Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, November 18, 2013

Mkuki ni kwa Nguruwe-30‘Mhh, kweli umenifungua masikio, hayo yaliyokukuta ni makubwa, mimi niliona nipo kwenye mitihani, lakini wewe ilikuwa zaidi, sasa ikawaje?’ nikamuuliza.nikitaka kufahamu mengi kuhusu maisha ya huyo mama, ambaye nilimuita dada...

Aliendelea kunisimulia maisha yake na mume wake ambaye sasa ni marehemu...

*******

`Mimi sikukata tamaa na mume wangu, niliendelea kumsubiria, nilimuomba mungu, kuwa ipo siku,atajirudi, na kunikumbuka , lakini haikiutokea, mimi nikaendele kuishi kijijini, nikijitegemea, wazee wakaingilia kati , akaitwa, na mbele yao akakubali kuwa mimi ni mke wake na ni wajibu wake kunihudumia.

‘Sasa kwanini unamfanyia hivyo mwenzako?’ akauliza

‘Nilipitiwa tu na mihamgaiko ya kutafuta riziki’akasema.

‘Hizo riziki unamtafutia nani?’ akaulizwa

‘Mimi na familia yangu..’akasema

‘Mbona hukimbuki familia yako, au familia yako ni akina nani?’akaulizwa

‘Ni mke na watoto wangu, lakini pesa haitoshi...mambo mengi mjini, ...’akajitetea

‘Sasa unasemaje, ?’ wakamuuliza akasema, yeye atajitahidi, na b ado ananitambua mimi kuwa ni mke wake,na akaambiwa aniombe msamaha kwa hayo yalitokea, akafanya hivyo, nikajua kuwa kweli yamekwisha, lakini aliporudi mjini hali ikawa ile ile...tukachoka, tukaamua kumuacha aendelee na maisha yake, na mimi nikajibadili, na kutafuta njia ya kujiajiri...

Bahati nzuri, walikuja wawekezaji wanasaidi wanawake waliokatiza masomo kwa uja uzito na mimi nikajiandikisha, ufadhili ukanisaidia nikaanza kusoma, nikafanya mtihani wa darasa la saba nikafaulu kwenda. Kidato cha kwanza, nikasoma hadi nikamaliza kidato cha nne, nikafulu kwenda kidato cha sita...hutaamini, nilifaulu, nikajiandikisha chuo kikuu....

‘Ukiniona hivi huwezi amini, lakini nilikanyaga chuo kikuu, watu hawajui, hata huyo mume wangu alikuwa hajui..hamna aliyemwambia,maana haulizi hana habari na mimi, ..ni kama hana mke, ..mimi niliamua na nikafanikiwa, lakini sikuwa kumpinga kuwa yeye sio mume wangu.

‘Alishangaa siku moja nipo Dar, nahutubia akina mama mpango wa kuwawezesha wanawake walikatisha masomo kwa ajili ya uja uzito, sijui ilitokeaje nay eye likuwepo kwenye huo mkutano, nilipomaliza kuhutubia akanifuata na kuniuliza

‘Wewe mwanamke, umawezake hayo yote?’ akaniuliza na mimi nikamjibu

‘Ni kutokana na hayo uliyonitendea, nashukuru sana...’nikamwambia, na akaniomba msamaha, mimi nikamwambia mimi sina kinyongo na yeye na bado mimi ni mke wake, lakini siwezi kwenda kwake, maana bado nipo kwenye hiyo adhabu aliyonipa...

Kuna kipindi aliniambia amenipa adhabu, ya kulazimisha kuolewa na yeye kwahiyo nisihangaike, ...na ndio maana nikamwambia mimi bado nipo kwenye adhabu yake...nikaondoka kesho yake sikufika nyumbani kwake, nilimwambia naogopa yasije yakanikuta yale yaliyonikuta kipindi cha nyuma.

Sasa ikawa yeye anakuja nyumbani, na kuomba msamaha, na mimi niliendelea kumwambia kuwa mimi ni mke wake, asiwe na wasiwasi, sina kinyongo na yeye, nab ado nipo kwenye adhabu yake...

‘Ina maana alipokuwa akifika, alikuwa anakuja kwako, au kwao , ?’ nikamuuliza

‘Alikuwa anakuja kwao, mimi nilikuwa naishi na babu na bibi, ...sikumkubalia kuja kulala kwangu, nikimwanbia bado nipo kwenye adhabu aliyonipa...hali hiyo ilimtesa sana,...akahangaika, sijui kwanini aliamua kufanya hivyo...sikugeuka nyuma,...’akasema.

‘Mtoto naye akawa anakuwa akasoma, hadi sekondari, na hatukutaka msaada wake,..ila aliendelea kumtambua kama baba yake, nilimwambia huyo ni baba yako,usije hata siku moja ukamkana, au kumsema lolote baya, na alinitii, ila hatukutaka msaada wake, tena, hata akituma pesa kwa ajili yetu na familia sisi tulizichukua na kwenda kutoa sadaka...huo ukawa ndio msimamo wetu...’

