Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, October 23, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-13Wazazi wangu walikaa muda mrefu baada ya kuoana bila kupata mtoto, wao wenyewe walijionea ni kawaida tu, wakijua kwa vile hawana tatizo lolote la kiafya ni swala la muda tu, kwani walishachunguzwa na kuonekana kuwa hawana tatizo. Wao walijipa matumaini kuwa ipo siku watapata mtoto, hawakujali sana, lakini ndugu na majirani, walikuwa ni tatizo, hawakuisha kuwasumbua, na ndio waliochangia hata wazazi wangu waanze kuhangaika.

Kuhangaika kwao ndio kunanitia uchungu,maana hata nikifika jijini,sipendi watu wanione,…wakiniona naangaliwa kwa jicho baya, nanyoshewa vidole,nanyanyapaliwa kwa kitu ambacho hata sikijui, na sina uhakika kama ni kweli au …mungu mwenyewe ndiye anajua.

Wazazi wangu walikuwa kila wakikaa, hodi ikipigwa, wanaogopa hata kufungua mlango,maana mtu akija mazungumzo ni hayo hayo,..

‘Nyie mbona hamzai,ina mana hamtaki watoto?’ wakawa wanaulizwa.

‘Bado hatujajaliwa, ipo siku tutapata watoto kwani yote ni majaliwa ya mungu’akasema mama na baba.

‘Nyie kaeni kusema hivyo hivyo…ni majaliwa ni majaliwa siku zinakwenda, mnatakiwa muhangaike, mengine yanahitajika kuhangaika, sio yote yaliyopo yapo kama yalivyo, kuna nguvu za giza, hangaikeni…’ siku alikuja mmoja wa ndugu zao, akawa anawashauri.

‘Lakini ndugu yangu, tumeshakwenda hospitalini wakatuchunguza afya zetu na kumchunguza mke wangu njia za uzazi, wakaona hakuna tatizo, na mimi mwenyewe walinichunguza wakaonahakuna tatizo, kwahiyo mimi nionavyo ni mipango ya mungu,’akasema baba.

‘Hili siwakatalii,huko ni kwa wataalamu wa kisasa, lakini zamani hatukuwa nao, tulikuwa na njia zetu za asili na zilikuwa zikitusaidia, wapo watu wa namna hiyo hadi sasa, wana dawa, wana njia za asili za kuzindua kizazi kilicholala, ‘akasema huyo mzee,

Hata alipoondoka wapendwa hawa wawili walikaa na kujadiliana, wakaona hayo yote ni majaribu, wakijikita kwenye mambo hayo huenda wakaingia kwenye mitego ambayo hawakuipenda. Wakakubalina wazidi kuvuta subira.

Wazazi wangu walikuwa ni watu wenye msimamo wao, na kwa vile walikuwa wameishi mjini Arusha na kuishi na wazungu, na wasomi mawazo yao yalikuwa hayafanani sana na pale kijijini, licha ya kuwa walikuwa mara nyingi wanarudi na kuishi hapo kijijini.

Baba yangu alikuwa mafanyabiashara, alianzia mbali sana, na kuna muda alikuwa tajiri ,kuna muda alifirisikia , kwahiyo alikuwa akijua amisha yote, na hakuwahi kukata tamaa. Na kipindi hichoanasakamwa, alikuwa yupo kijijini, alikuwa kafungua duka kubwa hapo kijijini.

Mama naye hakukosa watu wakumshauri,na siku hiyo alikuwa akisemwa na mama mkwe, ambaye aliona kuwa hunda mama ana tatizo, ndio maana hawataki kwenda kwenye sehemu nyingine, wakiwa na maana kwa wataalamu, waganga wa miti shamba. Mama mkwe baada ya maongezi,alisema;

‘Au labda kama mnajijua kuwa hamzai, maana tusije tukawa tunahagaika kuwauliza kumbe wenyewe mnajijua kuwa ni tasa’yalikwua maneno ya mama huyo,ambayo yalimuuma sana mama, akijua kuwa hana tatizoo kama livyo mume wake, lakini alitulia tu,akimuheshimu mkwe wake.

