Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, May 22, 2013

WEMA HAUOZI-10



Mama akaendea kuongea;

Nilipohakikisha kuwa yule mwanaume, keshaondoka, kwa haraka nikarudi ndani, na nilipofika, nilimkuta babu yako, ndio anamsogolea yule mwanamke, na panga likiwa limeinuliwa juu, na yule mwanamke , rafiki yangu alikuwa kapiga magoti, huku kainua mikono juu, akiomba msamaha..…

‘Baba unataka kufanya nini…..’nikasema huku nikimkimbilia na kujaribu kuudaka ule mkono wenye panga, na nilikuwa kama nimechelewa , maana lile panga, lilishashuka,na lilikuwa likitua kichwani mwa yule mwanamke, nikaweka nguvu zangu zote, kwanza kwa kumsukuma huyo mzee, na pili kuudaka mkono wa huyo mzee ulioshikilia panga.

Babu yako ana nguvu, japokuwa alikuwa kazeeka, lakini nguvu zake zilikuwa pale pale, maana hata kumbipa kikumbo cha kumsukuma kwa nguvu zote, lakini hakutikisika, ilikuwa kama mtu anapiga kikumbo mti ,mnene, …..lakini hata hivyo, kwa kuwahi kuudaka ule mkono, niliweza kupunguza ile nguvu kushuka lile panga, na likawa limemgonga yule mwanamke kichwani.

Kutokana na ile hali ya kutumia, nguvu nikajikuta nimemdondokea yule mwanamke, na sote wawili yaani mimi na yule mwanamke, tukaanguka chini na kulaliana, na baba alikuwa bado na lile panga mkononi, akitaka kulitumia tena, lakini akashindwa kufanya hivyo kwani mimi nilikuwa juu ya yule mwanamke nimemlalia na hiyo ndio ilikuwa salama yake.

Akiwa anatetemeka kwa hasira babu yako akalitupa lile panga chini na kugeuka, akatembea kwa mwendo wa tambo,….hadi dirishani na kuangalai nje, huku mwili mzima ukiendelea kumtetemeka kwa hasira,…sijui alikuwa akiwaza nini, kwani baadaye akageuka, na kipindi hicho nilikuwa nikimsaidia yule mwanamke kukaaa vyema.

Yule mwanamke rafiki yangu alipomuona babu yako kageuka, akajua atamreejea tena….na kwa muda alikuwa akielekea pale lilipokuwa panga,….yule mwanamke kuona hivyo, akajua salama yake haipo tena,akanisukuma,….haraka akasimama, na bila kujali, alivyokuwa, maana kule kuanguka chini, nguo zake hazikuwa zimemfunika vyema, yeye akainuka, na mbio akaelekea mlangoni, akafungua mlango hakugeuka nyuma, akakimbia, na mimi nikamshukuru mungu

Babu yako akalifikia lile panga lake, akaliokota na kulishikilia mkononi, huku mkono ukiwa umetuna na kuonyesha nguvu, kuashiria kuwa alikuwa kalishikilia kwa nguvu, alilishikilia lile kwa muda huku akiwa kaliangalia, na baadaye bila kugeuka kuniangalia , akasema;

‘Bahati yake, lakini bado hajaniponyoka….hawa watu hawastahili kuishi, maana ni sumu ya maisha ya watu, kazi yao kubwa ni fitina, na mfitinashaji ni zaidi ya mchawi…..watu wanakimbilia kuwaua wachawi, na ingelikuwa basi wanawau kweli wachawi, lakini wao wanawaua watu wanaowafikiria kwa dhana zao kuwa ni wachawi, na kuwaacha hawa watu wabaya …..hawa watu ni wabaya zaidi kuliko mnavyowafikiria, wana sumu kali zaidi ya nyoka mwenye sumu ya kuua, na mimi mzee jemedari wa vita, nimeamua kupambana nao, usiku na mchana…..’akasema na kuliinua panga lake juu, halafu akaondoka.

‘Sasa baba unakwenda wapi…?’ nikamuuliza huku nikijizoa zoa kumfuata.

‘Hiyo sio kazi yako, mimi sasa ,….nipo vitani, …..’akasema na kutoka nje kwa hatua za askari wakiwa vitani.

