Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, April 9, 2013

Uchungu wa Mwana Aujuaye ni mzazi-81-hitimisho-1Kilikuwa chumba cha chini kwa chini, na giza lilikuwa kali sana, kiasi kwamba hata masikio hayakuweza kuhisi kitu, zaidi ya jinamizi la kuhisi kuwa kuna kitu kinapita. Pale kitandani, alilala mwanadada mmoja, akiwa kavaliwa rasmi, hakutaka kuvalia nguo za kulalia, akijua kuwa yupo vitani. Kwa hali kama ile hakuweza kumwamini yoyoye, hata yeye mwenyewe hakujiamini, akijua kuwa anaweza akapitiwa na usingizi.

Akashikilia bastola yake Mkononi vyema na kuhakikisha kuwa alivyolala, anaweza akajihami bila wasiwasi, akavuta pumzi na kuhesabu dakika kumi za kupata usingizi, dakika kama hizo kwake zinatosha kabisa, akafumba macho, lakini haikuwa rahisi rahisi kupata usingizi, kwani kila alipofumba macho alijikuta kama anaota ndoto mbaya, akaona hakulaliki.

Akafumbua macho na kuanza kuangalai giza, akaona hakuna tofauti ya kufumba au kufumbua macho, kwani vyote kwake ilikuwa ni giza totoro, akaona ni vyema akili yake ipange mambo mapema kabla hakujapambazuka. Akawaza;

Huu ni muda wa mwisho katika mpangilio wa maisha yake, na juhudu zote za kimaisha hapo ndio sehemu ya kujua mbivu au mbichi. Alikumbuka wenzake alio kuwa nao, ambao, wengine wameshatangulia mbele ya haki, yote ni kwa ajili ya kufanikisha hilo, alipowakumbuka akaguna na kusema;

‘Hayo ndio matokea ya vita, kuna kufa na kupona, ukifa , basi umekwenda kupumzika, lakini ukipona, hutakiwi kurudi nyuma, ….na kuosnga mbele, ….hadi hapo utakapopata ushindi, uipata ushindi inategema na malengo yako, kama hukuwa makini unaweza ukajikuta ukiambulia kusononeka huku wenzako wakifaidi matunda ya jasho, hilo kwa mwanadada huyo alipa kuwa halitawezekana.

‘Mimi ndiye jemedari wa hii vita, hata kama kuna viongozi, …..wanajiita viongozi, kazi yao kukaa ofisini, lakini mimi ndiye mpiganaji, nastahili kufaidi matunda ya jasho langu…nitapambana hadi nione kila kitu kipo mkononi mwangu…’akasema na kunyosha mkono kulenga shabaha…..’ akatabasamu.
Akainua kichwa na kuangalia huku na kule, na pale pale akakumbuka jambo, …akaanza kuwaza, kuhusu vita iliyopo mikononi mwake, alijua wapinzani wake wa karibu keshawamaliza, lakini kuna mpinzani mmoja mkubwa,…..akageuza kichwa na kuangalia mlangoni, …akatikisa kichwa na kusema kimoyomoyo.

‘Huyu haniwezi, ….’akasema kwa sauti.

Japokuwa haniwezi, kwa silaha, lakini ataniweza kwa akili, yeye anajua sheria, na kwa sheria anaweza akatumia mbinu kuhakikisa kila kitu anakipata yeye mwenyewe,….akamkumbuka jinsi  gani allivyoweza kuwahadaa wengine na mwisho wa siku yeye mwenye akashauri kuwa dawa ya kuwashinda wengine ni kuwaziba mdomo…

‘Kwanini tuwaue, ..hawa ni wenzetu?’ akauliza huyo mwanadada.

‘Hakuna siri ya watu wengi, hawa wote unaowaona, wakitishiwa kidogo na polisi watasema kila kitu, dawa yao ni kuwalipua, ..na hakuna haja ya kutumia mikono yetu, dawa yao ni ndogo tu, ….’akasema huyo mwanaume.

‘Dawa yao ni ipi?’ akauliza.

‘Watajiua wenyewe, ….’akasema na kweli ndivyo ilivyotokea, kila mmoja aliitwa kwa wakati wake ,akapewa pesa kidogo na kutumwa kwenda kumwinda, mwenzake,….na mwenzake huyo huyo akapewa pesa kidogo kwenda kumwinda huyo anayemuwinda yeye, ikawa kuwinda kwa kuwindana, na wakajikuta wakiuana wenyewe kwa wenyewe.

