Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, July 5, 2013

WEMA HAUOZI-31


 Kwakweli mshituko uliotokea kwenye hiyo familia ulikuwa mkubwa sana, ulikuwa ni msiba mkubwa, na ulitokea pasi na matarajio, japokuwa msiba hauna hodi, Wake za marehemu na watoto walilia hadi kuzimia....…..

Msiba huo ulivuruga msimamo wa familia ukizingatia kuwa ndugu huyo ndiye aliyekuwa kichwa cha familia, na yeye aliweza kuiunganisha hiyo familia kuwa kitu kimoja na kuhakikisha kuwa mila na desturi zao zinafuatwa….japokuwa mara nnyingi alitumia ubabe, na wanasema kwa ubabe wake ndio maana alifanikiwa, kuwaunganisha wote….


 Pamoja na ubabe wake, watu wengi walimpenda sana, kwani wakati wa furaha alikuwa mtu wa furaha, na wakati wa kazi ilikuwa ni kazi..hakutaka mzaha, na ukiangalia ndivyo inavyotakiwa katika jamii zetu za sasa, uwe mtu wa kati na kati,…...

‘Hili limetokea, kama familia tunatakiwa tuwe kitu kimoja….’akasema mzee wao ambaye ndiye baba peke yake aliyekuwa kabakia kwenye hizo familia, na alitakiwa kushika hatamu kwa muda, hadi hapo watakapomkubali ndugu mwingine kushika uongozi wa familia.

‘Kinachohitajika kwasasa na muhimu sana, kama desturi za mila yetu, ni kumzika jamaa yetu haraka iwezekanavyo….’akasema mzee mmoja wao, katika ukoo lakini hakuwa mwanandugu wa moja kwa moja, na yeye kama mzee wa jamii, akatoa ushauri wake,na watu wakaitikia kwa kichwa.

‘Mimi siafiki hilo la kuzikwa kwa haraka….’akasema wakili mwanadada aliyekuwepo hapo kwenye msiba.

‘Kwanini unasema hivyo?’ akauliza huyo mzee na kwanini ukadakia kusema, wanawake, hawatakiwi kudakia dakia mmbo, kwanza tulia mtapata nafasi ….wewe kwanza ni nani kwenye hii familia?’ akahoji kuonyesha alikuwa ahmfahamu vyema.

‘Samahani mzee kwa kudakia, mimi ni mwanasheria, na itakuwa sio vyema, mimi nipo hapa, mambo yaende au tudai mambo kinyume na sheria, za nchi na taratibu zake, pia tutakuwa tunaficha ubaya kama umetendeka….kiutaratibu, kwanza inabidi tutambue ukweli wa kifo cha marehemu....’akasema na yule mzee akamwangalia yule mwanadada kwa macho makali.

‘Usituletee mambo yenu ya mjini, mtu keshakufa hata akikaa mwezi, utafufuka, au hata mkimchunguza ndio atazindukana, siku yake ilishafika na asingeliweza kuishi kama ahadi yake imeshafika…cha muhimu ni kumsitiri ..’akasema huyo mzee akiwaangalia watu.

‘Hilo sio tatizo mzee wetu, kuzikwa atazikwa, lakini cha muhimu ni kujirizisha je kweli amekufa au ameuwawa…maana huyu mtu hali yake ilikuwa njema kabisa,…akiwa pale hospitalini, hakuonyesha dalili za kuumwa, kilichomfanya akafikia hali ile ni kuwa aligoma kula, na walipomuwekea dripu a maji, hali yake ikwa njema, na akakubali kula….akawa hana tatizo tena , mara gahfla, tunasikia kafa, kwanini kitokee kifo cha ghafla hivyo, kwanini hamjiulizi hilo swali..?’ akauliza mwanadada.

