Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, October 23, 2013

Mkuki ni kwa Nguruwe-15‘Mhh....kama mtoto wake anafanana na watoto wako, ina maana mtoto wa huyo rafiki yako atakuwa anafanana na mume wako au sio?’ akaniuliza, ni swali lililonifanya niwaze sana japokuwa sikuwa nimelipenda kwani lilikuwa likilenga fitina.

Kama kuna kitu nisichokipenda katika maisha yangu ni uzushi wenye lengo la ufitinashaji, hasa kwa watu wanaopendana na kuaminiana, mimi namwamini sana rafiki yangu, mimi namwamini sana mume wangu. Na rafiki yangu huyo tunapendana sana, nawatu wengu hawafahamu kuwa urafiki wetu huo hakuanza leo, ni kutoka shuleni, na zaidi ya hayo, nilimchukua rafiki yangu huyo akawa mikononi mwangu nikamjenga, akawa jasiri, na yeye aliniona mimi zaidi ya rafiki, aliniona kama dada yake,japokuwa kiumri tulikuwa sawa.
`Sasa iweje anifanyie hayo wanayohisi watu...’

Nilipoona kauli za huyo dakitari zinaelekea kwenye hiyo fitina, nikapanga kuzikataa na kama akiendelea kuongela hilo, nilipanga kumzimba mdomo, na ananifahamu nilivyo, ndio maana pale aliposema;

‘Mhh....kama mtoto wake anafanana na watoto wako, ina maana mtoto wake anafanana na mume wako au sio?

Nilifahamu ana nia gani kwngu, ndio maana nikamjibu kuwa, watoto wangu wanafanana pia na baba yao mdogo, kwahiyo huenda, shemeji yangu huyo akawa na mahusiano ya rafiki yangu, lakini kwa vile rafiki yangu hakupenda kuzalilika kwa kutembea na kijana mdogo, akaona anifiche,..

Hilo linawezekana pia, lakini pia kufanana kwa sura sio lazima kuwa mume wangu au mdogo wangu ndio baba wa mtoto wa rafiki yangu, ...inaweza ikatokea, ...mbona hayo hawayaoni....au kwa vile wana chuki na ndoa yangu ndio maana wanataka kuniharibia, ama kwa hilo hawanipati ng’ooooo

Nilijiona naandamwa na mawazo, wakati najiandaa kuondoka, na hata tulipokuwa ndani ya gari, akili yangu ilikuwa kichanganua mambo, ...na nilijipa tumaini pale niipokumbuka kauli yake ya kushindwa pale aliposema;

 ‘Yawezekana,.kuwa huenda mdogo wa mume wangu anaweza kuhusika na mtoto wa rafiki yangu.’ Na hili nililiwekea asimilia nyingi kwa vile kwanza mtoto huyo anafanana kabisa na sura zao, na mdogo wa mume wangu anafanana sana na kaka yake. Pili tangu rafiki yangu huyo ajifungue, mdogo wa mume wangu amkuwa kama ananikwepa...

Lakini kwanini alitoa hi kauli , ina maana kuna ukweli anaoufahamu, na kauli hiyo ilinifanya intake kumuuliza maswali mengi, nikaikumbuka ile kauli yake alivyosema;

‘Lakini mwisho wa siku ukweli utajulikana....’

 Je ni ukweli gani huo, ikawa ni fumbo jingine, ambalo liliachwa kichwani mwangu bila kupata majibu, na kwa hali hiyo nikajikuta nikikunja uso kwa hasira, sikupenda tabia ya namna hiyo, ya kunichezea, akili yangu, na kila tukiangalia na huyu jamaa nijakuta nimekunja uso kwa hasira, ndio maana akawa ananisihi mara kwa mara, na hata tulipokuwa kwenye gari aliniambia tena;

`Mpendwa,nakuomba tafadhali,...ukifika kwa mume wako, hakikisha unaonyesha tabasamu,....usije ukamuonyesha mume wako sura ya chuki, na mkiongea naye , kama atakuwa akikuuliza maswali yenye mlengo wa kuongelea mambo yatakayomuumiza moyo wake, hasa kwa tukio hilo lililopelekea kupatwa na haiyo jail,wewe uwe makini wa jinsi gani ya kumjibu , majibu yako yasimfanye ahisi vibaya, na kuona kuwa hujamsamehe,....’akasema

Kwa muda huo tulikuwa tumeshafika mapokezi na tulikuwa tunasubiria muda wa kuingia, kwani walisema madakitari wapo kwenye shughuli zao, tuwape muda....

