Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, May 23, 2013

WEMA HAUOZI-11




Mama akawa anaendelea kunisimulia kuhusu maisha yake kuthibitisha yale aliyonismulia babu, na safari hii alionekana akiongea kwa hisia iliyojaa huzuni, ….na hata machozi yakaonekana kumlenga lenga,machoni….

Hali ya mume wangu ilikuwa mbaya sana, ilifikia hatua tukasema sasa ndio safari imefika, tukabakia kusikilizia, maana kutokana na kuumwa ugonjwa wa kifua kikuu, na kwa ubishi wake,akawa bado anakunywa, na kwasabbu ni mzaifi, pombe kidogo, inamlewesha sana na mabaya zaidi akawa hataki kula,…’hapo mama akatulia kidogo, halafu akasema;

‘Sasa ndio likazuka hilo la kapigwa, siamini kuwa walipigana, hakuwa na nguvu za kupigana, nay eye anajua hilo, labda kuongea, oooh, mume wangu mbishi, sasa sijui labda walibishana na huyo mwenzake ndio walifikia hatua hiyo, au labda huyo jamaa alipotoka kwangu, akaona hasira akazimalizie kwa mume wangu…sijui, na sikutaka kuulizia, kwani hatukuwa na muda huo tena

‘Ila kwa ujuma kipigo alichopigwa sio kipigo cha kitoto, maana hata pale aliposafishwa uso, …uso wote ulikuwa umevimba hata macho yalikuwa hayaonekani….uso umehumuka….alibadilika kabisa….

‘Huu ni unyama…..’akawa anasikitika yule dakitari aliyekuwa akimsafisha huyo mgonjwa, na hakuvumilia, akamuita muuguzi mwenzake, ambaye alikwenda kumuita polisi, na polisi alipomuona huyo mgonjwa,….

‘Huyu mtu ni mwizi…?’ akauliza

‘Hapana tulikuta akipigwa na mwenzake…’tukasema

‘Ulevini sio..?’ akauliza

‘Hawakuwa ulevini, tuliwakuta njiani, na inavyoonyesha walikutana, kwani huyo mwenzake alikuwa kwangu, na alipotoka akakutana na huyu mgonjwa,….ni mgonjwa, kama unavyomuona, hakukuwa hata na sababu ya kugombana na yeye…’nikasema.

‘Haiwezekani, lazima kuna sababu, …..na ni bora huyo jamaa tumkamte, na ataeleza vizuri….’akasema huyo askari, na kweli, hawakupoteza ,muda, waliondoka kwa haraka kwenda kumkamata huyo jamaa aliyempiga mume wangu, lakini walipofika waliambiwa mtu mwenyewe yupo taabani, hajiwezi na yeye, amekuwa kama kachanganyikwa, na muda huo alikuwa kafungwa kamba.

‘Kuna tatizo gani kwenye hiki kijiji ….?’ akauliza huyo askari polisi akimgeukia kiongozi wa serikali mwenye dhamana hapo kijijini.

‘Tatizo ni hawa watu wachache wanaojichukulia sheria mikononi mwao, tunajaribu sana kuwaelimisha lakini inakuwa vigumu kwao kutuelewa,…nafikiri imefikia hatua sasa sheria ichukue mkondo wake, maana hata sisi viongozi tunakuwa katika wakati mgumu, na hata kutishiwa maisha yetu, ….watu wengine hasira zao ni mbaya sana…’akasema huyo mheshimiwa.

‘Kwanini hamtoi taarifa, mnasubiri hadi hali iwe mbaya kiasi hiki, …..taarifa nyingi za vifo visivyojulikana zimefika ofisini, na ukichunguza, hakuna ushahidi, hakuna maelezo mazuri ya kutusaidia, sasa mnafikiri sisi tutawasaidiaje…mkilinda uhalifu, mjue ni kama mtu anamlinda nyoka mwenye sumu ndani ya nyumba yake, ipo siku itamuuma….’akasema huyo askari

‘Tumeshaleta taarifa hiyo kwa maandishi, na jibu tulilopata ni kuwa mtalifanyia kazi, sasa sisi mlitaka tufanye nini zaidi…’akalalamika huyo mkuu.