‘Ikatokea wazazi wakaingilia kati, hadi tukasuluhishwa...nikaona haina haja, na kwa vile mimi nampenda mume wangu, nikakubali yaishe, tukaanza maisha mapya,..lakini kwa masharti kuwa mimi nitaendelea kuishi huko huko kijijini, sikutaka kuja mjini kuonekana na wanawake zake, na yeye akaendelea kutesa na wanawake zake, siku akijiskia anakuja huko kijijini namkaribisha mume wangu, anakaa siku mbili anaondoka zake, nimezoea, sina shida naye, mpaka umauti ulipomkuta.

‘Nilikuja kuajiriwa na kampuni isiyo ya kiserikali kwa ajili ya kusaidia akina mama waliokatiza masomo kwa ajili ya uja uzito, kwahiyo sikuwa na shida, ya kumtegemea mume tena,...sikuwa namfuatilia maisha yake, na mengi nilikuwa naambiwa na watu tu...mtoto wangu ndiye aliyejitahidi kumfuatilia na kujaribu kumkanya, lakini hakumsikiliza mtu, alidai kuwa hayo ndio maisha yake, mtu asimuingilie.

‘Sasa kwanini nije kuchukua urithi wake, .kwanini nije, kuchukua mambo yake, ambayo hatujui yametoka wapi...sisi tuliamua kila kitu chake tukiuze, tulipe watu, na kama hakuna watu tutatoa sadaka, na ilikuaj kugundulika kuwa ana watoto wengi wa nje, ana madeni,...na hawo waliowafanyia ubaya, ni wengi, tukajaribu kuwalipa lipa na kuwaomba msamaha, na hili zoezi ndilo tunaendelea nalo,....’akasema.

‘Kwahiyo ndio maana mlikuwa mnanitafuta?’ nikamuuliza

‘Ni pamoja na hayo, ila cha muhimu kwenu ni huo mkataba, tulitaka kujua ukweli, na kama tulivyohisi, tumegundua kuwa ni yale yale ...kwahiyo, tunaomba, mtuambie tufanye nini, kwani sisi hatutaki kitu chochote cha kwake....’akasema

‘Je unafahamu lolote kuwa mkataba huo umetokana na kugushi mkataba mwingine uliokuwa halali?’ nikamuuliza

‘Nimesikia hilo kwa wakili wetu, na yeye alisikia kutoka kwa wakili wako, ...’akasema.

‘Je mna amini hilo, kuwa mume wenu alikuwa na hisa kwetu?’ nikamuuliza

‘Sisi hatuna haja ya kupekenyua ukweli, ukweli mnaufahamu nyie..sisi hatuna haja na hizo hisa, hata kama kulikuwa na ukweli, hatuna haja nao....tulishaanza maisha yetu, hatukuwa tunamtegemea yeye, kwanini sasa kafariki tuanze kugombea mali yake, kama walivyokuja watoto wake wa nje kuja kugombea mali yake....sisi tuliwaambia kuwa kama wanahitaji mali ya marehemu, basi wakubali na madeni yake, na alipopigwa mahesabu ikaonekana madeni na mengi, kuliko, wenyewe wakakimbia.

‘Hayo ni ya mume wako, sasa tuongee kuhusu mume wangu,...kwanini mnamtetea ?’ nikamuuliza

‘Sisi hatumtetei, ila tunatimiza wajibu wetu, yeye kama wengine, ni miongoni mwa watu walioathirika kutokana na tabia ay mume wangu....anahitajia kupata haki yake,...alihadaiwa, na akajikuta anatoa hisa kwa mume wangu, tunahisi kuwa hisa hizo hazina uhalali....ndio maana tunahitaji kurejesha kila kitu chenu,...’akasema

‘Kwa vipi?’ nikamuuliza

‘Kutokana na mkataba,...hatuna jinsi nyingine, sisi tunajitoa kwenye huo mkataba, na kuuvunja , usiwepo ,...ndio maana mwanasheria wetu anauanyia kazi, ila tunahitajia msaada wenu, ..mume wako kasema wewe ndiye kikwazo, ndio maana tumekuwa tukijitahidi kuja kuonana na wewe, na sasa tumekuona tunaomba msaada wako, tulimalize hili...’akasema.

‘Nkushukuru sana kwa kuwa mkweli kwangu na kunielezea sehemu ya maisha yako, na mimi sina kinyongo na nyie tena, ...ama kuhusu maswala ya mume wangu, hayo haywahusu, nawaomba msiingilie kabisa maisha yangu na mume wangu,...kama mnataka kumsaidia kwa hilo, nyie mshaurini aulete mkaatba wetu wa awali, ambao alikubali kuubadili, ...hilo tu, ...’nikasema.

‘Sisi hatuujui mkataba huo’akasema huyo mama

‘Hata mimi siujui huo mkataba wenu  mnaouongelea maana ulitengenezwa kimbinu kutoka na kuvunja mkataba watu wa awali bila mimi kujua,...kwahiyo huo mkataba mlio nao ni batili,..’nikasema.

‘Kwahiyo nyie au wewe unataka sisi tufanye nini?’ akaniuliza.

