Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, May 17, 2013

Kipaji ni rasilimali aliyokujalia muumba wako



Unapopanda mche au mbegu kwenye ardhi, unatarajia mavuno ambayo yatakuwa mbegu kwa mavuno mengine. Lakini mavuno hayo yanatategemeana na jinsi gani ulivyoiboresha hiyo ardhi, na mazingira mazima ya eno hilo.

Kwa utaalamu wa kilimo, mimea mbali mbali, ina stahili yake ya udongo, ndio maana kahawa ya kagera haistawi vyema Kilimanjaro, japokuwa zote ni kahawa. Mahindi na mharage yanahitaji aina fukani ya udongo ili yazae vyema, japokuwa sasa hivi kuna utaalamu wa kuboresha ardhi, lakini kama huo uboreshaji utakosekana, basi ina maana mazao hayo yaliyopandwa kwenye udongo usiostahili hayatastawi vyema.
Wakati nikiwaza hili nikajikuta nikiwazia watoto wetu,….nikaangalia haya matukio yanatokea katika dunia yetu hii, nikakumbuka usia wa babu yangu.

Wajukuu zangu, watoto wa leo, yaani nyie, ndio mtakaokuwa chachu ya amani kesho na kesho kutwa, mjue msipojiweka sawa, kimaadili, mkakazania elimu yenu, mtarajie mavuno mabaya baadaye . Ni sawa na kama vile tunapanda mbegu ya mahindi mahali ambapo, hapana mbolea 

…..Na hata kama pana mbolea, lakini bado tumepanda kwenye udongo usiostahili….leo mlitakiwa msome kwenye shule zilizo na vifaa vya kisasa ili mjue sayansi muwe madakitari, lakini wapi…hata chaki ya kuandikia hakuna….tutafika kweli’

‘Lakini wajukuu zangu msikate tamaa….kama mnajitambua wenyewe, na mnajua nini kipo mbele yenu, msikate tamaa, sisi hatukata tamaa, ndio maana mumezaliwa nyie….cha muhimu sana tambueni vipaji vyenu vya kitaaluma vitawasaidia sana….’

Ni kweli kila mtu amejaliwa kipaji chake, huenda hilo watu wengi hawafahamu, inawezekana vipaji vikalandana, hiyo sio tija, lakini cha muhimu kwanza ni kukitambua kipaji ulichobarikiwa nacho ambacho ukikitambua vyema, utaweza kufanya jambo fulani kwa uwezo mkubwa, kuliko mwingine ambaye hana kipaji hicho. Kuna vipaji vya kujifunza, hilo hatukatai, lakini vipaji vya kujifunza, mtu hawi na wito nacho, kwake yeye ni sehemu ya kukidhi matakwa fulani tu.

Wakati watu wanahangaika kutafuta ni kwanini watoto wetu wanafeli mitihani,…elimu inazidi kudorora, na kujikuta tukilaumiana kuwa kwanini watoto wetu hawafanikiwi kwa kiasi kikubwa, nafikiri pia tungeliliangalia hilo la vipaji kwa watoto wetu, kama sehemu mojawapo yakuwezesha kuboresha elimu za watoto wetu kwa kiasi kinachotakiwa.

Ili kulitambua hili kwa mapana, chukua watoto kadhaa wafundishe hesabu kwa mtizamo sawa, jitahidi sana somo hilo lieleweke kwa kila mmojawapo, utagundua kuwa kati yao kuna watakaoelewa zaidi yaw engine na wengine wanaweza wasielewe kabisa. Sasa je utasema hawa wasioweza kuelewa kabisa au wameelewa kidogo, hawana akili, hapana, kila mtu anakili,…, lakini ni kuwa taaluma hiyo wanaojifunza sio kipaji chao.

Ni kweli ni muhimu, kila mwanafunzi akajifunza karibu kila kitu, (kila somo), maana maisha yetu ni kila kitu, huwezi ukasema nisisome kabisa somo fulani, mfano hesabu kwasababu sio kipaji changu, lakini maisha yetu yanakuhitaji kujua hesabu, ili uweze kwenda na maisha ya kawaida, kuna mambo yatakuhitajia kujua hesabu,kiinhereza, sayansi jiografia nk …., ndio maana kila mmoja anatakiwa angalau ajue kila somo kwa manufaa yake ya baadaye. Lakini kwa muda gani?

