Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, March 8, 2013

Uchungu wa mwana Aujuaye ni mzazi-69



Mama Maua alipofika kwa mume wake, alikuwa kama kachanganyikiwa na kila alipojaribu kutuliza kichwa alishindwa , na kila akijaribu kushughulikana na wateja, alijikuta akikosea kurudisha chenji za watu, hata mume wake ikabidi aingilie kati, na kumuuliza mkewe, kulikoni;

‘Vipi mwenzangu upo sawa kweli?’ akauliza mume mtu.

‘Nipo sawa,..kwani vipi?’ akajitahidi kuwa kama kawaida.

‘Hapana nakuona haupo sawa, maana tangu uje, unakuwa kama mtu aliyekutana na jinamizi, na kila akiliwazia anakuwa kama anashituka….niambie ukweli huko ulipokwenda kumetokea nini, maana hata wateja wanalalamika, …na kinachoniogopesha ni hayo maneno ya watu, kwani nimesikia kuwa huko ulikotoka kuna kamata kamata ya wauza madawa ya kulevya’ akasema Mume wake.

‘Kwahiyo na mimi umeniweka kwenye hilo kundi,….au ?’ akauliza mama Maua akijaribu kujishughulisha na kazi nyingine, na mume akamsogelea,….akamshika begani.

‘Hapana, sijakuweka kwenye hilo kundi mke wangu, …ila ninachotaka ni kujua kama kuna tatizo lolote ili tuweze kulitfutia ufumbuzi kwa pamoja, ujue wewe ni mke wangu, na tatizo lako ni langu….au umeanza kuwa na yako peke yako?’ akauliza mume mtu.

‘Hapana mume wangu,….hakuna tatizo …. hayo niliyokutana nayo huko naona usijiingize, …..nataka wewe utilize kichwa chako kwenye mambo yetu ya biashara, ….kwani sote tukiachanganyikiwa biashara itakufa,…na mzigo tulio nao ni muhimu sana, ili tuweze kupata pesa za kununua mzigo mkubwa wa kuondoka nao…hayo ya huko….aaah.’akasita kuendelea kuongea.

‘Sikiliza mke wangu…..mimi na wewe ni kitu kimoja, na mke au mume akikwaza na jambo, wote wanatakiwa kuhisi…na hali uliyo nayo, imeshanigharimu na mimi, ….hapa nilipo sitaweza kutuliza akili yangu mpaka nijue ni nini kinachokusumbua….’akasema.

Mama Maua alijua kama asipomuelezea mume wake, tatizo alilo nalo, mume wake hataweza kutulia, ataendelea kumuuliza, na haikuwa nia yake kumuhusisha na hayo aliyokutana nayo huko, …..akili yake ilikuwa ikiwaza mengi, ….mara amuwazie binti yake, mara….

‘Mume wangu,…..nakuomba utilize kichwa chako, kwani mambo niliyokutana nayo huko ni ya kuumiza kichwa, na hayatakuweka katika hali njema……na nikujuavyo, hutayaweza, san asana, utazidi kunichanganya kichwa changu, nakuomba uniachie mwenyewe’akasea Mama Maua.

‘Nimeshakuambia kama usiponiambia nitaendelea kukuliza, na hilo litanifanya nisiwe na amani kwani wengi wanaongea mengi,….na utanifanya nihisi mengine, kumba sivyo ilivyokuwa….niambie huko umekutana na masahibu gani?’akauliza kwa sauti ya juu na hapo mama          Maua akaacha kazi liyokuwa akifanya, na kuja kukaa karibu na mume wake.

‘Haya nitakuambia,….maana na wewe ukiang’ang’ania jambo huliachii…japokuwa nikujuavyo, sizani kama utaweza kulifuatilia,..na kwa vile umetaka, mimi nitakuambia, nione hekima yako’akasema mama Maua na kuanza kumuelezea mume wake.

********

‘Mume wangu, ni kuhusu yule binti wetu, binti yako wa kufikia, nimekutana naye,….’akasema Mama Maua.

