Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, September 18, 2012

Mbio za sakafuni huishia ukingoni-sehemu ya tatu-1‘Je ulipotoka pale ulikuwa una uhakika kuwa wewe ndiye uliyemuua huyo mwanamke, maana hujasema wazi wazi hapo awali akitika maelezo yako, umesema kabla hujaweka silaha yako vyema ulisikia mlio?’ akaulizwa huyo mwanamke msimuliaji wa sehemu hii.

‘Kiujumla pale mimi nilikuwa sitambui,kama nilivyosema awali nilikuwa kama naota, na pombe zilikuwa zimenitawala kichwani, kwahiyo sikujijua ninachokifanya, au nilichokifanya, ninachikumbuka ni kuwa, niliitoa ile bastola, na kwa hasira nikawa na lengo la kumuua huyo mwanamke, nakumbuka kabisa hivyo, na lakini sikumbuki kumuua, ….’alisema huku akiwa anajaribu kukumbuka kitu.

‘Kipindi kile mlikuwa mnabishana na huyo mwanake, na alikuwa hajakujua wewe ni nani, na sijui kama anakufahamu kwa sura kabla,. Na wakati mnabishaan ndio ukaitoa hiyo bastola kwa hasira, ina maana hukusiki mtu mwingine akifungua mlango?’ akaulizwa.

‘Hapo siwezi kukumbuka vyema, maana kichwa kilikuwa kimejawa na mawimbi ya hasira, nilikuwa nimeghadhabika kupita kiasi, na akili yangu ilikuwa haifikirii kingine zaidi ya kuua, kwahiyo sikuwa na mawazo mengine kuwa kuna mtu kaingia au la..sikumbuki,kabisa’akasema na halafu kama anakumbuka jambo akasema;

‘Ila kweli, kuna muda nilihisi mabadiliko ya hali ya hewa, maana kama upo kwenye chumba, na kimefungwa, hali ya hewa huwa nzito,lakini ghafla kuna kuja kitu kama upepo, hali ya hewa hubadilika,….nahisi kitu kama hicho lakini sikuwa na uhakika’akasema.

‘Hali ya hewa hiyo ilitokea dirishani au mlangoni, maana chumba kipo ndani , na mtu akifungua ili kuwe na hali ye hewa nyingine, inabidi uwe ni mlango wa nje,…?’akaulizwa tena, na yule mwanamama akakaa kimiya akijaribu kukumbuka, lakini hakuweza kusemakitu, akakaa kimiya.

‘Na hebu nikuulize kuhusu silaha yako , hasa baada ya kutoka hapo, ina maana , hukuweza kuikagua hiyo silaha yako, …maana kama imetumika ungeliigundua, hukunusa….hapo ninataka kujua kuwa kweli kama silaha yako ilitumika?’ akaulizwa.

‘Silaha ilitumika, sio kwamba risasi haikufyatuka, ilifayatuka, hili nina uhakika! ‘akasema na kumanya muuliza swali kutulia kwa muda, na kuonyesha kuwa anakuwa na wasiwasi na maelezo ya huyo mwanamama. Huenda kweli aliua.

‘Hebu elezea vizuri hapo, maana kama bastola yako ilitumika, kwanini uwe na shaka kuwa sio wewe uliyeua, je uliweza kusikia mlio mwingine zaidi ya mlio wa bastola yako?’ akaulizwa.

‘Ni kweli bastola niliyokuwa nayo ilifayatuka, lakini nina uhakika ilifyatula na risasi ilitoka kabla sijaielekeza kwa huyo mwanamke, inawezekana iligonga sakafuni au eneo karibu na kitanda, ….nahisi hivyo, maana sikumbuki kabisa kumlenga yeye’akasema.

‘Hapo sasa lipo tatizo, maana kama silaha yako ilifayatuka, na unasema akili yako haikuwa sawa, inawezekana kabisa ulimuua wewe, lakini kwa vile mambo yote hayo yalitokea kwa haraka, na wewe pombe zipo kichwani, na….’akaambiwa.

‘Mimi sijui, maana hapo nachanganyikiwa,….hata hivyo, akili yangu inasema sijamuua mimi, lazima kuna mtu mwingine alifanya hivyo, makusudi, ili nionekane ni mimi, …’akasema.

