Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, June 19, 2013

WEMA HAUOZI-22


Siku ya kesi ikafika, watu wakajaa mahakamani, utafikiri kulikuwa na ushindani wa namna fulani, hata ilibidi walinzi wafanye kazi ya ziada kuweza kuwadhibiti watu waliotoka kusikiliza hiyo kesi,

‘Ni kwanini watu wamekuwa wengi kiasi hiki?’ akauliza mwandishi mmoja wa habari.

‘Ni kwa vile kesi hii ina utata, na watu wamejikuta kwenye ushabiki wa pande mbili, wengine wakisema wapo upande wa mwanamke, kwa vile kuna haki za kutetea haki za mwanamke wanaozulumiwa haki zao, utakuta kundi wengi wao ni wanawake, na wengine wanadai ni ujanja wa mwanamke, kutaka kupata mali ya mwanaume kwa vile tu ameishi naye, …’akasema huyo mtu.

‘Kwani wewe unasemaje kuna ukweli wowote kati ya hayo mawili na upo upande gani?’ akauliza mwandishi wa habari

‘Katika dunia ya leo lolote linawezekana, siku hizi watu hawajali kuzusha uwongo na kudai mali isiyo halali hili lipo na linawezekana, sitaona ajabu kwa huyo mwanamke kufanya hivyo, lakini pia kuna hai ya wanandugu kuja kudai mali ya ndugu yao, wakati hata hawajui hiyo mali ilichumwaje, na wakishapata wanawasahau hata hao mayatima na mjane…., yaani watoto, wanatelekezwa kabisa..kwahiyo ukinuliza mimi nipo uapnde gani, siwezi kukuambia…’akasema mmoja wa watu waliohudhuria kwenye hiyo kesi.

‘Kwahiyo wewe kwa uoni wako, unafikiri hili linawezekana likapata ufumbuzi mbele ya mahakama?’ akauliza mwandishi.

‘Tatizo kubwa ni mambo ya kisheria, maana mnapoishi ndani , kati ya mke na mume, huwa hatujali mambo tunayoona ni madogo mdogo, kama kwenye hii kesi, kunahitajika stakabadhi za malipo, fikiria malipo ya wakati gani….ukiangalia makaratasi kama hayo wengine tunafungia maandazi au kuchana chana baada ya tendo likishapita, je inawezekana kweli huyu mwanamke akapata hizo stakabadhi zinazohitajika, na kama asipopata hizo stakabadhi ndio basi tena na huenda ilikuwa haki yake kweli , je atafanyaje….’akasema  mama mmoja aliyehojiwa.

********

Sisi tulifika mahakamani mapema, na kukaa sehemu zetu, na baadaye akafika wakili wetu ambaye lwa muda huo alitokea  Dar, siku hiyo hakulala nyumbani kwetu kama alivyokuwa alitarajia mwanzoni, kwani alisema kuna mambo alihitajika kuyafuatilia, na pia kazini alikuwa na kesi aliyokuwa akiisimamia.

Alipofika akatusalimia, akatabasamu, lakini lilikuwa lile tabasamu la kujilazimisha, usoni alionyesha huzuni fulani, moyoni niliwaza kuwa huenda ni kwasababu ya hii kesi yangu, au vinginevyo inawezekana ni kutokana na kutokuelewana kati yake na mchumba wake. Nikamwangalia nikitaka kumuuliza kuwa hana hakuata tatizo lolote, lakini kama vile alifahamu, na huenda hakutaka kuulizwa maswali binafsi akasema;

‘Msiwe na wasiwasi…hii kesi tutashinda tu, cha muhimu ni sote tuwe na lengo moja, na kujitahidi kufuata yale yote niliyowaelekeza, na nimejaribu kuwahusisha watu wa haki za binadamu, wataalamu wa dini, ili tuone watatusaidia vipi kuhusiana na hili swala, na utakuta wote walikuwa wakisisitiza ushahidi wamesema hawapendi kuingilia mambo ya kimahakama, na ili kuhalalisha madai yetu ni vyema tukajitahidi kupata ushahidi wa kuonyesha wazi kuwa ulilipwa hizo pesa, wao kama watalaamu wa Nyanja zao, hawataweza kusaidia zaidi…’akasema.