‘Wameshajiua, na pesa badi ipo mikononi mwetu….’akasema huyo mwanaume.

‘Kweli wewe mjanja…’akasema huyo mwanamke.

‘Ndio katika maisha haya lazima uwe mjanja, vinginevyo, hutaweza kushinda, …na ilivyo hivi sasa huwezi kumwamini yoyote, na dawa ya ushindi ni kubakia peke yako, kama walivyosema hakuna siri ya watu wawili’akasema na huyu mwanadada alipokumbuka hayo maneno, akainuka haraka pale kitandani.

Kama mshale akajikuta yupo sakafuni akiwa tayari kwa lolote, akapapasa macho…huku akijiuliza kichwani, ina maana kweli aliona kitu, au ni macho yake tu, au ni hisia zake akiwa kwenye mawazo ambayo yaligeuka kuwa kama ndoto, ….akawa kapiga goti, mwendo wa kuwa tayari kama mkimbiaji wa mbio, akalenga bastola yake kwenye kile alichohisi ni mtu….

Kile kitu hakikosogea, akajivingirisha mara mbili na alipotua alikuwa karibu na kile kitu alichokiona, kulikuwa hakuna kitu,…ni mlango, lakini ulikuwa umefunguliwa nusu, na yeye alikumbuka kabisa kuwa alkuwa kaufunga, japokuwa sio kwa ufungua, akainuka na kuegemea ukuta, huku bastola ikiwa tayari kwa lolote lile;

‘Huyu kama ni huyu mshenzi, ni lazima nimuondoe, kwanza atakuwa kaonyesha kutoniamini, najua hatuaminiani, lakini yeye keshajionyesha mapema…nisipomuondoa yeye anaweza kunimaliza, na mimi sasa nahisi kuchoka….’akasema huku akijaribu kuondoa uchomvu wa machoni.

Taratibu akawa anajisogeza hadi kwenye kiwashio c lakini yule mwanamke alihisi kulikuwa na kitu kabla, akasogea ukutani na kha taa ukutani, akawasha taa, kinyume na makubaliano yao.

‘Kwanini unawasha taa?’ sauti ikasikika nyuma yake na haraka akageuka bastola ikiwa mkononi.

‘Nilijua tu kuwa umeingia chumbani mwangu, na hili ni kinyume na makubaliano yetu’akasema.

‘Ni kweli lakini katika hali tuliyo nayo, hakuna wa kumwamini mwenzake…’akasema huyo mwanaume, naye kiwa kashikilia bastola mkononi.

‘Ni nini unataka?’ yule mwanamke akauliza.

‘Bila shaka unajua ni kitu gani nakitaka….nimeshahisi kuwa unaweza ukanisaliti muda wowote, kwahiyo ni bora tukagawana kila mtu akajua ustaarabu wake’akasema huyo mwanaume. Yule mwanadada akaona kidole cha yule jamaa kikicheza cheza kwenye kiwambo cha kufyatulia, akajua huyo jamaa ana dhamira ya kweli ya kumuua, akawa anatafuta sehemu ya kuchupa, wakati na yeye akifwa keshakifikisha kidole chake kwenye kiwambo cha kufyatulia risasi. Hapo ujanja ni kupata…

******
Akiwa kitandani usingizi ulikuwa hauji, na alijua kuwa vyovyote iwavyo, hivi sasa polisi wanaweza wakawa wamejizatati na kugundua mengi kuhusu kuroroka kwao, na huenda wameshagundua kuwa sasa hivi wapo Dar.

Japokuwa usingizi haukuwepo, lakini mara kwa mara kulikuwa na usingizi wa mang’amung’amu, ulikuwa unamjia na kuondoka, na kila ulipomjia, alijikuta anawaza kama vile anaota,….

‘Watu wote wanauhusika ambao wanaweza kujua wapi tulipo wameshaondoka dunia, waliobakia ni wale ambao hawajui lolote, ….mtu wa hatari aliyebakia kwa sasa ni huyu mwanamke, na kwa hali ilivyo, siwezi kumwamini hata kwa sekunde moja, …yapo mawili, kugawana na kila mmoja akashika njia yake, au kummaliza kabisa….’akasema huku akivuta sigara yake.