‘Hivi kusamehe huko ni kwa kuigiza, maana hadi sasa, hata sijui namsamehe kwa kosa gani...’ nikasema.

‘Kiukweli kwahivi sasa inabidi ufanye hivyo, kumbuka kupona kwa mume wako,pamoja na tiba anayopata, lakini kwa kiasi kikubwa, atahitajia sana faraja, hasa kutoka kwako, ....sijui kosa alilofanya, lakini inaonekana kwake ni kubwa sana, ...kwahiyo uamuzi ni wako, kama unataka mume wako apone kwa haraka fanya hivyo, igiza kuwa umemsamahe, kama hujafikia uamauzi wa kumsamehe....’akasema

‘Kwangu kumsamehe sio tatizo , tatizo ni kuwa, mimi natakiwa kumsamehe kwa kosa gani...mbona hutaki anieleze kosa alilolifanya, kwani siku ile yeye mwenyewe alionekana kutaka kunielezea, wewe ukamzuia kiujanja...sijui kwa maslahi gani’nikasema.

‘Kosa hilo mimi na wewe hatulifahamu, kwahivi sasa halijafahamika, ni kukisia tu, hata sisi hatutaki kumshinikiza aeleze ilivyokuwa, hata askari waliokuja kuchukua maelezo yao tuliwaambia wasimuulize chochote kuhusu ilivyotokea,..bado muda wa kumuuliza hayo,....ipo siku yeye mwenyewe atakuambia, na mimi siku ile nilifanya hivyo kwa masilahi yenu, hasa ya afya yake...ila kimtazamo wangu, nahisi yeye anafahamu kuwa wewe unafahamu hicho alichokitenda, au kosa alilolifanya, ...’akatulia.

‘Mimi nitafahamuje hayo mambo ya kufikirika, maana hayo yote ni dhana, tena dhana potofu, na kama ungelimfahamu vyema mume wangu, na hata huyo rafiki yangu usingelikimbilia kujenga dhana kama hizo,....ndio hapo siawaelewi,..eti nafahamu, nitafahamu vipi, halafu nihangaike kutafuta ukweli’nikasema.

‘Ok, kama hufahamu lolote ni bora iwe hivyo, na mwanzoni nilikushauri tuutafute ukweli, lakini kutokana na hali ilivyo, mimi ningelikushauri usahau hayo yaliyotokea, na uangalia mambo ya mbeleni, ...kwanza cha muhimu,tuone kuwa mwenzetu huyu, anaondoka kwenye hiyo hali aliyo nayo...’akasema.

‘Hilo ndilo la muhimu, ...ila nataak kujua , na sitaacha kutaka kujua, ni kitu gani kilitokea, hadi ikafikia hapo, na je hizo dhana zenu potofu zina ukweli gani,...nataka kuyajua hayo ili nafsi yangu itulie, hamjui jinsi gani ninavyopata taabu kuwaza jambo lisilojulikana, na jambo lenyewe linaonekana sio jema kawa jinsi ninavyowaona, kwa jinsi mnavyoigiza, na sijui mnataka nini...’nikasema.

‘Kitu kimoja ufahamu ,kama mtu anafikia kukuomba msamaha, ina maana jambo hilo lina uzito fulani, kwake kinafsi na kwako pia,....japokuwa ukimtendea mwenzako jambo lisilopendeza, hata kama ni dogo kiasi gani ni vyema kiuungwana ukamuomba mwenzako msamaha,...’akasema.

‘Mimi ninachotaka kujua ni jambo gani lilitokea hadi mume wangu akataharuki kisai hicho, na je linahusiana vipi na rafiki yangu,... maana kila tukiongea na wewe unapenda kumchomekea rafiki yangu, kama vile kuna kitu kimefanyika kati yao wawili, kitu ambacho nakiona hakipo,na kama rafiki yangu huyo angelikuwepo, lingekuwa ni rahisi kwake kuligundua , namfahamu kikazi, na sijui kitu gani kimemkumba, hadi kubadilika kwa muda mfupi, sijui, na hilo tena linakuwa tatizo jingine, nahitajika kulijua, maana yule nilikabidhiwa mimi na wazazi wake, sipendi aje kupata matatizo...’nikasema.