Nilijaribu kutoka na mimi ili nimuwahi, ili ikiwezekana, nimzuie,….hata kwa kumsihi…lakini haikusaidia kitu, alikuwa keshafika mbali. Maana babu yako ana mwendo wa haraka sana, na uzee wake huo, lakini aliweza kutembea kwa mwendo kasi , kuliko vijana wenye nguvu zao.

‘Oh, …Sijui nifanyeje,….’nikawa nahaha, nashika hiki hakishikiki, na huku naongea peke yangu kama mtu aliyechanagnyikiwa;

‘Na huyu mume wangu naona kachelewa kurudi,….siku hizi kaamua kulewa tuu, pombe na yeye , ..’nikawa naendelea kuongea peke yangu, na ghafla  nikasikia kilio, kilio kilichoashiria hatari, nikajau kuna janga tena limetokea……

********

Nikawa nakumbuka babu alivyokuwa akielezea sehemu hiyo, na muda huo alikuwa kaegemea kiti chake cah enzi, kikinesanesa, alisema;

‘Nikiwa na panga langu mkononi, nikaelekea sehemu jengo langu, kwani mama yako aliamua kunijengea nyumba ya kisasa, sio ile ya miti na majani,….na ujenzi ulikuwa bado ukiendelea, sikupenda kubakia pale nyumbani kwa mama yako, kwani akili yangu ilikuwa imesimama kufikiria zaidi,…kilichokuwepo ndani ya akili yangu ilikuwa hasira, kisasi….

Nilijua kabisa , ndivyo nilivyokuwa nikiwaza kuwa kama nitakuwa karibu na mama yako nitashindwa kutimiza malengo yangu,…..nipo vitani, na ukiwa vitani, rafiki yako ni yule atakayekusaidia kumshinda adui yako…hekima za utu uzima kwa muda huo zilikuwa zipo mapumziko,…na mimi nilijiona nadaiwa kwa kutokuweza kumlinda mke wangu hadi akafanyiwa hicho alichofanyiwa,…..hata kama nitafanya nini, sitaweza kulipa, lakini….hilo linalowezekana kwa ajili ya wengine, lifanyike….

Nikawa natembea haraka haraka kijasiri, uzee, ulisahaulika…., na nilipofika kwenye njia ya makutano, inayoeleka kwangu, na ile inayoelekea kwa yule mwanamke mfitinashaji nikasimama, nakuangalia kushoto, kulia, halafu kuelekea njia ya huyo mbaya wangu,….kwanza inabidi uwe na malengo, huwezi kwenda kumvamia adui yako bila malengo….

Oh, sio mbali na pale niliposimama, nikawaona watu wawili wakigombana, na pembeni yake, alikuwepo yule mwanamke mfitinashaji, …..alikuwa kashika kichwa, na akipiga ukulele wa kuomba msaada, nakumbuka kuusikia huo ukelele, lakini sikuwa nimeujali sana, nilijua labda ni wale vijana wanaendelea kuteketea……nigeuka na kumwangalia yule mwanamke, nay eye akaniona

Yule mwanamke aliponiona, kwanza alipanua mdomo kuendelea kupiga ukelele, lakini, akatulia, hakutoa sauti, macho yake yakamtoka pima kwa woga, akaniangalia,…hakukimbia, akabakia kasimama kama kapigilia misumari,akijua kuwa sasa yupo hatarini, lakini haweza kukimbia…...

Mimi sikujali, nikamueleka na sikuwa ninawajali hawo watu wawili waliokuwa wakipigina, na kwakweli, walihitajia msaada, mtu wa kuwaamulia,…walionekana kuwa wameumizana sana, na sijui ilikuwaje, maana jicho langu lilimuona mmoja kati ya wale wapiganaji, na hisia za udugu, zikapenya ndani ya akili yangu, na kulegeza hisia za hasira,… nikamuona…alikuwa kachoka, na kama nisingelimuwahi, angelimalizwa na adui yake…

‘Baba nipo chini ya miguu yako, mume wangu atamuua, …..mwenzake, nakuomba nipo chini ya miguu yako, nakuomba uwagombolezee….’akasema huyo mwanamke mfitinashaji, huku sasa akipiga piga miguu chini, hakujua afanyaje, maana mimi ni adui yake, mumewe, anataka kuua, na yeye hawezi tena kugombolezea, kwani kwa muda huo, alishaumizwa, uso ulionekana kuvimba…..

