Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, August 22, 2013

WEMA HAUOZI-53



`Nikikumbuka hilo tukio, wakati mwingine najikuta nikicheka mwenyewe….’akasema mwanadada huku akicheka, akiendelea kuhadithia kisa hiki, …

‘Maana kwa jinsi gani nilivyotoka kwenye huo msitu, nashindwa hata kuelezea,hii ni kuona jinsi gani mwanadamu anavyoogopa kifo ambacho anahisi ni cha mateso…’akatulia.

‘Nashangaa sana pale mtu anapotaka kujiua, lakini mtu kama huyu mwambie, kuna nyoka au simba, aje amtafue ili afe, hatakubali…..’

‘Basi siku hiyo imebakia kama historia kichwani mwangu…

Kisa chetu kinaendelea hapo…

 Siku hiyo nilikimbia sijawahi kukimbia hivyo katika maisha yangu, ulikuwa unakimbia na ukigeuka nyuma unawaona wadudu wale wapo juu yako, karibu yako kabisa..wakiwa wanapanua midomo yao kutaka kukung’ata, siunawafahamu popo walivyo….’akasema mwanadada akimuhadithia mama kisa hiki.

‘Na cha ajabu japokuwa wadudu wale walikuwa karibu, lakini hakunigusa, alikuwa ule mlio wao huku akichezeza mabawa yake, na akipanua ule mdomo wake, unajikuta ukiogopa, na kuongeza mbio… nilikimbia na sijui wenzangu ilikuwa hivyo hivyo au vipi, lakini tulipokuja kuhadithiana kila mmoja alijikuta akicheka,…..’akasema.

‘Tuligundua kuwa lengo na nia ya wale ndege, popo, ilikuwa sio kutuzuru, nia yao ni kututoa msituni, na sio kutuuma, kama tulivyojua watafanya hivyo, na kama wangelitaka kufanya hivyo wasingeshindwa….’akasema

‘Cha ajabu nilipomaliza eneo la msitu tu na kuingia kwenye mashamba, maeneo ya wazi, kwenye mipaka ya msitu na mashamba ya watu, wale ndege walisimama na hawakuvuka ule mpaka, wale wadudu walibakia pembeni mwa huo mpaka wakiruka huku na huku, kuzunguka miti, kama vile wanafanya doria, mtu asirudi tena, na kama kweli wanahakikisha hakuna anayerejea, na wengine wakawa wanatukdolea macho kututisha…’.

‘Kwakweli sikuamini, nilisimama nikainama, na kujaribu kutafuata hewa, na baada ya dakika kadhaa za kutulia na kuhakikisha nipo salama, nikageuka kuangalia wenzangu, na niligundua kuwa kila mmoja alikuwa sehemu yake, akipumua kwa shida, na hakuna aliyekuwa anaamini kuwa katoka humo msituni salama,

Mara nikakumbuka, jambo, na hapo akili ikarejea kwenye mwendo wa kawaida, nikageuka huku na kule, nilikuwa nikiwaangalia wale waliokuwa  wamewabeba majeuhi, je na kwao ilikuwaje, je watakuwa wameweza kuwabeba hawo majeruhi, au wamewatelekeza, …nikaanza kutembea kuwafuata wenzangu, na bahati nzuri nikakutana na mkuu, akiwa kashikilia bastola, akiwa kama anawaelekezea wale ndege kama kuwatisha.

‘Mkuu unataka kufanya nini, hilo lililotupa ni dogo…unatafuta mengine tena….’nikasema na mkuu akaanza kucheka.

‘Hivi wewe unaakili kweli, yaani unacheka, wakati uliona jinsi gani hawa wadudu walivyokuwa wakitaka kutuuma….’nikasema na huyo mkuu akaendelea kucheka, na maaskari wengine waliokuwa karibu na wao wakaanza kucheka.

‘Nyie watu mnacheka u kwa vile hamjui historia ya hawa wadudu, sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili,…, nasikia ukikiuka msharti, kama uko huko msituni, ukajifanya unawinda kwa bunduki, hawa wadudu, wanacharuka hivyo hivyo, na ole wako, uwapige, watakufuata kwa wingi hadi nyumbani kwako, na watahakikisha wanakudonoa hado unabakia mifupa, hapo tu wametufukuza kwa vile hawakuwa nia  mbaya na sisi, huenda kwa vile hatukuwadhuru wao, ila tumekiuka miiko ya kupiga risasi….’akasema mmoja wa maaskari anayefahamu historia ya huo msitu.

