Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, April 4, 2013

Uchungu mwa mwana Aujuaye ni mzazi-79




‘Ni nani wewe….’akasema Maua, na kugeuka haraka kuangalia nyuma yake, na kujikuta wakiangaliana na mama yake mdogo,

‘Umejuaje kuwa nipo hapa ?’ Maua akamuuliza mama yake mdogo kwa mshangao. Mama yake mdogo alikuwa akiangalia barabarani, akiwa anaangalia gari la yule dakitari likiondoka.

‘Milioni mia mbili, ….hebu fikiria pesa kama hiyo ukiishika mkononi, umasikini wote bai-bai,….Unaona, hii ndio dunia..ujanja kupata sio kuwahi,….’akasema huku akiangalia juu, kama vile anawaza jambo fulani.

‘Nimekuuliza ulijuaje kuwa nipo hapa na huyu Dakitari?’ akauliza tena Maua.

‘Hiyo sio kazi yako, ….’akasema huku akiondoka, na wala hakujali kumsubiri Maua. Na Maua akamfuatili kwa nyuma hadi walipofika nyumbani.

‘Mimi nakushangaa, naona umekuwa mtu wa kunifuatilia kama kivuli, …..’akasema Maua.

‘Mimi sijakufuatilia wewe….nilikuwa nafuatilia mambo yangu, wewe endelea na gumzo lako na huyo dakitari wako, ….mimi sina muda huo…’akasema.

‘Mama , unajua haya yote yametokea kwa sababu yako,..na usikimbilie kunilaumu, kwani usingeliniingiza kwenye mambo yenu nisingelifikia hapa…..’akasema Maua.

‘Acha visingizio….ushamba wako ndio umefikisha hapo, na usinitupie lawama mimi kamwe, usipojifunza kwa hilo, usitegemee kuwa kuna mwalimu wa kukufundisha,…’akasema mama mdogo.

‘Sawa nashukuru….sizani kama ungelikuwa umenizaa ungelinifanyia haya,…’akasema Maua kwa uchungu.

‘Tatizo lako umeshahu kuwa nilikutoa kwenye umasikini, na kutokana na mimi mama yako ana nyumba, hayo yote hamuyaoni….’akasema huyo mama.

‘Yote hayo yamefanyika kwa mgongo wangu, mimi ndiye nimeumizwa, hadi haya yote yakapatikana..’akasema Maua.

‘Na utaumia zaidi…..’akasema mama mdogo huku akijiangalia kwenye kiyoo.

‘Sawa..ipo siku nitakipa..na mtajuta wote mlionifanyia haya…’akasema Maua

‘Haya endelea na usafi, maana leo ulinitegea, fua nguo, ukimaliza, pika,….mimi nakwenda kuhangaika, bila kuhangaika, hatuwezi kula…..wewe na hicho kimimba chako, jipweteka hapa nyumbani, mwisho wa siku utakula jeuri yako…..maana sasa hivi si unaringa, ngoja, ifikie muda wa kujifungua, ndipo hapo utakaponiona mimi ni nani’akasema.

‘Una maana gani kusema hivyo?’ akauliza Maua.

‘Utanielewa tu…mimi sio mtu wa kulea mmba za watu, …nilishakuambia mtafute mume wa kuilea hiyo mimba, hutaki, ukakimbilia kumuona dakitari, haya kakusaidia nini…?’ akauliza na kama vile kakumbuka kitu akasema;

‘Lakini sio mbaya, …nimefurahi kwamba kanifunua akili,..milioni ishirini…na ngapi vile…’akasema huku akionyesha kufurahi na kuondoka zake, na Maua kwa shida akawa anafanya hizo kazi za nyumbani.

*****

‘Maua umefika,samhanai kwa kuchelewa, na naona hapa tutaongea bila kusumbulia….’akasema docta huku akifunga mlango, na Maua akakaa kwenye kiti bila hata ya kukaribishwa, akasubiri Dakitari akae, huku akili yake ikiwa inawaza mambo mengi.