‘Tunahitaji maelezo ya kina, nyie hamsemi, ni nini chanzo, ni nani anahusika, mnafichana, mnaogopana, kama mkiogopana, eti kwa vile mtu fulani ni mchawi, basi…tutashindwa kufanya kazi yetu….’akasema huyo askari.

‘Tumekuelewa afande,….’akasema huyo muheshimiwa akionekana kuchoka.

‘Sasa sisi tutaanza kamata kamata, hasa kwa hawa watu wenye sifa ya hasira,. ….si wana hasira sio, basi kuna kazi ya kuondoa hasira zao, ….kama watu kama hawo wana hasira, sisi tutazimaliza,….kwanini wasitumie hasira zao kwenye kulima, au kuvunja mawe, wanazitumia kuharibu sura za watu….?’ Akawa kama anauliza huku akiwageukia watu waliokusanyika hapo.

‘ Mimi huyo mtu kama ningemkuta mzima, angejuta, maana hizo hasira zake zingeliishia pabaya….ole wake, na ole wanu,  mtu mwingine atakayejifanya ana hasira…basi atakuwa ndiye mfano, sasa na sisi tutazionyesha hasira za dola, na huyo mtu apelekwe hospitaki, atakuwa chini ya ulinzi mkali akipona ana kesi ya kujibu….’akasema huyo askari, na kuwaangalia watu waliokuwepo hapa, na baadaye akasema;

‘Mbona mnatupa shida sana hiki kijiji , mnataka tuwaonyeshe kazi yetu sio,…haya mtaiona, kuanzia sasa mtaiona kazi yetu..’akasema huyo askari, na kuondoka, na haikupita mtu, kundi la maaskari likaja na kuanza kuwazoa watu, kila aliyekutwa mitaani bila kazi akabebwa kwenye gari lao,….

******

Siku ya pili nilikwenda kumtembelea mume wangu, na nilimkuta akiwa bado kalala, uso kidogo ulikuwa unatazamika, uvimbe ulishaanza kupungua… nikamuamusha ili apate kunywa kifungua kinywa, lakini alikataa kabisa kunywa uji, alisema mdomo umevimba, na una madonda, hawezi kula. Nilikwenda kuongea na docta kungalia jinsi gani tutamsaidia, docta akasema;

‘Huyo kaumizwa sana mdomoni, …..mpe uji kidogokidogo,…baadaye tutamuwekea maji yenye lishe, ……lakini kwa sasa jaribuni kumnywesha huo uji kidogo kidogo…’akasema.

Tulifanya hivyo, lakini ilikuwa ni kazi ya kulishana kama mtoto mdogo, hakutaka kula kabisa, na muda wote alikuwa akilalamika maumivu, maana hata mbavu zilikuwa zimejeruhiwa, kifua ndio usiombe, alikuwa akikohoa utafikiri ni gari linapandisha mlima.

Kwa ujumla baba yako alikuwa katika hali ya kusikitisha sana,….kipindi hicho wewe ulikuwa mdogo,…na likuwa akikupenda sana. Na jinsi nilivyomuona mume wangu akiteseka vile, hata mimi hasira zilinipanda, na moyoni, nilikuwa sina amani tena na huyo mtu aliyempiga mume wangu. Nilitamani kama ningelikuwa mwanaume, niende nikapigane naye, hadi hasira zangu zishuke…

‘Mume wangu, jitahidi kula, maana usipokula dawa hazitaweza kufanya kazi….’nikawa namwambia lakini ilikuwa ni vigumu kwake, …..ilifikia hatua, ndugu zake walikuwa wanakuja, kuanza kumkaripia, lakini hawakujua kuwa yey hapendi iwe hivyo…ina maana hamu ya kula ilikuwa haipo tena.

‘Ni heri kufa kuliko haya mateso ninayoyapata…..kila sehemu inauma, ….mdomoni kuna vidonda, ….huyu mtu alikuwa akinipiga ngumi za mdomoni, sijui mdomo wangu ulimkosea nini…’akawa anaongea na sauti yake ilikuwa ikitoka kama mtu aliyezibwa mdomo.

‘Kama ningelikuwa na afya yangu, …asingeliweza kabisa kufanya hivi…..ningepambana naye kiume, lakini alijua kuwa sitaweza kujitetea, basi akanifanya gunia ….ole wake nipone….’akawa anasema huku machozi yanamtoka.

