Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, December 4, 2012

Uchungu wa mwana Aujaye ni mzazi-32
Marejeo: Kama mnakumbuka mzee mhasimu alituma kikosi kwenda kumuua kijana wa mzee mteule, je kikosi hiki kiliishia wapi, hebu turejee nyuma kwanza, ili tuweke mambo sawa kabla hatujaingia kwenye hitimisho la kisa hiki:

Kikosi cha mzee Hasimu, kilifika eneo waliloelekezwa kuwa wakivuka ziwa hilo la mamba hadi upande wa pili watafika eneo la bonde la mauti, na huko inawezekana ndipo huyo kijana alipojificha, kama kweli yupo hai. Wao huko wanapajua sana kwani mara nyingi wamekuwa wakiwapeleka wahalifu na wanajua jinsi gani ya kuvuka huo mto wa mamba.

Ikabidi maaskari hawo majasiri watumie mbinu zao za kivita, …maaskari hao ni miongozi mwa maaskari majasiri, ambao waliweza kufanya kazi yoyote, na kwa uchunguzi wao walishajua huko kuna watu wapo, lakini hawakuwa an uhakika, ni watu gani, na wengine walihisi huenda na makundi yale haramu, ambayo huishi kwa kula nyama za watu.

Watu hawo ni wale waliopewa adhabu ya kutupwa huko kwenye bonde la mauti, na kwasababu huko hakuna chakula, wakawa wanakulana wenyewe kwa wenyewe, na hali hiyo ikazoeleka, na hawo walibahatika kuishi wakajenga tabia hiyo, ya kula nyama za watu.

‘Kama sio hawo watu, basi, inawezekana kabisa akawa huyo kijana,…’akasema mmoja wa maaskari waliotumwa.

‘Kama ni yeye kwanini aishi maeneo ya huko, na kwanini harudi ?’ akauliza mmojawapo.

‘Hilo hatuwezi kulijua kwa sasa, …huenda kuna jambo analifanya, huoni watu wao walivyokuwa hawana wasiwasi, wakati sisi tunajua kuwa keshakufa, wao, wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, hii ni kumaanisha kuwa kuna jambo ametumwa kulifanya’akasema huyo kiongozi wao.

‘Mimi hainiingii akilini, jambo gani la kuhatarisha maisha yake….na siku zote hizo, na eneo lenyewe limejaa hatari tupu ’akasema mwingine.

‘Cha muhimu ni kuhakikisha tunatimiza tuliyoagizwa, hayo mengine hayatuhusu kwa sasa, na mkumbuke kama ni yeye, sio mtu wa mchezo, tunahitajika tujiandae kweli, na kama sio yeye, basi tunaenda kukutana na watu wala watu, na hawo hawana mchezo, ni kama wanyama.’akasema huyo kiongozi.

Wale maaskari walikwua ni majasiri, hawakuogopa kwa lolote lile, wakasema wapo tayari kukutana na hayo yote mawili.

Kikosi hicho kilipofika ufukweni, kwanza kilitumia mbinu zao za kijeshi za kuvuka huo mto|, kwanza ilibidi watafute wanyama, na wanyama hawo waliwaweka mbali ili wale mamba wakimbilie upande mwingine na wao wapate mwanya wa kuvuka, …

Zoezi hilo likafanyika, lakini ilibidi wavuke wawili wawili, …na wawili wa kwanza wakavuka, na walitakiwa wakifika huko kwanza  wafanye utafiti, ili kubainisha usalama, kabla ya kikundi cha pili hakijaenda,  walipewa masaa mawili, baadaye watoe ishara ili wengine wawafuate, lakini masaa mawili yalipita bila kutokea ishara yoyote…

Hapo mkuu wa hicho kikosi akaamurisha watu wengine wawilii waondoke kwa mtindo ule ule…na hao wawili, wakaondoka…na ikapita masaa mawili, hakuna ishara wala ya dalili ya watu kurudi, hapo huyo mkuu wa hicho kikosi akaingiwa na mashaka, alichofanya ni kutuma ujumbe makaoni ili wapate nguvu ya ziada, lakini nguvu hiyo haikupatikana kwa muda muafaka, wao wakawa wanaendelea na zoezi lao la kutuma watu wawili wawili.

