Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, October 31, 2013

Mkuki ni kw Nguruwe-19


‘Tutakuja kuongea hayo siku nyingine....kunjua huo uso wako please’akasema rafiki wa mume wangu

Tuendelee na kisa chetu....

*******

Ni kweli, muda ule nilikuwa nimeshakunja uso kwa hasira, na kingefuatia hapo ni maneno makali, lakini nikakumbuka onyo la rafiki wa mume wangu, na kunifanya nipitishe mikono usoni kama ninafuta fumbi usoni,...sikutaka nifanye makosa yoyote kwa mume wangu,....na katika maisha yetu, tulikubaliana kuwa mmoja akiumwa, mwingine ahakikisha anakuwa bega kwa bega, kumuuguza mwenzake, bila kujali kuwa tatizo hilo limetokana na nini, hata kama kuna unjikati wa mkataba, kwa hali kama hiyo mkataba unawekwa pe,beni kwanza.

Siku ile alipokuja rafki wa mume wangu akakatisha mazungumzo yetu, ilikuwa siku iliyofungua ukurasa mwingine, na kunifanya niwe mt wa kuwaza-waza sana, na tatizo ni kuwa mimi siwezi kuvumilia,...nikiona jambo linakwenda sivyo ndivyo, ni lazima nilifanyie kazi, ..na nitakuuliza tu,lakini mume wangu ni mgonjwa, siwezi kumuuliza, nikimuuliza nitasababisha makubwa ...iakbidi nimeze ndoana.nakutulia kimiya

Siku nilitaka niongee na huyo rafiki wa mume wangu, lakini alikuwa mjanja, alishagundua kuwa nataka kuongea naye, katika maswala ambayo hakutaka kujihusisha tena moja kwa moja,...na hata ilipofika muda wa kuondoka, alitafuta njia ya kunibana, akasema;

‘Sasa shemeji wewe bakia na mume wako, kwani kachoka, na ni bora ukae naye karibu hadi atakapopata usingizi..sisi acha tuondoke, na haihitaji kutusindikiza, ni muhimu sana ukawa karibu na mume wako kwa sasa..hii ni hatua nzuri, mume wako anaanza kujituma, viuongo vyote sasa vina mawasiliano...’akasema huyo rafiki wa mume wangu.

‘Sawa..hakuna shida...’nikasema

‘Rafiki yangu jitahidi sana kufuata masharti, jitahidi usiongee sana, au ukawa unafikiria sana, kwepa sana mawazo yanayokukwaza, ....ukifikiria sana, utajikuta unapata matatizo mengine makubwa, na utasababisha usipone haraka, na ukichelewa kupona, mimi nitamchukua zilipendwa wangu....’akamtania rafiki yake.

‘Thubutu...ukija kesho utanikuta natembea,..’akasema na wote tukafurahi, lakini mimi moyoni nilikuwa na yangu, nilikuwa nawaza kupita kiasi, huku nikijaribu kutabasamu, tabasamu la kubandika ...huku maneno ya docta yakiniumiza moyo wangu

‘Ina maana unanilaumu mimi, ...unanichekesha, kweli, ushindwe mwenyewe kuihudumia ndoa yako halafu uje kuwalaumu watu wengine, umesahau mara ngapi ninakuja kuongea na wewe na kujaribu kukuelekeza halafu wewe uannitolea nje, na hata kuhisi kuwa huenda nimetumwa na wazazi wako kuja kukuharibia ndoa yako, umeshahau hilo eeh, sasa unaona yamekukuta, unataka kunilaumu mimi...

Ina maana hata huyu ambaye amekuwa akijinadi kuwa ananipenda, na yeye pia sasa ananitupia lawama mimi, kuwa nimeshindwa kuihudumia ndoa yangu....hivi ni kweli au hawa watu wanatafuta njia ya kuona kuwa mimi na mume wangu hatupendani, au kuna kitu kingine kinatafutwa hapa....hapana sikubali, sikubali kabisa, ni lazima niwaonyeshe watu kuwa nilikuwa na nia njema, na mimi sijawahi kuvunja mkataba wetu wa kifamilia,....hata hivyo kama kuna lolote baya limetokea ni lazima nilifahamu, cha muhimu, lisije likagusa mkataba wetu.