Ndugu walipoona wanandoa hawa wawili hawajali,wakaanza kumnyoshea mama kidole moja kwa moja, kuwa yeye ni tasa hawezi kuzaa,na huenda kamfanyao kitu mume wake ndio maana hasikii ushauri wa wanandugu

‘Kama ni tasa inawahusu nini,mimi na yeye tumekubaliana iwe hivyo,’akasema baba kwa hasira.

‘Hapana ndugu yetu , usiseme hivyo, manpooana mnatarajia nini, kama sio kupata kizazi, ili kizazi hicho kiendeleze kizazi, kwahiyo kama mke wako ni tasa, tunakushauri ndugu yetu ukaoe mke mwingine’wakasema.

‘Mimi nimeshasikia ushauri wenu, kwahiyo tuachieni wenyewe tufikirie, maana huwezi moja kwa moja ukamnyoshea mke wangu mkono kuwa ni tasa, Je kama mimi ndiye mwenye tatizo, mtasemaje?’ akasema baba kwa hasira.

‘Sisi kwenye familia yetu hatuna hilo tatizo, ,tunajua ni mke wako,kwa vile keshakuweka sawa ndio maana hutaki hata kuhangaika, kama huwezi kuifanya hiyo kazi tutahangaika sisi wenyewe maana damu ni nzito kuliko maji, na tutahakikihsa kuwa huyo mke wako anakimbia hapo nyumbani’wakasema wanandugu  lakini baba kwa jinsi alivyokuwa akimpenda mke wake, hakujali akisema kimoyo moyo yeye hatishwi nyau.

Baba kipindi hicho ndio alikuwa kajiingiza kwenye biashara za madini, na katika heka heka za huko, akaumia, na kurudi kijijini, na pesa walizokuwa nazo, wakatumia kwamatiubabau hadi zikaisha, na hali ya babau haikuwa nzuri, na kipindi hicho hicho, ndio baba alishauriana na mke wake kuwa wahangaike kumtafuta huyo mtaalamu, kwani kumbe pia alikuwa mjuzi wa kutibu matatizo mengine.

‘Mke wangu tatizo hili linanipa wasiwasi sana, maana hata vyomvii vya uchunguzi kama x-ray, vinaonyesha sina tatizo, lakini mguu na kiuono, havitaki kuniachia, mbona naingiwa na wasiwasi’akasema baba.

Kwa hilo ikabidi waende kumuona huyo mtaalamu, na katiak kuelezea hilo, wakaambiwana huyo mtalaamu, kuwa tatizo lao, linahusiana na mgando wa damu, na asipoangalia huenda asizae tena, kwahiyo ni nyema ajitahidi angalau apate mtoto mapema.

‘Kwa vipi sasa mtaalamu, maana sisi tunachohitaji ni dawa hayo mengine hatuna umuhimu nayo, sisi hatujali kuwa tuna maadui, kama ni uadui wao waachie wenyewe’wakamwambia.

‘Sawa nendeni mii nitawatafutia dawa, kwanza chukua dawa hii ya kuyeyusha hiyo damu, halfu mkirudi nitawapa dawa ya kizazi, …’wakaambiwa.

Mambo hayo yakafanyika na yaliyofanyika zaidi ni siri yao baba na mama, mimi ninachojua ni kuwa mama akashika uja uzito na nikazaliwa mimi. Na ilikuwa furaha sana kwa familia hiyo, na ulezi wangu ulikuwa wa kinamna, maana ilikuwa kama mgumba kupata mtoto.

Nikalelewa kama yai, nilidekezwa sana, na kila nilichokitaka nilipewa, ilikuwa hata nikigombana na mwenzangu, hata kama mimi ndiye mkosaji, mwenzagu ndiye alionekana ni mbaya, na hali hii ilisababisha wengi kunichukia.

