Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, October 25, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzani-14Sasa turejee kule porini, kama mnakumbuka, yule mwanadada aliyemuokoa Maua, ndio alikuwa akihadithia kisa cha maisha yake, jinsi gani alivyoweza kuingia mikononi mwa hawo watu wa msituni. Na ukumbuke kipindi kirefu kimepita na sasa Maua keshafikia muda wa kujifungua, na anatakiwa kupelekwa karibu na lile bwawa la Mamba, ambapo anatakiwa akijifungua tu, hata damu yake haitakiwi iguse ardhi ya kijiji hicho.

Wao wana imani kuwa damu ya watu waliopotea na wakawa wametenda kosa ni najisi kubwa sana,inaleta mikosi, lakini ikifika mdomoni mwa mamba,mkosi ule hugeuka na kuwa ni baraka. Ndio maana Maua alitakiwa akijifungua tu,yeye atupwe ndani ya huo mto, akaliwe na mamba, ili kuleta baraka badala ya mikosi.

Hili lilikuwa likifuatiliwa kwa karibu sana na wazee wengine ambao ni wapinzani wa babu  wa mume wangu. Hayo yalifanyikwa kwa vile, kuna kugombea madaraka na visasi vya kihsitoria, vilivyokuwepo ndani ya eneo linalojulikana  kuwa eneo takatifu, Eneo hilo liliundwa na wapinzani wa kivita wa siku nyingi. Ilibidi ifanyike hivyo, ili kuweza kukutanisha koo zote na kuwa kitu kimoja, lakini hisia zilizopita zilikuwa bado mioyoni wa miongoni wa wakuu wa koo. …’akasema yule mwanadada wakati anamsimulia Maua.

‘Maua alitulia akivumilia uchungu uliokuwa ukiongezeka kila dakika, aliona ni heri avumilie hata kama ni kujifungulia hapo hapo, na yule mwanadada alikuwa akindelea kuelezea maisha yake.Moyoni mwa Maua aliona kama ingeliwezekana angejifungulia pale pale, lakini haikuwa rahisi hivyo,kwanii huyo mwenyewe anayemuhadithia alishapewa onyo kali,kuwa damu ikimwangika humo ndani, basi na yeye anatakiwa kuwa chakula cha mamba.

Yule mwanadada akatulia kidogo alipomuona Maua akikunja uso kwa maumivu, akamsogelea na kumchunguza, akatikisa kichwa kuashiria kuwa sasa muda unakaribia, na akawa kama anakumbuka jambo,akamwangalia Maua kwa macho ya huruma, lakini hakujua afanyeje, akasema;

‘Itabidi utusamehe tu,kwani kwa hali ilivyo, sijui kama mume wangu anaweza kufanya jambo lolote, kwani hadi sasa hajarudi,ina maana wamemkatalia, au kazuiliwa huko huko, hadi wahakikishe hilo wanalotaka kufanya limekamilika…’akasema.

‘Wewe usijali endelea kunisimulia, nikikusikiliza nasahau machungu, ingawaje hayasahauliki, ….endelea pale ulipoishia ulipoteza fahamu ukiwa umeshajitundika juu ya mti, ilikuwaje baada ya hapo?’akasema Maua akijafanya hasikii maumivu, lakini ….

‘Mimi nilipozindukana tu, nilijikuta nipo sehemu ngeni kabisa, maana ni kama upo kwenye kaburi, na na ndivyo nilivyoanza kuwaza kuwa nimeshazikwa sasa nipo kaburini, na kama kuna watu karibu, hwo ni malaika,  akili ilikuwa siyo yangu, na nilizindukana baaada ya kupiga chafya mara nyingi, na kila nikipiga chafya ndio akili inakuwa kama inazindukana.

Na kabla sijaelewa nini kinachoendelea mara nikahisi mtu yupo karibu yangu, kwanza mwili ulisismuka, nikajaribu kuiweka akili yangu sawa, je nipo hai au ni maiti, nikahisi huyo mtu akinisogelea, alikuwa ni mwanaume,lakini nilikuwa sijaweza kumuona sura yake vizuri akasema;.