Wazo la kuwa mwenzangu atakuwa kavunja mkataba, lilianza kugusa hisia zangu, nikawa naanza kupungua ila hali yangu ya kumuamini, nikaanza kuguswa na maneno ya watu, na hata kali ya mume wangu ukaniashiria kuwa kuna tatizo, na tatizo lenyewe sio dogo, na hata kama nitasamehe, lakini kuna kitu kinatulinda, kuna kitu tulikubaliana, na hayo makubaliano yapo kwenye maandishi,...mkataba wa hiari kati yangu mimi na mume wangu.

Sio mkataba wa ndoa,...ndoa ni sehemu mojawapo katika huo mkataba, tulikuwa na mkataba mkubwa unaoelezea kila kitu, ..kuna nakala ipo chumbani, lakini sikutaka kuigusa kwa muda, huo,..nikaona kesho yake niende ofisini....

                 *****

Kesho yake nilipofika ofisini, kwanza nilihangaika na maswala ya kikazi, ambayo yalinihitaji mimi, na nilipomaliza, nikawa nataafkari kitu gani kingine nifanye kabla sijaondoka. Sikuwa na haraka sana kwani hali ya mume wangu ilikuwa inaendelea vyema,na msaidizi wangu alikuwa akimuhudmia vyema kabisa,na kama kungelitokea chochote, nilimwambia anipigie simu haraka.....

Siku hiyo nilijiona sina raha kabisa, na ilitakiwa niwe na raha, maana mume wangu hali yake inaimarika, keshaanza kutembea kidogo kidogo....na alionekana kuwa na raha, kupita kiasi kama vile amesikia jambo kubwa ambalo analitegemea, ..sikutaka kumdadisi, sana, na nilianza kutokumuuliza maswali mengi, maana kila tukiongea, tunakimbilia kule kule, kwenye mambo yasiyohitajiak kuongea kwa wakati huu.

Kila siku nilikuwa nagundua mambo, na kunifanya nianze kugeuza fikira zangu nyuma, na hata akili yangu ilikuwa imeshaanza kugeuka, na kuhisi kuwa kuna tatizo kubwa tofauti na nilivyokuwa nikiwazia,..na tatizo hilo huenda ni katika vipengele vikubwa katika mkataba wetu...

Katika mkataba wetu wa kifamilia,....kuna vipengele vikubwa, ambavyo tuliviainisha na kukubaliana kuwa kukitokea kuvunjika kati ya kimojawapo, kutakuwa hakuna msamaha, na kimojawapo ni kukiukwa kwa masharti ya ndoa...kuna ufafanuzi wake,...ambao tulikubalia wote wawili, hakuna ujanja kwa hilo, lakini sikutaka klichukulia hilo kwa haraka, nikataka kwanza niwe na uhakika na jambo lenyewe, lakini kwa hali ilivyo huenda ikachukua mud asana kuupata ukweli, japokuwa nimesikia kuwa rafiki yangu anakuja, na yeye ndiye tegemeo langu la kuupata ukweli.

Lakini kuhusu mkataba, ni kati yangu na mume wangu, na mwanasheria wetu, hili lilifanyika kisiri, na halikuwa linajulikana kwa mtu mwingine yoyote,...na ndio maana nilipofika ofisini nikataka kujirizisha kwa kusoma baadhi ya vipengele kwenye huo mkataba wetu na nilitaka niwe na uhakika, wa ufafanuzi wa kimojawapo kwenye vipengele vya ukiukwaji wa msharti ya ndoa...hapo nikakumbuka hilo jambo muhimu la kuusoma mkataba wetu kabla sijarudi nyumbani.

`Yah, sasa naweza kuupitia mkataba wetu kidogo, kabla sijaondoka,, .....’ nikasema kwa sauti.

Nilipokumbuka hilo swala la mkataba wetu wa kifamilia, niliinuka kwa haraka kwenye kiti, nikasimama kwanza nikajinyosha, sikuwa na haraka, sikuwa na jambo jingine muhimu la kufanya,...kwanza nikapitisha mkono wangu kichwani nikiwaza kwanini nisumbuke kuangalia mambo ya mkataba, wakati sina uhakika na hilo lililotokea kwa mume wangu, ...

‘Ninachotaka ni kuuangalia na kusome baadhi ya vipengele,...sio lazima kuwe na uvunjwaji, lakini ni muhimu kujikumbushia,..’nikasema.

