Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, November 12, 2012

Uchungu wa mwana Aujuaye ni Mzazi-20




Kais, aliona ajabu sana, kwake ilikuwa kama vile anaangalia sinema ya ukweli, jinsi gani yule mwanaume alivyojitosa kuokoa maisha ya mtu mwingine, bila kujali kuwa yeye mwenyewe anajiingiza kwenye hatari, kwani kwa muda huo mamba wengine walishajitokeza, na kila mmoja akijaribu kuruka ili awahi kumnyakua yule mwanamke, wakiwa wamepanua midomo yao na kuonyesha meno yao makali. 
Yule mwanaume alijirusha kama wanavyoruka magolikipa kudaka mpira, na mruko ule alitua juu yam domo wa yule mamba, akaukanyaga kwa juu, na huku mikono yake ikiwa inamuwahi yule mwanamke kumsukuma mbali na ule mdomo wa mamba, uliokwisha panuliwa,na kwa haraka ya ajabu akajipinda, ili kuweza kumuinua yule mwanamke.Yote hayo yalifanyika karibu na ule mdomo wa mamba.

Nafikiri yule mamba alishikwa na butwaa maana alishajiandaa kuweka kitoweo mdomoni,lakini ghafla kimeondolewa kwa haraka, na huyo mwanamke akarushwa kwa mbele, na kwa vile isingeluwa rahisi kufanya mtendo hayo kwa haraka, na kwa wakati mmoja, mamba akabahatika kumdaka yule mwanaume mguu wake.

Ilikuwa sasa ni vuta ni kuvute, Kais alipoona hivyo, akajua na yeye hapo anahitajika kutoa msaada, licha ya kuwa nay eye huenda anajiingiza kwenye hatari, lakini akaona ajaribu bahati yake. Maisha ya kuishi porini peke yake yalishamjengea ujasiri, na moyoni alimshukuru bibi yake aliyemlea kwenye mazingira ya kuweza kusihi katika halii yoyote ile.

Alichofanya pale ni kuangali huku na kule, na kwa bahati nzuri, karibu yake kulikuwa na tawi la mti, wenye mwiba, lililovunjika, akalichukua na kukimbilia pale ufukweni, na kwa haraka akalichomeka, kweney ule mdomo wa mamba uliokuwa umefunuka kidogo, ukiwa umeshikilia mguu wa yule mwanaume. Aliweza kuupenyesh ule mti wenye mwiba, mdomoni mwa yule mamba huku akiaangalia wale mamba wengine wasije wakamrukia.

Naona ni kwa  mipango ya umngu, maana kutokana na ile mimba ule mtu aliouchomeka mdomoni wa yule mamba, yule mamba akihisi maumivu, akapanua domi lake zaidi na ndipo yule mwanaume akaweza kuvuta mguu wake.

Yule mwanaume, akajikokota hadi kwa yule mwanamke, na kumuinua akaanza kutembea naye kwenda mbali na ule mto, bila kujali kuwa kajeruhiwa, bila kumjali yule aliyemsaidia kumuokoa, alichokuwa akihangaika nacho ni yule mwanamke ambaye kwa muda huo alikuwa kaduwaa tu akishangaa kuona yale yanayotokea.

Kais, akawafuatilia kwa nyuma, huku akiangaza huku na kule, kuona kama kweli kuna usalama, na kuhakikisha kuwa hakuna watu wengine, asije akaingia mikononi mwa maadui, na alipohakikisha hilo, akawafuata hawo watu wawili hadi sehemu ambayo ilikuwa mbali na ule mto, na ilionekana ndio kutakuwa makao yao ya muda.

‘Umaumia sana, ni bora kwanza tukatibu hayo majeraha ya meno ya mamba, yanaweza kukuleta madhara..mguu unaweza ukaoza’akasema Kais. Yule mwanaume kwanza alitupa jicho kwa Kais, lakini kwa vile lile kofia lilificha kilakitu usoni mwake, Kais hakuweza kumtambua vyema.

Yule mwanaume akaangalia mguu wake, na ndipo akagundua kuwa kweli kaumia, na anahitaji matibabu, akainuka kwa shida na kuanza kuangali huku na kule, kutafuta dawa za majani.Ilionekana kuwa ni mtaalamu, kwani aligundua aina ya majani, na kuna dawa alikuwa nazo, akayatafuna yale majani na kuchanganya na ile dawa, akaanza kujiganga mwenyewe.