Tatizo hapa, ni jinsi gani ya kutambua vipaji vya watoto wetu toka utotoni, na je vipaji hivyo vitawekwa kwa madaraja gani, kwani tukizungumzia vipaji, tunazungumzia kwa lugha pana, yaani kwa ujumla wa maisha yetu….kuna vipaji vya michezo, vipaji vya kitaaluma na vipaji vya kiutendaji, vyote hivi vinatofautiana kati ya mtu na mtu…

Shule za awali zingelikuwa sehemu muhimu ya kutafuta vipaji hivi,…na kumbukumbu za mtoto huyu zianze kuhifadhiwa hapa, ili akifika shule ya msingi, walimu wanakuwa wakimfahamu mtoto huyu mapema, na itakuwa kwake rahisi kumfuatilia kwa karibu, kwa vile atakuwa keshajulishwa umakini wake toka huko awali na yeye ajue vipi atamkazania huyu mtoto zaidi , ili aweza kuendana na mitaala.

Hebu tuulizane vyema, kuna kumbukumbu gani mtoto wa chekechea anakwenda nazo na kukabidhiwa mwalimi wa shule ya msingi, kuwa huyu alikuwa vipi kwenye masomo yake ya awali. Hili halipo,….na halikadhalika kuna kumbukumbu gani za mtoto wa shule ya msingi anakwenda nazo sekondari , ili mwalimu wake ajue ni vipi mtoto huyu alikuwa….sina uhakika kuwa haya yapo. Sisi tunachofanya ni ule usemi wa kiingereza…`try and error’….au kubahatisha.

Zama hizi ni za kitekinolojia zaidi, kumbukumbu za watoto zinaweza kuhifadhiwa kwenye mitandao, siku hizi mitandao ipo wazi, ni swala la kutilia maananitu. Tukaondoa ubinafsi na kuwekeza kwenye elimu, tukatumia rasilimali za madini, kwa ajili ya elimu ya watoto badala ya kununua magari ya kifahari. Hili linawezekana,….

Kama tutaamua kuwa elimi ni muhimu kwa watoto wetu na vizazi vyetu, sio tu kwa familai zetu, bali kwa taiaf zima, na tukawa na mipangilia thabiti ya kuhifadhi haya, kwa ajili ya baadaye tunaweza kabisa. Na hili pia litatusaidia kupata viongozi waadilifu, maana kumbukumbu hazijifichi, ilimradi ziwe zinahifadhiwa kwa umakini na kwa usiri unaostahili kama kumbukumbu binafsi zinavyohifadhiwa, hadi hapo zitakapohitajika. 

Hili nalo tutahitaji wafadhili. Au kwa vile , huenda, hata ukiweka amira halitaweza kuhumuka tukapaat cha juu,…haya tusubiri hadi wenzetu watakapolala, huenda na sisi tutaamuka, na sijui labda ndio itakwua miwsho wa dunia. Twajidanganya tukizania mtoto ni mtoto wangu wa mwingine atajua mzazi wake.

Tunashinda kujua kuwa matatizo yanayoikumba dunia sasa hivi ni kwasababu ya kukwepa majukumu, kuwa kila mzazi ni mzazi wa kila mtoto, ubinafsi umetutawala, na kujiangalia sisi,…na wenyewe ndio sisi….au sio. Moto ukiwaka , wa majanga, matatizo, tujue chanzo ni sisi wenyewe…

WAZO LA LEO: Usikate tamaa katika maisha, kila mtu anacho kipaji chake ambacho akikitumia vyema kinaweza kuwa mtaji wa maisha yake. Tusibweteke kwa kuiga yale yawenzetu kwa vile wao wamefanikiwa zaidi, tukazania huenda na sisi tukifanya hivyo tutafanikiwa kama wao. Inawezekana mkawa sawa na yeye kwenye vipaji,….hilo hatukati, ni sawa kabisa, kama ni hivyo basi,jitahidi uwe kama yeye, au zaidi. Tatizo hap ni je umeshajichunguza na kugundua kipaji chako kipo kwenye Nyanja ipi, anza leo kukitafuta kipaji chako, ukikigundua, utafanikiwa kwa kiasi kikubwa, usikate tamaa.
Hebu msikilize LUCK DUBE HAPA 

Ni mimi: emu-three

4 comments :

Anonymous said...

Howdy just wanted to give you a quick heads up and let you know a few of the
images aren't loading properly. I'm not sure why but I
think its a linking issue. I've tried it in two different browsers and both show the same outcome.

Here is my web-site: friendmend.Com

Yasinta Ngonyani said...

Kila mtu sna kipaji chake kweli.
Nimependa simulizi hii. Hata ujirani mwema ni kipaji. Ahsante jirani mwema.

Anonymous said...

I used to be recommended this website by my cousin.
I am no longer certain whether or not this put up is written through him as nobody else recognize
such specific approximately my difficulty. You are incredible!
Thanks!

Feel free to visit my page - mammoth sea creature

Anonymous said...

naturally like your web-site however you need to check the spelling on quite a few of your
posts. A number of them are rife with spelling issues and I in finding it very bothersome
to tell the reality then again I will surely come back again.


My website; Www.Goolloo.com