Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, December 18, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-39




‘Mke wangu inaonekana wahasimu wameshakusanya kikosi chao cha maaskari na inaaminika kuwa wapo kwenye ngome yao muhimu, hatujui wana maana gani, na kwa hilo inabidi tujiandae kwa lolote na hata ikibidi kuingia vitani kwa maslahi ya wanajamii….’akasema mfalme.
‘Vitani……?’ ‘akauliza malikia mtarajiwa akiomba hilo lipitie mbali, na akabakia ameduwaa akimwangalia mume wake, je ni nini kitatokea hebu tuendelee kidogo na sehemu hii……

‘Mke wangu hali invyoonyesha ni kuwa wenzetu wamezamiria vita kiukweli, labda tutii matakwa yao, ambayo kuyatii kwetu ni kama kujitia kitanzi wenyewe,….’akasema mfalme mtarajiwa.

‘Kwani wao wanataka nini hasa, wanataka hayo madaraka, au kuna kingine cha zaidi?’ akauliza malikia .

‘Wanataka madaraka, wanataka waendelee kutawala kama walivyokuwa wakitawala na kijana wao awe ndiye mfalme wa jamii yetu, wakidao ndiye mfalme aliyetabiriwa’akasema mfalme.

‘Eti nini, kwa sifa gani alizokuwa nazo hadi wadaii hivyo, mbona hata wananchi watawacheka, maana huyo kijana hana hizo sifa kabisa, mimi mwenyewe nimekuwa nikilumbana naye kipindi ambacho haupo, akidai kuwa anioe kwa vile wewe umeshaliwa na mamba, …..hapana huyo hafai, ….na hilo la vita sizani kama wanaweza kufanya hivyo’akasema malikia.

‘Wewe kama mama lazima useme hivyo, kwa vile unawatetea watoto wako au sio?’ akasema mfalme kimzaha.

‘Sio kwamba na watetea, ….ila naona wao wanatumia mbinu za kushinikiza, kwasababu wenyewe kwenye imani zenu mlisema akitokea mfalme mtarajiwa hakutakuwa na vita tena, sasa kwanini wajiandae kwa vita?’ akauliza malikia.

‘Wao wanataka vita kwa vile wanadai kuwa mimi sio mfalme mtarajiwa, sina hizo sifa, na sifa hizo nimezishinikiza kwa vile nimekuoa wewe’akasema na kumwangalia mke wake.

‘Mimi mume wangu sipendi kabisa vita,….kama inabidi nitajitolea kwenda kuongea na wao, ili niwashawishi kusitokee vita’akasema malikia na mfalme akamwangalia kwa mshangao.

‘Wewe huwajui hawa watu, ….hata kama wewe ni malikia mtu waneyekuheshimu sana, hawataweza kukusikiliza kama matakwa yao hayajatimizwa, tunamfahamu sana huyo mzee,…ila mimi nilikuwa na mawazo mengine’akatulia mfalme.

‘Mawazo gani mume wangu, maana mimi naheshimu sana mawazo yako, huwa kila ukitoa mawazo yanakuwa yenye tija, hata wanachi wengi wanakusifia kwa hilo, na wana hamasa kubwa ya kuona mabadiliko, wenyewe wanasema hata kabla hujatawazwa, wameshaanza kuiona neema, wana uhuru, wana amani,…na maendelea yameshaanza kujitokeza’akasema malikia.

‘Mimi na wewe ni wazazi, japokuwa hatujabahatika kupata watoto, lakini tuna ile hisia ya kuwa na familia, hebu chukulia mimi naenda vitani nauwawa, utajisikiaje,….haya chukulia wale ambao ni hali duni kabisa, walikuwa wakimetegemea baab yao kwa kila kitu, na kaenda vitani kauwawa,….sizani kama inaleta picha nzuri…

‘Mume wangu unataka kusema nini….’akauliza malikia.

‘Ninachotaka kusema  ni kuwa vita sio nzuri, na ni vyema tukajitahidi kuikwepa kwa nguvu zote,…maana kila mmoja ni mzazi , na kama ikija vita uzazi huo hautakuwa na maana tena, kwani tutatarajia kupotea kwa watu wengi, wanawake wengi wtabakia wajane, watoto watabakia mayatima,….na vita kama vita haina macho, …sio tu wanaume ndio watauwawa, hata wanawake,watoto na wazee…

‘Sasa mimi nataka kulikwepa hilo, kwa kuchukua maamuzi magumu, ….’akatulia.Mkewe naye akatulia kuskia hayao maamuzi magumu.

