Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeSunday, August 18, 2013

WEMA HAUOZI-50
Hapa mwanadada anaelezea jinsi ilivyokuwa baada ya kuingia kwenye msitu, ulikuwa msitu mnzito, uliojaa wadudu, wanyama na hisia za kutisha, na wengi huwa hawapendi kuingia ndani ya msitu huo au kusimulia habari zake kutokana na historia yake, kuwa kulikuwa na vita nyuma na watu wakakimbilia hapo, kujificha na wengi wakapotea humo kabisa.

‘Huku kuna mambo mengi ya kutisha, historia inatuambia mababu zetu waliokimbia vita, au wale waliokimbia kodi walikuja kujificha huku, na kujenga mahandaki, …kama mnavyoona haya ni mahandaki, zilikuwa nyumba za mababu zetu…..’akawa anasimulia huyo jamaa ambaye ndiye kiongozi wa msafara akionyesha baadhi ya mashimi yaliyokuwa yameanza kujifukia.

‘Mimi mwenyewe nilizaliwa huku, kabla wazazi wangu hawajahama, na kukimbilia huko uraiani, wazazi wangu wanasema walikuwa wakionywa kuwa wasije wakahama na kwenda huko uraiani, waliambiwa kuwa wakihama huku na kuja kuishi huko uraiona tutauliwa, kwani watu wa huko ni wakatatili, wauwaji …lakini vijana hawakusikia wakati huo wazazi wangu walikuwa bado vijana, wanatoroka mmoja mmoja, na kubakia 
wazee….’akaendelea kusimulia.

‘Wazee wakabakia bila watu wa kuwasaidia wakawa wanajifia ndani ya mahandaki, hadi kizazi hicho kikapotea kabisa na ndio maana inasadakiwa kuwa kwenye mahadaki hayo kuna mizimu, mizimu hiyo ndio hawo mababu waliojifia wenyewe wakiogopa kutoka nje….’akasema.

‘Kwa mfano kule tulipotoka, wale sio wanadamu wa kawaida…’akasema na hapo mwanadada akaona aulize.

‘Lakini mbona wanaongea kama sisi…’

‘Ndio wanaweza kujigeuza hivyo, ..lakini hawana maisha kama yetu,…na niwaambie ukweli wapo mizimu wazuri na wabaya,hawo sasa hivi ni mashetani,…sio watu kama wale tuliokuwa tukiwajua, ukikumbana na hayo mashetani, yanaweza kukuzuru kama ni yale yenye tabia chafu…’akasema huku akiendelea kunyunyuzia vitu kama unga kila walipopita…na kuzuia upepo, ambao ulikuwa ukija, na kuondoka,na baadaye akatulia na kuangalia huku na kule, akatikisa kichwa na kusema;

‘Huku sasa hakuendeki, naona mambo magumu,…sijui tumepotea,au haturuhusiwi kuendelea mbele, naona ujuzi wangu wa zidi ya hapa sina, lakini twendeni,…..’akasema yule mtu huku akijitahidi kuuzuia ule upepo na usinge wake, na akiwa kama kashikilia kitu kizito mkononi mwake,

‘Sasa tufanyeje?’ akauliza mwanadada alipoona yule mtu anakuwa kama kabeba mzigo mzito, misuli imemtuna na jasho linamtoka

‘Sijui…sikuwa nimefikiria hili kabla, nilijua ni jambo rahisi sana kwa vile niliwahi kuishi huku nikiwa mtoto mchanga, na nahisi kuwa wakioniona wanaweza kunikumbuka na kunionea huruma maana ni damu yao….hata hivyo, nina imani kuwa hawataweza kutuzuru, tusonge mbele kidogo…tukikwama basi,hakuna jinsi itabidi turejee huko tulipotoka…’akasema

‘Kwahiyo, ina maana wao wanakufahamu wewe…kwanini usiongee nao?’ akauliza mwanasheria

‘Wananifahamu, nay a kuwa damu ni nzito kuliko maji,…lakini nahisi damu, nahisi ubaya mbeleni, kuna kitu ambacho sio cha akwaida,kilitendeka, sijui ni miongoni mwetu, au….hapa sasa inahitajika…maombi ya ziada, na kama kuna mmoja wetu ana damu ya mtu, kama kuna mtu mbaya bora aondoke…’akasema huyo mtu, na mara ule upepo ukatulia, na huyo mtu akaangalia tena huku na kule;

‘Naona mababu wametusikiliza kilio chetu, haya twendeni haraka kabla huo upepo haujarudi tena, huo sio upepo, kama mnavyohisi, ni kundi la mizimu, limekuja kutuangalia sisi ni nani, na wamegundua kuwa sisi sio watu wabaya, …hata kama yupo mwenye ubaya, sio mbaya wa kutishia amani yao.’akasema

‘Kwanini tusilimalize hilo kundu kwa risasi?’ akasema mmoja wa watu waliokuwepo kwenye huo msafara.

