Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, February 26, 2013

Uchungu wa Mwana Aujuaye ni Mzazi-65




‘Wote mpo chini ya ulinzi…’sauti kali ikasema na mara wakaingia askari watatu,..na baadaye akaingia docta, ambaye hakusubiri, alifululiza moja kwa moja hado pale alipolala yule mzee.

Sauti hii iliwashitua wote waliokuwepo humo ndani, na ilikuwa kama imewaziba mdomo kwa muda, na kuwashikilia viungo vyao na kuwa kama vile wamegandishwa. Ilionekana kila mmoja kichwani mwake, alikuwa akiwazia kosa lake,….na hata kutafuta njia ya kujitetea.

‘Kwa kosa gani….?’ Akauliza Malikia huku akijifanya anajiamini lakini moyoni alishashikwa na mshituka, hakutarajia kabisa kuwa hawo watu wangelifika hapo, na hata kama wangelifika, alijua ni baadaye sana.

Mara mlangoni akaingia askari mwingine ambaye alionekana ana cheo kikubwa kuliko wale askari wengine waliokuwepo mle ndani, akaingia kwa mwendo wa mikogo, hadi akafika mbele ya wale askari wengine, hakuwa na haraka ya kuongea, akasimama na kumwangalia Malikia moja kwa moja usoni.

‘Malikia,…..mmh, Malikia wa Mererani…natumai unanikumbuka..’akasema yule askari, na Malikia, akiwa anajifanya hajali akamwangalia mara moja, na kutembea hatua mbili pembeni, kama vile anakwepa kuangaliana moja kwa moja na yule askari, akasema;

‘Haina haja ya kukumbuka, kwani una tofauti gani na hawo askarii wengine, mimi ninachotaka kujua ni kwanini mnaingia kwenye majumba ya watu,…bila nidhamu na kuanza kuwatishia maisha yao,…..hivi ndivyo polisi wanavyotakiwa kufanya?’ akageuka na kumwangalia yule askari, ambaye alikuwa bado anamwangalia.

‘Nidhamu gani unahitajia Malikia,….hatukupiga hodi,…..na kwa hali ilivyo humu ndani, baada ya kupiga odi mara tatu bila jibu, tuliona ni wajibu wetu kufungua mlango na kuona ni nini kimetokea, na ukumbuke tulikuwa na dakitari, ambaye alishapigiwa simu kuwa mzee anaumwa, je ulihitaji tukae hapo nje hadi muda gani…..?’ akauliza yule askari.

‘Sawa, kaam ni swala la dakitari, ….angelitakiwa aingie yeye peke yake, lakini mlichofanya nyie, ni kutangulia na silaha zenu na mapingu mkononi, kama vile hapa kuna mhalafu,…..’akasema.

‘Halafu?’ akauliza huyo askari

‘Halafu nini…..uoni mlovyofanya,…docta alikuwa wa tatu kuingia, …na hawo askari wao bila kuuliza nini kimetokea , wanatuweka cini ya ulinzi, kwa kosa gani…hauoni tupo kwenye majonzi, badala ya kuleta ubinadamu, mnaleta ubabe wenu , haya tuambieni …kosa letu ni nini hadi tunawekwa cini ya ulinzi katika ali kama hii…?’ akauliza Malikia.

Inspecta wa polisi akageuza kichwa kuangalia kule kilipokuwepo sofa ambapo yule mzee alikuwa kalala, na kwa haraka akageuka kuwaangalia askari wake, halafu akamgeukia Malikia akasema;

‘Kwa hali ilivyo hapa , hatuwezi kuongea, maana dakitari yupo kazini, anahitaji muda, anahitajia utulivu,….nyie wote humu ndani kama mlivyoamuriwa mpo cini ya ulinzi, ….’akasema huyo askari.

‘Kwa kosa gani?’ aliyeuliza sasa hivi alikuwa ni Tajiri.

‘Kwa makosa mengi, kwanza, kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya,….kuua, …udanganyifu, blackmail, ubakaji…na mengine mtayajulia huko mahakamani, lakini kwa hivi sasa mpo chini ya ulinzi mnahitajika kituoni, …..’akasema na kuwaangalia maaskari wake.

