Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, July 15, 2013

WEMA HAUOZI-35


Kesi ilianza kwa kasi sana washitakiwa wote walikana mashitaka yao, na haikukubalika dhamana yoyote, kwasababu zilizotajwa kuwa ni za kiusalama kwao.Wanandnugu waliposikia hivyo, hasa akina mama ambao waume zao ndio hawo walikamatwa kama washitakiwa, walilalamika sana, na hata wengine wakatishia kuandamana.

‘Msifanye hivyo, jamani, kwasababu kushikiliwa kwa waume zenu ni kwa manufaa yao…kama hawana makosa wataachiliwa, lakini kwa uchunguzi wetu, tumegundua kuwa ni bora kuwashikilia huku, ili ushahidi usije ukaharibiwa, na pia tumegundua kuwa hata usalama wao upo hatarini, kama tutawaachia.’akasema mzungumzaji wa muendesha mashitaka hayo.

‘Kwa manufaa gani, wakati sisi tunakufa njaa…hamjui hawo wanaume ndio majembe yetu…tupeni basi pesa za matumizi’akalalamika mwanamke mmoja.

‘Je kama tukiwaachia wakauwawa, ..nyinyi hamjua jinsi gani hilo kundi lilivyojipanga, memeshuhudia mauaji mangapi hapo kijijini, hamjachoka nayo….Ni heri iwe hivyo, kwasababu hamjui kabisa ni hatari gani iliyowakabili hawo waume zenu, ..nyie nendeni nyumbani mkabangaize hicho kilichopo, na msije mkajaribu kuandamana, mtaishia wote jela…’huyo msemaji akawaambia, akijua kuwa kwa kuwaambia hivyo huenda hawo akina maam watatishika.

‘Kwasasa hatuogopi, kuishia jela kwani kuna tofauti gani, maana hivi sasa tupo kama wafungwa, hatuna uhuru, hatuna amani….bora tu tuje take huko rumande na waume zetu…ili muweze kutulisha na ikibid chukueni na familia zetu zote…watoto wanakufa njaa, wengine hawaendi shule kwasababu wanahitajiwa ada….’wakasema.

‘Ina maana hiyo ada imedaiwa kwa siku hizi chache tu, kama mlikuwa hamjaliap ada, hilo ni swala lenu, haliwezi likatokana na kukamatwa kwa hawa watu, maana hata wiki mbili hazijaisha…’akasema huyo msemaji.

‘Wewe kwasabbu muajiriwa, unajau utapaat mshahara, hujui maisha ya watu wa hali zetu, uispokuwepo kweney kijiwe kwa siku moja, hamli..tunabangaiza bora ziku ziende, …sasa siku ngapi tunagangaika kiguu na njia kufuatilia maswala ya waume zetu…’waakzidi kulalamika.

‘Lakini kwanini muwafuatilie, na sisi tumeshawaambia kwanini wamekamtwa, na wapo kwenye usalama,wasiwasi wenu ni nini…..?’ akauliza huyo msemaji akipandisha hasira.

‘Tatizo lako hujui maisha yetu, je tuspowaona hawo waume, wakatuelekeza wapi tungepate chochote, au kama ana akiba kaweka wapi tutawezaje kuishi..nyia hamjui maisha yetu…waume zetu ndio kila kitu, wao ndio wanatunza akina za ndani, wao ndio wadhamini, kama tukitaka kukopa,….sasa mnafikiri tutaishije…’wakalalamika.

‘Ina maana nyie waume zenu walikuwa hawawashirikishi kwenye maswala ay akiba au wapi kukitokea matatizo muweze kujikimu…?’ akawauliza.

‘Toka lini sisi wanawake tukashirikishwa kwenye mambo hayo…wewe sasa unataka kuingilia mambo ya ndani ya familai zetu…sisi tumeshakuambia, kama tusipowaona, kila siku hatutaweza kula…..na mkizidi kuwashikilia, tutakuja na familia zetu….’wakasema na wote wakasema

‘Sawa, tutawaletea watoto…muwaleee, ili muone ugumu tunaokabiliana nao….’wakasema kwa sauti.

