Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, November 16, 2012

Uchungu wa mwana Aujuaye ni Mzazi-24




‘Mzee mwenzangu, mimi nakupa siku tatu, kama huyo kijana wako hajaonekana, sisi hatuhitaji zaidi, tunamuhitaji malikia mtarajiwa, kama sheria zilivyo , kuwa mumewe akifariki, malikia anahitajika kutolewa ahpo alipokuwa akiishi na kuwekwa wazi kwa ajili ya mume mwingine…’akasema mzee hasimu.

‘Huyu malikia hastahili kukaa kwenye majozi kwa muda mrefu,taiaf lake linamuhitaji, anahitajika kukabidhiwa majukumu, ..mimi nawajua sana nyie, kwanza mumetumia mbinu za kumchukua, na sasa mnaanza kuumbuka, ….’akasema huyo mzee akiwa anamwangalia mzee mwenzake ambaye alikuwa katulia, na kimiya, akimsikiliza kwa makini.

‘Hebu jiulize mzee mwenzangu, toka lini, katika historia ya taifa letu hili, na hata huko tulipotoka hadi tukafik hapa kuanzisha hili taifa, lini, mfalme mtarajiwa, mtu ambaye tunamtegemea kuwa kiongozi wa taifa hili, aliwe na mamba…hii ni ishara mbaya kwenu, manhitajika kuliwazia hilo kwa makini, kuwa kuna kitu mumekosea…..’akasema mzee hasimu, na kutulia kwa muda, na mzee mwenzake alipoona kuwa huyo mzee hasimu katulia, na hana jingine la kuongea akasema.

‘Kwanza kabisa niwaambia kuwa mlilolifanya ni kosa kubwa,na mnajua nini sheria inasema nini kama hilo mlilolisema sio kweli, niwaulize ni nani kawaambia kijana wetu kaliwa na mamba,…hizo taarifa mumezipata wapi, na kama kungelikuwa na tukio la msiba, mngelisikia baragumu, mungeliona taratibu za msiba…hamuoni kuwa mnatuzulia msiba?’ akauliza Babu , huku akionyesha kushangaa, jinsi taarifa hizo zilivyowafikia hawa watu, na ilikuwa ni siri yao.

‘Hakuna siri hapa duniani, hasa jambo hilo likiwa ni msiba, najua mlifanya hivyo ili mpate muda wa kujipanga, ili muweze kuweka mambo yenu sawa, na ikiwezekana mmpate mrithi wake, hilo hatuwalaumu sana, kwasababu kila mmoja anajua uchungu wa kupoteza kijana muhimu katika familia…lakini sisi tunaomba taratibu zifuatwe, ili kuliwezesha taifa letu hili lifike kule tunakotarajia’akasema mzee wa sheria wa upande wa mzee hasimu.

‘Sisi sheria tunazijua sana, na taratibu za msiba zipo wazi, haiwezekani kutokee msiba katika familia, watu watulie kimiya,…hilo mbona hamlioni. Na wenzetu hili mlilolifanya linatuweka aktika mshaka na nyie,, kuwa huenda mna lengo baya kwetu sisi na familia zetu, ….’akasema mzee mmojawapo.

‘Lengo gani baya mzee wetu, sisi tumefanya nini kibaya, kama wenzenu, tumetimiza wajibu wetu,. Kuwa tumesikia taarifa ya msiba, tukaja kutoa pole, hizi ni taratibu zetu. Natumai kama tungelikaa kimiya mngelikuja kutulaumu’akasema mzee wa sheria upande wa mahasimu akijua kuwa hilo walilolifanya ni linaweza kuwaletea matatizo baadaye.

‘Tumewasikia, na tunachowaambia ni kuwa taarifa hizo sio za kweli, na kama mna ushahidi kuwa hiz taarifa ni za kweli tunauomba huo ushahidi, na kama hamna ushahidi, tunaomba mfute kauli zenu, na mwende mrudi na kipozoe, ..’akasema mwanasheria wa wazee wa babu.