Nikatembea hadi kwenye kabati langu maalumu, kabati hilo, huwa naweka kumbukumbu zangu muhimu, na hakuna mwingine mwenye mamlaka ya kufungua hilo kabati, ..na hata mimi mwenyewe ni muda mrefu sijalifungua hilo kabati, maana vyote vilivyopo humo ndani, sio mambo ya kila siku ya kikazi. Na humo niliweka nakala yangu ya mkataba wa kifamilia, mkataba uliojumuisha mambo yote, ya mali zote tulizo nazo kwenye familia yangu, mambo ya kijamii, kama ndoa, watoto...ni mkataba muhimu sana, japokuwa 
tulishaanza kuusahau.

            ********

Kabla sijaolewa, nilikuwa na ndoto ya kuwa na mkataba wangu na mume wangu, niliona kuna umhimu wa kuwa na kitu kama hicho,..ilikuwa kama fikira tu, na baada ya ndoa nikasahau, sikuona umuhimu wake tena, lakini siku ile,....sijui ilikuwaje....hapo nikakumbuka jinsi gani nilivyoingiwa na wazo tena la kuwa na mkataba wa kifamilia.

Nakumbuka siku ile baada ya kuongea na wakili wetu, ambaye tulimuhusisha pia na mambo yetu ya kinyumbani, baada ya kuongea nayeye na kumuelezea wazo langu hilo la siku nyingi, yeye aliniunga mkono, na kusema wazo hilo ni muhimu sana, lakini wanafamilia wengi wanaliogopa,...lakini halina shaka, kama watu watakubaliana.

‘Mimi napendelea kuwa na kitu kama hicho kwenye ndoa yangu na mume wangu....’nikasema‘Basi kama mtakubaliana, mimi nipo tayari, na nitawatengenezea mkataba mnzuri sana, na wenyewe mtaona jinsi gani utakavyowasaidia, ...ongea kwanza na mume wako mkubaliane, maana hilo ni swala la nyie wawili...’akasema.

Nikahamasika,na jambo hilo kuwa tuwe na mkataba wa kifamilia ambao utajumuisha mambo yote ya familia yetu, kuanzia ya kifamilia hadi ya mali zetu,  na hili nililifanya makusudi, ili hata nisipokuwepo, au mume wangu asipokuwepo kusije kukatokea mambo mengine ya kuja kuidhulumu familia yetu.   baada ya kuwaza sana hilo, nikaona nimwambia mume wangu, nakumbuka sana siku ile, maana nilikuwa kwenye uja uzito wa kwanza ..

Na jioni wakati tumepumzika, nikaona niongee na mume wangu, nilikuwa nipo kwenye mapumziko ya kujiandaa kwa uzazi wa kwanza, sikuweza kufanya mambo mengi, na hata zile pilika pilika za kila siku, zilikuwa zimepumzishwa, ....

‘Mume wangu kuna kitu nataka nikuambie...’nilimwamba siku moja, wakati huo nina uja uzito wa mtoto wa kwanza, na yeye akanisogelea na kushika shika tumbo langu, huku akitabsamu , akasema;

‘Usiniambia siku zinakaribia, maana nina hamu sana ya kumuona mtoto wetu huyu’akasema huku akiendelea kushika shika tumbo langu, na mimi nilimwangalia kwa upendo, maana siku mwanzo, hakuna mtu angeniambia kitu dhidi ya mume wangu nikakisikiliza, nilimpenda sana, na nilikuwa namuamini sana.

‘Usiwe na shaka mume wangu, siku yoyote kuanzia leo tunaweza tukaitwa baba au mama fulani, lakini sio hicho nilichotaka kukuambia.....’nikasema

‘Mhh, niambie...mama watoto wangu’akasema huku akiendelea kushika shika tumbo langu na mimi nikatabasamu, maana hata mtoto sijapata nimeshaanza kuitwa mama watoto. Kweli ndoa ina raha yake siku za upendo.

‘Kuna kitu siku nyingi nilikiwaza, na hasa baada ya kuona mimi na wazazi wangu tunaanza kuelewana, lakini nikahisi jambo, ...sina nia mabaya na wazazi wangu, au jamaa zangu, au jamaa zako, lakini haya hutokea sana katika  dunia hii, na sisi kama wazazi inabidi tuwe makini kwa hili...’nikaanzia mbali.

