Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, October 15, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-9



Miezi tisa ya machungu ,mateso,maumivu, ilipita kama mchezo, nikiwa ndani yam situ na mikononi mwa watu ajabu, kuna lipindi nilitamani nitafute kitu nijiue, lakini huyu mtu wa ajabu alikuwa anahakakikisha hakuna kitu karibu yangu, kwani alihakikisha kamba aliyonifunga nayo,ilinipa nafasi ya kufukia sehemu ya kujisaidia na upende wa pili, waliweka maji. Maji ambayo yalinisaida kutuliza kiu, maana mle ndani ya handaki kulikuwa na jito sana.

Kwasababu walinichukua nikiwa nimepoteza fahamu, kwa muda huo sikuweza kujua wapi nilipo, nilihisi ni ndani ya handani kwasababu ukiangalia juu unaona ukuta wa shimo. Siku niliyozindukana nilijikuta nimefungwa mwili mzima na majani, yanayotoa harufu mbalimbali. Kutokana na harufi zile nilishindwa hata kuhema, kwano zilikuwa kali sana na mdomoni nilihisi uchungu sana, ina maana nilikuwa nimenyweshwa dawa chungu, nikawa napiga chafya mfululizo.

Baadaye  huyu mtu wa ajabu ambaye nafikiri ndiye aliyenichukua kutoka kule nilipokuwepo,na kunileta hapo, alikuja na kusimama mbele yangu.

Mtu huyu alikuwa na mchomekundu, nywele laini ndefu, inaonekana hajawahi kuzinyoa, na akikuangalia macho yake yanatisha. Alikuwa an ngozi iliyoshupaa kama ya mzee, lakini kwa jinsi alivyokuwa akionekana hakuwa mzee, labda ni kutokana na wanavyoishi na vyakula wanavyokula.

Alikuwa na mkewe, wakawa wanaongea lugha yao ambayo sikuweza kuielewa, lakini yule mwanamke, alionekana tofauti kidogo kisura na huyo mwanaume, yeye alionekana kama sio miongoni mwao, mwili wake na nywele zake zilionekana tofauti.  Hata hivyo yeye  alikuwa kiongea lugha yao, huenda wanawake wapo tifauti na wanaume, niliwaza hivyo mwanzoni, lakini nilikuja kugundua kuwa yeye asili yake sio miongoni mwa hawo watu.

Yule mwananke  akanisogelea na kunishika, akaniuliza najisikiaje, hapo nikajua kuwa kumbe yeye anajua lugha  yangu. Nikajaribu kufunua mdomo,lakini mdomo ulikuw ani mzito kuongea, nikajitikisa na yeye akanielewa, akasogea pale nilipolala na kunigeuza geuza, akaninyosha viungo, halafu yule mwanaume akamshika begani,  wakaongea lugha yao , wakaondoka na kuniacha peke yangu.

Maumivu ya tumbo yalikuwa makali sana, na nikawa najisikia vibaya vibaya , na kuna muda nilijiona kama nataka kupoteza fahamu. Na hali hii ilikuwa ndio hali ya kila siku siku, hawa watu walihakikisha sitoki hapo waliponifunga, kazi yao ni kuniletea vyakula, ambavyo mwanzoni vilinipa shida sana,lakini ikafikia hatua nikaanza kuvizoea, nikawa nakula kuliko kawaida,na mwili ukaanza kunenepa, tofauti na nilivyokuwa mwanzoni.

‘Hali ya humu ndani mimi sitaiweza, nasikia kama kupoteza fahamu, na sijisiki vyema’nikamwambia yule mwananke.

‘Hiyo ni kawaida kwasababu ya ujazuito wako, baadaye itakwisha, kuna dawa tunakupa hizo zitakusaidia’akasema huyo mwanamke, ambaye alionekana kujua dawa nyingi, maana kila nilipolaalmika hali fulani aliondoka na kurudi na dawa ya majani, na kuniambia nitafune au ninuse, na utakuaj ile hali hupungua au kuisha.

‘Kwanini msiniruhusu kutoka nje, maana humu ndani hakuna hewa?’ nikauliza.

Yule mama akaniangalia kwa macho ya huruma, na hakunijibu haraka, alitoak kidogo, na baadaye akarudi, akiwa na maji ya moto, na dawa ambazo aliniambia zitanisaidia kupunguz aile hali ninayoiskia. Aliniangalai kwa muda, baadaye akasema;

‘Hawa watu ni waajabu sana, mume wangu ndiye aligundua pale ulipokuwa ukiishi, alikugundua siku nyingi, lakini aliogopa kukuchukua, akijua jinsi hali ya hapo kwao ilivyo,…’akasema.

