Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, September 3, 2012

Mbio za sakafuni,huishia ukingoni-Sehemu ya pili-1

     

Mara nyingi baada ya vikao vya chama huwa tunaingia mitaani, huko tunatafuta hoteli nyingine , tofauti na ile tuliyofikia, na mara nyingi yanayofanyoka huko, ni siri yetu na hawo wenye hizo hoteli. Kila mtu huwa ana hoteli yake, ambayo anaiamini. Hayo yote nilijifunza toka kwa wenyeji wa vikao kama hivyo.

‘Unajua kazi hizi za kisiasa zinahitaji kutulizwa, ….maana kujibizana kwenye vikao, kimuhemuhe cha kutokujua nini kitatokea, yote hayo yanaweza yakakupandisha shinikizo la damu, kwahiyo ili kuyakwepa hayo, tunahitaji viburudisho vya zaida..’akaniambia mzee mmoja.

‘Mbona tumeshakunywa na kula, kuna viburudisho gani zaidi?’ nikauliza.

‘Wewe, pale umekunywa kukiwa hakuna vinurudisho vya macho,….unajau mungu katujaliwa mapambo ya dunia, ukiyaangalia mweneywe nafasi inarizika,…hata unywe vipi, hata ule vipi, hata uwe tajiri kiasi gani, hata upate raha kiasi gani, hujakamilisha marizio ya nafsi yako, kama hujaona hakuna pambo la dunia, pambo la nafsi….’akasema huyo rafiki yangu.

‘Wewe tatiz la ni mshahiri, au muimba taarabu, pambo gani hilo, usiniambia kuwa….unanyumba ndogo’nikamwambia nikiwa siamini kuwa mzee kama huyu anaweza kuwa na haizo tabia.

‘Iiite nyumba ndogo, au vyovyote vile , lakini mimi naita pambo la moyo, ….ukinywa, ukila, huku yupo mbele yako, au pembeni yako anakupepea, unasahau dunia yote ya dunia,…unasahau machungu ya vikao, unasahau malumbano yasiyo na mpangilia kweney vikao, …ukitoka hapo akili imetulia’akasema.

‘Mmmh, ina maana hata wewe unafanya mambo hayo, huoni kuwa unahini ndoa yako, na ukijulikana na wajumbe wa kikao si ndio utaharibu jina lako…’nikasema kwa wasiwasi.

‘Kilammoja anajau hilo, hakuna wa kumdanaganya mwenzako, mimi namjua kila mmoja na mtu wake, hizo ni siri zetu, kinachotakiwa usiweke hadharani, ufanya kwa siri, na, ukifika huko utawakuta kila mmoja kajificha kwenye sehemu yake, hakuna anaymfiuatilia mwenzake,…’akaniambi.

‘Jamani hayo sasa mapya kwangu na sijui kama mimi naweza kuyafanya, mimi naheshimu ndoa yangu, na namuogopa sana mungu, maana lolote utakalolifanya kwa siri, ujue mungu yupo..anakuona’nikasema.

‘Sikiliza kijana, wewe si unataka kushinda siasa, wewe uliniomba kuwa nikufunde kuhusus mambo ya siasa, …’akasema.

‘Lakini hayo sio mambo ya kisiasa, huo ni …u…u’nikashindwa kutamka hilo nililolitaka kulisema.

‘Unataka kusema kuwa huo ni uchafu, ni uchafu gani unafanya, wakati ni sehemu ya kutoa kile ulichojaliwa, na unakula na mwenzako ambaye anakihitaji. Huo ni utu mwema, ubinadamu, …kwanini tule peke yetu, wakati wenzetu wapo na wao wanahitaji, ….na wanahitaji sana ni hawa akina dada zetu, mapambo ya dunia..’akasema akiangalia juu kama vila anaona raha fulani.’

‘Mimi hayo siwezi…’nikasema lakini yule mzee alinishika mkono, name nikamfuata kama vile mtoto anayemfuata baba yake, hadi kwenye hoteli moja iliyokuwa kando ya mji, huko akaongea na mwenye hoteli, tukapewa ufunguo, na kwenda chumba cha maalumu.