‘Kwahiyo kitu kikubwa kwa sasa,….ambacho ndio kinatubana kisheria,… ni jinsi gani ya kupata huo ushahidi, na kwa vile ni muhimu sana kwetu,  imebidi nilifuatiliea huko kwenye ofisi ulipolipiwa hizo pesa,japokuwa niliwahi kwenda na mchumba wangu kabla, na kipindi kile hatukuweza kupata ushahidi wowote, lakini safari hii niliamua kwenda kivingine, kama mpelelezi, nikijua sasa hilo ni jukumu langu… na huko nimelipua bomu, maana wao kama kampuni wamegundua mengi yaliyokuwa yakitendeka nyuma ya pazia,japokuwa mengine hayahusiani na kesi yetu…..’akatulia.

‘Kuna uchafu ulikuwa unachezwa huko na watu wachache bila kampuni kufahamu, na kwa vile watu hawo wachche wenye tamaa ya utajiri wa dhuluma waishajiamini, nina uhakika ndivyo walivyofanya kwenye malipo yako…..hwakujua kuwa za mwizi ni arobaini….’akatulia na kufungua ukurasa wa akiwa kama anasoma.

‘Wao kama kampuni walipogundua hilo wameamua kufanya uchunguzi wao wa ndani kwa ndani japokuwa walisema kwa sasa wale wote waliokuwa wakiharibu kampuni wameshaondolewa, ndivyo walivyoniahidi hivyo, lakini sikurizika nao, ndio nikaingia hadi ofisi za watu wanaoshughulika na mambo kama hayo ya ukaguzi wa mahesbabu, watu wa kodi, ili wafike na kuchunguza mambo ya kimahesabu,..

Wao wakakubli kunipa ushirikiano, kwani hata wao walikuwa na mpango huo wa kufanya ukaguzi wa mahesabu ya mambo yao ya kodi,moja baada ya jingine, baadhi ya mambo yakaanza kujitokeza, baadhi ya siri zikaanza kuvuja japokuwa…’akatulia kidogo huku akifungua makabrasha yake, na akawa anasoma jambo kwenye moja ya karatasi alizochapisha, …..halafu akasema;

‘Pamoja na juhudi zote hizo, bado kama sisi, hatujaupata ule ushahidi wenyewe tunaoutaka, lakini kwa hatua tuliyofikia inatoa matumaini…na tunaweza kumshawishi hakimu kuwa kuna jambo lilifanyika.’akasema.

‘Tunashukuru sana sijui tutakulipa nini…’nikasema.

‘Usijali,….hapa ni kufa na kupona, kwasasa hatutakiwi kufikiria maswala ya malipo, lakini kwa vile kwa namna moja au nyingine, kuna gharama tunazipata, kama usafiri, nauli ,uchapishaji na kupoteza muda wetu wa kazi, na nyie mnakuwa hamuwezi kujumuika kwenye kuzalisha, ….hii yote ni gharama, na mwisho wa siku gharama hizo zitahitajika kurejeshwa…..kesi kama hii mwisho wa siku, washitakiwa wakishindwa itawabidi walipe gharama zote….hilo nitahakikisha kuwa linafanyika…’akasema na kuanza kupekua makabrasha yake, huku akiangalia saa yake ya mkononi.

***********

Baadaye wakaanza kuingia washitakiwa, wakiwa wameongozana familia nzima, na walipoingia wakainua juu mkoba wao wakishiria ndio wenye vielelezo vyote vya kuonyesha kuwa hawakufanya hivyo kwa kubahatisha, na kama ilivyokuwa kwenye kesi ya kwanza,waliongozana na kundi kubwa la familia, wakiwa na sare zinazofanana. Katika kundi hilo, kulionekana utofauti kidogo na mwanzo, kwani kaka mkuu wa familia hiyo hakuweo.

Walipofika sehemu yao na kukaa, wakiwa wanamsubiri hakimu kuingia, mwanasheria wao, akawa anamtupia jicho la siri mchumba wake ambaye sasa anaonekana kama amewasaliti. Lakini mwanadada huyo alikuwa kama hajui kuwa watu hawo wapo, kwani alikuwa kainama akisoma makabrasha yake,  na wale wanafamilia wengine wanaotafuta chokochoko, hawakuweza kuficha chuki zao usoni, kwani kila mara walipokuwa wakigeuka upande wetu, walionekana wakikunja uso kwa hasira, na wengine wakionyesha ishara ya kuwa tutafungwa, au tutachinjwa, kwa kupitisha kidole shingoni, lakini hakuna aliyewajali.

