Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, November 8, 2012

Uchungu wa mwana Aujuaye ni Mzazi-19



Maua anasema maumivu ndiyo yaliyokuwa akilini mwake, na mwili wote ukawa kama umekufa ganzi, na kwa muda huo hakuwa anajua nini kinachoendelea, kuna muda alihisi kuwa yupo hewani,ikimaanisha kuwa amebebwa, na kwahiyo atakuwa anapelekwa ufukweni, ambapo anatakiwa akajifungua tu,anatupiwa  mtoni, akaliwe na mamba.

Kuna muda kutokana na maumivu, alikuwa akipoteza fahamu kabisa, na alipozindukana kwa safari hii ndpo akasikia kilio cha mtoto mchanga, hapo akajua keshajifungua, akajitahidi kujiinua ili amuona mtoto wake,angalau aione sura yake, kwani huenda hataiona tena , akainua kichwa kwa shida, huku macho yakiwa yamejaa machozi, na bahati nzuri yule mkunga akajua nini mama huyo anakihitaji, akamleta yule mtoto karibu yake.

‘Mtoto wako mnzuri, ..ana afya njema, usiwe na wasiwasi atalelewa vyema kabisa, na akikua atapata mume jasiri wa kumuuoa,ila wewe, huhitajiki tena kweney ardhi hii,na sisi tunatimiza wajibu wetu, kutokana na maagizo tuliyopewa, hatuna jinsi ya kukusaidia…’akasema huyo mkunga.

Maua alijaribu kufunua mdomo, akitaka kusema, wamlee mtoto wake vyema, lakini mdomo haukuweza kufunuka, akawa anaongea kihisia hisia, na kuomba kwa mungu mtoto wake asije akaangukia kwenye mikono mibaya na kupata taabu.

Maua anasema; ‘Nilimwangalia mtoto wangu kwa macho ya huzuni, nikijua kuwa ndio mara ya mwisho kumuona, na sijui atapelekwa kulelewa na nani, na hilo sikuwa na jukumu tena, kwani pale nilipo nilikuwa kama mfu tu.

Baadaye yule mtoto akaondolewa mbele yangu, na mimi nikafungwa fungwa na ile ngozi niliyokuwa nimelalia wakati wa kujifungua, wao walihakikisha kuwa hakuna damu inadondokea kwenye ardhi yao. Wakanifunga kama gunia au furushi bila kujali uchafu na damu zote zilikuwa zikizagaa mwilini hata kuingia mdomoni na puani.  Nikahisi maumivu na ilikuwa kama nakaribia kupoteza fahamu na mara nikasikia wale wakunga wakisema;

‘Tumeshamaliza kazi yetu, mnaweza kumchukua mtu wenu..’akasema mkunga mkuu, na mara wakaja maaskari wanaume wenye nguvu, wakaniinua juu kwa juu, huku wakihimizana kuwa wahakikishe hakuna damu yoyote inaangukia chini, na walipofika ufukweni, wakaniweka kwanza chini, na mmoja akasema;

‘Mbona leo ziwani kupo kimiya, sioni mamba hata mmoja upande huu, nilitaka nione jinsi gani anavyomtafuna mtu, maana ….huyu dada, namuonea huruma, lakini ….’mmoja akasema.

‘Wewe huwaoni hawo mamba, lakini wao wanatuona, wewe subiri tukishamrusha kwenye maji utakavyoona vumbi lao, ….huoni yale kama macho yanatutizama kule mbele’akasema mmojawapo.

‘Mimi ninawasiwasi, huenda mizimu na wazee hawalipendi hili tunalotaka kulifanya, hamuoni kuwa huu ni uuwaji , na tunamuua mtu asiye na hatia?’ akauliza mmojawapo.

‘Wewe unaona hivyo, lakini wakuu wameona vinginevyo,sisi kazi yetu ni kutimiza wajibu wetu kama maaskari watiifu, na kama ni lawama watazibeba wao wenyewe, …’akasema mmojawapo.