Huko hatukukaa muda, mara wakaingia mabinti wawili,……

**********

`Mume wangu nampenda sana, na ukizingatiwa jinsi alivyonipata kwa shida, nilijua kabisa na yeye ananipenda na hakuna atakayeweza kumhadaa, na sikuwazia hata siku moja kuwa atakuja kunisaliti, ….’akasema mke wa Kiongozi.

Mke wa kiongozi aliletwa hapo hospitalini akiwa hajitambui, baada ya kupata mshituko, uliosababisha shinikizo la damu.

‘Vipi imekuwaje tena, wakati uliniambia kuwa ulishapata dawa ambayo imeondoa hilo tatizo?’ mke wangu akamuuliza mgonjwa.

‘Hata mimi nilijua kuwa hilo tatizo limekwisha, na ukizingatia kuwa nilishajiweka katika hali ya kurizika na mimi nikawa najichanganya katika maisha ambayo sikujua kama na mimi nitaweza kuwa nayo, maisha ambayo hakuna angeliweza kuamini kuwa na mimi nilikuwa nimejihusisha nayo.

‘Maisha gani tena hayo, ambayo ulijihusisha nayo, na sisi sote tunakujua kuwa ni mke mwema,….?’ Akamuuliza mke wangu.

‘Haya maisha ya ndoa yasikie tu, usiwaone watu wapo mitaani, au wanapita njiani wakiwa wameshikana mikono ukawazia kuwa huenda hawana matatizo yoyote,…..kama sio hili ni lile. …’akasema ankutulia.

‘Kwahiyo na wewe ulishindwa kuvumilia hayo matatizo ndio shinikizo la damu likakuathiri tena?’ akaulizwa.

‘Wewe ni rafiki yangu, na nimekuwa karibu sana na wewe, na nilijaribu sana kukuficha mengi ya mimi na mume wangu, kwa vile najua ni wajibu wangu kama mke kufanya hivyo, lakini haya yaliyonifika yanahitaji mtu wa karibu wa kunishauri, maana sasa nipo njia panda,…..’akasema akionyesha uso wa kutahayari.

‘Sawa rafiki yangu, najua kweli umefikwa, na nitajitahidi kukushauri vile niwezavyo, maana mimi mara nyingi najua wewe ndiye wa kutushauri sisi kwa jinsi ulivyo, kila mtu anapenda tabia zako’akamwambia mke wangu.

‘Hapo ndipo tunakosea, maana sio kila mtu anakijua, kila mtu ana uazaifu wake,mimi ninaju hiki na kujitahidi kila niwezavyo, lakini kune mengine yanashindikana ambayo yule ambaye unayemuona hafai naweza akakupa ushauri wa maana zaidi, lakini inatakiwa kuangalia ni nani wa kuomba kwake ushauri, hili nimejifunza, na limekuwa fundisho kwangu…’akatulia na kujinyosha pale kitandani.

‘Kwani ni nini hasa kikubwa, ….hebu niambie tuone tutafanya nini?’ akasema mke wangu.

‘Tatizo huenda limeanzia mbali,….lakini mimi nimeinizwa tu kama chambo bila kujua, na ndio maana naogopa hata kumwaminimtu tena, maana yuleunayemuona ni rafiki , anaweza akawa adui mkubwa, bila hata yaw ewe kujua, maana hujui undani wake…’akainuka na kukaa, na kweli alionyesha kuchoka.

‘Matatizo yangu yalianza pale nilipoamua kujichanganya, na hili tulikubaliana na mume wangu kuwa ili tuweze kuweka misha yangu vyema ni bora na mimi nijishughulishe, na ili tufanikiwe, nahitaji kusoma kidogo kuhusu mambo ya biashara , tukakubaliana na nikaingia shule, …..’akaanza kuongea .

Huko shuleni, ni lazima uwe na marafiki ambao watakusaidia masomo, maana kichwa kilishaanza kushika mambo ya kidunia, sikujau kuwa nitaingia darasani tena, na ndiponikakutana na yule aliyenisaidia siku ile ya ndoa…’akajaribu kutabasamu.

‘Ina maana yale yaliyotokea siku ile ya ndoa ulikuwa ukiyajua,..?’ nikamuuliza.