‘Hiyo ni kweli, maana mimi mwenyewe niliongea naye, jana, na alionekana hana matatizo yoyote na akasema yupo tayari kusimama mahakamani kujitetea maana anaamini yeye hana hatia, na yupo tayari kuyafichua maovu yote…’nikasema nikichangia.

‘Na wewe ndio usiongee kabisa,  maana marehemu alikuwa akikulaumu sana…na haya yanayotokea kwasasa tutakulamu wewe…’akasema huyo mzee akininyoshea kidole kwa hasira.

‘Kunilaumu kwangu ni kawaida, maana tulikuwa tunasigishana kwenye mambo ya kawaida, na hilo ni la kawaida kwa wanadamu, lakini tukumbuke kuwa mimi sikuwa nafanya hayo kwa nia mbaya, nilifany ahayo kudai haki yangu , na ndio maana tulipofikia mahali hatuelewani, nikaamua kwenda mahakamani. Mbona mara ya mwishi nilipobahatika kuongea na marehemu, alinipoongeza kwa hilo na hata kunisfia kuwa nimekuwa jasiri, na nastahili kuwepo kwenye kundi lake la wanafamilia..’nikasema.

‘Usijitetee kabisa, na wala hufai kukaa kwenye familia hii, umekuwa gundu, …tena balaa mkubwa, hujioni, mumeo kafa, sasa huyu ndugu yetu ambaye alijaribu kukuweka sawa naye huyo kafa, hatujui ni nani atafuatia,…angalia msiba mingi inayotokea hapa, ukichunguza sana, unaambiwa imetokana na wewe na hawo unaoishi nao……angalia mwenyewe  tangu uingie kwenye familia hii ni matatizo, inakuwa kama wewe ndiye unaitafuna hii familia,..’akasema huyo mzee ambaye watu walimwangalia tu, maana wengi wao hawakuwepo hapo kiakili, msiba ulikuwa umewafika kiukweli.

‘Sio kweli…huyu mwanamama namsifia sana, yeye amekuja kuleta mageuzi makubwa kwenye hii familia, hata marehemu, alisema hivyo, ila yeye alikiri kuwa pamoja na hayo huwa hakubali kushindwa na mwanamke ndio maana alikuwa anajitutumua, ..japokuwa moyoni alishafikia sehemu akakubali yaishe, ila,…nahisi kuna shinikizo lilikuwa nyuma yake….’akasema mmoja wa wake zake.

‘Mimi sikubaliani na hilo kamwe,…ili hali iwe shwari kwenye hii familia, huyu mwanamke na watu wake waondoke,…yeye amekuwa kipingamizi hapa kwetu, ….hili kama wanafamilia, inabidi tuliseme na kulikemea, kama alivyokuwa marehemu, lisema kwenye kikao , tena mara nyingi,  yule ambaye hataweza kusimama na sisi sio mwenzetu…sasa inakuwaje tumkubali wakati marehemu alimkataa…’akasema huyo mzee.

‘Marehemu hakuwa amefikia hatua ya kumkataa…’akasema mkewe mwingine, lakini hakuweza kuongea zaidi akawa analia.

‘Huu sio muda wa kulumbana, tupo kwenye majonzi, kwanza tufikirie jinsi gani ya mazishi, mkumbuke huyu mtu ni mkubwa kwenye familia hii, kwahiyo watu watakuwa ni wengi sana…..kwahiyo gharama yake ni kubwa, siku hizi mfiwa badala ya kulia kufiwa, analia pia kuwa anahitajika kuwalisha waombolezaji,…analia na gharama,… sijui dunia hii ya sasa imekuwaje..zamani mtu akifiwa , kila anayekuja kwenye msiba anakuja na kitu, vyakula, nyama…kuni, maji….lakini sasa ni kufaa kufaana,…badala ya mfiwa kusaidiwa, anajikuta kwenye wakati mgumu, wa kufikiria jinsi gani ya kuwalisha watu watakaofika kwenye msiba…..’akalalamika huyo mzee.

