Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, September 11, 2012

Mbio za sakafuni huishia ukingoni-sehemu ya pili-4



Mchana ulikuwa wa  pilika pilika, kukutana na wateja, na kugongana katiba bei mpaka unafiki mahali unauza kitu chako,sikuamini , maana bidhaa nyingi zilinunuliwa kwa baei kubwa ambayo sikuwahi kuuza kabla, nikagundua kuwa kumbe wenzangu hawa wanaochukau bidhaa zangu na kuja kuuza huku walikuwa wakipata faida kubwa sana.

‘Unaona ,hiindio biashara, ndio maana hawa wanzetu wakiwa na kikao huku, tunafanya kile tuwezalo tuje huku, …’akasema mwanadada.

‘Kweli nimeamini, kumbe ndio maaana mpo juu kibiashara, …mumenifungua macho, safari nyingine sibakia nyuma’nikasema.

‘Muda bado wa kuchuma, pesa, ngoja jamaa watoke kwenye mikutano yao, ….hawa waliokuja ni wachache tu, ambao wengi walikuja kusikiliza , wapo ambao wanalipwa marupurupou ya hali ya juuu, wapo bado kwenye kikao, ..’akasema.

‘Ina maana kuna wengine watakuja?’ nikauliza.

‘Kwani umewaona wenyewe  hapa,…saa zao bado, wakaitoka kwenye vikao vyao utawaona,  ..’akasema na yeye akaondoka na kuniacha nikiendelea na kuuza bidhaa zangu…na kila muda nilipokuwa sina mteja, nikawa namuwaza mume wangu kwani nilikuwa sijajua wapi alipo, na niliogopa kumuuliza mwenzangu, kutokana na masharti niliyopewa,kuwa tusiongee lolote kuhusiana na hilo lililonileta hapo.

****

‘Mke wangu kama ulivyosikia , leo ndio kikao maalumu cha kusikiliza maombi yetu,kwani wamemuweka mtu mwingine kinyume na makubaliano ya mwanzo,na kwa ajili hiyo tumeweka pingamizi, kwahiyo leo ndio siku ya kusililizwa hilo pingamizi,…’akanimambia ,mume wangu.

‘Sawa mimi ninakusikiliza wewe, maana najua nini kitafuata baada ya hayo maelezo yako hayo, lakini ukumbuke kuwa sasa hivi hata biashara zetu hali ni ngumu sana, hapa nilipo nawaza jinsi gani ya kujikwamua…’nikamwambia mume wangu.

‘Lakini mke wangu haya si kwa ajili ya maisha yetu ya baadaye, kwani nafanya haya kwa ajili ya nani kwa sio kwa ajili ya familia…hebu niambie?’ akaniuliza.

‘Najua  hilo, lakini unaweza ukatumia nguvu nyingi pasipo na sababu, na hapo ukapata vsingizio vya kufanya mengine yasiyokubalika, lakini mimi sitaki kusema mengi. Ninachoweza kusema nikukutakia safari njema na mafaniko mema, na ukifika huko usisahau kunisalimia wote hasa wale wanakutuliza mawazo baada ya kikao..’nikasema na yeye akacheka akijua kuwa nafanya utani, akaniangalia mara moja na alipoona namtizama akaangalia pembeni.

‘Hakuna anayeweza kunituliza mawazo zaidi yako mke wangu, ni kwa vile ni mbali, ilitakiwa tuwe pamoja, au safari twende pamoja?’ akauliza.

‘Kama ulikuwa na lengo hilo ungeliniambia toka mapema, il niweke mambo yangu vyema,. ..nahisi kuniambia muda kama huu ,na kesho ni safari ni kunitega….,’nikasema.

‘Sio kukutega mke wangu, najua kuwa kuna mambo yetu ya biashara ambayo usipokuwepo wewe hayatawezekana, na kama ulivyoniambia jana kuwa kuna mizigo mingine unapeleka Morogoro, sio mbaya, lakini mimi sipendi biashara hizi za safari ndefu, …siwi na amani kabisa’akaniambia.