‘Kwani kuna tatizo kutoka kwa wazazi wako tena?’ akauliza.

‘Hapana, hili ni kati yangu mimi na wewe, na familia yetu inayokuja, hatujui tutapata watoto wangapi, na hatujui watakuwa wakike na wakiume wangapi, ....hilo mimi sitaki kuweka mipaka, au wewe unasemaje?’ nikamuuliza.

‘Mke wangu, umeshaanza kuwazia kupata watoto wengi, wakati siku kadhaa nyuma, wakati unahangaika na mauimvu ya tumbo na kuchoka, ulisema waziwazi kuwa taabu unayoipta hutaki tena kubeba mimba..’akasema.

‘Hiyo ni kawaida,mwanzoni mimba inatesa, lakini inavyozidi kukua, unazoea, japokuwa mmh, yasikiane tu haya mambo, nyie wanaume, mngeifahamu tunavyopata taabu, mngetuunga mkono, mngetuonea sana huruma ....lakini hata hivyo sipo huko kwenye kuzaa kwangu, nipo kwenye baada ya kuzaa, maisha yetu , mali zetu, na mipangilioa ya kila siku, maana hilo ndilo muhimu sana....’nikamwambia.

‘Mhhh, mhh, niambie....’akasema huku akikaa vizuri na kuniangalia machoni.

‘Nataka tuwe na mkataba wa kifamilia...’nikasema na yeye akawa kama anashituka halafu akapepesa pepesa macho.

‘Mkataba wa nini tena,..tuna ndoa, cheti cha ndoa ni kila kitu, unahitajia mkataba gani tena, huniamini au kuna nini umekigundua dhidi yangu, familia yangu au yako?’ akaniuliza kwa mashaka.

‘Niliongea na wakili wetu wa kampuni,.....ambaye kama unavyojua, anashughulika kwenye kampuni zote mbili yangu na ya kwako pia, mimi sina lengo la kuingilia kampuni yako saana, lakini hili la mkataba ni kwa ajili ya mali zetu zote, zikiwemo kampuni zetu,  ili kusije kukatokea sintofahamu baadaye....’nikasema.

‘Mhhh, okey, niambie maana mpaka sasa sijakupata vyema, na hata hivyo huyo wakili hajaongea na mimi... kwahiyo sijui unachotaka kusema’akasema.

‘Ni hivi, katika maswala yote ya mali, kama hakuna matatizo, hakuna shida, lakini kukija kutokea matatizo, watu , binadamu tulivyo, cha kwanza kukimbilia ni mali, hutaamini, watu mlikuwa mnapendana, mnasaidiana, ni marafiki, lakini kukitokea mfarakano kidogo tu, wote akili na macho ni kwenye mali...na huenda watakaotaka kuingilia mali kwa pupa ni wale ambao hawajui kabisa hizo mali zimetoka wapi...zimepatikanaje,.....ndio hulka ya binadamu, kuangalia kwenye kupata na kutumia, sio kwenye kuhangaika....’nikasema.

‘Mke wangu mbona unanitia wasiwasi, ina maana unaogopa kuwa ukienda kujifungua ....unaweza ukafa, au unawaza nini, mke wangu kuzaa ni kawaida tu, hutapata lolote baya...hutakufa bwana, usinitishe..usinitie wasiwasi na majonzi, hakuna shida, huna matatizo yoyote, docta kasema sasa kwanini unakuwa na wasiwasi’akasema.

‘Mimi siongei hili kwa vile nakwenda kujifungua, hapana, naliongelea hili kwa ujumla wake, ni jambo la maisha yetu,...na ukumbuke mume wangu, sisi kama wandamu, hatuna mamlaka na mungu, kuwa nitaishi muda gani au nitakufa lini,...unaweza wewe ukatangulia, mimi nikabakia, au mimi nikatangulia wewe ukabakia, hayo ni mambo ya kawaida katika maisha yetu ya kibinadamu.

'Lakini hata hivyo ni vyema tukawa na utaratibu mzuri tu, tukajiandaa kwa lolote lile, hata kama tupo hai, bado mkataba unaweza kutusaidia katika maisha yetu, tukawa na utaratibu mnzuri tu kwa nia njema,...na hatuombei, maana sisi ni wanadamu,kama kutatokea mfarakano wowote, makataba huo utakuja kutusaidia...’nikamwambia.