‘Mimi ndiye niliyekuokoa ukiwa pale juu ya mti ,na kiiutaratibu natakiwa mimi niwe mume wako..’akasema na kunishika usoni,

‘Kwanini mnifanyie hivi, na utanioaje bila ya rizaa yangu, na hapa nipo wapi?’ akauliza huyo mwanadada.

‘Kuna mawili ya kuchagua ukatupwe kwenye mamba uliwe kama kafara au uolewe na mjukuu wangu, na hili linatakiwa lifanyike haraka sana,kabla ya saa kumi na mbili’ nikasikia sauti nyingine ikitokea humo humo ndani sikuweza kumuona muongeaji.

Na huyo alikuwa akiongea kwa lugha ya kwao iliyochanganyika na lugha ya kwetu. Hawa watu wanaweza kuongea lugha yao na lugha yetu kidogo, na nilikuja kugudua baadaye kuwa huyo alikuwa ni babu yake. Na wakati huo akili yangu ilikuwa haijakaa sawa, pale nilijua kuwa mimi na maiti tu, na kwahiyo mimi sina cha kuamua ni kuacha hawo watu sijui ni malaika au ni wachawi, wafanye wanalolitaka.

‘Ina maana mimi hapa ni maiti?’ nikajiuliza na kabla sijapata jibu, nikahisi mkono ukinigusa usoni. Ulikuwa mkono ulikakamaa,na ulikuwa na manyoya, nikashituka na kuinuka kwa haraka nikiwa naogopa, nikihisi huenda ni mnyama. Na hapo nikakumbuka ya nyuma, kuwa mimi nilikuwa nimejinyonga, na mimi ni maiti na huenda hawa watu ni wachawi, wanaokwenda kwenye makaburi na kufufua watu. Nikiwaza hivyo sijui kwanini.

‘Usiogope …’sauti ikasema na maneno mengine ambayo sikuweza kuyaelewa maana yake . Nikatulia na kusema kimoyo moyo, toka lini maiti ikaogopa, nikageuza kichwa na kumwangalia huyo mtu au mnyama, nilikuta ni sura ya mtu, mwanaume.

‘Nilikuona ukiwa umening’inia juu ya mti na kamba ikiwa imekukaba, ikiwa na maana kuwa ulikuwa umejinyonga au kunyongwa, sasa….’sauti ikasema na kufuatiwa na maneno mengine nisiyoyafahamu vyema, ilikuwa lugha ya hawa watu ambayo nilikuja kujifunza baadaye, kumbe alikuwa akiniambia kuwa yeye wakati anapita kutoka mawindoni, aliniona nikiwa nimening’inia kama mfu,  akapanda haraka juu ya mti na kukata ile kamba.

Aliniambia kuwa, alishajua kuwa nimeshakufa,kwahiyo nia na lengo lao ni kunichukua mimi nikawe chakula cha mamba. Wao wana imani yao kuwa wakiona mtu wa aina zetu na kumpeleka kwa hawo mamba akamtoa kuwa chakula cha mamba inakuwa kafara na akiomba shida yake, anafanikiwa. Na yeye kwa muda hup alikuwa na shida sana, alikuwa hana mbele wala nyuma.

Akaniambai kwamba, alinichukua akanibeba,na kuanza kukimba naye hadi huko msituni, na waakti anafanya hivyo, alikuwa akiogopa wenzake wasimuona, kwani wakmuona itatokea vita tena ya kumgombea, kwani kila mmoja alikuwa katika mpango wa kuwinda watu wa namna hiyo, ili wafanikiwe, ndio imani zao.

Anasema lakini hata hivyo, ili afanikiwe ni lazima akutane na mmoja wa wazee wao, anayeheshimika yeye atafanya mambo yao, na matambiko yao, ili hata mwili wangu ukikabidhiwa kwa hawo mamba maombi yafanye kazi vizuri, na ili afike huko lazima atakutana na walinzi watiifu wa hawo wazee.

Kwahiyo alichofanya kwanza ni kuufikisha mwili wangu kwenye pango lake, humo, akanivikwa nguo za ngozi,ili kunificha, halafu ndio akanibeba, kwahiyo njiani walijua kwua kambeba mgonjwa au mtu wake, na kweli kila aliyekutana naye, alimwambia kuwa huyo ni mgonjwa anampeleka kwa tibabu wao, na walipotaka kumsaidia alikataa.

