Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, February 18, 2013

Uchungu wa Mwana Ajuaye ni Mzazi-63
Tajiri alikuwa kasimama mlangoni akiangalia nje, na huku akiwaza maneno aliyoambiwa na mjomba wake, na hakuweza kumshauri lolote, kwani hata yeye siku mmoja alishamshauri kuwa atafute mke ambaye wataishi naye, lakini aliona ajabu leo alipoambiwa hilo wazo amejikuta akiliping akilini.

‘Mjomba wangu,….leo nina furaha sana, umenina nimepona na nina nguvu, …hutaamini ni miujiza ya mungu…kaja binti mmoja, ..ooh, nilifurahi sana, …amekuwa ndio ponyo langu, mungu ana miujiza wake, ndio maana kasema tutafute wake, tuoe,..wake tunaowapenda’akasema mjomba.

‘Ina maana mjomba kwa umri huo unataka kuoa…kwanza kwani ulishamuacha mke wako wa kwanza?’akauliza Tajiri.

‘Na wewe tena, unakumbuka mwanzono ulinishauri wewe mwenyewe kuwa ni vyema kwa sasa ili, niweze kuishi kwa amani nitafute mke,….na ukanishauri kuwa mke wangu niliye naye atanitia vidonda vya kichwa hanifai…sasa mbna unanigeuka tena’akasema mjomba mtu.

‘Siku ile tulikuwa tukiongea kimzaha,….wewe kwa ujumla, una mke, na watoto wakubwa, ujue lolote utakalofanya sasa linaweza kukufanya usielewane kabisa na familia yako, hasa watoto wako…’akasema na kumfanya mjomba atulie,

‘Hilo nalijua,..lakini nikosane na familia yangu mara ngapi, hivi sasa naishi kama vile sina mke wala watoto. ..nilitimiza wajibu wangu wa kuwasomesha kwa gharama kubwa, hadi kusoma nje, lakini hakuna hata mmoja aliyenijali….nimeumwa humu ndani, ninewapigia simu, hakuna hata aliyenijali,…..wanasubiri nife waje warithi mali…’akasema kwa uchungu.

‘Wao wamekasirika kwa vile umeachana na mama yao, ukimrudia mama yao watakuwa karibu na wewe, kwahiyo cha muhimu ni kumrudia mama yao, na sio kuoa mke mwingine’akasema Tajiri,

‘Hakuna anayejua ni maisha gani nimeishi na huyo mwanamke…nimevumilia miaka mingapi, sina raha ya ndoa, mke yupo kama vile mtu wa kunifirisi, yeye muda wote ni kutaka pesa, kutumia kustarere..kujirusha,….hivi nyie mnajua ni nini mwanamke huyo amenifanya …..alifikia hata kuniwekea madawa….aah, wala sitaki kumuwazia tena’akasema kwa uchungu.

‘Mjomba hayo ulishaniambia….na kwakeli niliumia sana siku ile uliponihadithia na ndio maana nilifikia hatua ya kukushauri hivyo, lakini ….watoto wako watakuelewa…hilo ni swala la muhimu sana, kabla hujachukua maamuzi mengine’akasema Tajiri.

‘Hebu niambie, unanionaje leo, na siku zilizopita?’ akauliza mjomba akisimama na kutembea kwa madaha.

‘Mjomba..hata siamini…umebadilika, na kuwa na afya,...mpaka najiuliza ni dawa gani umetumia ambazo zimekuponya kwa muda huo mfupi,….’akasema Tajiri akitabasamu kwa furaha.

‘Sasa nikuulize, unataka nirejee kwenye kuumwa au unataka niendelee kuwa na raha, na afya kama hivi….’akauliza huku akiendelea kutembea kwa madaha.

‘Ninataka uwe na afya…na kama ni dawa zitumie vyema, …hizi zinakufaa sana, na nitafurahi nikija an kukuta katika hiyo hali,….kwani nilishafika sehemu ya kukata tamaa, na …’akatulia pale mlango uli[pogingwa.