‘Sawa..kwahiyo ulikuwa unataka kusema nini, ..tuwe na mkataba, kuhusu nini, ?’ akauliza akishika kichwa, nahisi alikuwa akiwazia mbali, na mimi nikamwambia;

‘Eheeeh, sasa tulia nikuambia, mimi niliongea na wakili wangu, akanishauri kuwa sisi ni wanandoa na pia mungu katujalia tukawa na kampuni, na bahati nzuri tuna kampuni mbili, kampuni ninayomiliki mimi , ina hisa nyingi za kwangu, na kampuni unayomiliki wewe ina hisa nyingi za kwako, ili kuonyesha umiliki, tulifanya hivyo kwa nia njema tu..sio kwamba kila mtu ana maisha yake, hapana, ni katika kutambulikana kwenye umiliki tu.’nikasema.

‘Sawa kabisa, na huo ulikuwa ni ushauri wako, japokuwa mimi nilitaka tuwe na hisa nusu kwa nusu kwenye kampuni yangu, maana mtaji karibu wote unatoka kwako na kwa wazazi wako...ila kampuni yako sikutaka kabisa kuwa na hisa, ukalazimisha kuwa na mimi ni lazima niwe na hisa, sikuona tatizo, kuna lolote limetokea hapo?’akasema.

‘Hapana hilo halikufanyika kwa nia mbaya...sote ni wazazi, na uchungu wa familia ulio nao wewe ni sawa na nilio nao mimi, ndio maana hakuna aliyefikiria kuwa ukipata hisa zote hizo, utadhulumu, au utakimbia nazo, ..hilo halipo, na utambua kuwa mimi nakuamini moja kwa moja...amini hivyo...’nikamwambia.

‘Sawa kabisa hata mimi nakuamini sana,...’akasema.

‘Sasa ni hivi, niliongea na wakili wetu, nikamwambia atayarishie mkataba, mkataba ambao, utagusa kila kitu chetu, kuanzia, mali, watoto na hata ndoa yetu,...hii itasaidia sana, ili tuwe makini na ndoa yetu, mkataba huo uainishe kuwa kama mmoja wetu atakiuka maswala ya ndoa, basi ...amevunja mkataba na mali kila kitu chake, kinachukuliwa,...unaweza hilo, nikuulize kwanza , maana mimi sina shida....’hapo nikatulia.

‘Una maana mtu akikiuka mkataba ndoa hakuna, hio sawa, lakini ukisema mali, mbona mali ni zako, na wazazi wako wanafahamu hilo, huoni kama utakuwa umejitendea isivyo halali,  au unataka kusema nini...’akasema.

‘Ndio hivyo, kwani wewe unatarajia kukiuka masharti ya ndoa?’ nikamuuliza.

‘Hapana, siwezi kufanya hivyo, nakupenda sana mke wangu, sizani kama kuna mtu anaweza kuja kunivuruga akili, ni nani anaweza kufikia uzuri wako, hakuna..kwahiyo mimi naunga mkono huo mkataba, tena bila wasiwasi....lakini naona kama mkataba huo utakudhulumu sana wewe, kama ikatokea....’akasema na mimi nikamkatisha na kusema;

‘Sawa mimi nilitaka nikuweke wazi kwa hilo,na nilimwambia wakili autayarishe, halafu tutakutana sote kwa pamoja tuusome, tuone kama kuna chochote cha kubadili, au kuongea, au kutokukubaliana, na tukiupitisha, basi utakuwa ndio katiba yetu ya familia, na nina imani kuwa hakuna atayekiuka huo mkataba, mimi sina shaka kwangu...’nikasema na kumwangalia.

‘Hata mimi..mimi sina shaka na hilo, ..wewe niamini mia kwa mia...’akasema.

‘Mimi nina uzoefu , mimi naheshimu sana hayo mambo ya mkataba, kwani nimeona jinsi gani unavyosaidia maswala ya kikazi, kama ni hivyo basi, kwanini mkataba kama hiyo tusiitumie kwenye familai zetu, ili kukwepa makatizo mbeleni,  tunaweza kutumia mikataba, kama katibaya kila siku ...ni wazo langu tu mume wangu kam unalaifiki sawa, kama unaona ni kikwazo katika ndoa mimi sitaki kulazimisha kitu kaam hicho, unasemaje...’nikasema.