‘Nyie mumeshatimiza wajibu wenu, ..nawashukuru sana, sisi au mimi sina kinyongo na nyie, au mume wako, ..yeye alifanya hayo aliyoyafanya, ...hayupo duniani, huwezi kumuhukumu maiti, anayehukumiwa ni yule aliye hai,..na huyo ni mume wangu, ..na hilo la mume wangu haliwahusu .....nafikiri umenielewa’nikasema.

‘Mdogo wangu, mimi nataka kukupa ushauri tu, ni ushauri wa bure, kama utauona una maana haya, kama ndio wa kupitwa na wakati haya, ukitaka kuufuata ufuate kama hutaki basi, ni hivi, hakuna nkataba wa ndoa aidi ya ndoa yenyewe, mkataba wa ndoa ni kiapo chenu cha ndoa, pale mliposimama wewe na mume wako, ukakubali kuolewa na yeye na yeye kukubali kukuoa,..’akatulia kidogo huku akionyeshea kwa mikono.

‘Huo ndio mkataba, na unakamilika kwa vile mliufanya mkiwa na mashahidi wakuu,  watu, mbele ya mawakili, wawakilishi wa kiimani, wanaoitwa  viongozi wa dini, au wahusika wa kuoesha,  na mungu akiwa ndiye hakimu wenu....ule ndio mkataba wa ndani ya nafsi zenu, kamwe, hauwezi kufutika, au kubadilishwa,...utaona kwenye ndoa kunakuwa na kisomo, kinachoelezea nini  ndoa, kuna maelezo mauri japokuwa wengi kwa wakati huo hatuwi makini kuyasikiliza, ule ndio mkataba wenu wa ndoa....’akasema

‘Nikuambie ukweli, sisi wanadamu , nikiwa na maana sisi wanandoa, hata kama tutajaribu kuwekeana mikataba mingine, tunayoona sisi ni kisheria zaidi, tukajenga ukuta wa kulindana, tukaweka na walinzi wa kutulinda, ndani na nje, ...tukafanya kila iwezekanavyo, ili mmoja asivunje miiko ya ndoa, kama mioyo yetu, kama sisi wenyewe hatukujibidisha hivyo, tukakubali mioyoni mwetu kuwa ndoa ni kati ya muma na mke, kuwa ina masharti yake, ambayo kila mmoja anatakiwa kuyatimiza kidhahiri na kificho,...kama hatutajua hayo sisi wenyewe, tukayakubali sisi wenyewe ndani ya nafsi zetu, haiwezi kusadia kitu,...kamwe, hatutaweza kufanikiwa....’akasema.

‘Mimi nakushauri kama mkubwa kwako, wewe ni mdogo wangu mbali tu, nimkuzidi kiumri, na huenda hata kiuzoefu, nimepata matatizo mengi, niliyokusimulia ni cha mtoto, hakuna haja ya kujitesa, hakuna haja ya kuhangaika sana, cha muhimu kwa  sasa ni kumsamehe mume wako,....kakosea na umeyaona makosa yake, hata kama hajaktamkia, maana madume, wanaweza kujifanya hawajakosea, lakini kiukweli kwenye nafsi zao, wanajua hilo, inawagusa...’akatulia kidogo.

‘Sisi wanawake, kwa waume zetu ni kama mama zao, tunabeba yote kama mzazi anavyobeba makosa ya mtoto wake, ..mtoto, anaweza kukosea sana, lakini mwisho wake kama mzazi, unamsamehe, unaona mtoto ni mtoto tu..na mume halikadhalika,...wengine wanaweza kuleweshwa na tamaaa, wakaghilibiwa, na wakafanya mambo ya kitoto...ukimuuliza anajifanya hajui, au hata kukataa, anakataa, sasa sisi tujitahidi tu kuwasamehe....’akasema na mimi nikawa natikisa kichwa kutokukubaliana na maneno yake.

‘Nikuambie tena,....wengine wanaweza hata kukubali makosa yao, lakini anakubali mdomono tu, mwingine anaweza asikubali, lakini moyoni kakubali makosa, ila anaogopa kuonekana kakosa,sasa mimi namfahamu sana mume wako,... kama kakubali kujirudi, kama yupo tayari kuishi na wewe, na kuwa hatafanya tena hayo makosa yaliyotokea,...basi msamehe, na huo mkataba hauna maana ..unaweza ukawepo na bado kwa siri akawa anaendelea kuuvunja, sasa inasaidia nini..mkataba mnzuri upo ndani ya mioyo yenu....’akasema.

‘Achana na kuhangaika na huo mkataba, ...wanajua wenyewe kwanini waliubadilisha, wewe shikilia mkataba wao ambao mungu anautambua, ..kaeni pamoja, jadilianeni, muone kosa lilikuwa wapi, lisahihisheni, muendelee na maisha, mkumbuke sasa mna watoto, na watoto walivyo, wanajifunza kutoka kwenu,...wakiona baba na mama wapo kitu kimoja, na wao wanajiwekea nadhiri mioyoni mwao kuwa nikiwa mkubwa, nikaoa, nitaishi kama walivyokuwa wakiishi baba na mama...lakini kama mtatenegana, unafikiri wao watajifunza nini, wataona kumbe kuishi kila mtu maisha yake, inawezekana, ndio mtindo wa maisha, lifikirieni hilo kwa ajili ya kizazi chenu...’akasema.

