Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, October 10, 2012

Uchungu wa mwana aujue ni Mzazi-6




Adam alifika mbele ya baba yake, ambaye siku mbili sasa hawasikilizani, maana wazo lake la kwenda Mererani, limekataliwa, na baba yake kamwambia achague mawili kwenda kusoma au kujifunza ufundi kwa baba yake mdogo.Yeye yote hayo mawili hakuyapenda, kichwani kwake kulijaa ndoto za utajiri, na matumaini yake makubwa ni kuwa akifika Mererani atapata utajiri kutokana na madini.

Akawa katulia kusikiliza ambacho baba yake amemuitia, alijua tu ndio hayo maswala mawili ambayo kila siku anapigiwa debe kuwa akasome, au ajifunze ufundi, lakini  alishawaambia kuwa kwenda kusoma watapoteza pesa zao bure, kwani kichwani kwake hakuna kitu cha kuweza kupokea elimu, kichwa chake kimejaa ndoto ya kupata pesa.

Mama yake alikuwa katulia akifuma vitambaa, na ilionyesha wazi kuwa hana raha, alikuwa kakonda kwa mawazo ya maisha magumu. Na Adam kila akiwaangalia wazazi wake na maisha waliyo nayo, huwa roho inamuuma, na mara kwa mara alikwua akijiuliza kwanini wao wamekuwa hivyo, wana kosa gani, mabona wengine wana mafanikio.

‘Lazima nitafute, sitaishi kwa raha,nikiwaona wazazi wangu wanasononeka, wanazeeka kabla muda sio wao, lazima nifike machimbi’akajipa moyo.

Alijaribu kuwaza mbali alipoamuona mama yake vile akifikiria kuwa huenda wazazi wake wamesigishana 
sababu yake, na kama ni hivyo, iliyobakia hapo ni kutoroka tu, kwa umri kama wake, hahitajiki kubishana an wazazi wake, anatakiwa aanza kutafuta maisha yake, `lazimz na mimi nifanye kama alivyofanya mjomba’.  Mara kwa mara alikuwa akiongea na mjomba wake kuhusu maisha, alikuwa madadisi na alitaka kujua jinsi mjomba wake alivyofanikiwa. Akakumbuka kuwa mjomba alitoroka kwao, akiwa darasa la tano,na kukimbilia machimboni.

Akagutuka pale baba yake alipoanza kuongea, na kutulia kusikiliza, ingwaje mawazo yake hayakuwa hapo, baba yake akasema;

‘Nimekuita hapa tena, maana baba ako mdogo, anasema kuna watu wanataka kuchukua nafasi yako, wanataka kujifunza ufundi kwake, sasa wewe una lengo gani maana tumekuuliza kuwa unataka kusoma, hujatupa jibu kwani kama unataka kusoma pesa inahitajika, na hali yetu ndio kama ilivyo, kwahiyo hili tunatakiwa tulijue mapema.

Kama unataka kusoma, familia yetu itajikusanya tuchangishane, hata mjomba wako kasema atatoa msaada wake, ili  uksome sekondari umekataa, hebu tuambia mtoto wetu unataka uwe nani katika dunia hii, dunia hii kama hujasoma, huwezi kuwa mtu, na umri kama wenu na karine yenu, utakuwa mgeni wa nani, ukisema umeishia darasa la saba tu, huoni kuwa utachekwa’akaambiwa na baba yake.

‘Kwani mjomba yeye alimaliza darsa la ngapi, yeye kaniambia,alitoroka shule akiwa darasa la tano na kukimbilia migodini, sasa hivi ni tajiri, anawaajiri watu waliomaliza chuo kikuu…hapo alipo ni kama mtu aliyemazlia chuoo kikuu, hajasoma wala hajasomeshwa’akasema Adam.

‘Unaona akili yako ilivyo changa, ina maana wewe unajilinganisha na mjomba wako, kwasababu ya  utajiri wake alio nao, ule ni utajiri wa kubahatisha, hebu jiulize wangapi wamekwenda huko migodini, mpaka leo hawana kitu, ina maana wao hawataki kuwa matajiri?’ akaulizwa.

‘Ni ujanja wako, unaweza ukawahi usipate, mimi najua nitapata tu, kama hujawa mjanja utabakia masikini, mimi nimeshajifunza mbinu nyingi toka kwa mjomba, nikifika pale najua jinsi gani ya kujichanganya, wenyewe mtaona’akasema akiwa na ndoto za ajabu.