‘Ilishawahi kutokea hivi karibuni kwa watu unaowafahamu?’ akauliza mwanadada.

‘Ndio kwa wawindaji na watu waliokuwa wakitafuta madini, kwani humo kwenye huo msitu kuna sehemu zina madini, ukiweza kuyafuma wewe unakuwa tajiri, lakini wengi waliobahatisha kuyapata, waliishia kugombana na kuanza kutupiana risasi, na hapo wakajikuta wakitolewa mbio na hawa wadudu…’akasema.

‘Sasa tutafanyaje maana tunahitajia kurudi, ili kukusanya ushahidi……’akasema mwanadada.

‘Kurudi kwa leo haiwezekani, huwezi kupita hapo, mpaka hawo wadudu waondoke, na kuondoka kwao ni mpaka waone sote tumeondoka eneo hili..’akasema huyo mtu.

‘Oh, wangeniuma nisingesita kutumia silaha….’akasema mkuu, na kumwangalia mwanadada, huku akiendelea kucheka, na alipomuona mwanadada akimwangalia kwa hasira , yeye akasema;

‘Duuh, kweli kifo kinaogopewa, sikujua kuwa mwanadada unaweza kukimbia kiasi hicho, maana nilikuwa nyuma yako, na nilikuona ukikimbia kama unapaa….’akasema mkuu, lakini alimuona mwanadada akihangaika kuangalia huku na kule, na hapo akauliza.

‘Unatafuta nini tena mpendwa, umesikia kuwa leo huwezi kurudi tena humo msituni…, au bado wewe una moyo wa kuingia huko msituni..kama upo tayari twendeni?’ akasema mkuu akijifanya yeye haogopi.

‘Mimi nawaangalia majeruhi,….je wamewahi kutolewa,au ndio wametelekezwa huko msituni?’ akauliza mwanadada, na hapo mkuu, akaangua kicheko tena na kusema;

‘Yaani sasa hivi ndio unalikumbuka hilo,wakati wewe ulikuwa ukikimbia hata bila kumjali mpenzi wako, watu kama nyie, ndio wale linapotokea tatizo kama hili, kama alikuwa na mtoto wake mchanga anambwaga hapo chini, au anamsahau kabisa, na anakuja kukumbuka baadaye …’akasema huyo mkuu huku akigeuka kuwaangalia wale ndege.

‘Sasa mwanadada, tufanyeje, turudi kuwafuata wenzetu majeruhi msituni,  kama kweli unawajali, kama kweli unampenda mpenzi wako, ….?’akasema mkuu huku akichekana na mwanadada akazidi kukasirika, akijua mwenzake anamzihaki na huo ulikuwa sio muda wa masihara, na mkuu alipoona hivyo, akachukua simu yake na kuanza kuwasiliana na watu wake , akasema;

‘Mumeshawafikisha hao majeruhi hospitalini?’ akauliza na kusikiliza kwa makini, halafu akageuka kumwangalia mwanadada huku uso ule wa kucheka ukiwa umebadilika, na kuwa uso wa kikazi zaidi akasema;

‘Wameshawafikisha majeruhi  hospitalini, na mwanasheria keshaingizwa chumba cha upasuaji,….hali yake sio nzuri….’akatulia huku akimwangalia mwanadada ambaye kwa muda huo alionekana mwenye huzuni nyingi.

‘Sikiliza mwanadada, kama mtu huyo ni wakupona atapona tu, na sote ndilo tunaloliomba, lakini ukumbuke kuwa hapa tupo vitani, na vitani usitegemee kushinda tu,kuna kushindwa, kuna kuua na pia ukubali kuwa kuna kuuwawa pia, huwezi ukaua tu,na wewe mwenzako dhamira yake ni hiyo hiyo kukuua,..kwa hali kama hiyo wewe ukiwa msitari wa mbele wa mapambano ukubali yote…’akasema mkuu, na mwanadada akamwangalia kwa macho yaliyojaa hasira,

Mkuu akageuka kuangalia upande mwingine, na kabla hajasema kitu mwanadada, akaishika bastola yake vyema mkononi na kusema;

‘Huyo mtu atakuwa kaelekea wapi?’ akauliza mwanadada, na mkuu, akamgeukia na kusema;

‘Kama bado yupo huko msituni, atakuwa kaliwa na hao ndege, lakini kwa hali iliyotukuta sisi, hata yeye sizani kama atakuwa kabakia humo msituni, huenda yupo mahali, anaugulia hilo jereha la risasi na huenda keshakufa….’akasema mkuu.