Na kwasababu hiyo, na mimi nikajenga tabia ya kiburi, nikawa hata walimu siwaheshimu sana, kwani nikichapwa naenda kusema nyumbani , na wazazi wangu wanakuja kugombana na walimu. Nikajiona mtoto wa kipekee sana.

Kipindi hicho baba hali ikawa nzuri, kipato chake kikaongezeka, kwani aliamua kufuatilia bisahara ya madini, akawa mmoja wa mawakala wa madini huko Mererani na huko akajenga kukawa kama nyumbani. 
Tukahamia huko na mimi nikawa nasoma shule za huko Mererani,….

Ndio maana hata nilipokuwa mkubwa huko nilikuona kama nyumbani, nilikupenda sana maana ndipo maisha ya raha yalipokuwa, kabla mambo hayabadilika, na hata yalipobadilika mimi niliamua kuwa huko ndipo kutakuwa nyumbani kwangu.

Mambo yalibadilika pale nilipokuwa na umri mkubwa, ghalfa nikaona watu wakiniangalia na kuanza kunong’ona, mpaka nikaingiwa na mashaka, na kujiuliza hawa watu kwanini wananiangalia na kuanza kuteta pembeni, nikajua kabisa walikuwa wakiniteta mimi, nikaamua kufanya udadisi , na ndipo mmoja wa marafiki zangu akaniambai ukweli.

‘Unajua watu wanasema sura yako inafanana sana na yule mganga, mtaalamu wa mambo ya uzazi, kwahiyo wanahisi kuwa huenda ndiye baba yako, maana hamna udugu wowote kwanini mfanane na yeye’akasema huyo rafiki yangu.

‘Mtaalamu gani huyo wa uzazi, mbona mimi simfahamu’nikauliza.

‘Wewe hujui, nimesikia toka kwa wazazi wangu wakisema kuwa baba na mama yako walipoona hawazai walikwenda kwa huyo mtaalamu, na huko huenda huyo mtaalamu aliwachezea ujanja na ndipo ikapatikana mimba yako’akasema huyo rafiki yangu,na kauli hiyo iliniuma sana,ikabidi niende kumuuliza mama.

Mama aliposikia hivyo, kwanza alishituka , na kuniangalia sana kwa makini, na baadaye akasema kwa hamaki;

‘Ninani kakuambia uchafu huo, sitaki hata kusikia kauli hiyo,unasikia, wewe ni mtoto halali wa baba yako, na huko kufanana wanakosema mbona mimi sikuoni, na hata kama mnafanana, binadamu hutokea wakafanana, achana nao’akasema .

Haya hayakuishia hapo kwani wandugu wale wale waliokuwa wakiwasakama baba na mama kuwa hawana watoto, na wanahitajika kwenda kwa mtaalamu, waligeuka  na kuanza kumsakama baba kuwa huenda mke wake katembea na huyo mtaalamu, kwahiyo ambane mama aseme ukweli . Baba mwanzoni hakujali hayo maneno, lakini yalipozidi sana, ikabidi amuulize mke wake.

‘Hivi kweli haya maneno unayaonaje, maana kiukweli, ukimwangalia binti yetu anafanana na huyo mtaalmu, imakuwaje, ina maana  kweli dawa zake zinaweza kusababisha hayo,au kuna mengine yalifanyika mimi siyajui’akasema baba. Na mama kauli hiyo ilimuuma sana , na toka siku hiyo wakawa hawalewani, mama alimwambia mume wake kuwa;

‘Mume wangu hivi na wewe umekubaliana na hayo maneno ya watu, kwani watu hawafanani, mimi sijawahi kufanya uchafu huo, na ningeliufanya saa ngapi na wakati wote tulikuwa tukienda kwake pamoja’akasema mama.