‘Sikiliza mtoto wetu, biashara ya madini ni sawa na bahati nasibu, ni biashara ya kubahatisha, haina muamala, ni hatarai tupu, wengi wamefia huko. Kitu cha muhimu kwako ni elimi, ukiwa na elimu maisha yako hayatakuwa ya kubahatisha, kwani elimu ni mwanga utakuangazia na kujua njia gani upitie’akaambiwa

‘Baba kwanini hamtaki kunipa hiyo nafasi, mimi naahidi kuwa hamtajuitia, nitahakikisha kuwa nawajenega nyumba za kisasa, kama za mjomba, mimi nakumbuka jisni gani mjomba alivyopitia, alishaniahadithia, na mimi nitakachofanya ni kukwepa yale magumu aliyoyoata na kutumia ujanja mwingine, nina uhakika nitafanikiwa, kwa ajili ya maisha yangu na nyie pia’akasema.

‘Ina maana huyo mjomba wako alikusimulia alivyofanikiwa, na akakushauri kuwa uende huko, …huyu mtu hana akili ehe, kama kweli kakushauri hivyio, atakuwa hana maana, lakini hawezi kufanya hivyo, hizo ni akili zako za kitoto tu’akasema mama yake kwa hasira.

‘Hajanishauri kitu, ila mimi mwenyewe nataka kwenda tu, yeye alinikanikatalia siku nyingi, najua kila mtu atanikatalia lakini nikifanikiwa hapa kila mtu atanisifia,…ataniona wa maana’akasema huku akiwaza jinsi gani atakavyo kuwa tajiri, na hatimaye, hata Maua akimaliza shule yake, atakuja kwake na kumuona wa maana. Sasa hivi kasoma, akimaliza hawezi kupenda tena, kwasababu hana elimu, hana pesa.

Alikumbuka barua ya mwisho kuwasiliana, na Maua, ilimtia hofu, aliposema kuwa anahisi ana dalili za ujauzito’

‘Ujauzito, ni nani huyo kampa mimba,…’akasema kimoyomoyo, na akawa na mashaka kuwa huenda keshapata mtu huko na ndiye aliempa hiyo mimba. Hapo akaona aachane naye, licha ya kuwa alikuwa kimpenda

‘Najua atakuja kunitafuta siku akisikia kuwa mimi ni tajiri..lakini kama ana mimba mimi siwasiliani naye tena, na wala asinijue’akajipa moyo,lakini akaapa kuwa hatawasiliana naye tena, hakujibu ile barua ya mwisho akaichanachna kwa hasira, mawazo yake akayaelekeza kwenye kutafuta utajiri, kwa kupitia kwenye madini, na si kwingine ni kwenda Mererani.

‘Huyo mjomba wako mliongea nini?’ mama yake akamuuliza, na kumkatisha mawazo yake, ilionyesha kuwa mama yake kakasirika sana, akihisi kuwa kaka yake ndiye anamharibia mtoto wake, tena wa kwanza.

`Nilimuulizia jinsi gani alivyofanikiwa, na mambo aliyokutana nayo huko ili hata nikifika huko na mimi nijue wapi pa kupitia,mimi sitaki kabisa kumtegemea yeye au mtu yoyote, mimi nataka nitafuta kwa njia zangu lakini niwe kama yeye, niwe na hali nzuri, ili na nyie pie mfaidi matunda ya mtoto wenu, sina nia mbaya,’akasema.

‘Alikusimulia nini…nataka kujua hayo aliyokusimulia hadi ufikwe na tamaa ya kwenda huko, ujue hapa kuna mengine yametokea, na usipoangalai utakwenda jela, …?’ mama yake akauliza kwa hasira.

‘Mambo gani mengine, mama, mimi muda wote nipo hapa nyumbani ,nikitoka ni shambani, sijajiunga na makundi mabaya, …kwanini nifungwe, ndio maana sitakii kuishi hapa, maana watu wanaweza wakafanya ubaya wao, nikasingiziwa mimi…’akasema huku akimwangali baba yake ambaye alikuwa katulia, akisikiliza

‘Kwanza tuambie huyo mjomba wako alikusimulia nini,kabla hatujakuambia mengine ambayo tumesikia,kama ni kweli mmh, sijui utakimbilia wapi, hebu niambie mjomba wako alikusimulia ninii?’ akuliza mama

Ndipo Adam akaanza kumsimulia jinsi walivyoongea na mjomba wake siku hiyo,..

***************

‘Ina maana mjomba hukumaliza darasa la saba, mbona unangea kiingereza safi kabisa?’ akamuuliza mjomba wake siku moja.

‘Mimi nimeishia darasa, la tano, nilitoroka shule, na hata kipindi nasoma, nilikuwa sifiki shuleni mara kwa mara nilikuwa naishia mitaani, baadaye niakona isiwe shida, nikatoroka shule, na kuingia Arusha, na huko ndiko nilipoanzia maisha yangu.’akamwambia mjomba wake.