‘Kiukweli nilikuwa siyajui, nilikuja kuyajua baadaye,…muda mchache tu pale alipokuja mama mmoja kwenye chumba nilichokuwa nimefungiwa, na huyo mama ndiye aliyenitoa kile kitambaa machoni, na mdomoni, maana nilifungwa machine na mdomi, na akanifungua zile kamba zilizokuwa nimefungiwa miguuni.

‘Kwa muda ule sikujua ni nani, maana alivyokuwa kavaa, ilikuwa sio rahisi kumgundua, alikuwa kajifunga mtandio shingoni, kama tai,  kavaa nywele za bandia ndefu, na machoni kavaa mawani mikubwa meusi, na akawa akijitahidi kuongea kwa sauti ya kuigiza ya mzungu anayejifunza Kiswahili….’akatulia.

Tofauti na alivyokuja mwanzoni,maana mwanzoni alikuwa mkali, akiongea kwa vitisho, lakini leo japokuwa alikuwa akiongea kwa laafudhi ile ile, lakini alikuwa akiongea kwa upole, na alionyesha kunijali,….akanisogelea na kusema;

‘Jamaa kaingia mkenge, hutaamini kuwa hakujua mpaka allipofunga ndoa, na wakati alipotaka kumfunua yule binti, shangazi yake akacheza mchezo , maana hakuwa na jinsi, japokuwa mwanzoni alinipinga sana, ….’akasema huyo mama sikujua ana maana gani.

‘Kwahiyo mpaka wanaondoka hapo, hakujua kuwa kaoa mke kanyaboya?’ akauliza yule mlinzi akicheka kwa kebehi.

‘Mpaka wanaondoka, …na nasikia hadi wanafika nyumbani kwao ,ambapo kulikuwa nasherehe kubwa, alikuwa hajajua hilo, na kivumbi ilikuwa wakati wapo ndani…’akasema yule mama huku akicheka.

‘Lete uhondo ilikuwaje?’

Walipofika ndani, ilikuwa ni utambuslisho kwanza kabala hawajaingi kwenye ukumbi maalumu uliaandaliwa, bwana akawa kasimama akiongea na wazazi wake, na yule binti, alikuwa kasimama na wapambe wake….muda huo bado kava lile gauni kubwa, na alikuwa bado kajifuka gubi gubi…‘

‘Aliyechokoza mambo ni shangazi wa bwana harusi, yeye akaenda na kushika bibi harusi wakaingi wote chumbani, …..na bwana harusi akafuta kwa nyuma, alisubiri kidogo kablsa ahjaingia ndani, akijua labda bibi harusi anaandaliwa , kichwani akijenga picha nyingi za kushinda na kumpata binti mrembo, mara shangazi yake akatoka haraka huku uso ukiwa umebadilika.

Bwana harusi hakujali hilo, yeye akaingi ndani taratibu,,….na kutupa macho pale kwenye sofa lililokuwa limewekwa hapo chumbani,…akapikicha macho,…ya kutokuamini, akangalai huku nakule, akimtafuta mrembo wake,…

‘Karibu mume wangu, nipo hapa, hakuna mwingine zaidi yangu…’akasema yule mwanamke kwa uso uliojaa furaha, na kebehi.

‘Wewe umeingiaje humu ndani, na mke wangu yupo wapi?’ akauliza kwa hasira, huku akingalai huku na kule.

‘Mke wako yupo wapi tena, mbona unanishangaza, mimi ndiye mke wako halali,…’akasema akimuonyesha ile pete aliyomvalisha pale wakati wanafunga ndoa.

‘Kumbe ndio maana hukutana nikiangalie wakati nilipotaka kukuangalia, wakati tunafunga ndoa, ningelijua ningelikufurumua pale mbele ya watu…na leo nitahakikisha unatoka hapa ukiwa ….’akasema na kumfuata akitaka kumpiga. 