Wiki ilipita, na baadaye hospitakini, walimruhusu wakisema kwa sasa kinachohitajika ni dawa, kula na kufuata masharti, haina haja ya yeye kuendelea kulazwa hapo hospitaini, akaendelee kutibiwa nyumbani. Na mmoja wa madakitari akashauri kuwa pia tunaweza kutumia tiba mbadala.

‘Siku hizi kuna dawa nzuri tu, ila muwe makini, sio dawa zote zinasaidia, na pia hakikisheni kuwa dawa hizi anazotakiwa kutumia,…za kifua kikuu, haachi hata mara moja….’akasema.

Sisi kwa uoni wetu mfupi, tuliona ni dalili ya kuwa hatapona tena. Tukamchukua hadi nyumbani, na ikawa kazi ya kumtibia kwa hizo dawa za kifua kikuu na dawa za tiba mbadala, kuna muda dawa hizo zilisaidia, lakini huyu mume wangu pale akipata nafuu kidogo anachojua yeye ni pombe. Akawa aanvunja masharti moja baada ya jingine.

Akaanza kuchoka , na hali yake ikazidi kuzorota, na alipozidiwa kipindi hiki, hali yake ikawa mbaya zaidi ya hata ile ya mwanzo, akawa ni mtu wa kitandani , kila kitu kinafanyikiwa kitandani, alibakia mifupa mitupu …ndugu na jamaa zake waliokuwa wakifika fika wakawa hawafiki tena, nikabakia mimi na yeye.

Babu yako ndiye aliyekuwa mtafutaji,…..mimi biashara zikasimama, na hali ilivyozidi kuwa mbaya, tukaanza kutumia mtaji, hali ikaanza kuwa mbaya zaidi, hata nyumba ya babu yako ambayo ilikuwa kukaribia kuisha ikabidi isimame, sikuwa na kitu tena, pesa yote ikaniishia vikabakia vitu vichache dukani. Na siku moja wakatuingilia wezi kwenye duka langu, wakakomba kila kitu,…tukabakia mkono mtupu, …

‘Hili sasa ni janga……’nikasema.

‘Hapa kuna kitu, nahisi kuna jambo linakwenda kinyume, …..’akasema babu yako. Babu yako sio mtu wa kukata tamaa mapema, na akisema jambo ujue kweli limemfika, na mara nyingi akisema jambo, ujue kuna ukweli ndani yake.

‘Baba unafikiri tumefanya nini kibaya hadi tukutwe na majanga yote haya?’ nikamuuliza.

‘Nahisi mume wako kuna makosa aliyafanya, ….nilijaribu kumdadisi sana, nimegundua kuwa kuna dhuluma aliifanya, na alipata muda wa kutubu, lakini hakufanya hivyo, alitakiwa  kwenda kwa huyo aliyemfanyia hivyo, angalau akamuombe msamaha, lakini hakufanya hivyo, na sasa…nahisi, keshachelewa…’akasema .

‘Baba una maana gani kusema keshachelewa….kwani sisi hatuwezi kufanya kwa niaba yake?’ nikamuuliza.

‘Hali yake ilivyo, inaashiria hivyo…hizi ndoto zangu sio za kawaida, naona nisafiri kidogo, nikirejea tutajua ni nini la kufanya, ….toba ni yeye mwenyewe mkosaji na mkosewaji,….nikirudi tutaliangalia hilo, kuna dawa zinahitajka, za tiba mbadala kwa matatizo kama hayo, unakumbuka zilivyomsaidia mwanzoni, ..zile hazipatikani hapa, na mpaka huko milimani…kwa wenzetu wacha mungu…’akasema na kweli kesho yake akazifuatilia.

Siku alipoondoka, mume wangu akawa kama kapata nafuu, nakumbuka usiku huo tuliongea naye sana, kiasi kwamba nilijua kuwa keshaanza kupona, akawa ananisimulia enzi nzetu za ujana, tulipoanzia urafiki wetu, akasimulia maisha baada ya mimi kupata ujauzito wako…yaani tuliongea saana,hadi raha, na moyoni nikawa anmuomba mungu hiyo hali iendelee kuwa hivyo, kwani ni dalili njema.. ..

‘Mke wangu, nataka kesho ukamtafute yule mtu wa ardhi, yule aliyetusaidia hadi tukaweza kuandikisha hati ya nyumba,….’akasema

‘Kwanini unasema hivyo?’ nikamuuliza kwa mshangao.