‘Sasa hapa ni kufa na kupona…inabidi na mimi niende huko, hapa atabakia mtu mmoja kwa ajili ya kutoa mawasiliano kama hatutarudi wote…nahisi huko walipokwenda wenzetu kuna tatizo,…ngoja nifike mwenyewe nijionee.’yule mkuu akamuamrisha mwenzake waondoke, na mmoja wao akabakia kama alivyoelekezwa.

*******
Maua alihisi mwili ukiisha nguvu, na hali yake iliendelea kuwa mbaya, …na kila alipojitahidi kutembea alijikuta akipepesuka kwa kizunguzungu, ikabidi yule mwanaume amsaidie, ili wafike sehemu salama ambayo huyo mwaanume alikusudia kuwa ndiyo sehemu salama ya kuvuka huo mto,..

‘Muda umekwenda sana, inabidi tufanye kila njia tuvuke upande wa pili, ….nahisi huko nyumbani nahitaji…ndoto za kuashiri, kuitwa kwangu zinanijia kila mara..hakuna jinsi inabidi tuondoke hapa, ikizingatiwa kuwa hali yako sio njema, hapa hakuna dawa sahihi ya matibabu yako, …..’akasema yule mwanaume.

‘Tutavukaje huo mto,…huoni hao mamba wanavyotuangalia kwa uchu?,’akauliza Maua.

‘Kwasasa hivi hakuna mamba, nafikiri kuna nyama au kuna kitu kimevut akuelekea sehemu nyingine,…hakuna mamba kabisa hapo mbele yetu..hawo unaowaona ni samaki, au kenge….’aaksema huyo mwanaume.

‘Sasa tutavukaje?’ akauliza Maua.

‘Kama tulivyokuja huku ndivyo tutkavyorudi huko, ila inabidi nifanye kazi ya ziada….maana hapa nipo peke yangu, nahitaji msaada wa kupata nyama, na kutengeneza nguo maalumu, za kujikinga…nah ii na kazi inayohitaji ujasiri, na kuondoa uwoga, na ….’akasema na mara wakasikia sauti.

Yule mwanaume akamvuta Maua hadi sehemu yenye majani wakalala, kujificha, na wakawa wanangalia kule sauti ilipotokea. Ilitokea karibu na ufukwenu, kuna watu wawili walionekana wakikatisha mto, kuja upande ule walipokuwa wamejificha, walikuwa na kitu kama boto la miti iliyofungwa kwa pamoja,…mmoja alikuwa akipiga makasia na mwingine akiangalia huku na kule.

Walipofika ufukweni, wakatoka na kuanza kusaidiana kulivuta lile boti la miti, na hapo hapo yule mwanaume akawatokea kwa nyuma na kwa haraka akawagonga na rungu kwenye vichwa vyao, wakadondoka na kupoteza fahamu, …haichukua muda akrudi pale alipokuwa kalala Maua, ambaye muda wote alikuwa akiwaza jinsi gani watavuka kwenye huo mto wa mamba..

‘Hawo walikuwa askari wa mzee mhasimu, walitumwa kuja kuniua…’akasema.

‘Umejuaje kuwa ni wao, na umejuaje kuwa wamekuja kukuua?’ akauliza Maua kwa mashaka.

‘Nimewasikia wakiongea wao wenyewe…lakini sikuwapa muda wa kupambana na mimi, maana hali tuliyo nayo haihitaji kutumia nguvu nyingi, tuna safari ndefu ya kuvuka huu mto, na maandalizi yake ‘akasema huyo mwanaume na Maua akamwangalia yule mwanaume kwa mshangao, jinsi alivyoweza kwenda kupambana na hawo watu na kuwashinda kwa muda mfupi, na hata kabla hawajatulia  vyema wakaonekana watu wengine wawili tena wakikatisha mto, kuja kule walipofikia wenzake…

`Hawa watatusaidia,, nahisi kuna kikosi kikubwa kinatumwa kuja huku…..kama wameweza kuvuka hivi, lazima kuna wengine watakuja, tunatakuwa kujua wanakuja baada ya muda gani,….na sisi tutazamia huko ziwani, na njia pekee ni kujua njia waliyotokea, ili tuifuate hiyo hiyo…’akasema yule mwanume.

