Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, August 15, 2012

Mbio za sakafuni,huishia ukingoni 4



Kila mfanyakazi tunayemchukua hakai hapa nyumbani, sasa nimechoka kabisa kutafuta mfanyakazi wa nyumbani, naona ni heri njifanyie kazi zangu mwenyewe, kwanza nililelewa kama mfanyakzia wa nyumbani…’akasema mke wangu.

Kipindi hicho maisha yetu yapo juu, tuna kila kitu, …lakini maisha ya ndani yalikuwa na mitihani yake, na ilionyesha wazi kuwa tulihitaji msaidizi, ili na yeye apate muda wa kufuatilia miradi yetu.Niliinuakichwa na kumtizama kwa macho ya huruma, …maanaalikuwa mtu wa pilikapilika, shughuli zandani, shughuli zamiradi, shughuli za kijamii, zote alikuwa akijitahidi kujumuika nazo.

Nilimwangalia na kutabasamu, na hapo nikakumbuka siku za nyuma, wakati akiwa binti, wakati nampigania kumpata, ilikuwa kama kampeni za siasa ambazo nilikuwa nikipambana nazo, na hata siku anaingia kwangu kama mke wangu sikuamini.

‘Unanikumbusha mbali sana mke wangu, sijui kama ningekukosa ingelikwuaje…’nikasema.

‘Siungeoa mke mwingine, wanawake tupo wengi,….’akaniambia huku akipanga panga vitu pale ndani, na mimi nikajikuta nikiwaza maisha yaliypita…

*******

Nilipomaliza chuo kikuu tu, nilianza maisha kwa kuajiriwa serikalini, na nilikuwa mmoja wa mameneja, na kwa ujumla nilijitahidi sana kwenye kazi yangu hiyo, kwani nilikuwa nakipaji cha kuwavuta wateja, kwahiyo maswala ya biashara yakawa yapo juu kweney hilo shirika langu,lakini mshahara wangu hakuwa mkubwa kiasi hicho.

Nikiwa nahangaika huku na kule kuweza kumudu maisha, maana pamoja ya kuwa sijaoa lakini nilikuwa na majukumu ya kuwasomesha wadogo zangu, nilikuwa na mjukumu ya nyumbani kwa wazazi wangu, achhilia mbali akina mjomba, ambao walikuwa bega kwa bega, kunisaidia kufanikisha elimu yangu.

Siku moja nikakutana na rafiki yangu. Yeye aliajiriwa kwenye mshirika ya watu binafsi, na mshahara wake ulikuwa mkubwa, kwahiyo hata maisha yake yalikuwa mazuri ukilinganisha na mimi, na kila tulipokutana alikuwa akinikoga kuwa mimi kazi yangu ni kuongea tu, na nimefanya makosa kukimbilia serikalini….

‘Wewe nimegundua kuwa,unafaa uwe mtu wa majukwaa, ofis haikufai, …’akaniambia siku moja.

‘Hilo ni moja ya malengo langu, lakini maswala ya majukwaa, maswala ya kisiasa, yanahitaji uwe umejiimarisha kwanza,….ipo siku nitatimiza lengo langu hilo la kuwa kiongozi…’nikasema.

‘Sawa,..tyaache hayo, maana wewe na ndoto zako za kuwa kiongozi, siziwezi,  hebu niambie utaoa lini?’ akaniuliza.

‘Swaali kama hilo, ninaweza kukuuliza hata wewe…hivi wewe utaoa lini?’nikamuuliza huku nikiwaza hilo swali, kwani nilishaulizwa na wazazi wangu, lakini sikuwa na jibu la haraka kiasi hicho.

‘Mimi sizani kama itapita mwezi, utasikia sasa hivii nikitagaza harusi yangu, mambo yameshajipa, …’akaniambia huku akishika kidevu chake.

‘Ina maana unaye mchumba tayari?’ nikamuuliza nikiwa na wazo jingine kichwani, namjau sana rafiki yangu huyu anao marafiki wengi wa kike, lakini wote walihsniambai kuwa hawafi kuolewa, na marafiki wakupitisha muda.

‘Hilo sio swali, nitaoa bila ya kuwa na mchumba…yupo msichana bomba, …mrembo,…!’akasema huku akionyesha tabasamu pana mdomoni, na kutikisa kiwati hake cha bei mbaya sakafuni, alionyesha kabisa kuwa ana furaha ya aina yake.

‘Mbona hujanitambulisha,…wewe ni rafiki yangu wa siku nyingi, na tumekuwa tukiambizana kuhusu maswala yetu,…’nikamwambia.

‘Hilo ni swala binafsi,…kwanza wewe sikuamini….maana tumetoka mbali,nakujau sana.’akasema na kucheka.