Wakili, aliyekuwa kimiya, akamgeukiwa Tajiri, na pale pale akafungua mkoba wake na kuanza kuweka baadhi ya nyaraka zake, ambazo alikuwa kazitoa awali wakati akiongea na Malikia, na yule Inspekta akawa anamwangalia.

‘Kila kitu kilichopo humu ni ushahidi ….rudini nyuma hatua tatu,…..’akaamrisha, na wakili aliposikia hivyo, akalifunga ule mkoba wake, na kuushikilia vyema mkononi, hakujali hiyo amri.

‘Muheshimiwa wakili, natuma umenisikia….weka huo mkoba wko hapo mezani, na rudi nyuma hatua mbili’akasema huyo askari.

Yule wakili akarudi nyuma hatua mbili akiwa kashikilia mkoba wake. Inspekta akamwangalia mmoja wa askari wake, ambaye alipoona hiyo ishara , alikuwa mbele ya yule wakili, na kumuonyesha huyo wakili aweke mkoba wake mbele yake.

‘Huu ni mkoba wangu una nyaraka za kazi, zangu, kuna nyaraka za wateja wangu,….siwezi kumpa yoyote, kwa vile ni ukiukwaji wa haki za wateja wangu…’akasema.

‘Tunakibali kinachoturuhusu kufanya hivyo….’akasema huyo inspekta na kuonyesha kibali ambacho kilimtaka kuchukua hizo nyaraka, ….kama ushahidi.

‘Siwezi hata kama mna kibali hicho, kwanza kwa kosa gani, pili, …..mimi ni wakili, na sheria zinanitambua kwa hilo,..tatu mnanivunjia heshima yangu kama wakili, kwani mimi ningeliweza kufika huko kituoni bila kutumia njia kama hii, kama mnaniona nina hatia, au wateja wangu wana hatia’akasema.

‘Sasa hivi wewe na wenzako wote hapa, ni washukiwa wa uhalifu, na kwa hiyo unahitajika kituoni, wewe na wenzako, ….kama wewe ni wakili, sawa, utafanya kai hiyo yako kwa ajili ya wenzako na wewe utafute wakili wa kukutetea kwa makosa yako, kama itaklubalika kufanya hivyo,….’akasema huyo askari.

‘Sijakuelewa vyema, ….ina maana na mimi mihalifu?’ akauliza.

‘Wewe ni wakili, na umesikia vyema kauli yangu, kuwa wote humu ndani mpo chini ya ulinzi, mengine yote mtayajulia huko kituo cha polisi, kwa makosa niliyowatajia awali…tuna ushahidi na hayo, sio kwamba tumekurupuka tu….muheshimiwa wakili’akasema yule askari.

‘Hata sisi, mbona sisi ni wageni tu’akalalamika mama mdogo.

‘Hayo yote utajielezea huko mbele, haya vijana wangu fanyeni kazi yenu….’akatoa amri, na kila mmoja wa wale askari aliyeingia hapo akawa anafanya kazi, yake,…kuchukua picha, kuandikisha kile kitu walichokihitajia, na kila mmoja alitakiwa kuandikisha kile kilichokuwa chake na kuweka sahihi yake, ….

‘Haya twendeni kituoni….’akasema huyo askari,

‘Kwa vile kuwepo kwetu humu ndani kunaweza kusababisha docta ashindwe kufanya kazi yake. Wakili akawa wa kwanza kuongoza njia, na akafuatia Malikia, na baadaye Tajiri, na wa mwisho kutoka alikuwa malikia, ambaye kabla hajatoka alipofika mlangoni aligeuza kichwa na kuangalia kule alipokuwepo Docta akiwa na yule mzee.

Docta alikuwa kainama, akipima mapigo ya moyo ya yule mzee kwa chombo chake, na yule mzee, alikuwa kageuza shingo akiangalia mlangoni.

‘Oh, kweli, hajafa…’akasema na mlango ukawa umeshajifunga.

********
Docta alibakiwa akiwa kashikwa na butwaa, kwani kwa taarifa alizopata, yeye alijua kuwa anakuja kuhakikisha kuwa huyo mzee keshakata roho, lakini cha ajabu….

‘Wameshaondoka…’alishituka na kuachia kile kipimo alichokuwa akikiweka vyema masikioni ili kujua mapigo ya huyo mzee, akainuka na akajikuta wakiangaliana na huyo mzee.

