Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, October 9, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-5Maua alikuwa katulia kwenye chumba huku akimuomba mungu wake, mwanzoni alikuwa anashindwa hata aombe nini. Akawa anajiuliza je nimuombe Mungu  anisamehe kwa hayanmakosa niliyofanya, lakini akajiuliza kichwani makosa gani, na kama ni makosa mbona ni yeye peke yake ndiye anayeadhibiwa, mbona mwenzake waliyeshirikiana naye , hayupo, je na yeye hastahili kuadhibiwa.

Alipowaza hilo akamkumbuka mwenzake, akakumbuka jinsi walivyokuwa wakiandikiana barua, lakini ghafla akawa hamjibu barua zake tena, hasa pale alipoandika kumuelezea jinsi gani anavyojisikia,na kumwambia anaogoa isije ikawa ni mimba. Ilikuwa barua ya mwisho kumwandikia, na hakuweza kupata jibu, na hata alipoandika nyingine, na nyingine, hakiweza kupata jibu kwa mtu aliyetokea kumpenda sana.

‘Hivi huyu mtu yupo aua kapotolea nchi gani, nakumbuka mara kwa mara anakwenda Arusha kwa mjomba wake, ambaye ni tajiri mmoja wa madini,na nia na lengo lake na yeye ni kujiunga kweney biashara hiyo, lakini kwanini asimwambia, au kumjibu baraua zake,lazima nimtafute tusaidiane hili tatizo’akasema huku akiangalia nje kwa kupitia dirishani.

Akawa bado anawaza ni mambo gani kwasasa anahitajika kumuomba Mungu wake, `Au  nimuombe Munguwangu anisaidie nisiweze kuangukia kwenye mikono ya baba, baba ambaye anataka kuitoa roho yangu, bila makosa, ‘ akasema na alipofikia kuwaza hili akatikisa kichwa na akili yake ikawa anajiuliza ‘Ina maana kweli mimi sio mkosaji,hivi kweli sistahili kuadhibiwa kwa kosa hili?’akatulia na kujarabi kutafakari zaidi. Hapo akakumbuka kauli ya baba yake, ambaye kila mara wakiwa naye alipenda kumuasa nayo;

‘Binti yangu nakupenda sana, na jinsi ninavyo kupenda,  nisingelipenda ukaja kuvunja huu upendo nilio nao juu yako, nakuomba  sana usije ukaniangusha, maana kila mtu hapa kijijini anakuona kama mtoto wa mfano, na mimi huwa natamba kwao kuwa  wewe ni binti mwenye akili, binti mwenye nidhamu, binti ambaye hakuna anayeweza kumfikia kwa jinsi ulivyo hapa kijijini’ilikuwa sauti ya baba yake.

Baba yake kweli alikuwa akimpenda, lakini sio ule upndo wa kumdekeza, kwani akifanay kosa alikuwa akiadhibiwa, mpaka anawaza vibaya kuwa baba yake anataka kumuua, na sio kweli anampenda kiasi hicho. Lakini kaam hajafanay kosa, baba yake alikuwa akribu sana na yeye na kila mwaka wakifanya sherehe za shule anakwenda kushuhudia mtoto wake akipewa zawadi ya kuwa mtoto wa kwanza, na wakirudi nyumbani huchinjiwa kuku kama zawadi maalumu. Na alipofaulu kwenda sekondari, baba alimnunulia zawadi nyingi sana.

`Sasa huyu ndiye binti , binti ambaye baba alikuwa akitamba kuwa ndiye binti wa mfano..’, Maua akajikuta akifuta machozi, akaliangalia tumbo lake, ambalo bado lilikuwa halijaonyesha dalili yoyote kuwa kuna kiumbe ndani , akakunja uso na kuanza kujpiga piga tumboni huku akilaani,i hicho kiumbe kilichopo tumboni,utafikiri ndicho chenye makosa akasema;

‘Wewe ndiye umenisababishia haya yote, sitaki hata kukuona, kwasababu bila wewe muda kama huu ningelikuwa darasani nikitafuta elimu. Elimu ambayo wazazi wangu walikuwa wakiiombea kuwa niipate na niwe mtu mashuhuri, na kila mara walikuwa wakinibashiria kuwa nitakuwa waziri.