‘Sasa hicho Kiingereza umejifunzia wapi, maana naona unaongea na wazungu, bila wasiwasi?’ akamuuliza.

‘Ukiwa na pesa kila kitu kinawezekana, mimi ni mjanja wa lugha, licha ya kuwa sijasoma hadi huko juu, lakini nikisikia watu wakiongea lugha yao nikatulia wiki moja tu, naiongea bila wasiwasi, kiingereza ni lugha kama lugha nyingine, hata hivyo, niliamua kujifunza lugha hiyo na masomo mengine, ili iwe rahisi kufuatilia miradi yangu, nakushauri mjomba wangu usome,usije ukaniiga mimi’akaambiwa.

‘Mjomba, mimi kwakweli nataka niwe kama wewe, ….hiyo ndiyo ndoto yangu’akamwambia. Mjomba wake akamtizama, na moyoni akajisemea, `huyu mtoto kaingiwa na tamaa, hajui jinsi gani nilivyohangaika, angelijua asingelifikiria hivyo’.

‘Mjomba maisha niliyopitia sio rahisi kama watu wanavyofikiria, nilipofika huko Mererani, nilipata shida sana, kuna muda nilitamani nirudi kijijini, lakini nia na ari, zikanituma nisikate tamaa, kwani nyumbani nilitoroka, nikirudi nitachekwa, nikajipa moyo kuwa ipo siku  bahati itaninyookea. Niliwahi kuumwa karibu ya kufa, ilifikia muda nikakata tamaa ya maisha kabisa, nilijua kabisa nitafia huko…
`Yaani mjomba wangu maisha ya kule sitaweza kuyasahau ….’akaanza kumsimulia jinsi gani alivyokuwa siku hiyo ambayo kwake ilikuwa ndio siku ya mwisho wa maisha yake,

***********

Siku hiyo, mjomba akasema alipanga kwa vyovyote ajitahidi kujiiba na kuingia kwenye shimo walilokuwa wakichimba, akiwa na nia ya kujaribu bahatii yake ya mwisho, hakuna aliyeruhusiwa kuingia, kwenye shimo bila kibali.Mchana kutwa alishinda humo ndani na wenzake wakichimba na mwisho wa siku wanaambulia posho na vijisenti kidogo.  Hali yake kiafya ilikuwa mbaya sana, kwani alikuwa akimuwa kifua na hakuweza kijitibia.

‘Hapa ukiumwa huna chako…’Rafiki yake akamwambia pale alipoanza kulalamika kuwa anaumwa, akaambiwa;

‘Ni bora utafute miti shamba  utafune, ipo miti shamba na mizizi inasaidia, ili mradi maisha yaendelee, huyu tajiri akisikia tukuwa unaumwa unafukuzwa kazi’mwenzake akamwambia. Basi kwa ushauri huo, akawa  anajikakamua na kweli akawa anatafuta miti shamba na siku zinakwenda, lakini hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya.

Kilichomfanya aingie tena shimoni, ni kwasababu wakati wanachimba mchana kuna sehemu aliiona, akahisi ni madini, hakuwa na uhakika kwa muda huo, alichofanya ni kupafukia vizuri, na kuamua kuwa usiku atafanya kila mbinu aingie ndani, aangalia kama ni bahati yake.

Alijua kuwa ni hatari, kwani wale walinzi walipewa kibali cha kuua, kama watanaona mtu anaingia kwenye hayo mashomo bila kibali. Kuna wengi wameshapoteza maisha kwa kujaribu kuingia. Yeye kutokana na hali aliyo nayo akanona,, basi lollote liwalo, ngoja akajaribu bahati yake.

Hakumwambia mtu, na mbaya zaidi ,usiku huo mvua ikawa inanyesha kwa wingi, kwahiyo watu wengi walikuwa wamjazana sehemu moja kwenye jengo lisilovuja,majengo mengi, waliyokuwa wakitumia ni ya muda, na mvua ikinyesha yanavuja, …

Alichofanya kwa vile kulikuwa na baridi, na hali yake kiafya sio nzuri, akaamua kumauzima mwenzake koti la mvua, na baridi,kwani alishaanza kutetemeka baridi, na hakuwa na nguo nzito. Alipohakikisha kuwa watu wamelala, kwasababu ya kuchoka. Yeye bila kujali mvua, akatoka nje, na mvua ilikuwa inanyesha kweli kweli, kiasi kwamba, mtua kiatembea anakuwa kama anaogelea. Kwa ajili ya mvua, alijua kabisa kwa muda huo walinzi hawpo makini, anajibanza hadi sehemu ya kuingilia kwenye shimo, akafungua ule mlangowa shimo, na kuingia.