Baadaye akabidi kiongozi mmoja wa serikali kuja kujaribu kuwaelimisha ili waelewe  kwanini imefanyika hivyo, na huyo kiongozi hakuwa na cha zaidi, akazidi kusisitiza kuwa kukamatwa kwa wanaume zao, ni kwa ajili ya usalama wao, kwani ilikuja kugundulikanana kuwa wengi  wao walikuwa hatarini kwasababu walitaka kusaidia kutoa taarifa za kundi haramu, ambalo ndilo limekuwa chanzo cha matatizo yote hapo kijijini.

‘Sisi ni serikali na moja ya kazi zetu ni kuhakikisha usalama wenu, na kwa vile tumegundua kuwa kuna watu wamejifanya wao ni zaidi ya sheria, wakajitungia mamlaka yako wenyewe, na kuanza kuharaibu amani ya kijiji kwa masilahi yao binafsi,tumeamua kupambana nao, na wote watafikishwa mbele ya sheria, na kuwajibishwa…na ili tufanikiwe hili, tulihitaji msaada wa raia wema, ambao baada ya kaunza kutimiza wajibu, hilo kundi likaanza kuwaatishia amani,na imegundulikana kuwa hata hawo wlaikuwawa kabla ni kwa ajili hiyo hiyo………

‘Msitudanganye…mbona wengine wapo nje….’akasema mmoja wa akina mama

‘Kwa vile pia hawa watu wamo ndani yenu, na mnaishi nao , itatuwia vigumu kwetu kuwalinda, ndio maana tumeamua kuwahifadhi sehemu ambayo ina ulinzi wa uhakika….na hawo waliopo nje, hawajatishiwa ..na tukigundua kuwa na wao wanahusika au kama wanaweza kutusaidia, na wao tutawachukua kwa nia njema…’akasema huyo mtu wa serikali.

‘Toka lini jela ikawa ni sehemu ya ulinzi,…mnataka kutuulia waume zetu bure…hilo hatukubali, kama wanahitajika kwa ajili ya ushahidi tu, kwanini muwashike, na kama mumegundua kuwa wana makosa,basi wakubaliane dhamana….sisi tumeshatimiza masharti yote ya dhamana,kwanini mnatukatalia, au mnatutaka na sie..tuwe tunakuja hapa kila siku….’akasema mama mmoja kwa sauti na wengine wakashangailia.

‘Sisi kama serikali, tumeliona hilo, na kwa vile tunajua ni nini tunachokifanya, hatutarudi nyuma, kwani tusipofanya hivi, ….baadaye mtakuja kutulaumu,..ni bora nusu shari, kuliko shari kamili…tunaomba mrejee majumbani kwenu msubiri kesi hii iishe, na tunaomba msaada wenu ili tuweze kulimaliza hili tatizo…haraka iwezekanavyo, na kama mnavyoona kesi hii imepewa kipaumbele, itasikilizwa ikiwezekana kila siku, ili iishe haraka….’akasema huyo mkuu wa serikali.

‘Sisi kama kesho wanaume zetu hawataachiwa, au kupewa dhamana, sisi tutaandamana na safari hiyo tutakuaj na familia zetu….’ Akasema huyo mama na wenzake wakamshangilia

Yule mtu wa serikali akamgeukia askari aliyekuwa na naye akamnong’neza kitu, na yule askari akaondoka, na baadaye wale akina mama wakatawanyika kurudi makwao. Na usiku wake baadhi ya akina mama wakakamatwa kwa kosa la kuchochea ghasia.

*********

‘Hebu tuambie haya matukio ya mauaji yanayoendeshwa hapo kijijini unayaelewaje, je kwa mafano  siku ya tukio la kuuwawa wale vijana wewe ulikuwa wapi?’ akauliza mshitakiwa mmojawapo ambaye baada ya kuuliza hili swali aligeuka huku na kule kama anamtafuta mtu.