‘Basi dawa na huyo binti…..kama unahitaji niwe na afya, na nguvu, ujue yote kayafanya huyo binti..’akasema bila kujali ni nani aliyepiga hodi.

‘Binti gani huyo mjomba…..’ilikuwa sauti ambayo ilimfanya mjomba anywee, akakunja uso kwa hasira, akaguka huku na kule, na baadaye akageuka kuangalia kule mlangoni, ..

‘Nani aliyekuambia uingie bila ruhusa yangu, je ungelinikuta nipo uchi….?’ Akauliza mjomba kwa hasira.

‘Nimeingia kwa vile nina uhakika upo sawa, na ninajua mpo kwenye maongezi na mchumba wangu…au nimekosea?’ akasema huyo aliyeingia, na akamsogelea mjomba kama kawaida yake, ya kumkumbatoa mjomba wake, na kuonyesha kweli anamjali,m kumbe akiangalia pembeni anamng’ong’a.

‘Hivi utaacha lini kufanya haya maigizo yako?’ akauliza mjomba na kufamya Malikia kutulia, akasimama na kumwangalia huyo mzee.

‘Vipi mjomba, kwani nimefanya makosa, nafanya haya kwa vile na kujali…nakupenda sana mjomba wangu, nikikuona wewe najiona kama nipo na wazazi wangu, japokuwa wazazi wangu hawanijali kma unavyonijali wewe….’akasema huku akijilazmisha kumkumbatia mjomba wake, na mjomba wake akatulia kama mti.

‘Kama ningelikunywa yale….ungemfanyia nani hivi..au hujui kuwa nimeyafahamu yote kuwa wewe ndiye uliyeweka sumu kwenye maji, sumu ambayo ingeniua taratibu na ionekane nimekufa kwa mshituko, au kwa shinikizo la moyo….’akasema huyo mzee akionyesha uso wa hasira.

‘Mimi hayo siyaelewi, na aliyetunga huo uongo ana lake jambo, kwanini nikuue kwa sumu wakati mwenyewe umeshajifia…..’akasema Malikia akiwa bado anaonyesha uso wa kushangaa.

‘Nani kajifia, utakufa na utaniacha nikiwa hivi hivi…..wewe binti mbona huna shukurani, nimekutendea mema mangapi, ….hivi nini unataka kutoka kwangu,….mali, au utajiri wa namna gani unaouhitaji kutoka kwangu, …nikuambie ukweli hata kama nitakuwa nimekufa,….sitaki kamwe uguse mali yangu,…ukiigusa tu, nitakujia kama mzimu, nitakumaangamiza….’akasema na kumfanya huyu binti arudi nyuma kidogo na kubakia mdomo wazi.

‘Hivi ndio yamekuwa hayo tena…..mzee, kumbe ulikuwa unanichezea shere kuwa unanijali, na kuniona ninafaa kwa kijana wako, ili unitumie kwenye biashara zako eeh, sasa kumbe unataka kupambana na Malikia wa ukweli ehe….sawa, utapambana naye, ….ukumbuke nina siri zako nyingi,..na nilishakuambai siku ukinichoka, ….basi dunia nzima itajua uchafu wako, na nikianzia kwa watoto wako…..’akasema huku akiwa kashikilia kanda ya video hewani.

‘Hilo halinitishi…’ yule mzee akasema na ghafla akashikilia mkono kifuani, na kuanza kuhema kwa shida, na huku akitafuta dawa yake kwenye meza..ikawa haionekani.

‘Dawa yangu ipo wapi…..’akawa anahaha huku na kule kuitafuta dawa yake, na Malikia akawa anamtizama kwa uso uliojaa ukatili, na pale Tajiri alipojaribu kuhangaika huku na kule kuitafuta hiyo dawa ya mzee yeye, hakusogea pale aliposimama, alikuwa akiwatizama kwa macho ya dhihaka.