‘Huyu kummaliza sio kazi rahisi….kupambana naye ni sawa na kupambana na `bataliani’, ni sawa na kupambana na kikosi kizima cha makomandoo….’akasema huku akigeuka kuangalia bastola yake iliyopo pembeni mwake.

‘Sasa nifanyeje?’ akajiuliza.

‘Aaah, mimi ni mwanaume bwana, siwezi kushindwa na mwanamke…’akasema na akatupa kile kichungi cha sigara, akaweka mkono wake kitandani kuikamata ile bastola yake, hakujua kuwa wakati anajinyosha, ile bastoal aliisogeza bila kujua,..

Mkono wake, ulipotua pale alipokuwa kaiweka bastola yake akajikuta anapapasa hewa,…hali ile ilimshitua sana, akainuka kwa haraka na kuangalia huku na kule, akiwa tayari keshahisi kuwa mwenzake keshaingia na kumuwahi,….

Alipohakikisha kuwa hakuna mtu, akageuka kuangalia kitandani, hakuwa na uhakika,…mtu pekee mwenye uwepesi, kiasi hicho ni huyo mwanamke,…hakuna mtu mwingine anayemfahamu angeliweza kuingia haraka kiasi hicho na kuichukua bastola yake, ….akasema huku akiangalia kitandani, …akaiona, kumbe wakati alipopitiwa na usingizi alikuwa kaisogeza ile bastola mbali na pale alipokuwa kaiweka….

‘Dawa ya kuondokana na huu wasiwasi ni kuhakikisha kuwa nipo peke yangu, kwani nikiwa karibu na huyu mwanamke ambaye anabadilika kama kinyonga sitaweza kuwa na amani….huyu mwanamke kanifanya nikaitelekeza familia yangu, yote nikimjali yeye zaidi,…lakini namjua hapo alipoa anatafuta njia za kunimaliza, kwasasa sina maana kwake…’akawa anaongea peke yake.

‘Kwana jiulize kama ni mpenzi wangu wa kweli, kwanini hakupenda tukalala chumba kimoja….’akasema huku akipuliza moshi wa sigara juu,

‘Kwa mtaji huo ana lake jambo, na mimi nimeshashituka, dawa ni kumuondoa ….’akasema huku akiwa kaishikilia ile bastola mkononi, akaangalia mlango unauelekea chumba alipolala huyo mwanamke.

‘Yeye peke yake ndiye aliyebakia , ambaye anajua kila kitu,…lakini lazima niwe na sababu za kumuendela , oh, sijui huyu jamaa tuliyemtua atakuwa keshamaliza hiyo kazoo tuliyomtuma,…sijapata taarifa yoyote, na kwa jinsi ilivyo siwezi kumpigia simu kwa sasa.

‘Lakini kwa jinsi ninavymfahamu huyu jamaa yangu, … docta kwa sasa atakuwa  maiti, kama kweli huyo mtu tuliyemtuma kafanya kama tulivyomuagiza,…..’akasema huku akiangalia kule mlangoni huku akikumbuka maagizo yake aliyompa yule mtu waliyemtuma kummaliza docta.

‘Pesa hii hapa, hakikisha unakwenda kummaliza yule docta,…yule tuliyekuonyesha mchana, uhakikishe kakata roho, ndio uje uchukue sehemu yako iliyobakia, na kama haikutokea hivyo, wewe mwenyewe utakuwa marehemu…’akamwambia huyu jamaa.

‘Mimi tena mkuu, hiyo kwangu ni kazi rahisi, ila naomba nikirudi hapa pesa yangu iwe tayari, maana sitaki kuishi haya maisha tena, nataka nitubu dhambi zangu niachane na hizi kazi za kuua watu wasio na hatia…,’akasema. Huyu jamaa alikuwa mtu wao muhimu sana, huwa akzi yake ilikuwa ndio hiyo….kuyakatisha maisha ya watu, na huwa akitumwa hafanyi makosa.

Jamaa hakujua kuwa wenzake walikuwa na malengo mengine, walijua kazi yake imekwisha kwahiyo akirudi kuchukua pesa yake iliyobakia na yeye utakuwa mwisho wake,…..kubakia kwake hai kungeliwaweka hawa jamaa kwenye wasiwasi na yeye ni lazima amalizwe.

