Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Saturday, September 22, 2012

Hapa ndipo msingi wa elimu yetu



Kuna siku nilipita mahali nikakuta mti ambao kwa wanaoujua historia yake, wanasema ni mti wa zamani sana, hata ukiuangalia, utakuwa mizizi yake ni mikubwa na shina lake ni imara. Sio huo miti tu, kuna yumba za kihistoria, kuna huko Bagamoyo na Kilwa, utakuta nyumba kama hizo ambazo zilijengwa miaka mingi nyuma na bado zipo, ingawaje hatutaki kuziweka katika hali ya uimara zaidi tena

Vitu kama hivyo vya kihistoria wanatakiwa watu ambao ni wataalamu wa ujenzi, wakaziboresha katika mfumo wake ule ule, uliokuwepo, bila kuharibu kitu,hiyo inawezekana, niliona wenzetu wa Ujerumani, wakijereshea nyumba zao za asili,kama zilivyokuwepo awali. Na huoni tofauti, au tunashindwa, labda mapaka kuwepo wafadhili,sijui!

Lakini haya yote hayakuwezekana kama kulikuwa hakuna `msingi’ imara wa majengo hayo, au mizizi  madhubuti wa miti hiyi. Ukianganlia mifano hiyo, utaona haina tofauti na maendeleo ya ujenzi, maendeleo ya kimaisha mengi hutegemea misingi imara iliyowekwa kabla.Kama hakuna misingi imara, hatutaweze kuendeleza hicho kilichopo, tutakuwa kila siku tunaanza moja.

Tulishuhudia mejengoya gorofa yakidondoka hapa nchini siku za karibuni, chanzo kilikuwa ni nini? Ni kutokana na kutokuwepo na msingi imara, ambayoo mtaalamu alitakiwa kuuweka, huenda mtalaamu alitoa tasmiini, nini kinatakiwa, lakini watelekezaji wakachakachua, nini kilitokea,tuliona wenyewe.

Nalizungumza hili nikijua kuwa leo watoto wetu wa darasa la saba wanafanya mitihani, mitihani ya `shule za msingi’ hata jina lenyewe linajieleza kuwa ni elimu ya msingi. Hii ilionyesha jinsi gani wenzetu walivyolifikiria hilo kwa makini. Kwani wenzetu waliobuni jina hili waliona mbali, wakijua kuwa huo ndio msingi wa elimu ya mtoto. Hapo ndipo kulitakiwa nguvu zote zielekezwe, ujuzi wa hali ya juu utumike, na ili msingi huo uwe imara, walihitajika `mainjinia’ wa hali ya juu wa kuwekeza msingi huo.

 Kwasababu hapo ndio msingi wa mtoto, ambaye tunatarajia atapanda kama gorofa linavypanda kielimu had kufika ngazi za juu. Sasa kama huyu mtoto hakujengwa vyema kielimu, kwa kuwekewa  msingi imara, kweli ataweza kufika huko juu tunapotarajia . Huyu ndiye mtalaamu tunayemtegemea na hapa ndio msingi wake ulipoanzia, je huyu kweli imwekwa kitaalamu(kitaaluma)

Kwetu sisi msingi wa elimu hatukuuchukulia kama msingi wa nyumba, tuliona ni sehemu tu ya kujifunza kusoma na kuandika, ambapo mtu wa kawaida anaweza akasimamia. Ndio maana walimu wake tunachukua wale ambao hawakufanya vizuri sana kwenye masomo yao, kwani tunachofanya sisi wale waliofanya vyema kwenye mitahani yao, ndio wanakwenda elimu ya juu. Huo ndio msingi wa  nyumba yetu, ambayo tutarajia iwe gorofa.

Angalia sasa jinsi mitaala inavyobadilishwa kila siku, ina maana tangu tupate uhuru hatujaweza kuwa ni mitaala thabiti, hatuna wataalamu walioweza kuweka mitaala imara ambayo tungeliweza kujivuna kuwa hii ndio mitaala itakayo jenga nyumba imara ya gorofa. Nasita hata kusema kuwa hapo sasa pamekuwa ni sehemu ya kujaribia kama ule usemi wa kiongozi wetu wa kichwa cha mwendawazimu, kila mtu akija anakuja na ufundi wake, unaujaribu labda kama utafaa. Sio nalaumu, lakni mimi nashindwa tu kuelewa mpaka lini!

Sasa hivi watoto wetu hawo wa shule za msingi, waliingia kwenye mitihani yao, na utaratibu mwingine mpya, na huo utaratibu tunaujaribu kama utafaa, baada ya miaka ya mtu mzima wa uhutu bado tunajaribisha, haya ngoja tuweke huo msingi wa majaribio wagorofaletu la elimu.