‘Malika umeichuka dawa ya mzee…?’ akauliza Tajiri, lakini malikia hakusema kitu, alikuwa kakunja uso na sura ya kikatili, ilidhiri machoni mwake…..na hapo Tajiri, akahisi huenda kweli Malikia kaichukua na kuificha,…akageuka kumwangalia Mzee wake akiwa kalala kwenye sofa lake, nguvu zikiwa zinaanza kumuuishia ….

‘Dawa….tafuta dawa yangu…..ooh, ….’akawa analalamika huku akihema kwa shida,….Tajiri, akamsogelea Malikia kwa nia la kumkagua, ili aone huenda hiyo dawa anayo mikononi,..lakini hakuona kitu, yule malikia alikuwa anamwangalia yule mzee anavyopata taabu huku sura ya kiuaji ikiwa imepamba uso wake hapo Tajiri akaamini  kuwa kweli Malikia ndiye aliyekuwa kaweka sumu kwenye maji ya huyo huyo mzee kwa nia ya kumuua

Hapo hapo  akakumbuka siku moja wakati wamejipumzisha na huyo binti , huyo binti aliwahi kumgusia kitu kama hicho,na mazungumzo yake, hakuyachukulia maanani, japokuwa yalimshitua sana…. hakuamini kabisa kuwa binti mrembo kama huyo anaweza kuwa na roho ya kikatili kiasi hicho, na leo imedhihiri machoni mwake, ….akshikkwa na butwaa huku akiyakumbuka yale mazungumzo yao siku hiyo…

*******

‘Tajiri, hivi unaonaje tukiwa na lile jumba la mjomba wako,..tukaishi pale na kulimiliki, na hata kumiliki mali yote ya mjomba wako?’ alikumbuka sauti ya Malikia ikinong’ona sikioni mwake wakiwa wamejipumzisha,

‘Tutamilikije kitu ambacho sio chetu…ukumbuke yule ni mjomba wangu, sio baba yangu, yeye ana familia yake..na ingawaje familia yake haipo hapa kwa sasa, lakini wanatambulikana kisheria kuwa ni watoto wake, na wana haki ya kumiliki hilo jumba na mali yote ya huyo mzee’akasema Tajiri.

‘Sikiliza…., wewe ndiye mtoto wake kwa sasa, ndio maana kakuweka karibu na yeye, na wewe keshakukabidhi madaraka ya kuongoza miradi yake yote….na keshakuandikisha kama mmoja wa watoto wake…kilichokuwa kimebakia ni kukuandikisha kama mrithi wake…na sasa.’akasema huyo malikia na kuinua kichwa kumuangalia moja kwa moja usoni

‘Kwanini unaongea hivyo..mimi sihitaji kuandikishwa kama mrithi, inatosha kwa fadhila alizonifanyia mjomba wangu, kwani sikiutegemea kabisa kuwa angelikuja kuniamini kiasi hiki na kunifanya niwe karibu na yeye hadi kunifanya mtoto wake,….’akasema huku akikwepa kuangaliana moja kwa moja na huyu mwanamke, kwani anajua nini kitafuta baadaye.

‘Mpenzi……yote hayo ni kwa ajili yetu’akasema Malikia akipitisha mikono yake mashavuni kwa Tajiri….

‘Ndio nakushukuru sana kwa juhudi ulizozifanya….lakini siwezi kwenda mbali kiasi hicho cha kudai urithi, wakati watoto wake bado wapo, na wana haki zote za mali ya wazazi wao’akasema Tajiri.

