Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, January 15, 2013

Uchungu wa mwana Aujuaye ni Mzazi-48





Mama Maua alizindukana na sauti ya kilio cha mtoto ilijaa masikioni mwake, na alichofanya na kujaribu kuinuka lengo lake ni kuingia ndani, kwani kwa mawazo ya haraka alijua kuwa mtoto wake yupo ndani, na hicho kilio kinaashiria kuwa anamuhitaji, huenda kakojoa au ana njaa….

Alijikuta akikosa nguvu, akajaribu tena kuinuka, na mara akahisi mkono ukimshika, na akageuka kuangali ule mkono, na mara akamuona mtu wake,. Mtu  wake ambaye yupo naye wakati wote, japokuwa siku nyingine anakuwa haeleweki, lakini siku akiwa na shida, akiwa anaumwa, jamaa huyu yupo karibu naye sana.

‘Kumetokea nini, mbona mwanangu analia,?’ akauliza mama Maua.

‘Ina mana hukumbuki, nakushangaa wewe unaikataa bahati, utapata wapi bahati kama hiyo, wenzako wanaitafuta wewe unajifanya eti siwezi kwenda kuishi porini, haya kaa na mimi , masikini mlevi, ila ukikaa na mimi uvumilie shida zangu’akasema huyo mwanaume.

Mama Maua akatikisa kihwa na kuanza kuwaza, na hapo kumbukumbu zikaanza kumrejea na wakati anawazo yaliyotokea, yule mwanaume akasema;

‘Wamesema baada ya siku saba wanaondoka, kama utabadili mawazo atatumwa mtu kuja kukuhukua wewe na mtoto, upo tayari?’ akauliza yule mwanaume.

‘Sipo tayari…kwanza sitaki hata kuishi hapa naona ni bora tuhame hapa kabisa, sitaweza kuvumilia kuihsi hapa tena’akasema mama Maua.

‘Hilo wazo hata mimi nilikuwa na mpango huo, nadaiwa kama nini, na natafutwa na polisi, bora tuhame hapa au bora nihame hapa, wewe unaweza kuwasubiri hawo watu wako wa porini, wakija mnaondoka nao, huo ni uamzuzi wako.

‘Nimekuambia siwezi kwenda huko, baada ya hayo yaliyotokea sitaweza kuangaliana na wao tena, uso wangu umejaa na haya,…,…na hapo kumbukumbu ya tukio zima ikaanza kumrejea kichwani.

********

Akakumbuka, kuwa walitoka yeye na Malikia kwenda kuwapokea wageni, na walipofikia pale waliposimama wale punda wawili ambao walikuwa wakikokota lile gari la miti lililojengwa na ngozi ya wanyama na kuwa na sehemu nzuri ya kukaa, na viti viwili ambavyo vilitenegenezwa kwa ngozi ya chui,..

Maua alishangaa, jinsi gani lile la miti, jinsi lilivyotengenezwa na kuzungushiwa ngozi za wanyama, na jinsi ngozi hizo zilivyoweza kutengeneza kitu kizuri kama kile, na alijua watu waliopo mle ndani ya lile gari, au chombo kilicchotenezwa na kukukotwa na hawo punda watakuwa ni watu mashuhuri sana…

‘Ina maana yule mwanaume aliyeniokoa atakuwa mtu mkubwa sana serikalini?’ akajiuliza nafsini mwake huku wakisubiri wale watu wawili wateremke,…na macho yake yalikuwa hayababduki kwa yule mtu, ambaye kwa wakati huo alikuwa akimsaidia yule mzee kuteremka kwenye kile chombo.

Yule mtu alikuwa kavalia nguo zile wanazovaa askari wa msituni, lakini nguo zake zilikuwa bora zaidi, na silaha yake ilikuwa begani kwa nyuma, ikining’inia. Huo ndio utamaduni wao, kuwa mwanaume muda wote huwa na silaha, mshale, kisu, fimbo….

Usoni kama kawaida yake mtu huyo, alikuwa kavalia kofia, kofia iliyoziba uso wake, kwahiyo usingeliweza kumuona sura yake. Lakini aliweza kumtambua kuwa ni yule yule mwanaume aliyeweza kumsaidia, na kumuokoa kwenye kifo. Ni yule yule mwanaume japokuwa alikuwa hajui sura yake, lakini moyo wake, ulikuwa ukimuwaza na kuiteka nafsi yake. 

