Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, October 5, 2012

Uchungu wa mwana aujue ni mzazi-4



‘Ndugu mtaalamu, jambo nililokuitia ni lile lile nililowahi kukuitia kipindi kile,unakumbuka tulivyoongea kipindi kile kumuhusu mdogo wangu, kipindi kile ndugu yangu huyo,alikuwa katika hali mbaya, maana tulishajua kuwa yeye sasa keshawehuka na kuwa  mwendawazimu, lakini dawa zako zikamsaidia.

‘Ulituambia kila ikifikia masika, sasa masika ndiyo hii, imebidi tukuite haraka, maana tumeshasikia tetesi kuwa ndugu yangu huyo keshaanza kuweweseka usiku, nahisi kuna jambo linaweza kutokea, na hili nililiweka akilini mwangu, ndio maana nikakuita, ili utusaidie, najua yote ni majaliwa ya mungu, lakini nyie mliopewa vipaji vya kuona mbali mtusaidie’akasema kaka mtu.

Yule mzee, ambaye kwa kweli ana umri mkubwa, akawa katulia kwa muda bila kusema kitu, akashika kidevu na kutulia kama anatafakari jambo, , akapiga chafya mara tatu,akatikisa kichwa kama wafanyambo mbuzi, akatulia kwa muda bila kusema jambo. Akasimama na kutembea huku na kule, halafu akasimama. Akasema;

‘Haraka, haraka,…jiandae, niliwaambia kuwa huyo ndugu yenu, asipotimiza yale aliyoambiwa na babu yake, huo ugonjwa hautaisha mwilini mwake, kuondoka kwake, ni yeye kukubaliana na msharti ya watu wake. Haya mimi sina uwezo nayo, zaidi ni kujaribu kuomba, ili yasitokee madhara makubwa, lakini….’akaangalia juu na kutikisa kichwa.

‘Tusaidie mtaalamu, maana sisi tumemshauri lakini yeye kasema hawezi kurithi mambo ya uganga, hataki hata kusikia’akasema kaka mtu.

‘Tatizo lake anachukulia vibaya, sio kuwa kila mganga ni mchawi, kuna tofauti ya mganga na mchawi, kuna tofauti ua utaalamu wetu na wengine. Sisi inatujia kichwani tu kama ndoto, na tunakuambia ni nini tatizo, na sisi maadui wetu wakubwa na ni wachawi, watu wabaya,ndio kazi yetu, na ndiyo kazi aliyotakiwa kuifanya.’akasema huyo mzee.

‘Sasa tutafanyaje?’akaulizwa.

‘Chakufanya hapo hakuna, maana waliotaka kumpa hiyo kazi wameshaondoka, na kauli yao ndiyo hiyo, ili asipatwe na hayo matatizo ni yeye kushika mikoba, aanze kuwatibi watu. Niwaambia ukweli yule babu yake namkumbuka sana, kipindi hicho mimi nilikuwa mdogo, babu yake alikuwa anaweza akakuangalia hivi, akajiwa na kitu kama ndoto, akakuambia una tatizo gani, na huyo ndugu yenu alitakiwa kuwa hivyo hivyo, je niwaulize haijawahi kutokea hivyo kwa huyu ndugu yako, kuwaambia jambo na likatokea... ?’ akaeuliza huyo mzee.

‘Mbona sisi ilifikia muda tukihitaji jambo lenye utata, tunakwenda kwake, tunamuuliza je, hili tulifanye au tusilifanye,basi akisema usifanye, halafu ukalifanya, lazima kutatokea tatizo, pia,anaweza kukuangalia machoni akakuambia unawaza nini, na ni kweli ni hicho hicho unachokiwaza. Na wakati mwingine anaweza kusema kuna mchawi anapita, yeye anamuona sisi hatumuoni, basi, mwanzoni tulimchukulia kama mtu aliyechanganyikiwa’akasema kaka mtu.

‘Sio yeye huyo, ana watu wake anaishi nao,wanamuekeleza hivyo, na kuna muda wanakasirika, maana anakiuka miiko,mfano,hatakiwa kwenye familia yake, mke azae kabla ya ndoa, hatakiwi mtu kukiuka masharti ya ndoa,kama kuwa na nyumba ndogo,haitakiwi kuiba, …yapo mashari mengi, kwahiyo ikitokea jambo limeenda kinyume na hayo msharti, basi hapo lazima damu imwagike..sasa nahisi kuna jambo limetokea, tusipowahi,  damu hiyo itamwagika, na ikianza kumwagika, sijui kama kutakuwa na mwisho mwema….’akasema huku akiwa anatizama huku na kule kwa wasiwasi.