Wakili, mwanadada alikuwa kainama akiendelea kusoma makabrasha yake hakutaka hata kutizama upande wa wahasimu wake hawo, na mara chache, alikuwa akiinua uso kuangalia upande ule anapotokea hakimu, na mara nyingi alikuwa akimtizama mteja wake na kutabasamu kunipa moyo.

‘Msijali tutakachofanya leo ni kuvuta muda, na baadaye nitaomba muda wa kuweza  kuleta ushahidi muhimu,maana nina imani polisi na hawo wakaguzi wa mahesabau  watakuwa wamegundua jambo…haiwezekani pesa ulipwe wewe na jina liandikwe mtu mwingine,….’akatulia akisoma jambo kwenye makabrasha yake.

‘Na cha ajabu huyo mtu aliyeandikwa kuwa ndiye aliyelipwa hajulikani wapi alipo….na kuna kitu kingine ambacho ndicho kilinifanya niwatafute hawo wakaguzi wa mahesabu, kwanini namba ya stakabadhi ya malipo,…katika mpangilia namba za risiti za malipo kwenye hilo faili lao, ambayo inaonyesha kuwa ndiyo iliyolipiwa hiyo pesa ni tofauti na namba nyingine…..haipo kwenye mtiririko wa namba ….’akasema wakili mwanadada.

Alitulia na kutuangalia kwa muda, kama vile anahitaji tuongee, na mimi nikaona nifungue mdomo na kusema;

‘Mimi nahisi kuna jambo….maana waliponilipa, nakumbuka kabisa walinitaka nisaini, halafu wakanipa kopi yangu, wakaniambia niende kwa karani mtoa pesa…na huko napo nikasainishwa….sasa sijui, na sijui kwanini siku ile sikuweza kusoma kila kitu….’nikasema nikionyesha huzuni usoni, na baba akasema;

‘Sisi tunakusikiza wewe wakili wetu, kama kweli umeamua kutusaidia, mungu akuongoze, na uipate haki kwa ajili ya mwanamke mwenzako…. Kama unavyoona mara nyingi tukishapata jambo, hatuna haja na kutunza stakabadhi za malipo,…na hata wengi hatusomi kabisa nini kilichoandikwa, .’akasema baba.

‘Haki itapatikana tu,…..ni kweli huo ni udhaifu wa wengi, maana unapolipwa pesa kuna stakabadhi ya malipo, mara nyingi hizi zinakuwa ni kitabu, na zenyewe zina namba zinazofuatana, moja , mbili tatu na kuendelea kwa mpangilia maalumu, sasa haiwezekani namba zifuatane, halafu ikifikia hiyo namba ya malipo yaliyofanyika …..iwe tofauti,…mia sita na mbili,…. halafu ikitoka hiyo namba, inaendelea katika ule mtiririko wa mwanzo, na kuendelea kwenye mfuatano wa kawaida…’akasema huku akijikuna kichwa kwa kidole.

‘Hapa wamebugi,..hapo kama walipanga hupo mpango, walijisahau….na ndipo unapoona kuwa njia za mhalifu ni fupi….wao walijua wakiharibu ile stakabadhi halali ya malipo, na kuweka nyingine watakuwa wameharibu ushahidi….’akasema na kuangalia saa yake. Halafu akageuza kichwa kuangalia watu waliohudhuria , lakini hakutaka kabisa kugeuza kichwa kuangalia upande ule wa washitakiwa, akasema;

‘Nashangaa kwanini hakimu kachelewa kuingia..’akasema na kabla hajamaliza, mara akaja mtu na kusema mawakili wa pande zote mbili wanahitajika ndani, kuongea na hakimu.

‘Nilijua tu kuna jambo….’akasema huyo mwanadada na kuinuka na makabrsha yake kuelekea ndani na huku nyuma yake akimfuta yule mwanasheria wa familia ya washitakiwa ambaye alishatambulishwa kama wakili wa hiyo familia, japokuwa walisema kuwa kwa vile yeye ni mmoja wa washitakiwa, basi watamtafuta wakili wao mwingine, lakini hadi muda huo huyo walikili wao mwingine alikuwa hajafika.