‘Nataka nimuone akiwa hai, na ikiwezekana niitumie silaha hii kwake…’akasema mwanadada kwa hasira.

‘Huwezi, unasema tu kwa hsira, lakini nikujuavyo wewe, huwezi kufanya kitu kama hicho,…’akasema mkuu, na kugeuka upande ule aliokuwa kaangalia mwanzoni, akatoa simu yake kutaka kuwasiliana lakini kabla hajafanya hivyo mara wakasikia sauti za mlio ya bunduki, upande mwingine nje yauka juu, na uanza kuzunguka zunguka huku wakizidi kutoa sauti za kutisha.

‘Nini tena hicho jamani, mnataka hawa ndege watuvamie tena,….aah’akasema mwanadada, na mkuu akamwangalia mwanadada na kusema

‘Vijana hawo, huenda wameshamnasa huyo mtu wetu…’akasema mkuu

Ilikuwa sio mbali sana na pale mkuu na mwanadada, wakakimbilia huko waliposikia huo mlio wa bunduki, na kwa mbele kidogo wakawaona wenzao wakihangaika, kama vile wanapambana na mtu, na mkuu na mwanadada wakawasoegelea wakiwa na tahadhari,silaha zao zikiwa mkononi tayari kwa lolote lile.

Walipofika walimuona yule jamaa akiwa keshazibitiwa, na mwili wake ulikuwa umelowana damu, japokuwa bado alikuwa akileta ubishi, na wale maaskari wakahakikisha wamefunga pingu mikononi na miguuni, na kumweka chini ya ulinzi thabiti,

Mkuu alimwangalia yule mtu, na kutikisa kichwa, akasema;

‘Kama isngelikuwa sheria, nisingekuwakilisha mahakamani, ningelihakikisha nachukua sheria mikononi mwangu, ….lakini,sheria inanifunga, najali sana mamlaka niliyopewa..’akasema mkuu, na mwanadada ambaye alikuwa karibu na huyu mkuu, alikuwa kaishikilia bastola yake, huku mkono ukiwasha, kwani hasira na chuki vilikuwa vimemzonga sana. Mkuu alihisi hiyo hali akamgusa mwanadada kwa mkono kumuashiria kuwa tulize hasira zake.

‘Na nawaambia ukweli, mkifanya makosa yakunipeleka jela nikiwa hai, hamtanipata tena….’akasema huyo jamaa kwa dharau.

‘Huna lolote wewe, uchawi wako umeshafirisika unafikiri hatukujui,…huna lolote wewe unakwenda kuozea jela…ara ya ngapi ni’akasema mkuu.

‘Mimi nawapa kama tahadhari, kwani mara ya ngapi nimehukumiwa kufungwa jela, lakini ipo wapi,..kwa sasa ni kweli, sitegemei huo uchawi, kama mnavyouita nyie, mimi nina ujuzi zaidi ya huo, uliza mimi nilikuwa nani wakati nipo usalama…..’akasema kwa  dharau

‘Hahaha…ulipokuwa usalama,..mtu kama wewe hustahili kuwa sehemu kama hiyo, na kama ulibahatika kuingia  uliingia kimakosa, ndio maana ukatolea, mtu kama wewe hustahili kufanaya kazi yoyote ya wito , una roho mbaya kama shetani…’akasema mkuu.

‘Hahaha, kumbe unajua ehee….Lakini ulizia nilikuwa nani …’akasema huku akitema damu chini.

‘Kama singelikuwa hili jeraha, watu wako hawa wasingeliniweza,..ila jeraha limegusa pabaya, …na nimeshaitoa risasi peke yangu, unaweza hilo,….nyie cha mtoto, nikitaka kufanya lolote hamniwezi,…ulizia huko nilipokuwa, wenyewe walisalimu amri,…’akasema akimwangalia mkuu kwa dharau

Mkuu alimwangalia kwa makini, na kweli alihisi moyoni kuwa mtu kama huyu sio wa kawaida kama kaweza kujitoa risasi mwenyewe, basi huyu mtu ni zaidi ya gaidi, ni shetani, hastahili kuishi, lakini moyoni aliogopa kufanya lolote, kama kiongozi, …na yule jamaa akaendelea kuongea kwa nyodo na kusema;

‘Hebu angalieni yote niliyoyafanya ni nani angeliweza kufanya hivyo, …mimi ni jembe, tena jembe ulaya, hakipatikani hivi hivi, na wajinga hawajui kulitumia, ndio maana najitumia mwenyewe, …mimi nina ujuzi wa kila kitu,….’akasema huku akitema damu ambazo zilitokana na kipigo, aliumia mdomono, kulionekana kuvimba.