‘Wewe ndenda tu, mimi siwezi kuingia huko kabisa….’akasema Maua akiajaribu kuinuka kutaka kuondoka, na yule mwanaume hakusema kitu , akawafuatilia wale watu, na baadaye alirudi, japo kuwa safari hii alichukua muda kidogo.

‘Sasa inabidi tuondoke, …usiogope, kila kiti kipo tayari….’akasema na Maua kabla hajajibu kitu akawa kesahashikwa mkono, na moja kwa moja wakaelekea ziwani pale walipotokea wale watu wawili.

‘Tuna masaa mawili ya kuvuka hadi kule…hawa watu walipeana masaa mawili mawili, kwahiyo wenzao watakuwa kwenye maji kwa sasa, ina maana hawo mamba watakuwa wamefukuziwa upande wa pili..hapa na sisi ndio tunatakiwa kuvuka….’akasema huyo mwanaume.

Maua aliogopa sana, kuingia ziwani, lakini kwa hali kama ilivyo, hakuwa na njia nyingine, ikabidi afuate kama alivyoelekezwa. Alivishwa moja ya mavazi ya wale maaskari ambao walijeruhiwa,….inavyoonekan huyo mwanaume hakutaka kuwaua,….aliwajeruhi, kiasi kwamba wasingeliweza kufanya lolote.

Safari ya kuvuka ziwa ikaanza, ilikuwa safari ya kuogofya, lakini kwa ujasiri wa yule mwanaume, walijikuta wapo ng’ambo ya pili,…na lakini kabla hawajafika mbali, wakahisi kuna watu upande wa pili, ikabidi, yule mwanaume, amshike Maua na kumzamisha ndani ya maji…wakawa wanatembea danii ya maji, wakiwa wametokeza vijito vya kutolea hewa kwa nje,…..

‘Sasa hawo wasiporudi, itabidi niende mwenyewe…lakini naona kwa mbali kama kiboti chetu kinaelea. ..hakina mtu kabisa…’akasema mmoja wa wale maaskari akionyeshea kule kulipokuwa na kile kiboti, walichokuwa nacho Maua, wakati huo walishazama kwenye maji, na walikuwa wanakaribia ufukweni.

‘Nimesikia kama sauti, maji kama yanavurugika….kama vile kuna mamba wanakuja’akasema askari mmoja.

‘Haiwezekani, ….wale wanyama tuliowaweka kule hawaweze kuisha kwa muda huo mfupi,…umesikia vibaya’akasema mmoja wa askri, ambaye alionekana ndiye kiongozi.

‘Hebu fanya uchunguzi , tuhakikishe hilo maaana wenzetu wameshaingia kwenye maji’akasema huyo kiongozi, na uchunguzi ukafanyika,…na yule jamaa akasema hajaona..na kwa muda huo, Maua na yule mwanaume, walikuwa sehemu ndani ya maji wamatulia, wakiwa wameweka aina fulani ya vijiti walivyoviweka mdomoni, vikajitokeza nje, kwa ajili ya kupumulia.

Baadaye wakaingia askari wengine, na pale juu wakawa wamebakia askari watatu, na ndipo yule kiongozi akatoa maagizo, kuwa sasa atabakia askari mmoja,…na wale wakaingia,  hapo yule mwanaume hakupoteza muda, kwani alihisi kuendelea kukaa pale ndani ya maji kutamuathiri sana Maua.

Wakajitokeza, na kipindi hicho yule askari alikuwa kaka chini, akiwa hana wasiwasi, na yule mwanaume akamvamia, na kumweka chini ya ulinzi. Yule askari alikuwa na wasiwasi sana, na kila mara alikuwa kimwangalia yule mwanaume, kama vile anataka kusema kitu, lakini hakuweza kufungua mdomo wake hadi alipoulizwa;

‘Huku makaoni kuna jambo gani linaendelea?’ akauliza yule mwanaume.