‘Unajua mke wangu nimekumbuka jambo…ile hati niliandika jina langu, na kipindi kile nilifanya kwa hasira, sasa nimegundua kuwa nilifanya makosa. Sikustahili kabisa kuandikisha jina langu, maana hii nyumba ni yako, ulijenga kabisa kwa pesa zako….sasa iweje, niandike jina langu….’akasema.

‘Lakini wewe ni mume wangu, na wewe na mimi ni kitu kimoja, ndio maana nikakubali tukafanya hivyo , mimi sioni ubaya…’nikasema.

‘Hapana kwa hali kama hii….inahitajika tubadi hiyo hatii haraka, ….nahisi nimetenda ubaya, ..je huoni kuwa nikifa watu wakiona hiyo hati, watakusumbua, …nawafahamu sana ndugu zangu, naomba kesho fanya hima tubadili hiyo hati ya nyumba..’akaniambia.

‘Mume wangu hilo lisikutie shaka, hakuna mbaya atakayekuwa na moyo sugu wa kufanya hivyo, wote wanafahamu kuwa nyumba hii ni yetu, japokuwa nimejenga mimi,….lakini mimi na wewe ni kitu kimoja. Hakuna asiyejua hilo, ndugu zako wote wanafahamu hivyo,..na kwanini ufikirie kufa, wakati hali yako inaonyesha kutengamaa….?’ Nikamuuliza.

‘Kufa hakuna hodi…..lakini dalili hazijifichi..mimi nikifa hakuna shaka, kila dalili ipo, na kwanini niendelee kuishi, na kukutesa mkewe, angalia unavyoteseka, nakuonea huruma sana mke wangu, angalia ndugu, jamaa wote wametukimbia, na hali inazidi kuwa mbaya, umaasikini umetuingia , magonjwa ndio haya, sio kwamba napenda kukutesa hivi…sipendi kabisa mke wangu…najuta sana kwani ukiangalia nahisi haya yote yanatokana na mimi…’akasema.

‘Kwanini unasema hivyo?’ nikamuuliza.

‘Mke wangu sikupenda kabisa kukusimulia maisha yangu ya gizani, …sipendi lakini wakati mwingine nahisi unastahili kuyafahamu….’akasema.

‘Mume wangu achana na hayo…wewe tulia, tuliza moyo wangu, tuganga haya yaliyopo, hali yako haitaki magumu, unatakiwa utuize kichwa…’ nikamwambia, lakini ilionekana kuwa alikuwa na dhamira yake, akasema;

‘Mke wangu nimepitia maisha mabaya,…kipindi kile ulipoonadoka, nilijiingiza kwenye kundi haramu, …na humo kwa tamaa ya kutafuta utajiri nilijikuta nikifanya mambo mabaya sana, yote ikiwa kutafuta mali,….na moyoni nilifanya hivi kwa ….. ili tukikutana niwe mtu miongoni mwa watu. Mawazoni nilijua utakuwa umekutana na tajiri, sasa roho ikawa inaniuma, kuwa huenda umenikimbia kwa sababu hiyo, sikuwa na mawazo kuwa umenikimbia kwa kitendo nilichokufanyia ….sasa sikutaka nishindwe kukupata,kwahiyo nikaanza kutafuta utajiri kwa nguvu….’akasema.

‘Lakini hayo yamepita mume wangu, sasa hivi umebadilika,yaache kama yalivyo …na ukipona unaweza kwenda kutubu dhambi zako kwa hawo uliowafanyia ubaya, kama unawafahamu…lakini hata hivyo hakuna ambaye atakuwa na kinyongo na wewe kwa hali uliyokuwa nayo….umeshateseka vya kutosha…’nikamwambia.

‘Mhh, utatubuje dhambi za kuua…’akasema

‘Ina maana uliwahi kuua?’ nikamuuliza.

‘Mke wangu, nakuambia nilijiunga na kundi haramu, kundi la ujambazi, na kuna wakati tulikuwa tunakwenda kupora kwenye maduka tukiwa na silaha, sijui wenzangu walizipatia wapi, na wao ndio walionifundisha kutumia silaha,….kwa vile niliona raha kuikamata, basi walipokuwa wakiamrisha ua….nafyatua, mke wangu nimeua,na kila nikiwaza hilo, ndio maana naishia kulewa ..’ akatulia kwa muda, halafu akasema;

‘Sijui kwanini nilibadiliak kiasi kile, lakini nilikuwa sipendi, kufanya hivyo, wenzangu walikuwa wakinisukuma nifanye hivyo, na kwa vile nilikuwa nikitafuta pesa, nikajikuta nimeingia bilA kupenda kwenye makundi haramu,….’akasema.

