Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, May 24, 2013

BARAZA LA VIONGOZI WA DINI


                                    Picha kutoka; http://sabahionline.com
Dini zipo nyingi, na madhehebu ndani ya kila dini ni mengi. Ili kuleta umoja, na kuondoa sintofahamu, minung’uniko, ambayo ndio inachochea mambo, mikutano kama hiyo wangejaribu kuwajumuisha viongozi wote wanaokubaliwa na watu wao, ili kila mmoja atoe mawazo yake, na baadaye wazame kwenye imaniza kweli za dini zao, ambazo ukichunguza kiukweli, zote zinahimiza amani, upendo, haki sawa.

 Mimi naamini kama viongozi wa dini wakitumia imani zao vyema, wakazieneza kwa waumini wao kwa hekima na busara, bila kuweka ubinafsi wa hisia zao, nchi hii itakuwa na amani, kwa vile bado wananchi wetu wana mioyo ya kiimani, hawajagubikwa na imani za chuki kihivyo. Na pia ukiangalia kiundani  viongozi wa kisiasa pamoja ya jazba zao, wakikutana na viongozi wao wa dini wanakubali ushauri wao, na wengine wanazitumia hata kwenye kazi zao.

 Kwa uoni wangu, wakati sasa umefika, nchi kama hii yetu kuwa na baraza la viongozi wa dini Tanzania, ambapo humo watakuwepo viongozi mbali mbali wa dini zote zilizopo nchini, bila kubagua, na viongozi hawo wawe wanaokubalika na waumini zao, wasichaguliwe kisiasa, na hili baraza liwe karibu na raisi, kama washauri wake kuhusu maswala yanayotokana na dini, ili raisi asipotoshwe, kwani kuna taarifa nyingine zikifika kwake zinakuwa zimeshachakachuliwa.

Baraza hili kila kukitokea tatizo wakutane, na sio kusubiri tatizo tu, hapana pia wawe na vikao vya mara kwa mara kwa maslahi ya taifa. Pia hii inaweza ikajenga hali ya kuzoeana kwa viongozi hawa wa dini, nah ii inakwena moja kwa moja hadi kwa waumini wao, na viongozi hawa wakiwa karibukaribu, wataweza hata kukosoana wenyewe kwa wenyewe, kuwa mwenzetu hapo umekosea, hebu tuambie imani gani inataka hivyo unavyofanya wewe. Lakini pia ni kupeana ukweli ili kila mmoja ajue dini ya mwenzake vyema.

 Zamani baba wa taifa, J.K Nyerere, alikuwa akikutana na wazee mara kwa mara, hii ina maana yake, kuna maswala ambayo yanahitaji busara za wazee. Akiona ni muhimu, na huenda anataak kuchukua hatua itakayoleta manung’uniko, kwanza anakwenda kuwaweka sawa wazee…kiukweli, na kihekima, kuna maswala ambayo yanahitaji busara za wazee, hata kiongozi uwe mzuri gani, bado kuna kukosea, na wazee wetu wanajua mengi, wanaweza wakakushauri jambo, ambalo lingesaidia taifa,…sisi sasa wazee tunawageuak na kuwaita wachawi…..balaa na laana

Kiukweli na kihali halisi kwa nchi yetu hii ambayo dini inaheshimika dini imeteka akili za watu, japokuwa wengi hawazifahamu dini zao vyema, na ndio udhaifu waliogundua wenzetu na wanataka kuutumia udhaifu huo kutugawa, na hapa ndio utaona umuhimu wa viongozi wa dini kuwa wanahitajika sana kutumiwa ili kujenga umoja, ili kuzijenga imani za watu wakawa kitu kimoja, na pale tunapozungumzia utaifa tuonekane watu wamoja, japokuwa  kiimani tunatofautiana. Raisi tumia baraza hili kupata ushauri, hawa ni watu wa hekima, na wana nguvu sana kwa waumini wao, na nguvu zao ni za kimungu.

