Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, November 21, 2012

Uchungu wa mwana Aujuaye ni Mzazi-26
Malaika wa Mererani kama anavyojulikana alikuwa kakaa kwenye, kwenye chumba cha hoteli,  huku kashika shavu, alikaa vile kwa muda akiwa kajiinamia, akili ikiwa imetulia bila kuwaza chochote, na baadaye, akageuka pembeni ambapo kulikuwa na simu yake , akaichukua na kupiga namba, lakini ikawa haipatikani, ….

Alipojaribu tena mara mbili, bila kupata majibu, akasonya na kuitupa ile simu kwenye kitanda, akasimama na kutembea hatua mbili mbele, halafu akatulia, na kugeuka kuiangalia ile simu aliyotupia kitandani, akaifuata tena,….akaichukua kwa haraka, na kutafuta namba nyingine.

‘Halloh, hebu niambie huyu Malaya ambaye ulimuona akiwa na Adam, anaishi wapi, au ni hawa wanawake wa kuja toka huko kijijini?’ akauliza.

‘Huyo ni mgeni kabisa, hatujawahi kumuona mwanamke kama huyo hapa Mererani, na inaonyesha ni wale wanawake wa kijijini haswa, tena sio kijijini ni wa kutoka maporini,….kwani hata nguo, na mitindo ya kusuka, ni ya wale watu wanaotoka huko ndani ndani, maporini’akaambiwa.

‘Kwahiyo ina maana huyo mwanamke alikutana naye huko kijijini, akampa mimba, sasa ndio amakuja kuleta hiyo mimba kwa Adam, na ndio maana kakimbilia kuja huku, …unasema keshajifungua, kwa gharama za Adam,…hiyo ni pesa yangu inateketea tu…’akatulia kidogo, halafu akasema;

‘Hebu niambie ilikuwaje, mbona hamielezi kitu cha uhakika, kwasaabbu sizani kama Adam ana mke, hajawahi kuniambia hivyo,….aliwahi kuniambia kuwa alikuwa na rafiki wa kike, lakini familia ya hawo wanawake, wakawa hawamtaki, na kama ingelikuwa ni yeye,…ningelijua, na huyo hawezi akawa hawo watu wa maporini….sasa, ilikuwaje?’ akauliza.

‘Kwa undani sana sijui, kama unavyojua kuwa nay eye alikuwa kajificha kwa ajili ya kuwakimbia askari, sasa gafla ndio nikasikia kaonekana akiwa na mwanamke mwenye mtoto mchanga,..nikawauliza mrafiki zake,ndio wakaniambia kuwa Adam, alijitolea tu kumsaidia huyo mwanamke’akasikia simu ikisema.

‘Unaweza kuamini kitu kama hicho kweli, kuwa Adam, kageuka msamaria mwema wa kusaidia wanawake asio wajua, kwa pesa gani aliyo nayo, ….Adam, kapata wapi moyo wa kusaidia, mtu, ..hilo siamini, lazima kuna kitu hapo, …mimi hili sijali hata akiwa na Malaya kibao, lakini kinachoniuma ni pesa zangu..’akatulia kwa muda.

‘Sasa bosi tufanyeje?’ akaulizwa.

‘Cha kufanya kwa sasa….ni kumtafuta na kujua wapi alipo, lakini muwe makini, maana polisi wanamtafuta, wakimkamata, alivyo, anaweza kutuingiza hatiani,…’akasema na kusonya.

'Je mna uhakika yeye ndiye aliyemlipia huyo mwanamke gharama zote?’ akauliza

‘Hilo hatuna uhakika maana hatujaonana naye tangu alipoonekana na huyo mwanamke’akaambiwa.

‘Sasa mtafuteni, na mjue wapi walipo, au huyo mwanamke anaishi wapi, nataka nikaonane na huyo 
mwanamke uso kwa uso, ili anijue kuwa mimi ni nani’akasema na huku akiwa kakunja ngumi.

‘Sawa bosi, tutamtafuta hawezi kujificha ndani ya mji huu, bosi…’akaambiwa.

‘Na nyie msipompata, kazi hakuna….’akasema na kuitupa ile simu kitandani tena akatulia na kurudi kukaa pale kwenye kiti chake, huku akiwa kaangalia juu, safari hii alikuwa kashika kidevu, akayarudia yale maneno ya mwisho ya yule mtu aliyempigia simu.