‘Sawa, hata mimi nipo mbioni , sizani kama nitamaliza mwezi….’nikasema nikiwa sina uahkika na huo usemi wangu,kwani nilikuwa bado sijaamua kuoa, mambo bad yalikuwa yakinichanganya.

‘Unamuoa nani…?’ akaniuliza kwa hamasa, na uso wake ukabadilika na kuonyesha wasiwasi.

‘Hayo ni maswala binafsi hayakuhusu wewe..’nikamwambia huku nikigonga na kidole kwenye meza.

‘Aaa-haaa, nimegundua ina maana wewe ndiye unayemfanya mchumba wangu, asikubaliane na mimi , kila siku ananiambia bado atanipa jibu,….sikiliza, wewe ni rafiki  yangu, sioni kwanini, uwe king’ang’anizi,  wewe bado hujakamilika kimaisha, wapo wanawake wengi, subiri ukikamilika kimaisha, utapata msichana mwingine…kwanini tuingie kwenye ushidani usio na maana’akaniambai rafiki yangu huyo.

‘Sijakuelewa, una maana gani kusema hivyo, kwani huyo unayetaka kumuoa ni nani,…?’ nikamuuliza huku nikiwa nimekunja uso kwa hasira.

‘Kwani wewe huyo unayetaka kumuoa ni nani, maana usije ukaleta yale maisha ya kishulehapa, …sasahivi tupo uraiani, tunahitajika kufanya kweli, mimi ninakushauri, kwanza jipange kimaisha,…, jenga nyumba, halafu nunua gari ….’akasema huku akiangalia gari lake, lilikuwa mbeel yetu.

‘Halafu .., ndio uwaze maswala ya kuoa, mimi vyote hivyo ninavyo, sina shida, hata wakisema mahara ni shilingi milioni ngapi,  nitalipa tu,..fikiria bibi yake, nimeshamjengea nyumba safi pale kijijini hakuna tena, sasa ….wewe tuliza kichwa,jenga nyumba kwanza, maswala ya kuoa yapo tu…’akaniambia.

‘Ina maana imefikia hapo rafiki yangu….!’ Nikasema huku siamini hayo ninayoysaikia toka kwa huyu rafiki yangu, maana kama ni huyo binti,nilisha jitambulisha hadi kwao, hadi kwa huyo bibi yake, na walishanitambua kamamchumba wa binti yao, sasa……

‘Rafiki yangu huko unapokwenda nikubaya,…sioni kwanini uwe unajenga ushidani na mimi, kwanini na wewe usitafute msichana mwingine, ….mpaka awe huyo, ilihali unajau kabisa mimi nay eye tunapendana….?’ Nikamuuliza .

‘Mnapendana…ni nani anayejua kwua mnapendana…’akasema huku kicheka, na kuniangalai kwa dharau.

‘Mimi nilishakuambai hilo, na ndio maana nikaliweka wazi kwako..’nikasema.

‘Lakini hukusema kuwa unataka kumuoa,…mnapendana, mbona mimii nlishakuonyesha wasichana wengi, nikakuambia kuwa tunapendana, lakini sikuwa na malengo ya kuwaoa,….sasa nimeamua kuoa, ndio nikamchagua huyo, kwanza hebu muangalie, yule binti,….anakufaa wewe kweli..’akaniambai huku akinitizama juu chini.

‘Siamini, kama na huyo, siamini….’nikasema.

‘Utaamini siku hiyo, ukiona tunakwenda Zanzibar kwenye asali ya mwezi….fungate al nguvu….’akasema huku akishika kidevu.

‘Unajidanganya rafiki yangu, hapo tunazungumza kuhusu pesa na maisha bado hujaangalia mapenzi, je huyo unayetaka kumuoa anakupenda,maana umeshaanza kuweka walakini, kuwa huy o unayetaka kumuoa anakuwekewa kiwingu, hajakupa jibu la uhakika,..au sio, ina maana hakupendi..’nikamwambia.

‘Ninajidanganya, unajidanganya,…mapenzi gani, bila pesa, hayo mapenzi yapo kweli,labda….huko kijijini, lakini yule keshaishi haa mjini, anajua nini maana ya pesa….nikuambie ukweli tafiki yangu,mapenzi ili yakamilike, unahitajikana wewe mwenyewe uwe umekamilika, habu niambie, kwa mfano  mumeshaoana, ndani hakuna kitu,kweli kutakuwa na raha, kweli kutakuwa na mpenzi hapo….acha ,mambo yako ya jukwaani bwana…’akaniambia.