‘Hapo kunahitajika mwanasheria,na mchunguzi makini, lakini siku zimepita, na hatujui nini kilifuata baada ya hapo, au kulikuwa na mtu wa kufuatilia?’ akaulizwa na yule mwanamama akakaa kimiya tena bila kusema neno.

‘Haya hebu niambie ilikuwaje baada ya pale, polisi hawakukushika au nini kiliendelea baada yaw ewe kutoka kwenye hiyo hoteli?’ akaulizwa.

‘Hapo sasa ndio naona ajabu, …kwani yaliyotokea kuanzia pale hadi hii leo, sijawahi kukamatwa, na wala hilo swala sijalisikia likizungumziwa, na imekuwa kama vile hakuna mtu aliyeuliwa siku ile ‘akasema.

‘Sasa wasiwasi wako ni nini?’ akaulizwa?

‘Mamboyameibuka tena, huyu muhasimu wetu kisiasa ameliibua tena hilo swala,kama silaha yake ya kumshinikiza mume wangu asiingie kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi’akasema.

‘Mimi haposijaelewa, maana kama ulivyosema, baada ya mlio wa hiyo bastola, wewe ulitoka humo ndani mbio, ukiwa umechangayikiwa, je ulikuwa na uhakika gani kuwa huyo mwanamke  kauliwa, maana unasema ulitoka mle ndani ukikimbia, na kesho yake ukasikia mwenzako akiongea na simu , na kuambiwa yule mwanamke kweli kauwawa?’ akaulizwa.

‘Ngoja nikusimulie ilivyokuwa pale….

Baada, na baada yap el hadi tunarudi Dar, ndipo utagundua kuwa huyo mchezo ulipangwa, na lengo hasa ni kuhakikisha kuwa mume wangu hapiti kwenye huo uchanguzi’akasema na kuanza kunihadithia sehemu hiyo.

******     

Wakati tunabisha na yule mwanamke, mume wangu alikuwa anaoga, nakumbuka kabisa kwani muda wote huo nilisikia maji yakimwagika bafuni, kwahiyo siwezi kumshuku mume wangu kuwa huenda ndiye aliyeamua huyo mwanamke. Na nakumbuka wakati natoka na lile sinia nikiwa nakimbia nje, kuna muda nilgeuka, na nilimuona mume wangu akitokea bafuni akiwa kachanganyikiwa, alikuwa kava taulo nab ado nywele zilikuwa na mapofu ya sabuni.

Ule mlio wa bastola, au milio ya bastola ilisikika vyema, kwahiyo nahisi mume wangu aliposikia hivyo alitoka bafuni akiwa anaogopa, na kutaka kujua kuna nini, na mimi nilishawahi kutoka mle, na kwa nje baadhi ya watu waliosikia hiyo milio, au mlio walishaanza kutaharuki.

Mume wangu hakupata nafasi ya kuniona kwa jinsi nilivyotoka mle, kwani alionekana kuchanganyikiwa, na sijui alipohojiwa na polisi, kama alihojiwa na polisi , alisema nini, kwani hata aliporudi toka huko Dodoma hakuwahi kuliongelea hilo tukio , kwani angelisema nini, na yeye mambo hayo yalikuwa ni siri yake.

‘Ina maana wewe hukuwahi kumuuliza angalau kiujanja ujanja?’ akaulizwa.

‘Nilimuuliza kinamna, lakini hakutaka kabisa kuongelea ya huko, yeye alisema mambo ya huko ni mabaya, lakini ana uhakika wa kushinda kwanii mambo yamewekwa sawa’ aliniambia.

‘Nikamuliza hakuna tukio lolote baya linaloweza kumuuingiza kwenye kashafa, kwani alishaambiwa kuwa achichunge na kashafa?’

‘Kashfa itoke wapi mke wangu, mimi nipo makini, na nina watu wa kuhakikisha kuwa hakuna kitu kama hicho, ila nimechoka, na sitaki kuyaogelea na huko, nasubiri matokea yake, kama nitapita au nitaondolewa’akasema. Na hakutaka tuyaongelee mambo ya huko toka siku hiyo.

‘Sasa kwa hali kama hiyo kwanini uwe na wasiwasi?’ akauliza.

