Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, October 3, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-3



‘Baba Maua hapa nilipo moyo wangu haunitulii, nahisi kama tutapokea taarifa mbaya’akasema mama Maua, huku akiwa kashikilia shavu.Mumewe akamwangalia kwa muda huku akiwa ananoa panga lake.

‘Hizo hisia zako mimi sizitaki, kwanini uwe unajipa wasiwasi, kabla ya jambo, huoni unajiumiza mapema, hata kama jambo hilo litatokea, kwanini usilisubiri kwanza, cha muhimu ni kukubali kuwa kila jambo kama limepangwa kutokea litatokea tu, jambo jema ni kulisubiri, ‘akasema.

‘Mimi namuwaza mwanagu huko shuleni, kwani taarifa hizo za mara kwa mara kuwa anaumwa, na hadi kufikia kudondoka mara mbili na hata kupoteza fahamu zinanitia wasiwasi sana’akasema mama mtu.

‘Lakini kule yupo shuleni, yupo na wasomi, walimu wao wanajua jema na baya kwa watoto, wanajua kulea hata kuloko wewe mzazi, na pia ukumbuke kuwa shule yao ipo karibu na hospitali kubwa ya wilaya, kwahiyo akizidiwa atapelekwa hukohospitalini, mimi hilo halinitii wasiwasi sana, labda kaam kuna jingine’akasema baba mtu.

‘Tatizo lenu wanaume, hamjui uchungu wa mtoto, sisi wanawake kwa vile tulibeba ile mimba miezi tisa na kupambana na machungu ya kuzaa, huwa kila ukiwa na wasiwasi na mtoto wako yale machungu ya uzazi unayahisi mwilini, ndio maana wanasema uchungu wa mwana aujue ni mzazi’akasema mama.

‘Lakini  hapo uelewe kuwa mzazi  ina maana baba na mama, kwasababu wakati upo kwenye uchungu na mimi huwa nakuwa kwenye uchungu pia japo ni wa kimawazo, nakuwazia wewe afya yako, na kuwazia wewe uzima wako, na hatima yake. Wewe huwezi jua jinsi gani tunavyojihisi wanaume pale mnapokuwa kwenye uchungu, sio kwamba kwa vile sisi hatubebi mimba ndio hatuhisi huo uchungu au kubeba mimba tumboni miezi sita ndio hatuna hisia ya watoto wetu,tunayo huenda hata zaidi ya nyie’akasema baba mtu.

‘Mimi kwa kweli namuwaza sana mtoto wetu, kama hatutapa taarifa nyingine inabidi kwenda huko kusikia nini kinaendelea’akasema mama huku akiinuka na kuweka vyombo vyake sawa, na baadaye akaingia ndani, na mumewe akamfuata, akitaka  waliongelee hilo swala vyema, kwani alishahisi kuwa huenda kuna jambo mke wake aanamficha.

‘Sawa mimi nitakwena kujua nini kinaendelea hatuwezi kuondoka sote, wewe utabakia na nyumba na mifugo, inabidi nikajue kuna nini, na kwanini mtoto wetu ashikwe na maradhi kama hayo wakati alikuwa hata tatizo kama hilo kabla’akasema baba mtu. Na mama akatulia kwa muda bila kusema neno, na mumewe akamkazi macho na kusema;.

‘Au una mawazo gani, maana ulivyotulia unanipa wasiwasi, na maneno yako kuwa wanawake ndio wana uchungu sana yananipa wasiwasi, usije ukawa unajua nini kinachimsumbua mtoto wetu, halafu hutaki kuniambia’akasema baba mtu akizidi kumkazi macho mke wake,ambaye alikuwa kainama chini.

‘Mume wangu ningelijua nisingelikuwa na wasiwasi huu hapa,kama ulivyo wewe ndivyo nilivyo mimi, ningelijuaje wakati mtoto yupo shule, lini mimi nilikwenda huko shuleni’akasema mama mtu

Mke wake akainua kichwa kumwangalia mume we, na moyoni akawa anahisi uwoga,uwoga ambao ulimtinga baada ya kusikia kuwa mtoto wao amedondoka mara mblli huko shuleni na kupoteza fahamu, na  amekuwa akindamwa na homa za mara kwa mara, moyoni alishaanza kuhisi jambo jingine, ingawaje alijipa moyo kuwa huenda ni hisia tu.

‘Hizi sio dalili za uja uzito kweli?’ akawa anajiuliza akilini, akainama chini akiwaza, na hapo hakutaka kumwangalia mumewe machoni, kwani mumewe akimwangali tu machoni, huwa ni mwepsi kugundua nini unachokiwaza, na mara nyingi alikuwa anaona ajabu kweli, jinsi gani mumewe alivyokuwa na ujuzi wa kumgundua nini anachokiwaza.

‘Mume wangu wewe una nyota ya uganga, ungelikuwa na tamaa, ungeshajiingiza kwenye mambo ya uganga wa kienyeji, maana ukimwangali mtu machoni, unagundua kuwa anawaza nini, na hukosei ,unajuaje?’ siku moja alimuuliza.

