Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, August 21, 2013

WEMA HAUOZI-52


Tulitoka nje ya lile pango huku tukiwa tumekata tamaa ya kumpata huyu mtu tena,ikizingatia kuwa yeye analifahamu hilo pango lilivyo, na sisi japokuwa tupo wengi, lakini njia za kupita zilihitajia mtu mmoja mmoja,…

Bado tukiwa na matumaini ya kumpata huyo mtu akiwa hai, tuliharakisha kutoka, ili kuungana na wenzetu waliokuwa wakijibisha risasi na huyo jamaa, na baadaye kukawa kimiya, ikiashiria kuwa huenda huyo mtu alishatoka nje,

Swali likawa je kama huyo mtu kawahi kutoka nje,  itakuwaje, kwani hatukukumbuka kumuacha askari zaidi ya mwanasheria, wote tulikimbilia kuingia ndani..na je hiyo amri ya kutokutumia risasi huko nje, itawezaje kuepukika, na mtu kama huyo?

Tuendelee na kisa chetu......

Tukajitahidi na sisi kutoka nje kwa haraka haraka, na tulipofika nje, tuliwaona askari wetu wamesimama huku wameelekeza silaha zao upande wa pili, kama wanawinda kitu, na mkuu ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka na bastola yake mkononi, akawauliza vijana wake

‘Yupo wapi’ akauliza

‘Mkuu kaingia kwenye hicho kichaka, na cha ajabu haonekani tena, lakini tuna uhakika yupo hapo, na tunahisi kuwa hayupo peek yake,…’akasema mmoja wapo, na wote wakaelekea kwenye hicho kichaka na kwa mbele wakaona watu wawili wakiwa kwenye mapigano na kila mmoja akiwa kamshika mwenzake mkono, ili kuzuia silaha yake, isielekezwe kwake.

Msaidieni mwanasheria, lakini msitumie silaha, kumbukeni tulivyoambiwa, ….’akasema mkuu, huku nay eye akielekea kule ambapo mwanasheria alikuwa akipambana na huyo mtu, na ilikuwa vigumu kuingilia kwani zile silaha walizoshika zingeliweza kufyatuka na kuleta madhara kwa yule ambaye angeliwakaribia, kwahiyo ikawa kutafuta jinsi ya kusaidia.

Mwanadada ambaye alikuwa nyuma akiwa na yule binti, alifika eneo hilo na kuona hiyo hali, na hapo akasema;.

`Mbona mumesimama, hamumsaidi mwenzenu…’akasema mwanadada, akikimbilia kule kwenye mapigano kati ya mwanasheria na huyo jamaa na alipofika tu, akasikia mlipuko wa risasi,…..oh, mwanasheria akapanua mdomo, na kudondoka chini, na yule mtu alipoona hivyo, akainuka kutaka kukimbia, lakini hakuweza hata kuinua mguu.

Risasi ililengwa bara bara, kutoka kichani, na yule mtu akatoa macho ya uwoga, na kudondoka chini, na hapo mwanadada na mkuu, wakawa wameduwaa, ina maana kazi yote imekuwa ni bure, ina maana masharti ya msituni yamevunjwa, na haijulikani ni kitu gani kitatokea.

Mkuu akamkimbilia yule mtu, na kuhakikisha hana silaha, na akamshika kuangalia kama yupo hai, na akainua kichwa kumwangalia mwanadada na kusema;

‘Mhh, haponi, unaona risasi ilipopigwa, kama akipona ni bahati yake…lakini ni nani kampiga risasi?’ akauliza huku akingalai upande ule aliofikiria kuwa huenda ndipo mpigaji alipokuwa, na eneo lile lilikuwa na kichaka, akasema;

‘Hamjamuona mtu eneo hilo?’ akauliza

‘Hakuna mtu, ila kuna dalili kuwa kulikuwa na mtu eneo hilo, atakuwa amekimbia, wenzetu wawili wanamfuatilia, na gari la wagonjwa limeshafika, naona wengine wanakuja kuwachukua majeruhi, …’akasema askari

‘Sawa, huyu …’akampiga na buti usoni

‘Bado yupo hai, mbona anaonekana kama kafa…’akasema huyo askari.

‘Acha afe, nyie hangaikeni na watu wetu, ..’akasema huyo mkuu, akimgeukia binti yake, na akamsogelea. Bini yake, alikuwa katulia kimiya, na alipoona baba yake anamsogelea akawa kama anaogopa, na kutoa macho,

‘Pole binti yangu, haya yamekwisha, usiogope tena…’akasema na huyo binti akawa anatoa macho kuangalia, na mkuu alijua kuwa binti yake anamuogopa yeye, na akawa anajitahidi kumsogelea huku akitabasamu, na hapo binti yake akainua mkono na kuonyeshea nyuma ya huyo mkuu.