‘Usije ukajaribu kitu kama hicho…huoni wamegundua dhamira yetu, ndio maana wameondoka, kwanza walikuwa wanatupima, kama tutafanya fujo….wakagundua kuwa hatuna ubaya, ila nahisi kuna kitu kibaya kipo maeneo haya….’akasema huyo mtu na walipofika mbele, wakaona msitu umefunga kote.

Kulikuwa na aina ya mimea iliyoota kama kamba, ikatanda kama nyavu, kiasi kwamba huwezi hata kupitisha mkono, na aina ya miti yenye miba mikali ilikuwa imesheni kila kona, hapo yule mtu akawa anahangaika huku na kule, kutafuta upenyo, lakini kulikuwa hakuna hata sehemu ya kuingiza mkono.

‘Tukiweza kupita hapa, basi tumeshafanikiwa…tutakuwa tumeingia sehemu ya watu wa zamani ambao ni wema, wanaweza kutusaidia’akasema

‘Basi tufyeke?’ akauliza mmoja wa watu waliokuwepo

‘Panga halikati hapa..wewe unaona ni majani lakini ni zaidi ya majani, …’akasema huyo mtu, na hapo hapo akatoa kitu kama unga na kuanza kunyunyuzia kuzunguka yale majani, na mara ukatokea moshi, ukatanda hewani, na ghafla kukatokea kitu kama mngurumo, au radi,…ilikuwa kali mpaka watu wakawa wanaziba masikio

Ule mngurumo ulipokwisha, mara yalemajani yakawa kama yanasogea, kama vile mtu anafungua mlango, na kukawa kunatokea barabara, inayoelekea mbele,..

‘Sasa tunaingia miji ya watu,….tuwe makini, usikanyage kitu, usiokote chochote, ….tembea kunifua mimi ninavyotembea…’akasema huyo mtu akinyata na kuruka pale alipoona kitu, na sisi tukawa tunafanya hivyo…’akawa anaendelea kusimulia mwanadada,akimsimulia mama yangu ambaye alikuja kunisimulia hiki kisa ninachowahadithia….

Na wote wakawa wanamfuatia nyuma,…. nyuma hatua kwa hatua hadi wakatokea kwenye mapango,…mapango hayo yalikuwa mengi, na ilionyesha kama nyumba za watu, kwani sehemu ya kuingilia ilikuwa kama inatumika, …

‘Kazi iliyobakia ni kulitafuta pango letu…’akasema na kuanza kunyunyuzia tena ule unga unga, na alipomaliza kukatokea sauti za kama watu wanaongea , sauti nyingi kisai kwamba huwezi kujua wanachoongea ni nini, lakini hakuna mtu aliyeonekana, na huyo mtu akasema

‘Hodi waungwana, tumekuja, sisi ni wageni wa mtu wetu, anayeitwa mtalaamu, je tumemkuta?’ akauliza na zile sauti zikanyamaza na mara kwenye moja ya pango, kukatokea mtu wa ajabu, uso wake ulikuwa kama upo kwenye giza, yanaonekana macho tu na na kumeta meta kama anawaka moto….

Yule mtu alikuwa kashikilia fimbo ndefu nyembamba,  na akawa kasimama tu,na uso ukawa anafunikwa unafunuka, na macho yakawa yanatuangalia , kama vile yanatusoma ndani ya mioyo yetu,  akaonyesha ishara, ambayo hatukuijua ile huyu muongozaji wetu akatuabia kuwa tumeambiwa tumfuate, na wote wakafanya hivyo, hadi pale kwenye mlango wa lile pango,….na yule mtu, au uso wa mtu , kwani kiwiliwili kilikuwa hakionekani, akaonyesha ishara, na huyo muongozaji akasema tumeambiwa tuvue viatu, na wakafanya hivyo na kubakia miguu mitupu, na halafu akaonyesha ishara ya kuwa waendelee kumfuata kuingia ndani ya lile pango.