‘Kwasababu hali ilivyoonekana, kuna uhakika wa jina lake kupita, na maadui zake wamelijau hilo, kwahiyo hilo tukio waliliweka kama silaha yao ya mwisho,  na sasa wamaamua kuitumia.’akasema.

‘Na kwa vile tukio hilo lipo moyoni mwa mume wangu, hakutaka lifichuliwa, kisiasa na kindoa, kwani anajua mimi sijui, na kisiasa, kuna namna walilikwepa huko, sasa mwenzake anataka kulifichua, na na inavyoonekana keshamwambia kama alivyoniambia mimi’akasema huyo mwanamke.

‘Hapo ndipo shinikizo la m oyo lilipofika mahali pake, wasiwasi ukamchanganya mume wangu na kupatwa na shinikizo la moyo, na aliandamwa na mwambo mengi aliyotegeshewa, ili tu asiwe na katika mpango huo wa uchanguzi, na mimi nikajikuta ninaingizwa tena kwenye huo mkumbo, na bila kujua shinikizo la damu likaniandama na mimi.

‘Sasa hamuoni kuwa ni kutegewa maana kwanza huna uhakika kuwa kweli huyo mwanamke aliuwawa, kiukweli, au sio?’ akaulizwa.

‘Kuwawa aliuwawa kiukweli, hilo nina uhakika,…’akasema

‘Uhakika kwa vipi?’ akaulizwa.

‘Baada ya ule mlio wa risasi yule mwanamke alitoa jicho pale kitandani huku akitoamlio wa ninakufaa, akiwa kashikilia kifuani, na niliona damu zikitoka kifuani, na mimi ndio nikaanza kukimbia’akasema huyo mwanamke, na kumfanya muuliza maswali abakie kimiya kwa muda. Na huyo mwanamke akaendelea kuongea kwa kusema;

Nilipofika kule hotelini kwangu, nilikwenda moja kwa moja hadi chumbani kwa rafiki yangu, nilikuta hayarudi, nikairudishia ile bastola pale nilipoichukulia, na kutoka mle ndani kwake kwa haraka, na wakati nafungua chumba changu, nilimuona akirudi akiwa na mwanaume….walionekana kuwa wamelewa kwani walikuwa wakipepesuka.

Sikutaka zaidi nikafungua mlango wangu na kuingia ndani, nilitafuta kidonge cha usingizi nikameza,nikalala fofofo, hadi alipokuja mwenzangu kuniamusha asubuhi, na aliponiamusha nilikuwa kama naota, sikuweza kukumbuka haraka matukio yote ya usiku….

********
‘Sasa tunaondoka hapa kwenye hii hoteli, tumeshatayarishiwa hoteli nyingine, ambayo huko ndipo tutaondokea, hapa hakuna heri tena’akaniambia mwanadada.

‘Lakini mimi nimeshakuambia kuwa nataka kuonana na hawo polisi ili niwaeleze yote yaliyotokea, maana kama kweli, nimeua, nistahili kuadhibiwa, lakini hisia zangu zinanituma kuwa sikuua, na kama nimeua sikuwa nimekusudia kabisa…’nikasema.

‘Sikiliza wewe, unasema kuwa hujaua kwa makusudi wakati umetoka na bastola hapa, nikuulize, ulikuja saa ngapi hapa chumbani kwangu ukachukua hiyo bastola, na kwanini uliichukua silaha yangu bila idhini yangu hilo kwanza ni kosa’ akasema kwa hasira.

Hilo la kusema hukukusudia , sikuelewi, silaha ulichukua ya nini kama sio kwenda kuua, angalia umbali uliopo hapa hadi kwenye hiyo hoteli nyingine, na ulipofika huko, sizani kama huyo mwenzako alikushambulia, hadi kufikia kuitoa hiyo bastola, alikushambulia,? Jibu ni hapana, yeye hakuwa na silaha yoyote…Hivi wewe vipi,’akasema huyo mwanadada.

‘Ukiongea na polisi na kujifanya wewe ni mtakatifu,ngoja niwaambie ukweli ulivyokuwa , kwanza watakucheka na nakuhakikishia utafungwa maisha kama sio kunyongwa, cha muhimu hapa ni kukimbia’akaniambia.