‘Yote hayo tatizo ni mimi, ….huenda angelichaguliwa mwingine, kama mfalme mtarajiwa kusingelikuwa na haya yote….sasa kumbe tatizo ni mimi,….mimi ni na thamani gani mbele ya watu , mbele ya roho za watu zitakazo teketea, ….yaani watu mamia wafe kwa ajili ya roho yangu mimi, mtu mmoja, hapana, hapo ndio naona lazima nichukuea maamuzi magumu’akatulia, na malikia akakodoa macho akiogopa kusikia hilo analohisi ndilo mume wake anataka kulisema.

‘Nimeonga na babu, kanipinga kwa nguvu zote….na kuniambia mimi nitakuwa msaliti….lakini uwezo wa mwisho ni wangu mimi, …lolote likitokea nitakayeumia sana ni mimi …najua wewe tupo pamoja, lakini mwisho wa siku kila mtu ataninyoshea kidole mimi,…ndio maana nasema nahitaji kuchukua maamuzi magumu, ….’akatulia.

‘Maamuzi gani mume wangu?’ akauliza malikia.

‘Wao unahisi wanataka tu hayo madaraka…hapana ni pamoja na roho yangu, hasa mimi na babu, kila kukicha wanatunga mbinu, na hata kama utawapa hayo madaraka, hawatatulia wakituoni sisi tunapumua…ndio tabia ya hawa watu, watu kama hawa hawatosheki hata kama ungeliwapa dunia hii yote, mpaka wasikuone hapa duniani….’akatulia.

‘Kwahiyo unataka kusema nini mume wangu…..?’ akauliza malikia.

‘Kwanza nahitaji maoni yako, …Je tufanyeje ili kuepushja hivi vita, je upo tayari kwa mawazo yangu,na maamuzi yangu magumu, hata ikibidi …..ndoa…’kabla hajamaliza mlango ukagongwa, na malikia akabakia ameduwaa. Mume akasimama na kwenda kumuona aliyegonga, na akaingia babu, akiwa na wasaidizi wake.

Wote walipoingia wakapiga magoti mbele yake, na kumuacha kijana wao akiwa ameshangaa, na akaanza kuwainua mmoja mmoja, lakini walikuwa wametulia huku wameinamisha vichwa vyao chini.

********
Mfalme mtarajiwa akaitisha kikao cha usalama, na viongozi wa kivita na pia aliwahusisha viongozi  wa usalama wa raia na wote wakafika kumsikia mfalme mtarajiwa anataka kusema nini. Baada ya kuongea na vikosi hivyo, akawaambia alichokusudia na wao wakamwambia kama sio yeye,  wao hawatamkubali mwingine yoyote.

Baadaye akaitisha mkutano mkuu, ambao mwanzoni alipanga uwe wa wajumbe wawakilishi tu, na wakuu mbali mbali wa koo, ili asikie maoni yao. Kikao hiki badala ya kuja wawakilishi pekee, wakafika watu wengi, kwani kila alieyesikia kuwa kiongozi wao ambaye walikuwa wamemsubiria miaka mingi anataka kukaa pembeni ili kuepusha vita, aliona afike asikie kwa masikio yake mwenyewe.

Na hapo mfalme mtarajiwa akajua kuwa sasa haongei na wawakilishi tu, anaongea na sehemu kubwa ya wananchi wanaomtegemea kwa lolote lile, hakutaka kuwaficha alianza moja kwa moja kwa kuwapa taarifa kuwa wahasimu wameingia msituni, na inavyoonekana wamejiandaa kwa vita,…

‘Najua mtauliza kwanini, ikiwa bado mfalme hajatawadhwa, na kwanini wafanye hivyo, wakati tunatarajia ujumbe muhimu toka huko makaoni…ujumbe huo utakuja, lakini unakuja kwa ajili ya kusikiliza tuhuma zilizopelekwa kwao, ndio maana hata shughuli za kutawadhwa kwa mfamle mtarajiwa zimesitishwa kwa muda…’akasema mfalme mtarajiwa.

‘Tungelikuwa wakorofi, shughuli hizo zingelifanyika kwani yale muhimu yaliyokuwa yakitarajiwa na wanachi yalishatimia,….lakini hatuna haraka na hilo, kwani uongozi bora ni ule unaojali matakwa na masahi ya raia wote, ikiwemo wao….’akasema mfalme mtarajiwa.