Mwanadada, anasema walijikuta wakiingia kwenye hilo pango, na kulikuwa na kitu kama milango mingimingi, na mlango mmoja ukafunguliwa, na hapo wakajikuta wapo kwenye sehemu kama chumba kikubwa kiasi……ilikuwa ni nyumba iliyonakishiwa na udongo, kama vile ukuta uliowekwa maru maru…..za rangi mbali mbali….na kwa mbele yao kulikuwa na milango mingi na hawakujua kitafuata nini baadaye

Mara ikatokea fimbo, ilikuwa ya yulee mtu akaelekea kwenye mlango mmojawapo uliokuwa mbele yao, na ile fimbo ikagusa na ule mlango ukafungua, na yule mtu wao muendeshaji wa huo msafara, akawaambia wameambiwa waingie  na walipoingia wakajikuta kwenye eneo pana kama ukumbi, ukumbi usio na viti wala meza, lakii cha ajabu kulikuwa na harufu za vyakula kama hotelini.

Walipogeuka nyuma hawakuona mtu , na ile sura iliyokuwa ikiwaongoza, yenye fimbo haipo tena, wakatulia na mara wakasikia sauti ikisema

‘Karibuni wageni…tuwasaidie nini’sauti ikasikika bila kuonekana mtu
Mwanadada akasema kwa jinsi alivyokuwa kachoka alitamani kusema anahitaji chakula na maji lakini akasita, akikumbuka kuwa walipewa tahadhari ya kutokushika chochote mpaka watakapopewa maagizo, na yule mtu waliyeongozana naye, kapiga magoti na kusema

‘Waungwana tuna shida, tunamtafuta mtu wetu anajulikana kama mtaalamu, …

‘Mtaalamu,..huyu mtu sio mtu wa huku kwetu, …hatumjui’hiyo sauti ikasema na kukapita kitambo kidogo.

‘Lakini katuambia yupo huku, akiwa kwenye mateso kwa madhambi aliyoyafanya….’akasema huyo muongozaji wetu.

‘Hatuwezi kumkaribisha mtu kama huyo huku kwetu, mtu huyo anaonekana ni mchafu, mikono yake imejaa damu,….huyo atakuwa anaishi sehamu nyingine za walio hai,..lakini sio huku kwa wafu wasio na mdhambi…’akasema hiyo sauti.

‘Tunaomba utusaidie, ili tuweze kumpata’akasema huyo mtu.

‘Nendeni na n jia ileee, mtafika sehemu alipojificha,…’akasema na mara ikaonekana kitu kama njia, na ile sauti hakusikika tena, na akina mwanadada na wenzake wakabakia wenyewe, na yule mtu wao muongozaji, akasema

‘Twendeni….’na wote wakafuata ile njia na haikuchukua muda, wakajikuta wapo nje kabisa ya hayo mapango, na kujikuta kwenye nyika, sehemu ya kawaida, na hata walipogeuka nyuma hawakuona kitu zaidi ya yale majani yaliyojitanda kama nyavu.

Mara kwa mbali wakasikia kitu kama mngurumo wa pikipiki, na wote wakaambiwa wajifiche, na ile pikipiki, ilipofika pale walipokuwa wamesimama mwanzoni, yule mwendeshaji akashuka na kuvua kofia, hapo ikasimama kwa muda, kama anawaza jambo,  akaangalia huku na kule, na alipohakikisha kuwa yupo peke yake, akainama na akainua majani, yale majani yalikuwa kama mkeka uliotandazwa, na chini yake kulikuwa na mfuniko kama ile ya matanki makubwa, kumbe pale kulikuwa na mlango, na mara yule mtu akalisogelea lile pikipiki lake na kulisogeza hadi kwenye ule mlango, akawa analiigiza lile pikipiki, na alipomaliza kuliingiza yeye mwenyewe akaingia.

Na yale majani yakawa yanavutika kidogo kidogo hadi yakafunika eneo lote na kuwa kama kawaida, huwezi kujua kuwa kuna kiu kama hicho…

‘Mumeona, ….hapo ndipo anapojificha mtu wetu…’akasema huyu muongozaji.