‘Nawaambia ili mjue, kuwa mimi ninajua kila kitu, hebu niambieni ni nani angeweze kujenga lile handaki, simumeliona wenyewe, mtasema kaja fundi mkubwa toka huko majuu, hakuna fundi anayeniweza mimi, ukisikia mtaalamu, basi ujue mimi ni mtaalamu kweli, nyie mnasema mtaalamu kwa mambo hayo ya ushirikina, hilo lilikuwa kama chambo tu…’akasema kwa nyodo.

‘Hiki ki kichwa, niliwasoma watu, nikajua udhaifu wao upo wapi,….watu wanaogopa sana ushirikina, wanaogopa sana nguvu za giza,…ndio maana hata watu wa dini wanatumia mwanya huo kuwaogopesha watu, …na mjnja kama mimi nikaona nitumie mwanya huo…’akasema.

‘Nawaambia hili , kwasababu huenda msipate muda wa kuongea na mimi, msiponiua nitapotea na hamtaniona tena….’akasema.

‘Mimi nilifanya uchunguzi huo baada ya kufanya utafiti wa kisayansi, kuhusu hisa ua uzaifi wa mwanadamu, …uwoga, niligundua kuwa mwanadamu ni mwoga sana, hasa kwa yale ya kufikirika,…’akasema huku akikunja uso kuonyesha anafikiria jambo.

‘Na niligundua kuwa sehemu nyeti ni hiyo, ya dhana za uchawi, na hpo nikaanza kucheza napo,…kwa vile nina kipaji cha uganga, nina kipaji cha asili cha unajimu, utabiri, na hayo wanayoita mizimu, nikafahamu kuwa ninaweza kutumia kipaji hicho na kutajirika…..’akatulia.

‘Ni nani kakumbia kuwa waganga, watu wa namna hiyo hawatakiwi kuwa matajiri….hizo ni hisia hasi, ni hisia za watu wenye ubinafsi, na ni hisia za watu wasioenda shule…mimi nimeenda shule, na nikasoma zaidi ya kwenda shule, nafanya utafiti wangu mwenyewe, ukiingia kule kwenye handaki utaona chuo change, kuna maabara, ya kila namna, na hivi karibbu nilikuwa nafanaya utafiti wa kuunda silaha ya maangamizi…’akasema na watu wakawa wanamuangalia kama mwehu.

‘Shangaeni…lakini msishangae sana ya shetani, hayo ni cha mtoto kwa ibilisi….’akasema na kucheka kwa dharau.

‘Ndio maana nawaambia kuwa mimi ni jembe, lakini lipo kwa watu wasiojua kulima,…unajua kwanini nilishindwa kukaa jeshini,…kwasababu hiyo hiyo, kuwa unaongozwa na watu wasiokwenda shule, wanatumai nguvu nyingi bila akili, hawashauriki,…wao wanajua kushoto kulia, lakini hawajui kuna chini na juu, na kati ya kushoto na kulia…hawajui..hawaeelzeki, na baya zaidi kuna wanaojifanay miungu watu…’akatulia.

‘Afande, afande….ni nani atamuabudua binadamu mwenzake, binadamu ambaye hajui kabisa, silaha hiyo aliyosihika imetengenezwaje, hajui kabisa, uwezo wa mwanadamu upoje, katika jambo fulani…mii najua na naweza kukujua hivi sasa unafikiria nini….’akatulia.

‘Ndio maana siogopi, maana nimeshwafahamu lengo lenu ni nini..namuogapa sana huyu mwanamke…hiki nacho ni kichwa kingine…’akasema

‘Lakini sio kumuogoa kwa kuogopa mtakapofikiria nyie…naogopa akili yake…na sijui alinigunduaje, …alinichota kiajabu na kuniweka ulingoni, mwa mahakama, na hapo, akajumlisha na kutoa, akanigundua…na mtu kunigundua mimi, sio mchezo…’akatulia.