‘Shughuli za kila mwaka za mavuno,…na mwaka huu tunatajia kumpata mfalme…’akasema huyo askari akitamani arudi huko makaoni akashuhudie hizo shughuli, mawazoni akiwawazia mabinti warembo wakiimba na kushangilia.

Yule mwanaume hakutaka kumuuliza maswali mengi yule askari, akamfunga vyema na kamba, halafu akamvuta kwa ndani ya kichaka, akihakikisha kuwa kamziba mdomo, na akawa anasubiri, na baadaye kwa mbali walionekana wale maaskari wakija toka kwa mbali, walionekana kwenye boti nne tofauti zikiwa na watu watatu watatu,…wakafika ufukweni.

‘Haiwezekani, yaani mtu mmoja kawazidi nguvu wote, nimewachukua nyie nikijua nimechukua majembe, ina maana huyo mtu yupoje, huyo mtu atakuwa ni nani ..’yule kiongozi wao akawa anaongea huku akiwa kajawa na hasira, akijua hataeleweka na wakubwa zake wakirudi huko mikono mitupu, na majeruhi.

‘Kwakweli hata sisi tulishangaa sana, kwani alitutokea kwa kutushitukizia, na ni mwepesi sana, na ana nguvu za ajabu. Cha kushangza ni jinsi alivyokuwa kava,….’akasema mmoja wa majeruhi.

‘Alikuwa kavaa vipi,…?’ akauliza huyo kiongozi, na wakatio huo, alikuwa akimsaidia mmoja wa majeruhi kutoka kwenye maji, …, na kabla hajamweka vyema, mara  wakavamiwa,…jemedari hakutarajia hili vamizi  hata pale alipojaribu kujietetea hakuweza ,alishitukia akigongwa kichwani na kupoteza fahamu.

Kipigo alichokipata kilimpoteza fahamu, akafungwa kamba, na kuweka pembeni na wale majeruhi Wenzake wawili walishikwa na butwaa, na hawakupata muda wa kushika silaha zao, wote wakawa wamelala chini.

‘Sipendi niwaumize, lakini najua jinsi gani mlivyolelewa na viongozi wenu,…na kuanzia sasa natak mfuate amri yangu, kama mnataka salama yenu,…’akawaambia huku akiwafunga kamba, na kuwaweka pembeni.
Baadaye yule mwanaume akamwendea Maua na kumwambia, waondoke hapo haraka, kwani kunawezekana kukatumwa kikosi kingine, na hali waliyo nayo, watazidiwa nguvu. Wakaondoka hadi walipokaribia eneo ambalo wanaweza kuona maeneo ya makazi.

‘Kwa hali ilivyo, siwezi kurudi na wewe huko nyumbani, inabidi nitafute sehemu nikuache….na kabla hawajamaliza wakaona kundi la maaskari, wakiwa wamevalai vizuri, na mmojawapo akiwa juu ya punda akiwa kapambika, …kwa jinsi walivyokuwa hawakuwa na wasiwasi, walikuwa wakitembea mwenda wa taratibu kuelekea huko makaoni.

‘Yule ni kijana wa mzee hasimu, nahisi kuna jambo ….’akasema huyo mwanaume alichofanya ni kumpeleka kwanza Maua sehemu ya usalama, na kumwambia;

Wakati kaachwa pale, akiwa kachoka, kwani mwili ulikuwa hauna nguvu, baada ya safari ndefu, baada ya mapigano, na yeye kujitolea kumsaidia huyo jamaa aaliyeficha sura yake kwa kofia ya ngozi ….na haat kujeruhiwa tena…akawa anatamani kulala tu.

