Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, November 5, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni Mzazi-17Ukelele ule uliwazindua walinzi wa eneo hilo, na kujiweka tayari kusikia amri ya mkubwa wao, lakini walishangaa kuona kimiya, na wakati huo msaidizi wa mkuu wa ulinzi alikuwa akihangaika kumtafuta mkuu wake, alipoona kuwa mkuu wake hajarudi, akaona achukua hilo jukumu, kwani huenda ni tatizo kubwa sana, japo kuwa alionywa kuwa asiingie humo ndani;

‘Mimi natoka kidogo, nemitwa nyumbani  mara moja, mke wangu anatarajia kujifungua, naona kuna dharura, sasa wewe angalia hapa mlangoni, hakikisha haingii mtu humo ndani, hata wewe sioni haja ya kuingia humo, maana kilichopo humo na mwili wa wa mtu, ambaye inatambulikana kuwa ni maiti…’akasema mkuu.

‘Sasa kwanini tunalinda maiti mkuu, ..?’ akauliza msaidizi wake, licha ya kuwa alijua kuwa wanafanya hivyo kutokana na amri ya mzee kiongozi wao.

‘Hilo sio swala la kuuliza, najua unajua jukumu lako nini, mimi sitachukua muda mrefu, na usimwambia mtu yoyote kuwa nimetoka’akasema na kuondoka kwa njia za kujificha, hakutaka ajulikane kuwa kaondoka humo, maana hakuruhusiwa kuondoka hapo, hadi Mzee arudi, lakini mke wake ambaye yupo karibu kujifungua kamuita huenda anahitaji msaada.

Alipotoka hapo, alikimbia moja kwa moja hadi nyumbani kwake, na alipofika, alimkuta mkewe anahudumiwa na wakunga, na ilikuwa kama vile alikuwa akisubiriwa yeye kwani alipokanyaga seheu ya kuingilia ndani,  mara, akasikia kilio cha mtoto mchanga kuashiria kuwa mkewe kajifungua, ….na vigelegele vikasikia.

Alitulia kidogo, akisbiri amri ya wakunga, na baadaye yulemkunga mkuu akatoka na kumuashiria kuwa anaweza kwenda kumuona mkewe.

‘Umejuaje kuwa mambo tayari?’ akamuuliza, na yeye akatabasamu, huku akijiuliza  kichwani mbona amesikia kuwa anaitwa na huyu mkunga anaongea kama vile hajui kuwa anaitwa, hakujali akaingia ndani kumuona mkewe, na kwa furaha ile hakukumbuka hata kumuulizia mkewe sababu ya yeye kuitwa kwa haraka hivyo.

‘Nawashukuruni sana , na sina muda wa kukaa ,kwani nimeachiwa kazi kubwa huko, naombeni mumuhudumia mke wangu na nikipata muda nitakuja’akasema baada ya kumwangalia mkewe na mtoto. Moyoni alikuwa na furaha sana, lakini kwa upande mwingine alikuwa akisikitika maana kipindi kama hicho alihitajika kuwa karibu na mkewe , lakini majukumu ya kikazi hayakumruhusu.

Alitoka pale akagundua kuwa katumia muda mrefu tofauti na alivyotazamia, kwa haraka akaingia njia za vichochoroni, na alipofika sehemu ya njia panda,ambapo angeliweza kuonekana, akaingia vichakani na kukatisha mmoja wa msitu, akijichukua tahadahri zote za kutokuonekana na mtu yoyote.

Msitu huo anaujua vyema, kama jemdari, alijua kila eneo, na wapi apite ili afike sehemu anayotaka kufika, na kwa muda huo alitaka atokee eneo la sehemu yao takatifu. Alikuwa akitembea mwendo wa kasi, na mara   akajikwaa,….

