Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, January 1, 2013

Kitanda Usichokilalia hujui kunguni wake


 
Baba Tv haiwaki…..’sauti ya mtoto wangu ikaniamusha asubuhi na mapema mwanzoni nilijua na hizo kelele za nje za usiku za kusherehekea mwaka mpya, lakini nikakumbuka kuwa tulishaambiwa kuwa dunia imebadilika inaelekea kwenye mfumo mwingine, mfumo ambao, maisha yake hayatakuwa na cha bure tena.

‘Baba hajanunua king’amuzi….’akasema mtoto mwingine. Niliposikia hivyo hapo roho ikaniuma, nikainuka kitandani, na kupikicha macho, sio kawaida yangu kuchelewa kuamuka, lakini mawazo ya usiku kucha yalinifanya nishindwe kulala.

Nikamtuma mtoto akanunue mkate,…kwa bajeti yangu, sikupenda kufanya hivyo, lakini nilijua kuwa huenda kumuonyesha mtoto kwa mfani itasaidia. Mkate ulipoletwa nikawakalisha watoto, na kuushika mkate juu.

‘Huu ndio mshahara wangu,…huu ndio mfano wa mshahara wangu,….ada aenu za shule, ni zaidi ya huu mshahara wangu..ina hutuwezi kulipia ada zenu zote kwa huu mshahara wangu, kwa muhuma mmoja tu, ndio maana nataka kwenda kuongea na walimu wenu angalau tuweze kulipia kwa miezi miwili miwili, kidogo kidogo…

‘Kama watakubali, basi katika huu msharaha, robo tatu yake, itakuwa ya kuwalipai ada zenu za shule, ..mkate utabakia kiasi gani?’ nikawauliza.

‘Robo…’wakasema pamoja.
Nikaondoa robo tatu ya mkate tukabakiwa na robo, nikainua ile robo ya mkate, nikasema;

‘Hii robo iliyobakia ndio bajeti ya mwezi, hapa tunahitajika tule, tuvae, tulipie kodi,…hebu niambie nitaukatakata vipi huu nkate ili vitoshe hivyo vitu vingine..haiwezekani au sio?’ nikawauliza kwani walishasema haiwezekani.

‘Ndio maana yake, haiwezekani ….ndio maana seehmu ya kununulia king’amuzi kwa hivi sasa haipo,…tuombe mungu, huenda mwaka 2013 ukaleta neema, ili tupate pesa ya kuongezea mkate wetu, bila hivyo…hatutaweza,..’nikasema na watoto wakainamisha vichwa chini, kwa huzuni….

Kabla sijaweza kuwafafanulia vyema watoto wangu, nikasikia nje watu wakiongea, na mazunguzmo yao yalinifanya nivutike kuwasikiliza,

‘Umeshalipia pesa za maeneo, maana nasikia watu wameshaanza kupimiwa maeneo yao?’ sauti ikasema.

‘Sijalipia, pesa nitapatia wapi, wakati mtoto wangu kafaulu, nahitajika kumwaandalia sare za shule, kuna ada….’sauti nyingine ikasema

‘Hongera, hata wa kwangu kafaulu pia, lakini sitampeleka huko kwenye shule za kata, maana kutoka hapa mpaka huko shuleni ni kumtesa mtoto. Usafiri wa kufika shuleni ni mgumu, na hata ukipiga hesabu ya hiyo nauli kila siku na pesa ya matumizi, na muda wa kuchelewa , kupigana na makondakta, gharama yake ni kubwa zaidi ya ada ya shule za kulipia….’sauti nyingine ikasema.

‘Kwahiyo ina maana unampelekea mtoto wako shule za kulipia, ..heri yenu nyie wenye pesa , sisi hatuna jinsi,….huko huko, kwenye shule za kata,….maana pesa yenyewe ya kula ni matatizo, tunakula mlo mmoja kwa siku,asubuhi ukijaliwa ni chai ya rangi kwa andazi moja…sitaweza kulipia hiyo ada ya shule za kulipia…mimi na asenti Kikwete tu.’sauti nyingine ikasema.

‘Lakini mpendwa, hebu niambie nauli ya kila siku ya mtoto kwenda shule na kurudi ni shilingi ngapi,….na sizani kama mtoto atakwenda shule bila hata senti ya matumizi, na angalia umbali wa kutoka hapa hadi huko shuleni, ni zaidi ya nauli yako ya mtu mzima ya kwenda na kurudi kazini,…..’sauti ikasema.

‘Wewe unasema tu,…hiyo nauli naipata kwa kuuza vitumbua, lakini sitaweza kudunduliza hadi kupata hiyo ada kwa mkupua…., maana ili apate hiyo nauli, inabidi nijinyime, ..hapo hakuna jinsi, hutaweza kudunduliza,..ili upate ada kubwa, wakati huna pesa ya kula, kuna ugonjwa, kuna vitu vingi vinahitajia pesa…

‘Nikuambie ukweli, ukimpa mtoto nauli, unakuwa umefunga mikanda matumboni,….mnajinyima kula ili mtoto aende shuleni, au utabana bana au kukopa ili siku iende, hata kwa kushindia maji….sio rahisi kukuelimisha kitu kama hicho, kama haupo katika maisha yangu…’sauti ikasema.

‘Halafu nasikia jana wameshazima mitandao yao ya kuangalia runinga,…?’ sauti ile ikasema baada ya ukimiya. Hapo na mimi akanitonesha kidonda, nikikumbuka kuwa na mimi nahitajika kutafuta pesa ya kununulia hicho kidude..ili kuwe na amni ndani ya nyumba…

‘Kwani ulikuwa hujanunua hicho king’amuzi?’ sauti ikauliza kwa mshangao.