‘Ooh, sasa kwanini hukuja naye….nina hamu sana ya kuonana naye, unajua siku nyingi hajaja kututembelea, ni binti mwema sana, …..kwani imekuwaje, kuna taarifa gabi umepata, maana kama sikosei yupo Dar?’ akauliza

‘Hilo ndilo linaloifanya nisiwe na raha….kwani huko alipo yupo kwenye mitihani mikubwa, na..mpaka sasa siamini kuwa binti yetu kakumbwa na shetani gani’akasema Mama Maua.

‘Una uhakika na hilo, umeambiwa na nani, wewe usiwasikilize watu wa huku, wanaweza wakamzushia mtu mambo mengi….hata hivyo, huo ushetani ulioambiwa ni ushetani wa namna gani….?’ Akauliza mume mtu.

‘Yaani, …unajua nilpotoka hapa kwenda kwa yule rafiki yangu, ….aliniambia kuwa kamuona bint yetu…’akasema.

‘Kamuona wapi,….kwani alisafiri kwenda Dar?’ akauliza mume mtu.

‘Binti yetu yupo hapa Arusha,….na mambo anayoyafanya ni ya aibu matupu’akasema mama Maua.

‘Wewe, ndio hayo ya kusikia,…..kwani ulishuhudia kwa macho yako, maana kuna mambo ya kuambiwa, na imekuwaje afike huku,….?’ Akauliza maswali mengi.

‘Uhakika wa hilo  upi zaidi ..maana mimi nimewakuta,..kwa amcho yangu mwenyewe, ningehadithiwa, nisingeamini, lakini nimewaona kwa macho yangu mwenyewe, wakiwa chumbani..’akasema Mama Maua.

‘Wakiwa chumbani, …huyu huyu Maua ninayemjua mimi, haiwezekani, ina maana binti yetu, kafikia huko,….hapana sio  huyu Maua ninayemjua mimi, huyo ni mtu mwingine, una uhakika umemuona ?’ akauliza

‘Nimemuona, tukaongea naye….usinifanye mimi mtoto mdogo, mimi nisimtambue binti yangu mwenyewe, hata anenepe vipi, au ajichubue vipi, siwezi kumsahau mwanangu’akasema mama.

‘Mmmm ,..ina maana anafanya hayo bila aibu,…mbona anatuabisha, kama ni hivyo, twende tukamchukuea haraka, maana ataingia kwenye magonjwa….na kwanini afanye hivyo, ina maana hata pesa alizotutumia zimetokana na mambo hayo…..’akasema mume mtu akiwa anawazia mbali zaidi.

‘Mume wangu, kama ningelikuwa na uwezo ningelifika nikamfunga kamba nikamkokota hadi huku , tukarudi naye nyumbani,…lakini yule kwa sasa ni mtu mzima, ana akili zake, ..hata hivyo, yupo na mama yake mdogo….japokuwa sikupata muda wa kuonana na huyo mama yake mdogo, na kama ningelionana naye…..’akatulia.

‘Ina maana mama yake mdogo ndiye aliyemfundiaha mambo hayo…..kwahiyo sasa hivi ni mtaalamu, sio kama alivyokuwa mwanzoni muoga, …?’ akauliza mume wake.

‘Kama sio yeye, ni nani angelimfundisha mtoto wetu…mtoto yule nimemlea mwenyewe, hana tabia chafu kama hizo..kaharibikia kwenye mikono ya mama yake mdogo…na inaonyesha kuna shinikizo la nguvu, sio hivi hivi tu…’akasema.

‘Sasa unasubiri nini, twende tukamchukue….tukiwa wawili haitashiundika kitu,….mimi nitahakikisha kuwa ninamshawishi, hadi tunaondoka naye….’akasema mume, huku akifungasha vitu tayari kwa kuondoka. Na mama Maua akawa katulia tu, alikuwa kama hataki kwenda na mume wake.