‘Babu yangu alikuwa mtaalamu wa kijiji, enzi hizo, huenda nimerithi toka kwake, ila mimi mambo hayo siyataki’akamwambia. 

Basi ili kuhakikisha kuwa mumewe hagundui nini anachokiwaza, akawa anajitahidi kumkwepa ili wasiangaliane, na huku kichwani akiwa katingwa na mawazo mengi, akajisemea moyoni;

‘Mungu wangu kama ni ujauzito mbona itakuwa ni balaa,…..sijui kutakuwa na usalama gani hapa nyumbani, nimjuavyo mum e wangu, hatakuwa na subira, ni bora kama ni mimba nitafute njia za kuondoka hapa nyumbani mapema, nikajifiche mahali hadi hasira zake zipoe,na sijui huyo binti atakwenda kuishi wapi….hili ndilo linanifanya nisiwe na amani’akajisema moyoni, akikumbka jinsi mume wake alivyompiga dada yake wa tumbo moja karibu ya kumuua pale alipogundulika kapata mimba kabla ya ndoa.

Mume wake anasifika hapo kijijini kwa hasira za haraka , na akipandwa na hasira hakuna anayeweza kumuingia. Huwa akikasirika anakuwa kama mnyama, na watu wote humkimbia, kwani anaweza kuua, alishafungwa kwa kosa la kuua, ingawaje baadaye iligunduka kuwa mwenzake ndiye aliyesabaisha hadi yote hayo yakatokea, na baada ya kutumikia miaka kadhaa jela akatolewa kwa msamaha wa raisi.

Ilikuwa ni kosa la utani, wakati wanamgombea yeye kama mke mtarajiwa, na huyo rafiki yake, akasema kuwa yeye ni mwanaume zaidi ya mwenzake, ukazuka ugomvi, ugomvi ulisababisha mapigano ya hali ya juu, ni nani zaidi ambaye anaweza kumuoa yeye. Mapigano hayo yaliweza hata kuingiza vita vya familia mbili, hapo ndipp kijiji kikamjua huyu mtu kuwa akipandwa na hasira anakuwa kama simba. Aliweza kupambana na mgambo kumi wa kijiji na wote akawatupa chini kama takataka, na hakuna aliyeweza kumsogelea. Huyu mtu alipambana  na Simba peke yake na kumuua.

Siku dada yake alipogundulikana kuwa kapata ujauzito na aliyempa mimba hiyo ni mtu ambaye hakutakiwa amuoe, kaka mtu alitoka hapo mbio hadi kwenye hiyo familia ya huyo mwanaume  na kuanza kumpiga huyo mwanaume, hata ndugu za hiyo familia ilipoingilia haikuweza kumshinda nguvu,…aliwasambaratisha wote, ikabidi waite polisi, na hata polisi walipofika walishindwa kumkkamata, hadi wlipotumia risani za moto na kumjeruhi, na kupoteza fahamu kwa siku mbili.

‘Huyu mtu bwana akiongea huwezi jua kuwa ana hasira za kuua mtu, huwezi kabisa kumfikiria hivyo, ole wako akasirika, anabadilika kabisa, anakuwa sio yeye tena, ana hitilafu fulani kwenye ubongo wake, ni kama kichaa, lakini hakitokei mpaka akasirika, hiki ni cha kurithi, hakitibiki, cha muhimu huyu mtu msije mkamkasirisha’alisema mmoja wa madakitari, waliokuja kumpima huyu mtu kipindi alipoumizwa kwa risasi.

Mkewe anamjua vyema  mume wake, ndio maana kila mara akiwaza kuhusu mtoto wake,aliombea mungu isije ikawa ni mambo ya uja uzito. Lakini hilo hakulipa uzito sana, kwani anamjua vyema mtoto wake, walijitahidi sana kumlea katika maadili mema, na moyo hakutarajia kuwa anaweza kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi, na hata siku anaondoka walimtahadharisha na mambo kama hayo na yeye aliahidi kuwa kamwe hata danganyika, sasa ni nani kamdanganya, au ni hisia zake tu.

‘Haiwezani, haiwezekani, mungu niepushia na haya mawazo mabaya kwa mtoto wangu’akasema mama mtu.Mama mtu alishituka pale mumewe alipomshika bega, na kusema;

‘Hebu niambie kama unahisia zozote kuhusu mtoto wetu, unahisi anasumbuliwa na nini, au kakumbwa na mashetani’akasema baba mtu akijaribu kupata nafasi ya kumuangalia mkewe machoni, lakini mkewe alilijua hilo akajifanya anashughulika, ilimradi mumewe asimwangalia machoni.

‘Hapana mtoto wetu hawezi kukumbwa na vitu kama hivyo, nahisi kuna tatizo jingine’akasema mama mtu.