‘Tatizo hapa kuna ubaguzi, kila ikifikia ukoo wa hali ya chini, amri zinakuwa tofauti na za wale wa hali juu, na hili linaleta manung’uniko miongoni mwa watu. Kama haki haitendeki, kama hakuna usawa katika maamuzi ya kijamii, hakutakuwa na amani kamwe’akasema huyo askari ambaye alionekana na huzuni kuliona lile tendo likifanyika.

‘Ukianza kuwaza hivyo,hata hii kazi itakushinda,….’akasema askari mwingine.

‘Lakini nyie hamuoni, kuna koo, watu wake wakisema neno, linachukuliwa kwa uzito wa hali ya juu, lakini kuna koo, nyingine hata kama wanachoongea ni cha ukweli, na cha haki hawasikilizwi, watu wanachoangalia ni nani anayetoa hoja,kuliko ni nini sheria inasema kwa mataji huo tutaiangamiza nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe’akalalamika yula askari.

‘Kwani wewe shida yako ni nini, wewe hujatoa maamuzi, wewe kazi yako ni kutekeleza, kama ni lawama sio juu yako wewe’akasema mwenzake.

‘Mimi kama binadamu ina niuma, kuona kuwa kuna watu hawatendewi haki, kuna jamii, kuna ukoo nyingine hazipati huduma, au nafasi sawa na jamii nyingine, ukiuliza unaambiwa unaleta uchochezi. ..’akasema huku akimwangalia yule mwanamke ambaye alishaviringwa kwenye ile ngozi kama maiti.

‘Tatizo lako wewe ni muoga, huna lolote jingine…’askari mwingine akasema huku akimalizia kazi ya kumfunga funga yule mwanamke, ili kuhakikisha anaondoka na damu zake zote.

‘Mimi ni kweli naogopa sana,maana hata sisi watekelezaji tuna fungu la lawama,kwani leo ni kwa huyu kesho inaweza ikawa zamu yetu, huwezi jua, ….na hata hivyo, balaa likitokea halitachagua ni nani wa kumwangamiza…itakuwa kama zile gharika tunazosimuliwa na wazee wetu’akasema na kusogea pembeni.

‘Wewe kama unaogopa kaa pembeni, ngoja sisi tutimize wajibu wetu, sisi ni askari, tukipewa amri, hatutakiwi kusita, ni kutekeleza tu, mengine watajua wao watawala, na hiyo gharika ikitokea, ni kifo cha wote, ….haya inua huko, angalia huko, unaona hiyo damu ….’akasema mmojawapo, akimuelekezea mwingine, na yule askari mwingine akawa kaka pembeni akiangalia ziwani, na macho yake yalikuwa kama yameona kitu cha jabu, lakini hakuweza kusema neno.

Katika kuinua inua damu chache ikawa imedondokea chini, na hili halikutakiwa kabisa, na kwa imani zao inaashiria kuwa kutatokea jambo, kwani wamakiuka miiko. Na wale maaskari wakaogopa,wakijua ikijulikana wao watabeba lawama, mmoja wao akasema

‘Ifukie hiyo damu haraka…’na  mwenzake akafanya hivyo, huku wakiangalia huku na kule, na bila kupoteza muda, au kuangalia vyema kule kwenye mto wa mamba,wakajiandaa kumrusha huyo mwanamke kwenye maji, wakahesabu moja mbili tatu….

********
Kais, alifikishwa kisiwa, sehemu iliyotengwa kama jela, kila mkosaji hupelekwa hapo, na kuachwa aishi peke yake, bila chakula wala maji, baada ya siku kadhaa anakutwa ameshakufa , au kuliwa na wanyama, au kumezwa na chatu.  Hii ndio adhabu aliyopewa baada ya kupatikana na hatia ya kudanganya.