‘Mbona umetulia, …hutaki kwenda tukamchukue binti yetu,…sisi ni wazazi tusipochukua hatua, tutakuwa hatutimizi wajibu wetu kama baba na mama wa mtoto, au sio….?’ akauliza baba mtu

‘Tatizo ni kuwa keshabebeshwa mzigo,….’akasema mama, na kumfanya baba mtu kushituka, alikuwa kama kasikia jambo, lakini hakuwa na uhakika nalo, akasimama na kutulia, huku akiwa kaangalia pale alipokuwa akipanga vitu vyake, na baadaye akasema,

‘Una maana ana mimba,…kapata uja uzito….?’ akauliza na kujikuta akiacha ile kazi ya kufunga funga vitu.

‘Hilo ndilo tatizo, na ndilo tatizo linalomfanya asiachane na hawo watu….’akasema mama yake

‘Watu gani, ndio wateja wake ehe, sasa atajuaje kuwa yupi ambaye kambebesha huo uja uzito?’ akauliza.

‘Sio wateja wake wewe mbona unamfikiria mwanangu hivyo, sio hivyo, sio kwamba anafanya hivyo unavyofikiria wewe,….ila, yupo mzee mmoja, ambaye ndiye anataka kumuoa, …ni mzee sawa na babu yake’akasema mama Maua.

‘Eti nini….?’ Akamaka huyu mwanaume, na kutulia , alionekana kuduwaa, na mawazo mengi, na akawa hataki kumwangalia tena mkewe moja kwa moja usoni.

‘Ndio maana nilikuwambia mambo ya huko, usiyaingilie yatakuumiza kichwa bure…sasa unaona, unatamani, uondoke, usiyasikie….je niendelee?’ akauliza mama Maua.

‘Aaah, hapo sasa, ni tatizo….maana kama angelikuwa peke yake, ningesema hakuna shida, lakini kumbe ana mimba, ….na mimba yenyewe ni yam zee…ina maana huyo mzee ni tajiri sana?’ akauliza.

‘Kwani akiwa tajiri, uzee unabadilika,….aibu ya ipo pale pale, ukumbuke binti yangu bado mdogo …na alistahili apate mume,..aolewe..lakini sasa imekuwa hivyo, hata sijui uso wangu nitauweka wapi….’akatulia.

Mume wake ambaye alikuwa akipanga viu tayari kwa kuondoka, alanza kuvirejesha vile vitu kama ilivyokuwa awali, akaenda kwenye kiti na kukaa,….akiwa anaangalia barabarani, akisubiri wateja wa biashara yao….

‘Kwahiyo sasa unasemaje mume wangu, maana naona mpango wa kwenda huko umebadilika ..siulikuwa umejiandaa tuondoke, au?....’ akamuuliza na kabla mumewe hajasema kitu, yeye akamalizia na kusema; 

‘Mbona unaonekana huna mpango wa kuondoka tena, wewe ni baba na mimi ni mama wa binti yetu, huoni tusipochukua hatua tutakuwa sio wazazi, au nimekosea..?’ akauliza mama Maua.

‘Nimewaza sana, nimeona kweli hayo,…..yatanisumbua sana, na mimi nahitaji kutuliza kichwa changu kwa ajili ya biashara yetu, wewe endelea na hilo tatizo, mimi niache niendelee na biashara, maana tusije tukakosa kote’akasema.

‘Umebadilika kwa vile umesikia ni mja mzito au ?’ akauliza.

‘Hivi mke wangu,….mtu umeshasema ana mjua aliyempa mimba,…hata kama ni mzee, anastahili kulea mimba yake, haiwezekani sisi tuhangaike wakati muhusika yupo, wewe nenda kamshauri binti yako, aolewe,….asijali kuwa ni mzee….kwani wakati wanakutana hakuliona hilo…’akasema.

‘Sasa hilo linahitajika tuwepo wawili, ..ndio litakuwa na uzito’akasema mama Maua.

‘Hapana,…hilo halinihusu,..nisingelipenda kuingilia mambo hayo….wewe unastahili….unatosha kabisa, nenda,…mimi kazi za huku niachie…na kama mzee ni tajiri, basi, hakijaaharibika kitu, …mfundishe jinsi gani ya kumchuna buzi…..’akasema na kutabasamu, kama vile anacheka.