‘Docta, mimi sioni kwanini tuwe na mazungumzo marefu, kwani sizani hilo linahitajia kuongea, kama kwelii unamfahamu , au unafahamu ni nani aliyenipa huu ujauzito niambie ukweli nijua ni wewe au kuna mtu mwingine, …?’ akauliza Maua na docta akamwangalia na kutaabsamu.

‘Tulia mpendwa,…kwa hali ilivyo…nasita hata kukuambia ukweli, japokuwa nilimuahidi Tajiri kufanya hivyo…’akasema.

‘Kwanini docta…na najua kuwa unafahamu yote vinginevyo Tajiri asingelinielekeza nije kwako’akasema Maua akionyesha kukaat tamaa.

‘Kama niliyokuambia kuwa mimi ni dakiatari wa familia ya Mzee, na kwa vile nilikuwa nikimuhudumia Mzee, basi nikawa dakitari wa familia nzima,….kila kukitokea tatizo, la ugonjwa, wakawa wananiita mimi…na bahati niliyo nayo, sikusomea udakitari tu…..’akaanza kulezea.

‘Mzee, alianza matatizo yake, kitambo, na mimi nilijaribu kumuelekeza jinsi gani ya kuweza kuyakwepa hayo yanayoweza kumletea madhara, lakini mzee yule alikuwa mbishi sana,….Nilimwambia ili asiumie zaidi kwanza asiwe anabishana na mkewe, kwani chanzo cha matatizo yao kilianzia kwenye kutokuelewana kati yake na mkewe…’akatulia.

‘Maua nikuelezee ukweli, …ndoa ni nusu ya maisha ya mtu, ukishaoa, ujue kuwa kila kitu ni kimeshinikizwa kwenye ndoa, hata kuwaza, ….mawazo yako yote hayawezi kuwaza bila kuifikiria ndoa yako, vinginevyo unajiadanganya….’akasema na kumwangalia Maua.

‘ Mzee, alikuwa kajenga utaratibu wake ….na hata baada ya kuona alikuwa kaweka mipango yake, kuwa mambo yake, hasa ya kikazi, kibishara ni yake binafsi na mkewe ni mshauri tu, hakupenda kumshirikisha moja kwa moja…na chochoko zilianzia hapo….’akasema.

‘Katika maisha kuna kupanda na kushuka, ilifikia mahali akakwama, mkewe akamshauri,….na alimshauri 
kwenye mambo ya kishirkina,….wakati huo, alikuwa hana matatizo ya kiafya, kwahiyo kujuana kwetu hakukuwa kama ilivyokuja kuwa baadaye….’akakohoa kidogo kama kusafisha koo.

‘Mzee, akakubali, na wakafanya waliyoyafanya, na sina uhakika kuwa hayo waliyoyafanya ndiyo yaliyowasaidia,..hadi kufikia hatua hiyo….kama alivyoniambai mkewe….kuwa utajiri wote ulitokana na imani hiyo….’akatulia.

Maisha yakawanyookea, biashara ikapanuka, wakafungua kampuni, na hata kuwa na wafanyakazi, na pesa ikaanza kufanya mambo yake. Mzee, enzi hizo sio mzee, ni Tajiri…jina tajiri, lilikuwa jina la mzee, kipindi hicho,japokuwa halikuwa jina la kujulikana kama alivyokuja kulitumia mpwa wake…akawa sio mwenzetu. ..’akatulia.

Pesa, utajiri, usipouweza kuumiliki unaweza ukakuharibu, …mzee kipindi hicho hakuwa na wazo hilo, akawa anatumia, na huenda ndio ulikuwa muda wake, ili kujionyesha, basi akina dada hakucheza nao mbali, na hili likawa limemkwaza sana mkewe, …wivu, na ….ni kawaida kwenye ndoa….wakawa wanakwazana. Basi siku moja mkewe akadondoka kwa shinikizo la moyo….

********

 Siku mkewe alipodondoka ilikuwa ni siku ya sherehe za kuzaliwa mmoja wa binti zao, na mume akaaga kuwa anatoka kidogo, sijui ilikuwaje, mke akashituka na kuanza kuwafuatilia. Ni kweli kumbe mumewe alikuwa kaagana na mwanamke ….kwenye nyumba ya wageni.