Na kwa vile nilishamuona baba yako, akiwa taabani….kuwa ndiye anayepigwa na karibu kuuwawa,na huyo ni mume wa binti yangu wa kufikia , yaani mama, yako, hasira kwa huyo mama mfitinashaji zikawa zimeisha, na nguvu zikaelekezwa kwa huyo anayempiga baba yako. Nikainua panga, kwa nguvu, nikiwa nataka kufanya jambo ambalo kama lingelifanikiwa tungelikuwa tunazungumza mengine.

Lakini lile panga likiwa hewani, nikaligeuza, kwenye makili kukawa juu, na kwa haraka likatua kwenye mkono wa huyo jamaa anayekuwa akimsindilia baba yako, bila huruma, damu zikiwa zimejaa kwenye mkono na kwenye nguo zake, alikuwa na dhamira moja, ya kummaliza baba yako.

Lile panga lilitua kwa wakati muafaka, na sijui wazo la kuligeuza juu chini lilikujaje, labda ni huruma, labda…sijui ila liliokoa mengi, la sivyo, huyo jamaa asingelikuwa na mkono,…., kwani kuligeuza kule likiwa hewani, lilipunuza hata ile kasi ya kupiga, lakini lilifanya kazi yake iliyokusudiwa, likajeruhi, na kuvunja nguvu ya huyo jamaaa…likauumiza ule mkono ambao ulikuwa ukipiga, ukipiga, na kupiga, kwa lengo la kuua,…na kila pigo, lilikuwa likiashiria kummaliza huyo anayemuona ni adui yake..

‘Ooooh….’mguno wa maumivu ukasikika kwa huyo jamaa, na haraka akashikilia mkono wake na kugeuka kuniangalia. Na baba yako ambaye alikuwa akigugumia kwa kila kipigo, akiwa hana nguvu tena ya kujitetea, akalala chini….kuashiria kuwa yupo katika hali mbaya, alihitajia msaada wa haraka. Nikamsukuma huyo adui yake ambaye aliserereka hadi chini, alidondoka kama gunia, huku nikisema kwa sauti ya ukali.

‘Wewe unataka kuua…hivi wewe unapigana na mtu ambaye hana lolote, mtu huyo ni mgonjwa, kama una nguvu kweli pigana na mimi…uone ni nini nitakufanya…’nikamwambia huyo jamaa huku niligeuza lile panga tayari kwa pigo jingine….nikawa namwendea pale alipodondoka, alikuwa kakaa huku akshikilia mkono wake, akiniangalia kwa uwoga, …ujasiri, hasira vyote, vilinywea, huenda ni kutokana na maumivi aliyokuwa akiyapata kwenye mkono wake….

‘Baba tafadhali,….’nikasikia sauti….na moyoni nikasema; `huyo tena kaja hadi huku…’
 Ilikuwa ni sauti ya mama yako, alikuwa akija mbio mbio…sikugeuka kumwangalia, kwani huyu jamaa ninayeambana naye, sio mchezo na lengo langu ni kuhakikisha ninamaliza nguvu, lakini yule jamaa alikuwa kakaa, na sasa alikuwa akijitahidi kusimama, akigugumia maumivu, ilionekana wazi kuwa pigo lile la langa huenda limevunja mfupa wa mkono wa huyo jamaa.

‘Oooh…’akawa anagugumia, lakini mimi sikumjali, nikamsogelea kwa ujasiri, na yule jamaa aliponiona namsogelea, na panga mkononi, kwanza alitoa macho ya uwoga, na akapanua mdomo kutaka kupiga ukulele, na baadaye nikashangaa kumuona akiyumba upande kama vile ananikwepa,…, na ghafla akadondoka chini na kulala, akatulia kimiya, nikajua ni janja yake, lakini haikuwa hivyo, alikuwa kapoteza fahamu, na ndio ikawa ahueni yake.