‘Ina maana leo anakuwa bintu yangu..hakuhusu, ukumbuke kama singelikuwa yeye, tusingelijenga hiyo nyumba,…..na hiyo ni nyumba yake, kwani katia kila kitu…..kumbuka hilo’akasema mama.

‘Eti nini….sitaki kusikia upuuzi, huo, …yeye kasaidia , lakini sio kwamba nyumba nii yake…hata asingelisadia ningejenga …..usitake tuanze kuchafuana sasa hivi,…wewe nenda, …..naona ukiendelea kuwepo hapa hali ya hewa itachafuka….mimi nitaendelea na shughuli, ….

'Na hata kama mtakuwa hamjamalizana, mimi nitatangulia huko nyumbani, wewe kaa na binti yako, hakikisha kuwa huyo mzee, anamuoa…alee mimba yake, na mtoto wake…usije ukalogwa ukamchukua huyo binti, unajua adha ya kulea mtu mwenye mimba…na wakati mume wake yupo…..hakikisha huyo mzee analea mimba yake’akasema huku akiwa kakunja uso.

‘Imekuwa hayo sasa….nilijua tu,…maana huna uchungu naye, tangia mwanzoni ulikuwa humpendi, ulikuja kumpenda tu, pale alipotusadia kujenga hiyo nyumba, ..hapo ukamuona wa maana, na kila mara unatamba kuwa una binti…sasa imebadilika, huna mapenzi naye tena, …..’akasema mama Maua.

‘Hayo yote ya nini…….nenda, ….naona unapoteza muda, ,,,,,,’akasema huku akigeukia sehemu nyingine.

‘Wanaume..mnanishanagza sana, yaani unaona mapenzi kwa mtoto pale tu anapokusaidia, lakini akiwa na shida, huna mapenzi naye, ni sawa, utakuwaje an mapezi naye wakati hujui machungu ya uzazai,…kwako ni kutamba tu pale akiwa na raha,..lakini sio kwa shida, sawa……’akasema Mama Maua huku akindoka.

‘Wewe nenda bwana….nitaleaje mtoto, wakati mwenyewe yupo, starehe zao ndio ziniumize mimi, kama angelikuwa kafa,..hapo ningelisema, lakini mtu yupo, na huenda ni tajiri..hapana, sikubali, na asikanyage nyumbani kwangu,..labda akija awe anakuja na mumewe, ..na huyo mume wake, aje na mahari, na faini juu,..nitawapokea, vinginenvyo….simtaki, na wala simtambui..’akasema

‘Sawa, najua hilo,…lakini mimi ni binti yangu, …..ikibidi nitakuja naye, kwani nyumba kajenga kwa pesa yake….’akasema huku akiondoka.

‘Thubutu….kama unataka kuniona mbaya, wewe mlete huyo mwanao, nakuhakikishia kuwa mtaondoka wote….’akasema huku akipiga ngumi kwenye meza.

‘Tutaona, labda kama sio mwanangu aliyejenga hiyo nyumba….’akasema mama Maua, lakini hakusikia nini mume wake alichoongea, ….

*********

Tajiri, alikwenda moja kwa moja mkuu wa kituo, alichukua muda mrefu kuongea na kujaribi kumshawishi, lakini haikufanikiwa, kwani yule mkuu, alimwambia yeye keshakabidhi madakara kwa mwenzake, kwahiyo kama anataka kuongea na mwenye mamlaka aende akamuone huyo mkuu mpya wa kituo.

Tajiri hakukata tamaa, akamwendea mkuu mpya wa kituo, na alipofika, alimkuta akiwa kwenye kikao na watendaji wake, akajitambulisha;

‘Ohoo, safi sana umejileta mwenyewe,…tulikuwa na mpango wa kukukamata ,kwasababu kubwa, kwanza wewe ni shahidi muhimu sana katika kesi yetu hii, na kwa vile hili kundi linakufahamu kwa hilo, wanataka kukuua…..hiyo tuna ushahidi nayo’akasema huyo mkuu.

‘Hakuna mtu wa kuniua mkuu, ….usiwe na shaka na mimi’akajitetea Tajiri.

