Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, August 14, 2012

Mbio za sakafuni,huishia ukingoni 3




  ‘Achana naye yule, kwanini ubabaika na watoto wa mitaani, wewe ni mtu muhimu sana…’aliniambia rafiki yangu akiwa nyuma yangu,akinifuatilia….aliendelea kunihadithia rafiki yangu,huku akionyesha kuwa ana haraka.


‘We niache kwanza, hayo hayakuhusu…’nikasema.

‘Hapo hupati kitu, …..nakuambia ukweli….’akasema kwa dharau.

‘Sawa, sio mbaya….’nikasema huku nikijitahidi kumkimbilia huyo binti.

    Inabidi nije nikuelezee kuhusu huyu binti kwani ni mtu muhimu katika kisa cha maisha yangu….lakini kwa leo tuushie hapa, nawahi mambo fuani,maana sijakata tamaa na kushindwa kwangu,….sikubali kabisaa…’akaniambia rafiki yangu na tukaagana.

Sikuonana naye wiki mbili kwania alikwua akifuatilia kesi yake, na mara nikasikia anaumwa, na hali yake ni mbaya sana. Mimi kama rafiki yake nikafika hospitalini, sikumkuta, nikaambia kuwa keshatolewa, maana hayo matatizo hayahitajii kulazwa sana, anahitajika akaugulie nyumbani.Basi ndio nikamfuata huko nyumbani kwake.

‘Vipi rafiki yangu, imekuwaje, ….?’ Nikamdadisi.

‘Ni mitihani, siamini,…maana hili tatizo, limeanzia mbali,…nitakuja kukuhaidithia kwenye kisa ,kile kisa nilichokuwa nakuahdithia, ….najau kabisa limeanzia siku ile kule makaburini….’akasema huku akijaribu kukumbuka, akachukau leso na kufata mate mdomoni, huku akiwa kaegemea mto,alikuwa akiongea kwa shida, lakini ilionekana kuwa kuongea kwake huko kunamsaidia kupunguza msongo wa mawazo.

******

Nilikuja kumtembelea kwake baada ya kusikia kuwa anaumwa, na hali yake ilikuwa mbaya, …lakini isku nilipofika alikuwa hajamb kidogo, licha ya kuongea kwa shida, kutokana na mdomo wake kuvutika upande kwa ajili ya mshituko wa moyo.

‘Nashukuru sana umefika, maana siku ile nilipokutana nawe pale mjini , tukaongea kidogo, sikuweza kukueelzea kisa change chote nilikatiza kuwahi mambo fulani, najua wewe unapenda kuandika visa, kiandike hiki kisa changu, ili waje wakisome watu, wajifunze kuwa maisha haya sio ya kukimbilia kwa pupa, …ni kama mbio za sakafuni tu,mwisho wake ni ukutani tu….’akaniambia, na mimi nikafurahi maana nilitarajia kuwa huenda angelinigomea.

‘Sasa sikiliza, mke wangu hayupo, naona tuanze huko nilipokutana naye, ..maana yule binti niliyemjua sio huyu wa sasa, ni watu wawili tofauti, wewe mwenyewe utaona, …kabadilika kabisa, na hapa nilipo naogopa kabisa, kuwa huenda hata akaniwekea sumu..’akasema.

‘Kwanini iwe hivyo na huyo  ni mkeo.?’ Nikamuuliza.

‘Kwasababu mmh,  ….ukitaka kujua kwasababu kwa sasa utakuwa umekivunja hiki kisa katikati,, ngoja nikaunzie pale nilipokutana naye, ili uone binadamu tunavyobadilika, labda ni kosalangu, nahis hivyo,lakini ndio maisha yalivyo…..

************

Yule binti akaanza kunisimulia msiha yake,;

‘Nilikuona kwa mara ya kwanza ukutoa hotuba zao nikavutika sana na wewe, lakini sikuweza kuja mara kwa mara maana mimi naishi kama mtumwa, …mama mdogo hanipi nafasi hiyo, nikitoka shule mimi ndiye mtumishi wa nyumbani,….’ilikuwa sauti ya yule binti, baada ya kumkimbilia na kujaribu kumshawishi 

.Ingawaje mwanzoni hakukubali kabisa.

‘Wewe ulikuwa na dada mkuu, unatarajia nini kwangu,…unataka niishi shule kwa matatizo,…nyumbani nina matatizo kibao, na shuleni nako unataka niwe na matatizo, we niache nenda kwa huyo dada, usije kunitia matatani bure..'akasema huku akiwa anakwenda kwa mwendo wa kusua sua, kama vile anajiuliza asimame au asisimame.

‘Yeye alikuwa akiniaga tu, lakini mimi nilikuwa na maongezi na wewe hata yeye anajua hilo suiwe na shaka kuhusu yeye …’nikasema.

‘Maongezi gani na mimi,..wakati nyie ni watu wakubwa, mnatakiwa muongee na wenzenu wakubwa…’akasema.

