Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, August 21, 2012

Mbio za sakafuni,huishia ukingoni 5




Nikiwa bado nipo kwenye kochi nikiwaza ,nilimuangalia mke wangu, na kutabasamu, yeye aliponiona nikimwangalia nakutabsamu, akasimama na kukunja uso kwa hasira, alijua labda namsanifu, akasema;

‘Ina maana unaniona mimi mjinga nikihangaika na mikazi ya hapa nyumbani,…unanisanifu au sio..?’ akaniuliza huku akiniangalia kwa hasira.

Mimi nikamwangalia kwa makini bila kusema neno, alipoona siongei , akasema;

‘Sasa kuanzia leo tunapangia zamu, mimi nikipika wewe upige deki nyumba, au ufagie, sio kukaa hapo kwenye kochi na kukunja nNe, huku, unanicheka, unafikirii mimi hapa nafaidi, unafikiri mimi hapa nacheza,…’akasema kwa hasira na yeye akakaa kwenye kochi na kutupa vitambaa alivyokuwa kavishika mkononi.

Niliinuka na kuvichukua vile vitambaa, nikaanza kuvitandika kwenye kochi,huku kumbukumbu za nyuma zikiwa zimetanda tena kwenye ubongo wangu, nikikmbuka jinsi nilivyoweza kufanikiwa kumchukua, huyu binti,katiak dakika za mwisho, wakati kila kitu kilashakamilika na rafiki yangu ndiye alikuwa anasubiriwa afike, wafunge ndoa. Hali hii nilitarajia itakuwa pia kwenye mambo yangu ya kisiasa, lakini haikuwa hivyo, …..
********
Kila nikipiga simu ya yule binti ilikuwa haipatikani, nikaona ni bora nifunge safari niende huko  huko , kwani yeye alikwenda huko kijijini kumsaida bibi yake kazi na akiwa kwenye likizo fupi, likizo ambayo mwenzangu aliichukulia kinamna yake .

Mimi nilipofika ofisini, niliomba likizo ya zarura, na nikakubaliwa bila pingamizi,  na kesho yake nikaingia kwenye basi kuelekea huko kijijini. Nikiwa ndani ya basi nilimuwaza sana huyu rafiki yangu. Sikuamini kuwa angeinifanyia hivi, na niliumia sana pale nilipokumbuka kauli zake za zarau kuwa mimi sina chochote, na siwezi kushindana na yeye.

Nilijaribu kukumbuka maisha yetu ya shuleni, jinsi tulivyokuwa karibu, na jinsi gani nilivyokuwa nikimsaidia kimasomo, maana yeye alikuwa sio chochote, katika masomo, nilikuwa nikimsaidia sana, mpaka akafikia hatua hiyo,lakini sasa kimaisha yeye yupo juu, na mbaya zaidi hakumbuki fadhia zangu, anasihai kunisimanga. Nikaamini ule usemi wa kuwa kuwahi sikupata, ….

Nilikumbuka siku zile za mwisho zamitihani, ambapo alijua kabisa yeye anaweza akafeli, aliniambia;

‘Ndugu yangu nisaidie tu, ili nifaulu huu muhula wa mwisho (semester), maana nikifeli hapa,nimefeli mambo mengi. Wazazi wangu wamenihakikishia kwua nikfaulu na kupata cheti, basi, mambo safi kabisa huko duniani,tatizo ni haya mavitabu na mahesabu, …nikipata hilo ganda lao tu,utaona vumbi langu…’akaniambia.

‘Kwani huko duniani kwenye ajira hawaangalii kufaulu kwa mtu?’ nikamuuliza.

‘Aaa wapi, huko hawana habari na makaratasi yako , eti ulipata `A’ kubwa, hakuna kitu kama hicho, huko akili kichwani kwako, huko ni nini bosi anataka, ukimjulia bosi wako, basi umeula, kwanza tukitoka hapa unachotakiwa ni kuhakikisha unapata ajira sehemu yenye maslahi, na ili uipate nafasi kama hiyo, unatakiwa uwe na refa…huko hawaangalii maksi zako bwana..’akasema huku akikiuna kichwa.