‘Kwanini tufanye hivyo wakaitu tuna uhakika na hilo, …hatuhitaji kufanya hivyo’aaksema mzee hasimu kwa ujasiri.

‘Sawa kama mnajiamini kw hilo, basi sisi tunawaambia kuwa, kabla ya hizo siku tatu, kijana wetu ataonekana makaoni akiwa na mke wake, na najua siku za kukalia kiti chake zimeshafika, hatutataka tena kuzungushana, maana hapa mumekubali wazi kuwa ndiye mfalme mtarajiwa, na anastahili kukikalia kiti hicho, kauli yenu na wajumbe wenu wamelithibitisha hilo’akasema babu.

‘Ni mpaka…..maana hizi ni ndoto, hilo najua ni kupoteza muda tu, kama kweli yupo hai, tunamuhitaji afike na malikia mtarajia makaoni, na siku hizo tatu zikipita, tutakuja rasmi na anayestahili kuwa mfalme, Na tukija hapa tutamchukua kwa nguvu, na moja kwa moja tutamtawaza huyo anayestahili kuwa mfamle maana naona nyie mtatupotezea muda wetu,….hilo tunakuthibitishia, na mkikaidi, mnajua nini kitawatokea,..hamuoni majanga yanavyowaandama wenzetu…tusipoteze muda tena’akasema mzee hasimu.

Baadaye wakaondoka huku wakichekea kwa kebehi, na kuwaacha wazee wa kundi hili wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini, na kila mmoja akiwaza ni nini cha kufanya, kwani siku tatu, sio nyingi, na siku hizo zinaanzia muda huo.

‘Sasa mzee wetu tufanye nini, maana kauli yao hiyo ni nzito, na tumaikubali, hii ina maana kuanzia sasa tupo kwenye mtihani, tunahitajika tufanye juhudi za makusudi,…’akasema mzee mmojawapo.

‘Hilo wazee wenzangu lisiwatie shaka, kama limeandikwa halina mjadala, kwanza kabisa naomba mnipe muda wa leo, kesho tutakuwa tumefikia muafaka, lakini leo nahitaji muda wa kulitafakari hili jambo. Na pili tunahitajika kumuelezea vyema malikia mtarajiwa, ili asiwe na wasiwasi, na hili  linategemea wananchi wetu, kutokumshinikiza na tuhuma hizi, …kama ni kweli imetokea hivyo, tutawajibika’akasema huyo mzee wao.

Mzee yule alipotoka pale hakurudi kwake, moja kwa moja akaanza safari yake kwenda huko chimbukoni kwao, alijua kuwa huko ataweza kujua kila kitu , na nini akifanye kwa wakati kama huu, na kama kweli kijana hayupo hai, itabidi abakie huko kwa muda. Na kabla hajakatiza eneo lao, akakutana na malikia mtarajia, akionyesha huzuni kubwa usoni,

‘Babu naomba uniambie ukweli, je mume wangu yupo hai, au hayo wanayosema watu ni uwongo, na kama ni uwongo, kwanini mume wangu hajarudi, yupo wapi, na kwanini hamuniambii kinachoendelea hapa, na wakati mimi nastahili kuyajua hayo..’akasema malikia mtarajiwa.

‘Haya nitaongea na wewe, kwasasa hivi naitajika kufanya jambo, ila nakuahidi kuwa mume wako yupo hai, na hawo wanaozusha hivyo, ni kawaida yao, …..’

‘Babu…mimi nina mashaka…’akasema na akasita kumwambia kuhusu lile ua, kwani alikuwa bado na mshaka nalo, kwani ua lile lilikuwa na afya yake kabisa, hakikupita hata saa moja, liwe limenyauka na kukatikakatika…akatilia mashaka , akaona arudi tena kuliangalia vyema , lazima kuna kitu kimefanyika.

********
Wakati hayo yakiendelea mzee Hasimu, alifika makoni mwake na kikundi chake, na walimkuta kijana wao akiwa amesharudi, na wakaanza kumhoji amefikia wapi kwa kazi waliyompa.