‘Nakushukuru sana kwa ushauri wako dada yangu, lakini nilikuwa na swali nataka nikuulize,  je mume wangu aliwahi kukuambia kuwa ana mtoto nje?’ nikamuuliza.

‘Mhh, hajawahi kunitamkia hivyo, huwa naongea naye, kama dada yake, kama shemeji yake, tunataniana hapa na pale, hajawahi kuniambia hilo, siwezi kkuficha, ninachokumbuka, ni kuwa, kuna siku nimemuuliza, hivi yeye kwa sasa ana watoto wangapi, aliniambia kuwa tu ana watoto, hakusema idadi, na nilihisi kama ananificha jambo....’akasema.

‘Alisema ana watoto, ndio tuna watoto’ nikasema.

‘Hakusema wa kike au wa kiume, ila nakumbuka kauli yake aliyotoa ni kuwa, yeye atahakikisha watoto wake, wote, bila kujali ni mke au ni mume, atawaandikisha haki zao,....na alisema, wa kiume, ni lazima awe kiongozi wa wenzake...nakumbuka kitu kama hicho, na kwa kauli hiyo, nilifahamu kuwa mna watoto wa kike na wa kiume’ akasema.

‘Lakini hakusema kuwa ana mtoto nje ya ndoa...ila kasema tu, kuwa atawapa haki sawa, si ndio, kwahiyo hiyo kauli ya kusema ana mtoto nje, nahisi inaweza ikawa ni uvumi au kuna ukweli...?.’nikamuuliza huku nikionyesha kushangaa, na yeye akaonyesha kushangaa jinsi nilivyomuuliza, akaniuliza swali;

‘Kwani nyie mna watoto wangapi?’ akauliza huku akiangali huku na kule, kama anawatfuta watoto.

‘Mhh, usijali dada yangu, nilikuwa nakuuliza tu, hayo ni mambo yangu na mume wangu, tutaelewana tu...’nikasema.

‘Aaah, uliniuliza swali, nikakujibu, na wewe naomba unijibu swali langu...ili kama nina cha kukushauri, nitakushauri, sina nia ya umbea,...’akasema.
‘Kiukweli, sisi tuna watoto wawili, wa kike...’nikasema.

‘Basi labda mimi nilisikia vibaya, lakini nina uhakika, kutokana na kauli yake, ni kam vile mna watoto wa kike an wa kiume...hata kwenye mkataba wetu, kuna kitu kama hicho,...sikumbuki vizuri, na kwahiyo hapo siwezi kusema kitu,...nisije nikawa mbeya,, ila lisemwalo lipo, kama halipo laja....’akaniangalia kwa macho ya udadisi.

‘Nitaligundua tu, nina uhakika kabla ya wiki nitakuwa nimeshagundua ukweli...na hapo ..sijui, maana huo ni ushahidi tosha, wa kuvunja mkataba, na ndio maana wakakimbilia kuuharibu...hawatashinda kabisa, labda sio mimi...’nikasema.

‘Kwahiyo huenda hilo ndilo linafanya msielewane, ....na hilo hunda ni moja ya jambo linalovunja mkataba wenu...kiukweli hilo linavunja ule mkataba wa kiukweli wa ndoa, unapotoka nje ya ndoa umeshavunja mkataba, na ili mkataba huo uendelee kuwepo, ni nyie kukaa na kusameheana mkakubaliana, yeye mkosaji aseme ukweli, na wewe ukubali kumsamehe....kama kuna mtoto nje, ambaye humjui, basi jadilianeni muone jinsi gani mtamtambua huyo mtoto...vinginevyo, mtashindwa kupanga mambo yenu, kwani  kama yupo mtoto wa nje, yeye inabidi atumie gharama za kificho, anakudhulumu wewe na watoto...’akatulia huku akiangalia pembeni, hakutaka kuniangalia usoni.

‘Sasa ili kuliondoa hilo,...kwa vile..nasema kwa vile, kama lipo, unielewe vizuri hapo, maana kiukweli mimi sijui...kama limeshafanyika, na mtoto yupo, na yeye anawajibika kwake, na sijui labda huenda anawajibika na kwa mama wa mtoto pia, na kama bado  mtoto ni mchanga, ni lazima awajibike, hana ujanja hapo, na ni vyema, akuambie ukweli....muulize, kwa wakati muafaka, atakuambia...’akatulia.

‘Kwahiyo kumbe mna mabinti wawili, hamjajaliwa kupata mvulana....ndio maana niliwahi kusikia zamani kidogo, kuwa akizaa mtoto wakiume atakuwa katimiza ndoto yake...lakini ni zamani kidogo,...na halina maana kwa sasa..ila kaeni mliongelee kama wanandoa,....ili mambo yaishe, mgange yajayo..msisubiri mpaka kutokea msiba, mmoja wenu hayupo duniani  ndio hawo watoto wa nje, wanaanza kujitokeza, na kuleta mfarakano, kama ilivyotokea kwetu, japokuwa tumeshayamaliza kiaina, ..’akasema.