‘Oh, maajabu, ina maana….?’ Akauliza.

‘Nimefufuka, …na docta, nimegundua dawa,…hii ni dawa halisi, haina migogoro wala shaka, haihitajii kunywa au kumeza, ni dawa ya asili, aliyotupa mungu . Unajua mapaka sasa siamini, unaniona docta nipo mzima kabisa…’akasema na kuinuka kitandani, japokuwa alikuwa anayumba, lakini aliweza kusimama, na kuruka ruka.

‘Unaona docta, nipo fiti….chuma cha Mjerumani, unafanya mchezo nini, …ni dawa isiyo na longo longo’akasema huku akitembea huku na kule.

‘Sasa sikiliza, mimi ni docta, na inabidi ufuate masharti yangu, kama unajiskia vyema sawa, lakini nahitajika nikuangalie, na kukuchunguza, ili niwe na uhakika na hilo, rudi hapa kwenye kiti chako cha ezni nimalize kazi yangu.

‘Ina maana huamini docta, ….haya endelea na vipimo vyako, utathibitisha mwenyewe kuwa mimi ni mzima, …’akarudi pale kwenye sofa lake na kulala, na docta akaendelea na vipimo vyake, na alipomaliza akarudisha vifaa vyake kwenye mkoba wake na kukaa kwenye kiti kilichokuwa pembeni na hilo sofa.

‘Hebu niambie ilikuwaje, ina maana ulikuwa unaigiza kuwa ….upo taabani ….au uliigiza kuwa umekufa, maana watu wote walifahamu kuwa umeshakata roho…?’ akauliza huyo docta kwa mzaha. Mara nyingi hawa wazee wanajuana, na wakikutana katika hali ya kawaida wanaishia kutaniana.

‘Ndio maana nataka uweke hilo kwenye kumbukumbu zako za udakitari, ….kwanza nikuulize, hivi kweli kuna kitu, ukiwa na shinikizo la damu,….eeeh, hivi kuna kitu kinaweza kikatokea kikafanya hali yako ikarejea bila ya kutumia dawa yoyote?’ akauliza.

Yule docta kwanza akamuangalia yule mzee kwa makini, na akilini mwake, alijua kuwa huenda huyo mzee, anafikiria mambo ya kimizimu au imani, akawa hana uhakika na hicho mzee anachokisema…..

‘Inawezekana, ukumbuke shinikizo la damu, huja kutokana na mambo kadhaa, vyakula tunavyokula, mfumo wa maisha,…na ikitokea sababu mfano mshituko, ..mawazo nk…ndio hapo, unapatwa na hayo matatizo,….sasa kama kuna kitu ambacho kimetokea, kuweza ..kwa mfano kuzua mawazo, nk…inawezekana ukajisikia vyema’akasema huyo docta akiwa bado na mashaka kuwa huenda hajajibu swali la huyo mgonjwa wake.

‘Kwahiyo unanishaurije,…maana wewe mwenyewe umethibitisha hilo,….kama kuna kitu kama hicho kinaweza kusaidia, hata kuponyesha,….si vyema kuwa nacho,ikibidi moja kwa moja, …..?’ akawa kama anauliza, na kabla docta hajamjibu akaendelea kusema;

‘Docta… kiukweli, nilikuwa nipo karibu na kukata roho…sio kwamba nilikuwa naigiza, au kusingizia…, shinikizo lilikuwa baya kabisa…na nilikuwa nikihesabu sekunde, …nilishakata tamaa kabisa, nilijua ndio kwaheri….’akatulia huku akijiweka sawa pale alipokuwa kakaa. Na ili kumuonyesha docta kuwa keshapona, akainuka na kuanza kutembea tembea huku na huku.

‘Kwani ilikuwaje?’ akauliza docta akiwa anamwangalia mgonjwa wake, .

‘Ni huyo muhuni, …nimeshawaambia kuwa simtaki aingie hapa kwangu, maana kila akija, anakuwa kama katumwa kuja kuitikisa roho yangu, ili iligee na itoke,…akija hapahana subira, mwanzoni alikuwa binti mzuri, kumbe ni chui aliyevaa ngozi ya kondoo…’akaulia

‘Ni nani huyo unyemzungumzia?’ akauliza docta.