‘Lakini kwanini anajifunika usoni, anaficha kitu gani…?’ akajiuliza na kujiuliza vile , akawa kama anakwazika na hata kuingiwa  na wasiwasi kuwa huenda huyu mtu ana matatizo Fulani usoni, ndio maana hataki kuonyesha uso wake. Na alipowazia hilo akamgeukia malikia, kutaka kumuuliza, lakini kabla hajasema neno malikia akasema;

‘Wageni wapo tayari, ..kiutaratibu, mimi natakiwa niwabariki, baadaye utakuwa huru, kuwasalimia…’akasema malikia na kuwasogelea wale wageni, na wote wawili wakainama, na malikia akawashika, kwanza alianzia kwa mzee wao, na baadaye akafuatia kwa yule mwanaume. Yule mwanaume alitaka kulivua lile kofia alilokuwa kavalia, maana lilifunika kichwa na uso wote, huku likiacha sehemu ndogo ya macho ya puani,na mdomoni, ….

Malikia akaoenekana kama anamzuia yule mtu asivue lile kofia, na akamshika yule mwanaume kichwani akiwa bado kalivalia lile kofia lake. Maua akashangaa, kwanini malikia alimzuia yule mtu asilivue lile kofia, kwani ingelikuwa nafasi yake nzuri ya kumuona huyo mtu. Na kwa ahli ile, alitamani amwambie malikia amruhusu huyo mwanaume alivue hilo kofia.

Wale wanaume wawili, yaani yule mzee na huyo mwanaume,walipomaliza kubarikiwa, wakageuka kuelekea pale aliposimama mama Maua, na mama Maua hakujua afanye nini kwa wakati ule, alibakia akiwa kasimama, na walipomkaribia,, akainamisha kichwa kutoa heshima, na wale wanaume wawili wakafanya hivyo hivyo, na walipomkaribia, wakasimama.

‘Mama Maua hawa ndio wageni wako…kama nilivyokuambia na kukuahidi kuwa nitamleta yule mwanaume aliyekuokoa, na mwanaume mwenyewe ndiye huyo yupo mbele yako akiongozana na mzee wetu, mzee mteule, …..’akasema malikia huku akionyesha kwa mkono pale aliposimama yule mwanaume.

Mama Maua akamwangalia  yule mwanaume huku akionyesha kutahatari, na yale yote aliyojiandaa nayo hakuweza kuyafanya tena, angeliyafanyaje hapo mbele ya watu, na ikizingatiwa kuwa yupo na mzee wa heshima,mzee anayeheshimika sana huko msituni, na hakutajai kuwa mzee huyo naye angelikuwepo kwenye huo msafara…akajikuta akisema;

‘Nashukuru sana, karibuni wageni, nimefurahi kutembelewa na watu muhimu kama nyie, lakini mfalme yupo…..’akasita kusema huku akimtizama yule mwanaume aliyekuwa kavalia kofia, na yule mwanaume akageuka kule alipo mtoto, akaomba mtoto aletwe mbele yake, na yu;e mtoto alipoletwa, akampakata na kumwangalia kwa muda, halafu akamgeukia yule mzee, na kusema;

‘Unamuonaje mtoto huyu?’ Yule mwanaume akamuliza yule mzee huku akimwangalia yule mtoto kwa makini, na yule mzee akamshika yule mtoto kichwani kwa muda huku akiwa kafumba macho, na baadaye akawa anaongea huku kafumba hayo macho, kama vile anaongea tuka usingizini;

‘Nikimwangalia naona nuru, lakini ina madoa ya giza …hii ina ashiria vikwazo, ….mtoto huyu atakulia kwenye matatizo, kama hatutamchukua na kumsafishia njia yake. Mama yake hatamuweza,..atatupwa kwa mbwa mwitu, watu wabaya…. ni bora tuondoke naye, nahisi dunia anayokwenda kuishi haitamtendea haki’akasema huyo mzee.

Baaaye yule mzee akafungua macho yake na kutizama mbele, akayapangusa macho yake kwa kiganja cha mkono, halafu akamwangalia mama Maua, akasema;

‘Mjukuu wangu, hayo niliyosema sio yangu, huwa siku hizi naoteshwa na kuambiwa mengi, …ndio maana nikaamua kuja mwenyewe kukuona,…nafahamu maisha yenu, na nyie mara nyingi mnatuona kuwa sisi tunaoishi msituni bado tunaishi maisha ya gizani, yaliyopitwa na wakati, lakini mjukuu wangu,….maisha yetu yanafaida zake, ….’akatulia kidogo na kumwangalia yule mwanaume aliyevaa kofia.