*********

‘Nimewaita hapa kuhusu jambo moja muhimu sana, kuna kesi imetufikia ambayo inahitajika kusikilizwa leo, kesi hiyo itawagusa wahusika wa kesi yenu, na kwasababu hiyo tunahitajika kusikiliza kesi yenu kwa haraka, …..kwahiyo lengo la kuwaita hapa ni kuwekana sawa…japokuwa kesi inayokuja ni ya kutambulishwa na baadaye itahitajika kwenda kusikilizwa mahakama za juu,  kwani inavyoonekana kuna makosa ya jinai na mauji ndani ya hiyo kesi…’akasema hakimu.

‘Eti nini..na mauji..?’ akashangaa yule mwanasheria wa familia.

‘Ndio ….lakini kwasasa ninachotaka kuongea ni kuhusu hii kesi yenu kuna mawili, kwanza kuna wazo lililetwa mwanzoni kuwa hii kesi ingeliwezekana kusikilizwa kindugu na kumalizika,…hili sijui mnalionaje, kama mumekubaliana itaweza kusaidia sana, ili tupate kuimaliza kesi yenu , ili tuendelee na kesi hiyo nyingine….’akasema hakimu.

‘Muheshimiwa hakimu, hayo unayoelezea ni kweli sisi washitakiwa tulikuwa tayari kwa hilo, kuwa tukutane na wenzetu, ili ikiwezekana mambo haya tukayamaliza kinyumbani, …..kutokana na wao kukosa ushahidi …..na kama unavyoona kuna kesi hiyo nyingine ambayo inahusu wahusika wakuu wa kesi hii….ambayo sijui kama wenzetu wapo nyuma yake au….?’akawa kama anauliza huyo mwanasheria wa familia.

‘Kama nilivyokuambia hayo yametoka kwa upande wa vyombo vya usalama, kama unakumbuka kwenye eneo lenu kume kuwa na mauji ya mara kwa mara yenye utata, ..polisi walikuwa bado wanafuatilia , na uchunguzi wa polisi umegundua mengi, na kwahiyo kwa vile mahakama yetu ni mahakama ya mwanzo na kesi hiyo inahusu  makosa ya jinai na mauaji,….kwetu tutaitambulisha tu na kuipeleka mbele...'akasema hakimu huku akiangalia saa yake.

'Kwahiyo ndio maana ninahitajia kama hamjakuabaliana basi tuanze kesi yenu hiyo kwa haraka, vinginevyo tuiahirishe, …lakini kama mpo tayari,…tutaendelea, ili haki ipatikane na kama hampo tayari basi tunaweza kuihairisha hadi tarehe tutakayopanga baadaye…’akasema hakimu.

‘Sisi kwa upande wetu tupo tayari kulimaliza hilo tatizo kifamilia, sijui kwa hawa wenzetu ambao ndio walioshitakia, na sioni kwanini wasikubaliane na hili, wakati hali halisi inajionyesha, na hawana ushahidi wowote….’akasema mwanasheria wa familia.

‘Tuna mambo ya msingi tunayodai, na sisi tulileta kesi hii mbele yako muheshimiwa hakimu, kwa kuogopa  kuwa hili tatizo likisimamiwa na wanafamilia halitaleta ufumbuzi wa haki, ..ila kama watakubaliana na madai yetu ya msingi hapa mbele yako muheshimwia hakimu, sisi hatutakuwa na kipingamizi…’akasema wakili mwanadada.

‘Madai yenu ya msingi kama yapi?’ akauliza mwanasheria wa familia. Na wakili mwanadada akamwangalia hakimu kama anaweza kuingilia kati hilo swali. Hakimu akasema;

‘Madai yatu ya msingi ni kama yalivyoanishwa kwenye kesi yatu, na yalishasomwa mahakamani…..’akasema wakili mwanadada na hakimu akaingilia kati na kusema;

‘Kutokana na mashitaka yaliyoletwa mbele yangu ni kuwa nyie mlioshitakiwa mumemiliki nyumba na duka isivyo halali, na kwahiyo wao wanataka hati ya nyumba na duka kubatilishwa na kumilikishwa kwa mjane kwani  vyote hivyo alijenga kwa pesa yake mwenyewe, ….’akasema hakimu na kumwangalia wakili mwanadada, ili kama ana nyongeza, na kabla wakili mwanadada hajasema kitu, mwanasheria wa familia akasema;.