Mkewe akafika kwenye eneo la tukio, na akamfuma mumewe, …, akiwa na mwanamke, na mwanamke huyo alikuwa rafiki kipenzi cha huyo mkewe, hakuamini, na akili, ikishindwa kuhimili, mapigo ya moyo yakaongezeka, na matokea yake ni kudondoka na kupoteza fahamu….’ Akaangalia saa yake na baaadaye akamwangalia Maua.

‘Maua usione huu mwili, …kitu kidogo tu, kinaweza kikaharibu mpangilio wote wa mwili, na ukawa sio yule mtu wa jana, huyo mama akawa mgonjwa sana, …ikabidi huyo mwanadada alatwe hospitalini nilipokuwa nafanyia kazi kipindi hicho…, kipindi hicho huyo mwanadada anawaka kweli mrembo, japokuwa alishazaa watoto watatu….

Na ndipo nilipoanza kuzoeana na mke wa mzee, kwani alipofika hapo hospitalini, nikawa mimi ndio namtibia, na akawa kila mara akijisikia vibaya ananiita mimi, …na kipindi hicho sijawa mzoefu sana, na kufikia kiwango cha dakitari bingwa.

‘Nilimchukulia huyo mama , kama sehemu ya utafiti wa kazi yangu, nikawa karibu naye, na nikawa nikimdadidisi, kujua undani wa matatizo yao…. nikagundua kuwa ana mawazo sana, na mawazo hayo yalitokana na ndoa yake…wivu..chuki, na alikuwa tayari kulipiza kisasi…. Nilimshauri sana,…kuwa ajaribu kuhimili hayo yaliyopo mbele yake, kwani yana mwisho, na asipojitahidi hivyo, ataumia, na wenzake watachukua nafasi yake… nashukuru alinielewa, japokuwa kila mara alikuwa akiniambia;

'Wewe bado mdogo, hujui uchungu wa kuchukuliwa mume, ….’aliniambia na nilimuelewa ana maana gani, na nikajaribu nijuavyo kumuelimisha, japokuwa nilikuwa mdogo, ….lakini baadaye akatulia na tukawa kama marafiki.

‘Huyu mwanadada, kipindi hajaolewa alikuwa rafiki ya kaka yangu, na kipindi hicho  alitakiwa kuolewa na kaka yangu, lakini haikuwezekana, kwani mzee, alimuwahi na kumuacha kaka yangu akiteseka kwa mawazo, kwani kaka alimpenda sana huyo mwanamama….mimi nilikuwa mdogo, na nilimuonea huruma sana kaka yangu,…sikutarajia kuwa nitafanikiwa kuwa karibu na huyu msalati wa kaka yangu.

Kaka yangu alipomkosa huyu mwanadada, alikosa raha sana, ….unajua kaka yangu alimpenda sana huyo mwanadada hadi kupeana pete za uchumba, na ilibakia kidogo tu wafunge ndoa,…siku wakati wanasubiri hiyo ndoa, ndio huyu mwanadada akapotea ghafla, na kila wakienda kuulizia nyumbani kwao, hawatoi jibu lililo sahihi, kuonyesha kuwa walikuwa njama moja.

Kaka akawa mgonjwa…..hali halali......

Mapenzi hayana siri, kwani, baadaye tukasikia kuwa wamefunga ndoa na huyo mzee, na wanaishi naye…kaka aliumia,…unajua kuumia, …akawa kama mgonjwa, …mimi nilikuwa nampenda sana kaka yangu huyu, nikawa sichezi mbali na yeye, na ule utoto, ..nikimuona kaka yangu alivyobadilika, kakonda kama mgonjwa wa ugonjwa usio pona…nilikuwa nalia…na ilifikia hatua naapiza kuwa siku nikimuona huyo aliyemfanyia kaka yangu hivyo, cha moto akakiona….