‘Tatizo gani, mbona huniweki wazi, ….usije ukawa unalijua hilo tatizo na mimi huniambii, nakuomba tafadhali, kama kuna tatizo uniambie mapema, maana mimi sitakuwa na msamaha, sitakuwa na msamhana, narudia tena, mimi sitakuwa na msamaha, kama ni tatizo kama lile la shngazi yake, na ole wake ije itokee kuwa ni mambo yenu nyie wanawake ya kudanagnyika na wanaume, sijui itakuwaje, sitapenda nimuone huyo binti kwenye nyumba yangu,….hilo naliweka wazi kwako’akasema mumewe ka hasira.

‘Baba Maua unaongea kitu gani, huyo ni binti yako, na kama likitokea jambo kama hilo tunatakiwa tuwe na subira, tujue jinsi gani ya kumsaidia’akasema mama mtu.

‘Unaona….mimi nilishahisi kuwa una jambo unalijua na hutaki kuniambia, ndio maana unaongea hivyo, hutaki hata kuniangalia machoni, nakuapia kuwa kama ni hilo tatizo huyo binti asikanyage hapa nyumbani kwangu. Sitaki kabisa huo mkosi hapa nyumbani kwangu. Mtoto wa kwanza anizalie kihuni, haiwezekani, hilo kwenye family ayetu ni mwiko’akasema huku akishika kiuno.

Baba Maua usiseme hivyo, kumbuka huyo n binti yetu’akasema mkewe sasa akihisi miguu ikimwishia nguvu.

‘Najua huyo ni mtoto wetu, lakini katu sitakubaliana na uchafu huo, unajau kwenye familia yetu toka enzi za mababu, haijawahi kutokea hilo, aliyekuja kuharibu ni huyo dada yangu,na kiutaratibu alitakiwa ama auwawe, au afukuzwe kabisa kwenye familia yetu,watu wakalikumbati hilo,na matokea yake ni kuwa ni lazima litakuja kujitokeza tena, sasa sitaki lijitokeze tena kwenye family yetu, hasa ya kwangu’akasema huku akigonga ukuta kwa ngumi.

‘Hiyo ilikuwa zamani, kumbuka hizki kizazi cha sasa hivi kina mitihani mingi, mtu anaweza akabakwa,au akaingizwe kwenye vishawishi ambavyo atashindwa kuvumilia’akasema mama, na mumewe akamwangali mkewe kwa macho ya kutisha, akasema;

‘Mimi ,labda isiwe ni mimi, ikitokea hivyo, unavyowaza wewe, ….nitahakikisha naichachana hiyo mimba yake kwa mikono yang,hadi hicho kiumbe kitoke humo tumboni, na nitahakikisha huyo aliyempa hiyo mimba anakitafuna hicho kiumbe na kukimeza…..naomba isje ikawa hivyo, maana sijui..mungu wangu, naomba sije ikawa hivyo, maana ndoto za kuua zinaniandama…’akasema na kuanza kuondoka huku akihema kama samba, na kabla hajaugusa mlango kuufungua mara wakasikia hodi toka nje.

Mama akasimama kwa wasiwasi, na kumwangalia mumewe na mumewe akaangalia ule mlango , halafu akamwangalia mkewe, akasikiliza ni sauti ya nani, utafikiri ni usiku wakiwa na wasiwasi  wa mgongaji, lakini ilikuwa mchana wa saa nane, hisia zikawa zimegongana, kuna mtu na mtu huyo anataarifa zisizo njema;

‘Hodi hapa wenyewe , mimi ni mwalimu….’ile sauti ilipopenya masikioni mwa mama, ilikuwa kama mtu akamzaba kofi masikioni , na kuziba masikio yake, kichwa kikatanda ukungu, akahisi mwili ukimuishia nguvu.

Mama akaanza kutetemeka, akahisi damu ikimwenda mbio, shinikizo likaanza kupanda, na mara akashikwa na kizunguzungu, na kabla hajasema karibu akadondoka chini, baba mtu akawa  kaduwaa,  macho yakamfunguka kama vile kaona kitu cha kutisha, akainama kumwangalia mkewe, akageuza kichwa na kungalai pale alipoweka panga lake, na kabala hajatulia mlango ukafunguliwa……

NB Hebu niambie kama wewe ungelikuwepo hapo ungelifanya nini, sijui kulitokea nini, naomba tuvute subira.

WAZO LA LEO: Tahadhari ya jambo lolote ni bora, kuliko kusubiri litokee jambo, Kama kuna njia ya kujihami, kama kuna uwezekano wa kujikinga, ni bora tukachukua tahadhari ya kujikinga. Tusiwe wepesi w akuzarau, eti litakuja na litazoeleka, eti, ni tamaa, zinaweza zikazuilika. Tujue kuwa biandamu tonatofautiana, hulka tabia na uvumilivu. Tusicheze na maisha yetu ,tusicheze na afya zetu, …Wahenga walisema, kinga ni bora kuliko tiba
Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

My bгοthеr suggested I might
like this website. Ηe wаs entirely right. Thіs post truly madе my dаy.
You cann't imagine just how much time I had spent for this info! Thanks!
Here is my web site :: quick loans

Anonymous said...

Kama unaangalia muvie, napenda weye!