Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, September 28, 2012

Bora ya mchawi kuliko mfitinishajiKuna siku za nyuma, nilipita mahali nikakuta kuku wanapigana, na cha ajabu, watu walikuwa pembeni wakishangilia, na kila mmoja akimpa ushindi mmoja wa kuku wale. Na binadamu tulivyo watu walikusanyika na kuwazunguka wale kuku huku wakishangilia. Leo nimekuta jambo hilo, lakini cha ajabu baadaye kwenye hilo kundi la watu, kukatokea mzozano, kuna mmoja akdai kuwa mwenzake kamsemea mbovu, na badala ya kuangalia wale kuku,ikabidi watu wageuka kuangalia watu wakikabana na na kurushiana makonde,na kuishia kuumizana.

‘Jamani mbona mnakuwa kama hawa kuku!’akasema mama mmoja.

‘Na wewe mwanamke, usilete maneno yako  ya kejeri hapa, ninaweza kukuchenjia na wewe’akasema mmoja wa wale waliokuwa wakipigana.

‘Unajua tofauti yetu na hawa kuku, ni kuwa sisi wanadamu mungu katupa busara na hekima, ili tuweze kuwa na maamuzi sahihi’nikasema.

‘Ni kweli’mmoja akadakia.

‘Sasa hebu angalieni wale kuku, wamepigana mpaka sasa hawana nguvu, kila mmoja anapepesuka, hebu tujiulize wale kuku walikuwa wakipigania nini,?’ nikauliza.

‘Mmoja kaingia kwenye anga za mwingine, huoni yule mtetea aliyesimama pembeni, kila mmoja anataka kumuonyesha yule mtetea kuwa yeye ni zaidi ya mwenzake’akasema bwana mdogo mmoja.

‘Je na hawa waliokuwa wakipigana hapa sasa hivi wanataka kuonyeshana nini?’ akauliza jamaa mmoja.

‘Hawa naona bangi zinawakera kichwani, waacheni wapigane, wakiumizana watajifunza, kwani wahenga walisema ndugu wakipigana chukua jembe ukalime’akasema jamaa mwingine.

‘Hapana, sio vyema watu wakigombana mkawaachia hadi kupigana na kuumizana. Ni vyema ukiona watu wamekosana, ukawapatanisha, kwani kupatanisha waliokosana, ni jambo analolipenda sana mwenyezimungu. Na hebu angalia mataifa yanayogombana, nini kinatokea, kama sio watu kukimbia majumba yao, na kwenda kuishi ugenini, na ukiangalia sana wanaoumia zaidi ni watoto, wazee na akina mama. Je hapo kuna heri gani’ akasema mzee mmoja.

‘Kupatanisha waliokosana ni jambo la heri,na kama sote tutakuwa na mioyo ya kupaatnishana , dunia hii ingelikuwa ni uwanja wa amani na upendo. Cha ajabu ni kuwa dunia hii imegeuka kuwa uwanja wa fujo kwasababu tunaona raha watu waigombana, na baadala ya kuwapatanisha sisi tunazidi kuwachonganisha.

‘Hebu angalieni vyombo vingine vya habari, hasa hivyo vinavyoitwa vya udaku,ni nini wanachokifanya,je kinaleta heri, kama sio kufarakanisha. Haya angalieni mataifa mengine ambayo badalaya kupatansiha watu wanazidi kuwachochea, kwa kulalia upande mmoja, nia hasa ni nini kama sio ubinafsi . Kwa  mtaji huo dunia haitakuwa na heri kamwe, amani na upendo vitakuwa kama msamiati uliosahaulika.

Tupende kupatanishana ili tuwe na heri, na jambo hili mola pekee ndiye mlipaji, usifanye hivyo kwa jaili ya kujionyesha kwa watu ,au kwa kutafuta sifa, fanya hivyo kwa ajili ya mola wako ukitarajia heri nyingi baadaye, na kweli utaziona kuanzia hapa hapa dunia.

Mimi naona ajabu watu wanafarakana , na hata kufikia hatua ya kununiana, na wanaweza wakaishi hivi hivi masiku kadhaa , na hata miezi, kila mmoja hataki kuongea na mwenzake, na hutaamini ukiambiwa kuwa hawo ni ndugu baba na mama mmoja. Na ukichunguza sana, ni sababau ya kufitinishwa. Ndio maana wahenga walisema ni bora hata ya mchawi kuliko mfitinishaji. Hili jamani sio jambo jema na halina heri kwetu.

Tukumbuke kuwa sisi ni wanadamu, sio kuku au wanyama, tuna akili, na tumepewa hekima na busara, vitu ambavyo ni bure kabisa, havihitaji kununuliwa. Tutashindwa na  kuku, au wanyama wengine, ambao licha ya kuogombana  kwao lakini kesho unaweza ukawakuta wanakula chakula pamoja na hata kuingia banda moja mahali wanapolala.

 Amani duniani itatengemaa, kama sote tutajitahidi kuwapatanisha wale waliokosana kwa usawa, bila ya ubaguzi, bila kujali tofauti zao, kwani amani ikivurugika haijali hizo tofauti, kila mmoja aatingie kwenye hasara.

Ijumaa njema..


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

I dοn't even know how I ended up here, but I thought this post was good. I do not know who you are but definitely you are going to a famous blogger if you aren't alгeadу
;) Cheerѕ!
Also see my webpage: indianapolis emergency vet

Yasinta Ngonyani said...

ubinafsi ukizidi ndo mambo yanakuwa hivyo...ijumaa njema nawe pia na wote watakaopita hapa..