Kais aliona jinsi gani, yule mwanaume anavyopata taabu kuyaweka yale majani kwenye yale majeraha yake, akamsogelea na kuyachukua yale majani na kuanza kumsaidia kuyaweka kwenye yale majeraha yaliyosabaishwa na meno ya mamba. Na wakati anafanya hivyo, akawa mara kwa mara anajiiba kumwangalia yule mwanaume, hakuweza kuiona sura ya yule mwanaume vyema zaidi ya macho yaliyopo kwenye matundu ya lile likofia alilovyaa, lile likofia lilikuwa na sehem ndogoo ya matundu ya macho mdomo, na puani, na huenda huyu jamaa alifanya hivyo kwa sababu maalumu.

Kila alipotupa jicho, alikutana na macho ya yule jamaa akimwangalia, na alihisi tabasamu au hali fulani ambayo hakuweza kuigundua. Alipohakikisha kuwa keshamweka majani na ile dawa  kwenye yale majeraha, na kuyafunga vyema kwa kamba ya mti, akajiinua na kutaka kusogea pembeni, na katika kutaka kusogea kule akawa kajikwaa na kutaka kudondoka.

Yule mwanaume, ambaye kwa muda ule alikuwa akigugumia kwa amuimvu, maana ile dawa huvuta sumu iliyoingia mwilini, na ilitakiwa iwe hivyo, ili sumu yote iliyotokana na yale meno machafu ya  mamba itoke mwilini,vinginevyo mguu huo ungeliweza kuoza.Na dawa hiyo ikifanya kazi, kuna maumivu makali sana unayapa, na inatakiwa ujasiri wa hali ya juu kuvumilia, na mara nyingie mtu akifungwa hizo dawa,anatakiwa awe amefungwa mikono na miguu, ili asiweza kuiondoa ile dawa.

Kais alipojikwaa, akawa anaserereka kuanguka, yule mwanaume bila kujali yale maumivu anayopambana nayo akainuka, na kwa haraka akafika na kumdaka Kais, na Kais akawa kalalia mguu wa yule mwanaume,na akawa kama anaangalia juu, macho yake yakawa yamatizama moja kwa moja yule mwanaume..aliona macho kupitia kwenye matundu ya ile kofia.

Yule mwanaume akawa anahangaika kumweka sawa, huku akitaabika na maumivu. Kwa Kais muda huo alishasahau kuwa mwenzake yupo kwenye matseo ya mauimvu, na mguu mmoja hauna nguvu, kwahiyo alitakiwa ajitahidi ainuke kwa haraka, ili kumuokoa mwenzake kutokana na yale maumivu, lakini alijikuta akijilegeza ili tu apate mwanya wa kuyaangalia yale macho, na kutamani kama ingeliwezekana angelifikia lile kofia na kuliondoa, ili aione sura ya huyo mtu….

Kais, alihisi aina ya mvuto fulani, nafsini mwake, ni kama vile anamjua huyo mwanaume,ni kama vile amempenda kwa muda huo mfupi, hata kama hamjui, lakini itakuwaje kupenda mtu usiyemjua, na utampendaje ilihali uso hauonekani, akajiuliza bila kupata jibu….hisia na nafsi ikawa inatamani kama ingeliwezekana awe karibu yake hivyo hivyo.

‘Aaah,samahani ,nimesahau kuwa wewe ni mgonjwa…’akasema Kais, na kujikakamua kujinua kwenye miguu ya yule jamaa, ambaye alishazidiwa na kujaribu kumweka Kais chini ili aweze kujituliza, na katika harakati hizo, akawa kazidiwa na kujilaza chini huku akikunja uso kwa maumivu makali. Na muda huo Kais alikuwa kalala kwenye paja la yule mwanaume, na ndipo Kais akagundua kosa lake na kusema hivyo.

‘Unisamehe, maana haya maumivu, …aaah, ni makali kweli  sijui kama nitaweza kuyavumilia,….’akawa analalamika yule mwanaume na kwa muda huo akawa anaipeleka mikono yake kutaka kuindoa ile dawa. Kais alipoona hivyo, akajua hapo asipofanya juhudi ya ziada, huyo mwanaume mguu utaoza na utaishiwa kukatwa. Akaona ajitolee kwa kile kinachowezekana, na akitumia ujasiri, wa hadithii za bibi, akajitolea bila kujali hali yake aliyokuwa nayo.