Kumbe  ulikuwa  ni mtego wa wanyama, hakuuona, akajikuta akirushwa hewani na kuning’inia juu kwa juu, na haraka akatoa kisu kukata ile kamba, kabla mishale ya ule mtego haijafyatuka, kama ni mtego wa kuua mnyama, lakinikama ni mtego wa kumnasa tu mnyama, haitakuwa na shaka, lakini hakuwa an muda wa kuthibitisha hilo, na hata hivyo kumbe kisu kilikuwa kimedondoka chini wakati aanrishwa hewani.

Ni wakati anahangaika kujinasua ndio akasikia sauti ya mtu,au watu, akafanya haraka kujinasua kwa kutumia mbinu za kivita, akadondoka chini, alihisi alidondoka karibu na miguu ya mtu, lakini hakupata muda wa kumwangalia, kwani alishikwa usingizi mnzito…na alipoamuka ndio akasikia.

‘Mkuu vipi, unaumwa nini…

*******

 Huku makaoni, msaidizi wake alipoona mwenzake hayupo, ikabidi achukua hatua, kwani huo mlio uliashiria kuwa huyo bibi Tabibu huenda anahitaji msaaada wake, akaangalia huku na kule na kuwaashiria vijana wake wawe tayari kwa lolote, kwani yeye anakwenda huko ndani kuangalia kuna nini kimetokea,…

Mlio huo ulikuwa ni ishara kwa upande wa pili, kwani wao walishajiandaa, na walijua huo muda hautakuja tena , na ukipotea bila mafanikio watakuwa wamekosa kila kitu. Mlio huo uliashiria kuwa muda umefika, muda wa kumuokoa binti ambaye anasadikiwa kuwa huenda akawa malikia mtarajiwa.

Kama ilivyopangwa Vijana maaskari wenye sare inayotambulikana walifika hapo, wakisema wamesikia sauti na wametumwa na mkuu , kuangalia kuwa kuna nini kimetokea. Wale maasakri wakasema wakasita kusema lolote, na wale vijana, wakachukua nafasi hiyo kupita kwa haraka, na hata wale walinzi walipotaka kuwazuia wakawa wameshachelewa, wale vijana walisema wao wanafuata amri ya mkuu , jemedari wao.

Walipofika ndani, walimkuta yule msaidizi akijaribu kumuinua yule anayetambulikana kama bibi tabibu, na kabla hajafanikiwa kumuinua ndio akasikia hawo watu wakiingia, akasimama haraka akiwa keshatoa silaha yake, tayari kwa mapambano;

‘Bosi tumetumwa na mkuu, ngoja tukusaidie, maana bibi Tabibu tangu jana hali yake sio nzuri, tulimshauri apumzike, lakini akaona aje aangalie mara moja,… tunamuomba tumchukue akapatiwe matibabu huko nyumbani,…’akasema mmoja wa wale maaskari waliokuja, ambaye haraka alimfikia yule bibi Tabibu, na kumuinua,……

‘Sawa, lakini ni nani aliyewaruhusu kuingia humu ndani?’ akauliza yule msaidizi wa  mkuu.

‘Ni mkuu,….kapatwa na dharura kidogo, lakini atafika hapa muda sio mfupi, na hivi , cha muhimu ni afya ya huyu mzee wetu..au unasemaje mkuu’akasema yule askari wakati keshamweka huyo bibi tibabu begani kutoka naye nje.

‘Mkuu, kapatwa na dharura gani….?’ Akauliza, lakini wale vijana ambao ni wepesi, wakawa wameshatoka nje, na mmoja akasema;

‘Atakuambia mwenyewe akija….’wakawa wameshaondoka. Huyu msaidizi, akawa anajaribu kuwakumbuka hawa vijana, wanatokea kikosi gani, lakini hakuweza kuzikumbuka zile sura, kwani yeye anawajua karibu askari wote kwenye kikosi chake, akauangalai ule mwili, na alipohakikisha hakuna tatizo, akatoka mle ndani, akiwa na hasira kwanini hawo walinzi wamewaruhusu hawo vijana kuingia, na vijana wenyewe hajawatambua vyema ni akina nani.

