Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, August 13, 2012

Mbio za sakafuni,huishia ukingoni 2
Kila mtu kazaliwa na kipaji chake, mimi nilizaliwa na kipaji cha kuongea, kipaji hiki kilianza kuonekana wakati nipo sekondari, kwani kwa ajili ya kipaji hiki nilichaguliwa kuwa kiongozi wa shule, nilianza kama kaka mkuu, na hata nilipofika chuoni nilijulikana kama waziri mkuu.

‘Huyu ndiye waziri mkuu mtarajiwa…’alikuwa mmoja wa walimu wangu akipenda kuninadi katika moja ya shuguli zetu za kishule. Nami nikawanavimba kichwa, …na nikawa nikijiweka kinamna ili nifanane na hicho cheo.

Siku moja wakati natoa moja ya mihadhara ya kisiasa, tukiwa tumejumuika wanafunzi wengi, jicho langu lilitua pembeni mwa wasikizaji,ambao walikuwa wakiongezeka kila siku. Macho yana maajabu yake, kwani jicho langu lilipotua upende ule wa kushoto kwangu, moyo wote ulikuwa kama umeguswa na umeme, nikajitahidi kujihimili, lakini nilihisi kuwa nimeguswa na jambo lisilo la kawaida, nilihisi kama nimeona kitu ambacho ni muhimu sana katika maisha yangu.

Baada ya ile shughuli tukawa tunagawiwa vinywaji na chakula, na mimi nikawa naangaza huku na kule kama ninaweza kukiona kile klichoteka akili na moyo wangu, na nilipohakikisha kuwa , hakuna hicho ninachokitafuta,  nikamgeukia mmoja wa marafiki zangu,;

‘Hivi hapa wamealikuwa shule ngapi?’ nikauliza.

‘Shule nyingi tu, kama sikosei ni shule tano zilizokubali mualiko kimaandishi, lakini baadaye walikuja wengine kwa rizaa zao, kusikiliza hili kongamano, unajau siku hizi vijana tumeamuka, tunajaribu kuwa mbele, na  ile dhana ya taifa la kesho inaanza kufifia……’akaniambia rafiki yangu huyo aijaribu kudonoa moja ya maneno yangu niliyopenda kuyaongea.

‘Aaah, unajua kuna kitu ambacho kimenipata wakati nahutubu pale juu, sijui ndio mitahani au ndio majaliwa ya mungu,….;nikasema huku nikigeuka huku na kule.

‘Kitu gani kimekupata, usiseme umetupiwa majambo,maana dunia hii haina heri..?’akaniuliza rafiki yangu akijaribu kufuatilia macho yangu, huko ninapotizama.

‘Hapana sipo huko kabisa,.., hebu niambia shule gani za wasichana walioalikwa hapa?’ nikamuuliza.

‘Shule mbili za wasichana,….na hizi zingine ni za wavulana,…na kuna wengine wa shule z akaribu wamefika, wao wamevaa nguo za nyumbani,…kwani kuna jambo gani, ?’ akaniuliza.

‘Kuna msichana mmoja nimemuona, na nahisi kama namfahamu,alikuwa kaka pembeni, cha ajbu yeye alikuwa kama hanisikilizi, ila mara kwa mara alikuwa akinitupia jicho, na kuniangalia kwa makini,sina uhakika kuwa ni mwanafunzi au ni wasicha wa uraiani, maana nilimuoa akiwa kasimama pembeni kabisa peke yake,  halafu akakaa na kushika shavu, na usimamaji wake, ulikuwa aina yake, kwani alionekana mwingi wa huzuni…’nikasema.

‘Alisimamaje,?’ akaniuliza na kujaribu na yeye kuangalia huku na kule, kama vile na yeye kavutika na hilo nililomuambia.

‘Alikuwa kasimama peke yake, huku kashika shavu, halafu alikuwa ananiangalia bila kupepesa macho…’nikasema.

‘Unamfahamu kweli au ndio umeshazimia kwake, sema ,mimi naweza kumtafiti na kumpata, yupoje kisura,….ukinielewesha vyema nitakwenda kuzunguka kule walipo wasichana, na nitampata tu, kabla hawajaondoka,…’akasema rafiki yangu ambaye nimjuavyo ni mwepesi wa kufautilai majambo.

‘Fanya hivyo…ukimuona nitonye, …alikuwa kasimama peke yake mwishoni kabisa, ni mrembo kwakweli, na ni wale wasichana waliojaliwa urembo usio mithilika…’akasema

‘Oooh,nahisi kama nilimuona, ..ngoja nikamwangalai kama ndio huyo, nitamuona tu,..’akasema na kuondoka haraka, na mimi moyoni nikasema nimefanya kosa kubwa,lakini sikuwa an jinsi maana mimi pale sikutakiwa nionekane tofauti, kwani nilikuwa natayarishwa kama kiongozi mtarajiwa.