‘Inaonekana unamwamini sana rafiki yako, hujui kuwa rafiki yako anaweza kuwa adui yako mbaya kuliko unavyodhania,...maana yeye anakufahamu udhaifu wako, kwahiyo akitaka kukufanyia ubaya anaweza na ushindwe kufahamu...maana unamwamini, ubnakuwa kiziwi na kipofu mbele yake, ...ukipenda hata chongo utaliita ni kengeza..’akasema.

‘Acha fitina...huniwezi kwa mtaji huo..hilo niachie mwenyewe...nafahamu kabisa hakuna tatizo kubwa kwa watu hawo, huenda ni tatizo la ...mambo ya kibiashara, au...mh, siwezi kusema maana jambo gani linaloweza kuwaunganisha hawa wawili....na kwanini niwashuku wapendwa wangu hawa ubaya, hapana,...hizo ni fitina tu’nikasema

‘Kama una uhakika na hilo, hakuna shida, ila sisi kama madakitari, tunajaribu kukwepesha jambo lolote la kumkwaza mgonjwa, ....wakati kama huu sio wa kukaa na kulumbana naye kwa hayo yaliyotokea, upo muda utafika yeye mwenyewe ataamua kukuambia, hilo ni moja, na la pili, kama kuna tatizo ambalo linahitajia maamuzi, uchunguzi, jaribu kutumia hekima, maana kila mwanadamu hukosea, huenda kosa hilo, ni dogo sana ukilinganisha na makosa uliyowahi kuyatenda....’akasema.

‘Ina maana wewe hujui kosa alilolifanya rafiki yako, kama kweli lipo kosa, sijui ni kosa gani maana kama ananiomba mashamaha, naona lipo kosa, ...hebu sema ukweli wako, maana kama utanificha na siku nikaja kugundua, basi wewe nitakuweka kwenye kundi la watu wasio na umanifu kwangu, nitakuchukulia wewe kama adui yangu, anayenivizia kwa nyuma, ..na nakuambia ukweli, kama kuna jambo nzito,.. sizani kama nitakuja kukusamehe, unanifahamu nilivyo...’nikamweleza.na yeye akatabasamu, na bila wasiwasi akasema;

‘Kama ningelikuwa nafahamu ni kitu gani, ningelishakuambia, unaifahamu ninavyokujali,...lakini pia natawakiwa kuwa makini, kwani wote nyie ni mar na kwanini nisimame upande wa mume wako, kuliko kwako, ...mimi nakupenda sana wewe, na yote haya nayafanya kwa vile najali, nakujali na nitendelfiki zangu,...na inavyoonekana wewe unawaamini sana wenzako kupita kiasi,....na wameshakusoma udhaifu wako....'akasema mimi nikitabasamu kwa dharau.

'Mimi najaribu kukuweka sawa ili uzindukane, maana mimi nakujali sana wewe,na nakuahidi kuwa sitakubali upate shida wakati mimi naona, wakati mimi nipo hai....unakumbuka niliwahi kukuambia hilo kabla na hata baada ya wewe kunikataa...’akasema akinisogelea, na mimi nikarudi nyuma kumkwepa.

‘Unataka kufanya nini..’nikasema nikigeuka huku na kule kuangalia kama kuna watu wanaotutizama, lakini niliona kila mtu na hamsini zake, huwa sipendi jinsi gani huyu jamaa anavyofanya tukiwa karibu naye, ....

‘Sikiliza nilihskaukanya hii tabia yako ya kujiweka karibu karibu na mimi, kunishika shika, sitaki, ..sipendi maana watu wanaweza kujenga dhana mbaya ambayo haipo...sipendi, acha kabisa, kwani kuna siku nitakuadhiri vibaya sana...’nikasema kwa ukali.

‘Nimekuelewa mpenzi, ...mpendwa, samahani....nafaya haya bila kujijua,...’akasema.

‘Na mimi sio mpenzi wako..kumbuka hilo,...haya endelea na fitina zako, ulikuwa unasemaje..?’ nikamuuliza nikisawazisha uso wangu, maana nilishabadilika kwa hasira.