‘Umeulizwa swali, …kwanini unaogopa kulijibu, una wasiwasi gani, hakuna atakayekuzuru, ukisema ukweli…tumeshawahakikishiwa usalama wenu’akaambiwa.

‘Hamjui jinsi gani maisha yetu yalivyo hatarani, tumekuwa tukuishi kwa wasiwasi, kwani hata kama utakaa na kuongea na mke wako kumuhusu …’akasita kidogo.

‘Kumhusu nani, ni nani mnayemuigopa kiasi hicho, ….’?’ Akaulizwa.

‘Tatizo nyie mkiondoka hapa mnakwenda makwenu, sisi na familia zetu tunakuwa kwenye mashaka,naomba mtuelewe hivyo….’akasema.

‘Je ni nani aliyekuja kuwatishia amani mpaka mkawa kwenye mashaka..?’ akauliza na yeye akakaa kimiya, na sfari hii alikuwa kainama chini.

Wakili mwanadada akasimama na kumuangalai yule mshitakia, akasema;

‘Hivi unataka familia zenu ziendelee kuishi hivyo hado mwisho wa maisha yenu au unataka tatizo hili liishe…wewe ni mwanume kweli si kweli?’ akamuuliza. Na yule mtu akamwangalia huyo mwanamke kwa macho yaliyojaa mshangao.

‘Ina maana..una..ni…..’akasema kwa kigugumizi cha hasira.

‘Kama wewe ni mwanaume kweli, kwanini unamuogopa mwanaume mwenzako, kwanini unaogopa kujibu swali….?’ Akamuuliza.

‘Kama kungelikuwa na njia ya kulimaliza hili ningefanya lolote…na nisingeliogopa kukujibu hilo swali, lakini nijuavyo mimi, tatizo hili haliwezekani kuisha kwa njia hii mnayotaka nyie..’akasema.

‘Wewe unapendendekeza njia gani,ifanyike ili tatizo hili liishe..?’ akaulizwa.

‘Kwanza mumeshindwa kuwakamata baadhi ya watu, na mnakuja kutukamata sisi ambao hatuna lolote…hii ni kuonyesha kuwa hamna uwezo wa kupambana na hawo watu….’akasema.

‘Hawo watu ni akina nani, tuambi ili tuweze kuwakamata…’akaambiwa.

‘Kwanini niwaambie wakati nyie mumesema mumeshakamlisha uchunguzi wenu, na sijui ni kwanini mtukamate sisi wakati hatuhusiki kwa lolote lile…’akasema kwa wasi wasi huku akiinua uso kuangalia upande huu na ule..

‘Nimekuuliza mwanzoni wewe ni mwanaume au sio mwanaume, hukuweza kujibu ina maana hujiamini…..’akasema huyo wakili mwanadada akimkazia macho.

‘Mimi ni mwanaume….unataka nikuonyeshe vipi kuwa mimi ni mwanaume wkati unaniona kuwa mimi ni mwanaume…’akasema kwa sauti ya ukali.

‘Kuvaa nguo za kiuwanaume sio sababu, nyie si ndio majumbani mnatamba kuwa nyie ni wanaume hamtishiki..sasa leo vipi, mbona mimi mwanamke siogopi, nimesimama hapa kuwatetea ili haki zenu zipatikane, mbona siogopi mtu….?’ Akamuuliza na yule jamaa akajikuta akiinama chini.

‘Sasa kama wewe ni mwanaume, na unajua kutongoza…nionyeshe huo uwanaume wako….uniangalie kama mwanaume na unijibu maswali kama mwanaume…mbona inakuwa kama mimi ni mwanaume….’akasema huyo wakili mwanadada, na watu wakacheka na huyo jamaa akainua kichwa na kuangalia mbele.

‘Je huko unapoangalia, kuna mtu unamuogoa, ..yeye ni mwaume kuliko wewe?’ akaulizwa.

‘Hakuna mtu ninayemuogopa, mimi ni mwanaume…’akasema kwa ujasiri.