‘Utanisamehe, inabidi nifanya hivi ili kukusaidia….’akasema huku akamsogelea yule mwanaume na kumshika mikono yake yote miwili kwa mbele, na kwa kufanya hivyo, wakawa wamelaliana, Kais akiwajuu ya kifua cha huyo mwanaume ili kuweza kuzuia ile mikono isifike miguuni, huku kaishikilia mikono ya yule mwanaume mbali kabisa na kichwa, ilibidi atumie nguvu zake zote ili aweze kumzidi yule mwanaume , na hiyo ilisadia , kwani yule mwanaume kila alipojaribu kuinua mikono yake,  alishindwa, na hata alipofanikiwa kumzidi nguvu 

Kais, alijikuta mikono yake ikimshika mwili wa Kais, na akimshika, anatahayari, na kurudisha mikono yake.
Hali ile iliendelea, hadi muda ukapita sana, na dawa ikawa imefanya kazi yake,na maumivu yakaanza kuisha kidogokidogo na taratibu, hadi maumivu yakaisha kabisa. Na wawili hawa wakawa wametulia, huku Kais akiwa bado kifuani mwa huyu mwanaume, kalowana mijasho, na sasa kilichokuwa kikifanya kazi ni hisia za miili yao ambayo imekuwa imeshikana na kunataka kwa muda mrefu.

Mungu alipoumba mume na mke, aliwajenga kama sumaku, kama mmoja akiwa karibu na mwenzake kwa muda mrefu kuna hali ya mvutano inaweza kuwashika, na hasa ikiwa watu hawo hawana udugu wa karibu, na zaidi watu hawa wawe na hisia za namna ya kupendana, au kutaka kupendana.

Kwa ujumla hali hii ilimuathiri zaidi Kais,na ikizingatiwa kuwa yeye amekuwa porini kwa muda mrefu peke yake, akajikuta mwili wake wote ukilegea, na akajikuta akivutika na hisia za mwili wake na kufanya kile asichokitegemea, licha ya kuwa mwenzake alijaribu kujizuia, lakini mwishowe nay eye akajikuta akivutika kufanya kile mwenzake alichokiwa akikitaka.

Kilichokuja kuwashitua ni kikohozi,…na wote wakageuza vichwa vyao kutizama ni nani huyoo aliyewavurugia maisha ya dunia nyingine, maisha ambayo mungu mwenyewe anajua kwanini aliyaweka hivyo, kwani binadamu akiingia kwenye hisia za dunia hiyo ya hisia, anakuwa hajijui tena,  na akirudi kwenye maisha ya kawaida, huanza kujijutia, na wengine hata kulaani kuwa kwanini wamerudi kwenye dunia hiyo ya kawaida.

‘Oooh,…’akasema yule mwanaume na kuinuka sehemu ya kichwani na kukaa kwa haraka, hakuweza kusimama, kwani Kais alikwa nusu kamlalia,na alipogundua nini alichofanya akawa katahayari, akajifuta mchanga kwa haraka huku akiangalia kule kikohozi kilipotokea, akagundua wajibu wake, na alichofanya na kumuinua Kais ambaye alishazama kwenye kausingizi na kumlaza chini na wakati anafanya hivyo, akawa anamuangalia usoni, na baadaye akasema;.

‘Unanikumbusha mbali kweli wewe binti….’aliyatamka hayo maneno kwa taratibu,pengine akijua kuwa Kais kalala hatayasikia hayo maneno, na hata kabla Kais hajafungua macho yake kumtizama huyo aliyetamka hayo maneno, yule mwanaume akawa keshageuka na kuondoka kuelekea kule kwa yule mwanamke mwingine ambaye ndiye aliyekohoa na kuwazindua toka kwenye dunia ile ya hisia.

Na huku nyuma,  Kais, alikuwa kama yupo kwenye njozi, kwani sauti ile ilipenya kwenye ubibgo wake, na kumkumbusha mbali. Alikumbuka, kuna mtu alikuwa na sauti kama hiyo hiyo, na alikuwa mtu wa karibu, lakini hakuweza kumchanganua na kumtambua alikuwa nani. Akafungua macho yake na kuanza kuwaza yupo wapi.