‘Hakuna shida kabisa, mimi nipo pamoja na wewe, na nipo tayari kwa hilo...naliunga mkono kwa nguvu moja.’akasema.

‘Sawa kama umekubali basi, tuombe mungu, ...na ni vyema wewe ukakaa ni kuliwazia hilo kwanza, ili uone ni vitu gani muhimu vinahitajika kwenye mkataba huo, isiwe ni mawazo yangu tu, ....au  isiwe ni mawazo ya wakili wetu tu,...mkataba huo uwe kama katiba yetu..unaonaje..?’ nikasema.

‘Ni sawa kabisa mke wangu, umenifungua masikio, na hapa nilipo nawazia mengi, hasa nikiangalia familia yangu nilikotoka,..nilishuhudia ugomvi mkubwa nyumbani baada ya kufariki kaka yetu, alikuwa na mali kidogo, basi alipofariki, walitokea watoto wasiojulikana, kila mmoja anadai urithi, wazazi wao, wakaja juu, kila mmoja akidai kuwa mtoto wake anatakiwa kupata mali kutoka kwa marehemu kaka, kwasababu alizaa naye...ilituhangaisha sana, na mwisho wa siku mali nyingi za kaka ziligawanywa,....sasa mambo kama hayo tunaweza kuyakwepa, kwa kuyaweka kisheria, hata mimi nilikwua nawazia hivyo hivyo....’akasema.

‘Unaonaeeh, ndio hivyo, sasa hebu fikiria sisi hapa tuna makampuni mawili makubwa,....huwezi jua yakutokea baadaye,....huwezi jua maadui zetu wanatufikiriaje, kuna watu kila siku wanaota jinsi gani ya kuwadhulumu wenzao, hawafikirii kuhangaika, na kuzalisha, wanachofikiria wao ni jinsi gani ya kuwazidi wenzao ujanja ili mwisho wa siku wapate kile walichochuma wenzao, sasa ni muhimu hili tukalifikiria kwa mapana zaidi...’nikasema.

‘Mimi sina cha kufikiria zaidi, cha muhimu tukutane na huyo wakili tuone jinsi gani alivyoandaa, na kama kuna nyongeza mimi nitasema, na wewe pia utasema, ili mwisho wa siku tuwe na kitu kimoja cha watu wote, hilo naona lisichukue muda, hata leo, kama wakili keshaandaa, tunaweza kumuita...’akasema.

‘Hapana, sio swala la kuchukulia haraka haraka, inatakiwa wewe ukae, utathimini, hata kama kuna mtu mwingine unayemwamini, au mwanasheria mwingine kuacha huyu mwanasheria wetu, ukae naye ujaribu kuulizia, ..ili usije ukaingia kichwa kichwa na mwisho wa siku ukaja kunilaumu mimi....’nikasema.

‘Siwezi kuja kukulaumu, maana mimi nafahamu sana umhimu wa hilo, na nashukuru kuwa ulikuwa unawaza sawa na mimi nilivyokuwa nikiwaza, japokuwa mimi nilikuwa nachelea, usije ukaona nina tamaa,....’akasema.

‘Sawa tutamuita wakili wetu na yeye atatuonyesha hicho alichookiandaa, maana yeye ni mzoefu wa mikataba kama hiyo, ya kifamilia, kikazi na mingineyo, .....na sisi ni lazima tupitie kila kipengele tuone kama kinakidhi matakwa yetu, asije akaandika kwa ujumla, kumbe kuna mambo yanaweza kuja kutukwaza...ni muhimu sana....’nikasema na yeye akawa anatikisa kichwa kukubali, akionyesha furaha.

‘Sawa mke wangu, mimi sina shida kabisa mke wangu nakuunga mkono kwa wazo hilo la hekima, nipo tayari  kwa wakati wowote...’akasema.

Na baada ya siku mbili mkataba ukatayarishwa, baada ya kukutana na kupitia kila kipengele, na tukaongezea na mengine mengi, ilimradi uwe mkataba unaogusa kila kitu kwenye maisha yetu, na tukaupitisha , ukapelekwa mbele kisheria, na mwisho wa siku ukawa ndio katiba yetu.