‘Unakumbuka nilivyokuwambia siku ile, tukiagana,siku ambayo sitaweza kuisahau maishani, unakumbuka nilivyokuambia siku ile, ...kuwa nipo tayari kufanya lolote kuhakikisha kuwa hakuna atakayekuumiza, ...japokuwa ulinikataa,na kusema nisikufuate fuate kwenye maisha yako, lakini bado moyo wangu upo kwako...ndio maana bado natunza ahadi yangu’akasema na mimi nikajikuta nacheka kwa kebehi, nikasema;

‘Acha zako hizo, wewe sasa ni mtu mzima, una mke na watoto hutakiwi uwe na mawazo kama hayo, ina maana mpaka leo hujakubali ukweli, kuwa mimi nina mume ninayempenda zaidi yako, hata kama nilikupena kablsa, hata kama sasa nakupenda, nilikupenda,na nakupenda kama rafiki , ila ujuekuwa kupendana kuna kuzidiana, mume wangu nampenda zaidi yako wewe, ..tuache hayo yaliyopita maana hayawezi kusaidia lolote, hizo ni zilipendwa, hebu nikuulize ina maana mkeo humpendi?’ nikamuuliza.

‘Mkewe wangu nampenda, nilishakuambia hilo, nampenda tenasana, nampenda kama mke wangu, lakini wewe ndiye niliyekupenda kabla, na pendo la mwanzo, halilinganishwi na pendo la mbadala, maana ilibidi nimuoe yeye kwa vile wewe ulishanikataa, sikuwa na jinsi,na sikuwahi kukukataa hata siku moja, ....kiukweli wewe hujaondoka kwenye nafsi yangu..nilijaribu sana kukubembeleza, nilijaribu sana kukuondoa kwenye nfasi yangu, lakini mmh, mungu mwenyewe ndiye anayefahamu , na ni kweli  ....ilifikia wakati natakiwa nikakubali ukweli, lakini ilinitesa sana.’akasema na nikajikuta nacheka.

‘Hivi hayo maneno unaweza kuyaongea mbele ya mke wako, au mbele ya mume wangu?’ nikamuuliza nikimkazia macho na yeye akatabasamu na kuangalia pembeni, akasema kwa unyenyekevu.

‘Mke wangu nilishamwambia hayo, anayafahamu sana, na nashukuru mungu kuwa yeye ni mwelevu, na kama kuna mtu ambaye aliweza kunisaidia kuiponya nafsi yangu, iliyokuwa imeathirika, basi ni mke wangu, yeye alichukua nafasi ya udakitari wa kulitibu jereha ulilolisababisha wewe..., aliweza kunisaidia na kuijenga nafsi yangu ikubali hali halisi kuwa wewe sio wangu tena, wewe ulishakuwa mke wa mtu mwingine na mke wa afiki yangu, ...namshukuru sana kwa juhudi zake hizo,...na kiukweli hata kama angelikuwepo hapa angelithibitisha hilo...namshukuru sana mke wangu.’akasema kwa sauti ya huruma.

‘Mhhh, pole sana...’nikasema huku nikiguna kwa kebehi na nilipotaka kusema neno yeye akasema kwa haraka haraka;

‘Hata ,mume wako mara kwa mara tukiongea huwa namwambia hivyo japokuwa tunaongea kwa utani, ....niliwahi kumwambia kabla kuwa kama itatokea akakuumiza, kama atafanya makosa, basi ajue mke wake nitamchukua mimi....ni utani wenye ukweli ndani yake’akasema.

‘Usinichekeshe, ina maana mke wako mnaishije, kama moyo na nafsi yako ipo kwangu, kuna upendo gani kati yako na mke wako, kama muda wote unanifikiria mimi..na haya tusema mume wangu kaniumiza, au tukaachana utaweza kunioa mimi na kumuacha mkeo, au ndio nitakuwa nyumba ndogo?’ nikamuuliza.

‘Sijafikia huko zaidi, sijawazia kufanya hivyo,....kukupenda kwangu sio lazima nimuache mke wangu, kukupenda kwangu kupo moyoni, ..nafikiri unafahamu hivyo, na siombei uachike,japokuwa ikitokea hivyo na nikakuoa mimi ningelifurahia sana, lakini  sijasema nimuache mke wangu au wewe kukufanya nyumba ndogo,....’akasema.

‘Sikuelewi....una maana gani., na sihitaji kukuelewa, maana hilo halipo, na halitakuwepo...’nikasema.