‘Hakuna anayependa mambo kama haya ya kwenda masafa, hata mimi mwenyewe sipendi safari zako hizo za kila siku kwenda huko kwenye vikao, lakini hakuna jinsi,..cha muhimu ni kujua wewe ni nani…’nikamwambia.

‘Sawa mke wangu, mimi nakuelewa, ila nilikuwa nauliza , ulisema kuwa ukitoka huko Morogoro utangaalia kuwa unaweza kwenda mbeel kidogo, mbele kidogo wapi, …?’ akaniuliza.

‘Huo mzigo ukiisha, nitarudi huku Dar, ili nichukue mwingine, lakini kama hautaisha hapo Morogoro, ninaweza kusogea mbele zaidi, kuwafuta wateja huko walipo,….siku hizi unatakiwa kuwafuata wateja walipo…’nikamwambia, na kabla hatujaongea zaidi simu yake ikaita, na kama ilivyo kawaida akatoka nje, na mimi nikapata mwanya wa kumuandalia  safari yake, huku nikiwaza mazungumzo yangu ya mwisho na mwanadada.

********
‘Siku ile baada ya harusi mume wangu alikuwa mtu wa kulewa, na akirudi nyumbani hujibwaga kitandani, hakuwa na muda na mimi. Nikijaraibu kumuuliza yeye alidai kuwa hanitambui kama mke wake, kwahiyo niondoke hapo nyumbani kwake, lakini sikukubali, sikukata tamaa, nikujua mtaka cha mvuguni sharti ainame. Na jambo jingine lililonitia hamasa ni kuwa wazazi na ndugu zake walikuwa upande wangu…’akasema mke wa hasimu wa mume wangu.

‘Sisi tupo na wewe hatupendi ndugu yetu amuoe huyu mwanamke wake aliyemtaka bila ya kutuhusisha sisi, mke ambaye kila mtu anamtaka ni wewe,….wewe ulitambuslishwa kwetu, na sisi tukakukubali, sasa huyo mwingine katoka wapi, mke mwenyewe tunasikia ni mshamba wa huko kijijini, sis huyo hatufai,….’alisema mmoja wandugu za mume wangu.

‘Sisi siku zote tunajua kuwa wewe ndiye mchumba wa kaka yetu, tulishangaa siku ile alipokuja na kusema anataka kumuoa huyo mshamba,…eti anadai kuwa huyo ndiye alimpenda na kuna mtu anataka kumuonyesha kuwa yeye ni zaidi yake’akasema ndugu mwingine. Na hapo nikawa na amani kuwa sipo peke yangu.

‘Ina maana kutaka kukuoa wewe, ni kutaka kuonyesha kuwa yeye ni zaidi ya mume wako, sio kwasababu ya mapenzi, maana mimi na yeye tulianza mapenzi yetu toka zamani, na hadi kufikia kuvalishana pete, na wakati huo alikuwa akikufahamu, jiulize kwanini hakukuvalisha pete wewe…’akasema.

‘Nikuambai ukweli siku saba za mwanzo zilikuwa za mateso kwangu, maana huyu jamaa alikuwa akinywa pombe kupita kiasi, na siku nyingine alikuwa akirudishwa nyumbani akiwa hajiwezi, ikawa kazi yangu kumvua nguo,  hata kumuogesha, kwani wakati mwingine alikuwa kajichafua…kabisa. Yote hayo ilibidi nikubaliane nayo maana naweza kusema nimejitakia mwenyewe.

Siku ya nane ya mateso, kuzalilika zarau na hata kubigwa mangumi na mateke, ilileta matokeo yake, siku hiyo mume wangu alirudishwa akiwa hajiwezi anavuja damu, kaumizwa sana,nilishangaa rafiki zake badala ya kumpeleka hospitali walimleta nyumbani wakidai kuwa kakataa kupelekwa hospitalini,eti ana dakitar, ..hapo nikaanza kuogopa,nikai wake, na hata tulipowauliza imekuwaje, wao hawakutaka kuweka wazi sana, walisema;

‘Mambo ya walevi haya, kapigwa na mwenye mke, kaingilia anga zisizoingiliwa…’akasema mmojawapo

‘Mwenye mke…?,  ina maana kafumaniwa?’ nikauliza.