‘Usijali ndugu, kazi zetu hizi zina malengo, na sote twatarajia hivyo, ..kuwa tukimaliza hii kazi, itakuwa ni hitimsiho la kutulia, ….ama kwa raha , au ….moja kwa moja, …yote sawa,….wewe kakamilishe hiyo kazi, na mshiko wako utaukuta hapa ukikusubiri…’akaambiwa na yeye akaguna na kuondoka.

Alipoondoka yule jamaa, akageuka na kuingia chumbani kwake, huku akiwaza hatima yake, akijuliza je na yeye kazi hiyo ikimalizika atafanyaje, na yeye akatubu dhambi zake na kutafuta sehemu ya kuishi, maana hatarajii kuwa polisi watatulia ….ni lazima watamtafuta usiku na mchana,…akachukua sigara yake na kuanza kuvuta huku akiangalia mushi wa sigara ukipotea hewani.

 `Nii muhimu kwanza huyu jamaa arejee…huyu huyu jamaa kabla sijammaliza, ninaweza kwanza kumtumia kummaliza huyu mwanamke,….’aliposema huyu mwanamke, akawa anaangalia chumba kinachoangaliana naye, japokuwa ilikuwa giza kali, lakini aliweza kuona sehemu ile ya mlango kwa hisia.

‘Lakini siwezi kumuua huyo mwanamke mpaka niipate ile hundi,….’akasema akikumbuka kuwa ile hundi ya kuchukulia pesa ipo mikononi mwa huyo mwanamke.

‘Nitakwenda kumpa taarifa kuwa kazi ya kummaliza mtu wetu muhimu imekamilika, iliyobakia ni kupanga jinsi ya kwenda benki kuchukua hizo pesa…hizo pesa hazina maneno, maana mmojawapo wa wathibitishaji wa kuchukua pesa za mzee ni mimi….hiyo haina shida, ilimradi tumeshapata sahihi yake….’akakuna kichwa.

‘Kwanza ni jinsi gani ya kugawana, maana huyu mwanamke, haaminiki….’akakuna kichwa huku akiangalia lile giza lililotanda mbele, lilikuwa giza nzito…na kila akiliagalia alihisi maisha ya kaburini, ambayo anahisi kuwa kuwa giza lake litakuwa kama hilo.

‘Aaah, kwanini naingiwa na wasiwasi wa kufa….’akachukua sigara yake na kuitia mdomoni. Huku akivuta moshi kwa kasi kabla haujaupuliza nje, akasema kwa sauti ndogo;

‘Ni lazima niwe makini na huyu mwanamke…ok,  lakini kwanza lazima tukubaliane, ….tugawane kila mmoja ashike mshiko wake….’akatupa kile kipande cha sigara na kuinuka pale alipokuwa amekaa na kuanza kutembea kule kulipokuwa na mlango, huku akiwa kashikilia bastola yake, hakumuamini yule mwanamke.

‘Na kama nitamkutaka kalala, nimammaliza hapo hapo…’ akasema huku akifungua mlango taratibu wa kile chumba ambacho ndicho alipo huyo mshirika mwenza, ambaye kwa sasa alimuona kama adui yake.

Mlango ulipofunguka, haraka akachepuka, na kuurudishia mlango kwa taratibu, hakuamini kuwa angeliweza kuingia kirahisi hivyo,…kwa makubaliano yao, huyo mwanamke hakustahili kuufunga mlango kwa ufunguo, ..na kweli ilifanyika hivyo…lakini kama alivyomfahamu huyo mwanamke, asingeliweza kuingia bila kupata pingamizi,….

‘Oh, simba wa vita kazidiwa….na inaashiria kuwa mwisho wake umeshafika, sasa kazi ni moja, ni kummaliza kabla hajanishitukia…. …’akawa anaongea akilini. Akasogea taratibu, akichelea kugusa kitu ambacho kitatoa sauti, akakumbuka pale walipokuwa wameweka begi lenye nyaraka na ushahidi mbali mbali, na humo waliweka kitabu cha hundi.