‘Maisha yenu yana mitihani mingi kuliko ya kwetu, kwasababu nyie mnafuata mambo yaliyoharibiwa na mashine,..sumu nyingi zimewekwa kwenye vyakula vyenu, mnajimaliza wenyewe na mambo ya anasa, ambayo sisi hatuna, sisi tunaishi kiasili zaidi…tunajali asili yetu, hatujikwazi kwa mambo yanayoharibu akili, mwili na uwezo wa kimwili..hutaweza kuelewa hayo, kwa vile akili zenu zimeshatekwa na usasa…huo mnaouita usasa,…’akasema yule mzee na kutulia.

‘Mimi sina uwezo wa kukushawishi zaidi, lakini nakuomba huyu mtoto mruhusu akaishi nasi huko makwetu, ili aondokane na shida ambazo kama utabakia naye zitakuja kumuandama, ….’akasema na baaaye yule mzee akamshika yule mtoto kichwa kwa muda halafu akamuachia na kundoka, kwenda kukaa pembeni. Pale alipokwenda kukaa, kulikwa na watu wawili waliokuwa wamefungwa kamba, walikuwa kama mazezeta…..

Yule mwanaume akainua kichwa na kumwangalia mama Maua, na yale matundu yanayoonyesha macho mawili yakamkumbusha Maua maisha yao ya kule bonde la kifo. Mama Maua akageuka na kumwangalia malikia, ambaye kwa muda mwingi alikuwa katulia huku kaangalia chini, akionyesha kuwa na mawazo mengi.

‘Japokuwa sikuwahi kufanya hivyo, lakini natumai lile uliloniagiza limekamilika, ….kuwa nisije kukuona bila ya kuwepo mtoto wako, japokuwa sio mimi niliyeweza kumleta mtoto wako, lakini nimefika ukiwa na mtoto wako…..samhani kwa kutokufanikisha hilo kwa wakati….’akasema yule mwanaume.

‘Nashukuru sana …..na namshukuru mungu kuwa nimempata mtoto wangu, hilo ndilo la muhimu….’akasema mama Maua.

Malikia akasogea karibu na aliposimama yule mwanaume, na akamshika begani, na yule mwanaume akageuka kumwangalia, na wakati huo yule mzee mteula, akasimama kwa ghafla na kuwasogelea pale walipokuwepo, kuonyesha kuwa alikuwa na jambo muhimu la kusema ambalo hakutaka lisubiri, na malikia lipomuona yule mzee kasogea karibu yao, akaondoa ule ,mkono begani kwa yule mwanaume na kusogea pembeni.

‘Nimeona niwaingilie kidogo, kwani hili ninalotaka kuongea ni muhimu lifanyike mapema, mnisamehe, maana maisha yangu sasa yanatawaliwa na njozi,….naomba rizaa yenu, ..’akasema yule mzee, na yule mwanaume akasema ;

‘Bila shaka mzee, endelea, uwanja ni wako…’akasema yule mwanaume na akamgeukia mama Maua na kusema;

‘Samhani mwenyeji wetu,…wewe ndiye muhusika mkuu hapa,ulitakiwa wewe ndiye utoe hicho kibali, nimekuingilia, nakuomba umsikilize mzee wetu kwa hiho anahotaka kusema, na samahani mtukufu malikia najua na wewe ulikuwa na lako la kusema, lakini lazima tuheshimu wazee wetu, kwani bila wao tusingelikuwa hapa…..’akasema yule mwanaume.

‘Bila shaka….’akasema malikia na kukatiza neno

‘Yule mzee akanyosha mkono wake kushiria jambo, na mara wakatokea maaskari wakiwa wamewashika watu wawili, mmoja alikuwa mzee, na hali yake ilikuwa mbaya, kwani alionekana kuchoka, na alionyesha kama anaumwa, mwili ulikuwa umevimba hata maho yalikuwa hayaonekani vyema,…na hali kama hiyo ilikuwa kwa mwanaume aliyekuwa pembeni yake…japokuwa alikuwa akionekana sio mzee, lakini kwa hali aliyokuwa nayo, alionekana kuchoka, kama mzee, na ….