‘Wenzetu, wamejifanya kuwa mimi sio huyo mfalme mtarajiwa, hata baada ya dalili zote zilizotabiriwa kuonekana…hii ni kwa vile wao walitaka kijana wao mdio awe mfalme. Wao wanadai kuwa ukoo wetu una kasoro nyingi, na kwahiyo haiwezekani mfalme akatoke kwenye ukoo wetu.

‘Na kwa vile ukoo wetu na wao umekuwa ni mahasimu wa kihistoria,  hawakubali kabisa tukae kiti kimoja, na hasa tukiwa sisi ndio watawala, huenda wangekubali hivyo kama wao ndio watawala na katikamaisha yangu yote toka utotoni sijaona wakikubaliana na jambo lolote lilitoka kwenye ukoo wetu.

‘Kwa vile hapa hatupo kisiasa zaidi, tupo kijeshi zaidi, nisingependa kuwapotezea muda wenu, lakini inabidi niwaweke wazi, ili wakati mkiziaga familia zetu huku majumbani kwenu, kuwa tunakwenda vitani mjue jinsi gani ya kuwaelezea, vita sio lele mama, vita inaleta majozni , inaleta umasikini ni kitu kisichopendeza kwa ujumla, kwahiyo faraja kwa familia zinahitajika …’akatulia kidogo.

‘Sisi hatupendi na wala hatutaki kulazimisha vita, lakini wenzetu wanaamua kuanzisha vita….na kama wanataka kufanya hivyo, hatutakaa hivi tu, wafanye wanalotaka,….tunahitajika kujihami, tunahitajika kuwalinda raia zetu, mifugo yetu na uhuru wetu, …..’akatulia na kuwaangalia wenzake.

‘Mimi kama ingelikuwa uwezo wangu, ningeliachia hii nafasi kwanza ili kuepusha hiyo vita, kwani uongozi ni kitu gani, na matakwa ya uma kwa masilahi ya uma, sio kwa matakwa ya watu binafsi …ndio maana nimewaita, kuwa ili tuepusha hii vita kwanini mimi nisijitoe kwanza, kwanini kuwepo kwangu kwa mfalme mtarajiwa iwe ni tatizo, au ni kwasababu ya ukoo wetu. Kama ni hivyo, basi mimi nipo tayari kukaa pembeni,….hili nimelileta kwenu kama wawakilishi wa wananchi, ili nyie mlifikirie kwa makini.

‘Labda niwaambie ukweli kuwa mimi sikuwa na wazo kama hilo kuwa mimi nitakuwa mfalme, sikuwa najua kuwa mimi ndiye mtarajiwa, ….japo kuwa babu alikuwa akiniambia kuwa kaota, au kaona dalili hizo kwangu….kuwa mimi huenda nikawa ndiye huyo mtarajiwa…alikuwa akiniambia hivyo kama utani tu,,,'
akasema akigeuka kule walipokaa wazee.

‘Nakumbuka hata siku ile nilipowasili hapa kama alivyotabiri huyo mtabiri, hakumini, na alinimbia kabisa, kuwa yeye alijua huyo mtu atakuwa mtu tofauti kabisa, hakuwa akiamini kuwa huenda nikawa mimi, japokuwa aliombea iwe hivyo, kwani alishaniona kuwa nina sifa zote za huyo mfalme mtarajiwa, lakini hata wenzetu, babu mhasimu anadai kuwa kijana wake ana sifa hizo hizo…’aliposema hivyo watu wakacheka kwa dhihaka.

‘Siri za mfalme mtarajiwa na dalili zake za mwisho zilitakiwa zitokee siku hiyo iliyotabiriwa, sio lazima niwe mimi hata kama ninazo hizo sifa, na hata nilipojitokeza siku ile sikuwa najua kuwa ilitakiwa iwe hivyo….hayo babu hakuwahi kuniambia….na kama mnavyoona ilivyokuwa kwangu mimi nilishapakwa matope, na hakuna aliyeniwekea akilini tena kuwa nitakuwa ndiye mimi mfalme mtarajiwa, ila wenzetu walijua sifa za huyo mtarajiwa na alitakiwa atokee vipi, ndio maana wakamuandaa kijana wao….’akatulia kidogo.