‘Kumbuka nilifanya haya yote, ili uwe karibu na mjomba wako, na hiyo ilikuwa hatua ya kwanza, na hatua ya pili ni kurithishwa mali zote kwako…..kinamna,……na hatua ya tatu ni kumiliki hizo mali, baada ya kinamna kufanya kazi yake…hilo mimi nimelipanga vyema kabisa..na nakumbia hilo, nikiwa na uhakika…’ akaondoa kichwa chake, na kukaa huku kaangalia pembeni na Tajiri akiwa kaangalia pembeni, kila mmoja akiwaza lake.

‘Nina uhakika kuwa wakili wa mzee keshaamriwa kukuandikisha wewe kama mrithi halali wa mali za mjomba wako…kama watoto wake watakaidi amri zake, kama watoto wake watamkana, kwani  wameshasema kuwa hawpo naye tena hadi hapo mama yao atakaporudi na kuwa mke halali wa mjomba wako….’akasema malikia huku kashikilia mikono kifuani, akiwa hamuangalii Tajiri

‘Ni nani kakuambia hayo?’ akauliza Tajiri kwa mshangao, kwani hayo aliongea na mjomba wake, na walipanga kuwa hayo yawe siri kubwa kati yao wawili na watatu wao akiwa wakili, na ana uhakika wakili wao asingeliweza kutoa siri kubwa kama hiyo.

‘Mimi sio mtoto mdogo, nilishakuambia hayo yote yapo kwenye mipangalio yangu,…na usizani hayo yanatokea tu…..mimi nipo nyuma ya kila jambo, na huko kurisishwa mali kwako kusingelitokea hivi hivi kama nisingelifanya mambo yangu ambayo sitaweza kukuambia…sasa wakati umefika, maana naona kuna kiwingi kinakuja….kinachofuata ni hatua ya tatu..ya kumiliki mali…hiyo lazima ifanyike kabla watoto wake hawajashituka….na hicho kiwingu hakijatanda’akasema.

‘Hivi wewe una nini…unataka nini zaidi..mimi hilo sitakubaliana nalo, na hata hivyo, utafanyaje ili umiliki mali ambazo sio zako….na hicho kiwingu ndio nini?’ akauliza kwa mshangao.

‘Sasa hivi mali hizo ni zako sawa si sawa…..hilo neno mali ambazo sio zako, liondoke mdomoni…wewe sasa hivi ndiye una haki zote za mali za huyo mzee…kinachotakiwa tu ni yeye afe, wewe umiliki kila kitu..na hilo ni muhimu lifanyike haraka iwezekanavyo’akasema malikia.

‘Unataka kusema nini?’ akauliza Tajiri kwa mshangao.

‘Hiyo ndio hatua ya tatu…lazima ifanyike…huyo mzee afe sioni haja ya yeye kuendelea kuwa hai, keshakula chmvi nyingi, ni wakati wetu kwa sasa, wewe huoni umri unakwenda, ulistahili kuwa na mke na watoto kwa sasa….na mke wa kuwa nawe nipo, sijahalalishwa, nataak tufunge ndoa, na tuishi kwenye lile jumba….’akasema Malikia akiwa kakunja uso, na kuonyesha uso wa kikatili, na Tajiri hakuamini kuwa mwanamke huyo ana mipango mibaya kama hiyo.

‘Siamini kabisa,…kumbe malengo yako ni mabaya kiasi hicho..siamini’akasema Tajiri.

‘Na bado …hujamjua malikia wa mererani vyema, utamjau pale utakapomiliki hilo jumba, na mali yote ya huyo mzee…lakini ukumbuke kuwa yote hayo ni kwa juhudi zangu, na kwahiyo unatakiwa uwe na mimi katika misha yako yote, vinginevyo….’akasema na kuinuka pale walipokuwa wamekaa kwenye sofa na akasimama kuondoka.

‘Usinitishe kabisa…’akasema Tajiri

‘Ninakuambia sio nakutisha….ukifanya kinyuma, yote hayo utayasahau na utarudi kule ulipotoka kwenye umasikini uliokithiri..na kurudi huko….ni hapo, kama utakuwa hai…’akasema na kugeuka akamkaribia na kumshikashika shika kifuani.