‘Wewe pumzika hapa, na utakula nyama hii…mimi nahitaji huko kwetu haraka, leo najua inawezekana ikawa siku ya mwisho, nimeota kuwa nahitaji haraka sana….na kama ulivyoona, hawa watu walikuja kuniua, lakini tumeweza kuokoka…..ngoja nifike huko nyumbani haraka, halafu nitarudi kuhakikisha kuwa upo mikono salama….’akasema

Alipotoka hapo, akalinyemelea lile kundi lilokuwa likiomgozwa na Kijana wa mhasimu,…na kwa vile hawakuwa na wasiwasi, na hawakutarajia uvamizi kama ule,  walijikuta wakizidiwa na hata walipojaribu kujiweka sawa walikuwa wamechelewa, ….huyo mwanaume akamshika yule kijana wa mzee hasimu, na kupitisha kisu shingoni mwake.

‘Cha muhimu ni kufuata masharti yangu , sipendi kuumiza mtu, najua kila mtu ana haki ya kuishi, lakini kama mkikaidi, sina jinsi, itabidi nitumie nguvu…’akawaambia .

‘Mimi nataka ushinde kiume,…tupambane kama mafahali ukinishinda mimi nitatii lolote utakalosema na mimi nikikushinda kichwa chako ni halali yangu..’akasema kijana wa Hasimu, akiwa anajiamini moyoni kuwa tamashinda huyu mwanaume , kwani alishachoka kwa kupambana na hicho kikosi peke yake. Yule mwanaume akakubali.

Mapambano yakaanza, ilikuwa piga ni kupige, …na kila hatua Kijana wa mzee Hasimu, aliona kaizidiwa tofauti na alivyofikiria,…na yule mwanaume ambaye alikuwa muda wote kava kofia ya kondoo, na kutoweza kujulikana, akaona asipoteze muda, akatumia ujanja wake wa mapigano, kwa kuhakikisha anamgonga yule kijana wa mzee hasimu miguuni, hadi nguvu za miguuni zikamuishia na akalala chini kuonyesha kuwa kashindwa. Askari wake alipoona hivyo wakataka kuvamia, akawasimamisha na kusema;

‘Ahadi ni deni, acheni …fuateni anavyotaka yeye…’akasema yule kijana wa mzee Hasimu, akiwa kaka chini akimwangaili huyo jamaa kwa mshangai, kwani hajawahi kupambana na mtu hodari kama huyo, akauliza;.

‘Kwani wewe ni nani?’ akauliuliza huyo kijana wa mzee hasimu.

‘Mimi ni mjumbe maalumu kwa ajili ya taifa hil teule, nimekuja na ujumbe maalumu, na nahitajika  kuufikisha huu ujumbe huko makaoni kwenu haraka iwezekanavyo’akasema.

‘Kama ni hivyo haina haja ya kutumia nguvu, kwani hata sisi tunakwena huko huko, leo kuna sherehe maalumu, ….’akasema kijana wa mzee hasimu.

‘Wewe kwasababu ndiye mshindi panda hii punda, sisi tutatembea,..’akasema huyo kijana wa mzee hasimu, akiwa kasahau masharti aliyopewa kuwa anatakiwa kuingia makaoni akiwa juu ya punda.

‘Lakini wewe ni mkuu, unatakiwa uwe juu ya huyu punda…’akasema huyo mwanaume.

‘Hapana kwa heshima yako, na kwa vile ni mgeni wetu muhimu, nakuachia wewe upnde huyu punda’akasema huyo kijana wa mzee Hasimu, na kweli wakakubalina na kuanza kuondoka kuelekea huko makaoni, na muda huo ulishafika jioni

Mionzi ya jua linalikucha likawa linawapiga kisogoni, huku wakitembea kuingia makaoni, na wakati huo huko ndege anayeaminika kuwa ni ndege wa neema, akawa analia, …na wale askari waliondamana na huo msafara walikuwa wakijua kuwa siku hiyo ni siku maalumu siku ya maombi , ni siku ya kutoa shida zako, wakawa wanaharakisha ili wafike makaoni haraka na wao wakajumuike kwenye hayo maombi.