‘Ndugu mpendwa, sisi sio watoto wadogo, hii kazi nimeianza muda mrefu, na nawajua sana hawa watu wa namna hii, hawa watu wanaoendesha hii biashara, hawajali maisha ya watu, ….kama mtu fulani ni kikwazo, hawasiti kumtoa roho….wana mbinu nyingi sana, hatuwezi kufanya makosa, na sitaki kupoteza mtu muhimu kwenye kesi hii….wewe ni mtu muhimu kwangu…..hutaondoka hapa leo’akasema mkuu wa kituo.

‘Haiwezekani, ujue mzee wangi ni mgonjwa, na….mambo yote yananitegemea mimi….’akajitetea.

‘Hilo tumelifikiria, na ….pale kwa mzee wako tumeshaweka walinzi, ….hata hivyo, familia yam zee imesharudi,watoto wake wamesharudi jana, walifikia hotelini, na tumeonag nao, wamesema watakuwa karibu na mzazi wao kuanzia sasa’akasema huyo mkuu.

‘Oooh, sasa unaona,…..’akajikuta akisema, na akili ikawa kama imepigwa na mshituko,….akawaza mengi, kwani alijua kuwa kwasasa hatakuwa na usemi, wowote kwenye familia, na kuna mengi alistahili kuyafanya kabla hiyo familia haijarudi, akasikia sauti ya Malikia ikisema akilini mwake;

‘Nakuambia ukweli….nenda kaonane na huyo mkuu sasa hivi….unanisikia lakini….ukumbuke, nina mambo yako mengi, mabaya yako ni mengi…, ambayo familia ya huyo mzee, wakiyaona, watahakikisha unakwenda jela, au unakufa, na hutaweza kurithi chochote kwenye hiyo familia,….nilitaka kumuonyesha mzee wako siku mbili zilizopita baada ya kusikia kuwa unataka kunisaliti, lakini, nikaona haina haja,…muda wake utafika tu, na….kama usiponitoa hapa,…hilo litafanyika…..

‘Kwakweli mkuu, mimi niacheni, nikaweke mambo yangu safi,…halafu nitakuja mwenyewe…’akasema huku moyoni akiwaza mengi, na alifikia kuwazia kufanya lolote, ilimradi huyo Malikia asije akakutana na familia ya mzee, kwani anaweza akaongea kila kitu.

'Ikibidi ni lazima nimuwahi .....ikibidi,....kama anavyowafanyia wengine, na yeye nimfanyie hivyo hivyo,...nimzibe mdomo,....nitaweza kufanya hilo, ila kwa vipi....'akawa anawaza akilini, na mkuu alikuwa akiendelea kuongea, japokuwa yeye hakuwa akimsikiliza kwa makini.

‘Huwezi kutoka humu, ….kuna mtu amekuwa akikufautailia nyuma, hadi unafika humu, yupo nyuma yako, lengo na nia yao ni kuona unafanya nini….Malkia kakutuma umtafutie dhamana, …..na nia yake, umdhamini, na hilo kama lingefanikiwa, ….wewe ndiye utakayekuwa wa kwanza kuiaga dunia…..kwahiyo hapa hutoki kwa usalama wako..kama kuan kitu cha kufuatilia, toa maagizo,…..kuna vijana watakwenda kufuatili, kwasasa hivi upo chini ya ulinzi’akaambiwa

‘Mchukueni huyu mkamuweke sehemu inayostahili, hakikisheni usalama wa eneo hilo,…na yule jamaa aliyekuwa akimfuatilia, hakikisheni mnamkamata mara moja,…kazi imeanza’akasema huyo mkuu, na Tajiri akachukuliwa na kupelekwa sehemu isiyojulikana.

Huku nyuma mzee akazindukana, na alijikuta akiwa kazungukwa na mabinti zake, waliotoka huko Ulaya, hakuamini macho yake;

‘Hivi naota au ni kweli?’ akauliza.