Kais mwanzoni hakuogopa, akijua keshatimiza ahadi yake kwa mtu aliyempenda,akijua kwa vile hata huyoo mwanaume anampenda huenda akafanya juhudi za kumuokoa, masaa yakawa yanakwenda, masiku na miezi ikapita.

Kais, akawa anaishi peke yake lakini hakukuta tamaa, na alijitahidi kutafuta chakula , huku akijificha kila anapoona watu wanapite kwa mbali. Hakutaka kabisa kurudi kwao, kwani alijua kikutana na huyo babu wa mume wake atamuua, alikumbuka jinsi alivyokuwa akitaka kutoa kisu pale alipojua kuwa mjukuu wake kamuoa mtu asiyestahili, na kama asingelikuwa mzee mwingine kuingilia kati, sasa hivi angeshakuwa maiti.

‘Mzee mwenzangu, usije ukafanya jambo baya sehemu kama hii,….’yule mzee mwenzake alimkaribia na kumshika ule mkono uliokuwa tayari unata kisu pale kiunoni, tayari kufanya jambo ambalo lingeashiria umwagaji damu, na ilikuwa sio sehemu ya kufanya tendo kama hilo.

Kiimani zao mzee, kama yule akiinua kisu tayari kwa kufanay teno la mauaji, hatakiwi kukiriudiaha hivi hivi, vinginevyo inatakiwa kuotoa kafara,na ndivyo alivyofanya huyo mzee baada ya kutoka hapo, alichinja mbuzi, na kutoa kafara.

‘Huyu binti anatakiwa kushiktakiwa kwa kudanganya na kuifedhehesh familia na ukoo wetu, ..’akasema huyo mzee, na wazee mashuhuri wakakutana haraka na hukumu ikatolewa, kuwa huyo binti hastahili kuolewa tena na mjukuu wao,kwani kwanza ni muongo, pili kaifedhehesha familia na ukoo, na kwahiyo anatakiwa kuhukumiwa.

‘Adabu yake ni kutengwa na familia na ukoo, na hilo litafanyika kwa yeye kutupwa kwenye kisiwa cha kifo, akaliwe na nyoka, au akafe na njaa’akasema mzee anayetoa hukumu.

‘Imekubalika,….’wakakubali wenzake, na binti huyo akachukuliwa juu kwa juu na kupelekwa nje ya eeno hilo, ambapo unavuka mto, na kufikia sehemu ya mwiinuko kwenye miamba mikali had sehemu iliyo kati kati ya miamba, ambapo watu hawawezi kufika, na hapo aliachwa.

Walipomfikisha hapo, walimuachia maji kidogo na punje chache za karanga, kama walivyoamrishwa, na kuondoka zao.

Kais,alibakia pale akiwaza jinsi gani atafanya, kwani alijua kama atatulia pale pale, ni lazima atakufa sio kwa njaa tu, bali kuliwa na wanyama wakati hasa michatu. Na muda ulikuwa umekwenda sana, na hapo wakati anawaza akakumbuka jambo.

Alikumbuka kuwa wakati anachukuliwa na wake askari bibi alimsogelea kama anamuaga na haraka na kwa uficho, akamwekea kikasha kwenye ukunjo wa nguo yake, hakujua ni kitu gani kwa muda ule. Alipokumbuka hivyo,akakitfuta kwenye ule mkunjo akagundua kuwa ni kiksha, kubunda kilichofungwa kama binzari, akakifungua na kukuta unga, akaunusa, na kupiga chafya.

Akili yake ikaanza kuwaza ule unga ni wa nini, ndipo akakumbuka, kuwa unga kama huo, alimsikia bibi yake akisema kuwa ukijipaka harufu ya kibinadamu inapotea, kwahiyo hata kama ni mnyama mbaya hataweza kugundua kuwa kuna binadamu mahali hapo. Na harufu kama hiyo huwafukuza wanyama wabaya.