‘Sasa, hebu angalia muda kama huu mimi nipo jela, nikiwa hapa kifungoni, naogopa hata kukutana na mtu aliyekuwa akinipenda sana, mtu  aliyeweka tegemeo kwangu kuwa mimi ni mtoto wa mfano siku moja nitakuwa waziri wa Afya, je huu ndio uwaziri,…’akatulia na hapo akamkumbuka mama yake, taswira ya jinsi mama yake alivyo huko kwa sasa.

‘Huenda mama yangu sasa atakuwa anapata kipigo kwa ajili yangu,’akawaza huku akijaribu kuivuta sura ya mama yake akilia na kumuombea msamaha kwa baba yake, akama alivyokuwa akifanya siku akikosa na baba yake akiwa akimuadhibu. Alikumbuka barua aliyoandikiana na mama yake siku za mwisho, kwani mama yake ni mpenzi sana wa kuandika barua.

Kwenye barua ya mwishio mama yake alimuandikia barua kuwa kila akimuwaza anavyoumwa moyo wake unamwenda mbio, akihisi kuwa huenda kuna baya linakuja, ana mstari wa mwisho wa hiyo barua mama aliandika,`je binti yangu una tatizo gani, usije ukanifanya nikafa kabla muda sio wangu’

Na mara mawazo yake yakakatishwa na sauti za watu waliokuwa wakiongea nje, ilikuwa ni watu wanapita, au wamesimama kwa nje wakiongea, na akatega masikio kusikiliza wanaongea kitu gani, akasogea dirishani na kuchungulia, kwa kupitia kwenye kipenyo, ndipo akawaona akina mama wawili, waliokuwa wamesimama, inaonekana walikuwa wametokea huko nyumbani kwako;

‘Mhh, mimi kule siwezi kurudi tena, …maana nilivyosikia ile sauti kama ya Simba anayenguruma nikajua kuna Simba’akasema huyo mama mmoja.

Yule mama mwingine akaangalia nyuma, kule walipotoka akionyesha kuogopa, akasema;

‘Unafikiri kwanini huyo mzee kaacharuka kiasi kile, na ina maana hiyo sauti ilikuwa ikitokea mdomomi mwake?’ akauliza mwenzake.

‘Haijulikani, lakini mara nyingi ikitokea hivi kuna sababu ,unakumbuka kipindi kile ilikuwa dada yake kapewa mimba na yule muhuni wa kijiji, ilikuwa ni aibu kwao, maana yule mhuni kila mtu alikuwa hamtaki, sasa binti mrembo kama yule anakwenda kupewa mimba na mvuta bangi, …kwakweli hata kama ingelikuwa wewe ndiye mzazi ungelikasirika sana’akasema mmojawapo.

‘Lakini hawa watu wanaojifanya wasafi  sana, mdio maana  Mungu anawapa majaribu, ili wajifunze, kwasababu sio kwamba wengine wanapenda haya yatokee kwa watoto wao, kila mzazi anajitahidi iwezekanavyo, lakini kizazi hiki kipo kwenye majaribu mengi, sasa wenzetu hawa wanafikia kutamba kuwa kwao ni familia iliyonjema, haifanyi makosa na watoto wao ni watoto wa mifano. Mimi nahisi kuna mtoto kaharibu’akasema mmojawapo,

‘Inawezekana ni yule binti yake anayesoma sekondari, huenda keshapewa mimba, nilisikia kuwa alikuwa akiumwa umwa,na sijui ni nani kampa hiyo mimba’akasema

‘Haiwezekani, yule binti wa mfano, mbona itakuwa ni aibu kwa wazazi, mmh,maana kila mara wanavyopenda kujinadi eti wana binti wa mfano, haya tukione, na sijui ni mtoto wa nani kampa hiyo mimba, maana sijui ataishi wapi, kwa huyo mzee, inabidi ahame.

‘Atakuwa kapewa huko huko shuleni, maana hapa mvulana aliyeonekana kuwa akribu naye ni yule mtoto wa Mererani,….’akasema.

‘Yule mimi najua ni mmoja wa ndugu zao’akasema mmoja, na wakatulia wakiangalia uapnde ule wa njiani, nafikiri kuna sauti inatokea kwa mbali, wakawa kama wanataka kuondoka, na mmoja wao akasema;
‘Mbona sijamuona huyo binti mwenyewe, hapana sio yeye, kama ingelikuwa ndio yeye tungelimuona pale nyumbani’akasema .