‘Mimi sio mtu mkubwa,mimi ini mwanafuzi tu, ….nakuomba uteremke huko kwenye basi uje tuongee huku chini kidogo’ nikamwambia  kwani wakati huo alishaingia ndani ya basi, lakini baadaye alikubali nakuteremka , tukasogea pembeni na kuanza kuongea na hapo ndipo akanipa kisa chake cha kusikitisha na mama yake wa kambo..

‘Mama yangu aliachika mapema, ….’akasema.

‘Kwanini aliachika..?’ nikamuuliza.

‘Mimi sijui maana aliachika nikiwa mdogo,nisiyejua nini kinaendelea, na hata leo baba hajawahi kuniambia ni kwanini alimuacha mama yangu na kumuoa huyu mke, asiye na huruma hata kidogo..’akasema.

‘Mama aliniacha nikiwa bado mdogo, ….mwanzoni kulitokea ugomvi kati ya mama na baba, kila mmoja akinitaka mimi, na mwishowe ikafikia muafaka kuwa niishi na bibi yangu, .... Kwani wakati huo baba alikuwa na mpngo wa kumuoa mke mwingine..nahisi huenda matatizo na mama yanahusu huyo mke mwingine, sina uhakika, kwani hata bibi hakuwahi kunisimulia.

Mimi na bibi tuliishi maisha ya shida, maana kijijini ni shida tupu, umasikini ulituandama, lakini ndio maisha yetu, niliyazoea, nikawa nasaidiana na bibi, ambaye watoto wake hawakumjali sana, …nyumba yake ilikuwa ya majani, wakati watoto wake mjini wanaishi kwa raha, …nikijaliwa kupata kazi nitahakikisha kuwa namjenga bibi yangu nyumba…’akasema huyo binti.

‘Kwanini sasa watoto wake hawamjengei mamayao nyumba ya maana?’ nikamuuliza.

‘Watamjengea vipi waache kuwajengea wake zao, na kujenga huko ukweni, ili waonekane wa maana, kwanii nyie wanaume mna maana, ….nasikia baba kajenga huko kwa mke wake, nyumba ya maana tu, mama yake anaishii kwenye nyumba ya nyasi, na hata pesa za matumzi hatumi, mpaka bibi alalamike wee, sijui akichoka ataishije, natamani nirudi nikaishi naye, nimsaidie, …lakini mimi hayo hayanihusu sana kwa sasa ipo siku nitamsaidia…’akasema.

‘Haya niambie kuhusu maisha yako, ilikuwaje baadaye….?’nikamuuliza, nikiwa na hamu ya kumjua huyu binti vyema, maana akiongea utatamani umsikilize, sikutaka sana kujua maisha ya kijijini maana kweli mengine yanasikitisha, hata mimi kuna muda nilijisahau, lakini nashukuru niliwahii kuwajenga wazazi wangu nyumba ya maana’akasema rafiki yangu huyu, huku akifuta mate kwa leso yake.

Yule binti akaendelea kunihadithia maisha yake, akasema;

 ‘Baada ya kumaliza darasa la saba, baba akanichukua ili nisomee huku mjini. Kwa mara ya kwanza nilfurahi maana nakwenda kusomea mjini. Kila mtu kwenye umri wetu huo alitamani sana kuja kuishi huku mjini. Lakini nilipoika na kukaa wiki moja tu, nilimkumbuka bibi yangu ambaye alikuwa akinipenda sana….nilitamani nirudi huko kijijini, lakini sikuwa na jinsi, maana nilijua nina malengo ya misha yangu ya baadaye.’akasema kwa huzuni.

‘Mama alinifanya mimi ndiye mfanyakazi wake wa nyumbani, kila kazi ni mimi,nilitakiwa niamuke saa kumi na moja kasoro, ili nihakikishe nimefanya usafi wa ndani, nimefua nguo za mtoto, maana yeye alikuwa na mtoto mdogo, nifue na nguo zao, halafu nipike chai, nitenge mezani, wao wakiamuka wanajiandaa wanakunywa chai, hao wanaondoka zao kazini….sasa na mimi hapo Napata muda wa kujiandaa kwenda shule…’akasema.

‘Kwani hapo unapoishi sio mbali na shule, na mtoto anabakia na nani?’ nikamuuliza.

‘Ni mbali, lakini hawanichukui kwenye gari lao, wanamchukua mtoto wao hadi shule ya chekechea anayosoma. Mimi napewanauli ya daladala, wanasemawakinichukua mimi watachelewa,  kwasababu ya kuogopa foleni, …mimi hilo sijali’akasema na kukunja uso kwa huzuni.

‘Nimezoea maisha ya shida, kama wasingenisimanga, sioni taabu,huwa napannda daladala, hadi shuleni, nikifika shuleni nimechoka kutokana na kazi za asubuhi, wakati mwingine najikuta nimelala darasani. Na ikifikia jioni nakimbilia nyumbani nakutana na kazi zile zile, …kitanda kwangu ni kuanzia saa sita za usiku, na hapo nipo hoi, sijui kama kuna home work ,….yaani we acha tu..’akasema.

‘Sasa kwanini humwambii baba yako, akatafuta mfanyakazi wa ndani….?’ nikamuuliza.