‘Sio kwamba muda wote nakufikiria wewe..hapana hilo ni jambo lipo, kuwa nakupenda, lakini sio kwamba ni jambo la kunifanya nisimpende mke wangu, nampenda sana mke wangu, kwani pamoja na yote hayo, alikubali ukweli, akanisaidia, na anaendelea kunisaidia kuponyesha jeraha uliloisababisha wewe....’akasema.

‘Mhh, usinitwike, mzigo nisiostahili, mimi sijasababisha jereha lolote kwako, kama ni jeraha umejisababishia mwenyewe, maana hatukuwa tumeoana, tulikuwa marafiki tu, na unakumbuka wakati ulipotaka kunichumbia nilikuwambia nini, kuwa mimi bado sijafikia umauzi wa kuwa mchumba au mke wako, nahitajia muda wa kufikiria, sikuwa na malengo ya muda mrefu na wewe,...na baadaye nikaja kukuambia kuwa nimempata ninayempenda zaidi yako, je ulitaka tuishi kwa kudanganyana...?’ nikamuuliza.

‘Hilo siamini,..eti ulikuwa hunipendi, , huwezi kunidanganya mimi, ninafahamu fika ulikubali kuolewa na mume wako, kwa nia ya kulipa fadhila, moyo na nafsi yako ilikuwa kwangu, hilo nina uhakika nalo, ila kwa vile wewe una tabia yako, kuwa ukitaka jambo liwe, huwa hugeuki nyuma, hata kama litakuleta madhara, wewe unataka ulifanye tu, au ulipate,hata kama litakuumiza, sio vizuri hivyo huoni sasa mnavyoishi, hamna raha, tusidanganyane ndoa yenu haina raha, na kosa ni maamuzi yako ya haraka, ya kujifanya mwema, eti unalipa fadhila.....’akasema na mimi nikatabasamu na kusema.

‘Hayo yamepita tugange yaliyopo na yajayo, ambayo ndiyo ukweli wenyewe, wewe una mke wako, na mimi nina mume wangu, tusiingiliane, na tusiharibiane ndoa zetu, heshimu ndoa yako, na mimi niache niheshimu ndoa yangu..hayo ya kusema hatuishi kwa raha, ni hisia zako potofu, na kila ndoa ina matatizo yake, sio kwamba ndoa yangu ni ya kimiujiza, sisi ni wanadamu ....’nikasema.

‘Hilo nalifahamu, lakini sitakubali mtu akuumize, hilo ni ahadi yangu, hata kama hutaniamini hivyo, hata kama hutakubaliana na hilo, hilo ni nadhiri kwenye nfasi yangu, hadi naingia kaburini,hata kama hutakuwa mke wangu, lakini mapenzo kwako yapo pale pale ...’akasema na mimi nikajikuta nikimwangalia kwa mashaka.

‘Hivi wewe mwanaume una akili kweli....sikiliza, wewe ni msomi, dakitari, nilitarajia wewe kunionyesha njia na masimamo wa mambo kama haya, ambayo tunahitajika kukubali ukweli, umesahahu kazi yako eehe..unajiona wewe ni bora, sio wale, au yale unayoyashauri kwa wenzako, ukumbuke kuwa na wewe ni mwanandoa na una ndoa yako, unavyowashauri wengine, na wewe ujishauri pia.’nikasema.

‘Sijasahau mpendwa, hata nikiwa dakitari, ubinadamu na utashi wa kupenda upo pale pale...nashukuru kuwa na wewe unalikubali hilo, kuwa ukiwashauri wenzako na wewe ujishauri hivyo hivyo,....ukumbuke ulismhauri nini rafiki yako....’akasema na kuniangalia machoni.

‘Kwani nilimshauri kitu gani kibaya..?’ nikauliza kwa mshangao.

‘Kama sio kibaya kwanini unapata shida...kwanini unataka kujua baba wa mtoto wake ni nani, kwanini haya yanatokea, ...nalitumai ungelikaa kimiya na kumpa mwenzako hongea kwa kufuata ushauri wako...’akasema.

‘Kwani mimi nimefanya nini kibaya, kwani nimemshutumu kwa hayo aliyoyafanya, ...wewe hujui tu, mimi nilikuwa nye bega kwa bega, kumpa hongera, na mengine ya kutaka kujua baba yake, nafanya hivyo kwa vile mimi ninakaa naye, ni kama mzazi wake, nataka kumjua ili nijue jinsi gani ya kumlinda, hakuna tatizo hapo...’nikasema.