‘Oh, ….hayo yamepita mume wangu, kama ulifanya hivyo, na umekiri makosa yako, mungu atakusamehe, iliyobakia sasa ni wewe upone, na ukipona kama nilivyokuambia utakwenda kuwaomba msamaha, hawo uliowakosea…’nikamwambia.

Mke wangu,…sizani kama nitapata muda huo..naomba iwe hivyo, na kweli nikipona, itakuwa kiguu na njia kwa kile niliyemfanyia huo ubaya,…..nikipona, nitakuwa mtu mwema sana,..nitaacha pombe, nitaacha sigara, nitakuwa mcha mungu,….nikipona mke wangu,…sitarudia tena, nakupenda sana mke wangu, …’akasema na usingizi ukawa unatunyemelea, na kabla hajalala, akasema.

‘Ukumbuke mke wangu kufuatilia kubadilisha hati ya nyumba, ni muhimu sana….’akasema na usingizi ukampitia.

**********

Nilipoamuka babu yako alikuwa amerudi na dawa na alikuwa kakaa nje, na kuzianza kuzitengeneza, na mimi, nikadamka kwenda kumuona huyo aliyetusaidia kubadili hati ya nyumba, ….maana kulikuwa na mwendo kidogo wa kutembea. Niliamua kufanya hivyo, kwani mume wangu aking’ang’ania kitu, hatatulia mpaka ukitekeleze. Basi nikafanya hivyo, kwani hata babu yako alikubalina na hilo kabla ya kuondoka nilimwangalia mume wangu ambaye likuwa bado amelala, na alifunua macho kidogo, akataabsamu akasema,

Hapo mama akatulia, …na machozi yakaanza kumtoka, nilitamani nimwambie mama asiendelee kama kuongea huko kunamzidishia uchungu, lakini sikuweza kumnyamazisha , nilitaka nijue yote, na alipotulia kwa muda, akasema;

‘Hilo ndilo tabasamu la mwisho la baba yako…lipo akilini mwangu wakati wote….’akasema na kuinama, baadaye akainua kichwa na kuendelea kuongea akasema;
Mume wangu alipotabasamu hivyo, akasema; ‘Nenda mke wangu, ni muhimu sana, nakupenda sana mke wangu, ..’akafumba macho, na mimi nikajua kuwa amelala.

‘Baba nitarudi mapema tu, kama nikichelewa, naomba umnyweshe huo uji upo tayari kwenye chupa,…’nikamwambia babu yako.

‘Usiwe an shaka, kwanza hiyo dawa yenyewe inahitajika kuweka kwenye uji,…kwahiyo hilo niachie mimi, huyu ni mtu wangu tunajuana, nikimnywesha mimi atakunywa, siunona wewe mwenyewe……’akasema babu yako, na ni kweli ukitaka baba yako anywe uji au ale chakula, uhakikishe babu yako yupo.

‘Mimi nitaiweka hii dawa kwenye uji kabla ya kumnywesha,….hii dawa akiinywa tu, kesho utaniambia,..atakuwa mzima kabisa, cha muhimu asirudie tena pombe..’akasema na mimi nikaondoka.

 Nilifika kwenye ofisi za wilaya, na kuingia ofisi za ardhi na majengo, lakini huyo mtu anayehusika na kubadili hati, alikuwa kasafiri, ila walianiambia kuwa akirudi watamtuma afike kwangu kwa haraka, ila walinishauri kuwa inahitajika pia huyo mume wangu andike barua ya kuomba hayo mabadiliko, ikiwa na sahihi yake, halafu baadaye kuna fomu za kujaza. Basi nikaondoka nikiwa sina mashaka,….sikuwa nimelitilia maanani sana, kwahiyo nikarejea nyumbani.