‘Nimefukuzwa na askari wao, …wamenifukuza kama mwizi, hawajui kuwa mimi ndiye mfalme wao mtarajiwa’akalalamika Yule kijana.

‘Wamekufanyaje, kwani ulitimiza yale tuliyokuagiza uyafanye?’ akaulizwa.

‘Nilifanya vyema kabisa, mimi wakati naongea na huyo malikia mtarajiwa, wenzangu walikuwa wakifanya yale tuliyokubaliana, na yalileta matunda, kwani Yule binti, alipofika kuliangalai lile ua lake, alilikuta limesambaratika, akaanguka na kupoteza fahamu’akasema.

‘Limesambaratika, ..?!..kwani ndivyo tilivyowaagiza, ilitakiwa mlilegeze kwa moto, ili lionekane limenyauka, na sio kuliharibu, hamuoni hapo mtakuwa mumetilia shaka, …’Mzee hasimu akasema.

‘Ina maana hilo ua lilikuwa limestawi vyema, mimi nakumbuka mtaalamu wetu alituambia kuwa kama ua hilo lipo na afya yake huyo kijana atakuwa bado yupo hai, mbona basi tumekurupuka kwenda huko?’ akalalamika mzee mmojawapo.

‘Hilo sikuwa nimeliwaza mapema, na sikuwa na imani na hizo kauli za yule mtaalamu, mimi huwa simwamini sana mambo yake’akasema mzee hasimu , huku kiwaza hilo alilolifanya kijana wake, na ndani ya moyo wake, akawa anaingiwa na mashaka na matukio hayo, kama kweli huyo mtaalamu alivyosema ni sawa, basi,  ina maana huyu kijana atakuwa bado yupo hai,….

‘Hata mimi nalitilia shaka hilo, maana lile ua, kwa taarifa za Yule mtaalamu, ndio dira ya kuomuonyesha malikia mtarajiwa kuwa mume wake bado yupo hai au keshafariki, na kama walilikuta hilo ua bado linachanua basi huyo kijana yupo mahali, na yupo hai’akasema mzee wao mashuhuri.

‘Na kama yupo hai, hapo tutahitajika kuwajibika,…na mjue tumeshafika kule kwa wazee wenzetu, tukahami, kitu ambacho, hakipo, na walituasa kwa hilo kuwa turejee na kuja kufuta kauli yetu, tukakana,sasa kama ni kweli kuwa huyo kijana yupo hai, tunahitajika kuwajibika kwa hilo,…na mnajua adhabu yake?’ akauliza mzee wa sheria.

‘Adahabu yake ni nini?’ akaulizwa.

‘Mnapomzushia mwenzenu msiba, nyie mnawekwa kundi moja na wachawi, na adhabu ya mchawi mnaijua, …’akasema huyo mwanasheria akiwaangalia wazee ambao walibakia mdomo wazi wakiwa hawaamini hiyo kauli, walianza kuingiwa na wasiwasi.

‘Lakini adhabu zetu zote, zinaamuliwa na wajumbe, kama nusu ya wajumbe wakikubalina, mzee wetu ambaye ni mkuu wa familia na koo zote, unahitajika kwanza kujiuzulu, pili kuondoka kwenye eneo takatifu, ili adhabu kali itolewe juu yako…’akasema mwanasheria wao huku akionyesha wasiwasi, kwa kauli ile, lakini ndivyo ilivyo, na anastahili kuliweka hilo wazi.

‘Adhabu gani nyingine, na sisi ndio tunaotunga sheria, kama hicho kipengele kipo, tunahitajika kukiondoa haraka’akasema mzee hasimu na wajumbe wenzake wakamwangalia kwa kushangaa.

‘Hatuwezi kukiondoa, na ukumbuke kuwa wenzetu pia wana mwanasheria wao, ambaye kwa pamoja tulikubaliana hilo, kuwa tutazilinda hizo sheria, kwa mamlaka mliyotupa, na najua haweze kwenda kinyume chake, …ila kinachoweza kusaidia hapo ni kuwa wajumbe ndio wenye maamuzi ya mwisho wa kuzitekeleza hizo sheria kwa kura zao’akasema mwanasheria huyo.