Akauchukua ule unga na kujipaka mwili mnzima, na kwa vile alikuwa anahisi kiu akaona atembee tembee, huenda akapata choc kwani anavyojua kwa mbele sana ndipo ule mto wa mamba hote cha kula. Alitembea kwa muda, na kupanda kwenye miamba, na kushuka hadi akatokea sehemu ambayo mto unaanzia, na hapo akajua kuwa keshaokoka, maana hapo anweza akaishi, na kupata maji, na alihakikisha anajenga makao yake, kwani kama atarudi huko kwao, atatupwa na kuliwa na mamba, yeye keshatengwa na jamii, hana ndugu tena, na maisha yake yapo mikononi mwake mwenyewe.

Alichofanya ni kutafauta sehemu salama, akajua kuwa juhudi zake ndzo zitamuokoa, akaanza kutafuta sehemu yenye maji salama, na baadaye akaanza kutafuta samaki na chochote kinacholika,…

‘Mito mingu huku inaishi mamba, ukiinama kunywa maji, au kunawa, wanakuvamia’akakumbuka hiyo kauli toka kwa bibi yake, na kwahiyo walikuwa wakiogopa kukaribia kwenye mito au mabwawa yaliyotuama na hata wakipita maeneo kama hayo huwa wanaogopa kuinama kunawa,kwani wanasema mamba yeye akiwa majini anakuona na anatulia kimya ukiinama tu anakuvamia.

Siku zikaenda, …mwezi ukaisha, miezi ikapita,akagundua kuwa yeye ni mja mzito, kwahiyo kwa vyovyote anatakiwa kutafuta njia a kuondoka hapo mahali, kwani kuishi peke yake inaweza ikaleta matatizo, na alijua kuwa kiutaratibu zao, mtu akiwa mja mzito, hatakiwi kuzurika mpaka ajifungue.

‘Lakini siwataki tena watu wangu, wameshanisusa, na wanajua nimeshakufa, nitatafuta njia ya kutoka huku, na kwenda nchi nyingine…’akasema na kuanza safari ya kutafuta njia ya kuondoka hapo, alitembea sana, hadi akatokea kwenye mto kubwa, akaukumbuka kuwa huo ndio ule mto wa mamba.

Mara kwa mbele akaona kitu cha ajabu,mwanzoni alijua kuwa ni mamba,lakini baadaye akaona kuwa ni kitu kama gunia,…au furushi la kitu kilichofungwa kwenye ngozi ya wanyama, na ilionekana kam gunia. Akalifuatilia kwa macho, kwani lilikuwa likitembea juu ya maji, kama mtumbwi.

Mara ghafla akaona maji yakitibuka, akatoka mtu, ambaye kumbe alikuwa ndani ya maji huku kalishikilia hilo gunia akiogolea ndani kwa ndani, kama vile hataki aonekane. Na alipofika ukingoni, akatjitokea na kulibeba lile gunia  hadi sehemu kavu.

Kais, alijificha akiogopa, kwani alihisi huenda ni hawo watu aliowahi kusikia kuwa wanakula nyama za watu na huenda huyo mtu alikuwa keshamuua mtu na hapo anataka kumfanya kitoweo. Lakini kitu cha ajabu ni huyo mtu kuwa ndani ya mto huo wa mamba bila kuliwa na hawo mamba,…

‘Huyu mtu alikuwa kajifunika uso wote, inavyoonekana hakutaka kabisa sura yake ionekane,kwani aliachia sehemu ya macho ya puani, na mdomoni, lakini sehemu nyingine zote zilikuwa zimefunikwa na kofia kubwa, alilolivaa.

Mara akamuona yule mtu akilifungua lile furushi, na kweli ndani yake kukatokea mtu , ambaye alimuona kama ni mwanamke.Na yule mwanamke alikuwa kalowana damu, akahisi kuwa huenda huyo jamaa alimuua huyo mwanamke kabla ya kumleta sehemu hiyo, akasubiri aone nini hatima yake.