‘Lakini yule ni nani?’ akauliza mwanasheria

‘Hahahahaha..ina maana mumeshamsahau mtu wenu , yule ndiye mtaalamu, ..keshajibadili, ..kuanzia siku alipoondoka pale mahakamani, alijibadili, kwa kuvua yale manguo aliyokuwa akivaa, na ngozi ya kichwani ambayo ilikuwa na ndevu ndefu…sasa hivi anafanana na ……’akasema na kusita kidogo

‘Anafanana na kiongozi wa kijiji…’akasema mwanadada, na wote wakageuka kumwangalia mwanadadam na mwanadada akasema

‘Nyie hamukumwangalia vyema alipovua lile kofia, kwa vile mlikuwa mkiogopa, mimi nimeweza kumwangalia sura yake, anafanana kabisa na kiongozi wa kijiji, utafikiri mapacha…’akasema mwanadada.

‘Kwani hawa watu wawili ni mapacha?’ akauliza mwanasheria.

‘Hapana sio mapacha, lakini ilitokea kufanana sana, kila mmoja ana mama yake, ila baba yao ni mmoja, na kila mmoja kachukua tabia ya mama yake…’akasema huyo mtu wao.

‘Sasa tufanyeje?’ akauliza mwanadada.

‘Kwanza na ni muhimu, huku hakuruhusiwi kupigana kwa risasi, milio ya bunduki hairuhusiwi eneo hili,…kwahiyo kinachotakiwa na kutafuta njia za kumkamata, sina uhakika huko ndani kupoje, …’akasema huyo mtu.

‘Sio kama huko tulipotoka..?’ akauliza mmoja wa watu wa usalama.

‘Hapana, kule uliona kulivyokuwa, kule sio kwa kawaida,..yale ni makaburi….’akasema na watu wakashangaa, nay eye hakusema jambo jingine akawa ananyunyuzia  unga unga hewani, na baadaye katulia.
‘Hapa sio eneo la mizumu….na eneo la kawaida, tu, kwahiyo mtu wetu anaishi maisha ya kawaida 
tu….’akasema

‘Tufungue tuingie….’akasema mmoja wa watu wa usalama..

‘Subirini….’akasema mwanadada alipoona ishara kwenye simu yake, na ilikuwa ni meseji, ikimwambia kuwa mtaalamu haonekani kawapotea watu wake.
Na yeye akawajibu kwa ujumbe wa maneno kuwa wameshaona wapi anajificha, na anahitaji msaada wa maaskari

‘Tuelekeze wapi mlipo, tupo  na askari wa kutosha,…’ujumbe wa maneno ukasema na mwanadada akamsogela yule mtu wao na kumuuliza hapo walipo ni wapi

‘Waambie tupo milimani,kwenye mapango ya watu wa kale, wakifika waache mapikipiki yao kwenye mwanzo wa milima, hakuhitajiki kelele za mingurumo au milio ya bunduki, na wafuate njia ya kale, watafika sehemu ambayo tutawapa ishara, na watatuona wapi tulipo…’akasema na mwanadada akaandika ujumbe

‘Mbona tupo karibu na sehemu hiyo…’ujumbe ukasema na mwanadada akamwambia huyo mtu wao

‘Basi waambie wasubiri, ….’akasema na hapo akatoa ule usinge wake na kuunyosha juu, na kupuliza mwanzo kwa nyuma kule anaposhika, na yale manyoya ya ule usinge yakawa kama yanapepea angani..

‘Waambie waangalia hewani, wataona kitu kama mshale na waufuate huo mshale unaoelekea angani…’akasema na mwanadada akaandika hivyo..

‘Sasa tuwasubiri wenzetu, na nina shaka, huenda huyu mtu keshatuona…’akasema huyo muongozaji

‘Kwa vipi?’ akauliza mwanadada, na yule mtu akawa anaangalia huku na kule, na kwa mbele akaona mtu mkubwa, na kusema

‘Baadhi waende kwenye ule mti wachunguze kuna nini, hayo mnayajua nyie, sio utaalamu wangu…’ akasema na watu wawili wa usalama wakafanya hivyo, na mmoja akarejea na kusema;

‘Kuna waya wa antenna, na juu uliokwenda juu kabisa kileleni mwa huo mti, na mwisho wake kuna antenna ….inayofanya kazi, …’akasema

‘Mnaona hayo ni mambo yenu, kama mnajua jinsi ya kuizima fanyeni hivyo haraka…’akasema na yule mtu akatoa simu yake na kuandika ujumbe kumuelekeza mwenzake aliyemuacha huko, na baadaye ukaja ujumbe kuwa haiwezi kuzimwa, labda ukatwe ule waya.