‘Nimekuelewa dada yangu, nakushukuru kwa ushauri wako,...lakini hayo ya mume wangu, yaacheni kama yalivyo, ninafahamu jinsi gani ya kufanya, nilitaka kuwa na uhakika tu, kama kweli ana mtoto nje, maana tetesi kama hizo nimeshazipata kwa watu zaidi ya mmoja, na sitaki watu kumzushai mume wangu, hata mimi sitaki kumuhisi mume wangu kwa kitu ambacho, tulishakubaliana, na kipo wazi, ..ndio maana nachelewa kumuuliza, kwani anafahamu amzara yake... yeye, hajawahi kuniambia na huenda kaam ni kweli basi anaogopa kuniambia ukweli, sijui kwanini...nafahamu kwa vile anajua ni nini kitafuata baada ay hapo...sasa anamficha nani’Nikasema.

‘Je akikuambia ukweli, utamsamehe?’ akaniuliza.

‘Alishachelewa kuwa mkweli kwangu , kwahiyo hata akiniambia sasa hivi , aatsema kwa vile, ...ni kutokana na shinikizo, hata hivyo  anahitajika kusema huo ukweli, ...hana hiari ....hebu nikuulize dada, kama mimi ningepewa mimba huko nje, tuseme mimba tu, achilia mbali kupata mtoto, akajua hivyo, au hata akasikia kwa watu kuwa mimba ya mke wako ni ya mtu mwingine,...achilia mbali maswala ya mtoto na mimba, je angelisikia kuwa natembea na mwanaume mwingine wa nje, kwa mtiazmo wako wewe unafikiri ingalikuwaje?’ nikamuuliza.

‘Hahaha eti nini, wala usiwaze hivyo, kwanza kwa sisi wanawake ni aibu, uwe kwenye ndoa halafu unatembea na mwanaume mwingine, usifikirie jambo kama hilo...sio kwa wanawake tu, ilitakiwa iwe hivyo kwa wanandoa, lakini kama nilivyokuambia awali, hawa wenzetu hawana uvumilivu, inapofika kwenye .....hicho chakula, unanielewaeeh, ?’akasema huku akicheka.

‘Nimekuelewa dada, ila nauliza hivyo maana ndoa ni mashikamano ya mume na mke, na kila mmoja anawajibika kuitii ndoa yake, na kama ulivyosema hayo yapo kwenye mkataba wa asili wa ndoa,sasa kama yeye kafanya hivyo, na mimi ningelifanya hivyo, ingelikuwaje, au mkuki ni kwa nguruwe tu, ....’nikasema.

‘Mdogo wangu, nijuavyo mimi, eeeeh, unasema nini , uwe na mimba ya mwanaume mwingine, wala usiseme hilo, ndio maana wale iliyowatokea hivyo, kwa bahati mbaya labda,hawawezi kusemi kabisa, inakuwa siri yao, inabakia kusema anafanana na mjomba wa shangazi,  maana kiukweli asilimia kubwa ya wanaume hawana huruma na hilo, wangelikutimua, na talaka yako ikakufuata nyuma, ...wewe, uwe na mimba ya mume mwingine, mbona utajikimbia ....lakini mdogo wangu usifanye mambo kwa kujilinganisha na wanaume..wewe unachotakiwa ni kutimiza wajibu wako tu...’akasema.

‘Kwanini huo wajibu uwe ni kwa mwanamke tu,...mimi hapo ndio nashindwa, kuelewa, sijigambi kuwa nina uwezo, lakini huenda hayo yalikuwa yakifanyika kwa vile mwanamke hana uwezo, mimi namshukuru mungu kanijalia, nina uwezo wa kiuchumi, sio haba na ni uwezi wa kiasili, toka kwa wazazi wangu, kwahiyo sina ....sitakiwi niwe mtumwa, kwa nini niwe mtumwa,..niteseke, nikubali kunyanyaswa..hapana,...,

‘Dada huenda yeye akafikiria vibaya akaanza kusema kwa vile....na sio naongea kwa vile, kiukweli sisi familia yetu, toka enzi za mababu tuna hali nzuri, na kwahiyo  ukinilinganisha mimi na mume wangu, mimi nina uweo zaidi yake, mimi hayo sijawahi kuyawazia, nilimuheshimu mume wangu,kama mume wangu, sikuwahi kumvunjia heshima yake, sasa kwanini asifikiria hivyo, kuwa sisi ni wanandoa nah tuna mafungamano na wazazi wetu, wazazi lao ni lao, na sisi ni sisi, ......sipendi kuongea hivyo, lakini ilihitajika yeye ajivunie kuwa kapata mke asiyejali hali iliyopo, yupo tayari kuishi na yeye bila kujali hali za kiuchumi, kapata mke mwenye kumsaidia, ki hali na mali, ....kwakweli,mimi sitakubali hilo....’nikasema.