‘Mzee usijali hilo tutajipanga vyema …ndio maisha yetu, hatuna jinsi, sisi kama wanandugu tutwajibika kukamuana, na kila takayekuja kwenye msiba, ni lazima atoe mchango, tutaweka vijana kila kona kukusanya michango, vinginevyo hatutaweza kuwalisha watu….’akasema mchangiaji.

‘Na lini tutamzika marehemu….?’ Akauliza mmoja wapo.

‘Kwa taarifa za polisi, wamesema kuna watu wamelalamika kuwa marehemu kapewa sumu..hakufa kifo cha kawaida, kwahiyo mpaka uchunguzi ufanyike….’akasema huyo mzee.

‘Ni nani huyo aliyelalamika, …..kwasababu wanandugu ni sisi, ni nani tumjue, ambaye kachukua jukumu bila ya sisi kujua,…., anataka mwili wa ndugu yetu uchezewe, tusikubali kabisa…’aaksema yule mzee wa mwanzo.

‘Hilo halina mjadala mzee, ilimradi limeshafika polisi, hakuna jinsi,…, ni kazi ya polisi na wameshamzuia, mpaka wamafanyie uchunguzi….’akasema huyo mzee.

‘Kwanini …kwanini,…mbona kila siku mnaleta mambo mapya,…na haya ndiyo yanaharibu baraka, kiujumla hilo halipo kwenye mila zetu,….tunaweza kugundua bila ya kumchana chana marehemu, tukalizuie, ndugu yetu hawezi kwenda kuchezewa chezewa na visu..’akasema huyo mzee.

‘Nimeshakuambia kuwa hilo halipo kwenye mamlaka yetu, ukumbuke kuwa huyo walikuwa naye, na wanawajibika kwa hilo, ..wao wameshindwa kumlinda…kwahiyo wanataka kujirizisha, na kama ikigundulikana kuwa kafa kwa sumu basi wao watawajibika iweje mtu aliyekuwa kwenye mikono yao, alishwe sumu, pia sisi kama wanafamilia tutamtafuta huyo mtu kwa njia zote, na atawajibika….akasema mzazi wa hiyo familia aliyebakia.

‘Oh, sasa hilo ni tatizo….mtazua mengine yasiyo na msingi….haya fanyeni mtakavyo, …..’akasema huyo mzee na akamgeukiwa mzee mwenzake waliyekuwa naye, wakawa wanaongea chini kwa chini kwa kunong’ona,.

‘Na kwanini wewe unapinga hayo, hayo ni kwa manufaa yetu, tujue ni nani alikuwa nyuma na hilo…’akasema ndugu mmoja wa marehemu.

‘Aaah, mimi sipingi kwa nia mbaya, ila naona kama sio halali ndugu yetu kuchanwa chanwa tena….mnatafuta nini keshakufa basi, …tumuombee huko aendapo, hakuna cha zaidi tutakachokipata….sasa kama hamnisikilizi mawazo yangu , naona niondoke, nitakuja baadaye’akasema huyo mzee, akamgeukia mwenzake, na wote wawili wakaondoka.

Wakili mwanadada akasogea pembeni na kupiga simu polisi, ….

**********

Tukiwa na wakili mwanadada kwenye msiba, tulianza kuongea maswala mbali mbali, na mara tukajikuta tukimuongelea mdogo wake marehemu, yaani mchumba wake mwanadada wakili. Mazungumzo haya yalianza tu pale mdogo mtu ambaye alikuwa hana nguvu kabisa alipofika kutusalimia na kutaka kujua kama kuna kitu chochote kinahitajika.

Kwa muda mfupi ndugu huyu alikuwa amekonda, , kiujumla msiba huo ulimchukua kupita kiasi, na kwa mtizamo wa hiyo familia yeye ndiye alitakiwa kuwa kiongozi wa hiyo familia japokuwa walikuwepo kaka zake wengine, ambao hawana uwezo wa nafasi hiyo, lakini kwa vile ni wakubwa wanaweza kuleta kipingamizi, na hiyo itamfanya huyo mwanasheria kuwa na wakati mgumu.