‘Mtaalamu sasa tifanyeje, maana hatujui nini kinachoendelea huko tuasidie kama inawezekana tukazuis hiyo damu isimwangike’akasema kaka mtu akiwa na wasiwasi, maana anamjua vyema ndugu yake,mambo yakimuanza hapo, hakuna wa kumshika.

‘Kuna kamba nilikuambia uitafute, unazo?’ akaulizwa.

‘Ipo, lakini ni yas iku nyingi unakumbuka tokakipindi kile..sasa sijui kama ni imara tena’akasema.

‘Tafuteni nyingien imara haraka,…..’akasema huku akitikisika.
Kaka mtu akaagiza mtoto kwenda kununua kamba dukani haraka, na wakati wametulia, mara yowe kilasikika kwa mbali. Yule mtaalamu akasimama, na kutega sikio, akasema;

‘Haya kumekucha, ….tayarisha kamba twende huko kwa ndugu yako tumuwahi kabla hajainua mguu, sasa hivi kuna mambo nimeyaomba, hajainua mguu pale aliposimama, tukichelewa akiinua mguu tu, basi, damu inamwagika, na itakuwa damu ya familia yake mwenyewe..hayo yatakuwa yanatokea mara kwa mara kama  asipotii hiyo amri..haya twende’akasema na kabla hawajafungua mlango, kelele ikasikika kwa nje.

‘Baba mkubwa,mimi ni Maua, nyumbani huko hakukaliki baba kaabdilika tena ….’ilikuwa sauti ya Maua ikitoka nje.

                         **************

‘Habari za hapa mzee, mimi ni mwalimu wa shule anayosoma mwanao Maua,nimekuja na…’akasema yule mwalimu akiwa kasimama kati kati ya mlango, na alipotupa macho mle ndani, akashangaa kumuoma mama mmoja kalala sakafuni na ule ulalaji wake hauokuonyesha heri. Akasita kuingia ndani, akainua uso na kumwangalia yule baba aliyesimama huku akiwa kaangalia upande wake wa  kushoto.

Yule mwalimu akageuza uso kuangalia ule upande wa kushoto, akaona panga limeegemezwa ukutani, lilikuwa kali sana. Akajiuliza moyoni kwanini huyu mzee kasimama, huku kaduwaa, na huku anaangalia lile poanga, badala ya kumsaidia yule mama aliyelala pale sakafuni,na ule ulalaji sio wa heri. Akageuka nyuma kumwangaia Maua. Maua hayupo!

Maua hayupo mbona nilikuwa naye muda wote, akashikwa na mshangao,kwani alijua kuwa Maua yupo nyuma yake, lakini hayupo na hajui kaenda wapi, lakini akajipa moyo kuwa kwa vile wameshafika nyumbani kwao huenda kacheupa kidogo, cha muhimu ni kuongea na wazazi wake kwanza,na kuwakabidhi mtoto wao ili yeye awahi kurudi  huko sheleni.

‘Samhani mzee, nimegonga mlango mara nyingi, nikaona kimiya, na Maua akanishauri niufungue tu, kwani hata yeye…’akageuka teana nyuma kuangalia kama Maua karudi huko alipokwenda,  lakii hakuwepo.

‘Ndio maana mimi mwenyewe nikaamua kufungua mlango, na naona kama mama kaanguka chini, kwani kuna tatizo gani mzee?’ , akauliza mwalimu. Lakini huyo anayemuita mzee alikuwa katuliakimiya kama kaganda, kinahocheza ni mboni za macho, zikizunguka kuangalia kule kwenye panga, na kule mkewe alipolala. Ila kila akitaja jina Maua, aliona kama yule Mzee akitingishika, na sura inaonyesha hasira.

  Mwalimu alipoona hiyo hali akahisi kuna tatizo, akaona labda amsogelee yule mama ili aone atatoa msaada gani,na kabla hajafanya hivyo, akajikuta akipigwa kikumbo na watu wanne walioingi kwa kasi wakiwa na kamba mikononi.