‘Baba…..mwache, utaleta makubwa zaidi….’akaita mama yako, na nilipogeuka nilimuona akiwa kamshikilia mume wake, baba yako alikuwa kajaa damu mdomoni na puani, na alionekana katika hali mbaya sana, ..nikageuza kichwa huku na kule, na mara uso wangu ukakutana na yule mwanamke mfitinashaji,…hasira zikanipanda, na yule mwanamke akafahamu hilo, akatimua mbio…

Watu wakawa wamefika kwa wingi, na wale walioshuhudia huo ugomvi, wakawa wanahadithia, mimi sikuwa na cha kuongea, nikawa nahangaika na baba yako,…na hatimaye, tukafanikiwa kumpeleka hospitalini, akiwa taabani.

‘Sijui kama atapona…’nikasikia watu wakiongea, na hapo hasira zikazidi kunipanda, nikijua kuwa hawo ni watoto wangu japokuwa sikuwazaa mimi, na kama nimeshindwa kuwalinda ni nani atawalinda. Unajua unaopokuwa mtu mzima, haijalishi kuwa una uwezo, au nguvu kiasi gani, mtoto bado unamuona kama ni mtoto, na unajiona wewe una nguvu zaidi yake, japokuwa sio kweli….
Kwa hasira nikawageukiwa watu waliokusanyika hapo, nikasema kwa sauti ya ujasiri;

‘Nawaambieni nyie watu mumetangaza vita dhidi yangu….na sasa ni vita kwa yule yoyote anayehusika na hili ajue kuwa yupo vitani na mimi….ambaye yupo uapnde wangu ni yule atakyenisaidia kuhakikisha hawa wanahusika na hili, na pia hawo wanahusika na mauji ya mke wangu, wanasambaratika na kusahaulika kwenye hiki kijiji….’nikasema kwa sauti, nikiwa nina uhakika kuwa watu watakwenda kumwambia huyo jamaa na jamaa zake.

‘Yeye anajifanya ana nguvu hapa kijijini, kuwa anaweza kupiga wenzake kama watoto wadogo, sasa atakuja kupambana na mimi,…’nikasema nikiangalia ule upande aliolala yule jamaa, alikuwa bado kpoteza fahamu.

‘Na ole wake, huyu mtu apoteze maisha, ….ajue ni mimi nitalipiza kisasi kwake, labda ahame huu mji, na akihama nitamfuta huko huko….mjue sasa ni jicho kwa jicho….’nikasema kwa hasira na watu wanaonifahamu wakaguna, na wengine wakaana kuondoka wakiogopa, hasa pale niliposimama. Mjukuu wangu usnione hivi na huu uzee, lakini ninapobadilika, natisha….walikimbia…’ Babu akasema ajiangalia maungoni mwake.

Japokuwa nilikuwa mzee, lakini historia ya ushujaa wangu ilikuwa inatambulikana, kwani enzi nzetu, tulikuwa na mapigano ya hapa na pale, kugombea maeneo, mifugo, na mimi nilikuwa mmoja wa majemedari walioaminika kwenye ukoo wetu, na hakuna aliyeweza kupambana na mimi, hadi nikawapewa uongozi wa ukoo wetu.

Kwahiyo kwa wanaonijua, hasa wazee wa rika langu na waliokuja baadaye , karibu karibu na marika yetu, walijua nimemaanisha nini, na haraka haraka wakakutana , na sikujua walikutana saa ngapi, maana wazee toka vijiji vya jirani, waliokuwa wamehama, waliitwa, wkajipanga kuja kulisuluhisha hiloo jambo kabla mambo hayajafika kubaya.

Kesho yake asubuhi na mapema, wazee wa huo ukoo wa huyo jamaa wakafika kwangu, wakiwa na ngombe, na mazao kwa kufuata mila za kwetu, kunapotokea jambo kama hilo, suluhu kwa mkosaji, ni kuja na ngombe dume, kuja kumuomba yule aliyekosowa na wanakuja wazee wenye busara, sio wazee tu, kwani enzi nzetu, kulikuwa na wazee walioheshimika,….wakiongea jambo, linasikilizwa, linaheshimika, na hawaongea maombo ovyo ovyo tu kama siku hizi…
Sikutaka hata kuongea nao, nikawaambia;

‘Suluhu hapa ni huyo jamaa apone, …akifa hakikisheni na huyo aliyempiga…huyo mgonjwa, maana mnamuona wenyewe ni mgonjwa, hajiwezi…yeye anakwenda kutunisha misuli kwake, anakwenda kummalizia, haoni aibu….sasa kama akifa hakikisheni na yeye mnamuua wenyewe,….’nikasema huku panga likiwa mkononi.