‘Huyo wanayemuita Malikia’akasema huyo mzee, na docta aliona sio vyema kumkumbusha hayo yaliyopita, akataka kubadili mazungumzo lakini yule mzee akaendelea kuongea;

‘Huyo binti nia yake nife arithi mali yangu, ..’ akasema huyo mzee.

‘Kwa vipi arithi mali yako, kwani yeye anastahili vipi kuwa marithi wako?’ akauliza docta.

‘Docta sikuamini niliyoyaona leo, sikujua kuwa nimezungukwa na wauaji, ….unajua docta kwa hivi sasa wewe ndiye naweza kukuamini kuwa ni rafiki mwema kwangu, ….mpaka sasa hainiingii akilini kuwa rafiki yangu wa toka utotoni kumbe ndiye adui wangu mkubwa’akatulia na kushika kidevu.

‘Mzee, naona tusiongee hayo, unajau unahitajika kupumzika,…..’akasema docta, na kwa kusema vile akiwa na wasiwasi na afya ta huyo mzee, akawa kama vile kamwambia huyo mzee aonyeshe kuwa ni mzima au vipi, kwani yule mzee, alisimama na kuanza kuruka ruka.

‘Docta Nipo fiti…..unaniona, usiwe na wasiwasi kabisa, mimi sio docta kama wewe, lakini kwa mwili wangu, najijua vyema kabisa, hali niliyo nayo, sio ya kubahatisha tena, na ili niweze kuendelea hivi hivi nahitajika kuongea, na kutoa hili ninalotaka kukuelezea;….’

‘Ok, endelea, maana hata mimi nina hamu ya kusikia,…’akasema docta, aliogopa kuangalia saa yake, akijua huyo ni mmoja wa wateja wake wakubwa, hatakiwi kuwakirihisha japokuwa alikuwa alihitajika huko hospitalini.

‘Kumbe umzaniye kuwa ndiye rafiki, anaweza kuwa adui wako mkubwa…nimekosana na mke wangu,..nimkosana na familia yangu, kumbe adui yangu yupo karibu yangu, anajifanya rafiki mwema, ananishauri, tena kisheria, kumbe sheria zake ni za kimitego…’akatulia.

‘Ina maana unamzungumzia wakili wako?’ akauliza.

‘Huyo ni nyoka mkubwa…yeye akishirikiana na yule rafiki yangu mwingine…hutaamini, ni watu niliosoma nao, tunatoka kijiji kimoja, wazazi wetu walikuwa kama mtu na kaka yake, leo hii…aah, kweli dunia imekwisha’akatulia.

‘Nilipoambiwa mara ya kwanza, sikukubaliana, na nilifanya uchunguzi wa kina,lakini sikuona huo ubaya wao nikaona kuwa huenda ni mbinu za watu za kutaka kunigombanisha na marafiki zangu, ..na sikuamini hadi leo niliposikia kwa masikio yangu mwenyewe…’akatulia.

‘Nitahakikisha wanalipa….na wataozea jela, yeye anajifanya ni wakili, lakini mimi najua sheria zaidi yake,…sheria nyingine nimezijua kutokana na yeye mwenyewe na pia uzoefu wa kimaisha umenisaidia sana,…nimejifunza mengi, na mengi hayo ni pamoja na sheria,kwahiyo hanibabaishi, …..hizo alizokula zinamtosha, lakini atanirejesha kwa kuozea jela…’akatulia.

‘Yeye kumbe ndiye kiongozi wa kundi lao, yeye akishirikiana na huyo rafiki yangu mwingine na huyo kimwana wao, wanayemuita malikia….wamakuwa wakihadaa watu, wakichukua mapicha mabaya, na kuwatishia watu kuwa wasipolipa pesa wanazohitajia wanawalipua,….pia wamekuwa wakiuza madawa ya kulevya..na hata mimi walitaka kunishirikisha,…lakini uzee ulinisaidia’akatulia.

‘Ulifanyaje…’akasema docta na muda huo akaangalia saa yake, na huyo mzee akatambua kuwa docta anahitajiak sehemu nyingine.