‘Akae pale ..ooh, yule mzee akicharuka hivyo anaua, ..kwahiyo atakuwa kafichwa mahali, na inavyotakiwa kama imetokea kitu kama hicho, huyo binti hatakiwi kabisa kukaa kwenye nyumba ya ndugu yao yoyote, maana huyo mzee akiingiwa na hilo tatizo, anajua popote alipo, hasa akikaaa kwa ndugu wao wa damu. Kinachotakiwa ni yeye akakae mbali na ndugu yao yoyote.’.akasema na maneno haya aliposikia Maua akashituka.

‘Kumbe hapa nilipo hakuna usalama ngoja niondoke hapa haraka. Akajiandaa na kuanza kutoka nje, na wakati anafungua mlango, akaona kwa mbali kundi la watu likija kuelekea hapo nyumbani, kundi hilo lilikuwa likija huku likipiga ukelele, kama vile wanamkimbiza mwizi, kwani mbele yao kulikuwa na mtu katangulia akikimbia, kuja muelekea wa hapo nyumbani, alipo Maua.

‘Oohoo, yule ni baba anakuja kwake’akasema  Maua na haraka akatokea mlango wa nyuma, na kuanza kukimbia. Hakuangalia wapi aanpokimbilia, muelekeo wake ni kukimbia mbali na hpo nyumbani, na huko alikokimbilia ni kuelekea msituni.

Msitu aliokimbilia unajulikana kama msitu wa kifo. Msitu huo una wanyama wa kila namana na wanakijiji wanautambua kama msitu wa kifo Huku ukiingia ujue unakwenda kujitafutia kifo chako mwenyewe. Kwa Maua hakuwa na jisni, kwani kif kingne kilikuwa kinamjia, na muuaji si mwingine ni baba yake.

*****
Mama Maua alipofumbua macho na kuona watu wamejazana mle ndani na wengi wao wakiwa ni wanaume akajua kuna tatizo kubwa limetokea na akili yake ilimtuma kwa haraka kuwa  tatizo hilo ni msiba.
‘Kuna msiba wa nani?’ akajiuliza akilini, akaanza kuwaza  familia yake, kwanza aliangalia kulia kwake,hakuona mtu wa familia yake, si mume wake wala watoto wake, akaangalia kushoto kwake, hakuona kitu, akageuka huku na huku akimtafuta  mtu, lakini akili hapo haikujua inamtafuta nani.. oh, akakumbuka….Maua,

Lakini Maua yupo shuleni, akajaribu kuinua kichwa, licha ya maumivu aliyokuwa akiyasikia, akinua kichwa na kuangalia kwa nyuma kiasi kichwa kilivyoweza kugeuka,akamuona mumewe akiwa kafungwa kamba mwili mzima, na kwa muda ule alikuwa ndio anajikakamua kuinuka, na alishangaa kumuona mumewe akisimama kiajabu kama roboti, na alivyoona hivyo, kumbukumbu zikaanza kumrejea, akakumbuka kuhusu mwanae, akageuka huku na huku na mara akamuona mwalimu.

Maua  yupo wapi’ alikumbuka kuisikia hiyo sauti, sauti ambayo baadaye ndio iliyosababisha mengi, ndiyo iliyomzindua. Na hapo, akaona sipoteze muda, akajitahidi kusimama na nia yake ni ili amfikie mwalimu amuulize ni nini kimetokea huko shuleni kwa mwanae, na alitaka kwanza aongee na yeye kabla hajaongea na baba yake, kama kuna kitu kibaya asimwambie kwanza mume wake, kwani baba mtu akisikia itasababisha mengi mabaya, huwa akipandisha hasira mambo yataharibika.

Mama hakuwa amejuwa kuwa mambo yameshaharibika, akataka kugeuka kumwangalia mume wake asije akamtizama akiongea na mwalimu, alitaka aonge na huyo mwalimu kwa siri, na ikibidi watoke nje, lakini alijikuta mwili hauna nguvu, mwili wake ulikuwa kama buwa la muhindi lililokauka. Akamgeukia mwalimu, akamuona macho yake yote yakiwa yanamwangalia baba Maua kwa woga.

Mbona mwalimu yupo peke yake, ina maana kaja kuleta taarifa ya msiba, kuwa huenda binti yake kafariki, hapana, haiwezekani, ….akainuka pale alipokuwa kalala na kwa muda huo, ndio akasikia ule mngurumo kama wa Simba.

‘Oooh, huo mlio tena, mbona balaa..’, akaukumbuka huo mlio.