Basi akafika huko kwenye eneo ambalo wao wanaliita eneo takatifu, ni eneo wanapoishi wazee na wakuu wa jadi. Na kwa vile yeye mwenyewe ni ukoo wa wakuu wa jadi, haikuwa vigumu kwake, aliweza kuingia hadi sehemu inayostahili, akauweka mwili wangu, na kumtafuta mtu wake ambaye nib au yake, mmoja wa watu mashuhuri humo.

‘Babu nimekuja, nimekuja kwa jambo muhimu sana, kama unajua hali zetu kwa sasa ni ngumu, na inavyojulikana tunatakiwa tutafute damu ya kuwapa mizimu yetu na damu nzuri ni ile ya hawa watu wa waliopotea,’akasema.

‘Kwahiyo umeshampata ?’ babu akamuuliza.

‘Ndio nimempata..’akasema.

‘yupo wapi, ni mwanamke au ni mwanaume?’ akaulizwa

‘Ni mwanamke’akasema na babu yake akahema,kwa muda, akazungumza maneno yao ya maombi, halafu wakaongozana hadi pale alipokuwa kaniacha, lakini alipofika pale hakunikuta. Ikabidi ashituke na kuanz akutafuta huku na kule.

‘Niliuacha mwili wake hapa, kuna mtu kauchukua’akasema na msakao ukaanza , na sikuweza kuonekaan kwa haraka, ndipo babu akaitisha kikao cha haraka cha wazee humo ndani, na babu alikuwa mmoja wa wakuu, anayeheshimika, wakuu mle wakakutana na kuanza kusikiliza hilo tatizo.

‘Jamani mnajua hapa ni sehemu takatifu, na tendo lililofanyka hapa ni tendoo ambalo halistahili sehemu kama hii, kwanza kabla ya yote naomba yule ambaye aliuchukua mwili wa kafara ulioletwa na mjukuu wangu ajitokeze kabla hatua nyingine hazijachukuliwa.’ Babu akasema na watu pale walikuwa wakimuogopa sana.
Mara akatokea mmoja wa wazee wa pale, ni mkuu na yeye, akakohoa na kusema kwa sauti ya kutisha,;

‘Una uhakika na hilo unalotaka kulisema; kuwa mwili wa kafara uliletwa hapa, huoni kuwa unakwenda kinyume na maadili yetu, kuwa ili mwili utambullikane kama ni mwili wa kafara kwanza huyo mtu anatakiwa kweli alistahili kuadhibiwa, na pili kama keshakufa, uchunguzi ufanyike ijulikane kafa kwa kitu gani,na kabla ya kufa alikuwa na makosa, yanayostahili kuadhibiwa...na hili linatakiwa lipitie kwenye utaratubu wa mila na desturi zetu?’ akasema huyo mzee.

‘Kwanini nisiwe nauhakika wakati mjuu wangu ndiye aliyeuokota huko nyikani, na aliukuta ukiwa umejitundika, ina maana kuwa huyo mtu aliuliwa kwa makosa,au aliamua kujiua mwenyewe na hilo ni kosa,kwahiyo anastahili kuliwa na mamba wetu’akasema babu.

‘Naona mzee mwenzangu unaanza kukiuka mamb muhimu ya hapa , hii ni sehemu takatifu, na tunatakiwa tuihehimu, na ili mtu wa namna hiyo, akubalike kuwa anafaa kwa kafara ilihitajika tukutane,na tupitishe hukumu kwa pamoja je hilo lilifanyika?’ akauliza huyo mzee.

‘Hili lingelifanyika, nilitarajia baada ya kuuona huo mwili, niwaite tukutane, na nilipofika sehemu aulipowekwa huo mwili tukakuta haupo, je huoo mwili upo kwako?’ akauliza huyo mzee.

‘Kwanza tumalize moja, ukubali kuwa umekosea,’akasema huyo mzee ambaya mara nyingi amekuwa mpinzani wa babu wa mume wake,na wamekuwa wakishindania madaraka, na hata ilifikia hatua waliingia kwenye mapigano, kati ya familia hizo mbili.