‘Sasa kwa akili zenu ndogo, hebu jiulizeni lile handaki lilijengwa na nani kama lilivyo, ile ni mikono yangu …ni nani angeliweza kufanya haya yote peke yake, ni akili yahali ya juu, na bado kama mtaniachia huru, kama mtanifunga, mjue nitafanya mabaya zaidi ya hayo, ….moyo wangu unatamani kuwa mfalme chini ya ardhi….mnaweza hayo…’akasema kwa dharau na mwanadada, akainua bastola kutaka kumaliza kazi,lakini mkuu akamuwahi na kumzuia mwanadada, asifanye hilo alilotaka kulifanya.

‘Ole wako…..uombe mwanasheria apone, la sivyo, nitahakikisha nakupeleka huko huko mkakutane kwenye mikono ya sheria isiyodanganyika..’akasema mwanadada, na yule jamaa akamwangalia mwanadada kwa dharau, na kusema;
‘Napenda sana mwanamke kama wewe, mwenye kujiamini, lakini huyo ndugu yako, eti mkuu, hana lolote, ….ndio maana hata binti yake, akamkimbia na kuja kwangu, …lakni namuheshimu kwasababu ni baba mkwe..hahahaha….binti yake kazimia kwangu,…mimi ni mtaalamu wa kila kitu, jembe…’akasema kwa dharau akimwangalia mkuu kwa macho yanayosinzia sinzia,kuonyesha kuwa nguvu zilikuwa zikimuishia, huenda ni kutokana na kupoteza damu nyingi,na mkuu akamwangalia kwa hasira, na alichofanya ni kumpiga teke la tumboni, na huyu jamaa akainama na kuguna kwa maumivu.
‘Mhh, hapo sasa wewe mwanaume…lakini hujafanya kitu, ni kama kumpiga paka kwa fimbo…hahahaha…hamtaki niwasimulie mengine, shauri lenu,msije mkawa mnazua, sikilizeni kutokwa kwangu mwenyewe,hahahaha….’akacheka kwa dharau

‘Mpelekeni kituoni na hakikisheni hapati nafasi yoyote ya kutoroka, akitoroka na nyie muhakikishe mnacha kazi,….mtawajibika, tunataka aone kuwa sis hatutanii…kama anatumia vumba sisi tunatumia chuma…na ole wako, ujifanye mjanja,…nitakutafuta hadi huko ardhini unaposema unataka uwe mfamle, na tutakuzika huko huko…’akasema mkuu, na yule jamaa akacheka kidogo, na kumgeukia mwanadada, akamwangalia kwa macho yaliyochoka, halafu akatabasamu kwa dharau na kusema;

‘Mpenzi, pole sana, mchumba wako, kashetangulia,…lakini kiukweli sikuwa na lengo la kumuua, yule ni rafiki yangu, kanisaidia mambo mengi sana, bila ya yeye kujua,…ni bahati mbaya, wakati tunazuiana, risais ilifyatuka, sikuwa na nia hiyo, ….sio mbaya wangu yule, kwanini nimuue…’akasema na kujifanya ana huruma.

‘Ila nakuahidi kitu kimoja, sitakutupa, usiwe na wasi wasi mimi nipo nitachukua nafasi yake…’akasema na mwanadada, aligeuka na kwa haraka akatupo teke lililompata huyo jamaa tumboni, na yule jamaa aliguna na kukunja uso kwa machungu, na akahema mara moja na kusema;

‘Mhh,..unapiga teke kama mwanaume, oh,.....'akakohoa kwa muda, halafu akainua kichwa huku mate yakimtoka na damu akasema;

'Lakini, sikilizeni ni..niwaambie ukweli, ni bora mniue, kwani nikipata nafasi , nitahakikisha kuwa haya yote mliyonitendea mnayapata vile vile jino kwa jino…nawahakikishia hilo, mtaona….na wewe uta…shukuru kuwa umenipata mimi ns io huyo jamaa yako mnafiki, leo kwako kesho kwa mwanamama, ….’akasema na maaskari wakamkokota na kumuingiza kwenye karandinga

NB. Kumbe hatujafika kwenye hitimisho …haya huyo ndiye mtaalamu, sema wewe


WAZO LA LEO: Ubaya sio sifa ya kujisifia, matendo mabaya sio sifa ya kujisifia mbele za watu, ni kama mtu anajitembeza uchi mbele ya watu akipata kuwa yeye ni mjanja, huo sio ujanja ni ujinga. Ukiwa na hali kama hiyo ujue umeshatekwa na shetani, na unahitajika kutubia na kujirudi haraka iwezekanavyo.
Ni mimi: emu-three

No comments :