Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, November 6, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni Mzazi-18



 Maua alijaribu kuficha uchungu, uchungu wa uzazi, aliona ni heri kama inawezekana ajifungulie humo humo ndani,alijitahidi sana, lakini ikafikia muda hakuweza tena kuficha yale maumivu, maumivu makali yalimjia ,akakunja uso, na kushika tumbo, ….na wakati huo mwenzake alikuwa akitizama nje, hakuwa amemtizama Maua, ikawa ndio heri kwake, na mwenzake  akawa anasema;

‘Hicho ndio kisa changu cha kuwa mwenyeji , na kuolewa na hawa watu wa msituni, na nimeishi nao hadi sasa najua mila na desturi zao, na tunasubiri muda ufike niingie sehemu hiyo inayotambulikana kama sehemu takatifu, ingawaje wenzetu bado wameweka pingamizi kuwa hatanitambua hadi miujiza yote ikamilike, kwani walitaka niolewe na mjukuu wao….’akasema.

‘Lakini muda utasema, siku ikifika hakuna pingamizi tena, hata wao wanajua hilo. ..’akasema huyu binti huku akizidi kuangalai nje.

Yale maumivu yakapita, na Maua akaweza kutoa sauti huku kijasho kikimtoka, akasema;

‘I-ina maana wao hawajakukubali kuwa wewe ndiye malikia mtarajiwa ?’ akauliza

‘Kukubali moja kwa moja hawajakubali, kwani wanaona wakikubali wataumbuka, ila heshima zote ambazo nastahili nazipata,kwa mfano pale inapotokea tafrija ambayo wakina mama wanahitajika, wanahakikisha nimefika,na kupewa kiti maalumu…kama malikia mtarajiwa’akasema.

Maua akatulia, kwani alihisi maumivi mengine yakija kwa kasi, akainama ili mwenzake asione, na mwenzake alikuwa akiangalia nje, alikuwa na wasiwasi wa mume wake, kwani ilitakiwa kwa muda huo awe amesharudi. Moyoni akahisi kuna tatizo, akageuka kumwangalia Maua, ambaye alishajikausha kwani yale maumivi yameshapita.

‘Hawa watu pamoja na kupigana kote, lakini inapofika sehemu ya imani yao, wanaogopa sana, wote wanahisi kuwa mimi ndiye malikia mtarajiwa, na wakinifanyia lolote baya , maafa yatawaandama, na kinachofanyika kwa sasa ni kunishawishi mimi niolewe na mjukuu wao, au waniteke kimawazo na kuwaona wao ni watu wema, …

'Wanajua kabisa kwa kuolewa na mjukuu wao ni kitu ambacho ni kigumu sana, kwani mume wangu ameshawashinda, na ukishinda basi wewe ndiye unastahili kuwa mfalme mtarajiwa’akasema.

‘Sasa kikwazo ni nini?’ akauliza.

‘Kwanza muda haujafika kwa mimi kutawazwa, lakini pia mume wangu anahitajika kuonyesha kuwa kweli anastahili kuwa mfalme, na pamoja kuwa aliwahi kuua simba, lakini anahitajika kufanya mambo mengine makubwa, ….wana imani kuwa mfalme wa nchi ni lazima awe mtu jasiri, mtu ambaye uwezo wake sio wa kawaida’akasema.

‘Kwahiyo hata hilo bado linasubiriwa…yaani mpaka atende mambo ya ajabu, kama asipotenda na wewe umeshaolewa naye itakuwaje?’ akauliza, huku akijinyisha kidogo, kwani maumivu yalishapoa, na alihisi huenda hali ikatulia,…..hakujua nini kitafuata baadaye.

‘ Yule mtabiri, alisema malikia mtarajiwa ataolewa na mume jasiri, mume ambaye atakuwa naye anatenda mambo yasiyotendeka, ya ujasiri, kusaidia watu, …’akasema na kumwangalia Maua.

‘Kwani hayo ya kusaidia watu, …na na….’akasema Maua huku akijikunja, maumivu yalikuwa yanakuja kwa kasi.

‘Ndio hilo nalo ni moja ya miujiza iliyotabiriwa kuwa kama kweli mume wangi ni mfalme mtarajiwa, atakuja kufanya jambo la ajabu ,  mimi mwenyewe nimeshuhudia mengi aliyoyafanya , na nimefikia hatua ya kuamini hivyo , kwani mume wangu ni mtu ambaye amekuwa kila siku akionyesha uhodari, akisaidia watu, akifanya mambo ambayo wengine wanashindwa kuyafanya.