‘Hebu niambieni, huyo mgonjwa ana nguvu gani ya kupigana, mtu mwenyewe mnamuona keshajifia,….anaumwa,….kabakia mifupa…keshaisha, bado mtoto wenu anatunisha kifua, anapiga kama mtu anayeua mnyama….mngaliona jinsi gani alivyokuwa akimsindilia mwenzake migumi, msingelifika hapa,…..kwakweli suluhu hapa hakuna, nendeni kwa huyo jamaa yenu, shujaa wenu, mwambie akijtundike kamba, kabla sijakutana naye…………..’nikasema na nilikuwa naongea kwa hasira kweli kweli.

‘Mzee mwenzetu, hawa ni watoto, na sisi tunatakiwa tuwaonyeshe kuwa sisi ni wazee wao, tuwafunde,…maana kama unavyoona, dunia ya sasa sio kama ile ya kwetu….watoto wa siku hizi hawana adabu, hawasikilizi wazee wao, sasa sisi ni wazazi tunahitajika tujitahidi hivyo hivyo…kwa ujumla kakosa sana, katuabisha sana, ndio maana sisi wazee tuliobakia ambao tunaheshimu mila na desturi tumeamua kuja kukuona.

‘Mzee mwenzetu… kimila mtu jasiri, mwenye hekima, huruhusiwi kupigana na mgonjwa, au kupigana na akina mama, au kupigana na wazee wasiojioweza, lakini mwenzetu huyo hasira zimemtawala…hana adabu,…hatusikii….wazee tumemchoka, tunakiri hilo, lakini yeye asiwe kisingizio cha kuvunja udugu, mshikamano…na kuvuruga amani za eneo letu hili….’akawa anaongea kiongozi wa wazee wao.

‘Sasa kama hasira zimemtawala, tunataka tuzione kwenye uwanja wa mapambano….si ndio anavyotaka,, kuonyesha kuwa yeye ni mwanaume….sasa mwambieni kuwa leo nataka kuonana na yeye kwenye uwanja wetu wa mapambano,…mimi na yeye, nimemaliza….’nikasema na kugeuka na kuwaashiria kwa mkono waondoke.

‘Mzee mwenzetu, tunakuomba tena sana,….maana hata hivyo jamaa mwenyewe mkono umevunjika, imebidi na yeye apelekwe hospitalini, amefungwa muhogo, …sasa kawa kama kachanganyikiwa kila anayemsogelea anamuogopa,…sasa hivi anamuogopa kila mtu, ….utafikiri anaona vitu gani. Hata mkewe hivyo hivyo amekuwa kama kachanganyikiwa, wote sasa ni wagonjwa, wamelazwa wodi ya vichaa, hawajiwezi, wapo taabani….’ Akasema huyo mzee, akionyesha masikitiko .

‘Wakati mke wangu anaungua, wakati haya yanatokea kwenye familia yangu, hamkusikitika, mnasikitika kwa ajili ya familia yenu, hamuhisi wenzenu wnavyoumia, ….kama kweli mlikuwa mkijali, mngelihisi maumivu ya wenzenu, kama nyie, hamuwapendi majirani zenu, mkajipenda wenyewe, mnafikiri salama itakuwapo…..’nikawaambia.

‘Mzee mwenzetu, tunajua tumekosa, na ndio maana tupo hapa, tunakuomba sana,familia kwa hivi sasa ipo kwenye hali ngumu,….tunakuomba tuikoe hiyo familia kabla mambo hayajawafika pabaya….tunaelewa ni nini kitafuata baada ya hapo…sisi wazee tunalifaham hilo, …kizazi hicho kitakwisha, kitasahaulika, na huenda chuki hizo zikasambaa, na….kuvuruga mshikamno wetu, ….tunakuomba ulione hilo kwa hekima zako jemedari….tunakuomba, ten asana…’akasema huyo mzee.