Wakati anamsogelea huku akijuta kwanini hakuweza kumfungua pale na kumwangalia, alikumbuka kichwani, jinsi ilivyokuwa, akakumbuka pale kwenye ndoa, alipojaribu kumfunua,ili amuangalie usoni, lakini binti yule alikataa, …Yeye mwenyewe kwa kujiamini, kwani alijua kuwa ni yule binti mrembo, anaona aibu, na kwa vile ndoa imekuwa kama ya kualzimishwa, akasema haina haja , ilimradi ndoa inafungwa, wataonana mbele kwa mbele.

Ndoa ikafungwa, na vigelegele vikatanda hewani, huku shangazi wa bibi harusi akiwa haamini kuwa mpango umewezekana, na hadi wanaondoka pale alikuwa hajaamini, …..

‘Ina maana huyo shangazi wa bibi harusi alikuwa akiyajua hayo?’ akaulizwa.

‘Nilimweleza huo mpango saa chache tu, kabla hawajafika hawo waowaji, alipinga vikali, lakini nikamwambi akubali asikubali hilo litafanyika,…hakuwa na jinsi, hata hivyo ,hata yeye alikuwa kaipnga vikali hiyo ndoa, isifanyike, lakini waume waliikomalia,…si wameshakula hela za watu…’akasema huyu mama.

‘Basi mambo yaliyofuata hapo ilikuwa kivumbi na jasho, kutupiana maneno ya jaziba, na baaadaye yule mkewe,..maana ni mkewe tena, akasema;

‘Wewe….tulia kwanza, usiharibu siku yetu muhimu..nikuulize hivi wewe kila siku nilipokuwa nikikuuliza kuwa kweli unanipenda, ulikuwa ukinijibu nini….?’ Akauliza yule binti akiwa keshatulia, na alijau jinsi gani ya kumuingia huyo jamaa, na wakati huo yupo tayari kwa lolote.

‘Yale yalikuwa ni mapenzi ya kudanganyana tu, sikuwa na mpengo na wewe…..’akasema huyu jamaa akiwa kakakasirika, na alishatayarisha ngumi, lakini mkono ukawa mnzito.

 ‘Hivi wewe ulitarajia nini kwangu, kuwa uuchezee mwili wangu tuuu…eehe, na mwisho wa siku uende kuoa mke mwingine’ akasema huyu binti akiwa kashika kiuno, hakuogopa, na alikuwa tayari kupambana.

‘Hatukuwa na makubaliano hayo, wewe ulichohitajia ni pesa zangu, na ulizipata , na mkataba wetu ukaisha, mambo ya ndoa yalikuwa sio makubaliano yetu, mimi na wewe’akasema huyu jamaa akiwa kawaka, na ile suti aliiona inambana.

‘Hiyo haipo, ulisema mwenyewe kuwa mambo yako yakiwa sawa tutafunga ndoa, unabisha hukusema hivyo,….sasa mimi ni mkeo halali, …naona mambo yako yameshakamilika, ndio maana ukatayarisha hiyo harusi ….na tukafunga ndoa, …ugomvi upo wapi,…ukumbuke pale,  ulikubali mbele ya mashahidi kuwa upo tayari kuwa na mimi….kwa raha na shida…kama ulivyotamka siku ile tulipofunga uchumba mimi na wewe…umesahau…’akasema yule binti akimsogelea kutaka kumkumbatia na yule jamaa akamsukuma.

‘Mimi hiyo sikubali, utaondoka hapa nyumbani sasa hivi…’alisema yule mwanaume na kumshika huyo binti mkono, huku akimvutia  nje,na watu waliposikia vurumai huki ndani, mmoja aikabidi agonge mlango kuuliza kuna nini, na kablahajagonga vyema mlango ukafunguka na jamaa akaonekana akivutana na huyo binti, na shangazi mtu ambaye alishawaita wazazi wa bwana harusi akaingia ndani na kuanza kuwasuluhisha.

‘Jamani msijaze watu, tulieni, wazee wamekuja tutafute suluhisho…mkileta vurugu, mtaumbuka wenyewe…’akasema shangazi.
‘Na kweli ataumbuka….mimi ni mkewe halali…’akasema yule binti.
Baadaye wazee walikutana akiwemo bwana ba bibi harusi, wakaanza kuhojiwa, na binti akajieleza;

‘Huyu bwana simuelewi, kakubali mwenyewe kufungandoa na mimi, tangu siku nyingi, na mbele ya wakuu, alikubali kuwa yupo tayari kufunga ndoa na mimi..’akasema yule binti.