‘Unaota baba…..lakini ndoto ya ukweli…baba sis tumerudi, na lengo letu kubwa ni kuwa pamoja na wewe….na ikibidi tunahitajia mama arudi,….hilo halina mjadala kwa sasa, kama unatuhitajai watoto wako, basi tunahitaji mama awepo hapa, ….tunataka familia yetu iwe kitu kimoja’akasema mmoja wa mabinti zake.
‘Mbona mnapeleka mambo hayo kwa pupa, hivi mnamfahamu mama yenu …mimi ni baba yenu, nimeishi na mama yenu, namfahamu ilivyo, maisha yangu na mama yenu yalikuwa ni mateso makubwa,, hadi nikafikia kupatwa na maardhi haya, hamuoni kuwa akirudi hapa, atakuja kunimaliza?’ akasema.

‘Baba sis tumekaa na mama, tumehakikisha kuwa tabia zake za zamani, zimekwisha, tulimtafutia mtu, mtaalamu wa saikolojia, akawa anamfunza, ….kwasababu baba, mambo mengine, yanatokea, lakini hatutaki kuangalia chanzo chake…..mengine ni ugonjwa wa kiakili, sio lazima uumwe kihivyo....'akasema akionyeshea mkono mwilini.

'Sio lazima uumwe..., kama wewe hivyo, hapana kuna magonjwa mengine yanatokana na msongo, yanatokana na historia,mengine kukosa elimu ya kimaisha , na hata ya kindoa. Mtu huyo ambaye amekaa na mama kwa wiki sasa, amegundua kuwa mama alikuwa hana msingi mzuri wa kimaisha, ….huko alikotoka, kwahiyo mlioana, akawa anaishi kutegemeana na mazingira ….’akasema huyo mwanadada.

‘Kama upo tayari tutafanya mpango mrudiane, na kama haupo tayari, …basi hebu tuambie ni nini malengo yako, maana tunavyokujua hutaweza kuishi peke yako bila mtu wa karibu na mtu wa karibu kwako ni mke…sisi watoto tupo, lakini kuna mambo hatutaweza kukufanyia kama huna mke,….’akasema binti yake mwingine.

‘Wewe sasa umeongea la maana, mimi nilikuwa na mpango….sawa mama yenu anaweza akarudi, akaishi hapa,lakini sizani kama nitakuwa na raja naye tena,….moyo wangu kwake, umeshaingia kutu,..aliyonifanyia ni makubwa sana, hata yeye mwenyewe anayajua….sitaweza kulala naye kitanda  kimoja…’akasema na kuangalia saa yake.

‘Kwahiyo unakubalia aje akae hapa, kama mke , ….mbona sielewi?’ akaulizabint mwingine.

‘Nyie sio ndio mnashindikiza kuwa arudi hapa, sawa arudi, lakini….nina imani hiyo kuwa hatuwaweza kuivana, na kumtaji huo, nahitajia kutimiza malengo yangu mengine’akasema baba

‘Kama yapi baba, kwa umri kama huo unataka kusema upo tayari kuoa mke mwingine?’ akaulizwa.

‘Umri sio tatizo,..tatizo ni amani ya moyoni, …na hiyo sitaweza kuipata kwa mama yenu kamwe, namfahau ilivyo, ..hata kama mtamtafutia dakitari gani, tabia yake haitaweza kubadilika,…..namfahamu ilivyo, nimekaa naye miaka mingi, nimejaribu kila njia, ….lakini hakuweza , na hata weza kubadilika’akasema baba.

Wale mabinti wakasogea pembeni na kuanza kuteta kwa suti ndogo na baba yao akawaangalia mara moja , halafu akageuka kuangalia dirishani, akionekana kuwaza jambo. Baadaye wale mabinti walimsogelea wakasema;

‘Kwahiyo baba…eeh, unasemaje….maana sisi ni watoto, na safari hii tumeamua kurejea nyumbani, na kuanza maisha mengine mapya….tunahitaji kuijenga familia yetu kwa pamoja, na kuendeleza shughuli zako,na ili tufanikiwe hilo tunahitaji ushirikiano wako….sisi baba tunakuhitajai sana, elimu tuliyopata tunataak tuitumie kwetu, kwako na kwa familia yetu, na taifa letu…’akasema binti.