‘Lakini kila lililopangwa kuwa litatokea ….litatokea tu, na huyo mtabiri aliposema hivyo, hakutaja ukoo gani, hakugusia hali ya huyo mtarajiwa, alitoa dalili tu….sasa kwanini wao washinikize kuwa kijana wao ndiye mtarajiwa. Hilo linajionyesha jinsi wenzetu walivyo, na kwa mtaji huo, kama watashika madaraka, ubinafsi utawekwa mbele,

‘Kama wao wataendelea kutawaa nina imani kuwa jamii yetu itaendelea kudumaa, na ubaguzi utaendelea kuwepo, hilo hatutaki liendelee kuwepo. Lakini sio hadi tufikie kwenye vita na kama tatizo ni mimi , basi kwanini ning’ang’anie hayo madakaraka….’akasema huku akiangalia mbele ya wananchi ambao walizidi kumiminika kwa wingi.
‘Baada ya mimi kujitokeza wenzangu wakakimbia na kujificha, na huko wakakusanya kikosi chao ,wakidai kuwa mimi sio mtarajiwa, mimi na ukoo wetu tumelazimisha iwe hivyo kwa vile eti kwanza nimetumia mbinu za kumuoa malikia, …

‘Sasa ukiangalia madai yao yanafanana na jinsi walivyokuwa wakimtengeneza kijana wao, ili aonekane ndiye mtarajiwa, kama ilivyo kwa mwizi mara nyingi humshuku mwenzake kwa jinsi anavyofanya yeye, na huhisi kuwa mwenzake ndivyo anavyofanya…’akageuka kuangalia kushoto halafu kulia,, halafua akaendelea kusema.

‘Hawa wenzetu hawakuishia hapo, wamepeleka malalamiko huko makaoni kutushitakia, wamesahahu kuwa walipokuwa madarakani walikuwa wakipinga kabisa makaoni kuingilia mambo yetu, na kila mara walikuwa wakisisitiza kuwa sisi tunahitajika kuwa huru na hatuhitajiki kuwategemea watu wa makaoni,-walitaka kila jambo tuliendeshe wenyewe, sasa imegeuka  wanataka makaoniI watusimamie mambo yetu, hata makaoni walipopata hiyo taarifa walishangaa…

‘Katika m oja ya amdai yao ni kuwa, kwa vile wanaamini kuwa mimi sio mtarajiwa wanataka niondolewe, na kuwe na uchaguzi wa huru na haki, …tusimamishwe kwenye kampeni mimi na kijana wao, ili aangaliwe ni nani anayefaa kuwa kiongozi…wakidai kuwa wana ushahidi na tumua nyingi dhidi yangu kuwa mimi sio msafi na nilistahili kuliwa na mamba’ akasema na watu wakaguna.

‘Wao wakatoa na angalizo kuwa kama tukikataa, inabidi niondolewe kwa nguvu, na  kwa hivyo ndio maana wameliweka jeshi lao kwa tahadhari kuwa kama sitakubalina na matakwa yao basi hawana budi, ya kuitisha vita,…ili awekwe mfalme anayestahili…je wao pekee yao ndio wanaomjua zaidi huyo mfalme mtarajiwe awe vipi, sasa wao wamgeuka kuwa ndio wenye mamlaka na uamuzi kuwa ni nani awe kiongozi.

‘Kwa hivi sasa wana kikosi kikubwa, …hatukutarajia hilo, kumbe waikuwa na mamluki waliotarajiwa kuwa ikitokea hivyo waitwe, ….na ukichanganya na propaganda zao, wameweza hata kuwaita askari wao wa zamani, wakiahidiwa kupata nafasi kwenye utawala na mali na kutokana na propaganda zao potofu ….

‘Kama mnavyojua wenzetu hawa walikuwa wakimiliki njia njia za kushawishi wananchi, na kidogo kidogo walishaanza kuwahadaa baadhii ya raia, ndio maana wameweza kukusanya askari kidogo kidogo, na sasa wamekuwa na kikosi kikubwa,japo kuwa kuna wenzao waliamua kujiunga na sisi, na tumewakaribisha, na kutokana na wao ndio tukagundua wapi walipojificha…’akasema mfalme.

‘Hatukuamini sana maelezo ya hao askari waliojiunga na vikosi vyetu, kiusalama na kiuataribu , ikiabidi tufanye uchunguzi, uchunguzi wa kina,…tukagundua kuwa ni kweli, kuwa wao wameshaliandaa jesho lao na wanachosubiri kwao ni kutafuta chanzo cha kuanza vita, na habari zilizopatikana huenda wakatuma wajumbe kuleta madai yao, na kama tusipoyatekeleza basi wao huenda wakatumia hilo kama sababu ya kuanza vita.