Baba akawa mtu wa mawazo, kwani ndugu, majirani wakawa wakimzonga, na hili likamfanya sasa afikiria kuoa mke mwingine, wazo ambao hakuwa anlo kabla, na  kwa msaada wa andugu zake ndipo akaoa mke mwingine, na mama akawa anasakamwa kuwa ni malaya, eti,kisiri alikuwa akitembea na huyo mtaalamu.

‘Mume wangu nakupenda sana, na tumetoka mbali, najua kwa hali ilivyo, hata kama nitaamua kuvumilia, bado utasakamwa, mimi siogopi kuishi na mke mwanzangu, lakini nashindwa kuishi na ndugu zako, na najua hayo hayataishai hapo, huyo mke mwanzangu nimjuavyo mimi,anaweza kutekwa na maneno ya ndugu zako, na mwisho wa siku tukawa maadui’akasema mama.

‘Mke wangu, mimi nimeamua kuoa mke mwingine ili nione ukweli, ili tuwahakikishie hawa watu kuwa na sisi tunaweza kupata watoto, na hayo wanayozungumza sio kweli, lakini bado ankupenda na nataak tuwe pamoja kwa hili’akasema baba.

‘Wewe unaamua kuoa mke mwingine kwasababu ya kupata watoto, je mimi, sitaki watoto?’ akauliza mama.

‘Kwahiyo ndio maana ukatembea na huyo mtaalamu, ili unionyeshe kuwa unaweza kupata mtoto?’ akasema baba, na kauli hiyo ilimuuma sana mama, akiumbuka kuwa hadi kwenda huko kwa huyo mtaalamu hakupenda, ni shinikizo lao, na hajui kabisa kwanini binti yake, yaani mim nafanana na huyo mtaalamu. 

Alihuzunika sana, na akawa hara raha, akakonda sana, kwani kila siku akawa anasakamwa na wandugu, wakawa wanamuita malaya, na mimi nikawa naitwa majina mbaya,hatukuwa na raha, …mwishowe mama akaamua moja kuondoka.

Baba alikuwa ananipenda kiukweli, …hakutaka kabisa kuniachia , walikubaliana na mama kuwa niwe huru, yaani siku chache nakaa  na baba na siku nyingine kwa mama, lakini kwa baba kulikuwa hakuna amani, nilionekana kama doa ndani ya familia.

Mimi nilipomaliza darasa la saba tu, nikawa mara nyingi naishi na mama, ambaye alikuwa huko Arusha alipoolewa tena na baba mwingine,na huko nikakutana na rafiki yangu mmoja, huyo ndiye alinifundisha mambo mengi. Kipindi hicho baba hali ya kiuchumi ilikuwa mbaya, alikuwa kauza kila kitu huko Arusha na kuhamia kijijini, na hata wakati wanaachana na mama alikuwa yupo kijijini.

Rafiki yangu huyo, alikuwa kama mimi, alikuwa mpenzi sana wa maisha ya Mererani, tukawa tunajadiliana jinsi gai ya kuishi hapo maeneo ya machimbo, na yeye akawa ananifundisha mambo mengi ya kikubwa, na ndipo nikajikuta name nimlowea, nikajua jinsi gani ya kupata pesa….

Kiujumla mimi rafiki yangu, maisha yangu, na ndugu yangu ni pesa, kama huna pesa, wewe na mimi ni paka na panya…..’akasema huku akikunja uso.

‘Mimi sina pesa,mimi ni masikini ,ndio nakwenda kutafuta maisha, ….’Adam akajikuta akisema hivyo.
Yule binti akageuka na kumwangalia Adam usoni kwa muda, akashika kidevu na kujikuna, halafu akasema;

‘Wewe siumeniambia mjomba wako, ni yule tajiri wa madini..au sio?’ akauliza na kutulia na kabla Adam hajajibu huyo binti akasema; ‘Kama ni yule mimi namfahamu sana’akasema huyo binti huku akitikisa kichwa kwa madaha.’ Akatuliwa kwa muda na baadaye akasema kwa ndogo;

‘Huwa anajifanya sana,haingiliki…..sasa, naona ataingilika tu….’akasema huku akiendelea kutikisa kichwa.