‘Aaah, Maua akajikunja na hakuweza tena kuhimili, akalalachini, ….’ Mwenzake akainuka, akashika 

kichwa, akawa anashindwa afanye nini, kwani muda kama huo mume wake alitakwia awepo, na walijadiliana na mume wake kuwa atakuja na kutafuta njia za kumuokoa huyo binti, lakini hajafika, …

‘Ooh, sasa nitafanya nini mpendwa…nakuonea huruma maana huyo mama akija, sitakuwa na la kufanya, na haitakiwi ujifungulie humu, na ukijifungulia hapa mimi na mume wangu tutakuwa chakula cha mamba…’akasema huku akiangalia huku na kule, na alipomwangalia Maua ambaye alikuwa chini katulia, hatingishiki

Akamsogelea na kumgusa, akamkuta yupo kimiya,….na mara Maua akainua kichwa na kupiga ukelele, ukelele uliosikia nje, ukelele ulioharibu kila kitu,maana hakukuwa an siri, mama mkunga ambaye alikuwa nje na kikosi chake watakuwa wameshasikia, na muda wowote wataingia…lakini kukawa kimiya,na mara vurugu zikasikika mlangoni kuonyesha kuna watu wengi wanakuja kwa kasi…na hapo Maua hakuweza kuhisi jingine zaidi ya maumivu.

***********
Mzee wa upande wa Maudui alikuwa akongea na wazee wenzake, na moja ya ajenda yao kubwa ni jinsi gani ya kuweza kumwangamiza kijana ambaye kila siku inaonekana ndiye atakayeshika kiti cha ufalme,na kwa vile keshamuoa binti, malikia mtarajiwa, na wameshaishi naye kipindi kirefu, hakukuwa na jinginela kufanya.

‘Mimi naona tukubali ukweli, kwani yote tuliyowahi kujaribu kuyafanya yameshindikana, na hili ni kuonyesha kuwa kweli huyo kijana ndiye chaguao la wazee wetu, ….’akasema mzee mmoja.

‘Kwanini ukubali kirahisi hivyo,hatujaambiwa kuwa huyo kijana ndiye chaguo la wazee, tumeambiwa juhudu za kijana yoyote ndizo zinamfanay awe mfalme, kumuoa huyo malikia sio tatizo, kwani anaweza akamuacha, anaweza akafariki….yoye hayo yanawezekana’akasema mzee kwa hasira.

‘Kwahiyo una maana tufanye jambo….hapana,hilo litaleta mkosi, ….’akasema mzee mwingine.

‘Mambo yatajileta yenyewe, ukumbuke kuwa hawa watu wamemchukua mtu ambaye hatakiwi kweney jamiii yetu, na akajifyungulia kwenye ardhi yetu, ni kashifa kwao, na niwajuavyo,wanaweza wakapuuzia hilo, na sisi tunahitajika tuwe makini, …hapo wakiteleza tu, tumewanasa, kijana yule tunamtupia Mamba na abu yake ambaye kamshupalia anafuatia na sisi tunamchukua malikia wetu…’akasema.

‘Unafikiri wanaweza kuafanay kosa hilo, akati kabisa wanajua kuwa huyo mwanamke hatakiwi kujifungulia kweney ardhi yetu,…?’ akauliza mmojawapo.

‘Kama wangelikuwa wana nia hiyo, huyo mwanamke asingelikuwepo huko nyumbani kwa kijana hadi muda huu, alitakiwa awekwe karibu na mto wa mamba, ile tone la damu lisimwagike kwenye ardhi yetu, lakini hadi sasa hivi nasikia bado yupo huko’akasema.

‘Na yule kijana wao yupo wapi, mbona haonekani?’ akauliza mmojawapo.

‘Labda yupo kambini, nasikia anasimamia kikosi chao, ..’akasema mmojawapo.

‘Mtafuteni, mjue wapi alipo, huyu kijana ana mambo ya ajabu anaweza akafanay mambo mengine ambayo yatamfanya aonekane mtu mashuhuri, fuatilieni, na ikibidi mumunyamaizishe hadi hilo tukio litokee, apoteze fahamu kwa muda…’akaamurisha mzee.

‘Sawa mzee, hilo litafanyika…’wakasema vijana makomandoo wakiondoka kufautilia nyendo za huyo kijana.