‘Ndio maana yake,…. lakini tumeyamaliza,…ni ajali kazini’akasema huyu rafiki yake naye akionekana bado kalewa. Iliniuma sana, licha ya kuwa nilijua mambo kama hayo kwa huyu mume wangu yanawezekana kuwepo, lakini baadaye sikujali nikasema tutabanana hapo hapo, mpaka kieleweke.

Kesho yake asubuhi, wakati namuuguza yale majeraha, baada ya dakitari kuondoka, tofauti na siku nyingine, alikuwa mpole sana, na aliweza kutulia nyumbani siku hiyo,labda ni kutokana na yake mjereha, aliona aibu kukutana na watu akiwa hivyo. Na lipofika mchana nikamuandalia chakula, nikiwa najua kama kawaida yake,atakipiga teke hicho chakula na kunivurumishia matusi na mateke, lakini haikuwa hivyo, alikula na baadaye akatulia, na mimi nilipoona hivyi nikaja na kukaa karibu yake huku najihami.

‘Mke wangu najua nimekukwaza sana….nisamahe ka yote, ingawaje umejitakia wewe mwenyewe haya yote…’akasema na kwa mara ya kwanza akatamka hilo neno mke wangu, sikuamini nikageuka kumwangalia huku usoni nikiwa nimejawa na tabasamu la kutokuamini, na baadaye machzo yakanitoka, sijui ni kwasababu ya furaha au ni kitu gani.

‘Unasemaje mume wangu, ..?’ nikauliza nikitamani arudie lile neno ‘mke wangu ‘kwa mara nyingine.

‘Nimefikiria sana, na baadaye nimeona sina jinsi, kwani yule mwanamke nasikia keshaolewa na yule mshamba mwenzake, hata hivyo, nitahakikisha nayasambaratisha maisha yao, nitahakikisha hapati raha, na ikiwezekana nitamzalilisha kila hatua,hadi aje kunipigia magoti…atajua kuwa mimi ni nani’akasema kwa hasira huku akigonga meza.

Mimi nilimuitikia kama mume wangu, lakini sikutaka hayo anayoyataka kuyafanya, kwani ukizingatia kuwa hayo yaliyotokea ni kwa manufaa yangu. Nilichofanya mimi ni kuuma na kupulizia, nikiwa na maana kuwa, tunayapanga pamoja, lakini tukitoka hapo natafuta njia nyingine ya kuyazuia kinamna,…

‘Kuna siku kabisa ilipangwa mbinu ambayo mume wako angalipata ajali, …lakini mimii nikafanya mbinu, na mipango hiyo haukufanikiwa, na sasa najua kabisa huko Dodoma kuna mipango mingi imepangwa, ambayo mimi sijaijua vyema, kwani nahisi walinigundua kuwa huenda mimi natoa siri zao ndio maana walikuwa hawanihusishi tena kwenye mipango yao.

‘Mimi hizi safari za kwenda Dodoma, zikuzipanga hivi hivi tu, kuwa labda nakuja kumfumania, hapana hayo nilishayapa mgongo, afanya atakalo, …lakini kuna kitu kinaniuma, na kinanifanay nijione kuwa nahusika, na huenda isingelikuwa mimi hayo yasingelikuwepo, na ndio maana nimekuwa nikijitolea kw ahali na mali kuhakikisha natimiza wajibu wangu.

Moja ya lengo langu la kwenda mara kwa mra huko Dodoma, ni kuwa mlinzi wa mumeo, hutaamini hayo, lakini najitahidi pale ninapoweza, na nina watu wangu wanaifanay hiyo kazi, sikustahili kukuambia hili,lakiini imebidi, na nimeapa kuwa nitahakikisha kuwa hakuna mabaya yanayotokea kwa mume wako.Lakini siku nilipogundua kuwa mume wako kajiingiza kwenye makundi haramu, makundi ambayo hayana mambo mame,….sikuamini, ….

