Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, June 7, 2013

TUMEPATA JIRANI MPYA


                                   http://www.swahiliabroad.blogspot.com/

Tumetumwa tukaambiwa tuje, toane tuongezeke, na tukiongezeka, ina maana tunakuwa na familia, na fmilia ya huyu na yule zikiungana tunapata jamii. Jamii ili ziweze kuishi vyema ni lazima kuwa na ujirani mwema. Nashukuru kwenye hii tasinia ya mitandao ya kijamii, tuna wanajamii wengi, majirani, na leo tuna bahati ya kupata jirani mpya, mwenzetu mpendwa, kwa jina anaitwa Justin Kasyome, na ukitaka kumjua zaidi tembelea blog yake anayojulikana kama;

 http://www.swahiliabroad.blogspot.com/

Tunaomba mumpokee kwa mikono miwili, kwani pamoja na mengine mengi anakuja pia kwa kuitangaza nchi yetu, ...kwenye utamaduni wetu, kwenye lugha yetu ya Taifa, kama blog yake inavyojielezea, wewe kama jirani mwema, husika kumtambulisha mwenztu huyu kwa wanajamii sote kwenye blog yako

 Kwangu mimi na Diary yangu tunasema tupo pamoja.

Ni mimi: emu-three

3 comments :

EDNA said...

Karibu sana jirani mpya

Inspiration stories said...

asante dada Edna ila nawe naomba unitambulish ekwako kama hautajali!

Yasinta Ngonyani said...

Twamkaribisha kwa mikono yopte miwili...KARIBU SANA.