Mwanzoni tulikuwa tukifuatilia sana, na ikawa kila mmoja ana hamasa na utaratibu wote, hadi tukawa tumeweza kushika kila jambo, na kila mmoja akawa na tahadhari , asije akavunja mkataba, na kila mara tunakumbusha,kama jambo limafanyika, sivyo ndivyo, utasikia `mkataba unasemaje...’ Basi ikawa maisha yetu ni mkataba, tkawa tumeiva katika hiyo hali, na hakuna aliyekuwa na matatizo na mwenzake, maana kila mmoja alijua kuwa mwenzake anafanya kutokana na mkataba.

Siku zikaenda, mambo yakwa mengi, watu tukajisahau,ikafikia hatua hakuna aliyejali kangalia mkataba unasemaje,ila kuna yale mambo ya msingi, kama ya ndoa, masilahi, na uwajibikaji,...mengina madogo madogo yakawa yanakikwa hapa na pale, hakuna aliyejali,...ilimrdi tunaaminiana...tukajisahau lakini maisha yakaenda mbele, maana kulikuwa hakuna matatizo.

Leo tatizo hilo lipo mbele yetu, na nahisi ni tatizo kubwa, linalogusa vipengele vikubwa ndani ya mkataba wetu,....nahis hivyo,...nikaona ni vyema niupitie tena mkataba wetu, japokuwa sikuwa nimefahamu ni tatizo gani ambalo limeweza hata kumchanganya mume wangu, na kama kuna ukiukwaji wa mkataba katika vipengele vikubwa, hapo kutakua hakuna jinsi....maamuzi yapo kwenye mkataba wenyewe, hapo nikajikuta nikihamanika kuusoma huo mkataba, sijui kama mume wangu anakumbuka hilo...nikawaza.

Atakuwa anakumbuka na huenda kinachompa shida ni kutokana na hayo tuliyokubaliana, ...kama ni hivyo , ...hakuna jinsi, cha muhimu ni apone kwanza, akipona tutaangalia mkataba unasemaje, ..je msamaha wangu upo kwenye mkataba, kuwa mtu akimsamehe mwenzake basi yamekwisha. Hilo halipo kama mtu kakiuka vipengele vikubwa, kwani kwenye mkataba kulikuwa na vipengele vikubwa na vidogo, kuna vipengele ambavyo mtu akivikiuka kwa bahati mbaya, anaweza kusamehewa, lakini kuna kikuika masharti ya ndoa, kusaliti ndoa,hapo hakuna msamaha.

`Ngoja nikausome tena...’ nikasema nikichukua funguo zangu, na kwenye hizo funguo, kuna ufunguo wa droo ya mezani ambapo hapo naweka huo ufungua wa kabati langu maalumu, niliuficha sehemu maalumu, hakuna mtu anayeweza kuupata.

Ufunguo ulikuwepo pale pale,....nikauchukua, na kusogea kwenye kabati, nikahakikisha nimefunga mlango wa ofisini, kabla sijafungua hilo kabati, maana sikutaka mtu aingie na kuja kunisumbua. Nikasogea kwenye lile kabati, na kuchuchumaa, maana sehemu nilipoweka hizo nyaraka ni sehemu ya chini ya hilo kabati, ...

Nikafungua kidroo hicho, kilikuwa na namna ya kukifungua, sio kwa haraka, ni kama unafuatilia namba, nikafuatilia kwa makini mpaka mlango wake ukafunguka...., nakumbuka kabisa wapi niliuweka ile nakala ilikuwa pembeni, na niliisimamisha,

Nikapapasa, nikasogeza mkono shemu yote ya ndani..hakuna kitu, kulikuwa na nyaraka zingine za benki, ambazo hazikuchukuliwa...hapo sasa, nikahisi moyo ukinienda mbio,....nikatulia kidogo, nikijaribu kutuliza kichwa.

‘Haiwezekani, nakumbuka kabisa huo mkataba niliuweka sehemu hiyo hiyo, kwa mara ya mwisho nilipouchkua na kuusoma kidogo, na sijaugusa tena toka siku hiyo, ni kweli kuna kipindi cha nyuma kidogo, nilikuwa nautoa mara kwa mara nikirejea baadhi ya vifungu, na kila nikimaliza kusoma naurejesha pale pale, na mimi ni hodari sana wa kuweka vitu vyangu kwenye mpangilio wake, na nahakikisha kila nikitoka ofisini kwenda popote, kila kitu nakiweka katika mahali pake kwa mapangilio wake, hilo sikosei hata mara moja.