Nilipokaribia nyumbani kwangu, nikahisi mwili ukinisisimuka, ….nilihisi hali isiyo ya kawaida ikinijia mwilini, nilihisi wasiwasi ..nikajipa moyo kuwa hakuna kitu kibaya kitatokea….nikafika kwangu na nikamkuta babu yako akiwa kakaa kati kati ya mlango panga likiwa mkononi.

‘Baba vipi mgonjwa anaendelea vipi?’ nikamuuliza huku nikitaka kumpita niingie ndani na nilihisi kama anataka kunizuia, lakini baadaye akasogea pembeni na kusema;.

‘Mwanangu…karibu ukae kwanza, maana hiyo dawa,….kama angeliwahi kuinywa, tungelizungumza mengine, lakini hakuwahi kuinywa,….’akasema na moyo wangu ukalipuka , nikahisi kizungu zungu, sikusubiri kusikiliza zaidi , nikampita baba kwa haraka na kuingia ndani.

Niliingia ndani alipokuwa kalala mgonjwa, nikakuta kitanda kipo kitupu….nikashikwa na bumbuwazi, maana mgonjwa alikuwa akihudumiwa kila kitu kitandani, nakujiuliza ina maana mgonjwa keshapona, …sikuamini, nikarudi hadi pale alipokuwa kakaa babu yako, nikamkuta kasimama kashika mashavu kwa viganja vyote viwili, huku kainama chini.

‘Baba mgonjwa yupo wapi, mbona hayupo ndani?’ nikauliza.

‘Kachukuliwa na ndugu zake, ….ndugu zake wamekuja hapa na vurugu nyingi, kulikuwa na mapigano hapa, ….wao wamesema wanamuhitajia ndugu yao , kwani wanataka wakamtibie wenyewe, wanadai wamegundua dawa ya kumtibia, na kuendelea kukaa hapa hatapona. Wanadai kuwa wewe ndiye kikwazo cha ndugu yao kupona, ….’akasema kwa hasira.

‘Wana maana gani hawa watu, siku zote nahangaika peke yangu na mgonjwa, hakuna hata mmoja aliyekuja kunisaidia…tunahangaika mimi na wewe baba yangu. Hebu fikiria wewe baba hujatuzaa, lakini umekuwa na uchungu zaidi ya ndugu wa kuzaliwa tumbo moja,….hebu fikiria baba hata kutoa dawa hata siku moja hawajawahi kufanya hivyo…sasa sijui leo wameona nini hadi kufikia hatua ya kuja kumchukua, hawa watu wana lao jambo …!’ nikasema kwa hasira.

‘Unajua nilipambana nao, lakini baadaye nikaona kwanini niwazuie…..huenda kweli wana dawa nzuri, zitamsaidia mgonjwa, basi nikawaacha wakambeba wakaondoka naye, na nilifanya hivyo kwasababu mume wako, baadaye alipenda iwe hivyo, nafikiri baada ya kuona vurugu imezidi,…kwakweli mue wako mwenyewe aliweza kuongea na mimi, akanisihi sana niwaachie wamchukue, na hata dawa nilikuwa sijampa, ndio nilikuwa karibu kumlisha , wkaingia….oh na ili kuondokana na vurugu hiyo, mume wako akasema ngoja wanachukue,….’akasema babu

Basi nilivyosikia hivyo sikuweza kutulia tena, moyo uliniua sana, …na kwa vile nawajua sana hawa watu, nilijua kabisa akifika huko hatapata huduma yoyote….wana lao jambo,….mimi sikukubali, nikamwambia babu yako ni lazima nifike huko kwa mume wangu, maana mimi ndiye ninayejua anatakiwa ale nini, na wao wanaweza wakamtelekeza…..babu akasema ni sawa, lakini ni lazima tuongozane naye, maana hawaamini sana hawo watu wanaweza wakanidhuru,…’akasema mama akiwa kashika shavu.

‘Basi tukaondoka na babu yako, akiwa na panga lake mkononi,tukaongozana naye, na tulipofika huko, hatukupewa nafasi ya kumuona, walikataa kata kata, wakisema kuna miiko ya hiyo dawa anayotumia, hatakiwi kuonana na mtu yoyote zaidi ya yeye na huyo mganga wake.

Basi tulikaa pale tukisubiria kama tutaruhusiwa kumuona, lakini walikataa kata kata, na hata ilipofika jioni, tukarudi nyumbani.