‘Oh, ni watu gani hawa?’ akauliza mama Maua.

‘Umeshawasahau,..huyo hapo ni mzee Hasimu na kijana wake…..wameomba na wao waje kwako,….labda nisiseme mengi, tunaomba waongee wenyewe…’akasema mzee mteule.

Mara wale watu wawili yaani mzee hasimu na kijana wake, wakajitutumua na kupiga magoti mbele ya mama Maua, na kwa jinsi walivyochoka, upigaji magoti wao , ulikuwa kama ule wa kulala kifudifudi…na wakawa wanajaribu kutoa sauti, lakini ilikuwa ni kwa shida, wakasema;

‘Samhani sana kwa hayo tuliyokutendea, tunaomba utusamehe….tunajua tulilokufanyia ni kosa kubwa, na mizimu imeliona hilo,…na hatutakuwa na ahueni hai hapo utakapotusamehe wewe na wengine tuliowahi kuwatendea ubaya….’wakawa wanaongea kwa pamoja lakini kwa kujibizana, mzee akiongea na kijana wake akifuatizia kwa nyuma.

Mama Maua alipogundua kuwa ni wale watu waliotaka yeye atupiwe ziwani ili aliwe na mamba, akahisi hasira ikimpanda na hapo hapo akageuka kuondoka, lakini malikia akamshika mkono na kuuminya ule mkono kuashiria kuwa asubiri,….

‘Tunakuomba utusamehe….mateso tunayopata ni makubwa sana…..’akasema yule mzee, huku mahozi yakimtoka.

‘Koo linawaka moto, tumbo linawaka moto, maji hayapiti…ooh, tusameheni wote, …wewe na mwanao’akasema yule mzee akijaribu kuinua kichwa, kumwangalia mama Maua lakini hakuweza na hapo mama Maua akawasogelea na kuwashika kichwani na akasema;

‘Mimi nimewasamehe, kwa vile mumekiri kosa lenu, ingawaje, kama ningelikuwa nimeliwa na mamba, nisingelikuwepo hapa leo, lakini nashukru mungu kuwa hilo halikutokea, na shukurani zangu zimfikie huyu mwanaume aliyejitolea kwa hali na mali kuhakikisha kuwa napona…’akasema mama Maua akimwangalia yule mwanaume.

Wale watu wawili mzee na kijana wake, wakaomba maji na kunywa, lakini kila wakimeza fundo moja, ilikuwa kama mtu anayekunywa kitu chenye kutia maumivu makali….

‘Inabidi wafanye hivyo, kwa kukiuka masharti ya maji ya yamini,….na wanatakiwa kuwapitia watu wote waliowakosea, kama bao wapo hai na kama wameshakufa, basi itawabidi wataabike hivyo hivyo hai hapo mizimu yao itakapowasamehe…….na kwa ajili hiyo, hata sisi inabidi tuhame hilo eneo, na kwenda sehemu nyingine…’akasema Mzee mteule.

‘Mnatarajia kuhama?’ akauliza mama Maua/

‘Ni kweli, ndio maana tumekuja kukuomba tuondoke pamoja, maana huko tunakohamia ni mbali na ni makazi mengine mapya….’akasema malikia.

‘Hapana mimi sitaweza kuondoka na nyie…’akasema mama Maua.

‘Basi tunaomba tuondoke na mtoto….’akasema mzee mteule.

‘Hapana siwezi kuachana na mtoto wangu, sitaweza kuishi bila mtoto wangu, yeye bado mdogo, anahitaji kuwa karibu na mama yake’akasema mama Maua. Malikia akamsogelea yule mwanaume aliyekwua kavalia kofia na kusema;

‘Mama Maua, niliwahi kukuuliza kuwa je, kama huyo mwanaume aliyekuokoa akisema yupo tayari kukuoa, na kuondoka na wewe utakuwa tayari, …je nikuulize kama huyo mwanaume akasema anataka kukuoa uwe naye karibu utakubali kuondoka na sisi?’ akauliza malikia, na yule mwanaume akaonekana kushituka na akamgeukia malikia kutaka kusema neno, lakini malikia akamnyamazisha.