‘Ok, tuyaacha hayo,, ila nakuomba unisikilize kwa makini, fanya kama nilivyokuambia,kama kweli unampenda mume wao, kama kweli unampenda mume wako apone haraka, fanya kama nilivyokuambia, ni bora uigize kuwa huna chuki, huna kinyongo naye huyajui yoyote yanayomzunguka na hayo aliyoyafanya, yapotezee, kuliko kuonyesha hiyo hali ya kukasirika, ...wakati kama huu anakuhitajia sana...’akasema.

‘Nimeshakuelewa, tunaweza kwenda...maana inachukua muda, ina maana hawo madakitri hawajamaliza kuwapitia waginjwa?’ nikamuuliza.

‘Tunaweza kwenda, ila hilo ni muhimu, kuliko kwenda kumuona na ukawa ndio chanzo cha kumfanya asipone, kwa hivi sasa yupo kama kapagawa, ukimuuliza jambo anakuangali tu machoni, haongei kitu, na docta wake kasema tumpe muda, ila akashauri wewe uje, ili tuone kama itasaidia, kila mtu anajiuliza je kuna kitu gani aliongea na huyo rafiki yako, mimi ninaona wewe ndiye unayeweza kuibadili hiyo hali, kama kweli unampenda mume wako....’akasema.

‘Kama nisingelikuwa nampenda, nisingelikubali kuolewa na yeye, na kuzaa naye watoto wawili, nampenda sana mume wangu na nitaendelea kumpenda, hata kama nyie mafitina mtaendelea kuchochea chuki na fitina zenu...’nikasema huku nikitembea kuelekea huko hospitalini na huyo docta alikuwa bado kasimama,kama vile haniamini.

‘Sawa nimekusikia, ila nazidi kukusisitizia, kuwa....kama hutaki mume wako apone haraka endelea kujenga sura ya chuki,sahau kabisa kujenga hiyo sura ya kuonyesha hasira na chuki, kwani kosa dogo, mbele ya mume wako, linaweza kuleta madhara makubwa sana, kwa sasa hivi akili na ubongo wake, hauhitaji mzigo wowote wa mshituko,au shinikizo la kumsononesha, usipofuata ushauri wangu.....utakuja kujilaumu mwenyewe, usije ukasema sikukukanya ...ni muhimu sana..’

Maneno hayo yalinifanya niwe kwenye mtego, na ulikuwa mwiba nisioweza kuutoa, nikawa nagugumia kimoyo moyo, japokuwa nilitaka kufanya jambo, japokuwa nilikuwa nataka kujua ukweli,kuna nini na kwanini ananiomba masamaha,....je ina maana nife na tai shingoni, hapana, kuna namna, ama kutoka kwake, au kutoka kwa mtu mwingine, ni lazima nifahamu ukweli,..nikakumbuka.

‘Ni lazima nimuona mdogo wake...huyu anaweza kujua jambo nikasema, na wakati huo tulikuwa tunaingia chumba alicholazwa mgonjwa...

NB:Je nitaweza kuvumilia....


WAZO LA LEO: Tunapopenda, tusiwe tumependa kupitiliza, na hata kusahau udhaifu wetu wa kibinadamu , mwenzako anaweza kukosea, mkosoe kwa hekima, usiogope kuwa ukimkosa mtakosana na wewe ukaamua kukaa kimiya, huko sio kupenda, ni kupondana kwani mwisho wa siki likahar elezaneni ukweli, japokuwa ukweli unauma, ...ila kwaibika jahaz mtazama wote. Kama mume au mke wako yupo kwenya hali mbaya ya ugonjwa, au yupo kwenye matatizo, basi uwe na hekima, usikimbilie kuhamaki, kulaumu, kuhusiana na hilo kosa, cha muhimu ni kuvuta subiri , hadi kuwe na wakati muafaka.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Pam said...

Huyu mdada anatia huruma kaingia shimo alilochimba mwenyewe..

Anonymous said...

[url=http://effexorgeneric.eu/]effexor generic[/url] [url=http://cleocin.in.net/]cleocin topical[/url] [url=http://colchicine.mom/]colchicine[/url] [url=http://buytadalafil.accountant/]tadalafil[/url] [url=http://buy-zithromax.cricket/]zithromax pack[/url] [url=http://buy-nexium.in.net/]nexium 20[/url] [url=http://cleocin-gel.mom/]cleocin gel for acne[/url]