‘Hali ya hapa kwao,kwani wewe sio kwenu?’ nikamuuliza.

‘Mimi ni wakuaj huenda kama wewe, lakini hilo kwangu sio la muhimu sana, la muhimu ni kuwa, mume wangu alikuchukua baada ya wawidaji wao kukugundua, na wakati wanapanag mipango ya kukukamata yeye akaja kukuwahi, ili kukuokoa ,na hatukutaka watu wengine wakuone kuwa kakuchukua yeye, lakini wamekuja kugundua kuwa wewe upo hapa.

`Kiutaratibu watu ambao sio kabila lao,hawatakiwi kuchanganyikana,mpaka wazee wahakikishe kuwa unakubali na kufuata mila zao,kuna taratibu zao, na kwanza pia ni lazima upitie kwa wakongwe wa koo, ambao ni wazee sana, wao wanajua siri nyingi za koo, na ni kama , wachawi kwani wanaweza kusema mambo yako, hata yale ya siri, sijui wanajuaje.

`Sasa wazee wamegundu akuwa upo hapa, na wazee wanadai kuwa wewe sio mtu mwema, wanadai ukikaa hapa unaweza kuleta mkosi, kwahiyo wanahitaji uuliwe, haraak iwezekaanvyo, lakini, wamegundua kuwa wewe ni mja mzito, sasa hicho ni kikwazo.Na kuuliwa kwako unahitajika upelekwe ukaliwe na mamba wao wa mizmu.

Niliposikia hivyo, kuwa natakiwa nikawe chakula cha mamba  mwili mzima ulizizima,hasa nikifikiria yale meno ya mamba, na natakiwa nikaatafunwe nayo, nikahema kwa wasiwasi.

‘Wanachosubiri ni wewe ujifungue,maana hawaweze kumuhukumu huyo kiumbe uliye naye tumboni mwako, hilo haliruhusiwi,kwani wanasema huyo kiumbe hana hatia, mwenye hatia ni wewe, ndio maana ukafukuzwa huko ulipotoka, sasa wanasubiri tu ujifungue,na ukijifungua kama ni mtoto mwanaume atapelekwa kulelewa na kundi la wapiganaji wa kijiji, na kama ni mwanamke, atapelekwa kuwa mhudumu wa wazee na wakuu wa koo za hadi hapo atakapopaat mtu wa kumuuoa’

Sikutaka hata kusikiliza hayo maelezo, nilianza kusikia kichefu chefu na moyo ukawa unanienda mbio, na yule mama akagundua na kunipa dawa, ambayo kila nikiitumia inaleta unafuu fulani, lakini kkwa muda ule haikusaidia kitu, nikawa nakijaza tu, ili nisikie nini cha zaidi.

‘Wanadai wewe ni kama uchafu uliotupwa, yaani huko ulikotoka umefukuzwa, na wao hawaweze kuwa jalala la kupokea uchafu’akasema huyo mama.

‘Waligunduaje hayo kuhusu mimi?’ nikamuuliza huyo mama.

‘Nimekuambia vigagula wao, wanajua mambo yasiyojulikana, wanakujua utafikiri walikuzaa wao, wamelezea maisha yako yote, toka ulipozaliwa hadi ukaenda kusoma, na ulianza shule nyingine ukiwa mja mzito,..

‘Mume wangu hana jinsi kwasababu yeye ni mtarajiwa wa kiti kimojawapo cha wakuu wa koo, na ili afanikiwe hatakiwi kwenda kinyuma na matakwa ya koo zao. Alitaka akusaidia kwa kukutorosha , ili uondoke zako, lakini kwa sasa anashindwa,kwani wanadai hutakiwi kuachiwa, mizimu yao inakuhaitaji, inahitaji damu yao, ili iweze kutulia, na kufanikisha mambo yao….sasa’akakatiza maana aliingia mume wake.
Mume wake akamshika bega ,inaonekana ni ishaar zao, huwa mara kwa mara akitaka kumwambia kitu mpaka amshike bega. Wakaonega kidogo, na baadaye wakatoka nje.