Mkuu, akashangaa, na akageuza kichwa nyuma, kuangalia ni nini binti yake anaonyeshea, na mwanzoni hakuwa na mawazo yoyote zaidi ya kuona kitu cha ajabu ambacho kilimfanya binti yake atoe macho, lakini alipoweka fikara zake vizuri, akagundua…

‘Oh, huyu mtu ka..ka….ka…’akashidw hata kumalizia na binti yake akasema;

‘Karuka kama ndege na kupaa hewani…’akasema

‘Haiwezekani….’akasema huyo mkuu

‘Ndio,huwa lile koti alilovaa akilinyosha, linakuwa kama mabawa ya ndege, na huruka kwa haraka haraka, kama anapaa…’akasema na mkuu, akamwangalia binti yake kwa mashaka, hakujua kuwa binti ake anamfahamu huyo mtu kiasi hicho, akasema;

‘Umejuaje hayo….?’ Akauliza na binti yake, akainama kwa woga, …..

********

Mwanadada akakimbilia pale alipolala mwanasheria na kumuinua kichwa, na kwanza aliangalia pale jereha lilipo, ilikuwa kwenye mkono wa kushoto, ni karibu kidogo na eneo la moyo,…akachukua leso yake na kuweka kwenye lile jeraha ili lisiendelee kuvuja damu, na mmoja wa watu wa usalama anayefahamu mambo ha huduma ya kwanza akafika na kuanza kumsaidia…

Na alipowekwa vyema, mwanadada, akamsogelea na kumwangalia huku akihisi mwili mzima ukimuisha nguvu, akakaa karibu na alipolala huyo mwanasheria, na kunyosha miguu yake, akainua kichwa cha mwanasheria na kukiweka mapajani mwake, na kujaribu kulia, lakini hakuna cha machozi, wala sauti ya kulia, akainama na akawa kama kamlalia kichwani mwanasheria huyo, na ghafla mwanasheria akafunua macho na kumwangalia mwanadada, akasema;

‘Naku-ku-penda sana mwana-na-dada, kumbuka hilo,..na..na siku zo-te zo-te nili-kuwa naji-ji-tahidi nikuambie kuwa hata iweje, mi-mi sita-kuacha…’akatulia kama anatafuta pumzi.

‘Tulia mpenzi usijilazimishe kuongea….’akasema mwanadada akiwa na macho ya huzuni, na akahisi machozi yakija kwa kasi machoni, lakini hakutaka yatoke ili kumpa moyo mtu wake.

‘Lakini kwanza…. i..i…libidi nitimize wajibu wangu wa kifamilia…’akasema na kuwa kama anahema kwa kasi, halafu akatulia, na mwanadada akamwangalia akihisi huenda keshakata roho, lakini mara mwanasheria huyo akafungua mdomo na kusema;

‘Kwa hali ilivyokuwa, ilibidi nitimize ahadi yangu kwa ndugu yangu kuwa nitailinda familia yake…’akaongea vyema na mara sauti ikakatika, halafu akasema kwa haraka haraka

‘Lakini moyoni nilijua kuwa nina ahadi yetu, kuwa tunahitajiak kufunga ndoa..na..na..ikumbuka sana hiyo ahadi, tuliyowekeana,kuwa ni lazima tufunge ndoa..ndo-ndoa….sasa sijui kama ita-we-ze-ka-na..’

‘Itawezekana mpenzi, usikate tamaa, nakuomba sana usiniache, tutimize ahadi yetu ya ndoa, tafadhali usiniache…nakupenda sana mpenzi, ….’akasema mwanadada huku akishindwa kuyazuia  machozi ambayo yaliazna kutoka kama maji.

‘Sijui…sijui..mwanadada..nahisi siku zangu zimefika, …, iliyobakia sio uwezo wangu tena, …namuachia mungu , kwani namuona kaka yangu akinisubiria kwenye makazi ya milele,..nakuomba sana, kama nitakufa,ilinde familia yangu, …'akasema huku akikunja uso kuonyesha maumivu.

'Nina...maana mwanamama na mtoto wake, wapeni haki yao …hilo lilikuwa ni jukumu langu..sasa, naona nimeshindwa kulitimiza, kaka zangu watanilaumu…la…la..kini, utaweza kunisaidia…niahidi kuwa utanisaidia hivyo…’akasema na kutoa macho kumwangalia mwanadada, na mwanadada akajitahidi kutabasamu na kutikisha kichwa kukubali huku akisema.

‘Usiseme hivyo, hutakufa mpenzi, ….mwanamama na mtoto wake tutaishi nao…..nakuahidi haki yao haitapotea, mimi na wewe tutahakikisha hilo…..’akasema huku akitaka kupiga ukelele kuwa wawaambie watu waharakishe kulete gari la wagonjwa, akaangalia lile jeraha, ambalo kwa muda ule lilikuwa halivuji sana damu…’halafu akageuka kumwangalia mwanasheria usoni, akamkuta keshafunga macho.