‘Ina maana kuwa ..’nikaishiwa hata la kuongea.

‘Ndio maana nataka tushirikiane kwa hilo, …lengo letu liwe moja, ikibidi hawa watu waje kushikana mikono wakubali matokea, yaani mume wangu na wa kwako waje wakubaliane na …’akasema.

‘Kwa jinsi nimjuavyo mume wangu sizani kama hilo litafanikiwa’nikasema.

‘Hata mimi nalijua hilo, lakini tutafanyaje …unakumbuka nilivyokuambia awali, kuwa vyovyote iwavyo, lakini sisi ni wanawake, tunaunganishwa na uasili wetu, kuwa sisi ni walezi, sisi sio walezi wa watoto wetu tu, lakini pia ni walezi wa familia, walezi wa waume zetu….’akasema mwanadada huku nikimshangaa.

‘Najua utashangaa hilo, lakini ukiolewa ujue hilo ni jukumu lako, jukumu la kuwalea wanaume zetu, tusilikwepe hili jukumu. Tukilikwepa ndiyo hayo machafu yanapotokea. Najua kabisa tukiwa pamoja na tukawa na lengo moja, tukajua majukumu yetu, tunaweza kuifanya dunia hii ikawa na amani, lakini tukiwa kinyume chake, …dunia hii haitakuwa na amani abadani,…’akasema

‘Sijui, nsikuelewi, maana kusema ni sawa, lakini jinsi gani ya kuwafanya hawa watu wakubaliane na sisi na kazi nyingine kubwa sana…sijui…hata hivyo sijakubaliana na hayo yako, kuwa mume wangu kajiingiza kwenye hayo machafu, …nimjuavyo mume wangu hilo haliwezekani. Labda…sijui wamempa kitu gani..’nikasema nikionyesha kuchanganyikiwa.

‘Ndio maana nikakutaka tuongezane huko ukajionee mwenyewe…

Nilipowaza hayo nikasema lazima nifike huko Dodoma nikajionee mwenyewe. Haya siku inakwisha, na jioni hiyo inaingia mbona sijamuona huyo mume wangu, …Na wakati nawaza hilo, nikaona gari likipita na kusimama mbele yetu, na walioshuka pale walikuwa watu wanne, wanaume wawili na wanawake wawili, na mmojawapo alikuwa mume wangu, nikasogea pembeni ili nimuangalia vyema nione wapi anapoelekea.

‘Ukimuona usichukue papara, nipigie simu kwanza, nitakuonyesha nini cha kufanya..’nikakumbuka hayo maneno, lakini mimi sikusubiri nikaanza kumfuatilia mume wangu huko anapokwenda…kwani hata hivyokila nilipokuwa nikimpgia simu mwanadada,ilisema namba hiyo inatumika’

NB. Haya jamani tupo makaoni, tuone nini kitatokea....

WAZO LA LEO: Maneno mengi pekee hayajengi, matendo na mipango thabiti inayotekelezeka ndiyo mafanikio ya jambo lolote.


Ni mimi: emu-three

7 comments :

Yasinta Ngonyani said...

mmmhhh hapa simulizi tamu nasubiri kuona kitatokea!!!

Precious said...

mmmmhhhh kwa kweli yataka moyo mambo ya ndoa na mahusiano kwa ujumla

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

If sоme one deѕіres to be updated with most
uр-tο-date technolοgies thеn hе
must be paу a viѕit this web page
and bе up tο dаtе еvеryday.
My website : best memory foam mattress

Anonymous said...

Whаt's up, always i used to check webpage posts here early in the break of day, as i like to gain knowledge of more and more.
My site: same day loans

Anonymous said...

Hi, І dо think this is аn excellent blog.
І ѕtumbledupon іt ;) I am gοing
to revisit yet again since I bookmarκеd it.

Mοney and freedom іs the greatest way to change, may you be гіch and
continue to helρ οther ρeople.
Also visit my page - instant payday loans

Anonymous said...

bοokmarked!!, I reаlly liκe your sitе!
Also see my web page :: quick loans