Tajiri akaguka na kulala huku upande , hakutaka kabisa kumuangalia huyo mwanamke, na siku ile  hakuweza kulala kabisa,…

******

Na leo anasikia kuwa Mjomba wake kakoswa koswa kunywa sumu ambayo inasadikiwa ilitegeshwa na huyo mwanamke….japokuwa baadaye mjomba wake, aliamua kutokumchukulia hatua huyo mwanamke, akidai kuwa haina haja, hayo maswala atayamaliza mwenyewe.

Tajiri, alihisi huenda ni kwa vile yeye alishamua kumuoa huyo mwanamke, kwani alishafikia hatua ya kumvisha pete ya uchumba, japokuwa baadaye alishangaa siku moja mjomba wake akimwambia kuwa aachane na huyo mchumba wake kwani keshagundua kuwa hamfai….sio mke mwema kwake.

‘Mjomba kwanini hanifai tena, na wakati mwanzoni wewe mwenyewe ulisema kuwa nimuoa…kwani ana kipaji cha biashara, na anaweza kuishi na sisi bila wasiwasi?’ alikumbuka jinsi alivyomuuliza mjomba wake siku ile

‘Nimegundua kuwa huyo mwanamke ni nyoka….hakufai, achana naye tafuta mke ambaye anastahili, na ataweza kushiririkiana na wewe…..nimefanya uchunguzi wa kina, nimemgundua,….kuwa sio mwanamke, na ana malengo mabaya kwako….na huenda kwangu pia….japokuwa kwangu hataweza …anajihanganisha tu…’akasema mjomba wake.

‘Mjomba unajua sana, kuwa huyo mwanamke nimetoka naye mbali na ….ni mwanamke anayejua mambo ya biashara , kama ulivyoona, kaifufua bishara yako na sasa miradi yako mingi inaendelea vyema, huoni kwa kumpinga, anaweza akaididimiza miradi yetu tena….?’ Akasema

‘Nani kakuambia kuwa yeye ndiye kaifufua miradi yangu…hilo sio kweli, miradi yangu ilififia kwa vile nilikuwa mwenyewe siifuatilii….na nilipoamua kuifuatilia ndio ikaanza kurejea kwenye hali yake, …kwani wakati naupata utajiri wangu wa mwanzo alikuwepo..hakuwepo…kuna mambo mengi yanaanyika ..na nitakuelekeza kidogo kidogo na wewe utajua kila kitu…’akamwambia.

‘Sawa mjomba, lakini mimi bado ninashindwa jinsi ya kumuacha huyo mwanamke, ….japokuwa kiukweli simpendi sana….nimempenda kwa ajili ya ucheshi wake na …..na….’akashindwa kumalizia.

‘Nina fahamu sana…haina haja ya kusema….ninamfahamu sana….ni mjanja, na anajua siri nyingi za wanaume, …..’akasema mjomba wake, huku akikunja uso kwa huzuni.

‘Unamjuaje huyo mwanamke …..?’ akauliza.

‘Hayo yasikuumize kichwa, ukumbuke kuwa wewe sasa ni mwanafunzi wangu, na kama nimeamua kukuweka karibu yangu, na….kwa vile watoto wangu wamenisusa, sioni kwanini usiwe mtoto wangu, nisije nikafa na mali hizi zikaingia kwenye mikono mibaya…..najua wewe unaweza ukazilinda, na ikibidi….utaweza kushirikiana na watoto wangu japokuwa wamedai kuwa hawan haja na mali yangu…’akasema kwa huzuni.

‘Lakini mjomba huoni hiyo sio sahihi, kwa vile una familia, una watoto wakubwa…hawatakuaj kunielewa, na hata jamii, itakuja kuniangalia kwa jicho baya….’akalalamika mjomba mtu.