‘Muheshimiwa hakimu, madai hayo sio sahihi….hilo la kuwa alijenga kwa pesa yake, sio sahihi, ….kwasababu tulizitaja, hata kama alijenga yeye, lakini alijenga kutokana na pesa za mumewe, kwani kipindi hicho mumewe alikuwa jela…..hata hivyo muheshimiwa hakimu,…sisi tupo tayari kukubaliana kuwa nyumba na duka viwe vya familia yaani mjane na mtoto wawe wakivitumia, lakini hati miliki,  bado iendelee kuwa mikononi mwa wanandugu hadi hapo mtoto atakapokuwa mkubwa, na tutaibadilisha na kumwandikisha huyo mtoto, hilo halina kipingamizi….’akasema mwanasheria wa familia.

‘Muheshimiwa hakimu, kutokana na maelezo ya mwenzetu huyu, kama alivyoelezea hapo, inaonekana moja kwa moja kuwa hatutaweza kukubaliana kwa hilo kama litapelekwa kusikilizwa kifamilia, ndio maana tulilileta mbee yako, …kwahiyo sisi tunaoshitakia, tunaomba kesi yetu iendelee, ama ianze leo, au kama ulivyosema kuwa kuna kesi nyingine, basi tunaweza kuiarisha kwa leo, hadi hapo itaposikilizwa tena,…..’akasema wakili mwanadada.

Hakimu akamgeukiwa mwanasheria wa familia , na kumwangalia kusikiliza atasema nini, na mwanasheria wa familia akasema;

‘Muheshimiwa hakimu, hawa wanataka kupoteza muda bure, hawana ushahidi wowote wa madai yao, inavyoonekana  ni ujanja wa kutaka kumiliki mali isivyo halali,…na kutumia siasa za hadaa, kwani sasa hivi wamakwenda hadi kwa watu wa haki za binadamu, ina maana hawaamini mahakama yako…?' akawa kama anauliza halafu akaendelea kuongea;

'Wamekwenda hadi kutafuta makundi ya kutetea haki za akina mama, wakati kesi ipo mahakamani, huku ni kuzarau mahakama yako….kw ujumla muheshimiwa hakimu, sisi hatukumdhulumu mtu, tumefanya kutokana na utaratibu wa kimila, kisheria…na kutokana na maandishi ya marehemu mwenyewe aliyotuachia….na kama tutafanya kinyume na hivyo alivyotaka marehemu, haitakuwa haki,....hebu jamani wenzangu fikirieni mara mbili, wewe ulikuwa hai ukataka mali zako zimilikiwe hivi na vile, sasa umefariki, waliobakia nyuma wanafanya kinyume chake, hii tutakuwa tunamtendea marehemu isivyo halali….'akasema huku akionyesha huzuni, halafu akamgeukia mchumba wake na kusema;

'Na huyu ambaye sasa anasema ni wakili wao, anatafuta mwanya wa kujijengea umaarufu tu, hakuna kitu kingine hapo muheshimiwa hakimu, ni kujitafutia njia ya kujionyesha kwa watu kuwa anaweza kazi, kwa njia hiyo hutafanikiwa kamwe, kama ni kweli onyesheni huo ushahidi, ushahidi upo wapi…?’akasema mwanasheria wa familia.

‘Hizo ni hoja zako, ….huo ushahidi utapatika mbele ya mahakama, ninakuhakikishia muheshimwa hakimu, hilo kuwa sisi tuna ushahidi wa kutosha, na kwanini nitafute umaarufu kwa kudai haki za wanyonge, hiyo ni zarau muheshimiwa hakimu, sikutegemea kuwa mwenzangu aliyesomea sheria angelizungumza maneno kama hayo…’akasema wakili mwanadada.

Hakimu alitulia kwa muda, baadaye akasema ,’Inavyoonekana hakutakuwa na ufumbuzi wa hili tatizo kama litarudishwa huko kwenye familia, kama ombi lenu la awali lilivyoletwa mbele yangu, na kwahiyo basi kesi yenu itabidi iahirishwe hadi hapo itakapotajwa tena,….na nawaomba sikuhiyo muwe mumekamilika na ushahidi na mashahidi ….sitavumilia tena malumbano ya kibinfasi, yasiyo na ushahidi, nyote mnafahamu vyema sheria …’akasema na mlango ukafunguliwa ili wanasheria hao watoke.

Mwanasheria wa familia alipotoka nje, akamshika wakili mwanadada mkono kumsogeza pembeni kaba hawajaingia kwenye ukumbi wa mahakama, ambapo kulikuwa na tangazo la kuahirishwa kwa hiyo kesi na kutajwa kesi nyingine itakayosikilizwa.