‘Bosi…bosi….bosi ...’ akasonya na kutulia, na mawazo yake yakahama kutoka kwa Adam, na kuanza kuwaza tatizo alilo nalo ambalo limemfanya hadi ajifungie mwenyewe kwenya kifungo cha hiari, akawaza jinsi gani atafanya ili aweze kutoka humo,….

*******

Malikia amekuwa kajifungia kwenye hicho chumba kwa siku nzima, hakutaka kutoka nje kabisa, kwani polisi walikuwa waklimtafuta, baada ya kugundulikana kuwa yeye ndiye aliyewaajiri vijana kwa biashara hiyo na madawa ya kuelevya. Hiyo sio mara ya kwanza kutokea jambo kama hilo, na kitu alichokizoea. Kinachomsaidia ni kuwa kama kuna mpango maalumu wa kusakwa wauza madawa ya kulevya, huwa ana watu wake wanaompa taarifa.

Siku hiyo alipopata taarifa, ndio siku alipopokea mzigio mkubwa, na baada ya kuusambaza kwa mawakala, wake, ndio akapokea simu kutoka kwa rafiki yake mmoja ndani ya polisi, ambaye alimpa taarifa kwamba kuna operesheni maalumu ya kukakamata wauza madawa ya kulevya na akaambiwa nini cha kufanya. Akakumbuka jinsi alivyoambiwa;

‘Nakupa taariha hii muhimu, kuwa kuna opereshemi maalumu ya kamata kamata, wauza madawa ya kulevya, na safari hii wameagiza vijana wageni kabisa, ambao sio rahisi kuwafahamu….’akaambiwa.

‘Sasa nifanyeje, maana kila siku nawapatia mshiko wenu, kwanini safari hii iwe hivyo, au hamjamkatia jamaa yetu fungu lake?’ akauliza.

‘Hilo ni jambo la kawaida ni moja ya operesheni zetu, cha muhimu ni wewe kuhakikisha huonekani kabisa,..’akaambiwa.

‘Yaani nijifunge mwenyewe, haiwezekani,…unajua kuna mzigo mkubwa, nispousimamia hawa watu wangu wanaweza wakanizika….’akalalamika.

‘Inabidi iwe hivyo, mpendwa, hali sio shwari,…kama inawezekana nenda kijijini kakae kwa muda, kukipoa ndio urajee’akaambiwa.

‘Niende kijijini, na huo mzigo, itakuwaje,…ndio nimeusamabza hata senti moja sijashika….hilo haliwezekani’akasema huku akikunja uso kwa hasira.

‘Basi tafuta chumba, jifiche, sehemu ambayo hakuna mtu anayepajua, na usitoke kabisa, sisi huku tutajua jinsi gani ya kutuliza hili jambo, kinamna..unasikia usitoke kabisa..’akaambiwa.

‘Nikifanya hivyo nitakusanya je pesa zangu, hamjui mshahara wenu unatoka wapi, ..’akasema kwa hasira.

‘Sikiliza mpendwa, anayeongoza hicho kikosi ni afande Komando..’akasema na Malikia akashituka kama vile kashituliwa na umeme, akasema kwa sauti ya wasiwasi.

‘Unasema huyo mwanaume mwenye sura mbaya karudishwa tena hapa…mungu wangu, …’akasema huku akiangalia huku na kule, kama vile anaogopa kuwa huyo Komando atatokea muda wowote hapo alipo.Kwa muda hup alikuwa kavalia kikazi, makoti na nguo ambazo huwezi kumzania kabisa anafanya shughuli kama hiyo.

‘Kama ni huyo mtu, nitatafuta chumba ambacho hakijulikani kabisa…mungu wangu, siwezi kwenda jela tena’akasema huku akiangalia huku na kule.

‘Kama utafuta ninavyokuagiza, hawezi kukuona, hawezi akazunguka kile hoteli, …na ikibidi tafuta hoteli za vichochoroni, au nyumba ambayo mtu hawezi kuhisi kuwa unaishi…kama unavyomjua huyu jamaa ananusa kama mbwa, sasa ni vizuri ukawa makini…..ukiona ishara yangu ujua yupo nyuma yako, …’akaambiwa.

‘Sawa, nitapambana naye, namuogoap kwa vile alishawahi kuniweka ndani, lakini safari hii tutakua naye sahani moja, na ikibidi …..anaweza akatangulia’akasema na kukumbuka jinsi gani alivyoweza kukamatwa na huyo askari.