‘Wajumbe ni nyie, na sisi tupo wengi zaidi, hapa kwanza ni sisi sote tuwe na msimamo mmoja, kuwa hiyo adhabu haiwezi kutolewa kwetu,  kwani taariza hizo zipo, na kwanini tufikie kuwaza hilo, kama huyo kijana yupo hai, inabidi tulifanyie kazi hilo’akasema mzee hasim.

‘Tulifanyie  kazi hilo kazi kwa vipi,kama yupo hai, sheria ipo wazi mzee, mimi naona tumeharakisha kukimbilia huko, niliwashauri mapema kuhusu hilo, mkasema mna ushahidi kuwa huyo kijana kaliwa kweli, sasa habari zimekuwa kinyume chake,…tuweni makini kwa hili, na kuanzia sasa tunahitajika kuwaweka wajumbe sawa, ili wawe pamoja na kauli yetu iwe nzito’akasema

Mzee hasimu akamwangalia yule mzee mwanasheria, na kimoyomoyo akasema; `huyu anahitajika kuondolewa kwenye hii kazi, anaweza kutusaliti kwa msimamo wake huu, hawa watu wenye msimamo mkali, hawastahili kupewa madaraka kama haya’ halafu akatikisa kichwa na kusema;

‘Hili swala, niachieni kwanza nilitafakari, nahitaji muda wa leo kulifanyia kazi, baaadaye nitawaita tujue nini cha kufanya, naombeni tukitoka hapa msimamo wetu uwe ni huo huo, kwasababu hatukukurupuka tu, tulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwa kijana wao hayupo hai, sasa kama hali imebadilika, sisi kama wahasimu tunahitajika kulifanyia kazi…’akasema kwa sauti ya ukali.

‘Lakini naomba tuwe makini kuanzia sasa , tufuate utaratubu, maana uchaguzi unakaribia,, tukienda kinyume,wananchi hawatatuelewa, tunahitajika tujipange vyema kuonyesha kweli tunahitajika kushika madaraka, mkumbuke wenzetu huko chimbukoni tulipotoka wanatufuatilia kwa makini sana’akasema mwanasheria wao.

‘Wewe usiwe na wasiwasi, …huku ni kwetu na hili taifa ni letu, hawawezi kutuingilia maisha yetu huku, na tukiamua kuwa hivi ndivyo msimamo wetu, wao hawawezi kuingilia, cha muhimu ni kujipanga na kuwa tayari kwa lolote lile. Hilo msiwe na shaka nalo,…mimi ni mzee wenu najua nini cha kufanya’ akasema huku akiinuka kuashiria kuwa kikao kimekwisha.

Mzee huyo alipotoka hapo akaenda kwenye chumba chake maalumu na kuanza kutafuta njia ya haraka, kwani kweli inaashiria kuwa huenda huyo kijana wa mhasimu wake yupo hai, na kama yupo hai, inabidi jambo lifanyike, akatoka pale na kumuita jemedarii wake wa majeshi;

‘Sikiliza tuma kikosi maalumu, cha makomandoo, wamtafute huyo kijana wa wenzetu, kwani tunahisi huenda bado yupo hai, na tunahitajika asiwe hai, fanyeni mfanyalo, lakini mwisho wa siku tunahitaji mabaki yake, yakionyesha kuwa kweli aliliwa na mamba,…’akaagiza huyo mzee,

Jemedari akamwangalia yule mzee, kusubiri amri nyingine, na alipoona hakuna jingine, akasema;

‘Hilo limefanyika mzee, ..usiwe na shaka, kazi hiyo itafanyika kama ulivyoagiza’akasema na kuondoka.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Someone necessarily help to make severely articles I'd state. That is the first time I frequented your website page and to this point? I surprised with the analysis you made to make this particular submit incredible. Excellent job!
Feel free to surf my blog ; casinoonlinereview9.co.uk