‘Anasema kwa juu huwezi kuizima, labda tukate huo waya…’akasema

‘Basi fanyeni hivyo haraka…’akasema huku akiendelea kungalia huku na kule

Yule mwanausalama anaondoka kumfuata mwenzake, baadaye walirudi wote wawili na kusema waliona huo waya ukiwa umetoka ardhini, wakaufuatilia , na kukuta kweli huo waya umezama kwenda chini, na hata walipojaribu kuuvuta haukuweza kuvutika….basi wakaukata.

‘Kama hakuna kitu kingine kama hicho, tutakuwa salama , hataweza kutuona, maana hana nguvu za misimu tena, huyo keshatengwa, anatumia ujuzi wake wa kiaskari…’akasema

‘Kwani mtaalamu ni askari..?’ akauliza mwanasheria.

‘Ndio alikuwa askari, aliyeasi, na kufukuzwa, na aliporejea akawa karibu sana na babu yake, na babu yake, upande wa mama yake, na huyoo babu yake, ni mtu wa huku milimani, wakamuombea apewe mikoba, na ndipo alipoapata huo ujuzi, japokuwa mizimu ilikuwa imeshaundua kuwa sio mtu mwema, …

‘Sasa kwanini walimpa hiyo mikoba?’ wakauliza

‘Ni ili iwe mitihani kwetu…ili haya yatokee, ili mjue kuwa sio kila mtu anayeshi kwenye wema ni mwema,yeye ni chui aliyevaa ngozi ya kondoo….mtakuja kumjua baadaye, ni ni mjnaja kweli kweli…’akasema huyo mtu.

‘Wewe umemfahamuje?’ akaulizwa.

‘Pamoja an kumfahamu katika hali ya kawaida, maana alikuwa ni rafiki yangu kipindi tunatafuta dawa, tulikutana huku huku milimani, mimi nahangaiaka na dawa na yeye halidhalika, tukapimana ubavu..maana haya mambo yetu mkikutana ni lazima kupimana …tukagunduana kuwa sote ni watu wa njia moja…’akasema

‘Tukawa tunakutana mara kwa mara…nilikuja kugundua kuwa mwenzangu ana tamaa, …tamaa za ujana, na mimi sikuwa an tamaa hiyo, tulianza kukosana, na kila mmoja akawa na maisha yake, na mimi nilihama kijiji hiki na kwenda kuishi kijiji cha jirani, sikujua ni nini kilitokea, hadi nilipoelelekezwa na mizmu…’akasema

‘Ulielekezwa kufanya nini?’ akauliza.

‘Kuja kumsaidia mama mkunga…’akasema

‘Kwa vipi?’ akauliza

‘Mama mkunga alitakiwa auwawe, kabisa, lakini haikuwa hivyo, aliokoka kwenye ule moto,.na maji yaliyomwagika kutoka kwenye mtungi, maji yale alikuwa akiweka kwa ajili ya kunywa, maji yale mara kwa mara alikuwa akiwapa watoto mayatima, yalikuw aya baridi sana,…’akatulia.

‘Baraka za wema huo, zikawa zimejiweka kwenye ule mtungi, na siku hiyo alipofikwa na janga hilo, baraka zile, ndizo zikatokea, na ule mtungi ulipopasuka yale maji yalikuwa ya baridi sana, yakapooza ule moto, na kupunguza ukali wake….’akatulia.

‘Kwahiyo kote kulizunguka moto, isipokuwa pale alipolala, kwani yale maji yalikuwa yametiririka kumzunguka, …na alipozindukana akatembea hadi msituni na huko akakutana na mimi, nikamweka hizo dawa, na majeraha yakapona…’akasema.

‘Ngoja ngoja …mbona huyo mtalaamu alisema ni yeye alifanya hivyo, akambeba na kumpelea porini…’akauliza mwanasheria.

‘Mengi aliyoyasema pale yana ukweli, kiasi fulani, lakini aliyapanga yawe hivyo…ni kweli alifika akamuona akiwa kalala pale kwenye maji machafu, aliyaona kama maji machafu, na alipomwangalia aliona kama ameshakufa,…akaondoka’akasema huyo mtu.