Akili ilipokaa sawa,  akabakia kuwaza, hii sauti aliwahi kuisikia wapi, licha ya kuwa haisikiki vyema kwa jinsi alivyoiskia. Lakini myoni, aliingiwa na shauku kubwa , kumgundua huyu mwanaume ni nani, lakini angelimgundua vipi, wakati kava hiyo kofia ya ngozi, iliyofunika, uso wote, na kuacha vitundu kwenye macho, masikio,na pua yake. Kukaa kwake porini mwenyewe kwa miezi mingi, alishaanza kujijenge hisia za kiporini, na kuanza kuondoa kumbukumbuu za maisha ya kawaida, lakini hiyo sauti alihisi aliwahi kuisikia kabla, na sauti hiyo ilizindua hisia zake nyingine, na badala ya kujutia lile tendo alilolifanya kwa muda mchache uliopita, akawa anatamani lijirudie tena.

‘Kwani wewe ni nani, na kwanini huvui hilo kofia lako?’ akauliza Kais akiwa amekaa pale alipokuwa amelele, huku akimwangalia yule mwanaume.

‘Siwezi kulivua kwasababu za kiuslama,na ni bora usinijue kabisa kuwa mimi ni nani,….’yule mwanaume akasema, na kwa vile lile kofia limembana sana mdomoni , sauti yake ilikuwa haitoki vyema.

‘Kwanini hutaki nikujue wakati inaonyesha sisi ni marafiki, wewe ni mtu mwema, …’akasema Kais.

‘Mimi nionavyo rafiki yako wa kiukweli, ni huyo aliyekubebesha huo uja uzito ulio nao….najua anakupenda sana,na wewe unampenda sana…’akasema huyo mwanaume, na kauli ile iliashiria hali ya wivu, lakini Kais hakuwa na uhakika na hilo akatulia huku akimwangalia huyo mwanaume.

‘Wewe hujui ni nini imetokea juu yangu, kama….’akakatisha maneno yake na kumwangalia huyo mwanaume, ambaye aligeuka na kuangalia upande mwingine, inaonyesha alikuwa akiwaza jambo, akasema kwa sauto ile ile isiyosikika vyema;

‘Nahisi hilo ulilofanyiwa ni dhuluma tu za dunia, nahisi ndio maana umetengana na huyo mwanaume aliyekupa huo uja uzito, labda nikuulize, ni nani mwenye huo ujauzito ulio nao, na kwanini upo huku kwenye kisiwa hiki cha umauti?’ huyo mwanaume akauliza.

‘Unavyoongea inaonyesha kama vile unajua ni nini kimetokea juu yangu ….niembie ukweli wewe ni nani, maana kama unajua ni nini kilitokea, ni heri ni kukimbie, maana mimi siruhusiwi kukutana na watu wangu tena, nimeshatengwa na jamii, mimi nastahili kuwa mfu, kuwa chakula cha chatu na mijoka…ndio maana nimetupwa huku kwenye kisiwa cha umauiti’akasema Kais.

‘Usilazimishe kile kisichowezekana, niamini mimi kuwa hili ninalolifanya ni kwa manufaa yenu,…ila kwa uwoni wangu , ingawaje sijui nini kilitokea juu yako, lakini nahisi sio sahihi kupewa hiyo adhabu,nafikiri, waliokufanyia hivyo, wamefanya hayo kwa  dhuluma tu, sizani msichana mrembo kama wewe ulistahili kufanyiwa hayo uliyofanyiwa, sijui umefanya kosa gani kustahili mateso kama hayo, na nashukuru mungu kuwa bado upo hai, na naahidi nitawalinda hadi nihakikishe mpo kwenye mikono salama..’akasema huyo mwanaume kwa sauti ya kukatika katika kutokana na lile likofia alilovaa.

Kais akainuka, na lengo lake lilikuwa kufanya juhudi hadi huyo mwanaume aliondoe lile kofia kichwani, lakini alipowaza sana, akaona haina haja,….akasema;

‘Toka lini haki, na upendo, vikatwala hii dunia,mimi tangu nizaliwe, naiona hii dunia kama ni sehemu ya wale wenye uwezo, ambao wana haki ya kuwatendea wapendavyoo wale wasio na uwezo. Wao wamejiona ni haki yao kufanya hivyo, na wana haki ya kuishi kwa raha,…..hata hawana huruma na wenzao ambao wanaishi maisha ya dhiki, taabu na mashaka…’akasema Kais.