‘Nina uhakika sijamuua mimi,…kuna kitu pale..’nikawa nasema huku natafakari.

‘Hujamuua wewe, wakati unasema ulikuwa na bastola,hadi wakati mnazozana , ina maana ulikuwa na mtu mwingine pembeni yako, ndiye aliyeitoa hiyo bastola na kumlenga huyo ….usitake kunibabaisha, hapa, cha muhimu fuata ninayokuambia mengine yataeleweka baadaye’akasema.

Basi sikubishana naye, tuliondoka pale hadi kwenye hoteli nyingine na huko tulibakia ndani, yeye alitoka mara kwa mara kufuatilia mambo yanavyokwenda na kumalizia kazi nyingine. Na kuna muda nilitoka pale ndani kusikilizia na kweli nilisikia watuu wakiongelea hayo mauaji’akasema.

‘Walisema nini?’

‘Walisema kuna Malaya kauwawa, na inawezekana ni katika kugombea mabwana, na polisi wanachunguza , kwahiyo wateja wengi wa hiyo hoteli wamaikimbia’akasema.

‘Na baada ya kusikia hivyo, nikaamua kusubiri humo ndani, na nilijiandaa kama nitasikia kuwa polisi wananifuatilia mimi, ninaondoka hapo na kwenda kujisalimisha mwenyewe, lakini mara kwa mara mwenzangu alikuwa akija kuniangalia na kunipa habari ni nini kinaendelea

Baadaye tukiondoka hapo na kuhamia hoteli nyingine ambapo ndio tuliondokea, na kabla hatujatoka huo mji tukasimamishwa na polisi.

NB: muda umeisha bado nipo café, simnajua tena mambo ya kubana matumizi.

WAZO LA LEO: Sio vyema kukimbilia kushutumiana pale kosa linapotokea, maana huenda hata sisi ni wakosaji tena ziaidi, kwani ilivyo sasa hivi ni rahisi sana kumshutumu mwenzako kuwa yeye kakosea, hafai, hajui, nk, wakati hata sisi tunakosea tena zaidi ya wenzetu.
Ni vyema kosa likitokea tuwe na hekima ya kuelezana, na jinsi gani ya kulitatua hilo tatizo ili kujienga umoja ,upendo na ushirikiano.


Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

Hongera kaka m3 sasa mambo ya kutwangana risasi.

Anonymous said...

Natumai upo mbioni kutoa kitabu, maana nimeona kuna uhamasishaji wa watunzi, ingawaje inaonekana wanahitaji damu changa,
lkn kama angalizo, kwanza kaza buti, lakini pili na uwe makini na hawo watu, wengine lengo lao ni kukusanya kazi za watu, wauze, na faida nyingi inakwenda kwao!

Amina K said...

jamaniii.

Anonymous said...

zdyossmva
http://www.guccigekiyasu.com/ gucci 財布
http://www.guccishinsaku.com/ gucci
http://www.gucciautoretto.com/ グッチ バッグ アウトレット
http://www.guccioutletja.com/ グッチ メンズ
sitekckca
[url=http://www.guccigekiyasu.com/#namljrtwl]グッチ バッグ[/url]
[url=http://www.guccishinsaku.com/#ssqcqbsxv]グッチ アウトレット[/url]
[url=http://www.gucciautoretto.com/#rhevvuhyr]グッチ バッグ[/url]
[url=http://www.guccioutletja.com/#bggxeqvtk]Gucci 財布[/url]
ufadehtcj
gucci バッグ
gucci
グッチ アウトレット
グッチ メンズ

Anonymous said...

I love your site, but honestly tell you that you need more for him to monitor those who commented with your records.

Anonymous said...

Carbs and glucose, which include sucrose, fructose, sugar and carbohydrates, Cheap Hot Couture Purses and in many cases sorbitol,gucci 財布, Michael Jordan Shoes in many cases are the subsequent at their very own most effective nourishing around fluid.
グッチ長財布,The girl gives
common potential customers so that you can customers just
like Frank Galliano together with gucci アウトレット,
Dior and after that hears his / her or her's thoughts plus vision for you to successfully obtain views regarding your girlfriend.Look at my homepage:http://gucciindex.com/
Here is my homepage グッチ アウトレット