‘Hilo lisikutie wasiwasi, ninajua nini ninachokifanya,….watoto wangu wamekataa kuwa na mimi, nimewajaribu, mmoja mmoja, hakuna aliyekubali…mali hiii ina masharti yake, sikuipata hivi hivi…na kila niliyemwambia mambo hayo aliniona mtu mbaya sana…hawajui kuwa hata mali walizo nazo huko zimepitia mkondo huo…’akatulia kidogo kama anawaza jambo.

‘Mkondo gani mjomba…..?’ akauliza Tajiri alipoona kuwa mjimba wake katulia.

‘Kwanza jina hilo la Tajiri, ndilo litakuwa jina lako popote, kama nilivyokuelezea awali..lina nyota yake, na imeshafanyiwa kazi,…pili, wewe utakuwa mtu wangu, ambaye nitakupa mikoba yangu….ili uuendeleze utajiri wangu….watoto wangu wote wamekataa…na kama na wewe hutaki basi, nitatafuta mtu mwingine..kaaa ufikiria, na ukiwa tayari utaniambia…’akasema huyo mjomba.

‘Mjomba mimi nipo tayari, …..mimi nahitaji niwe tajiri kama wewe, …kama kuna njia yoyote mimi nipo tayari….’akasema Tajiri kwa furaha na tangu siku hiyo akawa akionyeshwa njia za utajiri huo hatua kwa hatua na masharti yake…hadi akaiva, na kukabidhiwa sehemu ya mikoba.

********

Kumbukumbu hizi zilimjia kichwani…akimukumbuka mjomba wake ambaye alimuamini sana na walishafikia htua ya kushikamana kwenye biashara hadi kufichuliwa siri ya utajiri wa mjomba wake, ….akilini mwake hakukubali kabisa wazo la kumsaliti mjomba wake,… hapo chuki ikamsonga, ..akatamani amshike Malikia na kumtupia nje, lakini isingeliwezekana,…..akainua uso wenye chuki na kumwangalia malikia kwa hasira , na Malikia alikuwa akimwangalia kwa yale macho yake yanayoonyesha ukatili huku akitabasamu kwa zarau…na kwa sauti kama ya kunong’ona akasema;

‘Wakati ndio huu, tukichelewa hapa hatutapata kitu, ….hii ni hatua ya tatu na ya muhimu sana….haitachukua muda atakata roho,…na hatua ya tatu itakuwa imekamilika, …hili jumba na mali yake yote itakuwa mikononi mwetu….’akawa kama ananong’ona lakini aliinua ngumi na kuikunja, kuonyesha ushindi fulani.

‘Wewe ni muuaji, huna maana kwangu…hujui ulisemalo,…ngoja tumuite docta aje …hali ya mzee sio shwari, ’akasema Tajiri kwa sauti ile ile ya kung’onana, na huku akimwangalia mzee wake akihangaika kutafute, hewa, alikuwa akihema kwa shida, huku akiwa kashikilia kifuani…huku akimuonyeshea Tajiri, mezani ambapo huwa anaweka dawa zake…lakini kulikuwa hakuna dawa.

‘Mbona sionu kitu….’akawa analalamika Tajiri huku akihaha huku na kule…..na kila macho yake yalipokutana na ya mzee, alihisi huruma, …..na hata kutamani kulia, …lakini akawa anajitahisi kuizuaia hiyo hali….

Malikia akasogea pale mezani na kuangalia huku na kule,….kama vile anasaidia kutafuta, nia na lengo lake ni kupoteza muda, kwani alikuwa anajua hicho kinachotafutwa hakipo hapo mezani, na muda gani, na Tajiri alipomuona Malika na yeye anahangaika kutafuta, akaingiwa na matumaini, kuwa hatimaye mwenzake naye huruma imemjia wapo pamoja, lakini hicho kichupa chenya vidonge ndani yake hakikupatikana na bado mzee alikuwa kinyosha kidole hapo mezani huku akihangaika kutafuta hewa.