Na toka siku hiyo  wakawa kila mara wakija wanakuwa pamoja, na huyo mume hakutaka kumucaha nyuma mke wake, wakawa wanatoka pamoja, kwahiyo sikuweza kuongea  tena na huyo mama,  kwa kipindi kirefu, hadi siku moja, huyo mwanamke akaja akiwa peke yake, na alionekana mwenye huzuni sana, akanipa chakula , na kunichunguza tumbo langu, inaonekana anajua mambo ya uzazi,akasema.

‘Unakaribia kujifungua, na mtoto yupo salama tumboni, lakini yeye ndiye tiketi ya kifo chako, akitoka tu, wewe hutakiwi umaliza hata saa moja, unahitajika ukatupwe kwenye hawo mamba wa matambiko. Na damu yako haitakiwi ibakia kwenye aidhi hii, kwahiyo siku ya kujifungua unatakiwa upelekwe karibi kabisa na huo mto wa mamba.

‘Kuna mwanamke mmoja, atakuja kukuchukua, …ina maana hapa unatakia uondolewe, huyo mwanamke ndiye mkuu wa mambo yao kwa akina mama, na ndiye ambaye anatakiwa kuhakikisha kuwa damu yako haibakii kwenye ardhi yao.

Mimi nimemshauri mume wangu atafute mbinu za kukuokoa, lakini anasema kwake ni vigumu, maana hawo vigagula wanajua kila kitu, kwani wameshagundua kuwa tuna mipango ya kukusaidia ndio maana huko nje wameshaweka walinzi watiifu wa hawo vigagula, wananusa kama mbwa.. Kwahiyo wapo wanatakiw akuhakikisha kuwa kutoka hapa ni moja kwa moja kwenye  huo mto wa mamba.

‘Kwani wewe ni nani na umekujaje kuishi na hawa watu,?’ nikamuuliza, maana nilishajua mimi ni mtu wa kufa tu, na ni bora nijue huyu mwenzangu alikujae hapo. Nilipomuuliz ahilo swali, alitulia kwa muda bial kusema kitu, baadaye akasema;

‘Kisa changu ni kirefu sana, na sikujua kuwa ningeliweza kuishi na hawa watu hadi leo, na kwa vile kuja kwangu kwao, wanadai ilikuwa ni baraka ya familia zo, hawakunizuru. Na nashukuru kuwa mume wangu sio mtu mbaya na pia kwa vile nimeshazoea mila na desturi zao,najionea kawaida tu, lakini mwanzoni nilipata taabu sana. Niliingia mikononi mwa hawa watu siku ambayo sitaweza kuisahau maishani.

*******

Mimi nilikuwa naishi na mama  wa kambo,mama yangu aliachwa na sababu kubwa ni kuwa baba alimpata huyo mwanamke mwingine, na alitaka amuoe,lakini mama yangu hakukubali, basi mama yangu akaambiwa aamue mawili, kuwa akubali kuwa mke mwenza au kuachika. Mama kwa vile alikuw akimjua huyo mke mwenza na alijua kuwa hawatawezekana, yeye akaamua kuachika.Na kipindi hicho mama alikuwa mjamzito.

Ujauzito huo ulikuwa wa kwangu mimi. Taratibu za kuachika zilifanyika, licha ya mama kubembelezwa na familia yao, lakini yeye alikataa kata kata,lakini tatizo lilikuja kuwa mama alikuwa mja mzito, na kiutaratibu aisngeliruhusiwa kuondoaka hapo kwenye familia ya mume wake mpaka mamaajifungue, na mtoto anyonyweshe miaka miwli, ndipo mama aatandoke hapo kwenye miliki ya huyo mume ikabidi mama abakie hapo hadi alipojifungua na kunizaa mimi.

Alinilea hapo zaidi ya miaka mitatu, na wakati huo baba huyo keshamuoa huyo mama mwingine, na kipindi mama anaondoka huyo mama alikuwa mja mzito wa mtoto mwingine. Kutokana na masimango, mateso na vipigo, na hali ya pale, mama hakuwa na jinsi , ilibidi aondoke, ingawaje, hakupenda, ikiziangatia kuwa mimi bado nilikuwa mtoto mdogo. Kipindi mama anaondoka nilikuwa na miaka mitatu hivi.

‘Kama unataka kukaa hapa utakuwa ndiye mfanyakazi wa mke mwenzako, huoni sasa ni mja mzito, na wewe tumeshaachana, ‘akaambiwa na mume wake kipindi hicho huyo mke wake ana ujauzito wa mtoto wake wa kwanza.