‘Mimi sikujua nii wewe….’akajitetea huyu bwana harusi, akanyamazishwa. Na hata muda wake wa kujitetea ulipofika, alijikuta akiwa hawezi hata kuongea, kwa hasira na kutahayari.

‘Baadaye wazee wakatumia busara zao, maana binti alihojiwa na kuanza kujieleza vyema, kwanini kafanya vile, na ili kuthibitisha kuwa yeye ndiye aliyekuwa mchumba wake halali, kabla hajamtelekeza, akatoa vielelezo vingi vya picha kuonyesha kuwa yeye ndiye aliyestahili kuolewa na huyo jamaa, na jamaa alipoulizwa je, huyu aliwahi kuwa mchumba wake, akasema ndio, lakini hakuwa tayari kumuoa, kwani alishapata anayependa.

‘Hatukuelewi,kama mlifika hadi kupeana uchumba, ulitarajia nini..hebu jiweke wewe kweney nafasi yake, hebu jiulize wangapi waliokuwa wakimtaka, wakawa hawana nafasi hiyo tena, kwasababu ulishamvalisha pete ya uchumba, halafu baadaye unamtelekeza…hapo hujatuambai kitu, huyu sasa ni mkeo halali….’akasema mama mmoja.

‘Huyu ndiye bahati yako, haina haja ya vuruga, …’akasema mama yake mzazi, na wengi wakakubaliana na hilo, na jamaa alipoona hana wa kumtetea akaondoka hapo nyumbani, na kwenda kusipojulikana, haijulikanai kuwa atakubaliana na hiyo ndoa, au atafanyaje...lakini tumjuavyo, aatkuwa kwwney baa anakunywa …..’akamalizia yule mama.

‘Hakwenda polisi kuwafahamisha kuwa mchumba wake katekwa nyara?’ akaulizwa yule mama.

‘Hawezi kwenda polisi yule, anajua akifnay hivyo ataumbuka zaidi…’akasema huyu mama na baadaye akamgeukia huyo binti na kusema;

‘Usihofu binti, upo salama, ninachotaka ni wewe usiolewe na huyo muhuni, …kuolewa na yeye ni kama kumtupia mwewe kifaranga cha kuku, ….yule namjua vyema, naijua hadi familia yao, naona ajabu baba yako kukubali uolewe na huyo mtu wakati anawajua fika, lakini najua sio yeye, ila ni sababu ya mkewe,….’akasema yule mama.

‘Kwani wewe ni nani, na kwanini uwe na uchungu na mimi?’ huyo binti akamuuliza.

‘Hayo utayajua baadaye, ila nimekuja kukutoa wasiwasi, ili ujue kuwa haya hayakufanyika kwa nia mbaya, na mengine, ni mambo ya kupoteza muda, ili ijulikane kuwa tumekuteka nyara kwasababu ya kupata pesa, lakini sivyo hivyo kabisa…’akasema huyo mama.

‘Mbona mimi siwaelewi….’nikasema.

‘Utaelewa tu, ninachokuomba ni wewe kutulia, ndio maana nimekufungua kila kitu, ili uwe huru, ila nakuomba usifanya jambo jingine lolote kama la kutoroka, mwenyewe utakuja kufurahi kuwa kweli nimekuokoa kwa kutaka kupelekwa kusikokufaa kwa tamaa za watu. Najua ni jukumu langu kukufanyia hivyo….’akasema yule mama, na baadaye akawageukia wale mabaunsa na kuwaambia.

‘Sitaki mumusumbue huyu binti kuanzia sasa, maana lile zoezi la awali limeshakamilika, hakikisheni mnampa kila anachokihitaji, cha muhimu, ni usalama wake, mengine nitakuja mwenyewe kuongea naye,…’akasema huyo mama na kuondoka.