‘Haya kama wewe ni mwanaume nijibu mwaswali yangu kama mwanaume kweli….’akasema huyo mwanadada.

‘Ni nani huyo mnayemuogopa, huyo anayekuja kuwatishia amani zenu hadi muishi kwa maisha ya mashaka….?’ Akaulizwa.

‘Mimi nilishawajibi hilo swali….mliponiuliza mwanzoni..’akasema.

‘Huko uliulizwa kwa ajili ya kutafuta maelezo yako, hapa unaulizwa kwa ajili ya hayo maelezo yako yaweze kuwa uahshidi ili hawo watu wakamatwe….’akasema mwakili mwanadada.

Yule mtu akainama na akawa kama anafikiria jambo, na wakili mwanadada akamsogelea na kumshiak shavuni kwa kidole,

‘Hivi wewe kweli unaweza kumtongoza mwanamke…..’swali hili liliwafanya watu humo ndani wacheke, na huyo jamaa akainua kichwa na kuangalia kwa uso wa hasira, na kusema;

‘Hapo sasa umevuka mpaka…’akasema.

‘Kama wewe ni mwanaume na unaweza kumtongoza mwanamke, ongea na mimi, je hunioni mimi ni mwanamke, mbona nakuwa kama nakutongoza wewe,….’akasema na mara wakili ambaye alikuwa akiwatetea hawo watu akasimama na kusema wakili anamlazimisha mteja wake kuongea kitu ambacho hakijui.

Wakili mwanadada akageuka na kuwaangalia watu waliohudhuria hapo, akapitisha macho sehemu yote ya ukumbi , halafua akgeuka kumwangalai huyo jamaa, ambaye alikuwa akimwangalia na pale wakili huyo aligeuka, akainama chini, na watu walipoona hilo tendo wakacheka.

‘Je tukimkamata huyo mtu, ambaye unamuogopa, huyo mwanaume, anayetishia wau wanaojiita wanaume, utasema kila kitu unachokijua juu yake?’ akaulizwa.

‘Kwanza ni kumkamata, pili ni kuhakikisha kweli mumeweza kummaliza nguvu zake, ambazo sizani kama mna ubavu wa kufanya hivyo..’akasema na wakili mwanadada akamsogelea mwenzake na kumnong’oneza kitu, na yule muendesha mashitaka akasema;

‘Muheshimiwa hakimu, kama ulivyoona, washitakiwa wote wamekuwa wakiogopa kusema ukweli kama walivyoweza kuelezea, wakati wanahojiwa walipokamatwa, inaonyesha kuwa  kuna mtu ambaye anaonekana ni tishia katika kijiji, mtu huyo amekuwa ni chanzo cha haya yote, …kwahiyo muheshimwa hakimu, tupo mbioni kumkamaat huyo mtu kutoana na kibali chako, ili ukweli utolewe hadaharini….’akasema huyo wakili.

‘Kama mna ushahidi wa kutosha kumkamata kwanini hamumkamati…kuna tatizo gani,?’ akauliza hakimu.

‘Kutokana na taarifa za polisi, huyo mtu , kila wanapofika kwake, anakuwa hayupo,na hata barua alizotumiwa zimekuwa hazimfikii…cha ajabu wanadai, aliweza kufika hadi hapa, na kujieleza, na kwa vile ni mtu wa serikali, aliweza kujizamini, na hatukuwa na shaka naye , tulijua kwua leo atakuweo kwenye mahakama hii tukufu, lakini kwa taarifa tulizozipata, ni kuwa kapata ajali,…..’akasema na watu wakaguna kuonyesha kuwa sio kweli.

‘Mimi siamini haya, ina maana nyie wote mnashindwa kumkamata mtu kama huyo, sasa natoa amri akamatwe haraka an kuwekwa rumande, ili  kesho afikishwe hapa mahakamani, ili kujibu shutuma juu yake. 