‘Mimi nabakia hapa kwasababau ya mtoto wangu, kama unaniruhusu niondoke na mtoto wangu hata leo naweza kuondoka naye akiwa mkubwa nitamleta kwako’akasema mama.

‘Mtoto huyo sio wa kwako, makubaliano yaliyotambulikana ni kuwa wewe ukishajifungua mtoto unakaa naye hadi miaka miwili, zaidi ya hapo ni uamuzi wako tu, ila mtoto sio wa kwako tena, ukumbuke kuwa mimi sishindwi kumlea huyo mtoto,kwasababu ni damu yangu, na ikizingatia kuwa nina mke huyu mwingine, yeye anaweza kumlea, kwahiyo kama unataka kuondoka, njia ipo wazi, lakini mtoto wangu hatoki hapa nyumbani’akasema baba.

Basi mama akavumilia kwa muda huo uliokubalika , akiwa ndiye mfanyakazi wa hapo nyumbani, kuhakikisha anahudumia nyumba, anamsaidia mke mwenzake, na kwenda shamba, na huku akinilea mimi, maana ingawaje huyo baba alidai kuwa mimi ni mtoto wake, lakini hakuwa akinijali kimatunzo, zaidi alikuwa akimjali sana huyo mke wake.

Mama akawa anafanywa kama mtumwa,na huyo mke mwenzake akawa anamnyanyasa hata wakati mwingine kumchapa viboko.Ilikuwa kama watumwa waanvyofanyiwa,hana usemi,hana kujieteta, ikafika hatua mwili mzimzulijaa mizchirizi ya fimbo. Alivumilia kwasababu yangu, alitaka akiondoka niwe katika umri ambao sitapata taabu, na kweli alivumilia mateso  hayp hado nilipofikiamika mitatu.

Siku hiyo alipoonadoka, sitaisahau,maana hapo nyumbani kulikuwa hakuna chakula , kwani kilikuwa kipindi cha njaa, watu wanaishi maisha ya shida sana, na huyo mke mwenzake alishakuwa na watoto wawili tayari na mama ndiye mlezi, mama ndiye yaya, na ndiye jembe la hapi nyumbani.

Chakula kikipatikana kipaumbele ni familia hiyo,mimi na mama tunasubiri kama kuna mabaki,kamahakuna tunalala na njaa,sasa mama yeye alikuwa akihakikisha ananifichia chakula, siku hiyo wakagundua, baba na huyo mama wakatufuma tukila, walituavamia na kukimwagia kille chakula uchafu, na kutulazimiash kula na abada ya hapo wakamvua mama nguo na kuanza kumchapao fimbo, kama mwizi.

Mimi sikukubali, nikaingilia kati na kulala juu ya mgongo wa mama,ili fimbo hizo zisimchape mama, na bahati mbaya yule mama akanichapa mimi kichwani, nikapoteza fahamu, nakumbuka kabala fahamu hazijapotea kabisa, nilianza na maumivi ya kichwa, na giza likawa linanijia machoni taratibu.

Mama aliponiona katika ile hali hakukubali, alimvamia yule mwanamke, wakaanza kupigana naye, na mama kwa hasira akambamiza yule mama chini, na kipindi hicho alikuwa mja mzito, baba ambaye alikuwa pembeni na alikuwa kachanganyikiwa kuona mimi nalalamika kichwa halafu nimetulia kimiya, akajua huenda nimesha kufa, hakuwa anaona yale mapigano ya akina mama.

Alinifuta pale nilipolala, na akaninikuta ndio nageuza macho, akajua sasa wameshaua, akainuka haraka, na kipindi hichoo mke wake, keshabwaga chini, analalamika maumivu ya tumbo. Alipoona hivyo, akamgeukia mama, na kuanza kumsindilia mangumi,,mimi hapo tena sikuweza kuona, maana giza lilishatanda machoni,,…nikapoteza fahamu.

Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Duuh M3 huyo picha inatisha, kisa kipo powa, leo naona hata wazo la siku hakuna!

Anonymous said...

Woω, that's what I was looking for, what a data! present here at this webpage, thanks admin of this web page.
Also visit my webpage :: small loans

Anonymous said...

Thank you for sharing. Not to many people in your position are so gracious. Your article was very poignant and understandable. It helped me to understand very clearly. Thank you for your help.