‘Siweze kukubali makosa ambayo sijayafanya’akasema babu, kwani kama angekubali, ingebidi ashushwe daraja, kutoka kwa wazee wa juu hadi chini, ambapo asingeliruhusiwa kuingia kwenye uongozi au kushiriki kwenye maamuzi ya kimahakama.

‘Basi mimi naomba tuitishe baraza la wazee tuhukumu hili, maana tukiliachia likiendelea kuwepo heshima ya mahali hapa itaharibika’akasema huyo mzee mwenzake na hata kabla hajajibiwa akatoka ikiwa na maana anakwenda kuwaita wazee wa mahakama.

Shauri likapitishwa kuwa kikao hicho kifanyike,a usiku, sasa ukumbuke mimi natambulikana kuwa ni maiti, je maiti ingeliweza kukaa siku tatu, maana hiyo ilikuwa siku ya tatu , tangu nichukuliwe kule nilipokuwa nimejitundika. Wao wana dawa za kuufanya mwili usioze, lakini mwili ukikaa zaidi ya siku tatuu haifai tena kwa tambiko.

‘Babu akajaribu kuwaona wazee wenzake kulielezea hilo, lakini ilishindikana kwana kauli ya huyo mzee wao inahehimika , kwa vile ana wafuasi ambao wapo nyuma yake na ambao ni nusu ya wajumbe, kwani kwa muda ule alishatafuta wazee wa namna hiyo waliomunga mkono, na wakizidi nusu basi ombi lake linakuwa na nguvu.

‘Mjukuu wangu naona hilo limeshindikana, na iliyobakia hapa ni jinsi gani ya kujilinda ili nisije nikashushwa daraja, na pia kuhakikisha hawa watu watoi adhabu kubwa ambayo huenda ikaleta majonzi kwenye familia yetu.’akasema Babu.

‘Babu nisamehe,sikujua kuwa ninaweza kukuingiza kwenye matatizo kama haya ..’akasema mume wangu

‘Ndio maisha mjukuu wangu, katika maisha mambo kama haya hutokea, cha muhimu ni kujipa moyo na kutafuta njia ya kukabiliana nayo’akasema Babu.

‘Sasa tutafanyaje?’ akauliza mjuu wake.

‘Hapa  kwanza niachie muda nifikiri, na nitalifanyia kazi hili jambo,  kwani ni lazima nifanye uchunguzi nijue ni nini kilitokea, na kama kuna jambo tulijue tutafanyaje,maana mwenzangu asingelifanya haya yote kama hana ushahidi na anajua kuwa hata nikifanay nini sitaweza kumshinda, kwanza inabidi nitoke, kidogo’. Ikabidi Babu atoke humo asafiri sehemu ya mbali kwa haraka.

‘Huko alipokwenda ni kijiji ambacho sheria nyingi za mila zao ndipo zilipoasisiwa, wao walihamia hapo baadaye ili kutafuta maisha lakini sheria zao nyingi zinatoka huko walipozaliwa mababu wa mababu zao. Huko alitakiwa kukutana na wazee wa jadi , na pia kuna wataalamu ambao huangalia matukio kwa mbali zaidi. Babu aliwaendea hawo akijua ndio kimbilio lake, ….

Babu alipofika huko kwa hawo wataalamu ndio wakamuelezea ilivyokuwa, kuwa huyo binti hana hatia, ni binti aliyenusurika na uzalilishaji , na hata kuzaliwa kwake ni mizimu yao iliyobariki, na ilijulikana kuwa ipo siku atarudi hapo, halafu aolewe... Na wenzake walishajua kuwa huyu anaweza kuwa mmoja wa warithi wa mama wa ukoo, na ndio maana na hastahili kutupwa kwa mamba, na wenzake wanalijua hilo...’

‘Kwa vipi aolewe maana sisi tujuavyo ni  maiti’akauliza babu.

‘Huyo binti hajafa, kapoteza fahamu tu, lakini kama ikifika saa kumi na mbili anaweza asizindukane kabisa, kitakachomuokoa ni dawa nitakazokupa wewe, hata wao hawajajua kuwa huyo binti anaweza kuzindukana kutokana na dawa maalumu, wangelijua wangeshafikia mbali kufanya mamboo yao….’akasema huyo mtaalamu.