Tajiri hakukata tamaa, ilibidi aangalia kama mtu anayetafuta chembe chembe ya unga, ….lakini alichoona ni gilasi ya maji, yeye akajua kuwa huenda mzee wake anahitaji maji, akasogea na kumimina maji, na wakati anamimina hayo maji, mlango ukagongwa….

‘Nani…wewe, ….ni docta umefika,….. ingia….’ Akasema Tajiri kwa hasira akijua kuwa huenda dakitari keshafika, japokuwa walikuwa hawajampigia simu, kwani Malikia alikuwa kamzuga zuga hadi asikumbuke kumpigia simu huyo dakitari, na sasa ndio anakumbuka…..

Mlango ulipofunguliwa …akaingia wakili…akiwa na mkoba wake…hakuingia moja kwa moja ndani, alisimama pale mlangoni, huku akihakikisha kuwa mlango umejifunga nyuma yake….halafu akainua kichwa kumwangalia Malikia….

Na wakati huo Tajiri alikuwa akihangaika kumnywesha maji mjomba wake, lakini mdomo ulikuwa umeshafunga, meno yameumana…macho yametoka …kuashiria hali nyingine.

Mzee ambaye alishakata tamaa ya uhai, …. akageuza macho kuelekea mlangoni, akijua huenda ni dakitari wake…lakini alishangaa kuwa sio dakitari aliyeingia, aliyeingia alikuwa ni wakili wake….ambaye alikumbuka kuwa alimtuma….lakini aliingia peke yake akakata tamaa…kuwa sasa anakufa, akajaribu kuinua uso ili kumwangalia mjomba…ili sogee ampe maneno ya mwisho.

Mjomba wake au kama anavyojulikana kwa jina la Tajiri, alikuwa akihangaika huku na kule kutafuta dawa, na sasa alikuwa kashikilia simu, huenda akijaribu kumpigia dakitari wake….lakini kwa hali aliyokuwa akijiskia, mzee mzima alisema moyoni, `keshachelewa’….hali aliyo nayo mpaka dakitari afike, roho itakuwa imeshatoka…akahisi izraili anamjongelea….,

NB Tunaendelea kwenye hitimisho:

WAZO LA LEO: Ni bora tukajitahidi kutafuta kwa jasho letu, kuliko kutamani mali za wenzetu,...Tamaa ni mbaya, inaweza kukupeleka pabaya.


Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

Have you ever cоnѕidеred writіng an e-bοoκ or guest аuthoring on other websites?
I have a blоg centered on the same infoгmation уоu dіѕcuss аnd would rеally liκe to have you ѕhare sοme stоries/informatіon.
I knoω my ѵiewers wоulԁ enjoy yοur wοrk.
If уоu're even remotely interested, feel free to shoot me an e mail.

Here is my webpage casinoonlinecasin..

Anonymous said...

This post iѕ pricelеss. Нow
can I finԁ out more?

Feеl fгee to νisit mу ѕite cheat your way thindiet

Mumybrenda! said...

Hi miram mambo vipi mbona unabana hivyo jamani tokea tar 18 ujaweka newpost je kuna tatizo usifanye hivyo wadau tuna teseka come on!

Anonymous said...

Hi there eѵeryone, іt's my first visit at this web page, and article is truly fruitful for me, keep up posting these content.

Look into my homepage - spil dansk

Shalom said...

Jamani mbona hutumalizii umepotea au majukumu yamekulemea haya pole mwaya

emu-three said...

Wapenzi wa blog, nilitingwa na mitihani, ya kimaisha, ndio maana sikuweza kuwepo hewani. Kazi hizi za kujitolea zina changamoto nyingi, lakini nitajitahidi tukimalize hiki kisa, Mungu atatujalia kwani yupo pamoja nasi,