Mwanadada alihisi mwili ukimsisimuka, hasira chuki, ..na moyo wa kisasi ukaanza kumwingia kwa haraka sana, na hapo akamuweka mwaansheria chini taratibu , kwanza akambusu shavuni, na pili, akachukua ile bastola aliyokuwa nayo huyu mwanasheria, akaitayarisha tayari kwa kuitumia, na kugeuka pale alipolala yule mtu wao akiwa kajaa jaziba, na ….

Macho yalipotua pale alipokuwa kalala yule mtu, yalikuta hayupo, ooh, hayupo…akageuka upande waliposimama mkuu na mwenzake ambao walikuwa wakihangaika huku na kule kumtafuta huyo mtu na wengine walikuwa wakihangaika kuwabeba majeruhi, na akahisi huenda wameshambeba huyo mtu na kuondoka naye, lakini akili haikutaka kulikubali hilo, kwa muda upi wamembeba bila ya yeye kusikia , au kuwaona;.

‘Jamani mtu wetu yupo wapi?’ akauliza.

Na wote wakasimama kumwangalia mwanadada huku wakiwa hawaamini hilo lililotokea, na mkuu akasema;

‘Katoweka kiajabu…binti yangu anasema kamuona akiruka kama ndege,kwani koti lake lina mabawa, kwahiyo anakuwa mwepesi…tumejaribu kutafuta kila kona hakuna dalili ya uwepo wake…..’akasema huyo mkuu, akiwa bado hajaka tamaa…

‘Lakini alikuwa katika hali mbaya ya kukata roho, ndio maana hakuna aliyemjali sana, mimi mwenyewe nimeona lile jereha, na hali aliyokuwa nayo…’akasema mkuu, huku akiangalia huku na kule,na mara akaona michirizi ya damu ikielekea porini...akaitizama.

Akaanza kuifuatilia na kabla hajafika mbali mara kitu kama radi, kikasikika,upepo mkali ukaanza kuvuma, hadi miti inataka kung’oka, msitu mzima ukawa kama umeingiliwa na vitu visivyojulikana, makelele kama ya popo, na milio isiyo ya kawaida ikatawala, harufu mbaya kama uozo wa mizoga ukatawala puani, na hapo kila mmoja akawa anahangaikakuziba masikio.

‘Jamani hapa hakuna amani tena, tuondokeni haraka…’akasema mkuu, na mwanadada akageuka kumwangalia mwanasheria ambaye kwa wakati huo alikuwa kabebwa kwenye machela, akipelekwa sehemu ambayo gari la waginjwa lipo, maana huko juu kulikuwa hakupandiki na magari, na mwanadada hapo alishindwa kujizuia akajikuta analia na kusema kwa suati;

 ‘Nakupenda mwanasheria, nakuomba usife..ukiniacha nitabakia na nani….ooh, kwanini….’akawa anasema lakini sauti yake ilikatishwa milio ya ngurumo na sauti za milio ya popo, na walipoangalia juu wakaona popo wakija pale walipo kwa kasi, na hapo hakuna aliyesubiria, kila mmoja akaanza kutimua mbio kivyakeaf, 
kuelekea nje ya huo msitu…..

NB:JE kutatokea nin..ni sehemu ndogo ya tukio la msituni, tukirudi tunaingia kwenye hitimisho la kisa chetu,


WAZO LA LEO: Maisha ya binadamu sio ya moja kwa moja, kuwa utapata raha, siku zote, kuwa ndoto zako zitatimia kama ulivyopanga, kuwa utampata rafiki, au wote watakuwa wema kwako, mitihani ya aina mbali mbali inaweza kukutokea hadi ukafikia kusema kwanini mimi…ndio ni lazima useme hivyo, kwasababu uhimili wa kibinadamu una mipaka, lakini tukumbuke kuwa yote ni mapenzi ya mwenyezimungu, tusikate tamaa, na tujipe moyo, kuwa baada ya dhiki ni faraja.
Ni mimi: emu-three

2 comments :

Rachel Siwa said...

Hakika Ndugu Wa Mimi HUNA MPINZANI..MUNGU baba amekupa kipaji!!!

Hongera munooo..
Naunga mkono na wazola Leo.
Pamoja saana.

Anonymous said...

I loved as much as you will receive carried out
right here. The sketch is tasteful, your authored
material stylish. nonetheless, you command get bought an nervousness over that you wish be delivering
the following. unwell unquestionably come more formerly again since exactly
the same nearly very often inside case you shield this increase.


Stop by my homepage: the tao of badass review