‘Na bado….nawaambia na bado, yeye na wale wote wale walioshirikiana, kutaka kuiangamiza familia yangu,yatawapaat makubwa, mlikuwa kimiya wakati watu wanatanagza fitina, wanaitanagzia familia yangu mambo ya kichawi, mlikuwa hamuoni, nafahamu kabisa wengi wenu wenye maono ya mbali mlijua kabisa kuwa sio kweli…mke wangu yupo mbali kabisa na hayo waliyoyasingiziwa ….’nikawaambi nikawaangali wazee wale, ambao walikuwa wametulia kimiya.

‘Au ninaongopa, ni nani mwenye uhakika na huo uzushi animabie, ,…..aaah, sitaki kuwalazimsiha, kama kuna ambaye ana ushahidi wa kuwa mke wangu alikuwa mchawi animabie, ili na mimi niwe na amani….nani ana huo ushahidi, au twendeni tukale amini, kuwa kweli hayo yaliyozungumzwa ni kweli, kama ni kweli mimi niangamie, na kama sio kweli nyote mnahusika muangamie, twendeni tukale amini….’nikasema nikaanza kuondoka.

‘Mzee mwenzetu, sio kweli, tunajua kabisa kuwa huo ulikuwa ni uzushi….lakini watu wengi walikuwa wakimuamini sana huyo mtaalamu, na sisi hatukuwa na la kusema….hilo linahitajia kukaa kijiji kizima na kutubu, maana matokea yake ndio hayo yanaanza kutokea, mabya yatatuandama, na tujuavyo, mabaya yakiendelea yatatuasiri sote, …..’akasema huyo msemaji wao.

‘Sasa mnaanza kuogopa, kipindi kile mlikuwa mumejifungua ndani….au mnajidai kuwa hamukuwa an nguvu ya kumwambia huyo mtaalamu kuwa anachofanya sio kweli….kumsingizia mke wangu kuwa ni mchawi, hilo sijui mtalimaliza vipi….wote ni lazima waishie kubaya,…nawaambia ukweli, kilio changu, kilio cha mke wangu, alicholia wakati anaungua na moto, hakitaisha hivi hivi mpaka, wote waliohusika na wao wayapate kama hayo yaliyompata mke wangu ……’nikasema.

Mara ghafla, wale wazee wakapiga magoti mbele yangu….kwa wazee kama hawo kupiga magoti, ni jambo kubwa sana, na haijalishi una nguvu au hasira za namna gani, kama wazee wenzako watafikia hatua ya kukupigia magoti, inabidi usalimu amri, na hapo nikaduwaa, nikajikuta nimesimama mwii mzima ukinitetemeka kwa hasira, ….hadi nikawa sina nguvu tena, na sijui kilinikuta kitu gani,

`Mjukuu wangu, naona lwa leo tuusihie hapa maana hasira chuki…bado vipo moyoni,…nakumbuka hali niliyoiskia pale sikuweza kuvumilia, nikadondoak chini, na giza likatanda usoni mwangu, na sikujua ni nini kiliendelea hapo tena….’akasema babu huku machozi yakimlenga lenga

*****

NB: Tusemeje, tukatishe kisa, maana huenda nawaboa…sawa, tuombe mungu, akitujalia tunaweza tukaendelea

WAZO LA LEO: Inapotokea hali ya mtafarauku, watu wakakosa kuelewana, jambo jema ni suluhu, sio mababu,na suluhu haiji mpaka watu, wenye hekima wakutane, waongee na waone jinsi gani wataliondoa hilo tatizo.

Jamani Propoganda potofu, uchochezi, fitina, ni adui mkubwa, mkubwa zaidi ya bomu la nyukilia,..tuvikwepeni hivi vitu…tusione ni rahisi tu kuandika, kuongea,…madhara yake ni mbaya. Tukaeni, tuongeeni, na tuangalia wapi tumeteleza. Haya ni kwa maslahi ya vizazi vyetu, na taifa letu kwa ujumla, ubinafsi, hautatusaidia kamwe, tusipopendana, na kumpenda jirani yako,…haki ikatawala hakutakuwa na amani kamwe.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

I blog often and I genuinely thank you for your content. This great article has truly peaked my interest.
I will book mark your site and keep checking for new details about once per week.
I opted in for your Feed as well.

Also visit my homepage: http://hotgirlsexcam.com

Anonymous said...

Excellent post but I was wondering if you could
write a litte more on this subject? I'd be very thankful if you could elaborate a little bit further. Thank you!

Here is my homepage - party sex