Siku ile nzima sikumuona huyo mama, na niliweza kutembea humo ndani  kwenye hiyo nyumba, niliyokuwa 
nimeshikiliwa, sikuruhusiwa kutoka nje, niliweza kuingia chumba kimoja baada ya kingine, maana ilikuwa ni nyumba kubwa, lakini sikuruhusiwa kabisa kutoka nje,….hata ilipofika usiku.

Ilipofika usiku nilibakia kuangalia runinga, na baadaye usingizi uliponijia nikalala , na kesho yake, asubuhi nikiwa nimechoka na yale maisha, nikaanza kulalamika. Na nilipoona hawanijali, nikaamua  kulazimisha kutoka nje,na yule askari akanizuia, nikamwambia kwa hasira;

‘Mimi nataka kutoka nje, mbona mnanifanyia hivyo jamani, kwani mimi ni mfungwa hapa?’ nikauliza huku nikijisi kizunguzungu, maana muda mwingi niliokuwa hapo nilikuwa sijisikii kula,kwahiyo mwili ulikuwa hauna nguvu.

‘Wewe subiri kidogo, utaongea na mama,anakuja sasa hivi …’akasema huyo mlinzi ambaye
Na kweli haikupita muda, mara mlango ukafunguliwa, na wakati huo nilikuwa nimeinama chini, nikijizuia kulia, na nilipoinua kichwa na kuangalia kule mlangoni, ili nimuone huyo aliyeingia, nilibakia nimeduwaa, nikatoa macho ya kutoamini, na kabla sijasema neno, nikahisi giza likitanda usoni, ….

NB : Hii ni sehemu ya pili ya kisa chetu, maelezo ya mke wa jamaa, tuzidi kuwepo

WAZO LA LEO: Alipangalo mungu kuwa liwe,huwa...


Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

Hivi niulize kweli mtu unaweza ukaoa na mkafunga ndoa, bila kwanza ya kuiona sura ya unayemuoa!

Maana pale ukishafunga ndoa, unaambia umfunue umwangalia,lkn hapa kweli, mbona unamfunua baada ya kufunga ndoa, au sio jamani, maana mm sijao?

Unamfunua kwanza unamuona kuwa ni yeye, ndio ufunge ndoa au ndio munafunga ndoa kwanza halafu ndio unapewa ruhusa ya kumfunua usoni na kumwangalia, au unakwenda ndani kumuona kwa Waislamu,baada ya kufunga ndoa? Hapa kweli kuna fundisho, tuwe makini tusije tukaoa kanyaboya.

M3 twashukuru sana kwa kutujali, mm hapa nimepata fundisho, kwa wale tunaotarajia kuoa. Ubarikiwe sana

Anonymous said...

Kuoa kwa namna hiyo kumepitwa na wakati. Siku hizi mnapimana kwanza weeee, na baadaye ukiona safi, unajua sasa huyu tutaivana, ndio mnafunga ndoa.

Kwahiyo siku ya kufunga ndoa, unamjau mtu unayemuoa,au kukuoa, ipasavyo,hata akijibadili vipi utajua huyu ndio yeye, au sio yeye.

Hawa naona walifunga ndoa usiku, au kwenye kizakiza hivi au ndio hiyop laana ya kulazimisha kuoa, utaoaje mtu hakupendi.

LAKINI KISA KINAVUTIA, TUPE UHONDO M3,INGAWAJE UNATUBANIA KUIONA SURA YAKO!

Rachel Siwa said...

Mmmmhh kweli Mbio za sakafuni ndugu wamimi,Kazi muruwaa kabisa yaani naishiwa maneno.

Wazo Leo limenigusa sana.

Pamoja Daima!!!

Ammy K said...

mie hoi, napenda kusoma ila kazi nazo, bosi mkali, mpaka atoke ndo panya tutawale haaahaaaa.. kisa hiki naamini kina mafunzo mengi sana tu. mimi nakuombea tu ufanikiwe kutoa vitabu vya hadithi zilizopita hasa ile akufaae kwa dhiki daah ile ilikuwa funga kazi. kila la kheri mwaya.

Ammy K said...

raha ya harusi bwana harusi akufunue akuone bi harusi au sio jamani.

Interestedtips said...

wazo tamu kweli......pamoja sana....ila mambo ya kuoana bila kuonana mimi hilo nalipinga kabisa