 Wakati sasa umefika, na ninarejea usemi wangu, kuwa kama kuna kipindi tunatakiwa tuwe wamoja, ni kipindi kama HIKI, maana maadui zetu, wameshagundua udhaifu wetu, kwanza tunatatizo la elimi(adui ujinga), na sio kuzarauliana, lakini elimu inamsaidia mtu kuweza kupambanua mambo kwa uhakika zaidi, sisi elimu yetu bado ipo chini, utasema mbona kuna nchi za wasomi mbona wanagombana. Lakini elimi ninayoizungumzia hapa ni elimu ya utambuzi,…

 Lakini kubwa zaidi tuna udhaifi wa elimu ya dini, wakati tunajifanya tuwaumini, na hapo ndio watu hawa wanapotupatia,wanatuperekesha kama bendera fuata upepo, lakini ukichunguza sana, ni kwasababu waumini hawazijui dini zao vyema, na wanachokifanya ni kuwafuata watu(viongozi wao) kama ndio dini zao, hili ni tatizo na ni udhaifu unatumiwa kwetu, nah ii ni hatari.

Najingine kubwa kuliko ni hali mbaya ya kiuchumi,  umasikini uliokithiri, ambao pia unachangiwa na utofauti mkubwa wa walio nacho na wasio nacho, kwani adui yako muombee njaa. Imefikia hali ambayo ile hali ya kusaidiana imeanza kuondoka, na ubinfasi umetawala.

Mimi nina imani kuwa Taifa letu bado halijafikia kuitwa masikini wa kutupwa, kwasabbu wapo matajiri, ambao bado wana imani zao za dini, wakiamua, wanaweza wakatumia utajiri wao kuwekeza na kuwaajiri wale wasiojiweza. Na hapo ndio maana nasema kama kuna wakati tunahitajika kuwa pamoja ni sasa, kabla hatujaupanua huu wigo wa chuki, kwani utatoka kwenye imani za dini, utakwenda kwa walio nacho na wasio na nacho, na ukichunguza sana, nahisi watu hawachukiani kwasababu ya `dini’ zao, tuwe makini hapo,….sababu kubwa ni hali mbaya uchumi, haki haipo,….watu wameshaanza kuhisi hivyo. Kuna upendeleo unahisiwa, hili watu wanalalamika wanapuuzwa ….na hili litaondoka , pale watu tutakapowezeshana. Hebu tuliangalia hili nalo kiundani.

Wenye nacho wakumbukeni wasio nacho, timizeni kiukweli imani zenu, ..imani za dini zinatutaka hivyo, tupendane, tusaidiane, tuhurumiane…sasa nashangaa pale watu wanapotafuta njia ya kuwezeshwa wengine wanakataza, wakati wao wana hiyo mianya, je kweli tuna upendo wa dhati hapo,…tuungane tujadilaine hili na tutafute njia ya kusaidiana kwa upendo wa kweli.

Kama viongozi wa dini mtafarakisha watu, …tutakuwa na shaka na imani zenu, kwani tujuavyo sisi waumini wa kawaida ni kuwa, imani zote za dini zinafundisha upendo au sio?

Na pia kwa viongozi wa dini msimilikiwe na viongozi wa siasa, hawo ni waumini wenu pia, kama mtamilikiwa na viongozi wa siasa tutakuwa na mashaka na imani zenu, ina maana wao ndio wanawafundiha imani za dini, sio kweli, na pia wameshatuambia kuwa wao kama wanasiasa mambo yao hayana dini, kwanini mnatekwa na wao. …

Kwa hilo la viongozi wa dini kukutana hongereni sana, ila boresheni kwa kuwaongeza viongozi wengine wa dini zote, ili mjenge usawa, umoja na mshikamano wa imani zote.

WAZO LA LEO: Dini, zinatufundisha amani na upendo, haki za kila eneo, na mshikamano pale tunapokuwa na imani tofauti, je viongozi wa dini, mnafanya hivyo, na kama mnafundisha kufarakana, hiyo ni imani gani. Je ni kweli ni kuwa udini ndio unasababisha haya yote, nahisi tunahitaji kulichunguza hili zaidi, na hili mtalipata mkikutana mara kwa mara na kwa kuwa karibu na waumini zenu.

Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Hoja iliyokwenda shule-tatizo sehemu kama hizi hawafiki wao na udaku

Anonymous said...

safi kabisa kaka nakuunga mkono

Anonymous said...

Hoja iliyokwenda shule-tatizo sehemu kama hizi hawafiki wao na udaku