*****

Kiongozi unaitwa huku kwenye meza kubwa…’nikashikwa bega na mmoja wa waandaji wa hilo kongomano. Nilishituka kidogo, maana sikuwepo kimawazo, mawazo ambayo yalinipata siku ile yalikuwa mengine, mawazo ya kiutu uzima, sikuwa na kawaida ya mawazo kamahayo kabla. Nilihis kuwa huenda ni wakati umefika wa kuwa na rafiki wa kike.

Tulipokuwa meza kuu, nikapata mwanya wa kuongea tena, na kutoa moja ya hutuba zangu ambazo wengi walizipenda, na kila hatua nilisikia mkofi yakitanda hewani, na mimi nikisikia hivyo, akili inachanganya, mambo yanajipanga kichwani utafikiri, nilikuwa nasoma kwenye karatasi, ,…

Wakati naongea nikatupa jicho upande ule wa kushoto kwangu, na mara nikamuona rafiki yangu akiwa kasimama na msichana wakiongea kwa hamasa, mwanzoni sikujali, nikawa natoa mambo yangu, lakini mara ya pili macho yangu yalipotua pale aliposimama rafiki yangu, nikaweza kumuona yule msichana, ambaye alikuwa akijaribu kuaniangalia, lakini rafiki yangu alikuwa kama anamzuia asiwe makini na mimi, awe anamsikiliza yeye,nikajikuta ghafla nimeshikwa na bumbuwazi,..kumbe alikuwa yule msichana.

Nilimalizia yale niliyotaka kuongea na kurudi pale nilipokuwa nimekaa na hapo nikatupa macho yangu pale alipokuwa rafiki yangu, sikumuona tena, na hapo moyo ukaanza kunipiga kwa wasiwasi, kuna kitu kikaniingia moyoni, ilikuwa ni hisia ya ajabu. Nilijua huyo rafiki yangu alivyo, atakuwa keshaongea na huyo msichana na huenda mengi yameshatendeka, ..ndivyo nilivyowaza kwa wakati ule..wivu ukaniingia.

Ile shuguli ikawa imefikia tamati, na watu wengi wakawa wanakuja kunipongeza, na hata hivyo sikuwa makini na pongezi zao, nikawa namtafuta rafiki yangu kwa macho, hata hivyo sikuweza kumuona yeye wala yule msichana, na wakati naagana na washiriki waliokuwa wakitaka kunipongeza, nikageuka kuondoka, na mara nikajikuta nimesimama uso kwa uso na rafiki yangu, akiwa anaonyesha kutahayari, akasema;

‘Bwana wee,nimemtafuta huyo binti lakini sikumuona…’akasema.

‘Usinitanie rafiki yangu, wewe mwenyewe umaniahidi kuwa utampata, sasa hivi unabadili maneno…una uahkika na hayo unayoyasema kweli,….?’nikamwambia kwa kumuuliza, huku nikijifanya sikumuona akiwa kasimama na yule msichana.

‘Ndivyo nilivyokuwa nimeahidi lakini unajau tena wapo wasichana wengi, na sikuweza kumpata huyo msichana, labda siku nyingine…’akasema huku akionyesha wasiwasi.

‘Sawa hamna shida nitamtafuta mwenyewe…maana unaweza ukampa mshenga kazi, na mshena akageuka kuwa mtarajiwa….’nikasema huku nikiondoka na kuelekea kule walipokuwa wamesimama wasichana, na rafiki yangu akawa akinifuatilia kwa nyuma, baadaye yeye akasimama, na kuelekea upande mwingine.

 ‘Habari yao kaka, kiongozi…’sauti nyororo yaikasikika masikioni mwangu, ilikuwa ile sauti adimu, inayoweza ikaugusa hisia zilizoganda kwa baridi, ilikuwa ni sauti kike ambayo  ingeliweza kumliwaza yoyote hususani mwanababa. Na mimi nikageuka nikiwa nimeshajenga hisia kuwa huenda akawa yule binti, na nilipogeuka nikiwa na tabasamu mdomoni, nikitarajia hivyo,lakini kumbe alikuwa mmoja wa kiongozi wa shule hizo  za wasichana akitaka kuniaga.

‘Oh,kumbe ni wewe, nilikuwa na ….’nikasema huku nimeduwaa na kukata tamaa.

‘Ulikuwa umearajia mtu mwingine nini, niambie ni nani, nitakusaidia kumpata?’ akaniuliza huku akitabasamu.

‘Hapana, hakuna shida..’nikasema kwa kuona aibu.

‘Seme tu, najua ni nani, najua ni yule uliyekuwa ukimwangalia wakati ukiotoa vitu vyako pale jukwaani,yule ni mmoja wa wasichana wanasoma masomo ya kutwa, waliambiwa wafike kama wanataka, yeye yupo kidoto cha pili,……’akaniambia.

‘Ina maana uliniona nikimwangalia?’ nikamuuliza.

‘Hukuweza kujificha, na kwa vile na mimi nilikuwa nikikuangalia mara kwa mara ,niliweza kukuona ukimwangalia yule msichana kwa jicho la kujificha, na nikahisi umeguswa naye,… nilipoona hivyo, moyo wangu uliingiwa na muwasho, fulani, maana ….’akakatisha.