********
Kwa haraka wakatoka eneo hilo na kuingia msituni, halafu huko wakakutana na wazee, ambao, walimchukua yule anayetambulikana kama bibi Tabibu na kumuhudumia na alipopata fahamu, wakamvalisha nguo maalumu za harusi na kubadilishwa nywele, akavalishwa na kufanana na watu wa humo msituni,usingeliwezsa kujua kuwa ni mimi yule niliyetoka uraiani.

Baada ya kukamilika, nikarudishwa sehemu takatifu na mambo ya harusi yakaanza kufanyika kwa haraharaka, sikuwa najua nini kinaendelea kwa muda huo, woga ulishaniondoka, na kujihisi nipo dunia nyingine. Mara akanijia mzee, mmoja mwenye mvi nyingi, kichwani akasema;.

‘Binti hapa tunakwenda na muda, hili ni kwa manufaa yako na manufaa ya eneo letu, tunatarajia kuwa wewe ndiye malikia mtarajiwa wa eneo hili, ….’akasema mzee, na kunielezea kwa kirafu ni kwanini hayo yametokea, na ni nini wanachoamini.

Nilijitahidi kujitetea, lakini busara za huyo mzee, zilinizidi, , hata hivyo sikuwa na la kufanya, vinginevyoo ningelikuwa chakula cha mamba, au kuingia mikononi mw ahawo waasi, nikakubali shingo upande

Yule binti, ambaye ndiye mimi, nikakubali, sikuwa na jinsi, ikabidi niolewe na tendo la ndoa litimilizwe ili mambo yaende sawa. Kazi ikawa jinsi gani ya kuwashawishi wenzetu, kuwa mimi ndiye binti mtarajiwa yule waliyekuwa wakimsubiri, hilo halikuhitajia haraka, kwani kama ingelichukuliwa haraka, wenzetu wangelifanya fujo, hata kaunzisha vita.

Na hata hivyo kwa jinsi wanavyomjua yule mzee, vita haitaepukika kwani baada ya muda walisikia baragumu la hatari....Baragumu lililoashiria kuwa vita inakuja, wote wakasimama juu, na malikia mtarajia akabakia ameduwaa pale mume wake alipotoka nje na kurudi akiwa kashika upinde na mshale,, ....

'Mke wangu nahisi kuna vita, na nakuahidi nitakulinda hadi tone la mwisho kwani wewe ndiye ubavu wangu, na wewe ndiye malkia mtarajiwa, ...kila mtu anakuhitaji wewe,...'akasema na kuja kumbusu shavuni.


*******

Huku kwa maadui alipoona wale wameondoka, na mwili upo , akatoka na kuwauliza wenzake kwanini wamaruhusu watu kuinga humo ndani. Wao wakasema, hawo watu wamedai wametumwa na mkuu wao,.
‘Kamaunavyowaona wana sare za kikosi chetu, na hawakusubiri, walipitiliza, tulitaka kuwazuia lakini hatuhisi kuwa wanaweza kuleta tatizo, kwanini kuna tatizo mkuu?’ akauliza askari.

‘Wewe huoni kuwa hilo ni tatizo, hili lisirudiwe tena, huku haparuhusiwi kuingia mtu yoyote, hata mimi sikuruhusiwa, nimeingia tu kwa hii dharura, na hili lisijulikane kuwa limefanyika, vinginevyo, mnajua adhabu yake, mtakuwa chakula cha mamba.’akasema kwa hasira.

‘Ndio mkuu tumesikia,…’wakasema wale maaskari.

Yule msaidizi wa mkuu wao, jemdari wa kikosi cha mzee, adui wa mzee wa mume wangu, akawa na wasiwasi kuhusu mkuu wake, kwani alisema hatachelewa, na muda mrefu umepita, mzee anaweza akafika muda wowote, na akimkuta hayupo, wataulizwa na hawatakuwa na jibu la maana, akaona inabidi afuatilie , huenda mwenzake yup hatarini.