‘Na yeye nitahakikisha anapata taabu….na kukonda kama alivyomfanyia kaka yangu…’nikamwambia mama, na mama kipindi hicho anaumwa, akaniambia;

‘Mwanangu ukitaka maisha yako yawe mazuri, usipende kulipiza visasi…hata mtu akikufanyia ubaya gani, wewe uwe mwema kwake…’akasema mama. Na baadaye niliposikia kuwa mama kafariki, na chanzo ni hay ohayo….’akatulia na alionekana kama anajiwa na machozi, lakini akajikaza kiume na kusema;

‘Hawa watu walihamia Arusha muda mrefu, na kutokana na historia ya familia yao, watu wengi waliamini kuwa wana tabia hiyo ya kishirikina…mimi siamini sana mambo hayo, …na hata wazazi hawakupendezewa pale kaka alipoamua kumuoa huyo mwanamke,  kwa imani hizo hizo…na ilipotokea hivyo..kuwa huyo mwanamke kakimbilia kwa mwanaume mwingine.., kwao wao walishukuru sana…

Ghafla nikajikuta nipo na hawa watu tena…sikuyajali ya kale, na kwa vile nimeshakuwa mtu mzima, mwenye taaluma, nikajipotezea hayo na kuganga yalikuwepo mbele yangu. Na hata nilipokutana na huyu mwanadada nilimtambua kwa jina la shemeji na tukawa tunaitana hivyo…nilikuwa na hasira naye, kwa jinsi alivyomfanyia kaka yangu, lakini kwa vile yalishapita, sikuyatilia maanani sana.

*******

Tabia haina dawa, na ukiingiza ubongo wako kwenye imani, unaweza ukajikuta ukiwa mtumwa,…na huenda kama sio mtafiti, ukajikuta unajiumiza mwenyewe, kwa imani ambazo huenda hata sio za kweli…na ndivyo ilivyokuwa kwa huyu mwanadada.

Alipoletwa kwangu nikamtibia na kumpa ushauri nasaha, alikuwa akiitikia tu,..lakini alikuwa na lake moyoni,….kwani alipopona, alimua kutumia njia nyingine alizojua yeye…..nafikiri alipokutana na wazazi , kwani aliamua kwenda kupumzika huko kijijini kwao,..huenda wazazi au marafiki  walimshauri hivyo, au ni kutokana na maamuzi yake, au hizo imani za mapokeo bila kufikiria akazifuata….na akawa kama analipiza kisasi, kwani aliporudi toka nyumbani kwao, akabadilika…

Ndivyo maisha ya ndoa yalivyo…..mama huyo aliporejea mjini, alikuja kwa namna ya pekee kabisa, ile hali aliyokuwa nayo, ka kujifunga makanga, kujifunika, ikawa haipo tena…mavazi yakabadilika, …muonekano ukawa sio ule tuliokuwa tukiufahamu,….akawa mtoto wa mjini….kaamua na yeye kujirusha na wanaume wengine.

Alipokuwa huko kijijini, alikutana na kaka yangu, na watu walifikia kusema kuwa huenda, aliamua kumrejea aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, yaani kaka yangu…sina uhakika sana na hilo. Lakini ni tatizo lilozindua hisia zilizokuwa zimeshaanza kupoa, na ilionekana kama huyo mwanamke alikuwa an nia mbaya na familia yetu.

Kaka yangu alikaa muda mrefu bila kuoa,…akisononeka….na mama yangu akawa hana raha,...na kutokana na hilo, mama akashikwa na ugonjwa ..uliompelekea kupooza upande mmoja na hakukaa sana akafariki dunia...mama nilimpenda sana..oh, kipindi hicho bado nasoma, naletewa taarifa kama hiyo niliumia sana…niliporejea nyumbani na kuhadithia hayo…niliumia sana, nilitaka kwenda kwenye hiyo familia kufanya jambo baya, lakini wakanizuia….'akatulia akiwa kakunja uso.

'Anyway...yote yakapita, nikarejea masomoni....na hata nilipoondoka hapo nikawa nimerejesha moyo nyuma na kusema yote hayo ni mapenzi ya mungu....na yana mwisho wake...'akainama na kuwa kama anaomba

Na kipindi huyo mwanadada alipofika huko, alimkuta kaka ndio kaoa mke mwingine , baada ya kuachana na mke aliyekuwa naye awali….mke huyo aliyemuoa alikuwa na sifa zote za mke mwema, na wengi  tulitarajia kuwa wataweza kuishi na kaka vyema, lakini cha ajabu, kaka alipomuona huyu mwanadada, akamuacha mkewe…na kuanza kutembea na huyu mwanadada…niliumia sana nilivyosikia hivyo.