‘Yeye alipendekezwa na marehemu kuwa anastahili kuishika nafasi hiyo kama yeye akiondoka, na hata kipindi akiwa hai, pale panapotokea kikao na kama kaka yake hayupo, huyu ndiye aliywkuwa akikaimu nafasi yake.

‘Namuonea huruma sana mchumba wako, ataiweza kweli hii familia, maana ni kubwa na ina ubishi, na migawanyiko ya chini kwa chini, na ilivyo, ili uiweze hii familia inahitajia mtu mbabe, na huyu shemeji yako sio mbabe, anatumia busara tu…na elimu yake tu…?’ nikaanza kuongea na wakili mwanadada.

‘Sema aliyekuwaa mchumba wangu…’akasema wakili mwanadada akisisitizia hayo maneno `aliyekuwa mchumba wangu, na huku akimtizama huyo mchumba wake, ambaye alikuwa kakaa kwenye kiti, upande waliokuwepo wanaume huku kajiinamia.

‘Ina maana mlishafikia hatua ya kuvunja uchumba wenu?’ nikamuuliza.

‘Mhh, we acha tu,…ilibidi iwe hivyo, ili nimpe nafasi ya kuchagua…?’ akasema wakili mwanadada.

‘Nafsi ya kuchagua?...kuchagua nini tena?’ nikamuuliza na hapo akageuka na kuniangalia huku akijaribu kutabasamu.

‘Kati yangu mimi au wewe…’akasema huku akikaa vizuri, na baadaye akageuka kumwangalia huyo mchumba wake. K wa hali ile ilionyesha wazi anampenda sana mchumba wake, na alitamani aende akakae naye karibu ili aweze kumliwaza, …, lakini kulikuwa na msimamo fulani ambao alishauweka akilini mwake na hakutaka aonekane tofauti...

‘Huwezi ukasema hivyo, maana mimi sina ulazima kwake, na wala sina urafiki naye, wewe ni mchumba wake, na ulitakiwa usimame naye bega kwa bega, upiganie penzi lenu, na ukisema hivyo, kuwa ulimpa nafasi ya kuchagua mimi au wewe, unakosea kabisa…kwasababu mimi sijakubaliana naye kwa hilo…’nikasema.

‘Lakini mila na desturi zinamlazimisha afanye hivyo, marehemu ndugu yake yaani mume wako, walikubaliana hilo, na aliwahi kunielezea hata kabla mume wako hajafariki, na kipindi hicho nilichukulia kama mzaha tu, na nilimwambai kimzaha kuwa , nitafurahi sana nikiwa na mwenzangu kama mke mwenza…’akasema.

‘Ina maana upo tayari kuishi uke wenza?’ nikamuuliza kwa mshangao.

‘Tulikuwa tukiongea kama mzaha na sikujua kuwa inaweza ikatokea hivyo, imekuwa kama lisemwalo laja…mimi siogopi uke wenza, ….ila kwana kuwe na makubaliano ya dhati, na kama inabidi iwe hivyo, lakini kwa hali hii ya sasa, sioni kwamba kuna ulazima huo, pili kama uonavyo, yeye, hajawahi kuoa….’akatulia na kugeuka kuniangalia.

‘Ni kweli hata mimi hilo nimeliona….’nikasema kwa sauti ya unyonge.

‘Sasa atawezaje kuishi na wake, kama mke mmoja hajawahi kuishi naye, hawaoni kuwa wanamtwika mzigo mzito ambao hajawahi kuwa na uzoefu nao, ….na kwanini uke wenza?’ akawa kama anauliza.

‘Mimi sijui…’nikasema nikimwangalia huyo mchumba wake, na wakati huo alikuwa kainua kichwa na kutuangalia, sikujuwa alikuwa akiwaza nini, na akatoa leso yake kujifuta usoni, ….