‘Yote hayo utayapata mahakamani, …maana mimi niliamua kushirikiana na vyombo vya dola kuhakikisha kuwa kundi hilo linafikishwa kwenye vyomboo vya sheria, walifikia hatua ya kumrubuni mjomba wangu, ili aje aniibie, ili aniingize kwenye biashara hiyo, ..haramu….lakini nilimweka mjomba wangu kiti moto , nikamuasa hadi tukawa kitu kimoja….akakubali kuwa chambo’akatulia.

‘Kwahiyo yeye hahusiki?’ akaulizwa.

‘Yeye anahusika kama chambo tu….siunawafahamu polisi walivyo, wao wana mbinu nyingi, ……wanasema ili umkamte mwizi , unaweza ukatumia mwizi mwenzao….na kweli wamefanikiwa…utasikia mwenyewe siku kesi hiyo ikifikishwa mahakamani, ….’akasema na kurudi kwenye sofa lake akakaa.

‘Sasa mimi nakwenda,…’docta akamosogelea mzee, akainua mkono wake, na kusikiliza mapigo ya moyo, halafu akatoa kadi yake ya kumbukumbu akaandika, na baadaye, akachukua mkoba wake, akageuka huku na kule..

‘Kile kichupa cha dawa kipo wapi?’ akauliza.

‘Atakuwa kakificha huyo mwanaharamu..’akasema huku akiangalia huku na kule.

‘Oooh, mzee, zile dawa ni muhimu sana, usikae mbali nazo, nilishakuambia ukianza kusikia hali mbaya, meza kidonge kimoja tu….hali yote inakuwa shwari…sasa ooh, hebu niangalie kama nimekuja na akiba’akafungua mkoba wake, na kutoa kichupa kingine kikiwa na vidonge ndani yake.

‘Nilikuwa najua bado unzo, kwahiyo sikuhitajika kuja na dawa nyingine..lakini bahati nzuri kuna kichupa kilikuwepo, sasa hiki weka uchagoni mwako, pale unapokuwa umejipumzisha hakikisha kinakuwa karibu, ungelikuwa na mke, ingelikuwa haina shida….’akasema docta.

‘Sasa docta, nilikuuliza swali, je hii dawa iliyonitibu unaionaje, maana haihitaji hivi vidonge?’ akauliza huyo mzee.

‘Hiyo dawa, ninakushauri, uitumie, …uwe nayo karibu, lakini, imethibitishwa kitaalamu, maana dawa za kienyeji nyingine ni nzuri, lakini huenda zikawa na mdhara makubwa ambayo utakuja kugundua baadaye wakati umeshachelewa, ….nitahitaji kuiona hiyo dawa.

‘Sasa sikiliza,…’akasema na kuinua simu yake, akapiga na kuongea na mtu.

‘Namuomba huyo binti,…eeeh, Maua, aje hapa haraka’akawa anaongea na simu.

‘Lakini sasa mzee, mimi ninaondoka….nitakuja baadaye, kuiona hiyo dawa’akasema huyo dakitari.

‘Sawa wewe ondoka tu, …utakuja kuiona dawa yangu, maana nitafanya kila njia niwe nayo karibu, …docta hii nina uhakika ndiyo dawa ya matatizo yangu, ni ponyo la ugonjwa wangu, mwenyewe umethibitisha, kwani nilikuwa nachungulia kaburi, lakini sasa unanionaje, ….?’ Akawa kama anauliza na docta akawa keshaanza kuondoka na alipofika mlangoni, akageuka na kusema;

‘Kweli hiyo ni dawa …imekusaidia sana, ila hiyo ya kwangu hakikisha unakuwa nayo karibu….ni muhimu sana’akasema docta.

‘Docta, …kama nikiipata hiyo dawa…kitulizo cha moyo wangu, sitahitaji tena hiyo dawa yako….labda….’akasema na docta akatabasamu, hakuelewa huyo mzee ana maana gani akafungua mlango na kuondoka, na nje akakutana na akina mama wawili wakiwa wamesimama wakitaka kuingia ndani.

‘Oooh, jamani naombeni msimsumbue huyo mzee tena…..anahitajika kumpumzika’

‘Lakini kapiga simu akasema anahitaji kumuona binti yangu…’akasema mama mdogo.