‘Wenzetu hawa wameweka maslahi mbele, hawajali ni nini athari za vita hivyo kwa sasa…sisi kama rulivyowaambia hatutaki vita, na tutajitahidi kutafuta kila njia kuepusha hivyo vita, …na kama tatizo ni mimi ,basi nitaachia haya madaraka ambayo hayajaidhinishwa na uamuzi uwe mikononi mwa raia wenyewe, ….ila hatutaki wananchi walazimishwe, hatutaki kuje kutokea utawala wa kibaguzi, hilo ndilo tunalochelea.

‘Nilipolipeleka hili swala kwa wazee, kuwa ili tuepushe vita, mimi nipo tayari kujiuzulu, ili raia wamchague yule wanayemuona anawafaa, wazee wamepinga hilo kwa nguvu zote, kwani wao walikuwepo kipindi hicho alikuja huyo mtabiri, na wanasema kama atatokea kiongozi mwingine badala, ya huyo aliyetabiriwa, lhakutakuwa na amani tena….kwasababu wenzetu wameshajipanga kumuweka mtu wao…’akatulia.

‘Wazee wemesema uamuzi wangu huo haukubaliki, ni kama na wasaliti wananchi, wanachi ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakimsubiri mtawala wao, sasa amepatikana, na kwa tamaa ya wachache anapingwa, je sisi tuliokabidhiwa dhamana ya usalama tuna maamuzi gani?’ akatulia na kuangalia huku na kule.

‘Nimefikiria sana, na kutokana na mawazo ya wazee, nikaona ni vyema tukutane, pamoja na kujiandaa kwa vita kwani yote yanawezekana, ….nijuavyo wenzetu hawatatosheka na uamuzi wowote ambao utakuwa kwa maslahi ya wananchi, …..kwa mfano tukiamua upitishwe uchaguzi wa wananchi wote, na kama watashindwa, unafikiri nini kitafuta baada ya hapo…lazima watapinga, sasa tufanyeje?’ akawaangalia wanachi.

‘Ili muwe na maamuzi ya hekima kwanza angalieni familia zenu, angalieni uchumi wetu, angalieni hali zetu, kuwa tukiingia vitani, athari kubwa itakuwa kwa familia zetu, uchumi utaharibika, …halizetu zitazidi kuwa duni…hayo ni baadhi tu ya athari za kivita. Hatuhitaji kuingia vitani, sio kwamba mimi naogopa, hapana, ila naogopa athari zake, …ndio maana naona nijiwekewe pembeni niwe kama raia wa kawaida,…’akatulia.

Hapo wajumbe waliokuwepo, wakaanza kunong’ona, ilianza kidogokidogo, na baadaye ikawa kama vurugu, kila mmoja akitaka kuongea na kutoa lile lililopo moyoni, na mmojawapo akasema;

‘Hilo hatukubali kamwe….ina maana gani ya kusubiria miaka hiyo yote, kusubiria mfalme mtarajiwa, na sasa amepatikana, leo hii tukuachie eti kwa vile wanataka kijana wao awe ndiye mfalme kwa sifa zipi ambazo anazo …., hapana, hilo hatukubali, kama ni vitani tutaingia vitani’akasema mmojawapo na wengi wakashangilia.

‘Hayo ni maamuzi yenu, hamjaangalia maamuzi ya raia wote,….ambao ndio watateseka, ambao ndio waathirika wa pale wanapa-pambana mafahali wawili…tuwaonee huruma hawa raia, wametetseka vya kutosha, na kuwahurumia huko ndiko kunakonifanya mimi niondoke kwenye haya madaraka, ili kusiwepo na vita…’akasema.

‘Ni heri ya kuteseka, baada ya vita kuliko kuwa na utawala uliopia, kwasababu tulikuwa kama watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe…..ubaguzi, unyanyasaji na hali duni, zilituandama, tumevumilia hadi msimu uliotabiriwa, …tunakuomba usituache, kwa kufanya hivyo utakuwa umetusaliti’akasema mama mmoja ambaye alionekana kuchoka sana na hapo watu wakasimama na kushnagilia kwa wingi sana na hali hiyo iliendelea kwa muda mrefu.

