Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, July 9, 2013

KARIBU MGENI WETU MTUKUFU RAMADHANI


Ni mwaka jana tu tulikuwa na mgeni wetu huyu tunayetarajia kumpokea hivi karibuni, mwenyezimungu akitujalia. Na tulikaa naye masiku yasiyozidi siku thelathini,na baadaye akaondoka., na huenda wengi wetu mgeni wetu huyo alifika na akatuacha kama alivyotukuta. Tulisahau kuwa mgeni huyu kwetu ni neema, isyoyofanana na  kitu chochote na akija akaondoka bila ya wewe kutakasika basi tena, wewe upo hasarani

Mungu akipenda tutakuwa naye tena, na ni wakati wako huu wa kujirudi usifanye makosa kama ya mwaka jana, kwani  bahati wakati mwingine haiji mara mbili,…Mgeni wetu huyo akija, tunahitajika tufanye mambo muhimu yafuatayo;,

Kwanza ni, kuwa wapole, kupendana, kusaidiana, ikiwa na maana ya kurehemeana,

Pili tukiwa naye tunahitajika kutubu madhambi yetu kwa, kumuomba mola atusamehe yale mabaya , na maovu tuliyoyatenda, maana mwaka mzima kama binadamu tumekuwa ndani ya dimbwi la maasi, yapo matendo tuliyotenda kwa viungo vyetu, kwa dhahiri au kwa bahati mbaya , yawe ya kutenda, yawe ya kuona au kusikia, yote haya mgeni wetu atatusaidia tuyafute kwa sharti kuwa tuwe wakweli na tutubu ukweli wa kutubia.

Na ukishamaliza kutubia  unasamehewa na kuwa huru, mbali kabisa na madhambi, unakuwa msafi kama siku ile ya kuzaliwa,…unataka nini tena we mwanadamu,, baada ya hapo mgeni wetu huyo ataondoka,  akijua kuwa amekusaidia kuwa huru, kuwa mbali kabisa na madhambi ambayo yangekutia kwenye moto wa jahanamu.

Je wewe huoni umuhimu wa mgeni huyu, ..ni nini unahitajia katika dunia hii, . …angalia wangapi ulikuwa nao na sasa hawapo, kweli walipenda kuondoka, …na wao walikuwa wamekusduia kuwa mwezi huu ukifika watafunga, lakini mola keshawachukua. Basi kwa vile wewe umejaliwa kukutana na mgeni huyu tena, na umeshajua ni nini anahitajia,, kwanza jiandae kumpokea vyema…na kwa vile umeshajua kuwa mgeni wetu huyu ni mtakatifu, basi, na wewe jiandae kitakatifu kwa kuwa msafi wa mwili na roho.

Tuacheni dhana potofu za vunja jungu hizo dhana za kupandikizwa ili mvunje imani yenu, na mjikute mpo wachafu mkutane na mgeni wetu huyo tukiwa wachafu.,…je kweli unaweza kwenda kumpokea mgeni wako ukia mchafu,..haiwezekani.

Kwahiyo tujitahidi sana, tusiige tabia za ibilisi na shetani aliyelaaniwa. Kwani ukifanya hivyo, ukajiunga na hawo wanaovunja jungu, basi ni kama vile unamuaga shetani ….kuwa ooh, rafiki yangu unaondoka tutakutana mwezi ukiisha...

Cha muhimu ni kujikurubisha kwa mola wako, kwa kuanza kuandaa sehemu zako za ibada, ambapo utaweza kumkaribisha mgeni huyu,anza kwa kutubu dhambi zako kwa kuwaomba msamaha wale wote uliowakosea, wakumbuke mayatima, wakumbuke wagonjwa, wasiojiweza, wadaiwa, wanaohitajia ada za shule, ukumbuke kutoa sadaka, kuwaaombea waliotangulia, na kila mara mdomo wako uwe ukimtaja muumba wako.


Karibu mgeni wetu mtukufu Ramadhani.

Blog yenu ya Diary yangu inawatakia kila la heri, na funga njema yenye mazingatio kwenye mwenzi mtukufu wa Ramadhani.

NB: Nilikuwa nimefiwa na ndugu yangu, mungu amlaze mahali pema peponi, ndio maana sehemu inayofuata ya kisa chetu cha WEMA HAUOZI, haikuweza kuwepo hewani, tunajaribu kuiweka hewani, ...soooon


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Tupo pamoja m3

Yasinta Ngonyani said...

Kila la kheri kwa kipindi hiki cha ramadhani. Na polwesana kwa msiba.

Anonymous said...

POLESANA KWA MSIBA NA ASANTE KWA KUTUPA NASAHA NZURI ZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI NADHANI KILA ATAKAYESOMA HAPA ATAPATA CHA KUFANYA