‘Hatujakuelewa bado…’akasema

‘Huwezi kuelewa kwa ujanja wa huyo mtu, ambaye alikuja kugundua baadaye kuwa huyo mama hajafa, na ni kipindi mizumu imeshaanza kumsumbua, na alipouliza ni kwanini mizimu inamtenga akaambiwa, na hapo akaja na uwongo huwo, alishagundua kuwa huyo mama yupo hai, na huyo mama hajui ni nani aliyemtibia hayo majeraha yake…’akasema huyo mtu.

‘Kwahiyo hata huyu mama hajui kuwa ni wewe uliyemtibia?’ akaulizwa

‘Anafahamu…ila nilimwambia asiseme lolote kuhusu hayo yaliyotokea hadi muda muafaka ukifika, atakuaj kwuasimulia mwenyewe yote hayo mkimsimisha kutoa ushahidi…’akasema huyo mtu.

Mara sauti zikasikika na huyo mtu akatoa ishara kuwa wajifiche, na baadaye wakatokea watu wa mkuu wa kituo idara ya upelelezi, na walipofika pale wakawa wamesimama wakihangaika kutafuta wapi walipokuwa wakina dada.

‘Tupo huku….’akasema huyu mtu wao, na wale watu walikuwa tayari wametoa silaha kwa kujihami, na mwanadada akatokea, na wote wakakutana, na hapo mipango ya kuingia ndani ya hilo shimo au pango ikapangwa,

‘Hatuna uhakika huko ndani kuna nini, je ana silaha, je, ana watu wengine…’akasema mwanadada.

‘Silaha anaweza kuwa nazo, lakini anafahamu taratibu za huu msitu, hataweza kuzitumia, anaweza kutumia silaha nyingine, kama sumu, ..amabzo zinaweza kuwapofua, zipo kama tindikali, …ni hatari zaidi ya hizo silaha,…’akasema huyo mtu wao.

‘Sasa tufanyeje…’akauliza mwanasheria.

‘Hiyo ni kazi yenu, hayo ni mambo yenu, mimi nimeshamaliza kazi yangu,…naweza kuondoka…’akasema huyo mtu na mwanadada akasema

‘Hapana usiondoke tunakuhitajia sana, na nakuomba uwepo mahakamani kutoa ushahidi…’akasema mwanadada.

‘Mimi utaalamu wangu unaishia hapa,…zaidi ya hapo, nitakuwa nawadanganya, mambo ya silaha, na utaalamu wa antenna ni amabo yenu ya kisasa…’akasema huyo mtu.

‘Tunakuomba tu uwe nasi, maana tukiwa na wewe , kwenye huu msitu tunajisi amani, au kuna tatizo jingine linaliweza kukufanya usiwepo?’ akaulizwa.

‘Mizimu hainiruhusu kuingilia mambo ya huyu jamaa , nimeruhusiwa kisai hicho, …na baada ay hapo nahitajika kurejea kwangu, kama mtanihitajia zaidi mtakuja kijijini kwangu, na jinsi ya kutoka hapa hamtapata shida tena,…mtaongozwa vyema kabisa, msiwe an shaka, ila nawaomba msitumie silaha, …’akasema na akawa anajiandaa kuondoka.

NB: JE ni nini kitatokea.


WAZO LA LEO: Kuna historia ya mababu zetu, kuna historia ya misitu ya ajabu iliyogubikwa na maelezo mengi ya kusisimua, hivi haya yanaachwa yapotee hivi hivi....historia na visa vyake vinasisimua kwa ajili ya kumbukumbu za vizazi vetu..

Je kuna wanahistoria wameshafanya tafiti hizi, na kuweka kumbukumbu hizi za kale. Historia itatusuta pale tutakapobakia na historia za akina Kali Petre na akina Vasco Dagama, wakati huku wetu walikuwepo akina Mkwawa, Mangi. Nk, pia walikuwepo mababu zetu waliokuwa na fani za kila aina…tusiwe watumwa hata wa kihistoria, tusikubali kuwa tegemezi kwa  kila kitu, Jamani hata historia yetu tunahitajia wafadhili kutoka nje, .....

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Buenas Sólo quería decirte que algunas de las imágenes no se cargan adecuadamente.
He probado en tres navegadores diferentes y todos muestran los mismos resultados .


Feel free to visit my web-site ... skineart.com