Mama Maua akashikwa na mshangao akabakia kimiya kwa muda, na mara mzee mteula akasema kwa sauti ;

‘Mtukufu malikia hilo halitawezekana….’kabla hajaendelea malikia akaashiria kwa mkono kumzua yule mzee asiendelee kuongea;

‘Jamani mimi nayasema haya nikiwa na moyo wa dhati..huyu mama, ni rafikki yangu, na nampena sana, na ningelifurahi tuwe pamoja mimi na yeye. Nataka kulithibitisha hilo kwenu nyote kuwa mimi ni mama wa wote, na pia ni rafiki wa wote, …na urafiki wa kweli ni pale unapokuwa tayari kutoa kile unacchokipenda kwa mwenzako….’akatulia na kumgeukia yule mwanaume, akasema;

‘Mimi nipo tayari umuoe, huyu mama …’akasema malikia lakini mzee mteule akasogea na kusema;

‘Mtukufu malikia hilo halitawezekana…sikiliza ninayokuambia, ni kweli moyo wako upo razi kwa hilo, lakini kuna mengi huyajui, …’ na kabla hajamaliza kuongea mama Maua akasema;

‘Nawaombeni mnisikilize, …nashukuruni sana kwa moyo wenu huo, na nashukuru sana kwa mtukufu malikia kunipigania ili niolewe na huyu mwanaume,lakini mimi nashangaa, kwanini niolewe na mtu amabye simjui, …..kwanza naomba nimjue huyu mtu ni nani…’akasema mama Maua.

‘Kumjua utamjua tu, usitie shaka, lakini…’malikia akataka kuongea lakini mzee mteula akamzua kwa mkono, na kukawa na ukimiya kidogo, na mzee mteule akasema;

‘Wajukuu zangu,…kuna mambo mengine yanawezekana na mengina hayawezekani, ….najua wema ulio nao mtukufu malikia, lakini huyu mwanamama, ….haitawezekana kuolewa na ……’akasita kidogo, na baadaye akasema;

‘Naomba hilo mlizingatie,…ama kwa kuondoka na kuishi naye inawezekana,…na hiyo ndiyo ahueni yao, hasa kwa mtoto wake, huyo ni mtoto ambaye amekuliwa kwenye sehemu takatifu, anastahili kuwa nasi, ila kama atakwenda kuishi huko atakapoishi,…tuombe hayo yapitie mbali…’akasema mzee mteule na kuondoka kukaa pembeni.

‘Kwa vyovyote iwavyo, mimi naomba nikuone sura yako, wewe mwanaume uliyenitendea wema ambao siwezi kuulipa, na kama upo tayari kunioa mimi, basi …ukubali tusihi na wewe huku kwetu, na sio huko msituni’akasema mama Maua, na watu wakaguna

Malikia akawaonyueshea ishara ya kutulia.

‘Kwahiyo akikubali kukuoa, ukaishi huku kwenu, na yeye kwake, lakini atakuwa akija kila siku kukuona kama mke wake, ….hiyo inawezekana, je kwa wazo hilo upo tayari kuolewa na y eye?’ akauliza malikia.

‘Kwanza naomba nimuona sura yake’akasema mama Maua huku akiwaqzaia wazo hilo moyoni akisema huenda katika kufanya hivyo, anaweza akabadili maamuzi na kwenda kuishi huko msituni….akwa kamkazia macho yule mwanaume ambaye alikuwa kaduwaa, kama vile haelewi nini kinachoendelea.

‘Ya kwanza kwanza mengine baadaye, au sio?’ akasema malikia huku akitabasamu.

‘Sawa mtukufu malikia, naomba nimuone sura yake kwanza…mengine baadaye’akasema mama Maua, na malikia akatoa ishara kwa yule mwanaume avue lile kofia na yule mwanaume kwa taratibu akalivua lile kofia.

Mama Maua alijikuta akishikwa na butwaa, aibu ikawa imemjaa, akatamani kuwepo na sehemu akaficha uso wake,….hakuamini macho yake…na hapo hapo akahisi moyo ukimuenda mbio, isivyo kawaida, kichwa kikaanza kumuuma kwa nguvu sana…taharuki akahisi giza nene likitanda usoni, akadondoka na kupoteza fahamu.

NB: Haya tujadili, kweli yupo ambaye anaweza  kutoa anachokipenda kwa ajili ya mwenzake?

WAZO LEO : Tendalo utendalo, lakini ujue kila jambo lina mwisho wake.


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Wonderful рost hoωeveг Ӏ was ωоndeгing if yοu could write a lіtte moгe on this subject?
I'd be very grateful if you could elaborate a little bit more. Cheers!
Feel free to surf my web page ... bank lån