‘Unanichekesha kweli, runinga yenyewe, niliipata kwenye mitumba, ….na nilihangaika hadi kumalizia hilo deni, na huyo jamaa niliyenunua kwake, ilibidi anisamehe tu, maana alifuatilia wee, hadi akachoka,….ningemlipa nini.

‘Niliamua niichukue kwa mkopo,  kwa vile watoto walikuwa hawakai nyumbani,….kama wameamua kuwa ili uone mambo yao ni mpaka nilipie kila mwezi,kwa hali yangu …sitaweza kabisa, ni heri nikaize tu,  kama nitampata mtu wa kumuuzia hiyo runinga nitafurahi, …’sauti ikasema.

‘Tatizo lenu hamtaki maendelea mpo dunia ya kale, na ujue kabisa maendeleo ni gharama, sio rahisi kama unavyofikiria,…kila hatua ya maendelea inabebwa na gharama zake, na ili uweze kupata faida, inabidi uongeze juhudi, vinginevyo, utabakia kulalamika’sauti nyingine ikasema.

‘Najua wenye nazo mtasema hivyo, lakini …..’akatulia kidogo.

‘Lakini nini , mbona umesita kuongea?’ akaulizwa.

‘Nimemuona baba mwenye nyumba yangu, najua anakuja kudai pesa yake ya pango, na keshapandisha kodi ya nyumba, anadai gharama za uendeshaji zimepanda, sijui gharama gani wakati nyumba yenyewe hajawahi hata kuikarabati…..’sauti ikasema na akainama chini kwa huzuni.

‘Na baba yangu kaja toka huko kijijini , anaumwa, akisikia vurugu za huyu jamaa kudai kodi yake, atazidi kuumia,siunajue tena uchungu wa mwana kwa mzazi hauishi…sijui nifanyeje kumzuia asifike nyumbani….’sauti ikasema kwa huzuni.

‘Ndio hayo hayo ninayokuambia kuwa maendeleo yana gharama yake, …pesa ya kwetu thamani yake haipandi,….shilingi ya leo, kesho haina thamani, hebu niambie hivi leo unaweza kuipata shilingi ishirini, au kumi, ….hata ukiiona njiani huwezi kuikota. Na hata hamsini sasa ni pesa ya pipi…je unafikiria huyo mwenye nyumba atawezake kununua saruji, …’sauti ikasema.

‘Na huyo mwenye mshahara thamani ya pesa yake inashuka au inapanda…?’akauliza mwingine

Mazungumzo hayo yaliendelea lakini mimi sikuweza kuyasikia tena maana nilishazama kwenye kuwazia mshahara wa mwezi ambao upo pale pale,thamni yake kila siku inashuka,…japokuwa mambo yanapanda, gharama za kimaisha zinapanda, ….lakini kipato cha Mtanzania kipo pale pale…Mwaka mpya unaanza na mambo mapya.

Mwaka unapoanza, mambo mengi sana yanamkabili mzazi, kuna ada za shule, ambazo shule nyingi, wameweka kiwango kikubwa cha kuanzia mwaka,…tofauti na katikati ya mwaka, kuna kulipia kodi za nyumba, kuna malipo mengi ya kuanzia mwaka, na ukumbuke kuwa mwishoni mwa mwaka kulikuwa na sikukuu nyingi…sasa tena tunapata pigo jingine,…heri pigo hilo lingesogezwa hadi mwezi wa tatu,….

‘Najua nyie mtasema ni gharama ndogo tu, vijisenti tu,….kwa vile mnazo, lakini kama mngelikuwa katika hali kama yangu, msingeliweza kusema hivyo, maana siri ya mtungi aijueye ni kata…’nikasikia hiyo sauti ikilalamika na mimi nikasema ni kweli, kitanda usichokilalia huwezi kujua kunguni wake.

‘Ndivyo ilivyo, maisha ya sasa hakuna cha bure tena, tutalipia kila kitu, hewa, maji,..itafikia hata kuongea utatakiwa ulipie…maisha ya dunia yanabadilika siku hadi siku , ujima ujamaa, undugu, ..upendo hautakuwa na nafasi tena,,,,,maana hata ndugu yako akikutembelea hutaweza hata kumkirimu, …tutafukuzana ndugu ili tuweze kumudu maishi,hapo kutakuwa na upendo tena….hayo ndiyo maendeleo, ukiwa nacho utaweza kuishi, kama huna….

‘Ina maana kama sina…. sina uhai tena….?’akauliza

‘Jibu unalo mwenyewe, nikuuliza, kama huna king’amuzi utaweza kuangalai tena runinga?’ sauti ikauliza.

‘Utaona chenga chenga tu, huwezi kuona kitu.’sauti ikasema.

‘Sasa kumbe unajua..hayo ndiyo maisha, mwenye nacho, ataongezewa, kama huna kitu,..ulie tu…utaishia kuona chenga-chenga tu,, hata hicho kidogo ulicho nacho, watakuja kukunyang;anya , maana kuna kodi za watu, kuna kulipia majengo, dukani hakukamatiki, unafikiri hapo una maisha tena…wewe ni mfu tu.

Ni hayo kwa leo kutoka kwenye diary ya tarehe 1-1-2013Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

bear grylls messer
Review my weblog ... bear grylls messer

Rachel Siwa said...

Ujumbe huu kweli umetulia,Ndudu wa mimi wewe ni mwisho!!!!!!!Pamoja saaana....Mmhhh kweli kitanda usichokilalia hujui Kunguni Wake!!!!!!