 ‘Huyu mtu kapatwa na matatizo gani’ akasema na kumuita kijana wake mmoja na kumuelekeza afuatilie huko nyumbani kwa bosi wake kuhakikisha usalama wake. Na kweli huyo kijana akamfuatilia huyo bosi hadi nyumbani kwake, alipofika huko wakashangaa, kwani huyo mtu wanayemuulizia aliondoka hapo muda mrefu.

‘Msiwe na shaka nitafuatilia nijue wapi alipo’akasema yule askari na kuanza kufuatilia nyayo, wao wanajua njia zao, akazifuatilia hadi alipofika msituni, na kumkukuta bosi wake akiwa kalala kwenye majani, huku kamba ya mtego ikiwa pembeni mwake.

‘Bosi vipi leo kwa mara ya kwanza umeingia mtegoni, maana wewe hunaswi namitego kama hii, ulichanganyikiwa kidogo nini, na unaonekana haupo sawa, kuna tatizo bosi?’ akaulizwa.

‘Oh,kwani kumetokea nini, maana inaonekana nimepatwa na usingizi wa ajabu na hii sio kawaida yangu, lazima kuna kitu kimefanyika, ..’akasema na kuinuka huku akipepesuka, na yule kijana mlinzi akashangaa kwani hajawahi kumuona bosi wake katika hiyo hali.

‘Mkuu naona unaumwa, ..’akasema yule mlinzi, lakini mkuu wake hakujali haraka akakimbia kwa shida hadi kwenye eneo ambalo alikuwa habanduki, kuhakikisha hicho alichokuwa akikilinda kipo sawa, na alipoona ule mwili upo kama ulivyokuwa awali, akatulia na kutafuta sehemu kujiegemeza, na usingizi ukamshika tena.

‘Nafikiri mkuu anaumwa’yule mlinzi akamwambia msaidizi wa mlinzi.

‘Inaonekana …lakini mwache apumzike, kama anaumwa nitamuita bibi Tibabu atampa dawa, subiri kidogo, atulie’akasema huyo msaidizi wa mkuu.

Na mara Mzee kafika, akionekena kuwa na wasiwasi, aliulizia jemedari yupo wapi, masaidizi wake akamwambia mzee, yeye anahisi Mkuu anaumwa, lakini hatakii kupumzika.

Yule mzee, akaelekea ndani, na kwa muda huo jemedari,alishaamuka lakini bado alikuwa akipepesuka, na alipomuona mzee, akajikakamua , kuonyesha kwua hakuna lolote.

‘Wewe naona unaumwa, na nimesikai mke kajifungua, nenda kajitibie, kama utahidi msaada wowote niambie, hapa leo kuna wageni na shughuli muhimu sana, ….’akasema na kwenda kuchungulia ndani  baadaye akarudi pale alipomuacha huyo jemedari akasema.

‘Hutaamini, huyu huenda akawa ndiye yule malikia matarajiwa, nimeletewa hizi taarifa nyumbani, kwahiyo sasa hivi anakuja mjukuu wangu, tutamfungisha ndoa haraka, na mengine yatafuta baadaye, wewe nenda kajisikilizie hali yako na kumwangalia mkeo, nitakuhitaji baadaye kama utakuwa umepona….hii ni bahati kubwa sana’akasema mzee.

‘Hongera mzee,maana kijana akimuoa huyo binti, utawala wote utakuwa mikononi mwetu, na hawa maadui zetu, watatafuta sehemu ay kukimbilia’akasema jemedari.

‘Na nitahakikisha wanaondoka eneo hili, na tutabakia ukoo wetu tu, na wale ambao wapo karibu na sisi, …ngoja hili la harusi likamilike’akasema huyo mzee.