‘Kwahiyo unataka kusema nini?’ akauliza Adam.

‘Tatizo lako hutaki kunielewa,lakini utanielewa tu, nikuambie ukweli mimi sijawahi kupenda, na wala sijui kama kuna kupenda, wewe uliwahi kupenda katika maisha yko?' akamuuliza Adam.

'Kiukweli ndio,yupeniliyempenda sana, lakini sijui ypo wapi kwa hivi sasa, na najua huenda yeye kama nilivyoskia,ndiye kanisaidia safari hii iwepo haraka zaidi, kwahiyo huko alipo namshukuru sana, na kama tukikutana....'akatulia na kuinamisha kichwa.

'Hayo mimi sielewi,sijui kwanini mtu upende, hadi kiasi cha kuumia,ili iweje,..hebu niembie kama huna pesa unaweza ukaishi kwa raha, hata kama mnapendana?' akauliza.

'Ndio mbona wazazi watu..'akasema na huyo binti akamkatisha na kusema;

'Labda kuna mapenzi kama hayo, ya kudanganyana, kama hayo ya wazazi wetu,unaishi na mtu huku unaumia kila siku,....labda, huenda wewe ukawa wa kwanza kupendana na mimi,lakini tatizo ni hilo, mimi mpenzi wangu ni pesa, na najua wewe ….labda, kutokana na wewe nitapata pesa..nina uhakika na hilo’akasema yule binti na kuangalia juu huku akionyesha uso wenye tabasamu.

Adam,hakuelewa, akatulia akiwaza, na kutafakari, …..na hapo wakwa wameshanibgia Mererani.


NB: Hiki ni moja ya visa vilivyokusanywa kama Riwaya, ndio maana vinakuwa na wahusika wengi, lengo ni kufikisha ujumbe uliotokana na watu wengi,....na mara nyingi naandika kwa hali ngumu kidogo, muda unakuwa hautishi, sipati muda wa kupitia tena, ndio maana huenda sehemu nyingine nakatiza, lakini mwisho wa siku tutaona ni nini hasa tunatakiwa tukijue kwenye kisa hiki.

 Lengo langu ni kuwa hapa nipatumie kama sehemu ya kukusanya `kazi mbambali' ili baadaye tuweze kutengeneza vitabu, kwenye vitabu ndipo tutaweza kuviweka hivi visa katika hali iliyo bora zaidi.LAKINI ni kazi ngumu, ambo magumu sio mchezo .....tuombeane heri

WAZO LA LEO: Kumpenda mwenzako, rafiki yako,ni pale unapokuwa tayari kumpa,kumasaidia na kutoa kile unachokipenda sana, na upo tayari kukosa kwa ajili yake, hayo ndiyo mapenzi ya kweli, je katika dunia hii yapo?


Ni mimi: emu-three

5 comments :

samira said...

m3 pole na changamoto za maisha lakini usikate tamaa songa mbele tupo pamoja

Anonymous said...

Mungu atakujalia baraka kutokana na juhudi yako hii

Anonymous said...

I was сurious if you eveг considered chаnging the
ѕtructure of your ωebsіtе?
Ιts very well written; I love whаt уouve got tο say.
But maybe you could a little mοre in the waу οf content so people could connect with it bеtter.
Youve got an aωful lot of teхt for only having one or 2 images.

Maybe you could spаcе it out better?
Here is my web site : Tenant Screening Service

EDNA said...

Jirani umesalimika? nimepita tu kuacha zangu salamu.

emu-three said...

Jirani yangu Edna, nimashukuru mungu, hatujambo, kwa ule usemi usemao, KUFA HATUFI LAKINI CHA MOTO TUNAKIONA. Nashukuru kwa kujali ujirani, Ubarikiwe sana.