‘Sawa, ila msimsumbue….ooh, nimekumbuka na wewe binti niliyekutana naye siku ile, basi kadi yangu bado unayo…likitokea lolote nipigie, ndio wewe uliyenipigia simu eeh, unaitwa nani?’ akauliza.

‘Ndio mimi docta, mimi naitwa Maua, je huyo mzee anaendeleaje?’ akauliza huyo binti huku mama yake mdogo akiwa haamini hayo anayoyasikia, akashindwa kuvumilia, akasema;

‘Ina maana huyo mzee kafufuka, nilikuambia, huyo mzee ni mwanga, utajiri wake….’akasema na kukatisha huku akiziba mdomo wake kwa kiganja  cha mkono.

‘Hajambo kabisa…hutaamini, anadai kapata dawa ambayo ndiyo suluhisho la ugonjwa wake….mzee huyo ana matatizo…mtata kama nini…tatizo lake, anaamini sana dawa za asili’akasema huku akipanda gari lake na kuanza kuondoka, alipotoka nje ya geti, akakuta na boda boda ilyosimama ghafla mbele yake, na hapo hapo akatoka mama mmoja ndani ya boda boda hiyo, kwanza akawa anaingalia hiyo nyumba kama anahakikisha kuwa ndio yenyewe.

Ile boda boda ikaondoka, na kabla huyo docta hajaondoa gari lake, yule mama, akalisogelea gari lake na kusimama pembeni, na akawa anagonga kwenye kiyoo, na yule docta akashusha kiyoo, na kusema;

‘Nikusaidie nini mama ….?’ Akauliza huku akionyesha kuwa ana haraka, na hakutaka kupoteza muda mwingine kwani huko hospitalini anahitajika.

‘Samahani ndugu, ….wewe ndiye mwenye hii nyumba? ‘ akauliza huyo mama.

‘Hapana mimi sio mwenye hii nyuma, ila nilifika mara moja, ….ulikuwa unamuhitajia nani?’ akauliza docta, alisahau kulivua koti lake la udakitari, kwa ajili ya haraka.

`Wewe ni Docta, ooh,… samhani, lakini nilikuwa, naomba kuuliza…. nimelekezwa hapa kuwa ninaweza kumpata binti…ni binti yangu,....’akasema huyo mama

‘Binti yako ….?’ Akauliza huyo docta, akionyesha kushangaa, halafu akasema;

‘Anaitwa nani huyo binti yako, maana nyumba hii nijuavyo mimi, kwa sasa hakuna mabinti,…’akatulia kidogo halafu akasema;

‘Ndio wapo wafanyakazi wa kike, lakini ni akina mama sio mabinti, au labda una maana gani ukisema binti, …?’akauliza docta na muda huo alikuwa anataka kuondoka maana alishachelewa.

‘Yeye hakai humu, nafikiri amekuja hapa…sina uhakika kwa vipi, ila nimeelekezwa kuwa ninaweza kumpata humu kwenye nyumba hii,….yupo pamoja na mama mmoja, ni mama yake mdogo….’akasema huyo mama.

‘Huyo binti anaitwa nani?’ akauliza huyo docta, akiwa keshaanza kuliondoa gari lake

‘Anaitwa Maua, mimi ni mama yake mzazi…..’akasema huyo mama.

NB: Ukiona hivyo, ndio lala salama, msitie shaka, kisa kinaishia.

WAZO LA LEO: Tujitahidi kujenga urafiki, lakini pia tuwe makini na marafiki, kwani sio marafiki wote ni wema.
 

Ni mimi: emu-three

4 comments :

Shalom said...

Nimejifunza kitu kutokana na simulizi hii. Hongera sana miram

emuthree said...

Nashukuru sana Shalom kama kuna kitu umejifunza, ...leo nimeandika kila kitu, lakini kuweka hewani imegoma,...naendelea kujaribu, ikiwezekana, tupo pamoja, ikishindikana basi kesho tukijaliwa.

Shalom said...

Jamani naona hii itakuwa kesho.

Anonymous said...

It is the best tіme to mаke sоme plans
fοr the future and іt is time to bе hаpрy.
Ӏ've read this post and if I could I want to suggest you some interesting things or suggestions. Perhaps you could write next articles referring to this article. I want to read even more things about it!

Also visit my page ... casino online reviews