Mzee aliinamana akiwaza jinsi gani alivyoweza kughilibiwa na yule binti, hadi kuingia mle ndani na kufungishwa ndoa na kijana wake, hakuamini kuwa yule binti angelikwua mjanja hivyo, …

‘Huyu atakuwa alisaidiwa na hawa wenzangu,….’akasema akikumbuka tukio lilivyokuwa

********

‘Tayarisheni sherehe kubwa, na waalikeni wakuu wote, hasa majirani zetu, maana leo ni siku muhimu sana, ni siku ambayo kila mtu alikuwa akiisubiria…’mzee akawa anatoa amri huku na kule, na kujaribu kufuatilia kilajambo,ili kuhakikisha mambo yanakwenda vyema.

Aliingia kwenye ofisi yake na kuanza kuandaa baraza la mawaziri, akiwaangalia watu wake mashuhuri,ambao wataweza kuwa karibu na kijana wake,huku moyoni akisema;

‘Lazima mwanzoni nimuelekeze jinsi gani ya utawala, ni nanii anastahili kuwa nani kweney utawala wake, ili asije akaharibu’akasema huku akihakikisha watu wake muhimu wapo kwenye ordha yake, halafu akatoka nje.

‘Hawajamaliza tu,….hawa vijana bwana, ingelikuwa enzi zangu, …aah, mambo ningeshayamaliza mapema, sisi tulikuwa imara,..., lakini bado muda upo…’akasema huku akitembea kwa tambo, huku akiangalia upende ule wa maadui zake, na moyoni akisema;

‘Nyie sasa hapo hamtaonekena tena,hapo watakuja kukaa watu wangu muhimu,…’akatikisa kichwa na kutabasamu, akageuka na kuelekea huko walipokuwepo watu walioalikwa, na kila hatua aliona watu mashuhuri wakiingia, wakiwa wamevalia mavazi rasmi ya sherehe , akawa anawakaribisha kwa furaha, na kusema;

‘Mambo yameiva,mambo yamekuja kama yalivyotabiriwa…kijana wetu ameshinda, yupo anamalizia kazi’akasema na kuingie eneo ambalo kijana wao atafikia baada ya kumaliza kazi aliyokuwa akiifanya ili ile ahadi itimie….

**********

Kijana akiwa na furaha kuwa hatimaye keshampata malikia matarajiwa akasogea pale alipowekwa huyo binti,kwani alishazinduliwa na alikuwa kaka kwenye kiti maalumu, hajafanulia bado,kwani yeye ndiye aliyestahili kumfunua, hakutakiwa mtu mwingine kumuona sura yake kwa wakati huo.

Hata yule aliyempulizi hiyo dawa, alitakwa afanye hiyo kazi bila kumuona sura, akimuona sura yake atapata mkosi, kwani anayestahili kumuona sura yake, baada ya kutangazwa kuwa ni mchumba wa mtu, yupo tayari kufungishwa ndoa ni yule muoaji peke yake.

Yule mupuliziaji dawa alipofanya kazi yake, na kuhakikisha kuwa huyo binti keshazindukana, akatoka na kumuachia kazi hiyo shangazi mtu na watu wawili ambao walimvalisha nguo za harusi , na kuhakikisha kuwa hamtizami machoni , huyo muolewaji,.

Kinachofanyika ni kufunikiwa kitambaa kikubwa, na huyo muolewaji anaelekezwa afanye nini, na kukihitajika msaada, huyo binti anahakikisha kajifunika uso wake, na wenzake humsaidia bila ya kumuangalia usoni, na baadaye alipokamilika akapelekwa kwenye kiti maalumu, kikubwa kama kitanda, ili bwana harusi aje afungishwe ndoa,…

‘Ndoa ikafungwa, ikawa ni zamu ya bwana harusi kumfunua mkewe, na muda huo wazee muhimu wapo kwa pembeni na wanawake wakushangilia wapo karibu, na hayo yalitakiwa yafanyike haraka kutokana na muda uliopangwa,…na muda huo giza giza lilifanya wengi wasimuone vyema huyo binti, cha muhimu na bwana harusi kumuona.

Alikuwa keshavalishwa ki malikia mtarajiwa, mavazi ya kipekee yenye mapambo ya kila aina,..

Bwana harusi akasogea, na kumfunua mkewe akiwa na ndoto za ajabu kichwani, …ndoto za kumuona binti mrembo wa aina ya pekee, na kwa wakati huo wazo la kumkosa mtu aliyempenda sana lilishafutika kichwani, yeye alikuwa kwenye ndoto ya kumuoa binti malikia mtarajiwa, binti ambaye sifa zake zilisha elezewa na mtabiri,kuwa atakuwa mrembo, mwili wake laini, …macho yake malegevu…na sifa nyingi zilizokuwa zikiongelewa kila siku!