‘Kwana nichukue ile hundi na stakabadhi ya malipo…’ akasema akiiufuata ule mkoba, baada ya kuthibitisha kuwa mshirika wake kalala….na akakumbuka walivyokubaliana mchana, kuwa yeye kwa vile anaruhusiwa kuchukua pesa za mzee, na ni mmoja wa watu waliokuwa wamepewa mamlaka ya kuthibitisha malipo kama mwanasheria wa mzee. Hakuwa na mashaka kuwa watakwama kuzichukua hizo pesa.

‘Mimi sina shida, wewe kaa na hilo begi…., kwani najua mwisho wa siku mimi kama mwanasheria ndiye nastahili kwenda kuzichukua hizo pesa…’najua mzee yupo mahututi, hajaweza kuwaambia benki lolote, au polisi kwenda kuzuia malipo yoyote. Hilo nina uhakika nalo, kwani niliwasiliana na muhasibu wao akasema hakuna chochote,….mzee hali yake ni mbaya, hajitambui.

‘Kwahiyo kinachohitajika ni uharaka wetu….’akasema mshirika wake.

‘Ndio hivyo mpenzi, ukiwa na mimi ujua upon a kichwa….kila jambo linakwenda kwa mahesabu , situmii nguvu, natumia akili…..kwahiyo kaa na hilo begi, ili kukuthibitishia kuwa mimi ninakuamini….’akasema

‘Sawa….umeshinda kwa sasa, lakini safari nyingine, …sitaki kusikia hilo neno mpenzi…..mpenzi wako ni mkeo,…..toka humu ndani nenda kwako’akasema huyo mshirika.

‘Imekuwa hayo…..’akasema huyo mwanaume.

‘Ndio hivyo, na nahitajia kulala….sitaki usumbufu, nenda kwenye chumba chako, …ole wako uje kunsisumbua, nitahakikisha risasi zote zilizopo kwenye hii bastola zinaishai kichwani mwako….’akasema huyo mwanadada, akikunja uso kuonyesha kutokufurahishwa na hiyo hali, na wakati huo huyo mwanaume akitabasamu, huku akiogopa ile sura aliyoiona kwa huyo mwanadada, inayoashiria chuki, na ukatali wa kuua.

Akatoka na kwenda chumbani kwake, huku akisema kimoyomoyo, nitarudi tena hapa, na nikirudi hapa, huo uso nitausawazisha, ama kwa chombo cha moto, au kwa pesa…..

Wakati anawaza hayo alikuwa kachuchumaa pale chini akiwa kashikila lile begi, alihisi kitu, sauti, akaangaza macho, hakuona kitu zaidi ya giza nene…akataka kuinuka na kuhakikisha vyema, lakini kwa lile giza, hata kama huyo mwanamke atakuwa kaamuka, asingeliweza kujua kuwa yupo humo ndani, na kwa makubaliano yao , kwa ajili ya usalama, walitakiwa wasiwashe taaa.

Akalishika lile begi alizingusha sehemu ya kufungulia, huku akipapasa , na akiwa anatizama mara kwa mara kule alipolala mhasimu, wake, vidole vikitafuta sehemu ya kufungulia,, hakutaka kuondoka na begi lote,…akashika zipu yake, na kuivuta, na sauti ya mkwaruzo wa ile zipu ikasikika, ….akatulia, na kutega masikio, akaona kimiya,…

‘Bado kalala…’akasema na kuendelea na shughuli yake, lakini kabla hajaivuta ile zipu tena,  taa zikawaka, na yeye kwa haraka akasimama akiwa na bastola yake mkononi, tayari imelenga kwa adui yake. Na kwa kujihami akasema;

‘Kwanini unawasha taa,…’ akasema kwa sauti ya kukwaruza ikiashiria wasiwasi mwingi, huku kidole kikicheza cheza kwenye kiwambo cha kufyatulia bastola, hakuwa na mzaha tena, alijua akichelewa yeye , mwenzake atamuwahi, na muda kummaliza huyo mtu ni huo, kukipambazuka, huenda akakosa kila kitu. 

Akakiza kidole chake huku akijiandaa kuruka kwani alijua kuwa mwenzake anaweza akawa nay eye kafyatua bastoa yake.

Mlipuko mkubwa ukasikia, na kilio cha maumivu....WAZO LA LEO:Aliyezoea ubaya, akitendewa ubaya huhisi machungu mara mbili, kwani mkuki ni kwa nguruwe.


Ni mimi: emu-three

No comments :