Kwasababu mvua ilikuwa inayesha na jinsi kulivyofungwa, haikutakiwa pafunguliwe mpaka mvua iishe, yeye hakulijali hilo alichokuwa anajali ni malengo yake. Akaingia na maji yakawa yanaingia kwa ndani, na na kusababisha ule mlango usiweze kufunga vyema, yeye kwa muda huo hakujali sana alijua ataingia mara moja na kutoka.

Akaharakisha kuingia hadi sehemu aliyoiwekea alama, akachuka kichepe kidogo cha mkononi, alichokuwa kakificha na kuanza kuchimba. Wakati anachimba, alijialaumu kwa jinsi alivyoshindwa kufunga ule mlango, akawa na wasiwasi kuwa huenda maji yakaingia mengi na akashindwa kutoka.

‘Nitawahi kabla majai hayajazidi, na kesho wakigundua hawatakua kuwa ni mimi, na kama ni madini, nitatoweka asubuhi na mapema’akasema.

Haikuchuka  muda akagundua kile alichokiona mchana, akayakusanya yale mawe ambayo kwa muda huo hakuwa na uhakika nayo, akayaweka kwenye mfuko wa nailoni, na akawa bado anatafuta, tamaa ya kibinadamu ikamzonga, badala ya kutoka haraka, akawa anaingiwa na tamaaa huenda ataapta zaidi, mara akaoana maji yanakuja kwa kasi.

Akaanza kukimbilia njia ya kutoka, lakini maji yalikuwa yanakuja kwa kasi tena mengi, akaanza kuhaha, sasa akajua anafukiwa ndani ya shimo. Hakukubali akawa anapambana na maji, yanamrudisha nyuma, yeye anajaribu kusonga mbele. Mara akasikia mtikisiko, shomo lilikuwa linaanza kuporomoka.

‘Mungu wangu nisaidie, maana hii ndio niliona ni bahati yangu ya mwisho, sasa naona kama nitafia humu ndani.’akawa anaomba huku anapigana na maji,na kifusi , kuna muda maji na kifusi kinamfukia, inabidi aanze kazi ya kukichumbua hadi anachomoka, ….

Sasa shimo likaanza kutitia, madongo,maji yakawa yanakuja kwa kasi ,kuelekea ndani kule alipokuwa kasimama, na hapo ikabidi atafute sehemu ya upembeni kabisa asubiri, na kusubiri huko ina maana shimo linajifukia na huenda baada ya muda hewa itakuwa haipatikani tena, akajua sasa mwisho wake umefika.

Pale alipokuwa kasimama, alijihisi kabisa hana nguvu, kifua kinambana, anakohoa, lakini hakukata tamaa alihakikisha kuwa ule mfuko wake, kaufunga vyema ndani ya mwili wake, na mtu asingeliweza kujuwa kuna kitu kajifunga kwa ndani, na lile koti kubwa lilimsaidia ingawaje kwa muda ule alitamani kulitupa,kwani lilikuwa zito kwa kulowana na maji yaliyojaa matope.

Haikupita muda shimo likaanza kuporomoka, sasa hivi ilionyesha dhahiri kuwa  linajifukia lote, na hakuna njia tena ya kutokea nje.akawa anaangalia jinsi shimo hilo linavyoshuka na kujitahidi kukwepa udongo, ulikuwa ukishuka toka juu, na alishajua kabisa hakuna njia ya kuokoka hapo, na ndipo akaanza kuikumbuka familia yake nyumbani, baba na mama yake, kuwa ndio tena hatawaona mpaka siku ya mwisho, akaanza kutoa machozi na kujuta.

‘Oh wazazi wangu mnisamehe, yote haya niliyafanya nikijua kuwa natafuta maisha, sikujua haya yanaweza kutokea, nawaombeni sana mnisamehe, na tukijaliwa tutakuatana ahera…’madongo yakawa yanamporomokea na kumbamiza kichwani, …

NB: Haya ambo ndio hayo,

WAZO LA LEO: Tuwe na wivu wa kimaendelea sio wivu wa husuda, kama mwenzako kapata kapata kwa jasho lake, na wewe jitahidi upate kwa jasho lako, kwani riziki mtoaji ni mola, lakini na wewe ukijibidisha kuitafuta katika njia za halali.


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Maisha nikupambana, huwezi jua wapi pa kupatia, lkn elimu ndiyo dira, huyo jamaa alikuwa na tamaa ya pesa. Sijui ilikuwaje baadaye tunasubiri. Kazi nzuri mkuu

Anonymous said...

Hongera mkuu