‘Sawa mimi sina shida, nitakusaidia tu rafiki yangu, na wewe natumai huko duniani hutanitupa, lakini , tatizo lako hutulii darasani, vipindi vingi unakosa, na hata ukiwa darasani unaonekana huwi makini na anachofundisha mkufunzi,….’nikamwambia.

‘Hapa, mimi ninawaza kupata pesa tu, kupata pesa haihitaji mahesabu, magumu, …sasa nakuomba kitu wewe nionyeshe jinsi ya kulifanya hili swali,…wewe lifanye , halafu mimi nitanakili, mengine baadaye, na kwenye mtihani nitajitahidi tukae karibu, nikikuminya wewe usogeze karatasi yako karibu na mimi,nikitupa jicho moja, tu,nimeshalipata jibu,…siunanifahamu zangu, na huko duniani ndio hivyo hivyo, ukipata dili, ni mara moja pesa ipo kibindoni, huhitaji mahesabu makali….’akaniambia.

Ni kweli huyu jamaa alikuwa mwepesi sanawa kuibia,na hutaamini alifaulu kiajabu ajabu sana, na kama alivyosema kuwa tatizo lake ni kupata hicho cheti, akishakipata hicho cheti maisha kwake yamenyooka, na ndivyo ilivyokuwa, sisi tuliokuwa tukiumia vichwa kwa kukesha na kukokotoa mahesabu magumu, na kufaulu mtihani kwa maksi nyingi, ilikuwa ni kazi bure, mtihani wa maisha ukatuginga,….

******

Nilifika kijijini, na haraka nikapata baiskeli, na kuelekea huko  ndani ndani , ambapo mgonjwa akiumwa hubebwa kwa mkokoteni, au baskeli, na mara nyingi wajawaziti huishia kujifungulia njiani,…niliangalai ile hali ya maisha pale kijijini, nikaumia moyoni, na nikasema mimi nikiwa mbunge nitahakikisha najitahidi nipambane ana hii hali. Hapo ndipo wazo la kuingia kwenye siasa, likaanza kujijenga.

Nilipofika kule kijijini, nilimkuta bibi wa yule binti akiwa anafagia, aliponiona akasimama kuniangalia kwa makini, akauliza;

‘Wewe ndiye mchumba wangu?’ akauliza kwa mzaha.

‘Ndio mimi mumeo,…siku hizi unaniita mchumba wako tena, mimi ni mumeo…uchumba ulikuwa miaka ile….au umeshasahau…’ nikasema kitani huku nikimsogelea huyu bibi.

‘Siku hizi macho hayaoni vyema, nashukuru sana, maana hapa kijijini sasa natamba, hakuna mwenye nyumba nzuri kama hii…wewe ndiye peke yake unayefaa kumuoa binti,mjukuu wangu…’akasema.

‘Ina maana nyumba ndiyo mahari ya kumuoa binti yako…?’ nikamuuliza huku nikishangaa, kwani huyu bibi anajua kuwa mimi ndiye niliyejenga hii nyumba, kumbe ni mwenzangu, na sikuwa nalijua hili hadi aliponiambia jamaa yangu mmoja, na nilipomuuliza huyu binti, alisema yeye hajui ni kwanini anamjenga bibi yake nyumba.

 Yule bibi akaniambia, ‘Pamoja na hayo,…sasa nitajuaje kuwa kweli unanipenda, kama hukuonyesha kwa mifano kama hii,…karibu ndani..’akanipokea lile begi langu lilokuwa nimeweka zawadi,lakini hizo zawadi niliziona niliziona kama sio mali kitu ukilinganisha na hiyo nyumba, maana kijumla nyumba hiyo ilikuwa ninzuri, nasijui jamaa alitumia shilingi ngapi kuikamilisha, maana aliijenga kwa muda mfupi tu ….

*******

Baadaye alikuja binti mwenyewe, alikuwa kabeba mfuko, kuonyesha kuwa alitokea sokoni, na aliponioa alishituka na haraka akakimbia ndani kuweka ule mfuko, akarudi akiwa na huzni tele usoni, na kwa heshima akanisalimia, na kuniangalia kwa muda,  na hapo hapo machozi yakaanza kumtoka akasema, ….

‘Mbona umekuja ghafla, bila hata taarifa….?’ Akaniuliza, akionyesha kuwa na wasiwasi mwingi.