‘Kuna sababu za kimsingi, kama zipo mimi sizipingi,…kuwa mjane alizoea kuishi na mume, na sasa mume wake keshafariki, na hana uwezo wa kuishi peke yake..tunaweza kusema hilo linaweza kuwepo, kama njia ya kumsaidia mjane…lakini sio lazima, ….cha muhimu kwanza ni kumpa muda huyo mjane, ajitambue, ajipime, na akubaliane na hiyo hali….sio kulazimishana…kama atapenda kurithiwa, basi ni hiayari yake….’akatulia.

‘Kumbe wewe unakubaliana na hizo mila za kurithiana?’ nikamuuliza.

‘Wanasema ukifika kwa wenye chongo, inakubidi ufumbe jicho lako…kiukweli moyoni, sikubaliani nalo, lakini ukitaka kuondoa ubinafsi, na kuweka upendo mbele kuwa mwenzako keshafiwa, na hana jinsi, atasaidiwaje kijamii, maana hakuna mtu atakaye weza kumsaidia mtu baki…wewe ukishafiwa na mumeo, kama huna wazazi, kama huna ndugu, hata kama wapo, utakuwa ni mzigo sana kwao,….kwahiyo tufanyeje,…tusaidiane, na atasaidiwa vipi kwa urahisi ….wao waliona hivyo kuwa arithiwe, sikati hilo, kwasababu huyo mjane akiwa na mtu akatambulikana kuwa huyu ni mumewe atasaidiwa bila masharti …ukiwaza sana hilo na kuondoa ubinafs, …inabidi ukubali…..’akasema.

‘Kwahiyo kwa hali kama yangu , mfano ningekubali kurithiwa, ulikuwa tayari kuishi na mchumba wako…yaani uolewe na mimi niwe mke mwenza wako…kwanza kipi kitangulie hata sijui?’ nikauliza na kuguna kama nacheka.

‘Hilo lipo wazi, hajaoa, kwahiyo kwanza kazi kubwa ni ilikuwa ni kwake, kutafuta mke anayemfaa aoe kwanza, ….mimi nilimsomesha hilo, kuwa hajawahi kuoa, haiwezekani akimbilie kurithi, hana uzoefu wowote na mke..tunamtendea isivyo haki, …ndio maana nikimwambia tuvunje uchumba wetu kwanza, ili apate muda wa kutafakari hilo, mimi au wewe, ….’akatulia.

‘Yeye alisemaje?’ nikamuuliza kutaka kujua zaidi.

‘Mhhh, aseme nini, na yeye huku anataka na kwako anataka….nilimuona hana maana, hana msimamo, na mimi tabia yangu ni kuwa sipendi kuburuzwa hasa pale ninapoona kuwa nipo kwenye msimamo sahihi….mimi sijamkatalia mila zao, na nilijitahidi sana kujifunza mila zao kwa vile nilikuwa nampenda…’akasema na kumwangalia mchumba wake, na niliposikia hilo neno `kumpenda’ nikajikuta nikihisi vibaya, sijui kwanini.

‘Kwahiyo kumbe kweli unampenda mchumba wako, na kilichotokea kinakuuma sana…na kwa namna moja au nyingine, unaniona mimi kama mpinzani?’ nikamuuliza.

‘Nikuambie ukweli..nasema hivi na tunaongea kwa vile sisi ni marafiki, …kiukweli nampenda sana, lakini mimi msimamo wangu ni kuwa sitapenda kama hakuna upendo, sitaolewa, kwasababu kuna kuolewa,sitayumbishwa kwa vile yeye ni mume, na anachotaka yeye ni lazima kiwe hata kama hakina maana, hata kama  sio sahihi kwa vile yeye ni mume, basi tukubali, tuje tuumie sote…nilishamwambia hivyo,na nilimuona akiwa hana raha na msimamo wangu huo…kazoea amri za kwao, kuwa mume akisema keshasema, sio kwangu, kama ni sahihi haina shida, na sitapinga tu ilimradi kupinga, nitapima yale anayoyataka, na tukae tukubaliena kama mke na mume..’akatulia.