Mara yule mtu akacmhukua yule mwanamke na kumsogeza karibu na mto, akaanza kumuogesha yule mwanamke, hadi alipohakikisha kuwa damu mwilini zimekwisha, akasogea pembeni na kuwasha moto, akachukua majani na chombo kidogo alichokuwa kakibeba, akachota maji na kuyawekea jikono pamoja na unga unga, na baadhi ya majani.

Haikuchukua muda yale maji yakawa yanachemka,na yule mtu akachukua yale maji kwenye gome la kononokono, alilolitumia kama kikombe, na kuchukua yale maji yaliyochanganyika na ile dawa kumnywesha yule mwanamke.

‘Mbona hafanani na hawo watu wanaokula watu,huyu anaonekana kama tibabu, anamtibia huyo mwanamke…’akasema kimoyo moyo, akiwa kachuchumaa pale alipojificha. Muda aliokaa pale alijiona mwili umechoka, na hali aliyo nayo, hakuweza kukaa mtindo ule kwa muda mrefu, akajiinua, na kufanay vile alitoa sauti.

Yule mtu kule akasikia,na kuinua kichwa kuangalia ka tahdhari, akatoa kisu chake na kuanza kufuatilia huko aliposikia sauti, lakini kabla hajafika mbali,mara ikasikika sauti nyingine,akasimama, na kwa tahadahari akageuka, kumbe ni yule mwanamke,alikuwa keshazindukana.

Akawa katulia, huenda alikuwa akijiuliza afanye kitu gani kwanza, kwani yule mwanamke alikuwa akigaragara, kuonyesha maumivu, na pale alipokuwepo sio mbali na kwenye mto, na kulikuwa na muinuko, na kwa vile huyo mwanamke alizindukana na akawa kama anajinyonga, na bila kujua yupo wapi, akawa anaserereka kuelekea kwenye maji,.

Na kwa mbali walionekana mamba wakisogelea ufukweni, walishanona chakula.Yule mwanamume akaona hana jinni ni bora arudi kwenda kumuokoa yule mwanamke, na hapo Kais akaona ndio muda wa kutoka pale alipokuwa kajificha, na kama inawezekana akimbie au auatafute sehemu nyingie, lakini kwa hali aliyokuwa nayo, akaona huyi mtu anaweza kuwa msaada kwake.

Akamsogelea….na mara mamba akaruka toka kwenye maji, kumrukia yule mwanamke,na yule mwanaume naye akaruka kama mbizi kumuwahi yule mwanamke…..

*****

NB:Haya muda unakwenda kwa kasi, tuishie hapo kwa leo.

WAZO LA LEO: Kabla hujamuhukumu mwenzako jichunguze kwanza nafsi yako, huenda wewe ni mkosaji zaidi ya huyo uneyemuhukumu.


Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

kwakweli kipaji chako ni cha pekee sana. hongera sana. nafurahi kwamba umekipangilia vyema na sasa tunakwenda pamoja, mwanzoni ulikuwa unanichanganya kwa kuweka visa kibao kwa mara moja! asante sana kwa kuyafanyia kazi maoni yangu. umefikia wapi kuhusu kutoa kitabu? u have a great talent in writing stories!

emuthree said...

Nashukuru sana mkuu hapo juu, nashukuru kuwa nawe umenielewa, mm mtindo wangu wa kutunga hivi visa ndivyo ulivyo, ili kuleta tofauti kidogo na taratibu nyingine. Tupo pamoja, na nitajitahidi kadri niwezavyo, ili tuweze kuwa pamoja

Anonymous said...

Kisa kinavutia japo kinatisha hongera kaka

Anonymous said...

Nakupa hongera kweli una kipaji, na mm sioni ubaya wa mtiririko, unajua watu wengine wamezoea mtiririko wa moja kwa moja mapaka unajia nini kitafuata, lkn ww ni tofauti big up

Anonymous said...

bear grylls messer
Here is my blog :: bear grylls messer

Anonymous said...

Ubarikiwe saana, kazi ya mikono yake ikupe riziki ya halali. Tupo pamoja M3