Nakumbuka kabisa niliuweka pale pale..nikaingiza mkono ndani na kusogeza kwa ndani kabisa, kama umegandia kwa ndani, hakukuwa na kitu kama hicho, nikaanza kuhisi vibaya. Ni kawaida yangu, kama kuna kitu nakitafuta, na hakipo sehemu yake, au kama kuna kitu nimehisi kina tatizo, nikianza kujiskia vibaya, ujue, kweli kuna tatizo, mwili ukaanza kuhisi vibaya...sikuamini, kama huo mkataba haupo, na kama haupo, ni nani aliweza kufungua hilo kabati, .....

Nikasogea nyuma na kuangalia tena kwa makini, ..labda katika usafi wakati wanasukuma hilo kabati kupata nafasi,huenda huo mkataba ulidondokea kwa ndani, nikaanza kutoa kitu kimoja kimoja, ...lakini sikuona kitu kinachoitwa mkataba, na hakuna mtu wa kumuulizia, maana huo ni mkataba wangu na mume wangu....nikaishiwa na nguvu, sikujua kabisa ni nani kauchukua, maana ufunguo nilikuwa nao mimi tu,na nilikuwa nimeuhifadhi sehemu ambayo hakuna mtu angeliugundua,...

‘Ni nani huyu mwenye nia mbaya,kaweza kuugundua huo ufungua, na akautoa, na kufungua hilo kabati, halafu akaurudisha pale pale nilipokuwa nimeuweka, maana ufungua huo ulikuwa hauna akiba...na alijuje kuwa upo hapo, na anahusikanaje na huo mkataba, zaidi ya mume wangu na mimi,nikajaribu kuangalia tena kwa makini, lakini mkataba ulikuwa haupo....

Mkataba haukuwepo....

Matatizo yanazidi kuongezeka, kuna nini hapa....

NB: Hayo tena mambo yanazidii kuongezeka, kunani...tukutane kwenye sehemu ijayo.

WAZO LA LEO: Kama tutakuwa na taratibu za mikataba kwenye ndoa zetu, kwenye familia zetu, kwenye vikundi vyetu, kwenye maisha yetu,kwenye sehemu zetu za kazi, nk, tungeliepuka migongano na mfarakano, maana mambo mengi yangelitatuliwa kisheria. Familia nyingi zinajikuta kwenye matatizo,pale anapofariki mmojawapo, au pale kunapotokea tatizo, na kutokuelewana. Na mwisho wa mifarakano hiyo, au matatizo hayo, wahanga wa haya yote ni watoto na akina mama, ambao wanakuja kudhulumiwa haki zao. Je hatuoni kuwa ili kukwepa hayo yote, ni bora kukawa na mikataba katika maisha yetu? Tuliwazie hili na wanasheria watusaidie...

Ni mimi: emu-three.

4 comments :

Nancy Msangi said...

Mmmh, mambo yanazidi kuwa magumu cjui itakuwaje hebu tusonge nayo,

Nancy Msangi said...

Haya tena ngoja tusubiri itakavyokuwa, MN mmh!

Anonymous said...

best make-up for accutane users [url=http://fast-isotretinoin.com]Buy Accutane[/url] ipledge accutanecialis 40 mg safe [url=http://fast-tadalafil.com]Cialis[/url] buy viagra professional onlinecheap generic viagra 50mg [url=http://sildenafilusshop.com]Viagra[/url] viagra other medical usespropecia length of prescription [url=http://healthcarerxusa.com]Buy Propecia Online[/url] reputable foreign pharmacy finasteridelevitra with no prescription [url=http://fastshiplevitra.com]Levitra[/url] levitra online in australia

Anonymous said...

mexican cialis online [url=http://fastshipcialis.com]Buy Cialis[/url] cialis testimonialsclomid 5 day text [url=http://usfastmed.com]Clomid[/url] clomid no prescription fed ex shippinggeneric viagra at walgreens [url=http://fast-sildenafil.com]Viagra[/url] viagra labelsside effects of going off accutane [url=http://fast-isotretinoin.com]Accutane[/url] accutane and periodslevitra success rate [url=http://fastshiplevitra.com]Buy Levitra Online[/url] levitra grapefruit