Mmoja kati ya wale akatoa kitu kama unga na kukirusha hewani kuelekea pale aliposimama yule mzee mwenye nyumba, na mwingine akamsogelea yule mzee na kuanza kumfunga kamba mwilini kama vile mtu anafunga mzigo wa kuni,akamzungushia yule mzee kamba mwili mzima. Na cha ajabu yule mzee alikuwa kasimama tu hatingishiki….

Huyu mzee yaani, Baba yake Maua sasa alikuwa anatetemeka mwili mzima, na kilichosaidia ni kuwa yule mtu aliyamfunga kamba alikuwa karibu yake, akamdaka na kudondoka naye sakafuni, kama asingelikuwa yeye angelianguka vibaya,na kwa jinsi walivyomfunga, asingeliweza kujihami. Ssa alikuwa  katoa macho ya hasira, huku akichezesha mboni za macho huku na kule,hata pale alipodondokea, na macho yake yalikuwa yakiliangalia lile panga.

Mwalimu akageuka huku na kule kumtafuta Maua, hakuweza kumuona, na wakati huo, yule mama aliyekuwa kalala chini, alikuwa kaanza kupata fahamu, na alishangaa watu wamejaa nyumbani kwake, na wengi wao ni wanaume.Akawa naye anageuka huku na kule, labda alikuwa akimtafuta mwanae, akihisikuna baya limetokea.

‘Mfungani vyema huyo mtu  kamba , ongezeni na hiyo nyingine, ..’akasema yule mzee mmojawapo aliyekuwa akirusha mara kwa mara kitu kama unga. Na wale wanaume wengine wakawa wanahanaika wakihangaika kumfunga kamba yule Mzee,baba yake Maua, lakini cha ajabu hata walipokuwa wakikaza zile kamba, lakini kila alipokuwa akijitingisha na kuwa kama anajitutumua  zile kamba zilikuwa zikilegea na hata kukatika.

‘Niliwaambia ikitokea hivi muwe na kamba imara, nipeni hiyo dawa ya unga hapo, inabidi tumuongezee dozi, maana huyu si wa kawaida, muwe tayari kwa lolote lile, na bora huyo mama mumuto humu ndani…’akasema mzee mmoja na kuanza kumwagaia yule baba yake maua ile dawa usoni .

‘Kwani tatizo ni nini?’ akauliza mwlimu baada ya kuona kumetulia kidogo.

‘Tatizo ni nini..? hahaha , kwani wewe ni nani, usiyemjua huyu mtu, kama ungelimgusa yule mama,au yeye mwenyewe , ungeliweza kuziharibu nguvu za dawa nilizomzindika nazo, na huyu mzee angelipata nafasi ya kuinua miguu yake. Na  sasa hivi wewe na huyo mama mngelikuwa maiti…wewe hebu ondoa hilo panga,kalifiche mbali kabisa, hilo panga linahitaji damu ya mtu, na funga huo mlango imara kabisa. na mnasubiri nini kumtoa huyo mama, …’akasema yule mtaalamu.

Mwalimu akawa katulia akiaangalia hayo yanayotokea,alishindwa aanzie wapi, kwani mtoto wa watu aliyekuja naye hamuoni, na hajui wapi alipo, akageuza kichwa huku na kule, baadaye akauliza;

‘Maua yupo wapi, nilikuwa naye?’ akauliza, na alipotamka hilo jina, walisikia sauti ya mguno, halafu ikatoka sauti kama ya simba, na wote wakainuka wakitaka kukimbia, lakini kwa muda ule mlango ulikuwa umefungwa, na yule mama ndio walikuwa wakimsaidia kumsimamisha. Lakini wote waliposikia ile sauti, wakawa wametaharuki, na hata wale waliokuwa wakimsaidia yule mama wakamuachia na kukimbilia mlangoni tayari kwa kufungua mlango na kukimbia.

Lakini mlango ulishasindikwa, wakageuka kumwangalia mtaalamu, na yeye alikuwa keshafika mlagoni, akitafita sehemuya kutokea , watu wakabakia wameduwaa, na huku wakitazama wapi sauti hiyo ilipotokea, walipogeuza vichwa vyao, walimkuta yule mtu waliyekuwa wamemfunga kamba mwili mzima kama mzgo,akiwa kasimama vile vila na kamba zake na sasa akawa anazikatakata zile kamba kwa kujitanua , zikawa zinakatika moja baada ya nyingine…,

‘Iteni polisi…’akasema mwalimu, lakini hakuweza kumaliza kauli yake.kwani alikuwa ndiye ya kwanza kushikwa koo, ….

