na nilishaambia niharibu mikataba zote, na siku zilivyozidi kwenda, nimesikia shemeji akiuulizia huo mkataba, nikaona jambo jema kuondoa hili tatizo nikuuweka huo mkataba wa zamani, ili kaka akija akiuona, aurudishe kwa shemeji mambo yaishe...’akasema

‘Hapo pia kuna kitu unakificha, kama wewe uliona kuwa mkataba huo ni tishia kwenu, hasa kwa kaka yako, na mkakubaliana kuwa mikataba yote iharibiwe, ibakie hiyo mipya, ni kwanini ukaamua kuurudisha hapo tena,....kuna nini kilikusukuma kufanya hivyo, au ulitaka kuuficha hapo kwa muda ili baadaye uje uuchukue, maana ulishajua kuwa kule kwako hakuna usalama tena,..’kaulizwa

‘Mimi niliamua kuurudisha kwa nia njema,kama nilivyowaambia...’akasema

‘Kwahiyo huo mkataba kwa sasa upo wapi?’ akaulizwa

‘Nimefika leo kuuangalia, nimekuta kabati halifunguki....’akasema

‘Swali kubwa hapo ni kwanini uliurudisha?’ akaulizwa

‘Nilitaka kaka aje auchukue mwenyewe,...., sikutaka tena kuendelea kujihusisha na mambo ya familia, na niliona nafanya makosa, na nilitaka kaka na shemeji waelewane....’akasema.

‘Ina maana huo mkataba hadi hivi sasa upo kwenye hilo kabati...?’ mimi nikamuliza na akaniangalia akionyesha uso wa kunikasirikia , akasema;

‘Ndio upo humo kwenye kabati..., lakini kabati halifunguki kabisa, kama vile kitasa kimebadilishwa, kama likifunguka mtauona, upo .... maana mimi ndiye niliyeuweka leo asubuhi,...na kuna kitu changu kingine, sijui kama kipo humo au vipi....’akasema na mimi kwa haraka nikainuka na kuomba niende kwenda kuuangalia kama kweli ndio huo mkataba wetu wa zamani.

‘Nenda kahakikishe, halafu uje, tuendelee, maana huyu mtu asipotuambai ukweli, leo tunakwenda naye..’aaksema huyo ofisa.

‘Mimi nimeshawaambia ukweli, naomba niende nikamuone kaka, alinituma ...’akasema

‘Alikutuma huo mkataba, au?’ akaulizwa

‘Kuna vitu alinituma,....’akasema

‘Shemeji wewe nenda kahakikishe,..huyu haendi mahali, hadi hapo kitakapoeleweka, kuwa tunakwenda naye kituoni, au anafunguka, ukweli wake, ndio utakaomfanya sisi tumwamini, na vyovyote itakavyokuwa sisi tutakuwa upande wake, kumlinda,...’akasema huyo ofisa.

Mimi nikawa naelekea kwenda ndani nikasikia shemeji akiniambia;

‘Shemeji ...kama kuna kitu changu naomba uniletee, nahisi nimekiacha ndani ya huo mkataba...’akasema na mimi sikumjali nikaharakisha kwenda kufungua hilo kabati na wale watu wa usalama wakaendelea kumuhoji....

NB Ni hayo kwa leo


WAZO LA LEO: Katika maisha yako jifunze kuwa mkweli, na jitahidi usimamie kwenye haki, hiyo itakuwa kinga yako kwa hali yoyote ile. Uwongo, hadaa, mwisho wake ni kuzalilika tu.

Ni mimi: emu-three

No comments :