‘Yeye kama wanaume wengine ambao msimamo wao ni kuwa mwanaume ni kila kitu, watu kama hawo ukiangalia kwa makini, hawajui kabisa, nini maana ya upendo, nini maana ya uchumba, nini maana ya ndoa…wanachojua wao, ni tafsiri ya mume kuwa mmiliki wa mke, na kama unamiliki kitu, ina maana hicho kitu hakina nafasi ya kujietetea…’akatulia kama vie anayapima hayo aliyoyaongea.

‘Kwangu mimi hilo halipo..na kiukweli  wanaume wa namna hiyo, wanakosea, mke ni binadamu , na anayo nafasi sawa na mume..wakioana, wanatakiwa kuwa kichwa kimoja…..wakae waongee wajadiliane wakubaliane, lakini sio kulazimishana kusiko na msingi…kila jambo wewe unatakiwa useme, sawa mume wangu, nikukate sikio sawa mume wangu…haiwezekani.’akatulia.

‘Ngoja nikuulize wewe na yeye mlianza anzaje, maana inavyoonekana kwa wengi, wanaona kama hamuendani kivile?’ nikamuuliza na yeye akacheka, halafu akashika shavu, na kuanza kuelezea, jinsi gani walivyokutana na  huyo mchumba wake..

‘Sikujua kabisa kuwa nitakuja kumpenda mchumba wangu kiasi hicho….lakini upendo ulitokea tu pale aliponiokoa nikiwa kwenye kundi la midume miwili iliyotaka unibaka…..’akaanza kuelezea kisa chake na mchumba wake….

NB: Sehemu ijayo, tutagusia kidogo, jinsi mwanadada huyo alivyotokea kupendana na mchumba wake, je ilikuwa ni bahati mbaya, au kweli kuna upendo ndani yake, na je hawa wanawake wawili, watakuabalina kuishi uke wenza, ….

Je na wewe unasemaje. Najua ndugu yangu utasema `chesive, harikaa, ni kini icho…’ lkn zipo mila na desturi,….wanafanya hivyo, na wanaishi,….je zimefanikiwa,… je wewe unasemaje, …

WAZO LA LEO:Maisha yana mambo mengi, na hutaweza kuyafahamu yote, cha muhimu, unapokutana na mwenzako, hasa wale wanaojikuta kuwa na wapenzi, na huenda kukutana huko ni kwa mjini mjini,  hatujuani, wewe hujui kabisa mila na desuri zao, na pia huenda mila na desturi zenu zikawa tofauti kabisa.

Ni vyema, ukafanya utafiti, ukamjua mwenzako kabla hujachukua maamuzi ya kuishi naye kama mke na mume. Watumieni wazazi wenu au watu wazima kuzijua taratibu, mila na desturi za mwenza wako, japokuwa mke na mume, ni familia ambayo sio lazima iwe tegemezi na mila za wazazi wao…, nyie ndio mtapanga jinsi gani ya kuishi lakini hamuwezi mkajitenga kabisa na familia za wazazi wenu, au sio…


Ni mimi: emu-three

9 comments :

Unknown said...

ukewenza mwanzo ni mzuri bt mkizoeana sidhani km mtakuwa na maelewano tena ila na wanaume nao wanachngia wake zao kuishi kwa ubaya kwa kupenda sehemu moja, kwa upande wangu binafsi siupendi ukewenza.

Rachel Siwa said...

Hongera sana ndugu wa mimi kwa kazi nzuri...Mungu azidi kukubariki kila iitwapo leo..kuna mafunzo meengi sana kupitia kazi/maandiko yako.

Naungana nawe kabisa na Wazo la leo.