Kaka hakujua kuwa mwenzake anayafanya hayo kwa hasira za kulipiza kisasi kwa mumewe….anadanganyika, na wengine wakasema huyo mwanamke kamuwekea dawa kaka yangu ili awe naye, lakini sio kwa mapenzi ya nzati…kaka akawa kama mtumwa fulani wa huyo mwanadada..huwezi kusema kitu….wazazi wakawa hawana raha….yote hayo nilikuja kuhadithiwa …’akatulia na kulionekana chuki usoni na baadaye akasema

‘Tayaache hayo…tuendelee na ya kwetu….’akasema na kushika kichwa na alionekana kama anawaza jambo, halafu akasema;.

‘Baadaye huyu mama akamuacha kaka kwenye mataa, akamrejea mume wake huku Arusha, akiwa sio yule mama tuliyemjua kabla, aliamua kubadilika sana,…, akawa mtu wa starehe kupitiliza, analewa na kutembea na waume za watu bila aibu…ikawa na aheri ya mume wake…na ghafla kukatokea jambo lilozua gumzo kwa watu, maana mume wake nay eye alibadilika ghafla, ……’akatulia kidogo.

Mume wake akawa kama mjinga fulani, habanduki nyumbani, ….akawa hatoki, akitoka, anakuwa kama anajiiba, hata watu wakaanza kusema kuwa huyo mwanamama, kamtengeneza mumewe, kipindi hicho ni mwanadada, japokuwa alikuwa keshazaa, lakini alikuwa msichana mrembo….na wanaume waroho wakawa wanasogelea kila kukicha.

Hali ya mzee, ikawa ya mashaka, kwani alikuwa kama mtu anayetumia madawa ya kulevya,….zezeta , ikabidi afikishwe hospitalini, na mimi nikawa karibu naye, ….na tukawa tumezoeana sana, japokuwa ni mkubwa sana kwangu, lakini kama alivyokuwa mkewe tukajenga urafiki wa karibu, na ndipo akaanza kunielezea maisha yake, nikamjua na yeye vyema, kama nilivyomfahamu mkewe….

Nikawa nimeijua hii familia kama vile nimezaliwa ndani yake..na moyo wangu ukawa unanihimiza nitimize lile lengo langu la utotoni…kulipiza kisasi …..na huku moyo mwingine ukinikanya kuwa hayo hayana faida kwangu…..nikajikuta kwenye njia panda…

NB: Imenibidi niandike sehemu hii ndogo kwa shida,..ndio maisha,…na sasa tumesikia nauli hizo zinapanda…mbona kazi, ..kufa hatufi ila cha moto tutakiona. Usitarajie mwenye shibe akamjali mwenye njaa, watatezi wetu, viongozi wetu, hawawezi kamwe kujua shida zenu,…wao wana shibe, ndio wawekezaji wa usafiri, unatarajia nini.

Naomba….tusichoke kuendelea na hiki kisa, kwani ni visa vyenye mafunzo, na kila sehemu ina ajenda ya kuelimisha jambo fulani…na tuna imani kuwa tukimalizana na huyu docta, tunaingia kwenye hitimisho.

WAZO LA LEO: Tuwe makini kwa vijana wetu hasa wanapofikia ule umri wa `vishawishi’ tujaribu kujenga tabia ya kuwaweka karibu na kusikiliza matatizo yao, kwani muda huo unaweza ukawa mgumu kwao, na wasipopata msaada wa hekima, inawezekana ikawa ni chanzo cha kuharibikiwa katika maisha yao.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Hakika hapa pazuri na pananoga..ilausiwe sana kwenye njia panda...wala hatuchoki tupo pamoja...

Rachel Siwa said...

Ndugu wa mimi naona Kazi inapamba mto..MUNGU azidi kukusimamia na kubariki kazi za mikono yako!!

Pamoja sana Ndugu wamimi...