‘Hilo usemalo sio kweli, kuwa dunia hii ni ya kudhulumiana, kiukweli dunia hii ni sehemu ya raha, kupendana na kusadiana, ndivyo muumba alivyotupangia tuwe hivyo, tatizo niubinafsi na uchoyo wa nafsi zetu. Kama kila mtu angejenga upendo kwa mwenzake, akamhurumia binadamu mwenzake, mbona dunia hii haina shida. Utajiri na mali asili zilizopo hapa duniani zinamtosha kila mtu aishi kwa raha, lakini wachache wenye uwezo wameamua kujilimbikizia wao wenyewe…’akasema yule mwanaume.

Kais, alitamani yule mwanaume aendelee kuongea hivyo hivyo, utamu wa yale maneno, ulimuingia akilini na kumsisimua, na hapo alipo alitamani kuwa karibu na huyu mwanaume na kama inawezekana awe hivyoo hivyo maisha yake yote, lakini akajua kuwa huyo mtu huenda ni miongoni mwa watu wanaomjua, na akiondoka hapo huenda akaenda kutoa taarifa kwa yule mzee anye mchukia kila wazee wote duniani,na kijua kuwa bado yupo hai, atahakikisha kuwa anatupiwa kwenye mamba wamtafune baada ya yeye kujifungua.

‘Mimi najua wengine hatuna haki kwenye hii dunia, juhudi zote nilizozifanya zilinifikisha hapa nilipo, na hata wale niliowasaidia sijawaona wakija kuniokoa, wao wameshafanikiwa najua wapo kwenye raha zao.Na hawa walionifanyia hivi wameshajua kuwa mimi nipo tumboni mwa mijoka, nashukuru kuwa bado nipo hai, lakini….’akatulia Kais na kumwangalia yule mwanamke ambaye kwa muda huo alikuwa bado amelala.

Alikuwa hajajiwa na hilo wazo kabla, na hilo wazo lilipomjia akilini akashituka na kuanza kuoana aibua, akatahayari, na kuhuzunika, akajikuta akijuta, alijutia lile tendo alilolifanya muda mchache uliopita, na alijua ni kosa lake, kama asingelimlazimisha yule mwanaume kwa kutumia hali aliyokuwa nayo ya kupambana na yale maumivu, huenda huyo mwanaume asingeliweza kufanya hayo waliyoyafanya na kufuta matakwa ya nafsi zao,….akahisi kutenda dhambi kubwa sana, akamgeukia yule mwanaume, halafu akamwangalia yule mwanamke, ambaye bado alikuwa kalala na kwa huzuni akauliza.

‘Huyo ni mwanamke  ni mke wako,kwanini mumekuja maeneo haya mabaya, maeneo ya gizani, huku wanaishi watu wasiojua ubinadamu, maisha yao yapo gizani, yametawaliwa na mambo ya kale, na zaidi mumekuja huku kwenye kisiwa cha umauti kwanini mumefanya hivyo, usiniambie kuwa na nyie mumehukumiwa kama mimi…?’akasema Kais, huku akimwangalia yule mwanaume,licha ya kuwa nguo alizovyaa ni kama wanazovaa wanaume wa huko anapotoka yeye, lakini alimuona kama mtu tofauti na tabia yake ni tofauti na wanaume wa huko kwao.

‘Huyo sio mke wangu…ila nimejitolea kumsaidia, huenda nisingelifanya hivyo, ningelijutia maisha yangu yote, lakini naomba tusiliongelee hili kwasababu za msingi..kwanza tuangalieni jinsi gani tutaondoka hapa’akasema huyo mwanaume.

‘Kwenda wapi, mimi sirudi huko nilipotolewa,mimi nilishahukumiwa kufa, sasa unataka nirudi tena huko,hilo haliwezekani, kama ni kuondoka ondokeni nyie wawili, maana hawo watu wanguwakiniona najua nitakuwa chakula cha mamba’akasema Kais.

‘Kama ni hivyo,…. mimi nitawatafutia sehemu tofauti na hiyo, na ndio lengo langu kwa huyo mwanamke unyemuona hapo, kwani na yeye kanusirika kufa huenda kwa mambo kama hayo yako, na ninachotaka kukifanya nikumpeleka mbali kabisa na hiii jamii, ili mimi nirudi hukoo nilipotoka’akasema huyo mwanaume.

‘Kwani huyo mwanamke umemtoa wapi, nakwanini umeamua kumsaidia na wewe kwenu ni wapi?’ akauliza Kais.