Mlio huo ni mlio uliokuwa ukimtoka mume wake, siku zie alipoingiwa na tatizo, tatizo lililotokana na wifi yake yaani dada wa mume wake. Mumewe aliposikia kuhusu kupewa mimba kwa dada yake, hasira zilipompanda, akabadilika na kuwa kama mnyama, na akawa anaguruma kama Simba. Sasa huo mngurumo  umetokea tena, ni nani kasababisha hilo, akakumbuka mazungumzo yake na mumewe, kumuhusu binti yao Maua.

Nguvu za ajabu zikamuingia, na haraka akainuka, nia na lengo ni kukimbia na kumzuia binti yake asiingie ndani, kwani akiingia ndani ndio utakuwa mwisho wa maisha yake, na kilichomzidishia zaidi wasiwasi kama  ilivyokuwa wengine ni huo mlio , mgurumo kama wa samba aliokuwa akitoa mume wake. Huwa mara nyingi, watu wakisikia mlio wa samba mioyo yote huingiwa na wasiwasi. Watu husema hata wanyama wengine, wakisikia huo mngurumo, wanagopa, na kutafuta sehemu za kujificha. Watu wote mle ndani wakalimbilia mlangoni.

‘Mambo yameharibika..’akasikia sauti yam zee mmoja, akamtambua kuwa ni yule mzee, aliyekuja kipindi cha nyuma anajulikana kama `mtaalamu’ . Sasa kama mtaalamu yupo mbona  kashindwa kumdhibiti mumewe. Na kabla hajapata jibu, ndio akasikia mwalimu akisema;

‘Iteni polisi..’ na wakati anatoahiyo kauli, baba Maua likuwa keshafika karibu na huyo mwalimu, sijui kwanini alikuwa akimwendea yeye, na kauli yake aliyokuwa akitaka kuisema, ilikatishwa, kwani kabla hajaweza kumalizia, akawa keshawahiwa, aliinuliwa juu, juu kama kitoto,na kabamizwa chini, na kile kishindo, na uwoga, vikamfanya  kapoteza fahamu,…sasa kila mmoja akawa anahaha kuokoa roho yake, na kila mmoja alikuwa akishikilia mlango ili awe wa kwanza kutoka, na badala ya mlango kufunguka ikawa ndio umezuia kwa wingi wa watu.

‘Waliopo nje, mmoja mwenye mbio akimbie akamwambia Maua asikae hapo alipo, ahakikishe hakai kwa ndugu yao yoyote’akasema mtaalamu, na sauti yake hiyo ikamchongea, maana baba Maua alimgeukia yeye, na kabla hajamaliza akashikwa yeye na kuinualiwa juu juu akatupwa chini, na vifaa vyote alivyokuwa kashikilia mkononi, vikasambaratika aliguna mara moja na kutulia kimiya. Watu wote mle ndani wakjua huyo keshakufa, na kama waliamrishwa, walilala chini, kichwa chini, hakuna aliyetaka kuinua kichwa.

Mara mlango ukafunguliwa, walipoinua kichwa kuangalia ni nani kaufungua, ndio wakakuta mama Maua akiwa kamshikila mumewe mguu, akamzuia asitoke nje, mama alishaamua kujitosa yeye mwenyewe, kwanza kwa ajili ya kumuokoa mume wake,kwani alijua akitoka hapo, anaweza akakimbia na kupotea kusipojulikana, lakini zaidi ya hayo ni uchungu wa mwanae, kuwa akitoka hapo anakwenda kummaliza binti yake.

‘Mume wangu tafadhali, tulia…’akawa kamshikilia huku akiwa keshadondoka chini na alikuwa kama kapiga magoti. Huku kamshikilia mumewe mguu, mwanzoni mumewe hakumjali, na ilionyesha hana habari na yeye, hakufanya kama alivyowafanyia mwalimu na mtaalamu, akawa anajivuta huku akimburuza mkewe ambaye alikuwa kashikilia mguu wake.

‘Jamani nisaidieni mshikeni asitoke, akitoka hapa atakwenda kumuua binti yangu…’akawa anasema mama Maua huku kamng’ang’ania mumewe mguu, lakini kila mtu nani aliyekuwa na uwezo wa kuinua hata kichwa, wote walijfanya hawajasikia, wamalala chini huku wameangalai chini, kama vile watu wanapoingiliwa na wezi wanavyofanya.