Mara simu yangu yangu ikaita, nikaipokea kwaharaka bila kuangalia ni nani aliyepiga hiyo simu, na nilipoweka sikioni nikasikia ile sauti inayonikosesha usingizi. Nikamgeukia rafiki yangu, ambaye alionyesha wazi kuwa anajua ni nani huyo aliyepiga simu.

‘Nina mazungumzo na wewe ya haraka sana..’akaniambia.

‘Kuna nini kimetokea,?’nikauliza kwa wasiwasi, nikainuka pale kwenye meza nakusogea pembeni, rafiki yangu aakwa akinifuatilia kwa macho.

‘Wazazi wangu wameshapokea posa, ….’akasema.

‘Posa ya nani?’ nikauliza kwa hasira.

‘Posa ya kwangu, …na….sikuhusishwa kabisa,…, sijui nifanye nini…’sauti ya huzuni ikatanda masikioni mwangu.

`Unasema nini?’ nikauliza kwa hamaki, na simu ikakatika, na hata nilipojaribu kupiga tena ikawa haipatikani, nilipogeuka kumwangalia rafiki yangu, nikamkuta akiniangali kwa dharau, huku akiwa na tabasamu tele mdomoni. Aliangalia saa yake, na kuinuka,…. akanisogelea na kunishika bega, akasema;

‘Rafiki yangu pesa …ni kila kitu, ukiwa na pesa, na maisha mazuri, huwezi kushindwa maisha, utapata kila ukitakacho,nyumba nzuri, gari zuri…mke mzuri, huna shida,….’akaniambia huku akiniminya miniya kwenye bega, nilitamani niinuke nimtie ngumi,lakini nikatulia moyoni nikisema;

‘Sikubali….’ Yule rafiki yangu akawa anatembea pole pole akielekea kwenye gari lake, na huku akigeuza kichwa kuniangalia kwa nyuma, mimi nikasema;

‘Ina maana wewe rafiki yangu, umenigeuka tena…tulishakubaliana kuhusu huyu msichana, ukasema huna haja naye tena,…?’ nikamuuliza. Yeye akacheka huku akifungua mlango wagari lake, na baadaye akageuka na kuniangalia kwa dharau akasema;

‘Mimi huyo-huyo….kuwa nilikubaliana na wewe,..hahaha hayo ni maisha binafsi bwana..na kwanini nikubaliane na wewe, wakati yeye mwenyewe, huyo binti,  alishasema mwenye kisu kikali ndiye atakaye kula nyama, ….au umesahau,.. sasa ujue kuwa kweli mimi ndiye mwenye kisu kikali…’akasema huku akichezesha vidole kuonyesha kuwa yeye ana pesa.

Nikaduwaa,mwili wote ukaisha nguvu, ….niliumia moyoni, sijawahi kumia kiasi hicho, nikaingiwa na hasira, chuki, na …sijui kama ningelikwua na slaha pale ningelifanay nini,….lakini moyoni nikasema;

 ‘Kama yeye ana pesa, mimi nina mdomo, mimi ninacha zaidi yake yeye, ….nina penzi la kweli ,huyo binti ananipenda mimi kiukweli..hilo nina uhakika nalo…sijakata tamaa..’


NB: Hayo ni maisha ya mwenzangu huyu, je wewe uliwahi kukutana na mambo hayo, huo ni mwanzo tu, wamaisha ya  huyu jamaa kipindi kileeee,je….,ilikuwaje.

WAZOLA LEO:  Penzi la pesa halidumu,maana pesa ikiisha na penzi limeisha mapenzi ya kweli hutoka moyoni.

Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Hivi tukiweka waandishi wa stories kama hizi, tunaweza kukulinganisha na nani? Nawaza tu,hongera sana M3, SIONI MFANO WAKO HAPA bONGO, UNA KIPAJI!

Anonymous said...

Kuna blogs nyingi sana zimeibuka hapa bongo, na wengi wanaishiwa na kuanza umbeya, ww nakusifu upo na msimamo wako, endelea hivyo hivyo, usijali, ipo siku watakuona,ipo siku hawa watoa matangazo watakuona.
-Adili

Precious said...

Pesa pesa pesa pesa inavunja urafiki, undugu n.k utu umeisha kwenye jamii kwa ajili ya PESA. PESA lini utaiacha dunia hii iwe ya upendo, amani, mshikamano n.k.
M3 unatishaaaaaaaaa kwa kweli ni zaidi ya kipaji ulichonacho.

Anonymous said...

M3 MBONA LEO KIMIYA?

Rachel Siwa said...

Mmmmhh ndugu wa mimi kazi imeanza vyema, yaani Mungu yu pamoja sana tuu.Kipaji MUNGU Amekujalia.

Pamoja Daima.