Wazazi wenye uchungu na vizazi vyao, wamelalamika na utaratibu huoo mpya kwasababu,umeletwa muda mfupi kabla ya kufanya mitihani, hata kama wamejaribiwa, lakini tukumbuke huo ndiomsingi wa elimu, na hilo tunalotaka kufanya halihitaji majaribio,kwa unyetiulivyo, sijui kama hija yangu mnaielewa.i lakini ndio hivyo,hatujui ni kwanini ukaletwa huo utaratibu mpya,na kwanini ukaletwa  muda mfupi tu wakati watoto wanakaribia kufanya mitihani.

Tunaomba ili tufike mbali,sehemu hii tuwekee `mainjinia ‘ ambao wana elimu ya kutosha , wana uchungu na watoto wetu, ili kweli tuweze kuweka misingi imara, kama kweli tuna nia njema na kizazi chetu kijacha, kama kweli tuna nia njema ya kuleta maendeleo ya nchi yetu.

Vinginevyo tutaishia kila siku kuanzisha msingi mipya,wakati wenzetu wanaendeleza magorofa yao.  Na kinachofanyika sasa sio kuweka misingi mipya mimi naona kama vile tunaweka miti pembeni ili nyumba hiyo, isije ikaanguka!Kwani elimu ya miaka saba ingelijulikana matunda yake hata kabla ya huo mtihani, tujue mtihani sio tija, cha lazima ni ile miaka saba iliwekeza nini. Tusije tukawafunza watoto wetu kucheza kamari ya kubuni, na wenye bahati wakazipatia hizo namba!

Kwa uoni wangu mdogo, hili halitawezekana kama sehemu hiyo haitafanyiwa utafiti wa kina na kuweka watu wanastahili, wenye elimu ya `uinjinia’  na pia wawe na uchungu na watoto wetu. Sehemu hiyo isafishwe kabisa, na kuweka watu makini, wenye uchungu na watoto wetu.  

Tujua kuwa seehmu kubwa ya elimu hiyo ya msingi ambayo haina matokea mazuri, ni kwa watoto wetu wanaosomea kweney mavumbi, wenzetu watoto wao wanapelekwa shule za kimataifa je, sisi wakulima, sisi walalahoi, watoto wetu watakwenda wapi, baaada ya kuwekewa msingi huo wa vijumba vibovuvibovu, ambavyo kila baada ya mwaka, tunawekewa viraka na miti pembeni ili visianguke.

Wananchi tuamuke na tuhoji,…hili ni letu, na tusipohoji na kufuatilia mwisho wa siku inakula kwetu, hili ni jukumu letu sote, tusilale na kuiachia serikali, kwani serikali ni sisi, na hao waliowekwa hapo kusimamia elimu, tunawalipa sisi weyewe kwa kodi zetu, na ili wawajibike vyema tusaidiane nao, na moja ya msaada mkubwa ni kuhoji, kuuliza ili kujua, sio kukaa kimiya na kulalamika pembeini.

Tumuombe mungu awajalie watoto wetu wafanye mitIhani yao vyema kwa amani na usalama. Kwani wao hawajui ni nini kinachoendelea, matarajio yao ni kwenda mbali, na kwenda mbali kwako ni elimu hiyo waliyoipata kama msingi wao. Kama kwelii mabadliko yaliyowekwa yana nia njema, twakuomba mungu uyabariki, lakini kama yana nia ambayo haitasaidia baadaye, mwenyezimungu tunaweka kilio chetu mbele yako. Twakuomba utusaidie kwa maslahi ya vizazi vyetu na taifa letu kwa ujumla . AMIN


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Haya ni muhimu sana kwa mkuu wetu, kuhakikisha hicho kitendo cha wizara, kwanza kinasafishwa, na pili kiwekwe watu wanaostahili.

Tusiangalie uzoefu tu wa mtu, lakini ni vyema tukaangalia`utaalamu'wenye tija, utaifa na uadilifu. Mtu akivurunda tumuondoe.

Lingine kwa maoni yangu ni kuwa tusiweke mtihani wa mwisho kuwa ndio kila kitu kwa mtoto. Mtoto apimwe kila hatua na mtihani wa mwisho uwe ni sehemu ndogo tu ya kuhitimisha.

Ninashangaa sana eti hata hesabu inakuwa ni ya kuchagua, hamjui kuna watu wanabahati ya kukisia, hivi huyu aliyefanya hivyo hajui hesabu nini, maana yeye anafikiri hesabu unachagua kama masomo mengine. Sielewi.

M3 naomba maoni yangu haya uyawasilishe, kwani mimi ni mzazi na nina uchungu na kizazi hiki na nchi yangu.