‘Imebidi iwe hivyo, ili nije nihakikishe mwenyewe,maana mengi yametokea na mengi nimeyasikia na jinsi nilivyoona nahisi kuna jambo ….’nikasema, na wakati huo yule bibi alishatoa.

‘Najua unavyojisikia, lakini sina uwezo zaidi,…nashindwa kuhimili hii hali tena,….ungelikuwa kwenye sehmu yangu ungelinielewa, …. nasikitikika sana, na naomba ukubali matokeo,ili ..hata sijui niseme nini..’akainama akionyesha uchungu.

‘Nikubalije matokeo,…mbona sikuelewi ina maana mumeshaongea na huyo jamaa mkamkubaliana?’ nikamuuliza.

‘Wameongea na wazazi wangu, mimi nimekuja kujulishwa tu,….kuwa kuna mtu anataka kunioa na mahari imeshapokolewa, na zaidi ya hayo, wameshamjengea bibi yangu nyumba, wakasema sasa kama kweli nampenda bibi , nikubali kuolewa....maana nitajisikiaje bibi ambaye kijiji kizima wamekuwa wakimsifia, leo hii anafukuzwa kwenye hiyo nyumba....’ akasema kwa uchungu.

‘Mimi siamini hayo unayoniambia, ina maana wewe hujawahi kukutana na huyo mtu mkaongea , ukamwambia msimamo wako, au ndio mslishakubaliana naye, unanivunga tu hapa?’ nikamuuliza.

‘Huyu mtu , alikuwa akija mara kwa mara wakati nipo huko mjini, na nilishawahi kumwamia kuwa mimi sipo tayari kuolewa na yeye, akasema kuwa yeye ni chaguo la wazazi wangu, kwahiyo nijiandae kuwa yeya atakuwa mume wangu, mimi nilijua kwua ni utani tu, kumbe mwenzangu kazamiria,...kuna hata siku alitaka kuninunulia gari, mimi nikakataa’akasema.

‘Oh, sasa mbona hukuwa unaniambia yote hayo,....lakini sio kitu, cha muhimu ni misamamo wako, namjau yule mwenzangu, kazamiria shari,... kwahiyo wewe sasa unasemaje..?’ nikamuuliza.

‘Mimi nisemeje, kwa hali kama hiyo,…hebu niambie, …sio kwamba sikupendi, nakupenda sana, lakini ….angalia, hali ilivyo, nampenda sana bibi yangu, na kitu nilichokuwa nikikiombea ni yeye kuwa katika nyumba nzuri, na ukumbuke kuwa wazazi wangu wameshachukua pesa za mahari, na wamenitishia kuwa nikikataa kuolewa na huyo jamaa, wao hawana radhi nami…..’akaniangalia kwa macho yaliyojaa huruma.

‘Kwani mimi nisingeliweza kuyafanya hayo, ni swala la muda tu, na mapenzi yetu yanaingilianaje na hili la nyumba ya bibi yako,…?’ nikamuuliza kwa masikitiko.

‘Hebu niambie mimi nifanyeje kwa hali kama hii….?’ akaniuliza. Niliinama na kuwaza mpango wangu niliokuwa nimeupanga, kichwani mwangu,nikahisi hautafaa tena,.... nikamwamgalia yule binti,na wivu ukanitinga, ina maana nitamkosa huyu binti hivi hivi, hapana, lazima kufanyike kitu, lazima...

Na kabla sijasema neno, mara tukasikia sauti ya pikipki zikija kwa kasi, na kusimama nje ya nyumba, na ghafla mlango ukafunguliwa bila hodi.....sote tukageuka kumwangalia ni nanii huyo anayeingia kwa fujo, .......

NB. Mambo ndivyo yalivyo, lakini tutajitahidi kidogo kidogo.

WAZO LA LEO: Mapenzi ni kati ya wapendanao, wengine ni wasindikizaji tu.


Ni mimi: emu-three

3 comments :

samira said...

m3 mkasa umenoga tunasubiri next.
Eid mubarak

emuthree said...

Samira mpendwa, minalifaidhina, tupo pamoja, Mungu akipenda!

Anonymous said...

This text is invaluable. How can I find out more?
My website > It Works Body Wraps