‘Nimekuambia kuwa sitaweza kukujibu hayo maswali yako, na siwezi kabisa kukusimulia hayo, kwasababu ya usalama wake, na pengine wa kwako pia,  ni bora hata wewe usihangaika kuyatafuta hayo yaliyotakiwa kumkukuta huyo mwanamke, yachukulie tu kama ni dhuluma za wanadamu wengine wanaojali nafsi na tamaa zao..’akasema huyo mwanaume.

‘Kwa tabia hiyo lini dunia hii itakuwa na amani,maana kama kafanyiwa hivyo, kuna jamaa zake wanaompenda, na huenda atakuwa na mtoto, huyo mtoto akisimulia alivyofanyiwa mama yake, atajenga kisasi, chuki na hawo waliomfanyai hivyo. Na hata kama  huyo mtoto au jamii yako haitaweza kuwaona waliofanya hivyo, lakini kihisia watu waliotendewa hivyo huwa na kinyongo, na wakibahatika kuwaona watu wenye tabia kama za hawo waliowafanyia hivyo hasira za visasi hutawala nafsi zao…’akasema Kais.

‘Ni kweli, hayo yapo, na tunahitajika kubadili huo mtizamo,na wa kuibadili hiyo tabia ni mimi na wewe, kila mmoja kwa nafasi yake. Kwanza cha muhimu ni kujenga upendo,bila kujali huyu ni nani. Kusaidiana kwa hali na mali, na unaweza kumsaidia mwenzako bila kujali huyo unayemsaidia atakupa nini…nikiwa na maana umpende jirani yako, kama unavyoipenda nafsi yako, tukiwa hivyo, basi mbona dunia hii haina shida…’akasema huyo mwanaume.

‘Mbona unapenda kutamka hilo neno,….`haina shida..’ unanikumbusha zamani nilikuwa na rafiki yangu mmoja, lakini keshaoa,…nilimpenda sana, lakini tofauti za kibinadamu, tofauti na sheria za ajabu ajabu, zikanifanya nishindwe kuwa naye, na nilimuona kama mbadili wa mwanaume mwingine niliyempnda kabla yake na kwa vile ni wa ukoo wetu niliwza juwa huenda naweza kuolewa naye…lakini haikufanikiwa’akasema Kais.

Yule mwanaume akatulia kwa muda kama anawaza jambo halafu akasema kwa taratibu kama vile anawaza  hilo analoliuza asiliulize kwa namna ambayo inaweza kuharibu jambo, akasema;

‘Kwahiyo ulikuwa na wanaume wawili, wote unawapenda, sasa nikuulize swali, samhani kwa kuuliza hilo swali,….’akatulia.

‘Wewe uliza tu, usiogope, ….’akasema huyo Kais.

‘Kati ya hawo wawili ni nanii uliyempenda zaidi,huyo wa uko wenu auu huyo mwanume mwingine ambaye umemuelezea?’ akaulizwa.

‘Kupenda ni kitu cha ajabu sana, nilipogundua kuwa huyo mwanaume wa ukoo wetu sitaweza kumpata, nafsi yangu ikafa ganzi, utapendaje kusipopendeka?. Kwa bahati nzuri ndipo nikakutana na huyo mwanaume mwingine, niligundua kuwa na yeye nimempenda, naye akaonyesha kunipenda pia na anaweza akawa mume wangu…lakini haikuwa rahisi, kwa mnyonge hakuna kitu rahisi, kwa fukara siku zote ni taabu tu, hata pendo kwake ni shida, ….kwa kifupi wote niliwapenda wote, lakini kila mmoja kwa nafasi yake…’akasema Kais.

‘Kwa mfano wangetokea wote wawili ukaambiwa umchague yupokati ya hawo wawili ungemchagua nani?’akaulizwa.

‘Hilo swali ni gumu kujibu,….kwani sisi wanawake tuna mengi tunayoangalia kwa mwanaume, na jinsi tulivyoumbwa tunaweza kubadilika kama kinyonga…wote nawapenda, ila nitampenda yule ambaye atakuwa karibu nami, na akawa ananipenda kwa vyovyote vile. …ila kama nitakuwa nimeshaolewa na mmojawapo, na tukawa hatuna kipingamizi tena, mwingine hatakuwa na nafasi kwangu…’akasema Kais.