‘Baba …ooh, ukitaka ugomvi na baba uongee ubaya kuhusu mke wake, yeye anasema mke wake ni mzungu, hana tabia mbaya,..basi tena, mimi nimeshajionea kawaida, ndio maana nikikaa peke yangu namkumbuka mama yangu….nasoma kwashida sana, huenda ipo siku nitajitoa kwenye haya maisha,,’akasema.

‘Kwani mama yako yeye yupo wapi?’ nikamuuliza.

‘Kaolewa na mume mwingine na wanaishi Mwanza, huwa sina mawasiliano naye sana , na nikionekana nawasilina naye cha moto nitakiona…basi huwa sitaki hata kumpigia, kwanzamume wake aliyemuoa naye ni wale wale….sitaki hata kwenda kwao,naona ni heri nibakia hapa hapa hadi kitakapoeeweka….yote maisha.’akasema.

‘Pole sana, sikutarajia mrembo kama wewe uwe na maisha ya taabu kiasi hicho, Sasa nikuulize mwenzangu alikuambia nini kuhusu mimi?’ nikamuuliza.

‘Mwenzako yupo, ooh, yule mvulana, ..aaah, mimi sikuwa namsikiliza sana, anasema yeye ana pesa sana, …nikiwa naye sitakuwa na maisha ya shida, …hata sikuwa namtilia maanani, ila tu kwa vile alikuwa akinitoa upweke ikabidi nimsikilize’akasema na kunyamaza kimiya.

‘Mimii sitaki nikuharibie maisha yako, au kukudanganya sana, ila nakuahidi kuwa ukiwa rafiki yangu nitahakikisha kuwa hupati shida…’nikasema huku moyoni nikijua kuwa namdanganya, mimi mwenyewe kula kulala, wapi nitampatia hayo mahitaji yake , lakini niliona niweke karata kubwa zaidi ya mwenzangu.

‘Nyie wanaume bwana, kwani hayo yote ya nini, mimi bado nasoma na wala sitaki urafiki na mwanaume yoyote, nisije nikalikoroga, niliyo nayo yanatosha,…hata sijui kwanini nimekusimulia maisha yangu, labda…’akasema akitaka kuondoka.

‘Sikiliza, mimi nakuahidi kuwa hata kama ni ada nitajitahidi nikulipie..’nikamdanganya.

‘Kwani wewe unafanya kazi…wewe si bado mwanafunzi, usinidanganye kama mtoto, …?’ akasema huku akiniangalia kwa kujiiba, huku anatafuna ukucha.

‘Mimi sifanyi kazi ndio, lakini wazazi wangu hawana shida,….nikitaka pesa wananipa tu, hata hivyo, pesa za matumzi wanazonipa ni nyingi sana, kwanza chukua hizi hapa ukapande taksi…’nikataoa pesa nilizopewa kama zawadi wakati wa kutoa mada kwenye huo mkutano., nia na lngo langu ni kujifaharisha, ili tu nisije nikashindwa na yule rafiki yangu.

‘Aah,…mimi sitaki pesa yako, usije ukanitia kwenye majaribu bure…’akakataa kata kata, lakini nikamshinikiza kwenye mkono na kuondoka haraka.  Huo ulikuwa mwanzo wa  urafiki wetu, sikujua kuwa ndio chanzo cha uadui na rafiki yangu hadi hii leo,….uadui ulikuja kuingia hadi kwenye mamo ya siasa.

NB. Nitakuwa naandika kidogkidogo, ili na mimi nipate  muda wa kukipitia kisa kilichopita na kikiweka sawa, muda ndio huo huo, na jembe la kazini,..msijali tutafika tu, kidogokidogo

WAZO LA LEO:  Kila mtu ana mbinu zake za kutafuta maisha,lakini tuwe makini na mbinu ambazo mwisho wake ni majuto,…tukumbuke kuwa majuto ni mjukuu, huja baada ya kitendo.


Ni mimi: emu-three

9 comments :

Anonymous said...

Wengi wa wanablog hupenda kuweka picha zao, na inakuwa rahisi kuwajua , lakini wewe mbona haupo wazi, tungelifurahi kukujua zaidi, kisura, jina ...ni wazo tu mkuu, maana wewe ni mkali.

Anonymous said...

Duuh, nimekubali!

Yasinta Ngonyani said...

Kisa hiki kimenigusa ila mbaya nimejikuta nikisoma hiuku nikilia. Maisha kwa kweli ni mafundisho sana na kweli polepole ndio mwendo na mvumilivu hula mbivu...Nakubalina na mwandishi kuwa utakuwa ukiandika kidogokididogo itakuwa safi ukifanya hivyo. Kazi nzuri ndugu wangu.

Anonymous said...

Visa vyako vinavuta hisia kama vile unaangalia movie, wewe ungelifaa uwe mtunzi wa movie,ingekufaa sana!
Kazi nzuri m3

samira said...

well done m3 kisa kimeanza kusikitisha sana
tupo pamoja milele

Unknown said...

Kazi njema m3!

Unknown said...

Kazi njema m3!

Unknown said...

Kazi njema m3!

EDNA said...

Duuh jirani wewe ni nomaaa,endelea kutupa uhondo.