Kwahiyo kijana alishampenda kinadharia huyo malikia mtarajiwa, kama walivyo vijana wengine, ambao walikuwa wakiombea nafasi hiyo waipate, ….lakini nafasi hiyo ilitakiwa ipatikane kwa mtu mashuhuri, kutoka kwenye ukoo uliotambulikana, sio kila ukoo ungelipata nafasi hiyo, na ingawaje kulikuwa na koo nyingine bora, na kila ukoo ulikuwa akivutia kwake, lakini nafasi kubwa ilieelkezwa kwa ukoo wa huyu mzee.

Kijana akaishika ile nguo,na kuiinua, hatua kwa hatua,na macho yake yalipofikia kumwangalia huyo binti usoni,bila kujua akataka kuiachia ile nguo, lakini mkono ukashindwa kufanya hivyo, akabakia mdomo wazi, akashindwa kuamini, ina maana huyo binti malikia mtarajiwa anafanana na mtu aliyempenda, haiwezekani.

‘Haraka haraka jamani muda unakwenda…’sauti iaktoka nje na hawa wanandoa ikabidi wafanya haraka, kama walivyoamrishwa hakukuwa na muda tena wa kuchunguzana, akanyosha mkono juu kuashiria kuwa mambo tayari,viegelegele vikatanda, na watu wakaondoka kuwaachia uwanja , ili kazi nyingine ifanyike.

‘Hivi wewe sio Kais,..?’ akauliza pale walipobakia peke yao.

‘Mimi ndiye malikia mtarajiwa, ambaye maisha yako yote yalikuwa yakimtarajia, naahidi kuwa nitakuwa mke mwema na malikia mwema,karibu mpenzi wangu , maana muda unakwenda mbio, tunasubiriwa nje..’binti yule akatoa sauti,sauti ambayo ilikuwa kiburudisho cha huyu kijana kabla, huwa akiisikia mwili wake wote hujawa na raha, leo hii ….

‘Hata sauti kama yake….’akasema kimoyo moyo….na kuingia kwenye zoezi jingine.
Walipotoka hapo baada ya kumaliza hilo zoezi muhimu, wakiwa wameshikana mkono, wakaingia ukumbi wa sherehe, na wakati huo binti kajitanda inavyotakiwa, lakini aliwekewa kitambaa mbele usoni, hakutaka kuonekana mpaka amuone mzee, ..

Kiutaratibu ilitakiwa kijana amtambulishe huyo binti kwanza kwa mzee , mkuu wa ukoo, halafu ndio huyo mzee atawatambulisha kwa waalikwa wote, na ni kipindi hicho, wakati huyo kijana akielekea pale alipokaa mzee, huku akiwa na wasiwasi, akishindwa kujua ni nini kimetokea hadi iwe vile, kwani alikuwa hajajua kwanini huyo binti ndiye aletwe hapo badala ya huyo malikia mtarajia, moyoni, alisema huenda ni mbinu nyingine imetayarushwa na huyo mzee ili kuwazidi ujanja wenzake.

Akawa anamsogelea yule mzee, ambaye alikuwa kajawa na  furana kicheko hadi jino la mwisho, na wenzake wakijipendekeza kwake kwa furaha, huku mioyo yao ikiima, kwani kila mmoja alitaka kijana waoawe ndiye huyo anayemuoa malikia mtarajiwa, …

Kabla kija hajamfikia huyo mzee, mara akaingia kijana mmoja askari, na kumsogelea yule mzee, akamnong’oneza mzee sikioni. Yule mzee akainua uso kwa mshangao, akatikisa kichwa mara nyingi, akawakodolea macho wanandoa hawo, uso uliokuwa umejaa tabasamu na furaha ukageuka na kuwa uso mwingine tofauti.

Mzee, akakunja uso,…sura ikabadilika, unyama ukatanda usoni, na taratibu mkono ukashuka hadi sehemu anapochomeka kisu chake, …akaanza kukuvuta taratibu, …..
******

NB, Hii ni sehemu nyingine ya kisa chetu….najua itakuwa na makosa mengi, umeme umekuwa tatizo, lakini tuwepo pamoja, na ukiona makosa yasahihishe hata kwa ukimiya- kimya.

WAZO LA LEO: Kila lililopangwa na mungu kuwa litatokea, litatokea tu, sisi wanadamu hatuna mamlaka nalo, kwani kauli ya mwenyezimungi ni thabiti, akisema kuwa, hapo hapo huwa.


Ni mimi: emu-three

No comments :