Hii ni amri ya mahakama, na nikazi yako muendesha mashitaka kuhakikisha kuwa washitakiwa wote wanafikishwa mbele ya mhakama, na sio kuwashika baaadhi ya watu, na mwisho wa siku kunaonekana kuwa huenda kuna njama za kuwasaidia wengine, na wengine wanateseka rumande….’akasema hakimu.

‘Muheshimiwa hakimu, tutafanya kila tuwezavyo, na kesho atakuwa mbele ya mahakama yako tukufu….’akasema wakili na kesi ikaahirishwa na wale washitakiwa wakarudishwa rumande.

*****

Usiku huo wake mbali mbali walikamatwa, akiwemo mke mkubwa wa mjumbe wa nyumba kumi na wake za wazee mashuhuri , na hili likajulikana ni kuwa walifanay hivyo ili waume zao wajitokeze, kwani kama walivyodai wananchi watu hawo wameshindikana, na eti kila wakifuatwa majumbani kwao wanatoweka kiajabu..

‘Nyie ndio mtasaidia waume zenu kupatikana, na wasipopatikana mtaozea jela….’wakaambiwa, na kweli kesho yake asubuhi na mapema, waume zao wake, wakajitokea, kasoro mjumbe wa nyumba kumi na wazee hawo wakasema;

‘Tupo tayari kujibu hizo shutuma, tunaomba wake zetu waachiliwe kwanza….’wakasema.

‘Hiyo sio kazi yenu …ilimradi mumefika hapa, basi mtashikiliwa kwa vile mumevunja amri ya mahakama ya kuwataka muwepo kila kesi ikitajwa….na yupo wapo mjumbe wenu?’ wakaulizwa.

‘Kwani hamkusikia kuwa kapatwa na ajali , kalazwa hospitalini, kama mnataka nendeni mkamuone wenyewe, sisi tumekuja kwa ajili ya wake zetu…’wakasema.

‘Hawo kutoka kwao ni mpaka tujirizishe na usalama wao na usalama wa watu wengine, msiwe na wasiwasi wapo chini ya usalama…nyie mtashikiliwa kwa mujibu wa sheria….na kama huyo mnayesema kapatwa na ajali, kama sio kweli, mtawajibika kwa hilo….’akasema na mara wakili mwanadada akafika.

‘Nimefika huko hospitalini, mbona huyo mtu wanayedai kapatwa na ajali, hayupo huko hospitalini….’akasema na askari wake wakaangalia kwa mashaka.

‘Lakini tulipofia usiku tulimuona…akiwa kalazwa…’akasema huyo askari

‘Una uhakika na hilo?’ akauliza wakili mwanadada akimkazia huyo askari macho…..

NB: Je kuna nini kinaendelea hapo, je kuwakamata hawo akina mama itasaidia, je hizi hisia za watu kuwa hawa watu wana nguvu za ziada za giza zina ukweli,…

WAZO LA LEO: Kumekuwa na hisia na imani za nguvu za giza , hali hii imekuwa ikiwatia hofu raia wengi, hasa akina mama. Imani hizi, zimefikia mbali zaidi ya kutumia viungo vya watu, eti vinasaidia kuleta uatajiri au kinga…huu ni unyama, huu ni uakatili, wa hali ya juu.


 Dawa kubwa ya kushinda haya ni kwanza kujua kuwa nguvu za giza hazina uwezo kwa mwanadamu, hazina msaada wowote kwa mwanadamu, utajiri, ulinzi vinatokana na wewe mwenyewe sio nguvu za giza, kama kweli wewe unamuamini mwenyezimungu, ambaye ndiye aliyekuumba, mtegemee yeye na jibididhse kwenye uzalishaji mali wa kihalali, pili ili nguvu za giza ili ziweze kufanya kazi yake ni mpaka wewe uingiwe na hofu…. Basi jenga ujasiri, usiogope, mwamini mungu na kwa njia hiyo utaweza kuzishinda kabisa nguvu zote za giza.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Unknown said...

Kweli kabisa we ushasikia Ni nguvu za giza hlf bdo unazifuata, wape somo ndugu yangu kanisani au msikitini ndio kuna nguvu bwana.