‘Umuejuaje kuwa huyo ndiye malikia mtarajiwa?’ akaulizwa, na yule mzee akiwa na furaha akaanza kuelezea;

‘Nikiwa nyumbani, yule punde wangu akawa anaanza kujifungua, na ujuavyo, ukianza kuyanywa yale maziwa ya mwanzo, baraka inakujia, na ndivyo ilivyokuwa, kwani wakati nameza fundo la kwanza, mlango ukagongwa…

Walikuja wazee wawili toka ukoo wetu, wakiltea taarifa kuwa imegundulikana kuwa hapo kwenye eneo letu takatifu malkia aliyetabiriwa keshafika, na kama ilivyotabiriwa, kafika kwa aina ya kipekee kabisa.

‘Mbona hatujamuona?’ nikawauliza wale watu

‘Hakuna binti aliyefika eneo hilo kwa namna ya kiajabu?’ akauliza mzee mmoja.

‘Hakuna maana mimi muda wote nilikuwepo humo, sasa huyo binti angekujaje nisimuone?’ nikasema.

‘Hebu tuambia wanawake waliofika hapo karibuni?’ wakaniuliza.
Sikumbuki mwanamke aliyefika zaidi ya bibi Tabibu…’nikawaambia.

‘Huyo bibi Tabibu anakuja kufanya nini?’ wakauliza.

‘Kuna mwili uliofikishwa hapo, ambao tunajua kuna makosa yamefanyika, na tunataka kumshitaki mwenzetu, na tuna uhakika kuwa wamefanya kosa, na ikigundulikana ni kosa, huyo mzee na kundi lake itabidi wafukuzwe hapo, na huyo aliyeuleta huo mwili, anaweza kuwa chakula cha mamba, na hilo nimeshalifanyia kazi’akasema.

‘Huo mwili ni wa msichana, na hujuilizi tangu aletwe hapo, kuna dalili yoyote ya kuharibika, maana mwili hata ukiuweka dawa, unakuwa na hali fulani tifauti, je uliwahi kuuchunguza vyema, ?’ akaulizwa.

‘Hapana, sijafanya hivyo, sikupenda kuondoa ushahidi nia na lengo letu ni kumnasa huyu jamaa yetu,…’nikawaambia.

‘Huyo ndiye malikia aliyetabiriwa?’ akasema mzee mmoja.

‘Eti nini…?’ nikawauliza huku nikiwa siamni maneno yao.

‘Hilo ndilo lililotuleta hapa na sasa muda unakaribia kuisha, kwani huyo malkia natakiwa aozeshwe kabla ya saa kumi na mbili na tendo la ndoa lifanyike…na huyo atakayemuoa ili awe kahalalishwa kuwa mfalme, ,mume wa amlikia mtarajiwa…’akaambiwa.

‘Ooooh, kumbe,ndio maana, ..kweli, ..’nikasema na wao wakanipia maagizo na jinsi gani ya kufanya, wakanipa dawa za kumpulizia huyo binti, ili apate kuzindukana na akizindukana watafaunga ndoa na mjukuu wetu,…’akasema kwa furaha.

‘Kwahiyo ina maana sasa hivi wanafungishwa ndoa?’ akauliza jemedari

‘Ndio hivyo, mimi nimeshatoa kibali, na hilo zoezi linaendelea, na ……sasa hivi mjukuu wangu atakuwa mfalume mtarajiwa….wewe nenda kapate matibabu, upate nguvu,…..’akasema huku akiondoka kuingia ndani.