Siku zote anapokamatwa huwa ana mbinu nyingi za kupambana na askari wa hapo na wote anawafahamu vyema, anaweza akatumia pesa au akatumia urembo wake, lakini kwa huyu askari, ilishindikana, na akajikuta akiswekwa ndani, na kama isingelikuwa ukaribu wake na wakubwa wengine, angelifungwa muda mrefu, lakini huyo jamaa alipohamishwa hapo, akafanya mipango akatolewa.

‘Huyu mtu nina kisasi nay eye…’akasema kimoyo moyo. Lakini ni nani atanisaidia kwa kazi hii, maana kama huyu jamaa yupo, lazima nilipize kisasai, hawezi kunizalilisha kiasi hiki, mimi malikia wa Mererani, nisweke ndani, na nizalilishwe na wafungwa…hapana, lazima nimuonyeshe kuwa mimi sio moto wa karibu.

`Nitahakikisha safai hii, anatangulia kuzimu…….’akasema huku akiwa nani anaweza kumtumia kwa kazi hiyo, anajua vijana wake wote wanamuogopa sana huyo askari, na hapo akakumbuka, kuwa Adam hamjui huyo askari, anaweza kumtumua kuifanya hiyo kazi. Lakini Adam hajawa jasiri wa kuweza kuifanya hiyo kazi, na hata hivyo, badi mi mzembe, ….

‘Hata hivyo ninaweza kumkamatisha tu, lakini sasa ndio yupo na huyo Malaya wake, sijui nitampata wapi?’ akajiuliza

Akakuna kichwa, akijilaumu, kwanini alimuamini huyu Adam, tangu amuingize kwenye shughuli zake, amekuwa ni tatizo, na badala ya kumletea faida imekuwa ni hasara, imebidi atumie pesa nyingi kumuokoa na hata kumshikia dhamana….

‘Huyu mwanaume ana bahati sana, yaani namlea kama….nini sijui, hata siwezi kujua jinsi gani ninavyomthamini, kama vile mume wangu, ajabiu kabisa, sijawahi kufanya hivi katika maisha yangu, lakini ndio huyo anataka kunitosa.

‘Kwanza hivi anajiona ana nini cha maana, …huyu mtu ana bahati sana, hajui kuwa mimi sina mapenzi na mtu mzigo, mtu asiyena faida, kama isingelikuwa huyo mjomba wake, kwa vile nilitaka nimtumie ili nimuingie mjomba wake, nisingelimuingiza kwenye anag zangu...Lakini sasa nanona muda umefika, nitamtumia yeye,….siku zake zimefika, …’akasema huku akikuna kichwa.

‘Huyu mjomba bado sijamweka mikononi, na ili nimuweke mikononi nilitakiwa nimtumie huyo mwanaume, lakini mtu mwenyewe haelekei, sasa nifanyeje, ..’akawa aongea peke yake kama vile kachanganyikiwa.

‘Sasa tena hii habari ya kuwa na mwanamke mwenye kichanga, mbona huu sasa ni mzigo, maana hataweza kutulia kwenye kazi, …mimi siwezi, ..siwezi kabisa kulea mwanamke na mtoto mchanga…kwanza lazima nijua huyu mwanamke ni nani? Nikimpata nitahakikisha namtolea hasira zangu zote’akasema huku akijaribu kufumba macho.

`Kwa mtaji huu, lazima nitoke humu, …’ akasema na kuanza kutafuta nguo na nywele za bandia za kujibadili, …Lakini akili yake ilikuwa ikimuwaza huyo Komandoo, anamjau vyema, hata ujibadili vipi, kama akikamia kukukamata atakupata tu, ….ananusa kama mbwa…..

Akajiweka sawa kutaka kutoka, na kabla hajainua mguu kusogelea mlango, akasikia mlango ukigongwa, moyo ukaanza kwenda mbio,..mwili ukamsisimuka…akaangalia huku na kule,……..mlango uliopo ni mmoja tu, dirishani huwezi kutokea,…..akaangalia mvunguni, kama anaweza kuiingia, na hapo akakumbuka mzigo aliouficha mvunguni…

Mlango ukagongwa tena….

NB Nipo internet cafe, ...

WAZO LA LEO :Maisha ni kupambana ili upate mkate wako wa kila siku, ukikosa leo, usikate tamaa.


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Mbona kimiya mkuu