‘Nakuelewa mdogo wangu,lakini nakuonya usije ukatumia hali yako, kwa vile upo juu, zaidi ya mume, ukafanya kama wafanyavyo wanaume....nilitangulia kukuambia kuwa sisi wanawake, ni kama wazazi, ....katika maswala ya ndoa sisi tunawajibu wetu mkubwa, tunahitajika kuwalea wanaume kama watoto, hilo ni wajibu wetu,na tumshukuru mungu kuwa tumejaliwa kipaji  hicho na mungu,na wao kama wanaume wana vipaji vyao vya mambo mengine, na wana wajibu wao kama wanaume, japokuwa wengi wao wanatumia vipaji hivyo vibaya....sasa uwe makini kwa hilo.....’akasema.

‘Nimekuelewa, lakini hata sisi wanawake, tunajishusha wenyewe, tunahitajika kujitetea , pale tunapoona wanaume wanakosea, hatutakiwi kukaa kimiya, inahitajika kuwaonyesha kuwa na sisi tunahaki, ilimradi iwe ni haki kweli, sijawahi kumsaliti mume wangu,....sijawahi..sasa kwanini yeye afanye hivyo , sawa huenda nilikosea, kutokumuelewa, akawa na njaa, kama ulivyosema, nikamwambia asubiri, angeniliambia siwezi kusubiri..njaa ni kali sana, na mimi ningelielewa, sasa huenda aliona namnyanyapaa, yeye ni mwanaume, ana takiwa kutumia hekima na kunielewesha,....hapo mimi sielewi...’hapo nikatulia kidogo.

‘Nakuelewa sana mdogo wangu,...kuna makosa madogo madogo tunayoyafanya,kama wanandoa, na nazungumza hili kwa wanandoa wa kike,...na tunarudi kule kule, wanaume ni kama watoto inapofikia kwenye maswala ya mapenzi...inabidi nikuambie hilo, usije ukafanya makosa,...mume wako anakuja  kwako anataka chakula, ukamtolea nje, kwasababu mbalimbali huenda na nyingine ni za kimsingi au sio za kimsingi....unielewe hapo nitatumia lugha ya kiutu uzima zaidi...’akasema na mimi nikatikisa kichwa kuwa namuelewa.

‘Nimeshakuambia kuwa wanaume wanapofika kwenye swala la chakula, ....unaielewa hapo, ni kama watoto wadogo,....yeye kama alivyo mtoto, atakwenda kwa jirani huenda akakaribishwa chakula,au hata akaomba chakula japokuwa chakula kakiacha nyumbani,..., vyovyote iwavyo, na kwa vile uvumilivu wao ni mdogo, akimbiwa karibu hatakataa...unaona hapo, ni nani kalianzisha hilo, utakuja kumlaumu nani hapo....,wewe uliona ni kitu kidogo tu, chakula si kipo, atakula muda wowote, atakula baadaye, au sio...?’ akaniangalia kama ananiuliza.

‘Wewe  ukamwambia, subiri baadaye, au ukatumia lugha nyingine, mnazopenda kuzitumia, ‘sijisikii’...yeye akitoka hapo, kichwa kimeshabadilika, ....nikuambie ukweli, wao uvumilivu kwa hilo swala ni mdogo sana, akiwa na njaa, wengi hawawezi kuvumilia, huenda wewe utasema wanajilegeza, haya, sema hivyo,....utajuta, utaumia...acha kabisa hiyo lugha, nakueleza kama dada yako...’akaniangalia kwa makini.

‘Mwanaume akitoka hapo kwanza akilini anajidanganya kuwa  ngoja nikaondoe mawazo, anakwenda kutafuta  chachandu , ...pombe, ...hiyo ndiyo inakuja kuwaharibu akili kabisa,  basi tena akifika kwa jirani, hatasema nimeshiba, hatasema sitaki,...ukichukulia kuwa alikuwa na njaa, akaja kwako ukamwambia sijisikii, akenda akaongeza chachandu, njaa ikawa mara dufu,...unafikiri akifika kwa jirani, akiambiwa karibu atasema nini, akajivunga,atasema nitaonja kidogo, chakula hicho na njaa ya aina hiyo haina cha kuonja kidogo, inakuwa kama mlamba asali,halambi mara moja, kosa dogo, madhara makubwa ...kwa uwoni wako, hapo mara nyingi , ni nani atapata hasara...’akawa kama anauliza.

‘Sawa dada mimi nimekuelewa kwa hilo...ni kweli anayekuja kupata hasara  ni mwanamke, lakini sio mimi....’nikasema na yeye akanikatiza.

‘Anayekuja kupata hasara ni mwanamke, sasa kwanini tusilione hilo, kwanini tuuachie huo mwanya, tuliolewa pale kwa kazi gani...mimi mtaniona ni wa kijijini sawa, lakini kama mtaendelea kufanya hayo makosa, mtawatesa watoto,..mtapaat watoto wa nje, na bora wewe una uwezo wako, lakini wengine ndio akina sie, tunawategemea waume zetu kwa asilimia kubwa, tutafanya nini, kama tunalifahamu hilo tusifanye hayo makosa,..kama ana njaa, mope chakula...’akasema na kucheka.