Pamoja daima.

Unknown said...

Tha we eho he mtwi wngu, asikubali ukewenza kabisa bora akae na msimamo wake huo huo tang lini mapenzi yakagawanyika❓tuthiishane aha.

Unknown said...

Tha we eho he mtwi wngu, asikubali ukewenza kabisa bora akae na msimamo wake huo huo tang lini mapenzi yakagawanyika❓tuthiishane aha.

Unknown said...

Nyaaa,

Anonymous said...

shamballa beads wholesale uk
workforce . Most of these beloved a that your particular pleasantly surprised about apparent products are virtually assortment of are really a number of replications . in the with these types of number of rooting just after

WordPress can be a very well-liked CMS with in depth usages to get a array of web-sites and strong online applications. Being an open source CMS, it has gradually been becoming the choice of additional customers and webmasters about the globe. At present, webmasters and users favor WordPress conversion solutions to obtain a well-designed and totally functional web-site. The WordPress theme conversion just isn't a simple activity and calls for massive technical knowledge and sound domain skills. In the absence of those two important things, the conversion will not be a trusted, economical and helpful proposition. It has been offering top-class WordPress conversion solutions to let users meet their varied requirements. With WordPress already capturing markets and generating inroads into others' share, this organization is steadily increasing to deliver the most beneficial of WordPress conversion services to clients. Getting a strong and straightforward CMS implies it becomes rather quick process to handle web-sites and taking the most effective out of it.
The majority of us are familiar with the physical benefits of massage therapy. And, all of us know expertise first hand throughout our every day interactions, the unavoidable stresses of life. The majority of customers that seek out massage therapy typically do so to help alleviate the physical manifestation of their accumulated anxiety. And, it really is definitely properly warranted sought right after, as constant massage therapy aids to lessen your overall degree of physical discomfort, stiffness discomfort. In addition, it assists to raise the array of motion with the key joints inside your physique. Educated, intuitive skilled hands perform out the accumulated knots, tensions muscular adhesions that create more than time.
I'm also treated to views in the comfort of my garden space: a peep over the dividing wall reveals acres in the aforementioned rice fields. I have a private outdoor fish pond with stepping stones for the front door from the villa, and an open-air bathroom containing a bathtub shrouded within a mosquito net.
David Yurman replica jewelry is an excellent way for people with tight budgets to practical experience the luxury and design and style for which David Yurman is recognized. You'll find high-quality replicas in the marketplace which are just as lovely as the originals. Nobody would ever know it was not a genuine David Yurman piece.
il drago non è altro che Envy. Nel frattempo, un'altra associazione sta tramando nell'ombra: la Thule Society, capeggiata da Karl Haushofer. Questa associazione è alla ricerca della chiave di

Related information:
[url=http://crystalbeadsr7t9.unblog.fr ]crystal beads bulk
[/url]
[url=http://cheapshamballabeads.webs.com ]cheap shamballa beads
[/url]

Anonymous said...

Kaka m3, nakuonea huruma sana kwa juhudi yako hii , japokuwa kwa kweli tunafaidika, tunga vitabu jasho lako lisiende bure. Pia naona ajabu matangazo ya biashara yanawekwa kwenye blog zisizo na tija, na blog kama hizi hawaweki ni kwanini... Mungu atakujali tu ka kazi ya mikono yako

Anonymous said...

This will create a smooth, professional refinish on the bathtub.

What are the benefits of having a bathtub refinishing. Usually, the bathtub refinishing
kit that you purchased will have several chemicals that you will need to
effectively resurface your bathroom tub.

Also visit my web page: bathroom remodeling

Anonymous said...

Take your time and effort so that you'll be able to be assured that you have found the most effective automotive tools and equipment on your current needs. Bath tub liners come inside a variety of colors and resist chipping and scratches. If you intend on using a granite countertop installed, first choose the right.

Here is my webpage; bathtub resurfacing