‘Safi sana….kwa hilo tupo pamoja, kwani kuna mengi yametokea hapa, ….’akasema

‘Tumeshayasikia, na polisi wanafuatilia, na sisi tumewaambia polisi tutashirikiana nao, na kila anayehusika afikishwe kwenue vyombo vya sheria…..na hata huyo mjomba wako, ambaye tumegundua kuwa ni kigeu geu, anatafutwa kama almasi….na akionekana anaweza akuwawa….’akasema binti.

‘Haiwezekani….’akasema na kuinuka, …

‘Sasa baba unataka kufanya nini?’ akauliza binti.

‘Lazima polisi wamlinde, yule ni mtu muhimu sana katika familia yetu….anahitajika sana….huyo ni ndugu yenu, mnatakiwa muwe pamoja naye, ….ana mengi anayajua, ….hilo nawaambieni wazi, msije mkamtenga…huyo ni ndugiu yenu, kwa kila hali….’akasema.

‘Kama anahusika na uhalifu, ….kwkweli baba sisi hatutamkumbatia…acha sheria ichukue mkodno wake, na kama anahusika na lolote, baya, ….kwani kwa inaaminika kuwa alikuwa akitumiwa na yule mwanamke….kama sisi familia tutaligundua hilo, hatutamvumilia,…baba hilo tuachie wenyewe, kaam ni ndugu yetu , haina shida, lakini awe msafi’akasema binti.

Mzee akasimama, na akatizama saa yake, halafu akarudi kukaa, alikuwa akionyesha kutingwa na jambo, na wale mainti zake ambao wameamua kuwa akribu na baba yao, wakaona ni lazima wamsadie baba yao, …

‘Baba kuna kitu unahitaji…..tuambie baba kila kitu, sisi tuna hitajia uwe na afya njema, ….kama unahitajai jambo, tuambie’akasema na kabla hajamaliza mlango ukagongwa, na baba akainuka na kusema;

‘Ndio huyo, nataka niongee naye, na nikimaliza kukubaliana naye, nitamtambulisha kwenu rasmi.

‘Ni nani baba?’ akauliza.

‘Nitawaambia baadaye, …kwasababu ni muhimu sana kwangu, nahitajia amani ya moyo, nitulie, na tutulie kama familia, huyo ni dawa ya moyo wangu,….yeye ndiye aliyenitibia,…. yeye ndiye aliyeniokoa, kama isingelikuwa yeye, muda kama huu mngelikuwa mnanifikiria tu, je ….mtu kama huyo si muhimu sana katika maisha?’ akauliza.

‘Huyo ni muhimu, …..ni yule dakitari wako nini?’ akauliza binti.

‘Ni zaidi ya hayo….mtakuja kumuona, …na naombeni hilo mniachie mimi, ….na hamtalijutia,…naomba mnisaidia tulifanikishe, kama mnanipenda mimi baba yenu, na mnataka niwe na afya njema’akasema

‘Tupo pamoja baba..na tutafurahia sana kama utakuwa hivyo, tunajua kwa hali kama hiyo huenda ukampa mama nafasi nyingine katika maisha yako’akasema huyo binti, na alishangaa pale alipotaja mama yake, kwani mzee,alikunja uso, na kugeuka kuelekea mlangoni.

Mzee, alifungua mlango, na mara wakasikia akiguna na kusema;

‘Oh mama, umekuja….karibu sana, …..

‘Nimekuja kumchukua binti yangu…nataka niondoke naye’sauti ikasikika toka nje.

‘Hayo tutaongea mama….tulia mambo ya heri hayataki haraka….’akasema

‘Hayo sio ya heri, ….kama wewe ni mzazi kweli na unapenda watoto wa wenzako kama wa kwako, usingelifanya hayo, uliyoyafanya…..nakuomba kabla sijachukua hatua, unipe binti yangu niondoke naye, sina haja na chochote kutoka kwako…’sauti, ikasikika, na mmoja wa mabinti, akaona aingilie kati, kwani aliogopa baba yake asije akaingia kwenye msongo , na kuhatarisha afya yake.