‘Sasa cha muhumi hapa ni muda, kwanza chukua hizi dawa nenda kamnusishe puani, na akizindukana mfungisheni ndoa haraka, …’akaambiwa na babu akaingiwa na hamasa, kwani aliwahi kuota ndoto inayomuelekeza kuwa amtafutie huyo mjukuu wake mke, mke ambaye anaweza kusaidia familia yao kuwa watawala wa hilo kabila lao.

‘Lakini hilo linatakiwa lifanyike kabla ya saa kumi na mbili jioni , kwani  ikifikia hapo huyo binti hataweza kuzindukana tena, atakuwa keshakata roho, ..nyie cha kufanya ni kuhakikisha ndoa inafanyika,na baada ya ndoa inatakiwa kweli tendo la mke na mume liwe limeshafanyika, ili kuhalalisha na kuondoa kosa hilo ambalo mpinzani wako anataka kukushika nalo’ akapewa hayo masharti.

‘Lakini kwanini ,ina maana hawajui kuwa yupo hai, na kama wanajua hilo kwanini wanafanya hivyo makusidi ili huyo binti asizinduakne tena?’ akasema babu.

‘Hilo sio muhimu kwa sasa,….huenda bado hawajalifahamu hilo, kwasababu huu utaalamu tunazidiana, nyie fanyeni kwa upande wenu, ili mjiokoe, haraka, na mumuokoe huyo binti’, wa kusema lolote,..’akasema huyo mtaalamu.

‘Wenzenu hilo wamejpanga vyema,na mkifanya kosa, hamtakuwepo humo tena na mbaya zaidi yatawaandama, fanyeni muwezavyo, na swala la muhimu hapo ni muda.....’akasema huyo mtaalamu.
Babu aliondoka hapo akiwa na mawazo mengi, hakujua kuwa mwenzake kumbe muda wote huo, alikuwa abdo anamtafuta, yeye alijua kuwa wameshapatanishwa na uadui haupo tena, lakini kumbe wenzake wanahamu ya kuwaondoa humo kwenye uongozi na ikibidi waangamizwe yeye na ukoo wake.

 ‘Kwa jinsi ilivyo, na kwa vile ukoo wa huyu jamaa ni mkubwa na una wajumbe wengi, najua watampigia kura yeye ili aonekane ni mkweli’. Babu akachanganyikiwa maana huyo ni mjuu wake toka kwa binti yake kipenzi. Muda ulikuwa umekwenda kweli,na ilibidi arudi huko mapema, ili kumuokoa huyo binti, kabla hajafanyiwa lolote…

Babu alipofika tu, akamchukua mjukuu wake na kumsomesha, nini kinatakiwa kifanyike, kwa haraka, akawatafuta vijana wengine wawili wanaomtii  wa ukoo wao, na wakaanza kuutafuta mwili wangu ulipo, maana hadi muda huo nilikuwa kama maiti tu.

Walikuja kugundua kuwa nipo sehemu anayokaa huyo mshindani wake, ambapo ili uingie hapo nilipo  inabidi ukutane na huyo mshindani wake. Na yeye alijitahidi muda wote kuwepo hapo, na kama hayupo wanakuwepo walinzi wake watiifu.

NB    BLOG YENU INAWATAKIA IDD-EL HAJ NJEMA, 

Ni mimi: emu-three

4 comments :

Anonymous said...

A very impressive article. Well prepared. Very motivating!! Set off on to way

Yasinta Ngonyani said...

Kisa kinasisimua na kuogopesha....utamu unakolea. Nami nachukua nafasi na kuwatakieni wote IDD-EL HAJ NJEMA.

Anonymous said...

Vancouver led lighting store has over a hundred different kinds of products. Our LED lighting products mainly come from the factories in Taiwan, which could offer a cheaper price and good quality. Also, we can create any word or graphic in commercial LED lighting for our client and we will charge for a cheaper price than other companies. Please ask fo our employee for detail. http://www.vancouverledlighting.com/

Anonymous said...

bear grylls messer
Also see my page - bear grylls messer