Hali kama hiyo haikuwa mbali kwa kijana wa mzee Hasimu, yeye ndiye aliyekuwa akiongoza huo msafara, japo akitembea kwa shida, kutokana na maumivu ya miguu , hasa kwenye magoti. Moyoni, alikuwa na maombi yake, mojawapo ni kumombea mpenzi wake waliyetupwa kwenye bonde la mauti, na ya pili na kumpata malikia mtarajia, ili awe yeye ni mfalme.

Walipofika makaoni, wakajikuta wakipita kwenye barabra zikiwa zimejaa watu wengi, na wengi wao walikuwa wameinamisha vichwa kwa heshima, na ilionekana kama wapo kwenye maombi ya hali ya juu. Na wale maaskari walikuwa kwenye huo msafara wakajikusanya pembeni, karibu na mkuu wao ambaye ni yule kijana wa mzee Hasimu, na walikuwa kama wamemzunguka, kwahiyo hakuna aliyeweza kumuona vyema, na wao wakainamisha vichwa vyao, kuashiria kuwa na wao wamejiunga kwenye hayo maombi.

Hapo huyu mwanaume naye akakumbuka, kuwa kumbe ile siku imeshafika , siku ya maombi, na kila mmoja anatakiwa kuomba, kutoa dukuduku lake, kuhusiana na matatizo yake na kile anachokihitajia, …akaona inambidi ashuke kwenye yule punda akajiunge na wanajamii, lakini kabla ya kufanya hivyo, alihitajika kuvua lile likofia….na alipolivua lile kofia , mara kukatokea mtafaruku.

Licha ya kuwa watu walikuwa kwenye maombi, lakini wengi wao walikuwa wakijiiba-iba kuangalia huko  mbele, kuangalia ni nani huyo mfalme mtarajiwa, na hasa mzee Hasimu, ambaye alikuwa karibu sana na huo msafara uliofika, nay eye alikuwa kaingiwa na kimuhe-muhe cha kumuona kijana wake, akitawaza kuwa mfalme, na kwa muda huo alikuwa anajua kabisa kuwa aliyekuwa juu ya yule punda ndio yeye, ndio kijana wake.

Na hapo akawa anaomba, akimuombe akijana wake, afanikiwe katika kazi hiyo, na kuahidi moyoni kuwa atamsaidia sana, ili waweze kufikia lengo lao, ….akainua kichwa kuangalia mbele, kumwangalia kijana wake, kwanza akashngaa, mbona lile kofia sio kama lile alilompa huyo kijana, akasema kimoyo moyo, huenda kaamua kulibadili.

Akaendelea kuomba kuwa, kijana wake huyo amuoe malikia mtarajiwa wapate watoto majasiri wataoweze kuendeleza kizazi chao, asiwe kama mtoto wake mwenyewe ambaye alimzaa huyo kijana, mtoto wake huyo alikuwa mlevi, hana ujasiri kabisa, lakini kijana wake ambaye ni mjukuu wake, akawa kachukua ujasiri wake, ….
‘Namuombe apate watoto majasiri….’akasema na kuinua kichwa kuangalia mbele, huku akitaka kusema kuwa atahakikisha kuwa eneo takatifu linamilikiwa na ukoo wake peke yake,, lakini akakumbuka kuwa siku kama hiyo hutakiwi kuomba kitu kama hicho ni mwiko…lakini alishakiwaza, na kuwaza hivyo ni kosa, akajaribu kufuta hayo mawazo na kuangalia mbele tena.

Mara akamuona yule mpanda farasi, ambaye alijua kuwa ni kijana wake, akamuona akiinua mkono , kuvua lile kofia alilokuwa kalivaa…mzee hakuamini macho yake akapikicha macho kuhakikisha,.

Mzee huyu ana macho makali sana, licha ya uzee wake huo, lakini uwezo wake wa kuona uliwazidi hata vijana , …kwahiyo pale aliona bara bara, hakuweza kuhimili…akahisi kitu kikichoma kwenye moyo kama sindano,… akadondoka chini, na kupoteza fahamu.


 WAZO LA LEO: Kila tulitendalo tukumbuke kumuweka mungu mbele, na tunapomaliza tumshukuru yeye kwani bila yeye sisi sio kitu.
 
Ni mimi: emu-three

No comments :