‘Kwani wewe ni nani,…na kuna nini kinaendelea?’ akauliza pale alipofika mlangoni na kumuona huyo mama akiwa kasimama.

‘Muulizeni huyu mzee, kwani nyie ni akina nani?’ akauliza yule mama

‘Sisi ni watoto wa huyu baba….huyu ni baba yetu, …..tulikuwa nje, ndio tumerudi karibuni’akasema huyo mama.

‘Afadhali mumerudi huenda mtaweza kumtuliza baba yenu, maana makamo kama hayo, anafanya mambo ya aibu…na mimi kama mzazi sitavumilia,... sitakubaliana nalo,…hata kama...imefikia hatua hiyo’akataka kuongea na mzee akasema kwa haraka.

‘Mama hayo mambo yanatushudu wawili kwanza, usimwange mtama kwenye kuku wengi, tuongee kwanza wawili, halafu, muda ukifika nitajua mwenyewe jinsi gani ya kuongea na familia yangu’akasema mzee, na kabla hajamaliza mlango wa nje ukagongwa,….

‘Kuna watu wanaginga huko nje…’

‘Waingie, ni akina nani hao?’ akauliza baba.

‘Ni Maua na mama yake mdogo….’sauti ikasema

Mzee akatoka kwa haraka kwenda kuwafungulia mwenyewe, na kuwaacha mama Maua na wale mabinti wakiduwaa.

‘Inaonekana ni mtu muhimu sana kwa baba..’akasema mmoja wa mabinti.

‘Angekuwa muhimu asingelimpa uja uzito binti yangu’akasema mama.

‘Eti nini, uja uzito, haiwezekani mama,…baba yetu hawezi kuzaa tena, alishafungwa uzazi kutokana na matatizo ya kiafya…’akasema binti mmoja.

‘Oh, ….kwahiyo…..’mama akabakia akiwa kashika mdomo.

NB: Hatuzunguki, bali ndivyo ilivyokuwa na tunataka iwe kama ilivyokuwa, ni kisa kilichotokea na sisi hatutaficha kitu.

WAZO LA LEO: Tusipende kuzarauliana, na kuwahukumu wengine kuwa hawajui, au wanajua, kuwa ni wabaya au ni wazuri kutokana na maongezi, au kusikia tu. Watu hotofautiana katika tabia, kufikiri, kujieleza, na hali za kimaisha, huwezi ukatoa uamuzi wa moja kwa moja wa kumuhukumu mwingine, kwani anayemjua vyema huyo  mwanadamu ni mungu peke yake.


Ni mimi: emu-three

8 comments :

Rachel Siwa said...

Mmmhh Ndugu wa mimi weweni kiboko..kazi nzuri sana sana..Pia Asante kwa Wazo La Leo;ni Kweli tupu..MUNGU azidi kubariki kazi za Mikono yako..

Pamoja Sana sana Ndugu wa Mimi.

Yasinta Ngonyani said...

Hapa patamu kwa kweli...nimependa wazo la leo maana kuna wengi sana wanapenda sana kumlaumu mtu bila kujua chanzo chenyewe...kazi nzuru sana ndugu yangu..pamoja daima

Anonymous said...

That is a really good tip especially to those fresh to the blogosphere.
Simple but very accurate information… Thanks for sharing this one.
A must read article!

Also visit my web page :: online casino bonus

Anonymous said...

I am now not sure the place you are getting your info, but great topic.
I needs to spend a while learning much more or understanding more.
Thank you for magnificent information I was looking for this information for my mission.


Also visit my web page ... Online Playing Nevada - New Jersey.
my website :: Online Casino

Anonymous said...

lovely jubbly fantastic thanks so much

Also visit my web site payday loans

Anonymous said...

lovely jubbly fantastic thanks so much

Also visit my page: payday loans

Anonymous said...

lovely jubbly fantastic thanks so much

Feel free to surf to my page :: payday loans

Anonymous said...

lovely jubbly fantastic thanks so much

Also visit my web-site: cash loans