‘Dada mimi sijakubali hilo...na ni kwanini tuendelee kukubali hilo, hiyo njaa kwani mimi hainipati, na chakula kipo, ni swala la muda tu, kitapakuliwa kitaliwa, lakini kwa wakati muafaka, kwanini tuwe walafi...kila kitu kina mpangilioa, sio kila mara mmoja akisikia kuala basi, kula...hata afyta zitaharibika, mimi bado sijakubaliana na hilo,na ili hali kama hiyo iweze kuzoeleka, ni lazima tuamuke...'nikasema.

'Ni ,lazima tuanze kuwa na utaratibu, ni lazima tuanze mahali , maana njitolea kuanza, nikianza mimi na wengine watakuja kufuata...., ni lazima nimuonyeshe kuwa alichokifanya yeye sio sahihi, kama tangu awali angelikuwa mkweli kwangu, ningelikuwa na fikira nyingine, ningelimuelewa,...kama binadamu ningeumia kidogo, lakini mwisho wa siku ningekubali yakaisha, lakini kwa hatua aliyofikia kwa sasa, ....sijui..,sijui kama nitaweza kumsamehe....’nikatulia nikiwa kama nawaza.

‘Msamehe tu mdogo wangu....hutapoteza kitu hapo..yule namfahamu sana, ni mwanaume mwema sana, je ungalikutana na mwaname kama alivyokuwa mume wangu ungalisemaje.....’akasema.

‘Dada  baada ya wiki mimi nitawapa jibu langu, jinsi gani mnatakiwa kufanya, zaidi ya hayo, ni kuwaombia tu, kuwa maswala yangu na mume wangu niachieni mwenyewe..ninafahamu ni kitu gani cha kufanya, wala msisumbuke naye, yeye ni mtu mzima ana akili ya kujua jipi ni jema na jipi ni baya....kama anajiona yeye ameshinda, basi anajidanganya, ....nyie mtaona tu...’nikasema.

‘Ina maana hujanielewa, .....?’ akaniuliza na kuniangalia machoni, na mimi nikawa nimeangalia pembeni huku nimekunja uso, na nilipogeuka, tukaangaliana, aliogueza uso wake na kuangalia pembeni akasema.

‘Mhh, unanitisha....kwahiyo unasema baada ya wiki tuje...tunatarajia majibu yenu, mtakuwa mumeshamalizana, au sio, sisi tutajitahidi kusubiria, wiki ikiisha na sisi tutajua ni nini cha kufanya, na mwanasheria wetu atachukua uamuzi ambao tutaona sisi ni sahihi, kwasababu hatuwezi kusema kwa maneno huo mkataba haupo, tukauchana , nafahamu kuna taratibu zake , nafahamu wewe unafahamu zaidi kuliko mimi...’akasema.

‘Ninachoweza kukuambia kwasasa, ni hivyo, kwanza mimi siutambui kabisa huo mkataba wenu, maana ni batili,....sio halali,ni wa kugushi, na ukiendelea kuletwa kwangu nitawashitaki, ,...lakini kwa ajili yako na mwanao, kwavile nimewaona ni watu wema, nawashauri tu,  msubirie  baada ya wiki, au hata kabla ya hapo,  kama mume wangu atakuwa tayari kutimiza masharti yangu, nitawaambia, ni nini cha kufanyai..’nikasema

‘Sawa nimekuelewa, nashukuru sana,..wasiwasi wangu ni kuwa tunamchelewesha huyu mtoto, anatakiwa kurudi huko anapofanya kazi,, wasiwasi wangu ni kuwa kiondoka majukumu anamuachia mtoto mwingine, kuna mtoto mwingine wa mume wangu alizaa na mwanamke mwingine, wanakaribiana sana kiumri na mwanangu, naye kaingia kwenye fani hizo hizo za uwakili,lakini ni wale wenye pupa, kamlanda sana baba yake,....’akasema huku akisimama kutaka kuondoka.

‘Mtoto huyo kutokana na mirathi, mume wangu aliandika kwa wakili wake, kuwa, kama akifariki yeye, basi, huyo mtoto, ndiye atakayemkaimu mwanangu, ..sasa, tusipoliamaliza hili mapema, tukamuachia huyo mtoto, nina wasiwasi,kuwa mtakuja kusumbuana naye sana, bado  hajalisikia hilo la huo mkataba, kama angelijua kuna mkataba kama huo,sijui kama anglifuata ushauri wetu, kusingelikuwa na amani...ndio maana tunataka tulimalize hili haraka,iwezekanavyo, fikiria haya tunayoyafanya yeye aliyapinga vikali, lakini tulipomuonyesha madeni, ya marehemu, hakuonekana tena..’akasema.