‘Una maana gani kusema hivyo..?’ nikamuuliza.

‘Najua sisi wasichana kujielezea hisia zetu kwenu ni ngumu, lakini kama ningelijaliwa hivyo, na kuwa na huo ujasiri nisingelisita kukuambia ukweli wangu…’akaniambia yule mwanadada.

‘Wewe sema tu, mimi nimtu makini, na sijali kuwa wewe ni msichana, nitakusikiliza, ....hiyo ni kawaida tu..’nikamwambia, lakini kiukweli nilikuwa sipo makini na yeye , mawazo yangu yalikuwa mbali na kila mara nilikuwa najaribu kuangalia huku na kule kama nitamuona yule aliyeugusa moyo wangu.

‘Nimekuwa nikifuatilia sana makongamano ambayo na wewe umeshiriki,kwani hata mimi ni mmoja wa wapenzi wa haya makongamano,na natarajia kuwa mmoja wa wabunge watarajiwa, na kiujumla umekuwa ukinigusa, unvyoongea, na mwenyewe ulivyo, nahisi kuwa karibu sana na wewe saana…’akaniambia na kabla hajamaliza macho yangu yakatua upande wa pili nikamuona rafiki yangu akiwa kasimama na msichana, nikajua ni yule yule msichana,…nikageuka kuwafuata.

Nilipofika pale waliposimama, nikatulia kwanza ili nisikie ni nini wanachokiongea walikuwa hawajaniona, ndipo, nikamsikia rafiki yangu akisema;

‘Unajua mimi nimekupenda sana, na nimeona uwe rafiki wangu wa  karibu, achana na yule muongeaji wa jukwaani, hana kitu yule, …watu kama wale wanaopepeta mdomo hawajui kutafuta pesa, sisi ambao hatuongei sana tunajua pesa zilipo, hatuhitaji kupiga domo…’nikamsikia rafiki yangu akiongea na yule msichana. Hapo nikajifunza kitu, kumbe pesa nii muhimu,….

‘Kwani ukipenda ni lazima umtafute mwenye pesa, mimi nimevutiwa naye tu, ongea yake, na jinsi alivyo, sio kwamba nahitaji pesa zake, …’akasema yule msichana.

‘Hilo sawa, lakini una uhakika kuwa kweli yupo makini na wewe, maana mtu kama yule ana wengi, wengi wanamtizama yeye, wamatamani yeye, usije ukaumia moyo wako bure,…..achana naye, wewe uwe na mimi, nina uhakika hutaumia moyo wako….’na mara akageuka nyuma akaniona. Alishituka na kuanza kujibaragua, akasema.

‘Oh, kumbe umekuja nilikuwa nabahatisha, kama ndio yeye, …lakini nahisi sio huyu, ….’akasemam na mara nikasikia mtu akinishika bega, nilipogeuka nikamuona yule msichana niliyekuwa nikiongea naye mwanzoni kafika, na yeye akanikaribia na kuwa kama anapitisha mkono mgongoni mwangu, akasema;

‘Vipi mbona umenikimbia kabla hatujamalizana….’akasema na yule msichana mwingine aliyekuwa akiongea na huyo rafiki yangu akaona lile tendo la huyu msichana kupitisha mkono nyuma ya mgongo wangu, licha ya kuwa hakunishika maana alishituka na kuuondoa haraka pale alipowaona rafiki yangu na yule msichana.
Na yule rafiki yangu aliliona hilo tendo, na hakutaka kupoteza nafasi hiyo,akamgeukia yule msichana na kumwambia,….

‘Unaoan niliyokuambia….’Sikuamini kuwa rafiki yangu anaweza kufanay hivyo, na ghafla yule msichana akageuka kwa haraka na akaondoka, kuelekea kule walipokuwa wakisubiri gari lao, mimi nikashindwa kuvumilia nikamkimbilia.

‘Hebu subiri nikuambie, sivyo kama unavyofikiria wewe…’nikasema.

‘Hapana wewe endelea na msichana wako….mimi sihitaji marafiki wa kiume’akasema huku akiharakisha kuondoka na akaingia kwenye basi lao,…..

NB: Hapo ndipo mwanzowa ushindani wa maisha ulipoanzia, pesa , hadaa ikaanzia hapo.

WAZO LA LEO: Rafiki utakayemuona ni wa kweli ni yule anayejitokeza wakati wa dhiki.


Ni mimi: emu-three

4 comments :

Anonymous said...

story ya diary-yangu,nimeipenda sana wewe ni mtunzi bora..M,M

Anonymous said...

kisa kimeanza taratibu

samira said...

well come m3 nakujuwa sana mtu wangu unatufanya wapenzi wa blog tusicheze mbali na hapa
hata hivo siku njema

emu-three said...

Samira na wadau wengine nitajitahidi tuwe pamoja, nashindwa kupitisha siku bila kuandika chochote, maana kuandika ndiko kuwasilianana nyie, kwani...nawajali sana na nawapenda sana tuwe pamoja,

Nitajitahidi Insha-Allah!