Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, December 27, 2012

Chema chajiuza, na kibaya hujitembeza


 Ni masiku ya siku-kuu, na wengi wetu tupo majumbani, na wale waliotoka nchi za nje, wameshasafiri kwenda makwao kuwaona jamaa zao. Halikadhalika hata sie tunaokwenda kuhiji makwetu mara moja kwa mwaka tumejihimu, na vijizawadi, kwenda kuwaona wake zetu na familia.

 Basi bwana mimi na familia yangu tukajihimu na alifajiri na mapema, ili tuwahi mabasi ya kwenda huko wetu. Tukafika Ubungo, ile kuteremka tu kwenye basi, hawa jamaa ambao kweli walivalia nguo za kuonyesha kuwa ni wafanyakazi, au wapiga debe wa mabasi wakatuvaa, kila mmoja akianaadi basi analolipigia debe, na taharuki wengine wakashindwa kuvumilia wakadaka mizigo yetu.

'Twende huku twende huku, basi letu linaondoka mapema, ....' ikawa vuta ni kuvute.

'Jamani sisi tumeshakata tiketi, tunaomba mtupe mizigo yetu.

'Tutawabebea tu mzee...twende...'yule aliyechukua mizigo yetu akasema huku akiongoza njia.

Baadaye tulipata taarifa kuwa hawa wapiga debe wakifika tu na kujionyesha kuwa wao ndio waliofanikisha wewe kufika kwenye hilo basi mtakalopanda, anapata ajira yake ya siku kutegemeana na wingi wa watu aliopata.

 Hii imekuwa ni kero hasa kwa abiria maana huwezi kujua uaminifu wa hawa watu, wanaweza wakachukua mzigo wako, na ukifika kwenye basi unaweza kukuta kitu fulani hakipo, je utakwenda kumdai nani. Na kwanini hawa watu wakufaute huko kituoni na kudaka mizigo yako, kwanini wasisubiri kwenye ofisi zao. Mimi nijuavyo chema huwa kinajitangaza, hakihitaji kupigiwa debe.

Tabia kama hizi zimekuwa kila mahali, siku hizi ukitafuta chumba, au nyumba, au kama unataka kununua kitu chochote inabidi upitie kwa dalali, na huyu anahitaji ujira wake, hapo anaweka chake cha juu, na mtu kama huyu, au kama anavyoitwa `mtu kati' anaweza akaweka cha juu kikubwa kiasi kwamba mlaji anajikuta analipa gharama kubwa isivyo halali. Na huyu mtu kati, halipi kodi.

 Ni sawa hakuna cha bure siku hizi, hata ukiuliza njia kama umepotea huenda ikafikia kulipia , ndivyo dunia ilivyo, kama wanavyosema kufa kufaana, lakini tuwe waaminifu, tuwe na utu, na utu ndio uafrika wetu, kupendana na kusaidiana...tukiondoa utu, na kujali maslahi mbele,tunaumiza wengi hasa mtu wa mwisho ambaye anajikuta anabeba gharama kubwa sana isivyo halali.

Matendo mema, bidhaa njema, na huduma njema, hazihitaji sana kupigiwa debe, na kama ni lazima kuna utaratibu wake, na kwa vile huo ni utandawazi, basi wenye hayo makampuni, wajaribu kuweka utaratibu ulio sahihi....

Blog yenu inawatakia siku-kuu njema na heri za mwaka mpya wa 2013,


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

You have made some really good points there. I looked on the internet for more info about the issue and found most people
will go along with your views on this website.
My site :: tote bags wholesale

Anonymous said...

If you wish for to improve your familiarity just keep visiting this web page and be updated with the most up-to-date information posted here.


Look at my website; gta 5 facebook

Anonymous said...

This blog was... how do I say it? Relevant!!
Finally I've found something that helped me. Many thanks!