‘Msiwe na shaka na mimi, mimi simuogopi yoyote, ilimradi nipo kwenye haki yangu, wanachotaka kupata sio haki yao, .....kama kweli anaifahamu sheria, akasimamia kwenye haki, ataligundua hilo, lakini kama ndio hawo wenye tamaa, .....wanaotaka kuchuma bila kutoa jasho,...wakaamua kukimbilia kudai , mimi siwaogopi, kabisa, nafahamu jinsi ya kupambana nao,....hata akija mtu mwingine yoyote, mwenye ukali, au msomi, simuogopi kabisa dada yangu,kwani nafahamu ni kitu gani ninachokifanya, ninachokifanya ni kutetea haki yangu,....’nikasema.

‘Sawa mdogo wangu,...kwa hilo tupo pamoja, ... ila nataka kuja siku nyingine kuongea na wewe maswala ya uwekezaji,....nahitajia shule kutoka kwako, tukikutana tena tuongelee maendeleo, natumai utanipokea kama mwanafunzi wako..’akasema.

‘Unakaribishwa sana...’nikasema na mara simu yangu ikalia, nilipoangalia nikaona ni namba ngeni kwenye simu yangu,, ...sikutaka kuongea na mtu nisiyemfahamu kwa muda huo...tukaagana na mgeni wangu huo, huku simu inaendelea kulia, halafu nilipoona kaondoka, nikapokea na kuuliza

‘Nani mwenzangu...?’ nikauliza

‘Mimi ni mmoja wa watoto wa marehemu Makabrasha....’akasema

‘Sawa unasemaje?’ nikuliza

‘Nimesikia tetesi kuwa kuna mkataba unaoonyesha kuwa marehem alikuwa na hisa kwenye kampuni zako, sasa kuna hawa ndugu zangu wanajifanya wacha mungu, wamegawagawa mali za marehemu, utafikiri wao ni matajiri, mimi sijakubaliana nao...’akasema

‘Kwahiyo?’ nikawa kama nauliza.

‘Nasema hivi kama marehemu alikuwa na hisa kwenye kampuni zako, inatakiwa wote tukutane tukubaliane, hawezi kuja wao wenyewe na kuzigawa kaam walivyofanya kwenye mali zingine, mimi sitakubali hilo, tutaenda hadi mahakamani...’akasema

‘Nani kakuambia mambo hayo?’ nikamuuliza

‘Nimesikia tetesi...’akasema

‘Kwahiyo hata ukisikia tetesi kuwa wewe sio mtoto wake halali utazikubali?’ nikamuuliza.

‘Unasema nini?’ akauliza kwa hamaki

‘Kuna tetesii kuwa wewe sio mtoto wake, ni wa kusingiziwa, je unazikubali hizo tetesi?’ nikamuuliza.

‘Sikiliza mimi nakuuliza mengine wewe unaleta mzaha, sikiliza mimi nafahamu sana sheria, kama ni kweli nitafuatilia hadi mahakamani, ninawapa wiki mbili tu, hilo liwe wazi, na ...hizo tetesi zako, hawo waliokuambia waambie, hawana akili kwanini hawakusema hivyo wakati marehemu yupo hai...’akasema.

‘Nilikuwa nataka kukuonyesh a kuwa tetesi  sio ukweli wa mambo, kama ulisikia hivyo, ujue ni uvumi usio na ukweli, hakuna kitu kama hicho, ukitaka zaidi kamuone wakili wenu..’nikamwambia.

‘Mimi mwenyewe ni wakili, nitafuatilia mpaka nione mwisho wake...’akasema

‘Sawa, kama unaona ni haki yako fuatilia, ...ila ni vyema ukawa  na uhakika na hicho unachokidai,..na ni vyema pia ukafuatilia na madeni  yake kwani kwenye faida, ujue pia kuna hasara zake, kuna madeni, ya marehemu hayo uliwahi kuulizie’nikamwambia.

‘Mimi sijauliza maswala ya madeni,....unanielewa....’halafu akakata simu.

NB: Tuhitimishe? sehemu hii ilihitajia marekebisho mengi..lkn hatukupata muda,....


WAZO LEO:Kunapotokea mzazi mmoja kufariki hasa wa kiume, kuna watu wanajitokeza kudai, mali wakisema na wao wana haki ya urithi, watu hawa wakati wa uhai wa merehemu, walikuwa hawaonekani, na zaidi inawezekana kabisa marehemu alikuwa akiumwa kwa muda mrefu, lakini hawakuwahi kufika, angalau hata kusaidia kidogo, hata angalau kutoa pole, mzazi huyo kafariki, watu wanajitokeza, wanadai urithi. Huo urithi, umetoka wapi, ukumbuke hiyo mali ilitafutwa na watu, na hawo watu ndio hawo waliohangaika na marehemu, wewe unakuja baadaye unadai, mali, hiyo mali kwako itakuwa sio halali ...ni vyema tukajua kuwa, kila penya faida kulikuwa na gharama zake.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Yasinta Ngonyani said...

Mirathi...Hakika inaleta vita na chuki nyingi sana katika familia. Mzazi mmoja akifa basi inakuwa ni vurugu tupo ....si ndugu wa marehemu bali hata watoto ....wengine wanadai hadi kijiko..Kazziiii kwelikweli...