Baadaye walipotulia mzee mwanasheria akasimama na kuelezea sheria zilivyo inapotokea hali kama hiyo, na akasema kama mfalme ataamua kutafuta rizaa ya wanachi, inabidi wajumbe wapige kura kwanza, ili ionekane kuwa kweli wanamuhitaji au la…lakini kabla ya hapo kunahitajika maoni ya wajumbe, kuwa kwanini bado wanamuhitaji huyo kiongozi.

Basi yalifuata maoni na mawazo mbali mbali, na hatima ya yoye ilikubalika kuwa kama ikibidi ni heri waingie vitani ili kuinusuru hiyo hali, ili kuwalinda raia na mategemeo yao, ..na wajumbe wote waliamua kupitia raia mmoja mmoja, ili kupata rai zao, …..japokuwa kulikuwa hakuna muda wa hilo lakini walisema watajitahidi hilo lifanyike ili kuzima propaganda potofu.

‘Basi kama mumeamau hilo, mimi siwezi kuwasaliti, nipo pamoja na nyie, lakini msimamo wangu wa kuepusha vita upo pale, pale, nitajitahidi kuzungumza na wao, na kama kuna uwezekano huo, wa kukwepesha vita, nitaupa kipaumbele,…hata kama kuna njia nyingine inayofaa kukwepa vita, itabidi tuifuate…. lakini sio kwa kuwaachia wao madaraka,

Hapo watu wakashangilia kwa muda mrefu, wakisema yeye ndiye mfalme mtarajiwa, hawahitaji mfalme mwingine zaidi yake.

‘Cha muhimu ni wao wakubali kushirikiana kwenye madaraka,…nafasi hiyo tutawapa, kuna nafasi zo zipo wazi kwa ajili yao,  ili tuwe pamoja, hilo naona ndilo la muhimu, ….’akasema mfalme mtarajiwa.

‘Kwahiyo basi, japokuwa tulishajindaa kwa hilo, lakini ni vyema kuanzia leo tukawa tayari kwa lolote lile, na imebidi tuweke vikosi vyetu kwenye mipaka, na kuzunguka eneo ambalo ndipo ngome yao ilipo, ili wasiweze kutoka na kuvamia kwa haraka….

‘Hasa wakiona kuwa propaganda zo hazikufua dafu, basi wanaweza kuanza kutumia nguvu, ili kupaka matope, kuwa usalama hauwezi kulinda raia zake’akasema mfamle mtarajiwa

‘Kama mnavyojua ngome yao, hata kama tutawazunguka. Bado wana sehemu nyingi za kupenya na kuingia huko uraiani ndio maana kwanza niliwaita  wakuu wa ulinzi wa raia …..ili kuhakikisha kuwa raia hawazuriki kwa lolote lile au vikosi vyao kuingia uraiani na kujificha…hilo najua tulishaliweka tayari, hapa ninakumbushia tu’akasema mfalme.

Baada  ya kikao hicho, wataalamu mbali mbali wa kivita wakakutana, na wataalamu wa usalama wa raia wakajadiliana jinsi gani ya kuwalinda raia na mali yao, wakati mipango ya kujadiliana ikiendelea na wajumbe kusambaa sehemu mbali mbali kuelimisha wananchi.

Hayo yakiendelea kumbe mdudu mtu alishapenya na sumu kali, sumu yenye nia ya kuwaondoa wale wote watakaopinga maamuzi yao, ….kila kona na kila ukoo kukawekwa ndumilakuwili, …

Je hayo yaliwezekana, je nguvu ya uma na propaganda potofu ni nani zaidi..

WAZO LA LEO:Kiongozi bora ni yule anayejali maslahi ya wananchi wake kwanza kabla ya kujali maslahi yake binafsi

Ni mimi: emu-three

4 comments :

Anonymous said...

Pretty section of content. I just stumbled upon your web site and in accession capital to assert that I acquire
in fact enjoyed account your blog posts. Any way I will be subscribing to your augment
and even I achievement you access consistently quickly.
Look at my blog harga emas perhiasan

Anonymous said...

I know this site offers quality based content and extra information, is there any other website which presents such
stuff in quality?
Also visit my homepage : harga emas dunia

Anonymous said...

Wow that was unusual. I just wrote an incredibly long comment but after
I clicked submit my comment didn't appear. Grrrr... well I'm not writing all that over again.
Anyhow, just wanted to say wonderful blog!
My website > harga emas batangan

Anonymous said...

Asking questions are truly good thing if you are not understanding anything totally, except this
post provides fastidious understanding yet.
Feel free to visit my web site :: harga emas dunia