‘Baba hii sio haki, kwanini wananifanyaia hivi hawa watu, hawajui kuwa yule ni mume wangu na nina haki ya kuonana nay eye…..?’ nikamuuliza babu yako.

‘Mwanangu vuta subira, usilazimishe jambo, ….kila jambo huja kwa maana maalumu, hawa kuna kitu wanakitafuta kutoka kwa mume wako, na wanajua akiwepo na wewe hawatakipata….’akasema babu yako.

‘Kitu gani hicho…?’ nikauliza.

‘Kwakeli sijui, sisi tuvute subira, na tuombee kuwa wamemchukua kwa wema, najuta kuwa sikuwahi kumpa ile dawa, na kama angekunywa angalau kidogo, angelipata nafuu, sasa sijui huko watampa dawa gani….’akasema babu.

Tukafika nyumbani, na nilipofika nikahisii mabadiliko mle ndani, vitu vilivurugwa, na sijui hawa watu walikuwa wakitafuta nini…na nikaanza kuvipanga, taratibu ili huenda nikagundua kuna kitu gani kinakosekana, na wakati nahangaika kupanda vitu, ghafla mlango ukagongwa,..

‘Ni nani mwenzangu..?’nikauliza kwani babu yako aliaga kwenda kwenye eneo lake, kuangalia ujenzi, japokuwa umesimama.

Na mara yule mtu akaingia na babu yako alikuwa nyuma yake, na nilivyowaangalia machoni nikagundua kuwa kuna taarifa mbaya. Miguu ikaanza kutetemeka, mwili ukaisha nguvu kabisa.

WAZO LA LEO
: Mkishaona mjue nyie ni kitu kimoja, onyeshaneni upendo zaidi pale mnapokuwa kwenye shida,…hasa kipindi  mkiwa katika hali ngumu. Onyashaneni upendo pale mmoja anapokuwa anaumwa, ujue wewe ndiwe upande wa pili wa mwili wa mwenzako, usiondoke karibu yake, kwani ukiondoka karibu yake, upande uliobaki ni mbovu hautaweza kuhimili kusimama peke yake. Kumbuka rafiki wa kweli ni yule anayekufaa wakati wa dhiki.

Ni mimi: emu-three

9 comments :

Anonymous said...

Howdy I am so excited I found your blog, I really found
you by mistake, while I was researching on Yahoo for something else, Regardless I am
here now and would just like to say thanks for a tremendous post and
a all round entertaining blog (I also love the theme/design), I don't have time to browse it all at the moment but I have saved it and also added your RSS feeds, so when I have time I will be back to read a great deal more, Please do keep up the excellent work.

Take a look at my blog ... http://www.babesflick.com/category/273/lesbian-porn/

Anonymous said...

kusema ukweli kaka unajua kutoa mafundisho kwa njia ya hadithi. ubarikiwe sana.

Anonymous said...

It's hard to come by experienced people in this particular subject, however, you sound like you know what you're talking about!
Thanks

Here is my homepage; http://www.cfnmfever.net/

Rachel Siwa said...

duhhh ndugu wa mimi..Aminia sana..kuanzia kisa mpaka Wazo la Leo..unawazisha kwa sauti sana..MUNGU azidi kukubariki sana sana..tutafika tuu...

Pamoja sana.

Anonymous said...

Today, I went to the beach with my kids. I found a sea shell and gave
it to my 4 year old daughter and said "You can hear the ocean if you put this to your ear." She put the shell to her ear and screamed.

There was a hermit crab inside and it pinched her ear.
She never wants to go back! LoL I know this is completely off
topic but I had to tell someone!

Feel free to surf to my page paid surveys, http://paidsurveysb.tripod.com,

Anonymous said...

Saved as a favorite, I love your site!

Here is my blog post; quest bars

Anonymous said...

Wow, marvelous blog layout! How long have you been blogging for?
you made blogging look easy. The overall look of your web
site is excellent, as well as the content!

my homepage ... minecraft.net

Anonymous said...

Hey there! Do you know if they make any plugins to help with SEO?
I'm trying to get my blog to rank for some targeted keywords but
I'm not seeing very good results. If you know of
any please share. Appreciate it!

Have a look at my blog post: free music Downloads (twitter.com)

Anonymous said...

If you are going for finest contents like me, only pay a quick visit this web site everyday for the reason that it presents feature
contents, thanks

Here is my web-site - free minecraft games