‘Nyie mumefanya nini….?’ Akauliza kwa hasira huyo mwanasheria wa familia.

‘Kuhusu nini?’ akauliza wakili mwanadada akiutoa mkono wake kutoka kwa huyo mwanasheria wa familia.

‘Hii kesi mpya ambayo inamshitakia kaka yangu kuwa eti anahusika na kundi la mauaji hapo kijijini na nyie mlioipeleka polisi,…nina uhakika kuwa nyie ndio wahusika na lengo lenu ni kuipaka familia yangu matope, ionekane kuwa haitendi haki au sio….?’ akauliza.

‘Hiyo sihusiki nayo….kesi yangu ni hii iliyotakiwa kuwepo leo, hayo mengine, kama alivyosema muheshimiwa hakimu ni mambo ya usalama….kama kulikuwa na mauji,…kama kulikuwa na makosa, ni lazima wahusika wafikishwe mbele ya sheria…hilo sio ajabu, ….kuna kosa gani hapo?’ akauliza kwa mshangao.

‘Ninakuonya ….tena unisikie sana, usije ukafikiria kwa vile tuna mahusiano mimi na wewe ukafikiria nitashindwa kuitetea familia yangu, ….mapenzi hayawezi kamwe, kuweza kunifanya nigeuke nyuma na kuiacha familia yangu…..kama unahusika na hilo, tutafikishana kubaya…hili nakupa kama onyo, kama unataka kujionyesha wewe ni bora wa sheria, haya, tutaona mwisho wake utafika wapi…’akasema kwa hasira.

‘Tusitishane kwa lolote lile, …hiyo ndio kazi yetu, kwani tulisomea nini….wewe unachotakiwa kuangalia ni haki na sheria sio kutetea ndugu hata kama ni wahalifu. Na usipoangalia vyema, sizani kama kazi hiyo ya uwakili utaiweza…kwa mtindo huo, hii kazi hutaweza…ngalia ukweli, usizibe masikio kwa vile na familia yako,….nakushauri hivyo, kwa vile tumetoka mbali mimi na wewe…..’akasema wakili mwanadada.

‘Tutaona nini…nasema hivi mimi na wewe sasa hatujuani, tutajuana kwenye ulingo wa mahakama,…si ndio unataka iwe hivyo..tutaona….’akasema huku akiondoka kwa hasira.

‘Tutaona nini…hatutakiwi tuone, tunatakiwa sheria isimamiwe itakiwavyo, sio swala la kutishana na swala la haki na sheria,….unakaribishwa sana muheshimiwa, tutajuana huko huko mbele ya hakimu…’akasema wakili mwanadada, akiwafuata watu wake. Lakini machoni, kulishaanza kujenga ukungu wa machozi.

NB: Ukweli unauma, lakini mapenzi nayo mmmh….


WAZO LA LEO: Tusikubali kabisa katika maisha yetu tukatawaliwa na jaziba, mara nyingi jaziba, zinatusukuma kwenye kutenda ubaya zaidi ya ubaya uliotangulia, na kinachofuatia hapo kulipiza kisasi. Linapotokea tatizo, tuangalie sheria inasemaje, na ni vyema, ukapata ushauri kwa watu wenye busara kabla hujachukua maamuzi mengine, kwani huenda ikatoea sisi wenyewe ndio wakosaji, lakini kwa vile imetugusa wenyewe, na kwa vile hatuwezi kumudu hasira zetu, matokea yake ni jaziba. Na haki itendwe na kutolewa kwa usawa bila kubagua.

Ni mimi: emu-three

8 comments :

Unknown said...

Da imefika pazuri Sana dada upo juu. Na lazima hali itendeke hapo

Anonymous said...

Hello. And Bye.

Unknown said...

Pole na majukum dada vp mwendelezo lni❓ mn nahic kudata nkiikosa

Unknown said...

Pole na majukum dada vp mwendelezo lni❓ mn nahic kudata nkiikosa

Unknown said...

Pole na majukum dada vp mwendelezo lni❓ mn nahic kudata nkiikosa

Unknown said...

Pole na majukum dada vp mwendelezo lni❓ mn nahic kudata nkiikosa

Unknown said...

Pole na majukum dada vp mwendelezo lni❓ mn nahic kudata nkiikosa

Unknown said...

Pole na majukum dada vp mwendelezo lni❓ mn nahic kudata nkiikosa