Yule jemedari alitaka kujitetea kuwa haumwi, lakini akaoana haina haja, kwa vile amepata nafasi ya kwenda kuwa karibu na mkewe, na kichanga chao, akaondoka haraka kuelekea nyumbani kwao, na wakati anapita eneo la maadui zao, akaona sherehe za harusu zikiendelea, …

‘Hawa na wao wana harusi,ni nani anaoa na kuolewa,mbona sijasikia …?’ akawa anajiuliza mwenyewe, na alipomkaribia mmoja wa watu waliokuwa wakitoka huko akamuuliza, lakini yule mtu alisita kumwambia chochote kwani anamjua kuwa yeye ni nani, lakini kwa vile ilionyesha dhahiri kuwa ni harusi mmoja asiye na subira akasema;

‘Tumesikia kuwa ni mjuukuu wa Mzee anaoa,….’akaambiwa

‘Mjukuu wa mzee,…?!’ akauliza kwa mshangao, halafu akasema;

‘Anamuoa nani…mbona mimii sijui?’ akajuliza mwenyewe kichwani, huku akikumbuka kuwa hata kwao kuna harusi ya kisiri amayo wanajua kuwa wenzao hawajui. Akawa akiwaza je huenda harusi hiyo nayo inamuhusu huyo malikia mtarajiwa, na huyo malikia mtarakiwa wapo wangapi.

Alipoona anajiwa na maswalimengi bila majibu, akaona ajiondokee, kwani hamasa yake ilikuwa ni kufika nyumbani, kumuona mke wake na mtoto wao. Hata hivyo, kimoyomoyo akaahisi kulifuatilia hili jambo, ili ajue ni nini kinachoendelea, au atamtuma mmoja wa vijana wake afanye uchunguzi, maana yeye kama jemedari ni lazima mambo yote ya hapo hasa kwa maadui zake ayajue.

Alipofika kwake, akakuta vijana wawili maaskari wa msituni, wameshafika nyumbani, wakimsubiri akashangaa , na kuwauliza ni nini kilichowaleta, mmoja wao akasema;

‘Mkuu, malikia mtarajiwa keshapatikana, lakini inavyoonekeana wenzenu wametuzidi ujanja, keshaolewa na mjuu wa mzee wa kwao…

‘Eti nini?’ akashangaa.

‘Kwahiyo mzee, katutuma, kuwa tufike haraka,kwani anataka kuanzisha vita…kuhakikisha tunamteka huyo binti kabla haijafika saa kumi na mbili, hajaolewa, kabla….’

‘Hiyo ni ndoto…tayari keshaolewa, vinginevyo, labda kama tutnataka kuafanya maasi’akasema jemedari, huku akiingia ndani kusalimiana na mke wake na kichanga chake, lakini kabla hajatulia akasikia mlio wa baragumu, mlio ulioashiria hatari, akamgeukai mkewe na kichanga, na kusema.

‘Mke wangu, naona hali sio shwari tena, vyovyote iwavyo, nitawalinda kwa nguvu zangu zote, kwani nyie ndio familia yangu, nyie ndio changu, tuombe mungu iwe salama,na kama ni vita kuna kufa na kupona, yote yakitokea uyakubalia kwa moyo wako…’akambusu kwenye paji la uso, na kumwangalai mtoto wake, akakimbilia nje…

NB: Haya ndiyo maisha yetu yalivyo, kila mtu kajawa na ubinafsi, …hatako mwenzake apate, hata kama anajua kuwa huyo anatakiwa kupata kama yeye na ni haki yake, moyoni mwake hariziki, angalau mwenzake apate ili awe sawa na yeye, na atatafuta kila njia ya kuhalalisha ubinafsi wake,  je kwa mtaji huo tutafika. Tukutane sehemu ijayo.

WAZO LA LEO: Haki inapobezwa, na ubinafsi ukatawala dunia, chuki , husuda ndiyo itakuwa tabia yetu, na amani itakuwa msamiati wa kufikirika. Lakini tukumbuke, sote ni wanadamu tumezaliwa, na muda wa kuishi ni mchache tu, ni nini tunachokitafuta. Tukumbuke kuwa tupo safarini, na yote tutakayoyafanya hapo ndio akiba yetu ya huko kwenye maisha ya kudumu.


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Rachel siwa Isaac said...

Mmmmhhh Utamu kolea ndugu wa mimi...Pamoja Daima!!!!!!

EDNA said...

wenyewe mpoo? nilipita kutimiza wajibu wangu kama jirani mwema.