‘Je uliwahi kuolewa na mmojwapo kati ya hawo wawili?’ akaulizwa.

‘Niliwai kuolewa,na bahati nzuri ni kuwa tuliwahi kutimiza nguzomuhimu ya ndoa, ambayo zawaidi yake kubwa ni huu uja uzito,….lakini ndoa hiyo haikudumu, ikavunjwa kwa nguvu za wazee wenye itkadi zao, na kwahiyo hivi sisi sipo kwenye ndoa tena…’akasema huku akizua machozi kutoka.

‘Inaonekana ulimpenda sana huyo mwanaume…inavyoonyesha ulimpenda sana kuliko huyo mwanaume mwingine?’akauliza huyo mwanaume.

‘Unaweza kusema hivyo,kwasababu ndiye niliyeweza kumruhusu mwili wangu kwa mara ya kwanza, na hilo ndilo nililoahidi kuwa kati ya hawo wawili, atakayewahi nikamruhusu kuupata mwili wangu, ndiye atakyekuwa mume wangu wa kudumu…sasa ni nini nimefanya,…ndio maana inaniuma sana, na sasa nimekuwa kama…kama ….malaya…maana hata ‘akaanza kulia.

‘Kwanini unasema hivyo…?’ akauliza huyo mwanaume.

‘Kwasababu nimeshindwa kuzizuia nafsi zangu, na kuvunja kiapo changu, na nimeshindwa kuvumilia na kukulazimsiah kitu ambacho sikuwa nacho awali…najuta na naomba unisamehe sana…nakuomba sana tena sana, unisamehe kwa lile lililotokea …’akaanza kulia.

‘Sikiliza Kais….’akasema yule mwanaume,na Kais akashituka, huyu mwanaume kajuaje jina lake, akamwangalai yule mwanaume kwa makini, lakini yule mwanaume, akawa kama anainama chini, na hapo Kais, akaanza kuhisi jambo, akaanza kurudi kinyume nyume,….woga ukaanza kumjia, akajua huyo anaweza kuwa mmoja wa maaskari wa mzee wao,na anavyowajua hawo maaskari wa mzee, ni watiiifu sana, hawaweze kumsaliti hata siku moja yule mzee, aliyesababisha yeye kufikishwa mahali hapo.

‘Wewe ni nani….’akasema Kais, na alipoona yule mwanaume katulia, akageuka kwa haraka na kuanza kukimbia….

NB: Natamani kuendelea lakini muda huo umekwisha. Lakini naona kuna matatizo kwenye Google Chrome, sijui ni mimi mwenye au vipi, na hii imechangai sana nisiweze kuwa nanyi siku mbili zilizopita. Tukijaliwa tukutane sehemu ijayo

WAZO LA LEO: Tabia ni kitu cha ajabu sana, kila mtu ana tabia yake, ambayo huenda nii udhaifu alio nao, lakini wengi wetu hatupendi kuukubali kuwa tuna udhaifu huo na tunatakiwa kuondokana nao.
Kuna watu wana udhaifu wa matendo ambayo kijamiii ni mabaya, lakini ukiambiwa kuwa ana tabia hiyo ambayo ni mbaya na haipendezii kwa jamii, mtakosana, na huenda watu kama hawo wafikia hata kupinga kwa nguvu zote kuwa hawana tabia hiyo, au hata akikubali kuwa ana uzaifu huo, bado ataona kuwa kwake yeye ni haki yake kuwa nayo, na watatafuta mwanya, hata wa maandishi ya imani zao na kuyapotosha ilimradi, kuhalalisha matendo yao mabaya.

Tusijidanganye kwa hilo…kama metendo yako yanawakera wengine, kama matendo yako yamejengwa na ubinafsi, kama matendo yako yamejengwa na tabia za kiulevi, kiuchoyo, usengenyi, uchochezi,wizi, uzinzi,  propaganda potofu, nk, huo ni udhaifu, unahitajika kuondokana nao.Na kama umepata bahati ,mwenzako akaja kukushauri, akakupa neno la kuondokana na tabia hiyo, msikilize,na mshukuru sana kwa kuuona ugonjwa huo, kwani atakuwa ni dakitari wako mwema, na atakuwa kakuokoa kwenye ugonjwa mbaya wa nafsi.


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Hapa inaonyesha ulitulia wakati unaandika sehemu hii, HONGERA SANA MKUU