‘Huyo nuksi,... yupo wapi?’ akasikia sauti ya mngurumo mkali ikiuliza’

NB: Tupo pamoja

WAZO LA LEO: Imani zipo, na ni hiari ya kila mtu kuifuata imani yake, lakini sio vyema, kuwalazimisa watoto wetu kwenye imani ambazo hazitawaisaidia katika maisha yao ya baadaye, kwani kwa kufanya hivyo mnaweza mkawaathiri watoto wenu ,na hata kuitahiri familia na jamii yao ya baadaye. 


Ni mimi: emu-three

14 comments :

EDNA said...

Jirani umenena na wazo lako la leo....pamoja sana.

Anonymous said...

Hey! Someone in my Facebook group shared this site with us so
I came to look it over. I'm definitely loving the information. I'm book-marking and will be
tweeting this to my followers! Exceptional blog and terrific design.
Also see my web page - new releases movies dvd

Anonymous said...

Kisa kizuri chenye mafunzo, na wazo lipo makini sana, Ubarikiwe M3

Anonymous said...

Cool blog! Is your theme custom made or did you download it from somewhere? A design like yours with a few simple adjustements would really make my blog jump out. Please let me know where you got your design. Kudos

Anonymous said...

Doing these stretches may help relieve sciatic nerve pain is usually less common causes of backache.
A podiatrist could also occur due to medical intervention and alternative medicine.


Check out my webpage :: Miltona Acupuncture Back Pain
Here is my site : Miltona acupuncture back pain

Anonymous said...

Therе іs alѕo а Мassage fог her
fathег. When уou feel stгesѕ anԁ tension and improves flеxіbіlitу.
Ѕpeaκing at a presѕ сonfeгеnce focuseԁ mοstly on thе face.

In my class оn her last dаys to dо maκe-uρ ωork.
Јust rеmember the tωo C's - comfort and creativity. You should aim to relax your body. It actually took me and my adam was just not interested. In fact minerals, once crystallized, will set off a national debate over whether nursing homes are misusing them.

Review my homepage: sensual massage london

Anonymous said...

The unibody looks amazing and the rigid aluminum body is better than any we have seen.
The world of telephone communication have improved a lot in so many years that it has
become difficult to choose the right kind of system.
Whilst it has potential rivals, macbook air MB450 ( Z0FSQ ) still shocks everyone with its chic design as well as the rest.

Anonymous said...

This will help you to alter the quantity of blur easily and allow camera make other critical decisions when you are shooting.

Of course, doing backup is the best way to
avoid image loss. In order to remove the lens, depress the lens release button and rotate the lens clockwise.


Feel free to visit my web-site d7100

Anonymous said...

Demand is strong and expected to increase over the
coming year. Smartphone survey is an important app for Smartphone users that may keep them busy while giving some beneficial
results. If you don't like to cook or feel like you don't have time, there are apps for restaurants also.


my web-site ... samsung s4

Anonymous said...

It is also enabled with 4G LTE, 3G HSPA and NFC Connectivity.
The basic add-ons that can be considered include carry
cases, belt clips, batteries, chargers, travel adapters and many more.
Fastest mobile data connections (mobile Internet) are supported:
.

My website ... galaxy s4

Anonymous said...

I wanted to tell you that Ι normally viеw this blog
frοm my iphonе, whеn I'm on the way to work, and it is one of the handful of blogs that I have seen that look good on smartphones, and that'ѕ genuinеly remarkаble.


Also visit my weblog huge milf titѕ (http://hornymilfporn.blogspot.com)

Anonymous said...

You can also use some pre-programmed running trails to help you run
faster and boost your workout routine. There are
many online sports equipment shops where you can
browse all of their treadmills. A good rule of thumb
is that if you are taller than 5'5", get a longer belt.

Take a look at my website; treadmill reviews

Anonymous said...

Obviously, these needed someone skilled in antique sewing machine repair to keep them working smoothly.
It isn't hard to find if you know how to look and
where to look. Basic information about maintenance will be available in the
operating manual.

my homepage; best sewing machine 2014

Anonymous said...

While this is all well and good, in order to create the perfect home theater it is essential to learn how
to correctly setup a wireless system. That way, you can sit in various places in your room and shift speakers around until the sound quality is just what you want it
to be. Take your arms and point them straight
to the side (like you're getting ready for a sobriety check, I hear this
is how it starts.

Take a look at my site; home theater speakers