Baba Maua alipoona kashikiliwa mguu, akautumia mguu mwingine kumpiga teke mkewe , tele lile lilikuwa na nguvu zaidi ya tele la punda, lakini mama mtu aling’ang’ania ule mguu wa mumewe akijua sasa anaokoa maisha ya binti yake ni heri yeye afe kuliko kumuachia huyo mtu ambaye hapo alipo, sio yeye tena.
Teke la pili likamfikia mama wakati huo keshaanza kuona vinyota vyota usoni, mwili ukaanza kuisha nguvu,na mikono ukalegea, na hakuwa na nguvu tena ya kumshikilia, kwani fahamu zilianza kumpotea, na hata hivyo angalau alishaweza kupunguzia kasi  ya huyo mtu, kani kuna watu nje,  walishakimbilia huko alipo Maua, ….

Baba Maua akatoka nje, na kuanza kukimbia, alikuwa akikimbia kutokana na hisia zake, hisia zake zilimtuma kuwa Maua yupo kwa kaka yake…mbio za ajabu kabisa,kama mtu anapaa…

NB: Haya mambo ndio hayo, japo kwa shida, tutafika tu

WAZO LALEO: Usione kwa mwenzako ni rahisi, kwa vile wewe halipo kwako, tujue ugumu, au urahisi  wa jambo, au maumivu ya jambo ni  lile lile kwa kila mtu, liwe limetokea kwa mwenzio au kwako. Cha muhimu ni hekima na busara, ukijua kuwa leo kwake kesho ni kwako.

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

Hongera mkuu, kazi nzuri, lkn nina wasiwasi kuwa kuna wanaoneemeka kwa jasho lako, bongo hapa, watu wanapenda ubwete!

Rachel siwa Isaac said...

Duhhh..Ndugu wa mimi upo zaidi ya juuu!!
Asante kwa Wazo la Leo..maneno ya uhakika kabisa ,Pamoja Daima Ndugu wa mimiiiiiiiiii

Anonymous said...

I think what you published ωas aсtuallу very reasonable.
Hοωeѵer, think on this, suppose you wеrе to create a killer headline?
I meаn, I don't wish to tell you how to run your blog, but suppose you added a title to possibly get folk's attentiοn?

I mean "Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-5" is kіnda vanilla.
You coulԁ pеek at Yahoo's home page and see how they create article titles to get viewers to click. You might add a related video or a pic or two to grab readers excited about everything'νe gоt to saу.
In my οpinion, іt woulԁ maκe your posts a little livеlieг.
Feel free to visit my web-site :: payday loans uk

emu-three said...

Moja ya lengo langu wakati naanzisha hii blog, ilikuwa `KUKITUKUZA KISWAHILI'.

Imekuwa ikiniuma sana kuona lugha kama hii ambayo kwasasa inaongewa na watu wengi, haijapewa kiwangaoo cha kimataifa. SIJUI KWANINI.

Kwahiyo mimi imenivuta kuandika visa hivi kwa kutumia lugha yetu, na kutumia misemo yetu ya Kiswahili, ili kuwajenga watoto wetu waipende, na wakisoma waelewe nini maana ya misemo kama hiyo.
Kwa mtu ambaye hajui kiswahili, au hakitthamini ataona ni misemo tu, lakini misemo hiyo ina hekima sana.

Nawashukuru wale wote wanaonishauri kuwa niweke vichwa vya habari vya kuvutia, ili mtu avutike kusoma kilichopo ndani.

Ni sawa, sikatai, nitafanya hivyo, lkn, kwa nia njema ya kuelemisha, sio kibiashara zaidi

Ahsanteni na karibu sana

Anonymous said...

I am not sure wherе yοu're getting your information, but great topic. I needs to spend some time learning much more or understanding more. Thanks for magnificent info I was looking for this info for my mission.

Feel free to surf to my web-site: instant payday loans online
Here is my blog ... Pay Day Loans

Anonymous said...

Unquеѕtionably believe that ωhich уοu saіd.
Your fаvorіte reaѕοn appеaгed to be on the net the simplest
thing tο be aωare of. I sаy to
you, I definіtelу gеt irked ωhile
pеоplе think abοut worriеs that theу рlainlу
dο not knoω about. You manageԁ to hit the nail
upon the tοp as well аs defіned out the whole thing without haνing sidе-effectѕ , peοple
could taκе a signal. Will probablу bе baсκ to
gеt morе. Тhаnκs

my ωeb ѕіte :: Payday loans online no credit check
Also see my page - payday loans online